SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Darubini-2/Kuruani

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

MANENO  YENYE MIUJIZA MIKUBWA

NENO  مُّسَوَّمَةً  “MUSAWAMAH”

سُوۡرَةُ الذّاریَات

Sura Ya Al-Dhariyaat Aya Namba 24-34

هَلۡ أَتَٮٰكَ حَدِيثُ ضَيۡفِ إِبۡرَٲهِيمَ ٱلۡمُكۡرَمِينَ (٢٤) إِذۡ دَخَلُواْ عَلَيۡهِ فَقَالُواْ سَلَـٰمً۬ا‌ۖ قَالَ سَلَـٰمٌ۬ قَوۡمٌ۬ مُّنكَرُونَ (٢٥) فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجۡلٍ۬ سَمِينٍ۬ (٢٦) فَقَرَّبَهُ ۥۤ إِلَيۡہِمۡ قَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ (٢٧) فَأَوۡجَسَ مِنۡہُمۡ خِيفَةً۬‌ۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡ‌ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَـٰمٍ عَلِيمٍ۬ (٢٨) فَأَقۡبَلَتِ ٱمۡرَأَتُهُ ۥ فِى صَرَّةٍ۬ فَصَكَّتۡ وَجۡهَهَا وَقَالَتۡ عَجُوزٌ عَقِيمٌ۬ (٢٩) قَالُواْ كَذَٲلِكِ قَالَ رَبُّكِ‌ۖ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡعَلِيمُ (٣٠) ۞ قَالَ فَمَا خَطۡبُكُمۡ أَيُّہَا ٱلۡمُرۡسَلُونَ (٣١) قَالُوٓاْ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمٍ۬ مُّجۡرِمِينَ (٣٢) لِنُرۡسِلَ عَلَيۡہِمۡ حِجَارَةً۬ مِّن طِينٍ۬ (٣٣) مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلۡمُسۡرِفِينَ (٣٤)

TAFSIRI

24. ]e! imekujia hadithi ya wageni wahishimiwao wa (Nabii) lbrahimu? 25. Walipoingia kwake wakasema: “Salaam(Alaykum);” na (yeye lbrahimu) akasema:”Alaykumusalaam.” (Na katika moyo. wake anasema): “Ninyi watu nisiokujueni.” 26. Mara akaenda kwa ahali yake na akaleta Ndama aliyenona 27. Akampeleka karibu yao. (Hawakunyoosha mikono yao kula) Akasema: “Mbona hamli!” 28. Basi akawatilia shaka (katika nafsi yake na akawaogopa). Wakasema:”Usiogope,” na. wakamtolea habari nzuri za (kuwa Atazaa) mtoto mwenye Elimu. 29. Ndipo mkewe (Nabii lbrahimu)akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu na kusema: “Mwanamke mzee, Tasa(nitazaa). ·” 3o. Wakasema: “Ndivyo vivyo hivyo (utazaa,na hali ya kuwa wewe ni Tasa). Amesema Mola wako. Hakika Yeye ndiye Mwenye hekima, Ajuaye(kila kitu).” 31. Akasema, “Basi makusudio yenu (mengine)ni nini, Enyi mliotumwa?” 3l. Wakasema: “Hakika sisi tumetumwa Tukawaangamize wale watu waovu (watu wa Nabii Luti).” 33· “IIi tuwatupie juu yao mawe ya udongo (wa Motoni)”. 34· “Yaliyotiwa alama kwa Mola wako kwa ajili ya hao watu wanaopindukia mipaka katika maasia.”

SHEREHE

Alhamdulilah Leo nitaielekeza Darubini yetu katika Aya za Sura Ya Al-Dhariyaat kuanzia Namba 24  mpaka 34 ambazo zinazungumzia Kisa cha Malaika waliomzuru Nabii Ibrahim nyumbani kwake. Na habari  walizomletea za kushangaza.

Kwanza walimbashiria habari nzuri kwamba Mke wake aliyekuwa Mzee na Tasa kwamba atazaa.

Habari ya Pili ni  habari ya kutisha nayo ni kuangamizwa kwa wananchi wa miji ya  Sodom and Gomorrah (ndivyo Historia inavyosema kwamba mambo haya  yalitokea katika miji hii miwili) ambayo watu katika miji hiyo walizama kwa maasi makubwa ya Zinaa.

