UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
5. Jun, 2022
MAUMBILE YA BINAADAMU

Katika Sura ya Al-Muuminun Aya namba 12 mpaka namba 14 Mwenyeezi Mungu anatuelimisha Namna alivyotuumba katika hatua au Steps 7 zifuatazo:
وَ لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ سُلَالَةٍ مِنْ طِينٍ 1
* ثُمَّ جَعَلْنَاهُ نُطْفَةً 2
فَخَلَقْنَا
الْعَلَقَةَ
عَلَقَةً 3
فِي قَرَارٍ مَكِينٍ * ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ
مُضْغَةً 4 فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَامًا 5 فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْمًا 6 ثُمَّ أَنْشَأْنَاهُ خَلْقًا آخَرَ 7 فَتَبَارَكَ اللَّهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ
[المؤمنون: 12 – 14].
Pili=Manii
Kwanza= ni Udongo
Tatu=Kipande cha Nyama kidogo Kinachoninginia katika tumbo la uzazi
Nne=Kipande cha Nyama kilichokuwa Kidogo na ni mfano wa Chewing Gum iliyotafunwa
Tano=Vifupa vya Mwanzo kuanza kuota
Sita=Nyama (flesh) inayokuja kuvisha Mifupa hiyo
Saba=Kuzaliwa kwa Mtoto aliyekamilika
Hizi ndizo Stage au Step (Hatua) zinazofanyika katika Tumbo la kizazi (Tumbo la Mama).
Jambo la kushangaza ni Kwamba Ibara “Kuumbwa Kwa Binaadamu” pia imekariri katika Kuruani Tukufu mara 7 peke yake katika Aya zifuatazo.
1. { يُرِيدُ اللَّهُ أَنْ يُخَفِّفَ عَنْكُمْ وَ خُلِقَ الْإِنْسَانُ
ضَعِيفًا } [النساء: 28].
2. { خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ نُطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُبِينٌ } [النحل: 4].
3. { خُلِقَ الْإِنْسَانُ مِنْ عَجَلٍ سَأُرِيكُمْ آيَاتِي فَلَا تَسْتَعْجِلُونِ } [الأنبياء: 37].
4. { الَّذِي أَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ وَ بَدَأَ خَلْقَ الْإِنْسَانِ مِنْ طِينٍ } [السجدة: 7].
5. { خَلَقَ الْإِنْسَانَ } [الرحمن: 3].
6. { خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ صَلْصَالٍ كَالْفَخَّارِ } [الرحمن: 14].
7. { خَلَقَ الْإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ } [العلق: 2].
Na Ibara Nabii Adam ambaye alikuwa binaadamu wa Kwanza kuumbwa limekariri mara 7 tu katika Kuruani yote katika Aya zifuatazo:
1. { يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنْزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَ رِيشًا } [الأعراف: 26].
2. { يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُمْ مِنَ الْجَنَّةِ } [الأعراف: 27].
4. { يَا بَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِنْكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ آيَاتِي } [الأعراف: 35].
3. { يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِنْدَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَ كُلُوا وَ اشْرَبُوا وَ لَا تُسْرِفُوا } [الأعراف: 31].
5. { وَ إِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِنْ بَنِي آدَمَ مِنْ ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَ أَشْهَدَهُمْ عَلَى أَنْفُسِهِمْ } [الأعراف: 172].
6. { وَ لَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَ حَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَ الْبَحْرِ } [الإسراء: 70].
7. { أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَا بَنِي آدَمَ أَنْ لَا تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُبِينٌ } [يس: 60].
Kukariri kwa Ibara “Kuumbwa kwa binaadamu” na ibara “Nabii Adam” kunathibitisha kwamba Mwenyeezi Mungu ndiye aliyeumba kila kitu na Binaadamu wa kwanza alikuwa Nabii Adam.
Kwa Utafiti huu Nadharia zote nyinginezo kama vile Nadharia ya Darwin na Nyinginezo zinaanguka.
Nadharia hizo zinadai kwamba viumbe havikuumbwa bali vilizuka na kukua kufuatana na mazingara.
Kwa hiyo Kukariri mara 7 kwa ibara hizi tulizoziona katika Kuruani Tukufu kunathibitisha Stages au Hatua Saba za Maumbile ya Binaadamu. Allahu Akbar.
Hakuna Kitabu Duniani ambacho kimeelezea kwa njia rahisi na ya uwazi kwa hali ya juu mfano wa kuruani.
