UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
28/08/2022
Jumapili Jioni. Alhamdulilah Ninashukuru Mwenyeezi Mungu kunipa Nafasi hii kuwaletea Muujiza Mzuri kutoka katika Hotuba Na Mwongozo wa Mwenyeezi Mungu.
Hotuba Hiyo na Mwongozo huu hakuna mwingine isipokuwa Maneno Yake Matukufu yaliyohifadhiwa katika Kitabu Kitukufu cha Msahafu.
Mlango huu nimeuita Changamoto yaani Challenge
Mwenyeezi Mungu anawapa Viumbe Vyake Mtihani.
Kwa hiyo nitakusanya katika mlango huu kila Aya zinazohusu Changamoto
Na kwa kweli Makafiri Kuanzia Kushushwa kwa Kuruani Wamefeli Mitihani iliyotolewa Na Muumba
Makaburini kuna Vilio na Siku ya kiyama pia kuna Vilio. (Mwenyeezi Mungu atuepushie na Kutusamehe makosa na madhambi yetu).
Hebu Tuchunguze na Tuielekeze darubini yetu katika Aya Ifuatayo:
قُلْ لَئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنْسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَنْ يَأْتُوا بِمِثْلِ هَذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا
TAFSIRI
88. Sema “Hata wakijikusanya watu (wote) na majinni ili kuleta mfano wa hii Qurani basi hawangaliweza kuleta mfano wake; hata kama watasaidiana (vipi) wao kwa wao.,
SHEREHE
Aya hii ni mtihani mkubwa. Mwenyeezi Mungu aliyeumba kila kitu anatuambia kwamba Sisi Binaadamu wote tungekusanyika na Majini yote na kisha tukasaidiana kuandika Maandhishi mfano wa Kuruani basi tungelifeli. Hebu fikiri mtihani huu. Na kweli miaka zaidi ya Elfu imepita na hakuna aliyeweza kufanya hivyo.
Yaani Profesa wa Duniani ambao wana Elimu mbalimbali, Walio na PHD’s au Diploma nyinginezo mbalimbali wangekusanyika na kisha Majini yenye Elimu pia na wote wangefanya kazi kwa umoja kujaribu kutunga mfano wa Kuruani basi wasingeliweza kabisa. Kwa kweli huu sio Mtihani mdogo.
Hakuna aliyeweza na atakayeweza hata tufanye juhudi zote. Ujanja wetu na mali zetu zote zingetumika kwa kazi hii pia Ingelifeli.
MUUJIZA
Hebu Tuichunguze Mfumo au Structure tu ya Aya hii tuone Mpangilio wake wa Kiherufi na Kimaneno.
قُلْ لَئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنْسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَنْ يَأْتُوا بِمِثْلِ هَذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا
Kipande Cha Aya Kabla ya neno الْقُرْآنِ Kuruani kina Herufi 38
قُلْ لَئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنْسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَنْ يَأْتُوا بِمِثْلِ هَذَا
——————————–
Na Kipande Cha Aya Baada ya neno الْقُرْآنِ kina herufi 32
لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا
——————
Sasa tukigeuza Herufi hizi katika namba.
(Kama nilivyoelezea katika sehemu nyinginezo za Website hii kwamba Lugha ya Kiarabu inajulikana kama Alphanumeric kama lugha nyinginezo (kama vile Hebrew) za sehemu hiyo na wakati huo wa karne ya 7)
Wakati huo Kulikuwa hakuna Namba kama hizi tunazotumia leo na kwa hiyo Herufi zilitumika kama Namba. Kwa mfano
Herufi Alif Iliwakilisha Namba 1
Herufi Baa Iliwakilisha Namba 2
Herufi Taa iliwakilisha Namba 3
Na hivyo hivyo herufi zote zilipewa Namba.
Herufi Sin iliwakilisha Namba 60
Herufi Ghain iliwalilisha Namba 1000
Nitaishia Hapa kwani Nilikwisha Elezea Sehemu nyingine ya Website hii. Kitu muhimu uelewe Madhumuni Ya habari hii).
Nitazinukulu tena Vile Vipande vya Aya kisha tuone Maajabu yanayofuata:
1/قُلْ لَئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنْسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَنْ يَأْتُوا بِمِثْلِ هَذَا
——————————–
Na Kipande Cha Aya Baada ya neno الْقُرْآنِ kina herufi 32
2/ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا
——————
Ukigeuza Kipande cha kwanza katika Namba za hapo zamani utapata Jumla ya namba hizo ni 3214
Na Ukigeuza Kipande cha pili katika Namba za hapo zamani utapata Jumla ya namba hizo ni 4123
Hebu Angalia Namba Hizi Mbili zinavyoshangaza.
