UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
APPLICATIONS MBALIMBALI ZA AYA ZA KURUANI KATIKA MAISHA YETU
Kwanza ningependelea kuomba Dua kwa kusema “Alhamdulilahi Tunamshukuru Mwenyeezi Mungu kwa Kila alichoturuzuku na kwa kila asichotupa. Yote mawili ni Neema kubwa. Kwani anaturuzuku kitakachotufaa na Hatupi yale ambayo hayatufai au yenye Dhara.
Rehema ya Mwenyeezi Mungu ipo kila pahali kama alivyosema katika Kuruani Tukufu.
Mwenyeezi Mungu ameshusha Kuruani ili iwe mwanga Katika maisha yetu. Ametaka kutuinua Duniani na Akhera. Na Waislamu wa Kundi la mwanzo katika Enzi Ya Mtume Mohamad ﷺ walifahamu na kuamini hivyo na wakaitumia Kuruani kama ipasavyo. Elimu zao ziliwafaa wao na sisi mpaka leo. Walifanya kazi kubwa ya kusambaza Elimu hizo zilizogusia nyanja mbalimbali za Dini na Sayansi.
Waislamu wa mwanzo walichangia katika Kuendeleza Elimu za Kisayansi
Kwa Mfano Sheikh Al-khawarizmi (Mwenyeezi MunguAmrehemu) ndiye aliyeanzisha Elimu ya Al-Gorithm ambayo leo hii ndiyo Msingi wa Computer, Simu za mkono na Mashine mbalimbali za Vyombo vya habari. Laiti Mtu huyu asingevumbua Elimu ya Al-gorithm basi huenda leo hii kusingekuwako na Vyombo hivi vya kisasa vya Nyanja mbalimbali za Elimu.
Sheikh Al-Haitham (Mwenyeezi Mungu Amrehemu)ndiye wa kwanza kuanzisha Elimu ya Kupiga Picha na ndiyo msingi wa Camera, Video Na vyombo mbalimbali za aina hii yanayotumika katika kila nyanja za maisha.
Sheikh Abbas Ibn Al-Farnasi (Mwenyeezi Mungu Amrehemu) ndiyo wa kwanza aliyekuja na fikra ya Kutengeneza Mabawa na kisha akaruka na kuweza kupaa angani, ijapokuwa haikuwa Aeroplane lakini ndiyo wa kwanza kuja na Fikra hizo. Ijapokuwa alianguka mara ya kwanza lakini alijua kwamba Mabawa hayatoshi bali kuna mengineyo yanahitajika. Aliona Mkia ni Muhimu ili asianguke kama alivyoanguka mara ya kwanza. Ijapokuwa hakuja na Fikra ya kutengeneza Ndege lakini Ndiyo Msingi wa Kutengeneza Ndege. Elimu hiyo aliipata baada ya kumsoma Njiwa alivyo na yeye alifanya hivyo na Elimu hii ndiyo msingi wa Aeroplane tunazoziona leo Ukweli ni kwamba Marehemu Bwana Abbasi Ibn Al-Farnasi aliyezaliwa huko Spain na aliyekuwa Mwislamu ndiye aliyeanzisha ufundi wa kupaa angani.
(The Wright brothers may have invented the first motorised aircraft, but the 9th century engineer Abbas Ibn Firnas is considered to be the first human to fly with the help of a pair of wings built by silk, wood and real feathers)
Kuna Mifano Mingi ya Waislamu waliochangia katika Nyanja mbali mbali za Elimu ya Sayansi lakini katika Mlango huu inatosha Mifano hii mitatu.
Karne zilizofuata baadhi ya Waislamu walipuuza na kufanya uzembe wa kuifuata Kuruani kama ipasavyo na kufuata mataifa mengineyo yasiyo na Imani ya Kiislamu.
Mwenyeezi Mungu akipenda Katika mlango huu Nitakuwa nikiorodhesha Faida na Matumizi ya Aya za Kuruani katika Nyanja mbalimbali za Maisha.
Nitatumia Neno Applications za Aya za Kuruani. au Kwa kiswahili “Matumizi ya Aya za Kuruani”. katika Nyanja mbalimbali za Maisha.