Allahu Akbar.
Madakitari wakubwa duniani ambao wameonyeshwa Aya hizi zinazozungumzia Stages au Hatua za Maumbile pia wameshangaa sana. Na katika Madakitari hao Mmojawapo ni Keith Moore ambaye baada ya Utafiti wake kuhusu Aya hizi ilimbidi Aandike kitabu na akaongeza Katika kitabu hicho kwamba amesoma habari hizi kutoka katika Kuruani Tukufu. Unaweza kumsikiliza Hotuba yake katika Video ambayo nimeiweka katika website hii.
UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
5. Jun, 2022
ARDHI NA MATABAKA YAKE.

Ardhi ina Matabaka 7 na Tabaka la mwisho kuanzia Gamba la Ardhi kwenda chini ya Ardhi ni la Chuma. Kuruani imeashiria Kuweko kwa Chuma katikati ya Ardhi kwa kujaalia Sura Ya Chuma; Alhadiiyd. Mwenyeezi Mungu anasema katika Kuruani Tukufu: Sura Ya Tallaqa Aya Namba 12;
{ اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَ مِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَ أَنَّ اللَّهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا } [الطلاق: 12].
Kwamba Ameumba mbingu saba na Ardhi pia amefanya hivyo hivyo. Sayansi za kisasa zimethibitisha Ukweli huu. Angalia Picha niliyeiambatanisha hapa kwa majina ya Matabaka ya Ardhi.
Na la kushangaza zaidi ni Hesabu kuanzia Aya ya Kwanza ya Sura ya Al-Fatiha mpaka katika sura ya Al-Hadiyd Aya inayozungumzia Chuma yaani Aya namba 25 utapata Jumla ya Aya ni 5100.
Ukiangalia Picha hapa juu utaona Muujiza wa Umbali kuanzia Gamba la Ardhi mpaka katika Chuma iliyopo katikati ya Ardhi ni Kilometer 5100. Yaani Sura Ya Chuma ipo katikati sawa na chuma katika Ardhi kisha Umbali ni sawa sawa na idadi ya Aya za kuruani kuanzia mwanzo mpaka katika Aya ya Chuma. Allahu Akbar. Unaona Muujiza?
UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
5. Jun, 2022
ATOM YA CHUMA NA AYA ZA KURUANI TUKUFU


Aina Ya Chuma (isotope) 55.85 na pia kuna 56, 57, 58 na 59
Kuruani imekusanya Jumla ya Sura 114 na Sura ya katikati inaitwa Al-HADIYD yaani Chuma. Mpangilio huu siyo bure bure bali kuna Hekima kubwa. Mwenyeezi Mungu ameiumba Ardhi na kujaalia Chuma iwe katikatikati na hivyo hivyo amejaalia Kuruani iwe mfano huo na akajaalia Sura Ya Al-Hadiyd kuwa Katikati ya Msahafu. Sura ya Al-Hadiyd ni ya 57 katika Sura za Kuruani ambazo ni 114. Aya za Chuma katika Kuruani zinatufunulia Miashirio mbalimbali ambayo ina uhusiano na Elimu ya Chuma.
Kuna Aya Sita katika Kuruani ambazo zimetumia Herufi za lugha ya kiarabu 26 katika Jumla ya herufi 28. Katika Herufi zote 28 za Lugha ya Kiarabu ni herufi mbili tu ambazo hazikutumika nazo ni Herufi TWA na TA lakini zilizobaki zote 26 zimetumika katika Aya hizi sita zenye kuzungumzia Chuma. Jambo la kushangaza ni kwamba Chuma katika Ardhi ipo katikatiki. Matumizi ya herufi 26 katika kujenga Aya Sita zinazohusu Chuma na ambazo ni za pekee katika kuruani yote ni sawa na Alivyoumba ATOM ya chuma na kujaalia Protons na Electrons 26.
1. { قل كونوا حجاره او حديدا } [الإسراء: 50].
2. { اتوني زبر الحديد حتي اذا ساوي بين الصدفين قال انفخوا } [الكهف: 96].
3. { و لهم مقمع من حديد } [الحج: 21].
4. { و لقد اتينا داود منا فضلا يجبال اوبي معه و الطير و النا له الحديد } [سبأ: 10].
5. { لقد كنت في غفله من هذا فكشفنا عنك غطاك فبصرك اليوم حديد } [ق: 22].
6. { و انزلنا الحديد فيه باس شديد و منفع للناس } [الحديد: 25].
UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
5. Jun, 2022
METONIC CYCLE KATIKA KURUANI

Metonic Cycle ni Uhusiano unaosababishwa na Mwezi Na Jua.
Harakati za Mwezi katika kuizunguka Ardhi na wakati huo huo Mwezi na Ardhi kuzunguka Jua.
Kila baada ya Miaka 19 Mwezi Na Jua zinakutana na kukaribiana tena katika Positions au sehemu zake za asili.
Kuruani imetaja majina mawili katika Aya 19 na Kila Aya inaambatanisha Jua na Mwezi. الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ “Jua na Mwezi”
Nimeorodhesha hapa chini Aya zote 19 ambazo kila Aya inatumia ibara hii. الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ yaani “Jua na Mwezi”. Ukifikiri utaona Hayakupangika bure bure bali kimiujiza. Hizi ni Aya Pekee katika Kuruani yote.
The Metonic cycle is a period of 19 calendar years (235 lunar months), after which the new and full moons return to the same (or nearly the same) dates of the year. Therefore, 19 years from now, in 2034, we’ll again have another Blue Moon in July And 19 years after that, there will be another one, in July, 2053. There are 235 full moons (235 lunar months) yet only 228 calendar months in the 19-year Metonic cycle. Because the number of full moons outnumber the number of calendar months, that means at least seven of these 228 calendar months must harbor two full moons (235 – 228 = 7 extra full moons).
The cycle was discovered by Meton (fl. 432 bc), an Athenian astronomer.
AYA 19 AMBAZO ZIMETAJA MANENO MAWILI YA الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ
2. { يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ حَثِيثًا وَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ وَ النُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ } [الأعراف: 54].
1. { فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَ جَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ حُسْبَانًا } [الأنعام: 96].
3. { هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَ الْقَمَرَ نُورًا وَ قَدَّرَهُ مَنَازِلَ } [يونس: 5].
4. { يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ } [يوسف: 4].
5. { وَ سَخَّرَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُسَمًّى } [الرعد: 2].
7. { وَ سَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَ النَّهَارَ وَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ وَ النُّجُومُ مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ } [النحل: 12].
6. { وَ سَخَّرَ لَكُمُ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ دَائِبَيْنِ وَ سَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَ النَّهَارَ } [إبراهيم: 33].
8. { وَ هُوَ الَّذِي خَلَقَ اللَّيْلَ وَ النَّهَارَ وَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ كُلٌّ فِي فَلَكٍ يَسْبَحُونَ } [الأنبياء: 33].
9. { أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَسْجُدُ لَهُ مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَ مَنْ فِي الْأَرْضِ وَ الشَّمْسُ وَ الْقَمَرُ } [الحج: 18].
10. { وَ لَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ وَ سَخَّرَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ } [العنكبوت: 61].
11. { يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَ يُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَ سَخَّرَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ } [لقمان: 29].
13. { لَا الشَّمْسُ يَنْبَغِي لَهَا أَنْ تُدْرِكَ الْقَمَرَ وَ لَا اللَّيْلُ سَابِقُ النَّهَارِ } [يس: 40].
12. { يُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَ يُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ وَ سَخَّرَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ } [فاطر: 13].
14. { يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَ يُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ وَ سَخَّرَ الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ } [الزمر: 5].
15. { وَ مِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَ النَّهَارُ وَ الشَّمْسُ وَ الْقَمَرُ } [فصلت: 37].
16. { لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَ لَا لِلْقَمَرِ وَ اسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ } [فصلت: 37].
17. { الشَّمْسُ وَ الْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ } [الرحمن: 5].
19. { وَ جُمِعَ الشَّمْسُ وَ الْقَمَرُ } [القيامة: 9].
18. { وَ جَعَلَ الْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَ جَعَلَ الشَّمْسَ سِرَاجًا } [نوح: 16].
Mpangilio huu unathibitisha kwamba yule yule aliyesema katika Aya namba 19 kwamba siku ya kiama atakutanisha Jua na Mwezi
(وَ جُمِعَ الشَّمْسُ وَ الْقَمَرُ )
basi ni yule yule ambaye anayekutanisha Mwezi na Jua baada ya kila miaka 19.
Na mkutanisho huu ndiyo wataalamu wanatuambia kwamba ni Metonic Cycle.
Allahu Akbar. Angalia Muashirio wa Kumiujiza unavyoshangaza.
