UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MAPYA KILA WIKI
MLANGO HUU UTAKUSANYA AYA ZA KURUANI, HADITHI ZA MTUME MOHAMAD ﷺ NA HADITHI ZA QUDSIY AMBAZO NI KAULI YA MWENYEEZI MUNGU KUTAKUWA NA TAFSIRI NA SHEREHE ZAKE
24/09/2022
SUALA LA KWANZA
Alhamdulilah Mwenyeezi Mungu akipenda katika Mlango huu nitakuwa nikiwaletea vipande vidogo vidogo vya kila zuri. kwanza Vipande hivi vitaninasihi mimi mwenyewe na pia wewe msomaji wa Website hii. Kwa hiyo nakukaribisha kwa Salaam Tukufu inayosema. “Salaam Nyingi kwenu, Rehema na Baraka Za Mwenyeeezi Mungu Ziwafikieni popote mlipo” KIla Wiki Nitaweka Baadhi Ya Mambo ya Dini kwa Namba na Tarehe. kwa hiyo leo nitaanza na Namba Moja. Na Kabla ya kuendelea ningependelea kuelezea Tofauti kati ya Kuruani, Hadithi za Mtume na Hadithi za Qudsiy.
Kuna Tofauti baina ya Sunnah Za Mtume ﷺ na Hadithi za Qudsiy ambayo nilizungumzia katika Mlango wa “Elimu Za Kiislamu”. Kwa Kifupi Hadithi Qudsiy ni Ujumbe Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu lakini Imefikishwa kwetu kwa Lugha ya Mtume Mohamad ﷺ Yaani Maneno ni ya Mtume ﷺ lakini Ujumbe ni kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu. Na Kuruani ni Ujumbe kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu na Pia Lugha. Yaani Maneno ni Ya Mwenyeezi Mungu na Siyo yake Mtume.ﷺ Na Hadithi Za Mtume au Sunnah za Mtume ﷺ ni Mazungumzo na Vitendo vya Mtume ﷺ na Vile alivyokiri au alivyowakubalia Maswahaba zake. Ngoja nifupishe hapa chini ili ieleweke vizuri:
1/Kuruani ni Ujumbe kutoka kwa Mwenyeezi Mungu Mtukufu na Maneno ni Yake.
2/Hadithi za Qudsiy pia ni Ujumbe Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu lakini kwa Maneno ya Mtume Mohamad ﷺ
3/Hadithi za Mtume ﷺ ni Kila alichosema, kutenda na vile vitendo alivyowakubalia Maswahaba zake. ukichunguza utaona Hadithi za Qudsiy zinaishia Na “Alisema Mwenyeezi Mungu” na Hadithi za Sunnah au za Mtume Mohamad ﷺ zinaishia na “Alisema Mtume”. Je imeeleweka? Inshaallah Itaeleweka.
Siku ya Leo Aya mbili ningependelea kuzifasiri ni kutoka Katika Sura Ya Mohamad ﷺ Namba 18 na 19
فَهَلْ يَنْظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَنْ تَأْتِيَهُمْ بَغْتَةً فَقَدْ جَاءَ أَشْرَاطُهَا فَأَنَّى لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ ﴿۱۸
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنْبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَاللَّهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ وَمَثْوَاكُمْ ﴿۱۹
TAFSIRI
18. Kwani wanangoja jingine ila Kiama kiwajie kwa ghafula? Basi alama zake (Hicho Kiama) zimekwisha kuja. Kutawafaa wapi kukumbuka wakati kitakapowajIa?
19. Jua ya kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na (dhambi) za Waislamu wanaume na Waislamu wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi na mahali penu pa kukaa.
SHEREHE
Aya namba 18 inatujuulisha kuhusu Siku ya Kiyama. Aya inatuambia kwamba Alama za Siku ya Kiyama zimeshatokea. Neno أَشْرَاطُهَا maana yake ni Alama Zake. Kuna Hadithi za Mtume Mohamad ﷺ ambazo zimekusanya Habari za Alama Za Siku ya Kiyama na Baadhi ya Wanavyuoni wa Kiislamu wameandika Vitabu Vinavyohusu Alama hizi. Alama Zipo Nyinginezo na mojawapo ya Alama hizi ni Kuja Kwa Mtume Mohamad ﷺ na Ujumbe wa Mwisho wa Kuruani. Nimetaja baadhi chache katika Mlango wa “ALAMA ZA KIYAMA” lakini kuna nyinginezo ambazo bado kuzielezea.Iwapo nitazielezea itakuwa katika Mlango huo na siyo hapa. Katika Mlango huu nimegusia tu habari hii katika kuifasiri Aya ya Kuruani Tukufu.
