UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
DARASA KILA IJUMAA
MLANGO HUU UTAKUSANYA AYA ZA KURUANI, HADITHI ZA MTUME MOHAMAD ﷺ NA HADITHI ZA QUDSIY AMBAZO NI KAULI YA MWENYEEZI MUNGU KUTAKUWA NA TAFSIRI NA SHEREHE ZAKE
23/09/2022
SUALA LA KWANZA
Alhamdulilah leo ni siku tukufu. ni ijumaa. Mwenyeezi Mungu akipenda katika Mlango huu nitakuwa nikiwaletea vipande vidogo vidogo vya kila zuri. kwanza Vipande hivi vitaninasihi mimi mwenyewe na pia wewe msomaji wa Website hii. Kwa hiyo nakukaribisha kwa Salaam Tukufu inayosema.
“Salaam Nyingi kwenu, Rehema na Baraka Za Mwenyeeezi Mungu Ziwafikieni popote mlipo”
Mwenyeezi Mungu akipenda Siku za Ijumaa Nitaweka Kipande kimoja na Nitakitia Namba na kwa hiyo leo nitaanza na Namba Moja.
1/Kipande cha leo ni Hadithi Ya Qudsiy ambayo Ina nasiha Nzuri sana.
Kuna Tofauti baina ya Sunnah Za Mtume ﷺ na Hadithi za Qudsiy ambayo nilizungumzia katika Mlango wa “Elimu Za Kiislamu”. Kwa Kifupi Hadithi Qudsiy ni Ujumbe Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu lakini Imefikishwa kwetu kwa Lugha ya Mtume Mohamad ﷺ Yaani Maneno ni ya Mtume ﷺ lakini Ujumbe ni kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu. Na Kuruani ni Ujumbe kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu na Pia Lugha. Yaani Maneno ni Ya Mwenyeezi Mungu na Siyo yake Mtume.ﷺ Na Hadithi Za Mtume au Sunnah za Mtume ﷺ ni Mazungumzo na Vitendo vya Mtume ﷺ na Vile alivyokiri au alivyowakubalia Maswahaba zake.
Ngoja nifupishe hapa chini ili ieleweke vizuri:
1/Kuruani ni Ujumbe kutoka kwa Mwenyeezi Mungu Mtukufu na Maneno ni Yake.
2/Hadithi za Qudsiy pia ni Ujumbe Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu lakini kwa Maneno ya Mtume Mohamad ﷺ
2/Hadithi za Mtume ﷺ ni Kila alichosema, kutenda na vile vitendo alivyowakubalia Maswahaba zake. ukichunguza utaona Hadithi za Qudsiy zinaishia Na “Alisema Mwenyeezi Mungu” na Hadithi za Sunnah au za Mtume Mohamad ﷺ zinaishia na “Alisema Mtume”.
Je imeeleweka? Inshaallah Itaeleweka.
Katika Siku ya leo nitawaletea Hadithi Qudsiy.
Hadithi Hii ipo katika Volume au Kitabu cha Sunan Ya Tirmidhiy
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَقُولُ يَا ابْنَ آدَمَ تَفَرَّغْ لِعِبَادَتِي أَمْلَأْ صَدْرَكَ غِنًى وَأَسُدَّ فَقْرَكَ وَإِلَّا تَفْعَلْ مَلَأْتُ يَدَيْكَ شُغْلًا وَلَمْ أَسُدَّ فَقْرَكَ
2466 سنن الترمذي كتاب صفة القيامة والرقائق والورع باب منه
Hadithi Hii iliyotajwa na Abu Hurayra na ambayo inatokana na Mtume Mohamad ﷺ inasema kwamba
“Mwenyeezi Mungu anasema Ewe Binaadamu Fanya Ibada kwangu na mimi nitajaza Moyo wako na Utajiri na pia nitakuondolea Ufakiri na kama hutafanya haya basi nitajaza Mikono yako na Shughuli zisizo na mwisho na sitakuondolea Ufakiri.
ENGLISH
Abu Huraira reported: The Prophet, peace and blessings be upon him, said, “Allah Almighty said: O son of Adam, be free for My worship and I will fill your heart with riches and alleviate your poverty. If you do not do so, I will fill your hands with problems and never alleviate your poverty.”
SHEREHE
Ukifikiri Hadithi hii utaona mifano hii kila mara katika maisha. Wakati Binaadamu anashughulika na kazi sana usiku na mchana lakini mapato hayatoshi kujilipia Gharama za maisha. Kazi mchana na usiku lakini mapato hayana Baraka, na shida zipo pale pale haziishi. kazi zinafanyika kwa juhudi zote lakini bado ufakiri hauondoki. Na Mtu anajikuta anazunguka kama Pia, Na mahangaiko yasiyo na mwisho. Haya Mambo yapo kila siku katika maisha yetu na siyo geni. Na Iwapo mtu akafanya Ibada iliyo ya kweli na kujishughulisha na Yale yanayomridhisha Mwenyeezi Mungu basi kazi hazimchokeshi mtu na Mapato yatakuwa na Baraka. Yaani Mapato yatazidi na Kwa kweli huu ni ukweli ambao tunauona kila siku katika Maisha.
Mwenyeezi Mungu tutakutana tena siku ya Ijumaa na Mapya………….