UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
DARUBINI YA KWANZA KATIKA AYA YA KWANZA-SURA YA ISRAA NAMBA 17
Alhamdulikah leo nitaielekeza darubini na kudondoleza Machache kuhusu Aya ya kwanza ya Sura Hii Namba 17 ambayo yamebeba makubwa. Sura Ya Israa Imezungukwa na pia kubeba Maneno mawili Makubwa. La Kwanza ni SUBHANA na la Pili ni AL-HAMDULILAH. Sura Iliyotangulia Ni Ya 16 Nayo ni Al-Nahl Aya Ya kwanza imetaja neno SUBHANA
أَتَىٰٓ أَمۡرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسۡتَعۡجِلُوهُۚ سُبۡحَـٰنَهُ ۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ (١)
TAFSIRI
1 . Amri ya Mwenyezi Mungu itafika (tu); basi msiihimize; (Muitakidi kuwa) Yeye (Mwenyezi M ungu) katakasika na kila mapungufu na Katukuka na ushirikina wa (hao makafiri).
———————
Na Katika Sura Inayofuata Namba 18 Ya Al-kahf Aya Ya Kwanza Imetumia neno Al-Hamdulilah kama ifuatavyo
ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ عَلَىٰ عَبۡدِهِ ٱلۡكِتَـٰبَ وَلَمۡ يَجۡعَل لَّهُ ۥ عِوَجَاۜ (١)
TAFSIRI
1. Sifa zote njema zinamstahikia Mwenyezi Mungu ambaye amemteremshia mja Wake (Nabii Muhammad) Kitabu (kitukufu hiki); wala hakukifanyia kuwa na kosa (upungufu).
————————–
Kwa Hiyo neno Subhana katika Upande wa kushoto wa Sura Ya Israa na neno Al-Hamdulilah katika Upande wa kulia wa Sura Ya Israa kama tulivyoona katika Aya mbili nilizozitaja hapa Juu.
Na Katika Sura Ya Isaraa Aya Ya Kwanza Imetumia Neno Subhana kama ifuatavyo
سُبۡحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلاً۬ مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ ۥ لِنُرِيَهُ ۥ مِنۡ ءَايَـٰتِنَآۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ (١)
TAFSIRI
Utukufu ni wake yeye ambaye: alimpeleka mja wake usiku (mmoja tu) kutoka Msikiti Mtukufu(wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa BaytulMuqaddas-Falastini) ambao (tumeubariki na)tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake(Tulimpeleka hivyo) ili tumuonyeshe baadhi ya Alama zetu. Hakika Yeye (Mwenyezi Mungu) ni Mwenye kusikia (na) Mwenye kuona.
SHEREHE
Na katika Aya Ya mwisho wa Sura Hii imetaja neno Al-hamdulilah kama ifuatavyo:
وَقُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى لَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدً۬ا وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ شَرِيكٌ۬ فِى ٱلۡمُلۡكِ وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ وَلِىٌّ۬ مِّنَ ٱلذُّلِّۖ وَكَبِّرۡهُ تَكۡبِيرَۢا (١١١)
TAFSIRI
Na sema: “Sifa zote njema zinamstabikia Mwenyezi Mungu ambaye hakujifanyia mtoto wala hana mshirika (wake) katika ufalme wala bana raftki (wa kumsaidia) kwasababu ya udhaifu wa kuhitaji. Na mtukuze kwa matukuzo makubwa (kabisa).
SHEREHE
Kama Nilivyosema hapa juu mpangilio huu wa kushangaza. Maneno Mawili; Subhanaah na Alhamdulilah yamelizunguka Sura hii kiajabu.
Sura Namba 16 Aya ya Kwanza kuna neno Subhana
Sura Ya 17 ya Israa mwanzoni kumetumika neno Subhana na Mwishoni neno Alhamdulilah
Sura Ya 18 mwanzoni kuna neno Alhamdulilah
Je unaona Saini ya Mwenyeezi Mungu. Uchaguzi wa maneno na mpangilio wake tu unashangaza sasa je Maana ya maneno haya?