Mwenyeezi Mungu anatuambia kwamba Kiyama Kimeshafika yaani kipo karibu sana lakini binaadamu wengi hawajui na wengine hawaamini. Alama hizi zinathibitisha habari hii. Na kuna Hadithi ya Mtume ﷺ ambayo inataja na kufafanua Aya hizi inayosema:
Reference : Sahih al-Bukhari 5301
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، قَالَ أَبُو حَازِمٍ سَمِعْتُهُ مِنْ، سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ السَّاعِدِيِّ صَاحِبِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم “ بُعِثْتُ أَنَا وَالسَّاعَةَ كَهَذِهِ مِنْ هَذِهِ أَوْ كَهَاتَيْنِ ”. وَقَرَنَ بَيْنَ السَّبَّابَةِ وَالْوُسْطَى.
TAFSIRI
Suhail Ibn Saiid Asaadiy Swahaba Wa Mtume ﷺ alisema: “Alisema Mtume ﷺ Kwamba Ujumbe wangu na Siku ya Kiyama ni sawa na Hivi viwili. (Baada ya maneno haya) Akaonyesha Vidole vyake viwili. Yaani Vidole viwili vya Mwanzo.(Index and Middle Finger)na (Ukaribu wa Vidole hivi viwili unaonyesha Muda wa Kukaribia kwa Siku ya Kiyama kwamba ni Mfupi sana)
TRANSLATION
Narrated Sahl bin Sa`d As-Sa`idi who was a companion of Allah’s Messenger. That The (ﷺ)) Allah’s Messenger (ﷺ), holding out his middle and index fingers, said, “My advent and the Hour’s are like this (or like these),” namely, the period between his era and the Hour is like the distance between those two fingers, i.e., very short.
Na Aya Namba 19 Inatupa muongozo wa Kufanya kabla ya Siku hiyo ya Kiyama. Kwanza Tuelewe kwamba hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mwenyezi Mungu. Tunanasihiwa Tuombe Maghfira yaani Msamaha na pia kuwaombea Waumini wengineo. Na pia Mwenyeezi Mungu anatutahadharisha kwamba Hakuna kinachofichika kwani Harakati zetu zote zinaonekana na sehemu tunazoishi duniani Pia zinaonekana na kwa hiyo tusifikiri Maasi yetu ya kificho hayataonekana. Tunanasihiwa tujiandae kwa ibada. Na Kama inavyoeleweka KIla zuri ulifanyalo ni Ibada. Kufanya kazi kwa njia ya Halali ili kusaidia Familia yako ni Ibada. Ibada siyo Sala tu Msikitini bali ina maana kubwa sana.
25/09/2022
SUALA LA PILI
Alhamdulilah Leo Jumapili na siku iliyotulia vizuri. Hali ya hewa ni shwari isipokuwa kuna baridi kidogo. Kama nilivyoahidi kwamba ninapopata nafasi na Mwenyeezi Mungu anapopenda basi nitafanya Darasa kila siku. Kwa hiyo leo nitaleta baadhi ya Aya za kuruani na kisha tuzifasiri. Ni Aya chache lakini zina maana kubwa. Na siwezi kujigamba kwamba Tafsiri hii inatosha. kwa kweli Kuruani ni Muujiza mkubwa sana na Aya zake zina mengi. Na faida zake hazina mwisho mpaka siku ya kiyama. Kwa hiyo tupate faida angalau tonye moja katika Bahari katika haya machache ninayowaletea. Allahu Akbar.
