UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
Sauti mbalimbali za nyota inayoitwa Pulsar imerikodiwa hapa katika Video hii.
Wanasayansi wa elimu ya Sayari (Astronomers) wamegundua sauti hizi kwa kutumia Radioscope na vyombo vinginevyo vya kisayansi lakini ajabu ni kwamba Tunaelezwa habari hizi katika kuruani tangu miaka 1400 iliyopita.
NYOTA
NYOTA ZINAZOJULIKANA KAMA PULSARS KATIKA KURUANI
Mwaka 1968 Mwana sayansi kwa jina la Jocelyn Bell Burnell ambaye alizaliwa mwaka 1943 huko Ireland ya Kaskazini. Alitumia Radioscope (Darubini Ya Sauti)ambayo kazi yake ni kurikodi sauti zinazotoka angani na alishangaa kuona maandishi yanayochapishwa na Darubini hiyo ni tofauti na kawaida ya sauti nyingine zinazotokana na nyota nyiniginezo kama vile aina ya nyota zinazoitwa “Quasars”. maandishi haya yalirikodiwa katika “Chart Paper”. Wanasayansi wengine pia waliendelea na utafiti na wakarikodi sauti mbalimbali za nyota Pulsar. Nyota hizi zinapopungua nguvu (energy) na kufa basi huzunguka kwa mbio sana na mwishoni hutoa sauti za migongo mbalimbali. Sauti hizi zinafahamika kama ni mapigo ya moyo na mwenyeezi mungu ameapia katika Aya tatu za mwanzo za Sura namba 86 (Attwarki) aliposema:
وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ (١) وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ (٢) ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ (٣)
Tafsiri ya Aya hizi ni kama ifuatavyo:
1/Naapa kwa mbingu na kinachogonga
2/Na kipi kikujilishacho hicho kinachogonga
3/Ni nyota inayosababisha tundu (au shimo huko angani)
Hii ndiyo tafsiri ya kisayansi baada ya uvumbuzi wa sauti zinazotoka mbinguni na mwenyeezi mungu ameacha habari hizi zigunduliwe na wasio waislamu leo hii ile iwe hoja kwao na pia kutuzidishia imani waislamu. Neno “Attariki” lina maana ya kugonga. Kwa kiarabu ukisema “Man Yaturuku Albabu” maana yake “NI nani anagonga mlango” na Neno “Athakb” maana yake ni “tundu” na chenye kufanya tundu anaitwa “Athakibu”. Na neno hili pia linaashiria uvumbuzi mwingine wa “Mashimo Meusi” huko angani yanayojulikana kama “Black Holes” Na wanasayansi wanasema kwamba Nyota hizi “Pulsar” zinapokufa husababisha Mashimo Yenye Giza” katika hewa ya mbinguni.
Hapo zamani tafsiri zilizopita pia ziliwafaa watu hapo nyuma kwani kuruani ni muujiza mkubwa. Tafsiri hapo mwanzo japokuwa zilitofautiana kidogo lakini zilikaribiana na hazikupingana.
1/Naapa kwa mbingu na kila kijacho usiku
2/Na kipi kitakapokujulisha kipi hicho kijacho usiku (Nilichokikusudia).
3/Ni nyota inayonga’ra sana
Sauti ya mapigo ya moyo “heart beat”kama wanavyosema wanasayansi au mtu anapopiga hodi mlangoni ni sauti zinazofanana na sauti ya migongo ya nyota “Pulsar” inayotoka mbinguni. Sikiliza vizuri Video hii na ufikiri vizuri tafsiri ya aya za kuruani katika sura ya “Atwariki”
Kwa kawaida Mwenyeezi Mungu anaapia viumbe vyake alivyoviumba kuonyesha umuhimu wake na leo hii tunagundua sayansi ya hali ya juu.
Je mtume Mohamed alikuwa na vyombo vyote hivi vya kisasa kama vile “Radioscope” na Je alikuwa mtaalamu wa sayansi ya elimu ya fizikia ya anga(Astrophysics).
MWANGA
MBIO ZA MWANGA
KIPIMO CHA MBIO ZA MWANGA KATIKA KURUANI
kwanza tuielewe Formula ifuatayo ambayo inatuwezesha kuhesabu mbio za aina yeyote
Speed= Distance / Time ambayo ni Distance Divide by Time
Katika hesabu zetu tutatumia herufi “C” kama Mbio Za Mwanga (Speed of Light)
Ukipata kujua umbali (distance) na Wakati uliotumika katika umbali huo (Time) basi utagawanya wakati katika umbali na jawabu litakuwa ni Speed.
Wanasayansi ulimwenguni wamefanya juhudi kubwa katika kuelewa mbio za mwanga kama utakvyoona katika video hapa zinazohusika na Historia za harakati za wana vyuoni katika kupima mbio za mwanga.
Jambo hili lina umuhimu kwani mbio hizi zinasaidia katika kujua Energy au Nguvu ya vitu mbalimbali na pia nguvu hizi zinahitajika katika elimu nyinginezo. Video zinaelezea habari hizi kwa urefu.
Mwana sayansi maarufu anayejulikana kama Einstein Alikuja na Formula yake maarufu sana inayojulikana kwa “E= MC2”
ambayo inasaidia katika kutafuta Nguvu (Energy) ya viumbile mbalimbali.
“E” maana yake Energy
“M” Mass na
“C2” ni Mbio za mwanga (speed of light) Squared.