Sura Hii ya Israa imetaja safari ya Mtume ﷺ kwenda mbinguni na kurudi Duniani katika Usiku mmoja. Kwa kweli ni Muujiza siyo mdogo.
Sasa hebu tuichunguze kwa kugusia tu Aya ya kwanza ya Sura ya Israa. Allahu Akbar.Nayo ni kama ifuatayo:
سُبۡحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلاً۬ مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ ۥ لِنُرِيَهُ ۥ مِنۡ ءَايَـٰتِنَآۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ (١)
Kabla ya kuielezea Aya hii (Angalia Tafsiri Hapa Juu)Hebu kwanza tupeleke Darubini yetu katika Sura ya 16 yaani Sura Ya Nyuki (Al-Nahl) kabla ya Sura hii. Katika Aya ya mwisho mwenyeezi Mungu anasema
إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحۡسِنُونَ (١٢٨)
Katika Aya Hii Mwenyeezi Mungu anasema kwamba yeye yupo pamoja na wachamungu na wale wenye kutenda mema.
Ukiielekeza Darubini katika Sura ya Israa Aya namba 1 ambayo tumeitaja hapa juu utaona Mtume ﷺ ndiye kiongozi wa wachamungu na wenye kutenda mema kwani Alipazwa na kuwa karibu na Mwenyeezi Mungu na kufaridhishiwa sala 5 kwa njia ya mazungumzo kuliko kiumbe yeyote Duniani Ijapokuwa Nabii Musa alizungumza na Mungu katika Mlima wa Sinai lakini Mtume Mohamad ﷺ alialikwa na akasafirishwa ili aende akutane na Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Je nani aliyepata utukufu huu katika Dunia hii?
Kuna wachamungu na watenda mema ambao Mwenyeezi Mungu anakuwa pamoja nao lakini hakuna aliyebebwa na kukaribishwa na kuwa karibu na Mwenyeezi Mungu huko Mbinguni kama alivyopewa utukufu huu Mtume Mohamad. ﷺ
Sasa tuchunguze Maneno ya Aya ya Kwanza ya Sura Ya Israa tuliyoitaja hapa juu
سُبۡحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلاً۬ مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ ۥ لِنُرِيَهُ ۥ مِنۡ ءَايَـٰتِنَآۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ (١)
Katika Aya hii (Angalia Tafsiri Hapa Juu) Neno سُبۡحَـٰنَ Subhana lina maana ya “Kutakasika (kwa Mwenyeezi Mungu)na kila upungufu” yaani Mwenyeezi Mungu ametakasika na kila sifa za upungufu au sifa zozote zile za kidunia au kiulimwengu. Hana mfano wa chochote.
Katika Nahau au Grammar ya Kiarabu Neno hili linajulikana kama ISMU MASDAR yaani kwa kizungu NOMINAL INFINITIVE Neno hili siyo kitendo kilichopita kama vile neno linalotokana na neno hili SABAHA “Alitakaswa” au Kitendo cha wakati tulionao kama vile neno YUSABIHU “Anamtakasa” au Maamrisho kama vile FASABIH yaani “Mtakase” katika Aya Nyinginezo mbalimbali za Kuruani Tukufu.
Neno Hili “SUBHANA” limekusanya maana kubwa. Yaani Mwenyeezi Mungu ametakasika katika Kila wakati na kila mazingara. Mwenyeezi Mungu ametakasika katika kila wakati na kila sehemu ulimwenguni.Na Katika Sura hii ya Israa neno la kwanza la Sura hii ni “SUBHANA” limetumika kwa maana hii. Yaani neno hili halikufungamana na Wakati au chochote. Ni Neno “MUJARRAD” yaani neno la asili lisilo na nyongeza yoyote. Ni Neno ambalo halina Mfungamano na chochote. Ni MASDAR au INFINITIVE. (NOMINAL INFINITIVE).