Nimechagua Baadhi ya Aya kutoka katika Sura Ya Al-Maarij. Kuanzia Aya namba 6 Mpaka Aya namba 18
سُوۡرَةُ المعَارج
إِنَّہُمۡ يَرَوۡنَهُ ۥ بَعِيدً۬ا (٦) وَنَرَٮٰهُ قَرِيبً۬ا (٧) يَوۡمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلۡمُهۡلِ (٨) وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ (٩) وَلَا يَسۡـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمً۬ا (١٠) يُبَصَّرُونَہُمۡۚ يَوَدُّ ٱلۡمُجۡرِمُ لَوۡ يَفۡتَدِى مِنۡ عَذَابِ يَوۡمِٮِٕذِۭ بِبَنِيهِ (١١) وَصَـٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ (١٢) وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِى تُـٔۡوِيهِ (١٣) وَمَن فِى ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعً۬ا ثُمَّ يُنجِيهِ (١٤) كَلَّآۖ إِنَّہَا لَظَىٰ (١٥) نَزَّاعَةً۬ لِّلشَّوَىٰ (١٦) تَدۡعُواْ مَنۡ أَدۡبَرَ وَتَوَلَّىٰ (١٧) وَجَمَعَ فَأَوۡعَىٰٓ (١٨)
Kwanza ningeleta Tafsiri ya Aya hizi na kisha Nitafanya Sherehe.
TAFSIRI
6.Kwa hakika wao wanakiona kiko mbali (hicho Kiama)
7.Nasi tunakiona kiko karibu.
8.Siku mbingu zitakapokuwa kama shaba iliyoyayuka
9.Na milima itakuwa kama sufi (inayoruka)
10.Wala jamaa hatamuuliza jamaa (yake).
11.(lngawa) watafanywa waonane. Mwenye kosa atatamani ajikomboe katika adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa watoto wake
12.Na mke wake na ndugu yake
13. Na jamaa zake waliomzunguka kwa kila upande
14.Na (kuvitoa) vyote vilivyomo katika ardhi, kisha aokoke
15. Lakini wapi! Kwa hakika huo ni Moto uwakao (barabara)
16.Unaobabua mara moja ngozi ya mwili.
17. Utamwita kila aliyegeuza mgongo na akageuka (kuyatupa mafunzo ya Qurani)
18.Na akakusanya (mali), kisha akayahifadhi (bila ya kuyatolea Zaka wala sadaka).
SHEREHE
Ndugu Waislamu Aya hizi chache zinatisha sana. Tunaambiwa kwamba Kiyama hakiko mbali. Mbingu itageuka rangi na kuwa kama shaba iliyoyayuka na milima itapondeka pondeka na kuwa kama sufi Siku hiyo kila mtu atakuwa na lake. Hakuna atakayemkumbuka mwingine. Ijapokuwa watu wanaojuana watakuwa wakionana lakini siku hiyo inavyotisha watu hao hawatakumbukana tena. Inaonyesha kwamba Akili zitaruka kwa Adhabu ya Moto wa Jahannam.
Mwenyeezi Mungu anaelewa yatakavyokuwa siku hiyo ya Kiyama na yatakayopita katika Fikra zetu na kwa hiyo anatuelezea Fikra hizo kwa kusema kwamba:
Moto Huo (Mwenyeezi Mungu atuepushie) Utakuwa wa Hatari sana kiasi ambacho Mtu atatamani atoe chochote ili ajikomboe. Mtu huyo ambaye amefeli Mitihani ya Dunia atatamani arudi Duniani ili afanye yale aliyokuwa akipewa Usia na Manabii. Atatamani alipe chochote ili akombolewe na asiingie Moto huo. Atatamani Awatoe watoto wake wawe kama Fidia iliajiepushe na Adhabu hiyo ikiwa mtu huyo alikuwa na watoto Duniani. Atatamani Amtoe Mke wake iwapo alikuwa ameowa Duniani yaani Mke huyo awe Fidia na ili ajiepushe na Moto Huo. Na Pia Atatamani atoe Ndugu zake wote ili wawe Fidia na ajiepushe na Adhabu hiyo ya moto Mkali wa Jahannam. Lakini wapi haitafaa chochote. Moto unababua Miili na Utampata kila Kaidi aliyejiepusha na Usia wa Mitume ambaye tamaa yake ilikuwa kukusanya Mali tu na wala hatoi Sadaka Wala Zaka.