Na Adhabu yenyewe ni  kuangushiwa kwa Mawe ya Udongo wa Moto wa  Jahannam. Mawe haya Yametiwa Alama au Jina la kila atakayeangushiwa. Neno مُّسَوَّمَةً   “MUSAWAMAA” lina maana ya Alama yaani kila Jiwe limetiwa Alama ya yule litakalomuangukia. Hata huyo  mwenye  kukusudiwa angejificha haisadii kitu kwani Kijiwe hicho kingemtafuta popote alipo. 

Sasa Tujiulize Masuali.  Je leo hii binaadamu anajigamba kwamba ameweza kutengeneza Silaha za Mabomu ya  hali ya juu. Hakuna  Nchi yeyote duniani ambayo imeweza kutengeneza mabomu yenye kuweza kulenga Mtu kwa kumkusudia.  Ujanja  wote na kujigamba kwa nguvu walizonazo hawakuweza kuwa na silaha za aina hii. Sasa Ni nani mwenye nguvu?  Ni Nani  Mfalme wa Ulimwengu au Malimwengu? Mwenyeezi Mungu ameuliza swali hili katika Kuruani na akalijibu mwenyewe. Amesema Ni Nani Mfalme leo hii?  akajibu  “Lilahi Alwahid Alqahar”  yaani ufalme ni wake  mwenye nguvu  kubwa .

Ni yeye ndiye  ambaye ametuumba kwa kusema  “Kun Fayakun”  yaani Kuwa na Tukawa. Tumeumbwa kwa udongo. Allahu Akbar. Kisha Tunajigamba. Hatuna chochote. Maneno Matupu.

Haiwezekani kabisa. Baada  ya juhudi zote za wataalamu wa kivita wameweza tu kutengeneza  Mabomu ambayo  yanapoangushwa huangamiza wanaohusika na wasiohusika. 

Bure tupu, hatufui Dafu  Nguvu za Mwenyeezi Mungu hata kidogo. Allahu Akbar.

Silaha za Kisasa zenye ufundi wa hali ya juu wenye kutumia  LASER, au RADAR, au SATELITE na nyinginezo mbalimbali kama vile CLUSTER BOMBS.  zote hizi  ni silaha zinazoharibu kila kitu. 

Zinapotupwa  basi  huua wanyama, binaadamu, huvunja majumba na kuharibu Miti na Mapori.

Hebu tufikiri Sayansi za Mwenyeezi Mungu na uwezo wake.

Majiwe Yaliyoangushiwa Watu wa Nabii Lutt  yalikuwa yametengenezwa kwa Udongo wa Moto wa jahannam.  Mawe hayo madogo madogo yalikuwa yakishushwa kwa mpango wa ajabu na kuanguka kama vile mvua  lakini kila kijiwe kilikuwa Kinamtafuta anayehusika.

Yaani kila kijiwe kilikuwa kimetumwa kimfikie mtu anyastahiki adhabu na siyo  bure bure . 

Hebu  tujitulize, turudi nyuma kisha tufikiri.  Allahu Akbar.

MUUJIZA WA JINA LA MTUME  “YAHYA BIN  ZAKARIAH”