Angalia Maajabu. Neno moja tu limekusanya Mambo siyo madogo. Allahu Akbar.
Neno hili ni “MUTLAQ” yaani ni neno peke yake. Yaani kila kilichopo Ulimwenguni kinamtakasa. Neno hili halikufungamana na Chochote. Yaani hata kama Viumbe havimtakasi basi Kuna Vinginevyo ambavyo Vitamtakasa. Tupende au Tusipende. Tutake au Tusitake. Hakuna Budi bali itakuwa hivyo. Viumbe Tunavyovijua na ambavyo hatuvijui vitamtakasa. Na hii yote inatokana na Grammar iliyotumika hapa. Ni Neno lenye maana ya KUTAKASIKA kwa Mwenyeezi Mungu kabla ya Kuumba chochote na hata baada ya Kuumba. Yaani neno hili linathibitisha Kutakasika kwa Mwenyeezi Mungu kwa kila njia. Halina Mwanzo au Mwisho. Allahu Akbar. Allah Ametakasika kabla na baada ya Chochote ulimwenguni. Allahu Akbar. Angalia Kuruani ilivyobeba mambo. Neno Moja maana kubwa sana, tena sana.
Katika Sura ya Israa Aya namba 44 inathibitisha haya tuliyoyataja hapa juu
تُسَبِّحُ لَهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتُ ٱلسَّبۡعُ وَٱلۡأَرۡضُ وَمَن فِيہِنَّۚ وَإِن مِّن شَىۡءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمۡدِهِۦ وَلَـٰكِن لَّا تَفۡقَهُونَ تَسۡبِيحَهُمۡۗ إِنَّهُ ۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورً۬ا (٤٤)
TAFSIRI
44· Zinamtukuza zote mbingu saba na ardhi na vilivyomo ndani yake. Na hakuna chochote ila kinamsabihi (Mwenyezi Mungu) kwa sifa Zake njema. Lakini nyinyi hamfahamu kusabihi (kutukuza) kwake. Hakika Yeye Mwenyezi Mungu ni Mpole (na) Mwingi wa kusamehe.
SHEREHE
Mwenyeezi Mungu anasema katika Aya hii kwamba Mbingu Saba na Ardhi na kila kitu katika Mbingu Saba na Ardhi. Na kila kitu katika Viumbe vyake na hata vile ambavyo havina uhai vinamtakasa Mwenyeezi Mungu. Angalia Ukubwa wake Mwenyeezi Mungu. Allahu Akbar. Hakuna Sura iliyojaa TASBIH kwa wingi kama Sura ya Israa ilivyotaja neno hili.
Ni Sura pekee ambayo imetumia neno la kumtakasa Mwenyeezi Mungu kwa mara nyingi kuliko Sura zote za Kuruani Tukufu. Na Sura Hii imeanziwa na Neno la “Kumtakasa Mwenyeezi Mungu”. Kwa kweli ni Muujiza siyo mdogo. Na neno hili linaashiria Kusafirishwa kwa Mtume Mohamad ﷺ kwenda katika Ulimwengu Mwingine wa TASBIH. katika Hiyo ” ISRAA NA MIIRAJ” Ni Ishara kwamba huko alikopelekwa Mtume ni sehemu ya TASBIH au sehemu inayomtukuza Mwenyeezi Mungu.