SUALA ALILOULIZWA SHEKHE WANGU
Siku Moja Shekhe wangu aliulizwa Suali Kuhusu Aya Hizi kwamba Je Mbona Kaidi huyu ambaye Yupo tayari kutoa Kila kitu Duniani ili iwe fidia na Pia yupo tayari kutoa watoto wake, Mke wake na Ndugu zake ili wawe fidia mbona hatakuwa Tayari kuwatoa Wazazi wake?
JIBU LA SHEKHE WANGU
Juu ya Ukaidi wa Binaadamu hatakuwa tayari kuwatoa Wazazi wake kama Fidia. Kwa sababu Atakumbuka Amri za Mwenyeezi Mungu katika Sehemu mbali mbali za Kuruani zinazohusu Kuwatii Wazazi na Pia Nasiha Za Manabii. Kuna Hadithi za Mtume ﷺ mbalimbali zinazohusia Kuwatii wazazi.
BAADHI AYA ZA KURUANI NA HADITHI ZA MTUME ﷺ ZINAZOHUSU KUWATII WAZAZI
Kwa Ufupisho nimechagua Aya Moja na Hadithi Mbili za Mtume. ﷺ Kwa kweli kuna Aya na Hadithi zaidi ya Moja.
Sura Ya Israa Namba 17 Aya Namba 23-24
۞ وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُ وَبِٱلۡوَٲلِدَيۡنِ إِحۡسَـٰنًاۚ إِمَّا يَبۡلُغَنَّ عِندَكَ ٱلۡڪِبَرَ أَحَدُهُمَآ أَوۡ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل لَّهُمَآ أُفٍّ۬ وَلَا تَنۡہَرۡهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوۡلاً۬ ڪَرِيمً۬ا (٢٣) وَٱخۡفِضۡ لَهُمَا جَنَاحَ ٱلذُّلِّ مِنَ ٱلرَّحۡمَةِ وَقُل رَّبِّ ٱرۡحَمۡهُمَا كَمَا رَبَّيَانِى صَغِيرً۬ا (٢٤)
TAFSIRI
23.Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yoyote ila Yeye tu. Na (ameagiza)kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee, (naye yuko) pamoja nawe, au wote wawili, ·basi usiwaambie hata (neno) Ah! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa heshima (kabisa).
24. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa (njia ya kuwaonea) huruma (kwa kuwaona wamekuwa wazee). Na useme: “Mola wangu! Warehemu ( wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto.”
HADITHI YA KWANZA YA MTUME ﷺ
Hadithi Ifuatayo kutoka katika Sahih Muslim. Hadithi Inayotokana na Mtume Mohamad ﷺ kupitia kwa Abdullah na Wengineo katika Isnadi niliyoitaja hapa Chini.
حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنِ الْحَسَنِ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِي عَمْرٍو الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ “ أَفْضَلُ الأَعْمَالِ – أَوِ الْعَمَلِ – الصَّلاَةُ لِوَقْتِهَا وَبِرُّ الْوَالِدَيْنِ ”
TAFSIRI
Vitendo vilivyo bora sana ni kuswali kwa Wakati na Kufanyia wema wazazi.
TRANSLATION
The best of’ the deeds or deed is the (observance of) prayer at its proper time and kindness to the parents.
HADITHI YA PILI YA MTUME ﷺ
Hadithi Ifuatayo kutoka katika Sahih Al-Bukhariy. Hadithi Inayotokana na Mtume Mohamad ﷺ kupitia kwa Abiy Bakra na Wengineo katika Isnadi niliyoitaja hapa Chini.
حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ الْمُفَضَّلِ، حَدَّثَنَا الْجُرَيْرِيُّ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي بَكْرَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ” أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَكْبَرِ الْكَبَائِرِ ”. قَالُوا بَلَى يَا رَسُولَ اللَّهِ. قَالَ ” الإِشْرَاكُ بِاللَّهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ ”.