Katika kutafuta mbio za mwanga hapo awali wana sayansi wametumia majaribio mbali mbali mpaka mwishowe wakafanikiwa. baada ya miaka mingi ya majaribio na makosa (Trial and Error) –
-United States National Bureau of Standards C=299792.4574 +0.0011 km/sec
-The British National Physical Laboratory C=299792.4590 + 0.0008 km/sec
-17th Conference on measurement and weight standard C=299792.458 km/sec
HESABU KUTOKANA NA KURUANI TAKATIFU
Jambo linaloshangaza na linalotia mkazo kwamba kuruani ni muujiza wa miujiza mikubwa na kwamba tunapata namba hii tunapofanya hesabu kama utakavyoona hapa chini:
Kwa kutumia hesabu tulizopewa katika kuruani tunapata C=299792.5 km/sec
ambayo ni sahihi (accurate) kwa asilimia 100!!!!
namba zote hapa juu zilizotafutwa na wanasayansi ulimwenguni ni C-299792.5 kwani 2.45 ni sawa na 2.5
Kama tulivyofahamu kwamba vinavyohitajika katika kutafuta mbio za umeme ni vitu viwili umbali(distance) na wakati (Time)
Kwa kutumia Data katika kuruani utapata mbio hizi zilizotafutwa na wataalamu baada ya mahangaiko ya mda mrefu.
Wakati (Time) tumepewa katika kuruani kama alivyosema mwenyeezi mungu katika kuruani
Sura namba 32 aya namba 5
يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ ثُمَّ يَعۡرُجُ إِلَيۡهِ فِى يَوۡمٍ۬ كَانَ مِقۡدَارُهُ ۥۤ أَلۡفَ سَنَةٍ۬ مِّمَّا تَعُدُّونَ (٥)
Tafsiri Ya Aya Hii:
(Mwenyeezi Mungu) Anapitisha mambo yote yaliyo baina ya mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa siku moja tu ambayo kipimo chake ni miaka elfu mnayotumia nyinyi katika kuhesabu kwenu.
Mwenyeezi mungu anatupa wakati uliotumika nao ni miaka 1000 tunayoijua sisi nayo ni sawa na miezi 12000. (1000 miaka x 12 miezi ya mwaka=12000)
Katika Aya hii tunapata TIME nayo ni Miezi 12000 Na jambo la pili linalotakiwa katika kutafuta mbio za umeme ni Umbali (Distance)
Kuruani inatupa habari za Malaika ambao wanasafiri kwa muda wa miezi 12000 tunayoijua sisi na ambayo kwa mwenyeezi Mungu ni sawa na siku moja tu kwa time wanayosafiri hawa malaika. Kwa kifupi wanakwenda mbio sana.
Na wataalamu wa kiislamu walifanya mahesabu kutafuta mbio hizi wakazipata na ni muujiza pia kujua kwamba Malaika wameumbwa kwa “Mwanga” na pia wanakwenda mbio hizo hizo za Mwanga.
kama hadithi ya Mtume (Sala na Amani za Mwenyeezi Mungu zimfikie)iliyokusanywa na sahih Muslim inayosema:
وعن عائشة رضي الله عنها قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : “خلقت الملائكة من نور، وخلق الجان من مارج من نار، وخلق آدم مما وصف لكم” ((رواه مسلم)).
Tafsiri Ya Hadithi hii kwa lugha ya kiingereza:
Aisha reported: The Messenger of Allah, peace and blessings be upon him, said, “The angels were created from light, the jinn were created from a mixture of fire, and Adam was created as has been described for you.” Source: Ṣaḥīḥ Muslim Grade: Sahih (authentic) according to Muslim.
Maadamu tunajua Time wanayochukua Malaika katka safari hiyo basi tutafute Umbali (Distance) kisha tutafute Speed. (Distance = Distance/Time)
FORMULA YA KUTAFUTA MBIO ZA MWANGA (THE SPEED OF LIGHT)
C=12000 X 3682.07 km/h X 0.89157 X 655.71986 hrs Divide by 86164.0906 sec = 299792.5 km/sec.
Hapa Chini tunaelezea kwa kinaganaga kuhusu formula hii ili tuielewe vizuri:
-Namba 12000 Ni Miezi au TIME tuliyopewa katika kuruani sura namba 35 aya namba 5
-Namba 3682.07 km/hours Ni RELATIVE SPEED ya mwezi katika kuzunguka Ardhi Namba hii inatokana na formula ifuatayo:
“2 x Pi x R divide by T (Time)=3682.07 km/hours
-Namba 3682.07 km/h ni Radius ya mzunguko wa mwezi (Moon’s revolution) = 384264 km kugawa kwa Kipindi cha mzunguko wa mwezi (The period of the moons revolution) =655.71986 hours.
-Namba 0.89157 Ni Ratio ya COSINE “a” kutokana na Degrees 26.92848 ambazo zinapatikana baada ya kugawa siku za mwaka mmoja 365.25636 kwa kipindi cha mzunguko wa mwezi 27.32661 days Multiply na 360 Degrees
-Namba 655.71986 Hours Masaa ya kipindi cha mzunguko wa mwezi katika dunia Namba 86164.0906 Ni 1 day 23 hours 56 minutes and 4.0906 seconds ambayo ni sawa na 86164.0906 seconds. (sidereal system).
Kama tulivyoona Ukigawa Jawabu Utapata mbio za mwanga kwa kutumia habari tunazopewa katika Kuruani C=299792.5 km/sec
Je Unaona jawabu!!! Namba hii ndiyo iliyoshughulisha wanasayansi wakubwa ulimwenguni tangu karne na karne kuanzia Kipindi cha Galileo ambaye alizaliwa Mwaka 1564
Na namba hii inalingana na hesabu zilizofanywa na wana sayansi ulimwenguni. lakini jambo la kushangaza ni kwamba kuruani tangu iliposhuka kwa Mtume (Amani na Sala Zake Mola Zimfikie)
Hapo zamani karne ya Saba (baina na mwaka 600 na 700 wa kipindi cha Ukristo) inazungumzia utaalamu huu kwa hekima kubwa na baada yake wanavyuoni wetu waislamu Alhamdulilahi wametusaidia kutufahamisha habari hizi baada ya kufanya hesabu hizi.