Katika Aya ya kwanza ya Sura Ya Isra
سُبۡحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ لَيۡلاً۬ مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ ۥ لِنُرِيَهُ ۥ مِنۡ ءَايَـٰتِنَآۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ (١)
Mwenyeezi Mungu anamtukuza Mtume ﷺ kwa Kumwita kwa sifa ya بِعَبۡدِهِۦ ABDIHI yaani Mja wake. Kipande cha Aya سُبۡحَـٰنَ ٱلَّذِىٓ أَسۡرَىٰ بِعَبۡدِهِۦ kinasema kwamba “Ametakasika (Mwenyeezi Mungu) ambaye alimpeleka Mja wake” Neno ABDAN maana yake “Mja” ni utukufu kuwa Mja wa Mwenyeezi Mungu. Na utukufu mkubwa kuwa Mja kwa njia ya Ibada kwa kujitolea nafsi yako bila ya kujilazimisha au kwa udanganyifu. Ukiwa Mja wa kweli basi unastahiki kuwa na Utukufu wa hali ya juu. Mtume Mohamad ﷺ amepewa sifa ya kuitwa “Mja” kwa kustahiki ucha mungu wake wa hali ya juu na sifa nyinginezo mbalimbali zilizo nzuri.
Neno لَيۡلاً۬ lina maana ya Baadhi ya Usiku na siyo Usiku wote. Na iwapo neno Hili lingitanguliwa na Herufi ya Alif wa Alam likawa”ALLAYL” basi maana ingebadilika maana na kuwa Usiku wote kwani Alif na Alam inajulikana katika Grammar ya Kiarabu kama Alif na Lam ya “AL-ISTIGHRAQ” Je unaona undani wa Kuruani. Na ndiyo maana Mtume alipoletewa Ujumbe yaani Wahyi (Revelation) ijapokuwa Waarabu walikuwa hodari sana katika Lugha yao lakini walishangaa Lugha ya Kuruani kwani Ilishinda ufundi wao wa Lugha. Na sababi hii iliwafanya waukubali Uislamu kwa kuona Lugha ya kuruani siyo ya kawaida hata kidogo. Mtume ﷺ Asingeweza Kuja na Lugha kama hii.
Katika Kipande cha Aya
مِّنَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ إِلَى ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡأَقۡصَا ٱلَّذِى بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ ۥ
TAFSIRI
kutoka Msikiti Mtukufu(wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa BaytulMuqaddas-Falastini) ambao (tumeubariki na)tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake)
SHEREHE
Kuna Maoni ya Wanavyuoni waosema kwamba Masjid Al-Haram ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِ ni Mji wote wa Mecca na siyo msikiti au sehemu iliyozunguka Msikiti peke yake. Na Kuhusu BaytulMuqaddas-Falastini Yaani Msikiti wa huko Falastini. Ni Muujiza Mwingine wa Kuruani kuuita kama ni Msikiti wa Falastini kwani wakati huo wa Mtume ﷺ kulikuwa hakuna Msikiti kama Ulivyo leo. Kuruani imetaja habari hizi kwa njia ya Kimuujiza kwamba kutakuwa na Msikiti hapo baadaye Historia inasema kwamba Msikiti ulijengwa katika Mwaka 705 yaani baada ya miaka 73 ya kufariki kwa Mtume Mohamad. Historia inasema kwamba Jengo hilo la ibada lilijengwa na Nabii Ibrahim. Lakini Msikiti wa Kisasa kama tunavyoujua leo ulikuwa Umejengwa baada ya Kufariki kwa Mtume.ﷺ (The mosque is the second oldest in the world, after the Kaaba in Mecca. Although Muslim tradition dates Al-Aqsa back to Isaac’s son, Jacob, the mosque was first built at its present location by the Ummayad Caliph Abd al-Malik and his son al-Walid, and completed in 705 CE. Kipande cha Aya kinachosema بَـٰرَكۡنَا حَوۡلَهُ yaani Tumebariki Msikiti huo na Nje yake yaani sehemu iliyozunguka Msikiti huo. Baraka hizo hapo Nje ya Msikiti zinatokana na Msikiti. Yaani Huo msikiti Mtukufu umesababisha Baraka Itoke Nje na kubariki kila kilichozunguka msikiti huo. Allahu Akbar.