سُوۡرَةُ آل عِمرَان

Sura Ya Al-Imran Aya Namba 35-41

إِذۡ قَالَتِ ٱمۡرَأَتُ عِمۡرَٲنَ رَبِّ إِنِّى نَذَرۡتُ لَكَ مَا فِى بَطۡنِى مُحَرَّرً۬ا فَتَقَبَّلۡ مِنِّىٓ‌ۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ (٣٥) فَلَمَّا وَضَعَتۡہَا قَالَتۡ رَبِّ إِنِّى وَضَعۡتُہَآ أُنثَىٰ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا وَضَعَتۡ وَلَيۡسَ ٱلذَّكَرُ كَٱلۡأُنثَىٰ‌ۖ وَإِنِّى سَمَّيۡتُہَا مَرۡيَمَ وَإِنِّىٓ أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ ٱلشَّيۡطَـٰنِ ٱلرَّجِيمِ (٣٦) فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ۬ وَأَنۢبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنً۬ا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا‌ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيۡهَا زَكَرِيَّا ٱلۡمِحۡرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزۡقً۬ا‌ۖ قَالَ يَـٰمَرۡيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا‌ۖ قَالَتۡ هُوَ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِ‌ۖ إِنَّ ٱللَّهَ يَرۡزُقُ مَن يَشَآءُ بِغَيۡرِ حِسَابٍ (٣٧) هُنَالِكَ دَعَا زَڪَرِيَّا رَبَّهُ ۥ‌ۖ قَالَ رَبِّ هَبۡ لِى مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً۬ طَيِّبَةً‌ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ (٣٨) فَنَادَتۡهُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةُ وَهُوَ قَآٮِٕمٌ۬ يُصَلِّى فِى ٱلۡمِحۡرَابِ أَنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحۡيَىٰ مُصَدِّقَۢا بِكَلِمَةٍ۬ مِّنَ ٱللَّهِ وَسَيِّدً۬ا وَحَصُورً۬ا وَنَبِيًّ۬ا مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ (٣٩) قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِى غُلَـٰمٌ۬ وَقَدۡ بَلَغَنِىَ ٱلۡڪِبَرُ وَٱمۡرَأَتِى عَاقِرٌ۬‌ۖ قَالَ كَذَٲلِكَ ٱللَّهُ يَفۡعَلُ مَا يَشَآءُ (٤٠) قَالَ رَبِّ ٱجۡعَل لِّىٓ ءَايَةً۬‌ۖ قَالَ ءَايَتُكَ أَلَّا تُڪَلِّمَ ٱلنَّاسَ ثَلَـٰثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمۡزً۬ا‌ۗ وَٱذۡكُر رَّبَّكَ ڪَثِيرً۬ا وَسَبِّحۡ بِٱلۡعَشِىِّ وَٱلۡإِبۡڪَـٰرِ (٤١)

TAFSIRI

35· (Kumbukeni) aliposema mke wa Imrani(baba yake Maryamu katika kamwomba Mola wake): “Mola wangu! Nimeweka nadhiri kwako aliyomo tumboni mwangu kuwa wakfu (wa kutumikia mambo ya dini); basi nikubalie. Bila shaka Wewe ndiye usikiaye na ujuaye.” . 36.Basi alipomzaa, alisema: “Mola wangu! Nimemzaa mwanamke”. na Mwenyezi Mungu anajua sana aliyemzaa “Na mwanamume (niliyefikiri kuwa nitamzaa) si sawa na mwanamke.(niliyemzaa). Na nimempa jina Maryamu (mtumishi wa Mungu). Nami namkinga kwako, yeye na kizazi chake, (uwalinde) na Shetani aliyebaidishwa na rehema yako.”

37.Basi Mola wake akampokea (yule mtoto) kwa kabuli njema na akamkuza kukua kwema, na akamfanya Zakaria awe mlezi wake. Kila mara Zakaria alipoingia chumbani (kwake) alikuta vyakula pamoja naye (huyo Maryamu). Akasema; “Ewe Maryamu! Unapata wapi hivi?” Akasema: “Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila kuwaza (mwenyewe).”

38.Pale pale Zakaria akamwomba Mola wake akasema: “Mola wangu! Nipe kutoka kwako mtoto mwema. Wewe ndiye usikiaye maombi (ya wanaokuomba).”

39.Mara Malaika wakamlingania, bali amesimama akisali chumbani, kwamba Mwenyezi Mungu anakupa khabari njema za (kuwa utazaa mtoto; umwite) Yahya, atakayekuwa mwenye kumsadikisha (Mtume atakayezaliwa) kwa neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu (Naye ni Nabii lsa) na atakayekuwa bwana kabisa na mtawa na Nabii anayetokana na watu wema. (Nao ni nyinyi).

40.Akasema (Zakaria): “Mola wangu! Nitapataje mtoto, na hali uzee umenifikia, na mke wangu ni tasa?” Akasema (Mwenyezi Mungu): Ndivyo vivyo hivyo; Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.”

