UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MASUALA MAGUMU NA KUFELI KWA SAYANSI
Saturday 23 April 2022=22 Ramadan 1443
Historia ya Sayansi ni Ndefu. Sayansi ni Elimu ndogo Miongoni mwa Elimu mbali mbali za Kudunia. Matawi Yote ya Sayansi kama vile Formal Sciences (Hesabati na Logic etc), Natural Scienses (Physics, Biology, Chemistry etc) na Social Sciences (Sociology Psychology etc.) yamefeli kutatua Changamoto zilizotoka kwa Mwenyeezi Mungu. Na Huu ndiyo ukweli kwani yeye ndiye aliyeumba Sayansi hiyo na kwa hiyo amefanya iwe hivyo. Hakuna anayeweza kujigamba kwamba Kuna Elimu itakayoweza kujibu Changamoto ziliyotolewa na Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Baadhi ya Aya za Kuruani zifuatazo zinahusiana na Mitihani hiyo. Hakuna awezaye kupinga yaliyomo katika Aya hizi isipokuwa Mjinga na Mwongo. Ukichunguza historia ya Sayansi kuanzia hapo zamani, Miaka ya katikati mpaka kupitia kipindi cha Renaissance na baada ya hapo Kipindi cha Mapinduzi ya Kisayansi Na Mpaka Sasa katika kipindi cha Maendeleo ya Kisayansi hutapata Jawabu ya Changamoto zilizopo katika Aya Chache hapa chini. Hakuna aliyeweza kujibu masuala haya.
KUFELI KWA SAYANSI KATIKA KUTATUA MASUALI YA GHAYB
Sura Ya Al-Haj namba 22 Aya Namba 73
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ۬ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُ ۥۤۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَن يَخۡلُقُواْ ذُبَابً۬ا وَلَوِ ٱجۡتَمَعُواْ لَهُ ۥۖ وَإِن يَسۡلُبۡہُمُ ٱلذُّبَابُ شَيۡـًٔ۬ا لَّا يَسۡتَنقِذُوهُ مِنۡهُۚ ضَعُفَ ٱلطَّالِبُ وَٱلۡمَطۡلُوبُ (٧٣)
TAFSIRI
73.Enyi watu! unapigwa mfano, basi usikilizeni; hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu hawawezi kuumba (hata) nzi, na hata wakikusanyika kwa jambo hili. Na kama nzi akiwanyang’anya kitu hawawezi kukipokonya kwake. Amedhoofika kweli kweli huyu anayepokonya na aliyepokonywa.
SHEREHE NA MAONI
Mwenyeezi Mungu anatoa mfano na anatunasihi tuusikilize vizuri. Mfano Uliotolewa ni wa Nzi. Mwenyeezi Mungu anasema kwamba wale wenye kuabudu Mizimu, Mashetani, Masanamu, Jua, Moto na Kiumbe chochote katika Viumbe Vyake wanapoteza wakati wao bure kwani hivyo Viumbe vyake havina uwezo wowote wa kuumba chochote hata Kadudu kadogo kama vile “Nzi”. Kwa hiyo Kinachoabudiwa Ni Dhaifu na Pia Wenye Kuabudu Viumbe hivyo pia ni Dhaifu Mno. Binaadamu katika Dunia Nzima pamoja na Viumbe vinginevyo vyote Ulimwenguni wakikusanyika pamoja na kusaidiana basi hawataweza Kuumba hata Kadudu kadogo kama vile “Nzi”. Tangu Kuumbwa kwa Dunia Mpaka mwisho wa dunia hakuna aliyeweza na atakayeweza kufanya hivyo. Huu siyo mtihani mdogo. Ni Mtihani Mkubwa mno. Hebu fikiri mwenyewe. Maprofesa wa dunia nzima wanashindwa kuumba kadudu kadogo kama vile “Nzi”. Ukifikiri sana utaona Kwamba binaadamu ni Dhaifu Mno. Na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu anasema hapa ضَعُفَ ٱلطَّالِبُ وَٱلۡمَطۡلُوبُ (Dhau’fa Atwalibu Walmatluwb) Kwamba amedhoofika Binaadamu huyo ambaye Nzi atakaponyakua Chakula Chake hataweza Kumshika na kukipata tena chakula hicho na Pia amedhoofika Nzi yule pia kwa udogo wake. Sayansi za leo zinatuambia kwamba Nzi anapotua katika kitoweo chochote basi anakipulizia aina na sumu ambayo inakiharibu chakula hicho hapo hapo na inathibitisha habari hii kwamba hata kama utamshika Nzi huyo basi ukichunguza chakula hicho hakitafaa tena kwani kimepuliziwa aina ya Sumu ambayo imekiharibu na hakitafaa tena.
Sura Ya A;-Israa Namba 17 Aya Namba
85 وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلرُّوحِۖ قُلِ ٱلرُّوحُ مِنۡ أَمۡرِ رَبِّى وَمَآ أُوتِيتُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِ إِلَّا قَلِيلاً۬ (٨٥)
TAFSIRI
85.Na wanakuuliza habari ya roho. Sema:”Roho ni jambo lililohusika na Mola wangu(Mwenyezi Mungu). Nanyi hamkupewa katika ilimu(ujuzi) ila kidogo kabisa. (Nayo ni ilimu ya vitu visivyohusika na roho).