Kwanza Ningependelea kusema kwamba Tutatumia hatua zifuatazo.
1/Tunataka Kutatua Tatizo
2/Tafuta Aya Katika Kuruani ambayo imeashiria Kipengele angalau kimoja cha Tatizo Hilo
3/Fanya Utafiti katika Kuruani na Hadithi za Mtume ﷺ
Na pia wakati mwingine Inawezekana kugeuza Mpangilio huu kama ifuatavyo;
Kwanza
1/Katika Kisomo chako cha Kuruani Utakapoona Aya ambayo huenda inatatua Tatizo Lolote la kimaisha Uisome tena vizuri
2/Uifanyie Utafiti.
3/Na Utafute Jibu la Suala Lako.
Hizi hatua tatu zinatosha katika Utafiti wa kutatua Matatizo. Jambo zuri ni kwamba Aya za kuruani hazikosei. Ukilinganisha na Sayansi utaona kuna “Trial and Error” Method. Yaani kuna kukosa na kupata. Muda mrefu utapotea kabla ya kupata jawabu la tatizo lako. Lakini Kuruani ni safi na wala haibabaishi.
Sisemi kwamba Kuruani ni kitabi cha Sayansi lakini hebu tutafute majibu ya masuala yetu katika kuruani kwanza kabla ya kutapa tapa huku na huku.
Eintein ambaye alikuwa Mwanasayansi Maarufu ulimwenguni alifanya Utafiti na baada ya Muda wa Miaka karibu 10 ndiyo utafiti wake ulikubaliwa lakini hakuna aliyejua kwamba jawabu la utafiti wake lipo katika Kuruani Tukufu. Kuruani inasema “Tunatanua Ulimwengu”. Mwana Sayansi Einstein alipoandika Maandishi yake na kuja na Fikra hii ya “Expansion of The Universe” Kwanza ilipingwa na ikapita miaka na baadaye ikakubaliwa.
Sasa je angelikuwa Myahudi huyu Muislamu?
Je angelifanya utafiti katika Kuruani au hadithi za Mtume na kukuta Aya Hii?
Angelifanya hivyo basi asingekubali kushindwa Katika Mazungumzo na Wanasayansi wa wakati huo. Kwani Angelikuwa na Yakini kwamba Nadharia Yake ni Sahihi 100% na pia asingekubali kushindwa kimajadiliano.
Kuwakubalia Wanasayansi wote wa wakati huo ambao waliamini Nadharia za Newton ambayo inasema kwamba Ulimwengu hautanuki walisababisha Einstein kubadili Equation (Mathematical Equation)kwa kuongeza Namba inayojulikana kama “Cosmological Constant” na baada ya kudhihirika kwamba Hakukosea na alikuwa amesema ukweli basi alijilaumu sana kwa huongeza namba hiyo na hapo akasema kauli yake maarufu kwamba ni “Blunder of My Life” kwani alifuata Fikra za wengineo waliokosea wakati ambao alikuwa hakukosea.
APPLICATION NAMBA 1
MEDICINE-PSYCHOLOGICAL DISORDERS
1/Tatizo La Wasiwasi na Huzuni.(Stress and Depression-Maradhi Ya Moyo)
2/ Hebu tuchunguze Katika kuruani na Hadithi za Mtume Mohamad
Sura Ya Al-Raad Namba 13 Aya namba 28
3/ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَتَطۡمَٮِٕنُّ قُلُوبُهُم بِذِكۡرِ ٱللَّهِۗ أَلَا بِذِڪۡرِ ٱللَّهِ تَطۡمَٮِٕنُّ ٱلۡقُلُوبُ (٢٨)
Aya Hii inatibu maradhi yote ya Nafsi na Kukuondolea Matatizo ya kutafuta Madakitari.
Matibabu Ya Aya Hii: Mwenyeezi Mungu anatupa Dawa hapa ya Maradhi haya kwa kusema kwamba
28. (Nao) ni wale walioamini na zikatulia nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumkuinbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia.
Je Unaona Dawa Kubwa hapa? Huhitaji Madakitari. Dakitari Aliyetuumba amekwishatupa Dawa kubwa.