Mtume Alisema Nikujuulisheni Dhambi Kubwa kuliko Zile kubwa (Mnazozijua)? Wakajibu Naam Ewe Mtume Wa Mwenyeezi Mungu.ﷺ (Ya Kwanza) Ni Kumshirikisha Mwenyeezi Mungu (kama vile kuabudu Masanamu na Mizimu na Mengineyo) Na (Ya Pili) Kuwafanyia Ukaidi Wazazi.
TRANSLATION
Allah’s Messenger (ﷺ) said, “Shall I inform you of the biggest of the great sins?” They said, “Yes, O Allah’s Apostle!” He said, “To join partners in worship with Allah, and to be undutiful to one’s parents. “
26/09/2022
SUALA LA TATU
Hadithi Ifuatayo ni Ya Qudsiy Imekubaliwa na kukusanywa katika vitabu vya Mashekhe Wawili: Ab-Bukhari na Al-Muslim. Hadithi Hii Ni Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu na Akatuelezea Mtume Mohamad ﷺ Kwa Lugha na Maneno Yake. Lakini Ujumbe ni wa Mwenyeezi Mungu. Kwa hiyo siyo Kuruani au Hadithi za Mtume Mohamad ﷺ bali Hadithi za Qudsiy.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ” كُلُّ عَمَلِ ابْنِ آدَمَ يُضَاعَفُ الْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا إِلَى سَبْعِمِائَةِ ضِعْفٍ قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: إِلَّا الصَّوْمَ فَإِنَّهُ لِي وَأَنَا أَجْزِي بِهِ يَدَعُ شَهْوَتَهُ وَطَعَامَهُ مِنْ أَجْلِي لِلصَّائِمِ فَرْحَتَانِ: فَرْحَةٌ عِنْدَ فِطْرِهِ وَفَرْحَةٌ عِنْدَ لِقَاءِ رَبِّهِ وَلَخُلُوفِ فَمِ الصَّائِمِ أَطْيَبُ عِنْدَ اللَّهِ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ وَالصِّيَامُ جُنَّةٌ وَإِذَا كَانَ يَوْمُ صَوْمِ أَحَدِكُمْ فَلَا يَرْفُثْ وَلَا يصخب وفإن سَابَّهُ أَحَدٌ أَوْ قَاتَلَهُ فَلْيَقُلْ إِنِّي امْرُؤٌ صَائِم “
TAFSIRI
Abiy Hurayra (Mwenyeezi Mungu Amridhie) alisema Alisema Mtume ﷺ :
Kila kitendo kizuri cha Binaadamu Kitalipwa Baina Ya Thawabu Mara 7 mpaka 700 Na Mwenyeezi Mungu Akasema Isipokuwa Saumu. Hiyo Imefanywa kwa ajili yangu na mimi nitatoa zawadi yake. Kwani Mtu ameacha Matamanio ya Nafsi na Chakula kwa ajili yangu. Mtu aliyefunga Saumu ana Furaha mbili. Ya kwanza ni wakati wa Kufuturu na ya pili atakapokutana na Mwenyeezi Mungu. Harufu ya Pumzi ya mtu aliyefunga ni nzuri kwa Mwenyeezi Mungu kuliko Manukato Ya Marashi.Kufunga Saumu ni Kujikinga (Na Maasi hapa duniani na Moto wa Jahannam) Na siku ya Kufunga itakapofika basi asitumie Lugha Mbaya (Ya Matusi au Chafu) na asipaze Sauti ya makelele atakapozungumza Na Mtu Yeyote. (Katika Mazingara yeyote au Kugombana).Na Mtu yeyote atapomkabili kwa Matusi au Ubaya wowote au atakapojaribu kupigana naye basi amuambie “Nimefunga” au Mimi Nimefunga” (Yaani ajiepushe na Ugomvi).
TRANSLATION
Abiy Hurayra reported God’s messenger as saying, “Every [good] deed a son of Adam does will be multiplied, a good deed receiving a tenfold to seven hundredfold reward. God has said, ‘With the exception of fasting, for it is done for my sake and I give a reward for it. One abandons his passion and his food for my sake.* The one who fasts has two occasions of joy, one when he breaks his fast and one when he meets his Lord. The bad breath of one who fasts is sweeter to God than the fragrance of musk. Fasting is a protection, [i.e. from acts of disobedience in this world and from hell in the next. Pt. vi.] and when the day of the fast of any of you comes he must not use vile language or raise his voice, and if anyone reviles him or tries to fight with him he should tell him he is fasting.”