Hapa chini kuna Video tatu zinaelezea Mbio za mwanga na pia kufafanua umuhimu wake.
Umuhimu wa Speed of Light umeelezwa katika Video hii.
Historia Ya wanasayansi walioanza majaribio mbalimbali ya kutafuta mbio za mwanga ulimwenguni
Nadharia inayojulikana ulimwenguni kama
Energy=Mass X Speed of Light Squared imeelezwa hapa kwa ufupi.
MBINGU INA MATABAKA SABA NA ARDHI INA MATABAKA SABA
MATABAKA SABA YA MBINGU NA ARDHI NA UTHIBITISHO WA KISAYANSI NA AYA ZA KURUANI TUKUFU
Wataalamu wanathibitisha kwamba Anga imegawanyika katika matabaka saba yafuatayo:
1-Troposphere
2-Tropopause
3-Stratosphere
4-Ozone Layer
5-Mesosphere
6-Ionosphere (Aurora)
7-Exosphere
Na ardhi pia imegawanyika katika matabaka saba:
1-Solid Core (Iron)
2-Liquid Core (Iron)
3-Inner Mantle
4-Outer Mantle
5-Asthenosphere
6-Lisosphere (Upper Most solid Mantle)
7-Lisosphere (Earth Crust)
Huenda mgawanyiko huu wa Anga unahusu Tabaka la Kwanza tu katika Matabaka 7 ya Mbingu. Kuruani ipo mbele ya Sayansi. Uhodari wa Binaadamu wote tumeishia katika Mbingu ya Kwanza ambayo kuna Jua na Mwezi na Nyota na Mengineyo tunayoyajua. Matabaka Mengine 6 hatuyajui bado. Hakuna aliyekwenda huko.
Kuna migawanyiko mingine mbalimbali na majina mbalimbali na pia kuna migawanyiko mingine midogo chini ya migawanyiko hii mikubwa
Kuruani inathibitisha kuumbwa kwa mbingu saba katika Aya saba zifuatazo kwani Mwenyeezi Mungu anasema kwamba kaumba matabaka ya mbingu saba na jambo lingine la kushangaza ni kwamba katika kuruani zimeshuka Aya saba tu ambazo zina maneno “mbingu saba” je huoni alama za kushangaza kwani Mwenyeezi Mungu ndiye aliyeumba na aliyeshusha Kuruani hii.
1-Chapter (2) sūrat l-baqarah (The Cow)
هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ لَكُم مَّا فِى ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعً۬ا ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَسَوَّٮٰهُنَّ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَىۡءٍ عَلِيمٌ۬
(٢٩) It is He who created for you all of that which is on the earth. Then He directed Himself to the heaven, [His being above all creation], and made them seven heavens, and He is Knowing of all things.
2-Chapter (17) sūrat l-isrā (The Night Journey)
تُسَبِّحُ لَهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتُ ٱلسَّبۡعُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَن فِيہِنَّۚ وَإِن مِّن شَىۡءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمۡدِهِۦ وَلَـٰكِن لَّا تَفۡقَهُونَ تَسۡبِيحَهُمۡۗ إِنَّهُ ۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورً۬ا (٤٤)
The seven heavens and the earth and whatever is in them exalt Him. And there is not a thing except that it exalts [Allah] by His praise, but you do not understand their [way of] exalting. Indeed, He is ever Forbearing and Forgiving.
3-Chapter
(23) sūrat l-mu’minūn (The Believers)
( قُلۡ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ ٱلسَّبۡعِ وَرَبُّ ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡعَظِيمِ (٨٦)
Say, “Who is Lord of the seven heavens and Lord of the Great Throne?”
4-Chapter (23)
sūrat l-mu’minūn (The Believers)
فَقَضَٮٰهُنَّ سَبۡعَ سَمَـٰوَاتٍ۬ فِى يَوۡمَيۡنِ وَأَوۡحَىٰ فِى كُلِّ سَمَآءٍ أَمۡرَهَاۚ وَزَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَـٰبِيحَ وَحِفۡظً۬اۚ ذَٲلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ (١٢ :
Say, “Who is Lord of the seven heavens and Lord of the Great Throne?”
5-Chapter
(65) sūrat l-ṭalāq (The Divorce)
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَہُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىۡءٍ عِلۡمَۢا (١٢)
It is Allah who has created seven heavens and of the earth, the like of them. [His] command descends among them so you may know that Allah is over all things competent and that Allah has encompassed all things in knowledge.
6-Chapter
(67) sūrat l-mulk (Dominion)
ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ طِبَاقً۬اۖ مَّا تَرَىٰ فِى خَلۡقِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ مِن تَفَـٰوُتٍ۬ۖ فَٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ هَلۡ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ۬ (٣)
Who hath created seven heavens in harmony. Thou (Muhammad) canst see no fault in the Beneficent One’s creation; then look again: Canst thou see any rifts?
7-Chapter (71) sūrat nūḥ
أَلَمۡ تَرَوۡاْ كَيۡفَ خَلَقَ ٱللَّهُ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ طِبَاقً۬ا (١٥)
Indeed, We sent Noah to his people, [saying], “Warn your people before there comes to them a painful punishment.”
Na Aya inayothibistisha kwamba ardhi ina matabaka saba ni hii ifuatayo:
At-Talak 65 Aya Namba 12
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَہُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىۡءٍ عِلۡمَۢا (١٢)
Allah is He Who created seven Firmaments and of the earth a similar number. Through the midst of them (all) descends His Command: that ye may know that Allah has power over all things, and that Allah comprehends, all things in (His) Knowledge.