APPLICATION NAMBA 2
AGRICULTURE-IRRIGATION SYSTEM
1/Ukisoma Kuruani utakuta Aya Mbalimbali ambazo Mwenyeezi Mungu ameapia Baadhi ya Vile alivyoviumba. Kwa mfano Sura Namba 95 Aya Namba 1 Inayosema
وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيۡتُونِ (١)
1. Naapa kwa Tini na Zaytuni. (Chini ya miti hii amepala Utume Nabii lbrahimu na Nabii Nuhu).
Aya Hii Ina Mengi lakini katika Utafiti tuangalie Jani tu la Mtini peke yake.
2/Katika Utafiti tunakuta Majani ya Mti Huu yana mishipa ya pekee. Yamepangwa na Mwenyeezi Mungu kiajabu sana. Mpangilio kwa njia ambayo unaona kila mshipa kwa vizuri.
3/Baada ya Kuelewa Aya hii tunaona Fikra Mpya inakuja ni kwamba ikiwa mishipa ya Jani hili kazi yake ni kubeba maji na vyakula kutoka ardhini ili iwe chakula kwa jani hilo basi na sisi tunaweza kufanya hivyo hivyo kwa kukopi ufundi huu kwa kutengeneza mabomba ya Maji na kumwagilia Mashamba yetu. (Angalia Picha hapa Chini ya Mfano huu wa Mabomba Ya Maji katika Shamba) Je unaona Faida ya Kuisoma Kuruani na Kufikiri. Tunasoma Ufundi wa Mwenyeezi Mungu na kisha tunaukopi. Allahu Akbar,.
Angalia picha hapa chini ya Jani La Mtini na Mishipa Yake ilivyopangika. Mfano huu pia Umekopiwa na Wataalamu wa Irrigation System. Mfano Mzuri wa Pipes za Maji katika Kilimo. Ukilinganisha na Jani la Mtini utaona Lile Jani ni sawa na Shamba na Mishipa ya jani hili ni sawa na Pipes za Shamba.
Picha Ya Kwanza

Picha Ya Pili

APPLICATION NUMBER 3
Physics-Alternative Energy
Mwenyeezi mungu anasema katika kuruani tukufu
Sura ya Alfurkan namba 25 na Aya namba 53 kuwa;
“Ni yeye ndiye aliyeziunganisha bahari mbili; mojawapo ni yenye kunywika na ni matamu na nyingineyo ni yenye chumvi kali, na akajaalia kinga kati yao ili zisichanganyikane na zisiharibiane”
وَهُوَ ٱلَّذِى مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ هَـٰذَا عَذۡبٌ۬ فُرَاتٌ۬ وَهَـٰذَا مِلۡحٌ أُجَاجٌ۬ وَجَعَلَ بَيۡنَہُمَا بَرۡزَخً۬ا وَحِجۡرً۬ا مَّحۡجُورً۬ا
Huu ni muujiza katika miujiza yake mwenyeezi mungu.
Aya hii nimeizungumzia katika sehemu nyingine ya website hii. Kuna Ina mengi na kwa hiyo nitagusia tu yale ambayo ttunahitaji katika Mpango huu wa Applications.
1/Aya hii inasema kwamba Mwenyeezi Mungu ameumba na Kujaalia Maji aina Mbili. Yaani Matamu na Chumvi na Akajaalia Kuzuizi baina ya Maji haya mawili. Kizuizi hiki amekiita “Barzakhan”
2/Baada ya Kusoma aya hii tunaona Fikra Mpya inakuja ambayo inahusiana na Sayansi za kileo. Wanasema wataalamu kwamba Maji ya Chumvi yanahifadhi Joto la jua na kwa hivyo Ukiweka maji ya Chumvi Kidog Juu yake na Kisha Maji Matamu Juu kabisa basi utaona maji hayo yanagawanyika katika Sehemu Tatu.
Chumvi sana yatakuwa Chini kabisa
Chumvi kidogo yatakuwa katikati
Na Maji Matamu yatakuwa Juu
Hii ndiyo Sayansi inavyosema.