Maneno Yalivyochaguliwa na kupangwa. Huu siyo muujiza mdogo.
UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
5. Jun, 2022
COMMON AND LEAP YEAR

MANENO YALIYOCHAGULIWA KUASHIRIA COMMON NA LEAP YEAR
Neno سنة limekariri na kutumika katika kuruani mara 7 katika Jumla za Aya 7. na Neno سنين limekariri na kutumika katika kuruani mara 12 katika jumla za Aya 12. Kukariri kwa neno سنة kunalingana na Leap Years 7 ya Miaka ya Kiislamu na kukariri kwa neno سنين kunalingana na miaka 12 ya kiislamu ya kawaida “Common Years”.
Ukijumlisha namba hizi mbili 12 na 7 unapata namba 19 (12 + 7=19). Na namba 19 ni Jumla ya miaka inayojulikana kama Metonic Cycle. Nitazungumzia Makala nyingine inayohusika na Metonic Cycle Mwenyeezi Mungu akipenda.
Miezi ya kawaida ya Kiislamu ina masiku 354 na pia kuna Miezi ambayo ina masiku 355.
Miezi yenye masiku 355 inajulikana kama Leap Years na Miezi yenye masiku 354 inajulikana kama Miezi ya kawaida. (Common Years). Tofauti hizi zinatokana na mzunguko wa Ardhi katika kuizunguka Jua.
Ajabu ni kwamba Kuruani yote imetaja neno سنة mara 7 na Neno سنين mara 12. tu bila ziada au upungufu.
Ukifikiri utaona Neno سنة linawakilisha Leap Years na Neno سنين linawakilisha Common Years.
Hapa chini ni Orodha ya Aya ambazo zimetumia maneno haya mawili.
1. { يَوَدُّ أَحَدُهُمْ لَوْ يُعَمَّرُ أَلْفَ سَنَةٍ وَ مَا هُوَ بِمُزَحْزِحِهِ مِنَ الْعَذَابِ أَنْ يُعَمَّرَ } [البقرة: 96].
2. { قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ أَرْبَعِينَ سَنَةً يَتِيهُونَ فِي الْأَرْضِ } [المائدة: 26].
3. { وَ إِنَّ يَوْمًا عِنْدَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِمَّا تَعُدُّونَ } [الحج: 47].
4. { وَ لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَى قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا } [العنكبوت: 14].
5. { ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِمَّا تَعُدُّونَ } [السجدة: 5].
6. { حَتَّى إِذَا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَ بَلَغَ أَرْبَعِينَ سَنَةً قَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ نِعْمَتَكَ } [الأحقاف: 15].
وإليكم الآيات التي ذكرت فيها كلمة (سنين) وعددها 12 :
7. { تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَ الرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ } [المعارج: 4].
1. { وَ لَقَدْ أَخَذْنَا آلَ فِرْعَوْنَ بِالسِّنِينَ وَ نَقْصٍ مِنَ الثَّمَرَاتِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ } [الأعراف: 130].
2. { وَ قَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَ الْحِسَابَ } [يونس: 5].
3. { فَأَنْسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ فَلَبِثَ فِي السِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ } [يوسف: 42].
5. { وَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَ الْحِسَابَ وَ كُلَّ شَيْءٍ فَصَّلْنَاهُ تَفْصِيلًا } [الإسراء: 12].
4. { قَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدْتُمْ فَذَرُوهُ فِي سُنْبُلِهِ إِلَّا قَلِيلًا مِمَّا تَأْكُلُونَ } [يوسف: 47].
6. { فَضَرَبْنَا عَلَى آذَانِهِمْ فِي الْكَهْفِ سِنِينَ عَدَدًا } [الكهف: 11].
7. { وَ لَبِثُوا فِي كَهْفِهِمْ ثَلَاثَ مِائَةٍ سِنِينَ وَ ازْدَادُوا تِسْعًا } [الكهف: 25].
8. { وَ فَتَنَّاكَ فُتُونًا فَلَبِثْتَ سِنِينَ فِي أَهْلِ مَدْيَنَ ثُمَّ جِئْتَ عَلَى قَدَرٍ يَا مُوسَى } [طه: 40].
9. { قَالَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الْأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ } [المؤمنون: 112].
10. { قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَ لَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ } [الشعراء: 18].
11. { أَفَرَأَيْتَ إِنْ مَتَّعْنَاهُمْ سِنِينَ } [الشعراء: 205].