Yote haya yanatuzidishia imani kwamba kuruani ni kitabu chenye utukufu mkubwa sana. Allahu Akbar, Allahu Akbar.
MATABAKA SABA YA HEWA


MATABAKA SABA YA ARDHI
SAFARI ZA ANGA HAZIKUWAPO WAKATI HUO JE MTUME ALIJUA VIPI?
Tabaka hizi saba (tulizitaja hapa juu ) za anga zinatusaidia katika tafsiri ya aya ifuatayo:
لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ۬
Kisayansi Tafsiri itakuwa: “Mtasafiri Angani Kupitia Tabaka Baada Ya Tabaka”
Je Huoni Muujiza Mwingine Wa safari Za Angani. Leo Hii Watu Wamekwisha Kwenda Mpaka Katika Mwezi. Mwenyeezi Mungu anathibitisha hapa kwa kutumia Herufi Ya Lam na Nun ya Kithibitisho kwamba itakuwa hivyo Bila ya Shaka Yeyote. (“LATARKABUNNA” – لَتَرۡكَبُنَّ )
kuruani ni muujiza mkubwa sana na maneno yake ni ukweli mtupu na ya hali ya juu sana tena sana.
JUA NA MWEZI
Jua linatoa Nishati (Energy) kubwa kutoka katikati yake kwa njia ya kuathiriana baina ya Atoms za Hydrogen na hatimaye kuzalisha Element Nyingineyo inayojulikana kama Helium (Inajulikana kama Nuclear Fusion).Kwa hiyo Wataalamu wamekubaliana kwamba Jua lina hewa ya Hydrogen na Helium na hizi Element mbili ni katika aina za Elements zilizo nyepesi sana. Na Nishati (Energy) Ya Jua ndiyo huu mwanga wa Jua tunaopata Mchana wakati Jua linapon’gara.
Mwezi haitoi Nishati (Energy) Yeyote kwani hakuna Hydrogen inayosababisha Nishati ya Kuzalisha Helium. Na aina ya Elements zilizopo katika Mwezi ni Oxygen (60%), Silicon (16-17%), Aluminium (6-10%), Calsium (4-6%), Magnesium (3-6%), Iron (2-3%), Titanium (1-2%) na nyinginezo ambazo viwango vyake ni vidogo sana chini ya asilimia 1 (1%). Na hii ndiyo sababu Jua Lina Mwanga wake bali Mwezi hautoi mwanga wake bali ni Nuru ya Jua. Kun’gara kwa Mwezi ni sababu ya Jua. Yaani Mwanga wa jua unapiga Mwezi na kisha Mwezi unatumurika.
Historia ya Harakati za Jua katika kuzalisha Nishati ziligunduliwa katika mwanzoni mwa karne ya 21 yaani kuanzia mwaka 1920 ambapo Mtaalamu wa Astrophsics wa Kiingereza aliyejulikana kwa Jina kama “Arthur Eddington” aliyetangaza kwamba Nyota zinapata Nishati (Energy) kutokana na atoms za Hydrogen zinapoathiriana katika kuzalisha atom za Helium. Nadharia yake ilichapishwa katika “Internal Constitution of Stars”mwaka 1926 na ikawa msingi wa “Nadharia za kisasa katika elimu ya astrophysics” miaka iliyofuatia wataalamu wengine kama vile Robert d’Escourt Atkinson and Fritz Houtermans wakaendelea kufanya utafiti na kuweza kutupatia vipimo vya Nishati (Energy). Na Mtaalamu mwingine anayejulikana kama Ernest Rutherford akafanya utafiti wake katika mwaka 1934 na pia Mwanafunzi wake Mark Oliphant. Mtaalamu mwingine Hans Bethe akatoa mwanga zaidi kuhusu Nishati (Energy) katika maandishi yake yanayojulikana kama “stellar nucleosynthesis” alipoelezea kwamba kwa njia ya kuathiriana kwa proton-proton ndiyo Jua na Nyota zinatoa Nguvu ya Nishati (Energy).
MUUJIZA KATIKA KURUANI
Kama tulivyoona historia fupi ya Nguvu za Jua wataalamu kwa mara ya kwanza kushughulikia jambo hili ni mwaka 1920 yaani kabla ya hapo wataalamu hawakujua habari hizi wala Elimu hii. Sasa utashangaa kwani kuruani imeelezea suala hili katijka Aya moja tu (yenye maneno 11)kwa njia rahisi. Na wala siyo vitabu na vitabu au baada ya utafiti mrefu kama tulivyoona hapa juu. Mwenyeezi Mungu hahitaji hayo kwani yeye ndiye aliyeumba Jua, Nyota na kila kitu.
Mwenyeezi Mungu anasema katika Sura ya Furkan namba 25 aya namba 61
تَبَارَكَ ٱلَّذِى جَعَلَ فِى ٱلسَّمَآءِ بُرُوجً۬ا وَجَعَلَ فِيہَا سِرَٲجً۬ا وَقَمَرً۬ا مُّنِيرً۬ا (٦١)
Tafsiri Ya Aya kiswahili
Ni Mwenye Baraka yule aliyezijaalia (mikusanyiko ya) nyota (mbinguni), na akajaalia humo jua (lenye kutoa mwanga) na mwezi (unaong’ara)
Tafsiri Ya Aya Kiingereza
Blessed is He who has placed in the sky great stars and placed therein a [burning] lamp and luminous moon.