SHEREHE NA MAONI
Roho ni Uhai. Bila ya Roho hakuna uhai. Binaadamu wamejiuliza na wameuliza maswali mbalimbali kuhusiana na Roho. Hakuna aneyejua Roho ni kitu gani. Mtume Mohamad ﷺ alipoulizwa Roho ni kitu gani Mwenyeezi Mungu akashusha Aya hii inayosema kwamba Roho ni Jambo lake Mwenyeezi Mungu na hakumfundisha Binaadamu habari hiyo. Ni Siri Kubwa hakuna Anayejua au Atakayejua Mpaka Mwenyeezi Mungu akipenda. Na Mwenyeezi Mungu katika Aya hii anasema kwamba وَمَآ أُوتِيتُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِ إِلَّا قَلِيلاً۬ yaani “Sikukupeni Elimu Bali Kidogo” Kuna Mengineyo ambayo Mwenyeezi Mungu hakutufunulia. Na hata Maprofresa wa Dunia Nzima na Elimu zao zote wakikusanyika na kusaidiana kutaka kuisoma Roho hawataweza na wakifanya hivyo watakuwa wakipoteza wakati bure.
Sura Ya Luqman Namba 31 Aya Namba 34
إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُ ۥ عِلۡمُ ٱلسَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ ٱلۡغَيۡثَ وَيَعۡلَمُ مَا فِى ٱلۡأَرۡحَامِۖ وَمَا تَدۡرِى نَفۡسٌ۬ مَّاذَا تَڪۡسِبُ غَدً۬اۖ وَمَا تَدۡرِى نَفۡسُۢ بِأَىِّ أَرۡضٍ۬ تَمُوتُۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرُۢ (٣٤)
Kwa hakika ujuzi wa Kiama uko kwa Mwenyezi Mungu tu; naye Huteremsha mvua (wakati autakao), na anayajua yaliyomo matumboni(mwa viumbe wa kike-kuwa watazaa au hawazai, na watazaa wanaume au wanawake au wengi au kidogo. Hakuna anayejua isipokuwa yeye tu Mwenyezi Mungu); na nafsi yoyote haijui ni nini itachuma kesho, wala nafsi haijui itafia ardhi gani. Bila shaka Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi(ndiye) Mwenye habari (ya mambo yote).
SHEREHE NA MAONI
Katika Aya Hii Mwenyeezi Mungu anataja Mambo matano ambayo hakuna ayajuae isipokuwa yeye peke yake.
1/Kwanza ni Siku Ya Kiama hakuna Anayejua Tarehe ya Siku hiyo
2/Pili yeye ndiye anayejua Wapi na wakati utakaoshuka Mvua. Yaani yeye ndiye anayepanga Wapi kuwe na Mawingu ya Mvua na Wakati wa kushuka mvua hiyo na kadiri yake.Sayansi za leo zinasomea Mawingu ili kujua mvua itakaposhuka na wakati lakini Sayansi imefeli kujua kabla ya Mawingu hayo ya Mvua na pia mengi mengineyo.
3/Tatu hakuna anayejua yaliyomo Katika Matumbo ya Kizazi isipokuwa Mwenyeezi Mungu peke yake. Tabia, na Mengi mengineyo hakuna anayeweza kujua. Ijapokuwa Sayansi kwa kutumia Vyombo inaweza kujua yaliyo juu juu lakini kwa kweli hawawezi kujua mengi yaliyofichika kuhusu kiumbe (kama vile maisha atakapozaliwa kiumbe hicho) katika tumbo la kizazi.
4/Nne hakuna anayeweza kujua Utakachochuma katika maisha. Nani anayeweza kujua yatakayokuja? kwa kweli hakuna atakayeweza kujua chochote isipokuwa Mwenyeezi Mungu peke yake. Riziki yako na Mengi Mengineyo huwezi kuyajua.Huwezi kujua utachuma nini kesho.
5/Tano hakuna atakayejua Wakati na Sehemu ya Ardhi utakayofariki Dunia. Hakuna anyeweza kujua Siku hiyo isipokuwa Mwenyeezi Mungu peke yake na hii ndiyo Elimu ya Ghayb. Mwenyeezi Mungu hakumfunulia Yeyote na hata Mitume.
Hii ni Siri yake peke yake. Na huwezi kumwuuliza Kwa nini. Kwani yeye ndIye aliyekuumba na ndiye aliyeamua ibakie siri. Allahu Akbar.
PEPO, MOTO WA JAHANNAM, MALAIKA, MASHETANI
Viumbe vyote hivi kama vile Malaika na Sheitani, Na Maumbile yote kama vile Moto wa Jahannam na Pepo hakuna anayeweza kuvijua isipokuwa yale yaliyoelezwa katika kuruani na Hadithi za Mtume Mohamad ﷺ lakini Sayansi Imefeli kutuelezea Elimu Inayohusiana na Viumbe au Maumbile kama Haya. Allahu Akbar
CHANGAMOTO ZINAENDELEA……….