3/Angalia Picha ya Solar Pond hapa chini. Ziwa la Maji lililotengenezwa kwa ajili ya kuzalisha Umeme. Jua linapotua juu ya Maji joto linakwenda chini na kuhifadhika kwani Maji ya Chini ni Mazito na Yenye Chumvi. Katikati Ya Ziwa hilo kuna Hiyo “BARZAKH”c ambayo Wataalamu wametia Jina “Insulation Layer” na Juu yake kuna Maji Matamu. Joto l chini ya maji linatumiwa na Wataalamu katika kuzalisha UMEME.
Aya katika Kuruani haisemi kwamba Tunaweza kupata UMEME katika Maji hayo lakini Aya hii imetupa “RAW MATERIALS” au Vitu ambavyo vitahitajika katika Kutengeneza Ufundi wa aina Hii. Usisahau kwamba Mwenyeezi Mungu amesema katika kuruani kwamba Aya za Kuruani lazima Uzisome kwa Kufikiri. Ujitahidi kuzielewa na Kisha Ufikiri. Ukifikiri unaweza kuzalisha Mazuri Mengi katika maisha hapa Duniani. Allahu Akbar
Sisemi kwamba Solar Pond ndiyo njia nzuri kuliko zote na pia Kuruani haikusema hivyo lakini fikra inakuja unapofikiri Aya za Kuruani. Na hata hivyo kuna faida zake na Matatizo ya Solar Pond. Angalia Hapa Chini Habari kwa Lugha Ya Kiingere.za inayohusiana na Solar Pond
Advantages of Solar Pond
Saves money as the cost associated with it is only its initial cost. Very large area collectors can be constructed just with the cost of the clay or plastic pond liner.
This technology is attractive for rural areas in developing countries.
The accumulated salt crystals which is a by-product from solar pond can be used further.
Separate collector is not needed for this thermal storage system.
Environmental friendly.
Flexibility of location as they can be located anywhere regardless of the distance to the nearest power outlet provided that there is access to direct sunlight near the pond site.
Disadvantages of Solar Pond
The accumulated salt crystals have to be removed periodically and this adds maintenance expense.
Solar ponds require a significant amount of land area to function properly.
Can only operate in sunny days and if the site is shaded by tall trees or building, it may not work properly.
Proper algae and dust removal is needed as the thermal efficiency of a solar pond sturdily dependents on the clarity of the pond.
Applications of Solar Pond
-Power production: A solar pond can be used to generate electricity by driving a thermo electric device or a Rankine cycle engine. The organic working fluid produces mechanical power in a Rankine cycle, which in turn generates electrical power using an alternator.
-Industrial process heat.
-Heating animal housing on farms: In farms which have enough land for solar ponds, the low grade heat from them can be used for heating animal housing, drying crops etc.
-Salt production: Salt is obtained as the byproduct from solar pond. Solar pond can be used for purification of salt that is for the production of ‘vacuum quality’ salt.
-Aquaculture: Using the saline water from the solar pond fishes like brine shrimp can be grown.
-Heating and Cooling of Buildings.
-Desalination: The low cost thermal energy can used to purify water for drinking or irrigation.
Picha Ya Kwanza Ya Solar Pond

Picha Ya Pili Ya Solar Pond

Hii Ndiyo Solar Pond ambayo Wataalamu Wanatumia Maji Yaliyopigwa na Jua katika kutengeneza UMEME. Allahu Akbar. Je unaona Aya Ya Kuruani inavyosema kuhusu bahari mbili ya maji matamu na ya chumvi. Baina ya maji haya ya cumvi na matamu kuna sehemu inayojulikana kama Barzakh (Transit) na sehemu hii inasaidia maisha ya viumbe vinavyoishi katika sehemu hizo kuhama kwa kupitia hapo mpaka wanapozoea mazingara hayo na kisha watahamia upande wowote bila tatizo na siyo moja kwa moja kwani ni hatrari. Hapo katikati (Barzakh) maji yana chumvi ya katikati siyo kwa wingi wa kuleta madhara na siyo kidogo sana. Habari hii ni kweli. Angalia Picha hizi na Faida yake.
HUU MLANGO UPO WAZI NA MWENYEEZI MUNGU AKIPENDA BADO UNAENDELEA