12. { فِي بِضْعِ سِنِينَ لِلَّهِ الْأَمْرُ مِنْ قَبْلُ وَ مِنْ بَعْدُ وَ يَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ } [الروم: 4].
فهل جاء هذا النظام المحكم بالمصادفة أم بتقدير من العزيز الحكيم؟
Huu siyo muujiza mdogo. Kuruani inathibitisha Uhakika ambao hata Wanasayansi bado wanababaika. Allahu Akbar.
UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
3. Jun, 2022
MBINGU NA ARDHI
MATABAKA YA ARDHI

MATABAKA YA HEWA ANGANI

Mwenyeezi Mungu anasema katika Kuruani tukufu kwamba ameumba mbingu matabaka saba na ardhi pia hivyo hivyo. Kwa hiyo ardhi pia ina matabaka saba.
Mwenyeezi Mungu anatuthibitishia habari hii kwa kutuonyesha muujiza mwingine wa kushangaza.
Na muujiza huu ni kutuhakikishia kwamba kuruani ni Maneno yake.
Angalia mpangilio wa kushangaza. Yaani baada ya kutuambia kwamba ameumba mbingu matabaka saba na ardhi pia hivyo hivyo akaongeza muujiza mwingine kwa kutaja maneno haya mawili katika aya saba tu ya kuruani yote.
Kwa hiyo katika kuruani yote kumetajika maneno السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ kwa pamoja mara saba tu.
Hebu tufikiri mpangilio wa kimuujiza unaoshangaza. haiwezekani aya au maneno haya kujipangia hovyo hovyo. Aya hizi zimepangwa kwa ufundi wa hali ya juu na Muumba aliyeumba kila kitu. Allahu Akbar.
Nimeorodhesha hapa chini Aya saba zenye maneno haya mawili. Aya hizi zimetajika katika sura mbalimbali, na kama kawaida ya Aya za kuruani zilishushwa katika wakati , sehemu na mazingara mbali.
1- { إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ } [الأعراف: 54].
2- { إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ } [يونس: 3].
3- { وَ هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَ كَانَ عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ } [هود: 7].
4- { الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ وَ مَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ } [الفرقان: 59].
5- { اللَّهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ وَ مَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ } [السجدة: 4].
6- { وَ لَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ وَ مَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَ مَا مَسَّنَا مِنْ لُغُوبٍ } [ق: 38].
7- { هُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَ الْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَى عَلَى الْعَرْشِ } [الحديد: 4].
UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
3. Jun, 2022
KATIKA TUMBO LA UZAZI

Miezi ambayo mama anabeba mimba mpaka kuzaa ni Tisa. Huenda ikazidi au kupungua lakini kwa kawaida ni Miezi Tisa.
Muujiza wa Kuruani Ni Mkubwa sana na hauna mfano wowote tunaoujua na tusioujua katika Elimu zetu zote.
Sasa Kinachoshangaza ni kwamba Kuruani Yote imetaja neno خلقنكم “TUMEKUUMBENI” mara 9 tu peke yake katika sura mbalimbali ambazo zilishushwa katika wakati, sehemu na matukio mbalimbali.Hebu Tufikiri.
Kuruani haikushushwa kwa muda wa siku moja bali kwa muda wa miaka 23. Lakini mpangilio wake ni wa kimuujiza usio mfano. Hakuna anayeweza kufanya hivyoisipokuwa ni mwenyewe mwenyeezi mungu peke yake.
Mwenyeezi Mungu alikuwa akiongoza mpangilio huu na kuitunza mpaka leo.
Nimekusanya hapa Chini Aya Tisa ambazo zimetumia neno خلقنكم “TUMEKUUMBENI” ili ujionee mwenyewe. Allahu Akbar.
{ ولقد جيتمونا فردي كما خلقنكم
اول مره وتركتم ما خولنكم ورا ظهوركم وما نري معكم شفعاكم الذين زعمتم انهم فيكم شركوا لقد تقطع بينكم وضل عنكم ما كنتم تزعمون } [الأنعام:94].
{ ولقد خلقنكم
ثم صورنكم ثم قلنا للمليكه اسجدوا لادم فسجدوا الا ابليس لم يكن من السجدين } [الأعراف:11].
{ وعرضوا علي ربك صفا لقد جيتمونا كما خلقنكم اول مره بل زعمتم الن نجعل لكم موعدا } [الكهف:48].