SHEREHE
Baina Ya Thawabu 7 na 700 inategemea kitendo. Yaani Kitendo ndicho kitahukumu Tahwabu utakazozipata. Kitendo kikubwa utapata Thawabu zaidi ya 7. Kuhusu Saumu Thawabu zake ni kubwa zaidi ya 700 yaani Thawabu zake hakuna anayejua isipokuwa Mwenyeezi Mungu tu peke yake. Ni Thawabu (Special) ambayo kubwa. (Mwenyeezi Mungu atubariki tupate Thawabu hizo. Allahu Akbar).
27/09/2022
SUALA LA NNE
Hadithi iliyohadithiwa na Abdullah bin `Amr. Hadithi hii ipo katika Sahih Al-Bukhari. Ref 60
حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، عَارِمُ بْنُ الْفَضْلِ قَالَ حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ يُوسُفَ بْنِ مَاهَكَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ تَخَلَّفَ عَنَّا النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فِي سَفْرَةٍ سَافَرْنَاهَا، فَأَدْرَكَنَا وَقَدْ أَرْهَقَتْنَا الصَّلاَةُ وَنَحْنُ نَتَوَضَّأُ، فَجَعَلْنَا نَمْسَحُ عَلَى أَرْجُلِنَا، فَنَادَى بِأَعْلَى صَوْتِهِ “ وَيْلٌ لِلأَعْقَابِ مِنَ النَّارِ ”. مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلاَثًا.
TAFSIRI
Siku Moja Mtume alikuwa Nyuma yetu tulipokuwa safarini. Alipokuja akatukuta tupo katika kufanya Udhu wa Sala ambayo wakati wake umeshapita. Tulikuwa tukijipaka Maji kartika Miguu yetu kwa mikono iliyolowa(Tuliwa hatuioshi vizuri kama ipasavyo) kwa hiyo Mtume akatuambia kwa sauti kubwa karibu mara mbili au tatu “Okoeni mikono yenu kutoka katika moto” (Yaani Moto wa Jahannam)
TRANSLATION
Once the Prophet (ﷺ) remained behind us in a journey. He joined us while we were performing ablution for the prayer which was over-due. We were just passing wet hands over our feet (and not washing them properly) so the Prophet (ﷺ) addressed us in a loud voice and said twice or thrice: “Save your heels from the fire.”
SHEREHE
Hii Hadithi inatupa Nasiha ya kufanya Udhu kwa vizuri kama ipasavyo. Yaani Tuwe macho sana katika Ibada zetu zote. Na hasa Tohara. Tuhakikishe Nguo zetu ni safi kabla ya Sala. Tujiepushe na Najisi kama vile Chembe chembe za Mikojo na Uchafu wa aina yeyote ile. Kwani unapokwenda kusali ujue kwamba unakwenda kukutana na Muumba yaani Aliyeumba Ulimwengu au Malimwngu na Kila kitu na kwa hiyo siyo Mchezo. Tunaogopa Binaadamu wenzetu lakini hatuogopi aliyetuumba. Kwa hiyo Hadithi hii inatuonya tuwe macho katika Udhu na pia kuna Hadithi nyinginezo zinazohusu Tohara na Mengineyo.
05/11/2022
SUALA LA TANO
Jina la Mtume Mohamad limetajika katika kuruani katika Aya Nne zifuatazo:
1-{ وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ أَفَإِين مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَٰبِكُمْ وَمَن يَنقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَن يَضُرَّ اللَّهَ شَيْءًا وَسَيَجْزِي اللَّهُ الشَّٰكِرِينَ }
[آل عمران:144].
2-{ مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَٰكِن رَّسُولَ اللَّهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّنَ وَكَانَ اللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا } [الأحزاب:40].
3-{ وَالَّذِينَ ءَامَنُوا وَعَمِلُوا الصَّٰلِحَٰتِ وَءَامَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّءَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ } [محمد:2].