4123 3214
Ngoja nizipange Chini ya Aya tuone Maajabu
قُلْ لَئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنْسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَنْ يَأْتُوا بِمِثْلِ هَذَا/ الْقُرْآنِ / لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ
4123 3214
كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا
Angalia Namba Hizi Mbili.
Namba ya Pili ni kinyume ya Namba ya Kwanza. 4213 na kisha 3124 yaani Kinyume chake.
Hebu fikiri maajabu ya mpangilio huu. Hebu waza. Kuna siri gani imefichika hapa. Allahu Akbar.
Yaani Vipande vya Aya hivi ni kama
MABAWA YA KIPEPEO.
Mabawa Mawili ya Kipepeo yanafanana kila kitu. na pia Mfano mwingine ni Viungo vyako ninavyofanana. Mkono wa Kulia na Mkono wa Kushoto. Jicho la kulia na Jicho la Kushoto. Mguu wa kulia na Mguu wa Kushoto. Sikio la kulia Na Sikio la Kushoto ni sawa na Mfano huu wa mabawa ya Kipepeo.
Ukiwa Mchoraji utaelewa habari hii vizuri zaidi. Wasanii wanajua ufundi huu vizuri wanapochora.
Aya hii ina Neno KURUANI Katikati na Kila Upande wa neno KURUANI kuna Vipande vya Aya vinavyofanana kinamba. haya Maajabu ya kweli.
Je binaadamu anaweza kutunga Mfano huu. Huu ni mfano mmoja tu lakini kuruani ambayo haina mwisho wa maajabu. Kuna Mifano isiyo na mwisho.
Hii ndiyo Changamoto. Ni Jamba Jamba kama wanavyosema katika Kiswahili.
Hebu tuchunguze idadi ya Maneno na Herufi katika Aya Hii
قُلْ لَئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنْسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَنْ يَأْتُوا بِمِثْلِ هَذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا
Jumla Ya Maneno ni 19 na Herufi ni 76
Angalia Maajabu.
Herufi 76 ni sawa na 19 + 19 + 19 + 19 yaani 19 mara 4
Hebu fikiri mbona namba 19 imekariri hapa.
Allahu Akbar.
Je Namba 19 ni sawa na 1 + 9=10
na 10 ni sawa na 1 +0=1
Namba 1 Inamwakilisha Mwenyeezi Mungu peke yake? Mimi Najiuliza Suali?
Hebu Kumbuka Katika Sura Ya Al-MUdathir Mwenyeezi Mungu ameitaja Namba hii 19.
Mwenyeezi Mungu amesema katika Sura Ya Al-Mudathir Kwamba Amejaalia Waangalizi (Malaika) katika Moto wa Jahannam kuwa 19 na akaendelea kuuliza Kwa nini amejaalia hao Malaika kuwa 19?
Akajibu kwamba Namba hii ni kuwazidishia Imani Waumini. Na Akasema pia Kwamba Namba Hii itawavutia Watu wa Vitabu (Wakristo na Mayahudi) waukubali Uislamu na Pia Namba hii itawafanya Makafiri wababaike na kujiuliza
“Kwa nini Mwenyeezi Mungu amejaalia Malaika Hao kuwa 19?”
Ukifikiri sana utaona Maajabu sana Tena sana.
Aya ya Basmala pia inaherufi 19
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
Sura Ya Kwanza Kushuka ni AL-Alaq nayo ni Ya 19
Aya zake ni 19
Aya za Mwanzo kushuka za Sura Hii ya Al-Alaq ni
اقرا باسم ربك الذي خلق خلق الانسن من علق اقرا وربك الاكرم الذي علم بالقلم علم الانسن ما لم يعلم
Na Herufi zake ni 76
Na namba 76 ni sawa na 19 x 4
yaani 19 + 19 + 19 +19
Hebu fikiri maajabu haya yasiyo na mwisho.
Sasa nakuachia mwenyewe ufikiri.
Chukua Keki na Chai kunywa kwa Raha yako kisha Rudi usome haya kwa Raha Yako na ufikiri. Hakuna Haraka. Pole Pole.
Kwa leo naishia Hapa.
Miujiza Inaendelea kilicho muhimu ni Uzima.