لِنُرِيَهُ ۥ مِنۡ ءَايَـٰتِنَآۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡبَصِيرُ
Kipande hiki kinasema kwamba Sababu ya Kumpeleka Mtume ﷺ Huko Falastini katika Masjid Al-Aqsa ili Mwenyeezi Mungu amuonyeshe Alama (Miujiza au Mambo Makubwa) zake. Na Aya hii inaishia kwa Kusema Kwa hakika Mwenyeezi Mungu ni Mwenye Kusikia na Kuona.
kilugha Baraka Imefungamana na Msikiti. Na iwapo kungekuwako kwa Neno “Ma” baina ya Maneno BARAKNA na HAWLAHU yaani Kwa kusema BARAKNA MA HAWLAHU بَـٰرَكۡنَا ما حَوۡلَهُ basi maana ingebadilika na ingekuwa BARAKA hiyo imefungamana na Vilivyopo Nje ya Msikiti na katika hali hiyo hivyo vitu vingeondoka Basi na BARAKA pia ingeondoka.
Angalia Lugha Inavyobadilika katika Kuongeza au kupunguza kwa Herufi au vipande vya maneno. Wengi hawajui tofauti hizi. Kwa kuongeza Herufi Mbili tu yaani ما “MA” basi maana inabadilika. Kwa hiyo tuwe macho tunaposoma Kuruani tusije tukachanganya Mambo na hasa wale ambao lugha yao ya asili ni Kiarabu wanaweza kufanya hivo kirahisi kwani katika Lugha ya kila siku watu hupendelea kusema MA HAULAU kuliko kusema HAWLAU peke yake. Kwa hiyo tuwe macho sana katika Kusoma Kuruani. Kila Herufi, maneno, Aya na sura zipewe haki zake katika Matamshi na Maandishi.
Kwa kweli Maneno na Elimu ya Mwenyeezi Mungu haina Mwisho.Maelezo haya yote yalikuwa katika Aya Ya Kwanza ya Sura Ya Israa. Hebu Tufikiri. Na hata hivyo ni sherhe fupi ya Juu juu. Kuna mengi yaliyobebwa na Aya hii ambayo mengine hatuyajui. Allahu Akbar.
DARUBINI YA PILI NI KATIKA AYA ZILIZOTUMIA NENO “MWAKA” KWA KUTUMIA MANENO MBALIMBALI YENYE MAANA YA MWAKA (SYNONIMS) AU ( ARABIC-MURADAFAAT) LAKINI KUNA TOFAUTI YA HALI YA JUU KULINGANA NA MAZINGARA.
Alhamdulilahi leo Nitaielekeza Darubini katika Zile Aya zilizotumia Neno Mwaka, Kuna Maneno Yanayofanana na yote yana maana moja ya “MWAKA” lakini yana nyongeza kufuatana na Mazingara. Neno “MWAKA” katika Kuruani limetumika mara Nne.
Neno AAM
Neno SINA
Neno HAWLI
Neno HIJAJ
Hebu tuzilete hizo Aya kisha tuone Hekima kubwa ya haliya Juu katika Uchaguzi huo. Kuruani ni Muujiza mkubwa Sana. Kila Neno Limechaguliwa kiajabu. Hakuna Kosa katika Kuruani Tukufu. Ni wachache waongo na Maadui tu ndiyo wanaokataa kwa Ujinga na Kutokuwa na Elimu yeyote. Lakini Ukifahamu Ujinga Na Ukaidi utaondoka.