4-{ مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ تَرَىٰهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَٰنًا سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَىٰةِ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْءَهُ فَءَازَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ ءَامَنُوا وَعَمِلُوا الصَّٰلِحَٰتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا } [الفتح:29].
Katika Aya Hizi Nne kuna Aya Namba 3 ndiyo pekee inazungumzia WAHYI (Revelation) Yaani Kupewa Ujumbe kwa Mtume Mohamad ﷺ Aya hii Ipo katika Sura Ya Mohamad Aya Namba 2.
Ni Aya Namba 3 Hapa Juu na Tafsiri yake ni Kama ifuatavyo:
{ وَالَّذِينَ ءَامَنُوا وَعَمِلُوا الصَّٰلِحَٰتِ وَءَامَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّءَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ } [محمد:2].
TAFSIRI
1. Na wale walioamini na wakatenda mema na wakaamini yaliyoteremshwa juu ya Muhammad – nayo ni haki iliyotoka kwa Mola wao – hawa atawafutia makosa yao na atastawisha hali yao
SHEREHE NA MUUJIZA
Ahadi nzuri wanayopewa wacha mungu kwa malipo mema Duniani na Akhera. Kuhusu Muujiza ambao ningependelea kuuzungumzia ni Hesabu ya Herufi za Kipande cha Aya
وَالَّذِينَ ءَامَنُوا وَعَمِلُوا الصَّٰلِحَٰتِ وَءَامَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ
ambacho kinasema:
“Na wale walioamini na wakatenda mema na wakaamini yaliyoteremshwa juu ya.”
Kipande hiki ambacho kipo kabla ya Jina la Mtume Mohamad ﷺ kina Herufi 40. Kwa kweli inashangaza kwani mara ya kwanza kwa Mtume kuletewa WAHYI (Revelation) alikuwa na Umri wa Miaka 40!!!! Allahu Akbar. Huu ni Muujiza katika Miujiza Mingi ya Kuruani.
06/11/2022
SUALA LA SITA
SURA Ya Al-FIL (Tembo au Ndovu)
{ الم تر كيف فعل ربك باصحب الفيل (1) الم يجعل كيدهم في تضليل (2) وارسل عليهم طيرا ابابيل (3) ترميهم بحجاره من سجيل (4) فجعلهم كعصف ماكول (5) } [الفيل:1-5].
TAFSIRI
1.Je! Huoni jinsi Mola wako Alivyowafanya watu wenye ndovu?
2.Je! Hakujaalia vitimbi vyao kuharibika.
3.Na akawapelekea ndeqe makundi kwa makundi
4·Wakawapiga kwa mawe ya udongo wa kuchoma
5.Akawafanya kama majani yaliyoliwa (yakatapikwa)
KISA CHA KUSHUKA SURA HII.
Kisa hiki kilitokea kabla ya kuja kwa Mtume Mohamad Yaani kabla ya Kushuka kwa Kuruani Tukufu.
Sura hii inaeleza kisa kilichopita karibu ya Makka katika mwaka wa 570 A.C. Huko Yemen siku hizo ilikuwa imetawaliwa na Mahabashi.
Nao wakati huo walikuwa Masihia. (Wakristo) Liwalj wa Yemen aliyekuwa wakati huo hi Abraha.
Huyu Abraha alitaka kuwazuilia Waarabu wasiende Makka kuzuru Al-Kaaba (Mecca) kwa ajili ya Ibada za wakati huo kwa hiyo akajenga kanisa kubwa akalipamba vizuri katika mji wa S’anaa na akawalazimisha Waarabu wazuru kanisa hilo badala ya AI-Kaaba.
Atipokuwa hakufaulu, ndipo alipoazimia kwenda kuivunja AI-Kaaba huko Mecca na akakusanya Jeshi kubwa na yeye mwenyewe na baadhi ya watu wake wakapanda ndovu.
Na kwa sababu hiyo, mwaka ule Waarabu wakauita “Mwaka wa ndovuu, au “Mwaka wa wenye ndovu, nao ndio mwaka uliozaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.).
Abraha alipofika karibu ya Makka akawapelekea mtu Waarabu kuwapa habari kuwa yeye hakuja kuwapiga wao, bali haja yake ilikuwa wampe nafasi ya kuvunja AI-Kaaba!