Aya Moja tu imetosha kutupa Elimu yote iliyofanyiwa utafiti mbalimbali na maandishi mbalimbali ulimwenguni. Aya inatuambia kwamba Jua linatoa mwanga wake lakini Mwezi unan’gara kutokana na Jua. Kwa kutanua zaidi tutafasiri kama ifuatavyo “Mwenyeezi Mungu Mwenye Baraka amejaalia katika anga Mikusanyiko ya Nyota na akajaalia Jua letu ambalo linatupa Mwanga na pia Mwezi ambao unatoa Nuru kutokana na Mwanga wa Jua”
Hii inathibitisha kwamba Kuruani ni maneno yake Mwenyeezi Mungu na siyo ya kibinaadamu. Mtume Mohamed (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) ametufikishia Ujumbe kama alivyopokea. Je huoni Sayansi ya hali ya Juu iliyotajwa katika Karne ya 7 bila ya babaisho lolote lile wala kubuni. Allahu Akbar, Allahu Akbar.
JOTO LA JUA KWA KIPIMO CHA KELVIN NI 5778 NA KIPIMO HIKI KIPO KATIKA KURUANI TUKUFU
KIPIMO CHA JOTO LA JUA
Maajabu Ya Kuruani hayana Mwisho. Maajabu Juu Ya Maajabu. Hii inathibitisha kwamba yuleyule aliyeumba ulimwengu/malimwengu basi ni yule yule aliyeshusha Kuruani hii kwa Mtume Mohamed (Amani na Sala za Mwenyeezi Mungu zimfikie)
Mara ya Kwanza kutajika Neno شَّمۡسِ au JUA katika Kuruani ni katika Sura Ya Bakarah namba 2 Aya Namba 258 na Mara ya Mwisho Kutajika Neno شَّمۡسِ au JUA katika Kuruani Tukufu ni Katika Sura Ya Ashams namba 91 Aya Namba 1. Na ajabu isiypo ya mwisho ni hesabu ya Aya baina Aya hizi mbili ni jumla ya Aya 5778 na namba hii ni kipimo cha joto la JUA. Huu ni muashirio wa Kiajabu. Yaani Sayansi ya leo inagundua Joto hili kwa kutumia vyombo mbalimbali vya kisasa kama vile kwa kutumia chombo kinachojulikana kama spectroscopy kwa kuchambua mwanga na rangi(The sun’s temperature is measured by “spectroscopy” which refers to the analysis of light and color. The color of the light emitted from hot objects (also called “black bodies” in science) corresponds to certain temperatures. Astronomers can use spectroscopy to know the temperature of just about any clearly visible star). Ukitafuta katika Vitabu vya kisayansi au Mtandao kwa kutumia vyombo vya utafiti kama vile Google utapata Joto la Jua (Temperature of The Sun) ni KELVIN 5778. Sasa angalia muashirio huu wa kiajabu. Mbona namba hii ni idadi ya Aya zilizopo baina Ya Jua mara ya kwanza kutajwa katika kuruani na Mara ya mwisho kutajwa katika kuruani. Je Ndugu Binaadamu Mwenzangu hushangai Haya? je Huoni Ukweli wa Kuruani kwamba ni yake Mwenyeezi Mungu? Je Huogopi? Tumeona mara kwa mara kila tukihesabu katika Kuruani tunapata mlinganisho wa hali ya Juu na sio mara Moja bali mara chungu nzima. Je bado hatuamini Ujumbe uliokuja? Yaani Kuruani Tukufu? Mtume alijua vipi kipimo kama hiki ambacho hakikuwako enzi hizo za karne ya 7 huko Arabuni. Hiki ni kipimo cha kisasa. Mtume alisoma wapi? Huu Ni Muujiza ulio wazi kwsa kila Mtu.
Sura Ya Albakarah Namba 2 Aya Namba 258
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِى حَآجَّ إِبۡرَٲهِـۧمَ فِى رَبِّهِۦۤ أَنۡ ءَاتَٮٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ إِذۡ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ رَبِّىَ ٱلَّذِى يُحۡىِۦ وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا۟ أُحۡىِۦ وَأُمِيتُۖ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَأۡتِى بِٱلشَّمۡسِ مِنَ ٱلۡمَشۡرِقِ فَأۡتِ بِہَا مِنَ ٱلۡمَغۡرِبِ فَبُهِتَ ٱلَّذِى كَفَرَۗ وَٱللَّهُ لَا يَہۡدِى ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٢٥٨)
Tafsiri Ya Aya
Hukumsikia yule aliyehojiana na Ibrahimu juu ya Mola wake kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? lbrahimu aliposema: “Mola wanguni yule ambaye huhuisha na hufisha,” yeye akasema:”Mimi pia nahuisha na kufisha.” lbrahimu akasema: “Mwenyezi Mungu hulichomozesha JUA mashariki,basi wewe lichomozeshe magharibi.”Akafedheheka yule aliyekufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.
Sura Ya Ashams Namba 91 Aya Namba 1
وَٱلشَّمۡسِ وَضُحَٮٰهَا (١)
Tafsiri Ya Aya
Naapa kwa JUA na kwa muangaza wake
MBIO ZA MWANGA WA RADI KUTOKA ANGANI NA KURUDI KWAKE TENA ANGANI. SAYANSI HII YA KISASA INAKUBALIANA NA HADITHI YA MTUME MOHAMED (AMANI NA SALA ZA MOLA ZIMFIKIE).I
Hadithi Ya Mtume Inayohusiana na Siku ya Malipo au siku ya kiyama kutoka katika kitabu cha Muslim.