4I. Akasema: “Mola wangu! Niwekee alama(ya kunitambulisha kuwa mke wangu kishashika mimba nipate kufurahi upesi). Akasema: “Alama yako ni kuwa hutaweza kusema na watu kwa siku tatu isipokuwa kwa ishara tu. Na umtaje Mola wako kwa wingi ‘na umtukuze (kwa kusali) wakati wa jioni na asubuhi.”

SHEREHE

Hebu  tuelekeze Darubini  katika Sura Ya Al-Imran Aya namba 35 mpaka 41.  

Kisa cha Imran ni Muujiza Mkubwa.  Bwana Imran na Mkewe  walikuwa  Wachamungu.  Mkewe alipokuwa na Mimba alikuwa na hamu sana atakayezaliwa awe Mtawa katika Nyumba ya Ibada ya Bayt Almaqdas. Pia aliweka Nadhiri kwamba Mtoto huyo awe mtumishi wa Kazi zinazohusu Dini peke yake. Kwa Neno zuri ni Kufanya WAQF  yaani tamaa yake ajitolee mtoto huyo atakapozaliwa awe kazi yake ni hiyo tu.

Lakini baada ya tu ya Kuzaliwa haikuwa hivyo kwani aliyezaliwa alikuwa mtoto wa Kike na sivyo alivyofikiri kwamba atakuwa mtoto wa kiume.

Baada tu ya Kuzaliwa mtoto ambaye alitiwa Jina “Maryam” Baba yake mzee Imran akafariki Dunia. Ilipigwa  kura kwa kutumia mianzi katika chombo chenye maji kwa yule atakeyemlea Mtoto huyu na Mwanzi  wa Zakariah ndiyo uliokuwa haukuinuka katika Chombo cha maji na ikawa kura hiyo imemwangukia.

Kwa hiyo Bwana Zakariah ndiye aliyepewa madaraka ya Kumlea mtoto huyo.

Katika Maisha Yake na Mtoto huyu Bwana Zakariah aliona Karamah au Ajabu Ajabu ya Mambo mazuri mazuri ya kushangaza ya Mtoto huyu  Na mojawapo  wa mambo haya ilikuwa ni Chakula alichokuwa akiruzukiwa Mtoto huyu kimuujiza.

Zakariah akwamwuliza “Je Maryam unapata wapi Chakula hiki”

Na akajibu kuwa  “kinatoka kwa Mwenyeezi Mungu”. 

Inasemekana kwamba Chakula hicho kilikusanya vitu  mbalimbali ambavyo siyo vya kawaida na ambavyo  havikuzoeleka katika sehemu na wakati huo.

Basi baada ya kusikia habari hiyo  Zakariah akaomba Dua kwa Mwenyeezi Mungu amtatulie tatizo lake naye pia amruzuku Mtoto kwani hakuwa na Mtoto.

Na alipokuwa katika  Sala akasikia Mwito wa Malaika ambaye alimbashiria atapata Mtoto ana  jina lake ni  “YAHYA”

Habari hii ilimshangaza sana kwani Mkewe alikuwa amezeeka na ni Tasa yaani Hazai lakini alijibiwa na Malaika kwamba Amri ya Mwenyeezi Mungu akitaka kitu basi huwa kama atakavyo. Analokitaka basi huwa na hakuna kitakachozuia. 

Nabii Zakariah alifurahi sana na hapo hapo akataka apewe Dalili zitakazomjuulisha wakati mkewe atakuwa na Mimba akajibiwa kwamba hataweza kuzungumza kwa muda wa siku tatu isipokuwa kwa ishara tu. Iwapo akihisi hivyo basi ajue wakati umefika na kwamba mkeo ameshika mimba.

Jambo la kufikiri hapa ni  Jina la mtoto. Jina hili halikutoka kwa Zakariah bali Mwenyeezi Mungu mwenyewe. Huyu ni Mtoto pekee Duniani ambaye Jina lake limetoka Kwa Mwenyeezi Mungu Mwenyewe. Huu siyo Muujiza Mdogo.

