SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Miujiza Mipya

Miujiza Mikubwa

MUUJIZA WA KWANZA-WAUMINI WA PANGO

Alhamdulillah Leo tarehe 24/08/2023 namshukuru Mwenyeezi Mungu kunipa Uhai na uwezo wa kuandika habari hizi za kushangaza. Ni habari za kushangaza sana na pia ni njia katika njia mbalimbali zake mola katika kutunasihi na kutuhurumia katika muda mfupi sana wa maisha yetu hapa duniani. Yeye anatusaidia na kutuonya kabla ya kutuondoa hapa duniani. Na tukae tukijua kwamba tukiodolewa tu basi mtihani umekwisha na tutakuwa tukisubiri matokeo yake siku ya kiyama. Katika Mtihani huu kuna kupasi na kufeli na Muda wa uhai utakapokwisha tu basi hakuna kurundi nyuma. Kwa kweli hatari kubwa kwani kupasi mtihani malipo yake ni pepo na kufeli mtihani malipo yake anajua Mwenyeezi Mungu. Kuruani inatuambia malipo yake ni Moto wa Jahannam labda tuhurumiwe na tusamehewe na hii yote inategemea yeye Mwenyewe aliyetuumba analotaka huwa na asilotaka haliwi. Allahu Akbar.

Sasa Tuanze Kuchunguza Miujiza Mbalimbali kutoka katika kitabu kitukufu “Kuruani”

Tuanze na Kisa cha Watu wa Pango waliolazwa kwa muda wa miaka 309!!!!

Watu wengi wanafikiri utani. Kisa hiki kimetajwa katika Biblia na Kuruani. Maadamu kisa hiki kipo katika Kuruani Tukufu basi kaa ukijua kwamba Ni Habari ya ukweli. Na katika Mlango huu Nitadokeza uthibitisho ambao unatilia mkazo ukweli wa kisa hiki.

Hebu kwanza Tuinukulu Aya Ya kwanza ambayo inazungumzia kisa hiki.

Ni Aya ya kwanza kuelezea kisa hiki.

أَمۡ حَسِبۡتَ أَنَّ أَصۡحَـٰبَ ٱلۡكَهۡفِ وَٱلرَّقِيمِ كَانُواْ مِنۡ ءَايَـٰتِنَا عَجَبًا (٩) 

Tafsiri

Or dost thou reflect that the Companions of the Cave and of the Inscription were wonders among Our Signs?

9· Je! Unafikiri ya kwamba (wale) watu wa Pangoni na (wenye habari) zile zilizoandikwa (vitabuni) walikuwa ajabu ka iik&. ajabu zetu?

Nilitaja katika Milango mingineyo ya Mtandao huu kuhusu Muujiza mbalimbali wa kisa hiki. Kwa kifupi nilisema kwamba:

Aya hii ni ya kwanza katika kisa hiki kilichosimuliwa kwa Aya 18 za Sura Ya 18 ya Alkhf.

1/Muujiza wa kwanza ni Idadi za Aya 18 kulingana na Namba ya Sura ambayo pia ni ya 18

2/Muujiza za pili ni idadi ya Kurasa za Kuruani. Ukihesabu kuanzia Ukurasa huu wa Kuruani unaosimulia Kisa hiki mpaka mwisho wa Kuruani utapata Jumla ya kurasa ni 309 kulingana na muda waliolazwa watu hawa wa pango. Kwani walilazwa kwa muda wa miaka 309!!! Je unaona Muujiza mpaka karika Kurasa. Kila kitu kimehesabiwa. Allahu Akbar.

3/Muujiza wa tatu ni Maneno yaliyotumika katika kuelezea kisa hiki ni Jumla ya maneno 309 tu kulinagana na Muda wa miaka waliolazwa wartu hawa katika Pango.

4/Muujiza wa nne nitauelezea kwa picha ifuatayo:

PICHA NAMBA 1

Kama Inavyoelezea picha hii kwamba Aya Namba 9 inataja Majina Mawili ya sehemu waliolazwa wachamungu hawa kwa muda mrefu.

 ٱلۡكَهۡف

ٱلرَّقِيمِ 

Wafasiri wa kuruani wametupa Tafsiri mbalimbali kuhusu Majina haya mawili. Kuna wanaosema kwamba Pango hilo lilikuwa katika Bonde lililojulikana kama Raqiim. Wengine wanasema Raqiim ni Mji na wengine wanasema ni Kilima. Kwa kifupi ni majina ya sehemu ya watu hao waliolazwa kawa muda wa miaka 309. Ukichunguza Herufi za majina haya mawili. Alkahf na Alraqiim katika Kuruani utapata Muujiza mwingine wa kushangaza. Utakuta Herufi hizi zimetumika katika Kuruani katika jumla za Aya 1809 tu kutoka katika Aya 6236 za kuruani!!!. Jambo la kushangaza ni kwamba Aya hii ya kwanza ya kisa hiki na ambayo imetaja Majina ya sehemu hiyo waliolazwa watu hawa imetoka katika Sura Namba 18 Aya Namba 9 ambayo inaweza kuandikwa

18:09

Namba hii ni sawa sawa na Idadi za Aya zilizotumia Herufi za majina mawili Yaani 1809

Je unaona Muujiza? !!!!!!

Hii inathibitisha kwamba Kuruani ni Muujiza kwani hakuna anayeweza kuandika Kitabu kama hiki hata kidogo. Allahu Akbar. Jambo hili linathibitisha kwamba Kuruani ni maneno ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu na siyo upuuzi na hakuna kiumbe chochote akinachoweza kuandika kitabu na kukipanga kwa kuchagua na kuhesabu herufi, maneno na aya kwa mfano huu.

 5/Muujiza Wa Tano na ambao unathibitisha kisa hiki ni wa ajabu sana na ambao hakuna kiumbe chochote ambacho kinaweza kufanya ni kama ufuatao:

Idadi ya muda waliolazwa watu hawa katika Pango umetajwa katika kuruani katika Sura (Chapter) Namba 18 Aya Namba 25 tu katika kuruani yote sasa tuone maajabu yafuatayo:

Katika Kuruani Nzima kuna maneno 25 tu pekee ambayo yana thamani ya namba 309 na ambayo yametajika katika Jumla ya sura 18!!!!

Yaani Maneno 25 katika Sura 18 inaashiria ile Sura namba 18 Aya Namba 25 ambayo imetaja kwa uwazi wazi namba hii ya 309!!!!

MUUJIZA WA PILI-ASILIMIA 88 YA MAJI KATIKA MAZIWA

PICHA NAMBA 2

MUUJIZA WA TATU-ASILIMIA 100 YA KUCHEMKA KWA MAJI-(BOILING POINT)

PICHA NAMBA 3

MUUJIZA WA NNE- IDADI YA WAPIGANAJI WAUMINI WALIOSHIRIKI KATIKA VITA VYA BADR

PICHA NAMBA 4

MUUJIZA WA TANO-UMRI WA MIAKA 92 WA FIRAUNI ALIYEKUWA AKITAWALA KATIKA ENZI YA NABII MUSA

PICHA NAMBA 5

Muujiza huu bado unaendelea………………… Nikipata nafasi Inshaallah.. hivi karibuni…….