وعن حذيفة، وأبي هريرة، رضي الله عنهما ، قالا: قال رسول الله، صلى الله عليه وسلم: ”يجمع الله، تبارك وتعالى الناس، فيقوم المؤمنون حتى تزلف لهم الجنة، فيأتون آدم، صلوات الله عليه، فيقولون: يا أبانا استفتح لنا الجنة، فيقول: وهل أخرجكم من الجنة إلا خطيئة أبيكم ! لست بصاحب ذلك، اذهبوا إلى ابني إبراهيم خليل الله، قال: فيأتون إبراهيم، فيقول إبراهيم: لست بصاحب ذلك ، اذهبوا إلى موسى الذي كلمه الله تكليمًا، فيأتون موسى، فيقول: لست بصاحب ذلك؛ اذهبوا إلى عيسى كلمة الله وروحه. فيقول عيسى: لست بصاحب ذلك. فيأتون محمدًا صلى الله عليه وسلم، فيقوم فيؤذن له، وترسل الأمانة والرحم فتقومان جنبتي الصراط يمينًا وشمالاً، فيمر أولكم كبالبرق” قلت: بأبي وأمي، أي شيء كمر البرق؟ قال: “ألم تروا كيف يمر ويرجع في طرفة عين؟ ثم كمر الريح، ثم كمر الطير، وأشد الرجال تجري بهم أعمالهم، ونبيكم قائم على الصراط يقول:” رب سلم سلم، حتى تعدز أعمال العباد، حتى يجيء الرجل لا يستطيع السير إلا زحفاً، وفي حافتي الصراط كلاليب معلقة مأمورة بأخذ من أمرت به، فمخدوش ناج، ومكردس في النار” والذي نفس أبي هريرة بيده إن قعر جهنم لسبعون خريفًا. ((رواه مسلم)).
TAFSIRI
(Ili ipate kueleweka na kurahisisha kwa wasomaji nimetumia maneno yangu na wakati mwingine nimeongeza na kupunguza lakini maana ni ile ile sikubadili) Na Mwenye kujua Kiarabu basi aisome Hadithi hii hapa Juu ambayo ipo katika Sahih Muslim au Kw Lugha ya Kiingereza hapa chini.
(Hadithi) Kutokana na Hudhaifah na Abu Hurairah, Mungu awape radhi wote wawili, walisema: Mjumbe (Mtume) wa Mungu, sala za Mungu na amani zimshukie, alisema: “Mwenyeezi Mungu, Aliyetukuka, atakusanya watu siku ya Kiyama na Waumini watakuwa katika hali ya kusubiri mpaka Pepo itakaposogezwa, na waumini watamjia Adam, (baraka za Mungu ziwe juu yake), na watasema Ewe baba yetu, tuombee ili Pepo ifunguliwe, naye atasema: Je! hamkumbuki kwamba nilikufukuzeni Peponi? (Yalitokea hayo) kwa ajili ya dhambi ya baba zenu! Nendeni kwa Musa, ambaye Mweneyeezi Mungu alizungumza naye kwa ukamilifu, na watakapokwenda kwa Musa, naye atawajibu: “Sina uwezo huo, nendeni kwa Nabii Isa” ambaye ni neno (Aliyeumbwa kwa neno “kuwa” na ikawa) na roho (Aliyopuliziwa)kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Yesu atasema: “Mimi sina uwezo huo”. Kwa hivyo watakuja kwa Mtume Muhammad, (Mungu ambariki na ampe amani), Atawaombea kwa Mola na Milango ya Pepo Itafunguliwa. Amana na Rehema Zitaletwa na Kupangwa pande zote mbili za njia ya Kwenda Peponi. (Chini ya Njia Hiyo kutakuwa na Moto wa Jahannam) Kundi la kwanza litapita kwa haraka kwa mbio za Umeme. “Nikasema:” (Abu Hurayra Akamwuliza Mtume) Kwa Jina la baba na mama yangu, Huo mwanga wa umeme (au Mfano wa Umeme) ni kitu gani? “Akasema:” Je! huoni jinsi mwanga wa umeme unavyokuja na kurudi angani kwa muda mfupi sawa na kupepesa kwa macho? (Mtume akaendelea kuwahadithia Maswahaba kwa kusema) “Kisha kundi lingine (la pili) litapita kwa mbio kama upepo , kisha kundi lingine (la tatu) litapita kwa mbio za njiwa, Na Kundi lingine (la nne)litapita kama mbio za binaadamu (za kawaida), na mbio hizo zitategemea vitendo vyao .(Na katika wakati huo Mtume atakuwa karibu na Daraja Hilo huku akiwaombea Mungu akisema “Ewe Mola waruzuku amani, waruzuku amani, Na hivyo hivyo itaendelea mpaka kundi jingine litapita kwa kusota kwa matumbo kwa mbio ndogo sana. (kufuatana na vitendo vyao duniani ). (Kundi hili ni la wenye thawabu zisizo nyingi). Katika Pande zote mbili za Daraja kutakuwa na Kulabu (Hooks) ambazo zitawavuta motoni waliodharau Ujumbe wa Mtume. Kuna Wengine ambao wataangukia katika moto wa Jahannam. Abu Hurayra Akaongeza kwa kusema “Naapa kwa Yule ambaye anayeimiliki Roho yangu (Abu Hurayra)kwamba shimo la Jahannam ni refu sana kiasi cha urefu wake ni sawa na safari ya Miaka Sabini. (Hadithi Katika kitabu Cha Muslim)
English Translation
Hudhaifah and Abu Hurairah (May Allah be pleased with them) reported that they heard Messenger of Allah (ﷺ) saying, “Allah will assemble mankind, and the believers will stand till Jannah will be brought near them. They will then go to Adam (ﷺ) and say, `O our father, ask (Allah (SWT), that Jannah may be opened for us, but he will reply: `There was nothing that put you out of Jannah except your father’s sin. I am not the one to do that, go to my son Ibrahim (Abraham), the beloved man of Allah.’ Then Ibrahim (ﷺ) when approached, will say: `I am not the one to do that, for I was only a friend; and that is not a lofty status but ask Musa (Moses) to whom Allah spoke.’ They will then go to Musa (ﷺ) but he will say: `I am not the one to do that; go to `Isa (Jesus), Allah’s Word and spirit.’ `Isa (ﷺ) will say: `I am not the one to do that.’ So they will come to me; and I will stand and be given permission. Amanah and ties of relationship will be sent forth and will stand on the sides of the Sirat (that is, the Bridge set over Hell-fire) right and left, and the first of you will pass like lightning.” I said (that is Abu Hurairah (May Allah be pleased with him)” :I ransom you with my father and mother, what is like the movement of lightning?” The Messenger of Allah replied, “Have you not seen how the lightning goes and returns in the twinkling of an eye? Next (group will pass) like the passing of the breeze, next like the passing of a bird, and the next with the speed of a running man, according to the quality of their deeds. (During all this time) your Prophet (ﷺ) will remain standing on the Bridge saying: `O my Rubb, keep (them) safe, keep (them) safe,’ till men’s deeds are so weak that a man comes who will be able only to crawl. On both sides of the Bridge pronged flesh hooks, placed under command will be hung and will seize those about whom they receive command, some people being lacerated and escaping and others being thrown violently into Hell.” Abu Hurairah added: By Him in Whose Hand Abu Hurairah’s soul is, the pit of Jahannam (Hell) is seventy years in depth. [Muslim].