Al-Araaf Sura Namba 7 Aya Namba 130
وَلَقَدۡ أَخَذۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ بِٱلسِّنِينَ وَنَقۡصٍ۬ مِّنَ ٱلثَّمَرَٲتِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّڪَّرُونَ (١٣٠)
TAFSIRI
130. Na· hakika tuliwaadhibu watu wa Firauni kwa miyaka (ya njaa kubwa kabisa) na kwa kupungukiwa na mazao, i1i wapate kukumbuka
SHEREHE
Neno بِٱلسِّنِينَ “BISSINIYNA” lina maana ya Mwaka (Year) lakini limeambatana na Ukame na kufuatana na Mazingara ya adhabu aliyopewa Firauni yaani Ukame na Upungufu wa Mazao (Matunda). Kwa hiyo Mwenyeezi Mungu akalitumia Neno Hilo kwa ajili hiyo. Na Hakuchagua neno Lingine lenye maana Ya Mwaka katika SYNONYMS ya Neno Mwaka kama vile AAM au lingine.
———————
Sura Ya Yusuf namba 12 Aya namba 47-49
قَالَ تَزۡرَعُونَ سَبۡعَ سِنِينَ دَأَبً۬ا فَمَا حَصَدتُّمۡ فَذَرُوهُ فِى سُنۢبُلِهِۦۤ إِلَّا قَلِيلاً۬ مِّمَّا تَأۡكُلُونَ (٤٧) ثُمَّ يَأۡتِى مِنۢ بَعۡدِ ذَٲلِكَ سَبۡعٌ۬ شِدَادٌ۬ يَأۡكُلۡنَ مَا قَدَّمۡتُمۡ لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلاً۬ مِّمَّا تُحۡصِنُونَ (٤٨) ثُمَّ يَأۡتِى مِنۢ بَعۡدِ ذَٲلِكَ عَامٌ۬ فِيهِ يُغَاثُ ٱلنَّاسُ وَفِيهِ يَعۡصِرُونَ (٤٩)
TAFSIRI
47. Akasema:· “Mtalima myaka saba mfululizo kwa juhudi (yaani limeni miaka saba kwa juhudi kwani itaingia njaa kubwa baada ya myaka saba). Na mtakavyovivuna viacheni katika mashuke yake, isipokuwa kidogo mnavyokula (ili hivyo mnavyoviacha mule katika myaka ya njaa itakayokuja).”
48. “Kisha itakuja baadaye myaka saba ya shida itakayokula vile mlivyoweka, (yaani watu watakula ile akiba mliyoiweka) isipokuwa kidogo mtakachohifadhi (kwa ajili ya kupandia).”
49· “Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika. mwaka huo watu watasaidiwa na (Mwenyezi Mungu); na katika huo watakamua (vya kukamua).”
SHEREHE
Neno سِنِينَ SINIYNA katika Aya hii lina maana ya Miaka ya Ukame na neno عَامٌ۬ AAM lina maana ya Miaka ya Neema
————–
Sura Ya Bakarah Namba 2 Aya Namba 233
۞ وَٱلۡوَٲلِدَٲتُ يُرۡضِعۡنَ أَوۡلَـٰدَهُنَّ حَوۡلَيۡنِ كَامِلَيۡنِۖ لِمَنۡ أَرَادَ أَن يُتِمَّ ٱلرَّضَاعَةَۚ وَعَلَى ٱلۡمَوۡلُودِ لَهُ ۥ رِزۡقُهُنَّ وَكِسۡوَتُہُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ لَا تُكَلَّفُ نَفۡسٌ إِلَّا وُسۡعَهَاۚ لَا تُضَآرَّ وَٲلِدَةُۢ بِوَلَدِهَا وَلَا مَوۡلُودٌ۬ لَّهُ ۥ بِوَلَدِهِۦۚ وَعَلَى ٱلۡوَارِثِ مِثۡلُ ذَٲلِكَۗ فَإِنۡ أَرَادَا فِصَالاً عَن تَرَاضٍ۬ مِّنۡہُمَا وَتَشَاوُرٍ۬ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡہِمَاۗ وَإِنۡ أَرَدتُّمۡ أَن تَسۡتَرۡضِعُوٓاْ أَوۡلَـٰدَكُمۡ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِذَا سَلَّمۡتُم مَّآ ءَاتَيۡتُم بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ۬ (٢٣٣)
TAFSIRI
233. Na wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha; na ni juu ya baba (yake) chakula chao (hao watoto na mama) na nguo zao kwa Sharia. Wala haikalifishwi nafsi yo yote ila kwa kadiri ya wasaa wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake, wala baba (asitiwe taabuni) kwa ajili ya mtoto wake. Na juu ya mrithi (inapokuwa baba kafa) ni kama hivyo. Na kama wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa (kabla ya miaka miwili), kwa kuridhiana na kushauriana, basi si kosa juu yao. Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha (wengine wasiokuwa mama zao), basi haitakuwa dhambi juu yenu kama mkitoa (kuwapa hao wanyonyeshaji) mlichowaahidi kwa Sharia. na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayoyatenda.
