SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Alama Za Kiama

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

HADITHI  ZA MTUME MOHAMAD .ﷺ ZENYE  MIUJIZA 

Kuna baadhi  Hadithi mbalimbali za Mtume  Mohamad ﷺ ambazo hapo  zamani  yaliyoashiriwa hayakuwa na uhusiano na mazingara ya wakati huo.

Hapo zamani katika karne zilizopita yaani kuanzia karne ya 7 na  zilizofuatia mpaka Mwanzoni mwa karne ya 20 Elimu za Sayansi zilikuwa bado changa sana na Hadithi kama hizi zilikuwa mbali na fahamu na pia Elimu  za watu wakati huo.  Wanavyuoni waliziamini na kuziacha hivyo hivyo bila  ya kuzipinga.

Leo tunakuta Hadithi hizo zinaleta maana kubwa. Kwani hivi karibuni Utafiti wa kisayansi katika nyanja mbalimbali umegundua mengi ambayo yanathibitisha kwamba aliyoyazungumza Mtume Mohamad ﷺ  ni ukweli bila ya shaka yeyote.

Na hadithi hizi zimekuwa Muujiza kwani aliyoyazungumza Mtume ﷺ wakati huo yamegunduliwa hivi  karibuni.

Wakati huo kulikuwa hakuna vyombo vya utafiti kama Wakati huu wa kisasa.

Hadithi za  Mtume ﷺ  ni Wahyi kama inavyosema kuruani Tukufu.

Mfano unaposafiri kutoka mji na kuenda mji mwingine utakuta Barabarani  Vibao vya Kutujuuklisha  Umbali yaani Maili au Kilomita. Kama ni  Maili  100  baada ya kuendelea na Safari  utaona  80  kisha  60  kisha 50  kisha 10  na mfano huu huu  Mwenyeezi Mungu ameweka Alama za Kukaribia kwa Kiyama. 

Hadithi hii ina vipengele Vinne na kama sikosei na vyote vimetokea. na kama Katika Hadithi Nyinginezo za Mtume ﷺ zinazosema kwamba Kiyama Kimekaribia.

Na Kuruani pia inathibitisha  kukaribia kwa kiyama. Mwenyeezi Mungu anasema

اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانشَقَّ الْقَمَرُ

 “IKTARABA|TI  ASAAA” 

yaani  Kiyama Kimekaribia sana tena  bila Shaka na ndiyo maana Neno  “IKTARABATI”  lipo katika  “Passive Tense”  na Aya Hii pia inathibitisha Kupasuliwa kwa Mwezi. Katika Mojawapo ya Miujiza Ya Mtume Mohamad ﷺ  ni Kupasua Mwezi.

Hebu  tuchunguze Hadithi  mbalimbali za aina hii.

ALAMA AU FITINA KABLA YA KUTOKEA KIYAMA

HADITHI -1  (KITABU CHA FITNA  (AL-FITAN)

Jami` at-Tirmidhi Hadithi Namba 2181

حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ وَكِيعٍ، حَدَّثَنَا أَبِي، عَنِ الْقَاسِمِ بْنِ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا أَبُو نَضْرَةَ الْعَبْدِيُّ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى تُكَلِّمَ السِّبَاعُ الإِنْسَ وَحَتَّى تُكَلِّمَ الرَّجُلَ عَذَبَةُ سَوْطِهِ وَشِرَاكُ نَعْلِهِ وَتُخْبِرَهُ فَخِذُهُ بِمَا أَحْدَثَ أَهْلُهُ مِنْ بَعْدِهِ ‏”‏ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى وَفِي الْبَابِ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏.‏ وَهَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ لاَ نَعْرِفُهُ إِلاَّ مِنْ حَدِيثِ الْقَاسِمِ بْنِ الْفَضْلِ ‏.‏ وَالْقَاسِمُ بْنُ الْفَضْلِ ثِقَةٌ مَأْمُونٌ عِنْدَ أَهْلِ الْحَدِيثِ وَثَّقَهُ يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الْقَطَّانُ وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مَهْدِيٍّ ‏.‏

TAFSIRI

Abu Saeed Al-Khudri anaelezea kwamba Mtume ﷺ alisema

Swahili Translation

“Naapa kwa yule ambaye Roho yangu ipo mikononi mwake. Kiyama hakitafanyika mpaka Wanyama watakapozungumza na watu, Ncha za fimbo, Kiatu na Paja (lake) litakapomjuulisha habari za familia yake.

English Translation

(Abu Sa’eed Al-Khudri narrated that the Messenger of Allah (s.a.w) said: “By the One in Whose Hand is my soul! The Hour will not be established until predators speak to people and until the tip of a man’s whip and the straps on his sandal speak to him, and his thigh informs him of what occurred with his family after him.”)

SHEREHE 

Hadithi hii inashangaza sana. Hebu tujiulize Maswali.

Je Kabla ya Kiyama au kiyama kinapokaribia Vifuatavyo  vitaweza kuzungumza na Binaadamu?