SHEREHE YA HADITHI KISAYANSI
Katika Hadithi hii tunafahamishwa kuwa kuna siku Mtume (Sala na Amani Zale Mola zimfikie)alikuwa akiwafundisha Maswahaba kuhusu Malipo Siku ya Kiyama. Kutakuwa na Daraja ambalo watapita Watu kuelekea katika Pepo. Kufuatana na Hadithi hii, Mtume Mohamed ndiye atakayewaombea kwa Mola awaruhusu watu waingie peponi. Mtume akasema kwamba waliotenda Mazuri sana wataingia Peponi kwa kupitia Daraja Hilo kwa haraka kama mwanga wa Radi. Kabla ya mtume kuendelea na Mawaidha hayo Abu Hurayra akamwuliza Swali kuhusiana na Huo Mwanga wa Radi. Akamwuuliza Mtume Kuhusu Mbio Ya Mwanga Huo ni kama nini? Mtume Akamjibu kwamba “Je hujaona Mwanga wa Radi unapokuja na Kurudi (Angani) kwa haraka kwa muda wa kipimo cha kupepesa macho?” Katika Hadithi hii ningependelea kufafanua Habari za Mwanga wa Radi. Jibu alilotoa Mtume ni Jibu la Ajabu sana kwani Sayansi inayohusiana na Mwanga wa Radi imechukua Muda Mrefu kusomwa na Wataalamu wamepoteza karne zaidi ya moja yaani kuanzia karne ya 17 mpaka hivi karibuni wametumia Viombo mbalimbali kutuma Angani ili kusomea asili ya mwanga wa Radi. Kwani Radi ina hatari zake pia na Elimu hiyo ina umuhimu sana.
Ijapokuwa watu wanachukulia siyo muhimu lakini katika uwanja wa Sayansi hakuna dogo. Wamepoteza pesa na wakati kwa muda mrefu ili kujua Ni Nini Mwanga Wa Radi. Wanasayansi wamegundua kwamba Chini ya Mawingu kuna Negative Charge na Juu Ya Mawingu kuna Positive Charges.
Wataalamu wanasema haya kama hapa chini
(Small negatively charged particles called electrons are knocked off some ice and added to other ice as they crash past each other. This separates the positive (+) and negative (-) charges of the cloud. The top of the cloud becomes positively charged while the base of the cloud becomes negatively charged.ive Charge)
Na kwa Vile latika Ardhi kuna Positive Charge na Sayansi inatuambia kwamba Positive na Negative Charges zinavutana na Positive na Positive au Negative na Negative zinatengana.
Wataalamu wanasema pia haya kama hapa chini
(Like charges repel each other; unlike charges attract. Thus, two negative charges repel one another, while a positive charge attracts a negative charge)
Kwa hiyo Negative Charges za mawingu zitavutana na Positive Charges za Ardhi. Na zinapokaribiana na Kugusana husababisha Mpasuko wa mwanga na kuurudisha Mwanga Huo Angani Na kwa hiyo Mwanga wa Radi huja na kurudi angani.
Na muujiza mkubwa kwani Mtume alimjibu Abu Hurayra kuhusu Mwanga wa Radi kwamba ni “Mwanga ambao unakuja na kurudi angani kwa muda mfupi sana kwa kipimo cha kupepesa Macho”
Ijapokuwa Jawabu la Mtume halikuwa kumfundisha Abu Hurayra Sayansi Ya Radi au Mwanga wa Radi lakini ilikuwa Kumjibu Swali alilouliza lenye kuhusiana na watu wazuri watakaoingia peoponi kwa kutembea Juu ya Daraja litakalokuwa Juu ya Moto wa Jahnaam na Speed au Mbio za kila Kikundi watakazotumia kuingia Peponi kufuatana na Vitendo vyao duniani Yaani wale waliokuwa wamefanya mazuri sana duniani watatembea na kuingia peoponi kwa haraka kama Mwanga wa Radi na kwa muda ambao unafanana na Mpepeso wa Macho.
Muujiza Mkubwa wa kushangaza. Sasa Mtume alisoma wapi. Wakati wa hapo zamani Wagiriki waliamini kwamba Mwanga wa Radi ni Kiboko cha mungu wao waliomwabudu aliyejulikana kwa jina la ZEUS kama tunavyosoma hapa chini
(Zeus is the god of the sky in ancient Greek mythology. As the chief Greek deity, Zeus is considered the ruler, protector, and father of all gods and humans. Zeus is often depicted as an older man with a beard and is represented by symbols such as the lightning bolt and the eagle).