SHEREHE
Neno حَوۡلَيۡنِ HAWLAYNI katika Aya hii lina maana ya Miaka Ya Mabadiliko. (Aya hii imetanguliwa na Aya zinazozungumzia TALAKA na kwa hiyo kabla ya TALAKA na baada ya TALAKA kutakuwa na Mabadiliko katika Mazingara Ya Mke na Mume Pia. Kumetumika Neno HAWLI kama Separation au Kiarabu HAJIZ au Barrier yaani Kizuizi ambacho kinatofautisha baina Ya Wakati wa Ndoa na wakati baada ya Ndoa Kuvunjika. Lakini uissahau Neno HAWLI lina maana ya Mwaka. Kwa kifupi ni Mwaka Wa mabadiliko.
—————————-
Sura Ya Bakarah Namba 2 Aya Namba 240
وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنڪُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٲجً۬ا وَصِيَّةً۬ لِّأَزۡوَٲجِهِم مَّتَـٰعًا إِلَى ٱلۡحَوۡلِ غَيۡرَ إِخۡرَاجٍ۬ۚ فَإِنۡ خَرَجۡنَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡڪُمۡ فِى مَا فَعَلۡنَ فِىٓ أَنفُسِهِنَّ مِن مَّعۡرُوفٍ۬ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَڪِيمٌ۬ (٢٤٠)
TAFSIRI
240. Na wale wanaofishwa· (wanaokufa) miongoni mwenu na wakawacha wake, wawausie (mawarithi wao) kwa ajili ya wake zao kupata matumizi kwa mwaka mmoja bila ya kutolewa (katika majumba waliyokuwamo, ya waume zao). Na kama wanawake (wenyewe) wakiondoka, basi si kosa juu yenu kwa yale waliyoyafanya ·kwa nafsi zao wenyewe yanayofuata Sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima.
SHEREHE
katika Kuruani Neno HAWL lenye maana ya Mwaka limetumika katika Aya mbili tu nilizozitaja hapa juu. Na neno hili limetumika kiajabu sana.
Neno ٱلۡحَوۡلِ AL-HAWL katika Aya hii lina maana ya Miaka Ya Mabadiliko. (Aya hii Inazungumzia Mauti yaani Kufariki na kwa hiyo Kumetumika Neno HAWL kama Separation au Kiarabu HAJIZ au Barrier yaani Kizuizi ambacho kinatofautisha baina Ya Wakati Kabla Ya Kufariki Na Baada Ya Kufariki. Lakini uisahau Neno HAWLI lina maana ya Mwaka. Kwsa kifupi ni Mwaka Wa mabadiliko. Mabadiliko Kabla Ya Mauti na Baadaye.