1/Mnyama Wa  Pori au Baharini.  Neno  السِّبَاعُ   ni Predator. Mfano  wa Samaki ambao wanakula  samaki wengineo.  Au Mbwa Mwitu, Au Fisi.  Na wengineo.

2/Ncha ya Fimbo

3/Kiatu

4/Simu Juu ya Paja  La Mguu

Wanavyuoni wakati huo waliipokea hadithi hii na mfano wa Hadithi za aina hii na kuzihifadhi bila  kuzipinga au  kuzitilia shaka.

Tupo katika karne ya 21 na Mtume aliishi katika karne ya 7.  

Hebu tufikiri  karne ngapi zimepita?

Karibu   Karne  14  yaani miaka  1400  iliyopita. 

Haya yaliyozungumzwa ni karibu miaka 1400 iliyopita.

Sasa leo hii tupo katika Karne ya 21.  Ni Karne ya Sayansi za Hali ya Juu. 

Uamini  au Usiamini.  Wataalamu  wametengeneza Viatu ambavyo vina Simu.

Pia Wataalamu wametengeneza Fimbo zenye Simu  na hizi zina uwezo Mkubwa wa kuwasaidia Vipofu, Vilema, Wazee na Wenye maradhi mbalimbali. Fimbo  zenye uwezo wa kupeleka Habari  nyumbani ikiwa Mzee anayeumwa kama amepotea njia au kuanguka kwa sababu yeyote ile ya Maradhi.

Kwa kifupi Fimbo hiyo in uwezo wa Kuwasiliana na Watu ili  kumsaidi anayeitumia.

Na Simu za mikono  ambazo  mara nyingi huwekwa mifukoni yaani Karibu na Paja.  Simu  hizo  kwa wale wanotumia Bluetooth  huiacha mifukoni. Kwa hiyo Simu yako inakuwa Mifukoni yaani karibu na Paja lako. Na pia kuna Simu ambazo huwekwa Juu ya Paja na Kufungiwa hapo kwa mkanda maaalum ili kuidhibiti vizuri pajani. Inajulikana kama Thiphone. Angalia Video hapa chini.

Hebu tuichambue Hadithi  hii tena.

Tunaambiwa kwamba Kiyama Kitakapokaribia  basi kutakuwa na Alama Alama Mbalimbali  za kutujuulisha ili tujiandae kwa kubadili vitendo vyetu vibaya kabla ya wakati huo.

Baadhi ya Alama Mbalimbali  zimekwisha onekana. Kuna Vitabui mbalimbali vimetaja Alama hizo.

Kwa mfano  Kitabu cha Ibn Kathir  na wanavyuoni wengineo  wameandika Habari hizi kwa urefu. 

Kwa kifupi Katika Alama Zilizotajwa katika Hadithi hii temeona kwamba Alama za Kiyama  tatu  za mwisho zimekwisha  tokea.

1/Mnyama wa Pori  (Bado  kuonekana)

2/Fimbo Itakayozungumza  (imeshaonekana angalia Video hapa chini)

3/Kiatu kitakachozungumza (Imeshaonekana angalia video hapa chini)

4/Paja La Mguu  Litakalozungumza(Imeshaonekana angalia video hapa chini)

Nimeambatanisha Hapa Chini  Video za Viatu, Fimbo  “SMART CANE” na Simu ya Pajani. “Thipphone”  na Alhamdulilahi leo tarehe  26/08/2022 nimeambatanisha Habari ya Samaki kuzungumza. (Sina uhakika wa habari hizi) lakini  Gazeti maarufu la huko Marekani ndovyo linavyosema. Na ikiwa ni kweli basi inathibitisha  Hadithi tuliyosoma hapa juu kwamba Mnyama ataweza kuzungumza. 

VIDEO-1

Viatu Vilivyoshonwa na kutiwa Computer na Uwezo wa Kuzungumza. Je unaona Aliyotabiri Mtume Mohamad katika Karne ya 7 ? Allahu Akbar

Video-2

Fimbo inayozumgumza inajulikana kama “SMART CANE” ni mojawapo ya Maendeleo ya kisasa. Kama alivyotabiri Mtume Mohamad ﷺ hapo zamani. Allahu Akbar.

Video-3

Simu ambayo imefungwa Katika Paja. Simu ni ya kawaida lakini imefungw ana mikanda hapo mguni. Lengo ni kuidhibiti vizuri. Kwa lugha nyingine ni simu ya Pajani au THIPPHONE. Sikiliza Video inayohusu simu hii. La kushangaza ni Hadithi ya Mtume hapa juu.

Hapa chini Gazeti La Marekani BBC NEWS la mwaka 2003 linatuelezea habari ya samaki aliyezungumza kwa lugha ya kiyahudi na kuonya habari za kukaribia kwa kiyama. Kama hizi habari ni za kweli basi inathibitisha hadithi ya Mtume Mohamad ﷺ kuhusu Mnyama au Samaki atakayezungumza na Binaadamu. Allahu Akbar. Unaweza kusoma makala iliyokamili kwa kutumia anuani ya mtandao ufuatao:

http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/americas/2854189.stm