Wagiriki na pia kuna baadhi ya Mataifa mengineyo waliamini hivyo. Sasa Mtume alisoma wapi Sayansi ya hali ya juu kama hii wakati ambao kulikuwa hakuna aliyeyajua haya. Alikopi kwa nani. Wagiriki na wengineo walikuwa hawajui habari za asili ya Mwanga wa radi.
Wako Wengi wajinga ambao wanadanganywa kwamba Mtume alichukua elimu za hapo zamani kisha akaandika Kuruani. Huu ni uongo mtupu. Ukielewa vizuri habari hizi utaona ukweli kwamba Mtume aliyoyasema katika hadithi hii alikuwa Anasahihisha Itikadi za hapo kale.zisizo na msingi.
Mtume katika hadithi hii alikuwa akiwafundisha Maswahaba kuhusu Malipo ya Makundi ya watu mablimbali siku ya Kiyama au siku ya Mwisho. Lakini Muujiza Mungine unajitokeza leo kuhusu Elimu Ya Mwanga kama aliyodokeza katika Mazungumzo yake na Abu Hurayra.
Tukitazama Mwanga wa Radi hatuoni kuja na kurudi kwani ni haraka sana sasa Mtume aliona vipi? hii inathibitisha kwamba ilikuwa Wahyi na siyo yeye ndiye aliyezua.
Wanasayansi walianza kusomea habari hizi kuanzia karne ya 17 lakini hawakupata Jawabu kuhusiana na Mwanga Huu mpaka hivi karibuni baada ya kuja kwa Digital Camera ambazo kuna zile ambazo zinaweza kupiga picha kwa haraka kwa idadi picha elfu kwa kila sekunde moja.
Na Maajabu ni kwamba hata lugha za Wanasayansi wa NASA wanatumia maneno yale yale ya Mtume. Mwana Sayansi anayejulikana kwa jina Steve Goodman anasema yafuatayo
“A lighting strike can heat the air in a fraction of a second. When air is heated that quickly, it expands violently and then contraccts, mlike an explosion that happens IN A BLINK OF AN EYE”
Je unaona Maneno haya niliyoyapigia mstari IN A BLINK OF AN EYE” haya ni sawa sawa na maneno aliyotaja katika hadithi ya Mtume. ويرجع في طرفة عين (Mwanga Kurudi kwa Muda wa Kupepesa Macho) sasa unaona Muujiza wa kushangaza. Na maneno kama haya ndiyo yanayotuzidishia Imani kwamba Mtume ni wa haki na Mungu yupo. Allahu Akbar.
Wana Sayansi wanasema kwamba katika kila sekunde moja kunakuja Mianga ya Radi karibu Mia Moja inayokuja ardhini na katika siku nzima kunakuja Mianga karibu 8.000.000 ya Radi. Na haya tunayoambiwa ni Neema kubwa miongoni mwa Neema zake Mwenyeezi Mungu kwani Ardhi tunayoishi ime zungukwa na Umeme unapotokana na CHUMA katikati ya Ardhi na Mianga ya Radi inasaidia katika kusawazisha Umeme huu uliotuzunguka.
Kuna aina mbalimbali za Mianga ya Radi. Tutataja hapa baadhi tu ya aina hizo:
1-Mawingu kwa Ardhi-Cloud-to-ground lightning
2-Ndani Ya Wingu Moja-Intra-cloud lightning
3-Baina Ya Mawingu na Mawingu-Inter-cloud lightning.
4-Na kuna aina nyinginezo kama wanasayansi wanataja kama zifuatazo:
(OTHER TYPES OF LIGHTNING-There are numerous names and descriptions of various types and forms of lightning. Some identify subcategories and others may arise from optical illusions, appearances, or myths. Some popular terms include: ball lightning, heat lightning, bead lightning, sheet lightning, silent lightning, black lightning, ribbon lightning, colored lightning, tubular lightning, meandering lightning, cloud-to-air lightning, stratospheric lightning, red sprites, blue jets, and elves)
Muda wa Kupepesa macho pia ni mdogo sana na wanasayansi wa elimu ya Physics wantuambia kuhusu Muda wa kupepesa Macho kwamba;
(On average the human blink lasts only a tenth of a second which is 100 milliseconds. it can even last up to 400 milliseconds. To put it into perspective, the tick of a clock lasts 1 second, making it possible to blink 3 times during a single tick of a clock)
Muda huu wa kupepesa macho ndio ule ule muda unaochukua ule mwanga wa Radi unapokuja na kurudi. Kipimo hiki kinakubaliana na Hesabu za Physics (Physics Calculations).
Angalia Picha za Mwanga wa Radi hapa Chini. Kwa kweli inashangaza. Allahu Akbar.
Mtume alijua vipi kipimo hiki ambacho hata leo hii siyo rahisi kupima.
Wataalamu wametumia pia maneno yenye kulenga hadithi ya Mtume hali kwamba hawajasoma hadithi hii. Neno “Return” katika Ibara waliyotumia “Return Stroke” lina maana ya ويرجع au Kurudi (kwa ule Mwanga Angani).
Ama kweli Kuruani ni kitabu cha haki, na Mtume (Sala na Amani Zimfikie) ni wa Haki. Haya yote yanathibitisha kwamba Dini ya Kiislamu ni Ya kweli. Allahu Akbar. Allahu Akbar.


Picha Ya Kwanza inaonyesha Mwanga wa Radi unapotoka Mawinguni au Angani. Na Picha Ya Pili Inaonyesha Mwanga wa Radi Kutoka Ardhini na Kupanda juu
Angalia hapa chini Video ineyoelezea Mwanga Wa Radi au Umeme. Wanasayansi Wamepoteza Karne na Karne Kuusoma Na Mtume alisema kuhusu Habari hizi kuanzia Karne ya Saba Kabla Ya Sayansi yaani karibu baada ya miaka Elfu Moja.Allahu Akbar