{ منها خلقنكم وفيها نعيدكم ومنها نخرجكم تاره اخري } [طه:55].
{ يايها الناس ان كنتم في ريب من البعث فانا خلقنكم من تراب ثم من نطفه ثم من علقه ثم من مضغه مخلقه وغير مخلقه لنبين لكم ونقر في الارحام ما نشا الي اجل مسمي ثم نخرجكم طفلا ثم لتبلغوا اشدكم ومنكم من يتوفي ومنكم من يرد الي ارذل العمر لكيلا يعلم من بعد علم شيا وتري الارض هامده فاذا انزلنا عليها الما اهتزت وربت وانبتت من كل زوج بهيج } [الحج:5].
{ افحسبتم انما خلقنكم عبثا وانكم الينا لا ترجعون } [المؤمنون:115].
{ يايها الناس انا خلقنكم من ذكر وانثي وجعلنكم شعوبا وقبايل لتعارفوا ان اكرمكم عند الله اتقيكم ان الله عليم خبير } [الحجرات:13].
{ نحن خلقنكم فلولا تصدقون } [الواقعة:57].
{ وخلقنكم ازوجا } [النبأ:8].
UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
2. Jun, 2022
NENO “QIBLAH” KATIKA KURUANI TUKUFU

Tunapokwenda Hija tunaizunguka Jengo la Qaabah mara 7. Tunakwenda baina ya Safwa na Marwa mara Saba, Tunatupa Vijiwe Saba katika Jamrah kwa lengo la kumlaani Sheytan. Na Nyumba Hii ndiyo Tunayoielekea katika Sala Zetu Zote. Muujiza wa Kuruani ni kwamba neno “QIBLAH” limetajika katika Kuruani Mara 7 tu peke yake. Je unaona Vipimo vya kushangaza. . Allahu Akbar. Huu siyo Muujiza mdogo hata kidogo. Neno Qiblah limetumika katika Aya Zifuatazo:
1/ Sura Ya Al-Bakarah Aya Namba 142
3/ Sura Ya Al-Bakarah Aya Namba 144
2/ Sura Ya Al-Bakarah Aya Namba 143
4/ Sura Ya Al-Bakarah Aya Namba 145 (Neno Qiblah Limetajika mara Tatu)
5/ Sura Ya Yunus Aya Namba 87
Jumla neno Hili limetajika katika Kuruani Mara Saba Pia!!!! Angalia Muujiza. Allahu Akbar.
UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
2. Jun, 2022
KURUANI NI MUUJIZA MKUBWA KATIKA KARNE ZOTE

Kuruani Ni Muujiza Mkubwa ambao Tumepewa na Mwenyeezi Mungu.
Ikiwa ukubwa na utukufu wa yule aliyeumba ulimwengu ni mkubwa sana basi je Kuruani ambayo ni Mazungumzo yake yatakuwa vipi?
Mtume Mohamad ﷺ alipewa miujiza mbalimbali kuthibitisha utume wake na Kuruani ni moja ya miujiza hiyo.
Kila Mtume alipewa Miujiza ya kuthibitisha Ujumbe wa Muumba wa Ulimwengu.
Na kwa vile huu ndiyo Ujumbe wa mwisho basi Mwenyeezi Mungu amejaalia uwe na Miujiza mbalimbali kuthibitisha kwamba Ujumbe huu ni wa kweli.
Sayansi za kisasa zimefanya utafiti kwa kutumia Carbon Dating Technique na wanatuhakikishia kwamba Kuruani ipo vile vile kuanzia Karne ya Saba mpaka leo.
Huko Uingereza Katika Birmingham Library kuligunduliwa Msahafu wa zamani tangu karne ya Saba na walitumia utafiti wa aina hii na kugundua ukweli huu. Angalia Picha hapa Juu ya Msahafu huo ambao umetunzwa huko England na ambao unathibitisha kwamba kuruani imetunzwa kama ilivyo. Allahu Akbar.
Ujumbe huu (Kuruani) haukuguswa kwa kuongezwa au kupunguzwa Herufi, Maneno, Aya na Sura Zake kama ilivyofanyika katika vitabu vya binguni vilivyotangulia.
Kuruani ipo vile vile tangu iliposhushshwa mpaka leo kama Mwenyeezi Mungu alivyoahidi kwamba Atakitunza kitabu hiki.
Ni Kitabu ambacho kitabaki katika hali hii mpaka Mwenyeezi Mungu atakapopenda mwenyewe.
——————————————————————————-