Jambo la kushagaza ni Jina “YAHYA”  kwani Lina maana ya “KUISHI”  “UHAI”  na “KUISHI MILELE”  ni kama kwamba Mwenyeezi Mungu anaashiria kwamba mtoto huyu atakayezaliwa ataishi  Maisha ya Milele.

Nabii “YAHYA”  anajulikana katika Kikristo  kama “John The Baptist. Huyu alikuwa Mtume na alikuja kabla  ya Nabii Isa.  (Wakristo  wanamuita Yesu).

Muujiza Ni Kwamba Jina lake  lina maana ya  “UHAI WA MILELE”  lakini  aliuawa na kukatwa kichwa ili kumridhisha na Kumfurahisha Mchumba wa Mfalme  

Mfalme wa Palestini alijulikana kwa jina kama Herod Antipas na Mchumba wa Mfalme aliyejulikana kwa  Jina Salome 

Msichana Huyu alitaka kichwa cha Mtume huyu kiletwe Juu ya Sinia na akione. 

Inasemekana kwamba Mfalme huyu  alitaka Kumuoa Salome ambaye alikuwa Mtoto wa Kaka yake.

(Kuna kisa kingine ambacho insemekana kwamba Mwanamke huyu alikuwa Mke wa Kaka yake na siyo mtoto wa Kaka yake)

Mtume  Yahya  alipinga ndoa hiyo 

Salome alipendelea aolewe na Mfalme na kisha yeye pamoja na Mjomba wake watawale pamoja hapo Palestina. 

Kwa hiyo katika Sherehe iliyoandaliwa na Mfalme  Msichana huyu alipewa nafasi ya Kuimba na Kudansi na alifanya hivyo kwa ufundi wa Juu sana  mbele ya Mfalme mpaka Mfalme akaharibika Akili.

Kisha Mfalme akamuuliza anachokipenda kwani yupo tayari kumpa chochote.

Msichana huyu inasemekana alikuwa na uzuri na Mjanja.

Akajibu anatamani  Mtume   Yahya akatwe kicha na kisha aletewe kichwa chake ili kulipiza Kisasi cha Nabii Yahya kwani alipinga Ndoa yake.

MUUJIZA WA JINA “YAHYA”

Hebu  tuelekeze Darubini katika  Aya hapa Juu. Jina YAHYA  tumesema lina maana ya uhai wa milele sasa tujiulize Suali;  Je mbona  Mtume YAHYA  aliuawa?

Mwenyeezi Mungu amemwita  YAHYA  kwa maana ataishi Milele sasa Mbona Ni Kinyume?  

Jibu  la suala hili  ni Rahisi.  Tunapata Jibu katika Aya Mbili zifuatazo:

Mwenyeezi Mungu anasema katika Kuruani Tukufu Sura Ya Al-Bakarah na Al-Imran

سُوۡرَةُ البَقَرَة وَلَا تَقُولُواْ لِمَن يُقۡتَلُ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٲتُۢ‌ۚ بَلۡ أَحۡيَآءٌ۬ وَلَـٰكِن لَّا تَشۡعُرُونَ (١٥٤)

TAFSIRI

154. Wala msiwaite wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu ni wafu, bali wapo hai (Uhai wa Kiakhera yaani Wa Kiroho, hatujui Namna yake), lakini nyinyi hamtambui.

سُوۡرَةُ آل عِمرَان وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱلَّذِينَ قُتِلُواْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أَمۡوَٲتَۢا‌ۚ بَلۡ أَحۡيَآءٌ عِندَ رَبِّهِمۡ يُرۡزَقُونَ (١٦٩)

TAFSIRI

169.Wala usiwadhani wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu (maiti). Bali wapo hai, wanaruzukiwa kwa Mola wao

Angalia Muujiza.  Allahu Akbar.

Mwenyeezi Mungu hakukosea hata kidogo. Maisha ya Milele kwani Nabii Yahya Amefariki kifo cha Kidini. Huyu ni SHAHIDI  Allahu Akbar.  Na Shahidi  Ni HAI  Milele. Allahu Akbar.  Je unaona Kuruani Ilivyo?  Kila Neno limechaguliwa Kwa Hekima Kubwa sana tean sana.  Allahu Akbar.  Angalieni  Miujiza isiyo na Mwisho.