Wakati huo Waarabu wa Makka hawakuwa na nguvu za kuweza kupigana wala hawakuwa na mfalme, lakini walikuwa na mkubwa wao aliyeitwa Abdul-Muualib, babu yake Mtume Muhammad (s.a.w.).
Abdul-Muttalib akawapa amri jamaa zake wore watoke mjini wende majabalini na yeye mwenyewe akaingia katika Al-Kaaba, akamuomba Mwenyezi Mungu ainusuru nyumba yake tukufu, kisha akenda huko waliko kwenda jamaa zake, kumtazama huyo atakayejaribu kupigana na Mwenyeezi Mungu na kumvunjia nyumba Yake.
Abraha, baada ya kujua kuwa Waarabu wamekwisha jitenga, akajiweka tayari kuingia Makka na kuvunia AlKaaba. Papo hapo Mwenyezi Munau akamlete Jeshi Lake.
Kuna Maoni mbalimbali kuhusu Adhabu waliopewa Abraha na Jeshi lake. Tafsiri hapa juu inasema Walikuja Njiwa na Kila Mmoja wa Njiwa hao walikuwa wamebeba Mawe ya Moto Mkali na wakawa wanawarushia Na wakawa wanasagika kama majani yaliyotafunywa na kisha kutemwa. Hii ndiyo Tafsiri tunayoisoma hapa juu lakini kuna Wanavyuoni wanaosema kwamba Jeshi ya Abraha likaingiliwa na maradhi, wengine wakafa papo hapo na Abraha na baadhi ya askari wake wakawahi kurudi Yemen na kufia huko. Wanavyuoni wenaine wamesema kwamba inamkinika kuwa makusudio ya طيرا “Tair” katika Aya hii ni “viini vya ugonjwa” (germs). na Wanavyuoni wengine wamesema kwamba mapendeleo yake ni kuwa Mwcenyezi Mungu aliwatia maradhi mabaya, yakaharibu miili yao, hata wakawa kama majani yaliyoliwaliwa na wadudu au yaliyoliwa yakatemwa.
MUUJIZA WA KIAJABU SANA- SAYANSI
Sasa Angalia Maajabu Yanayofuata:
Sura Hii ni Namba 105 na namba hii inaashiria majabu makubwa sana. Mtoto wa tembo anapozaliwa kwa kawaida (Average) Uzito wake unakuwa ni Kilo 105!!!! Angalia Muujiza wa Kuruani mpaka katika namba ya Sura. Allahu Akbar.
Ukihesabu Herufi Kuanzia Mwanzo wa Aya Mpaka Katika Herufi ya Kwanza ya Neno Tembo Utapata Jumla ya Herufi ni 22 na ajabu ni kwamba Kabla ya Kuzaliwa Tembo anakuwa katika Tumbo la Kizazi kwa muda wa miezi 22!!!! je unaona Muashirio wa kiajabu? Allahu Akbar. Yaani Miezi 22 ni Gestation Period Angalia Kuruani ilivyobeba habari za Maajabu.
الم تر كيف فعل ربك باصحب الفيل
Ukihesabu Herufi kuanzia mwanzo wa Aya hii mpaka Herufi ya kwanza ya Neno Al-FIYL yaani Tembo ni 22
A baby elephant has a mass of 105 kg. The elephant increases in mass by 95 kg per year.
Ni Average na siyo FIX. Yaani kwa kawaida. Kwa hiyo usishangae ukisikia Kwamba Kuna Mtoto wa tembo aliyekuwa na uzito zaidi au pungufu ya 105. Hapa tunasoma AVERAGE.
Elephants are the largest land mammals in the world, so it’s perhaps not surprising that they have the longest pregnancy of any living mammal: African elephants are pregnant for an average of 22 months, whilst for Asian elephants it’s 18 to 22 months
Ni Average na siyo FIX. Yaani kwa kawaida. Kwa hiyo usishangae ukisikia Kwamba Kuna Mtoto wa tembo aliyekuwa Tumboni zaidi au pungufu ya Miezi 22 . Hapa tunasoma AVERAGE.