—————————-
Sura Ya Qasas Namba 28 Aya Namba 27-29
قَالَ إِنِّىٓ أُرِيدُ أَنۡ أُنكِحَكَ إِحۡدَى ٱبۡنَتَىَّ هَـٰتَيۡنِ عَلَىٰٓ أَن تَأۡجُرَنِى ثَمَـٰنِىَ حِجَجٍ۬ۖ فَإِنۡ أَتۡمَمۡتَ عَشۡرً۬ا فَمِنۡ عِندِكَۖ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أَشُقَّ عَلَيۡكَۚ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ (٢٧) قَالَ ذَٲلِكَ بَيۡنِى وَبَيۡنَكَۖ أَيَّمَا ٱلۡأَجَلَيۡنِ قَضَيۡتُ فَلَا عُدۡوَٲنَ عَلَىَّۖ وَٱللَّهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَڪِيلٌ۬ (٢٨) ۞ فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى ٱلۡأَجَلَ وَسَارَ بِأَهۡلِهِۦۤ ءَانَسَ مِن جَانِبِ ٱلطُّورِ نَارً۬ا قَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّىٓ ءَانَسۡتُ نَارً۬ا لَّعَلِّىٓ ءَاتِيكُم مِّنۡهَا بِخَبَرٍ أَوۡ جَذۡوَةٍ۬ مِّنَ ٱلنَّارِ لَعَلَّكُمۡ تَصۡطَلُونَ (٢٩)
TAFSIRI
27.Akasema: “Mimi nataka nikuoze mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane; na kama ukitimiza kumi ni hiari yako, lakini mimi sitaki kukutaabisha: utanikuta Insha-Allah miongoni mwa watu wema.
28. Akasema (Musa: “Mapatano) hayo yamekwisha kuwa baina yangu na baina yako; muda mmojapo nitakaoumaliza, basi nisidhulumiwe; na Mwenyezi Mungu ni Mlinzi juu ya haya tunayoyasema.
29. Basi Musa alipotimiza muda akasafiri pamoja na ahali zake ( watu wake). (Kurejea kwao Misri), aliona moto upande wa mlimani akawaambia ahali zake; “Ngojeni, hakika nimeona moto; labda nitakuleteeni habari za huko au kijinga cha moto ‘ili muote.”
SHEREHE
Katika Aya Hizi tunakuta neno حِجَجٍ۬ۖ HIJAJ yaani Pia lina maana ya Miaka. Ijapokuwa Neno Hili lina maana Ya Mwaka kama Maneno mengineyo tuliyoyataja hapa juu lakini Neno hili lina maana ya Ziyara. Nabii Musa Katika Aya hizi alipoozeshwa Mke aliambiwa afanye kazi hapo miaka Minane au kumi na baadaye akaondoka kama tunavyosoma katika Aya ya 29 hapa juu. Neno HIJAJ lina maana ya Miaka lakini Ni Miaka ya Ziyara tu. Yaani Ni Miaka ya Muda huo. Amekaribishwa kwa Muda. Na siyo Maisha Yote. Hakupewa Residence ya Maisha yake yote bali muda wa miaka minane au kumi. Kuruani imezingatia Mazingara hayo na imechagua neno HIJAJ ili likubaliane na Mazingara hayo.
Kila neno katika Kuruani limechaguliwa kwa Ufundi wa hali ya juu na hakuna binaadamu anyeweza kufanya hivyo hata ukiwa na PHD za Dunia Nzima. Ujanja wote unaishia katika Kuruani. Ni Muujiza siyo mdogo.
Soma unavyotaka lakini ukiielewa Kuruani utajikuta Mjinga na Huna Elimu ya Kutosha. Ni Muujiza Usio na Mfano. Kwa hiyo Tuwe na Adabu na Tujijue Ujinga wetu ili Mwenyeezi Mungu atufundishe Kuruani. Tukijifanya Werevu na Kuidharau Kuruani basi tutabaki wapumbavu milele na Elimu yako itakuwa haina Faida yeyote hata ungelikuwa Una Elimu za Dunia Nzima. Tuwe wanyenyekevu tunaposoma Kuruani na Kumwogopa Mwenyeezi Mungu kila wakati. Tusijivune na kujiona Wajanja.