SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Darubini-3/Kuruani

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

MTUME ALIYEPEWA UWEZO WA KUSIMAMISHA JUA

NABII  YUSHA BIN NUN

Katika Kuruani  kumetajika Mitume  25 ifuatayo:

Adam, Idris (Enoch), Nuh (Noah), Hud (Heber), Saleh (Methusaleh), Lut (Lot), Ibrahim (Abraham), Ismail (Ishmael), Ishaq (Isaac), Yaqub (Jacob), Yusuf (Joseph), Shu’aib (Jethro), Ayyub (Job), Dhulkifl (Ezekiel), Musa (Moses), Harun (Aaron), Dawud (David), Sulayman (Solomon), Ilyas (Elias), Alyasa (Elisha), Yunus (Jonah), Zakariya (Zachariah), Yahya (John the Baptist), Isa (Jesus) na Mohamad.

Kuna wengine wengi ambao hawakutajwa katika Kuruani. Kwa mfano  Mtume anayejulikana kwa Jina kama “Yusha Bin Nun”  (katika Biblia  Joshua)

Huenda Aya zifuatazo kutoka katika Kuruani Na Hadithi ya Mtume ﷺ zinamuashiria Mtume Huyu.

Hebu tuelekeze Darubini  yetu katika Aya za Kuruani na Hadithi  tupate Ushahidi wa Habari  inayosema kwamba Mtume Huyu  aliweza Kusimamisha  Jua Lisitue.

Kabla Ya Kupeleka Darubini  ningependelea  Kuelezea  Ukoo wa Nabii huyu.

Nabii Ibrahim  alizaa Watoto wawili

Ismael  na Isaac

Isaac akamzaa  Mtume  Yakubu  (Jacob) na Na Nabii Yakubu akazaa Watoto Kumi na Mbili. Katika Watoto hawa  12  Ambao wanahusika hapa ni  Nabii Yusuf (Joseph) Na Levi

Kwa hiyo  kutoka Katika  Ukoo wa Nabii  Yusuf  akazaliwa  Nabii  Yusha Bin Nun  na Katika Ukoo wa Levi akazaliwa Nabii Musa  (Moses).

Ni Ukoo Mrefu lakini nimefupisha. Yusha  baba yake ni  Ephraim ambaye alikuwa mtoto wa Nabii Yusuf.

Kwa kifupi Babu ya Nabii Musa na Yusha ni Mmoja  yaani Nabii  Isaac.

Baadhi ya Wanavyuoni wanasema kwamba Nabii Yusha ndiye aliyeongozana na Nabii Musa katika Safari yake.

Sura Ya Al-Kahf  namba 18 Aya Namba 60-64 zinazungumzia  habari za kijana Huyu ambaye aliyeongozana na Nabii Musa;

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَٮٰهُ لَآ أَبۡرَحُ حَتَّىٰٓ أَبۡلُغَ مَجۡمَعَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ أَوۡ أَمۡضِىَ حُقُبً۬ا (٦٠) فَلَمَّا بَلَغَا مَجۡمَعَ بَيۡنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُ ۥ فِى ٱلۡبَحۡرِ سَرَبً۬ا (٦١) فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَٮٰهُ ءَاتِنَا غَدَآءَنَا لَقَدۡ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَـٰذَا نَصَبً۬ا (٦٢) قَالَ أَرَءَيۡتَ إِذۡ أَوَيۡنَآ إِلَى ٱلصَّخۡرَةِ فَإِنِّى نَسِيتُ ٱلۡحُوتَ وَمَآ أَنسَٮٰنِيهُ إِلَّا ٱلشَّيۡطَـٰنُ أَنۡ أَذۡكُرَهُ ۥ‌ۚ وَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُ ۥ فِى ٱلۡبَحۡرِ عَجَبً۬ا (٦٣) قَالَ ذَٲلِكَ مَا كُنَّا نَبۡغِ‌ۚ فَٱرۡتَدَّا عَلَىٰٓ ءَاثَارِهِمَا قَصَصً۬ا (٦٤)

TAFSIRI

6o.Na (kumbukeni) Musa alipomwambia kijana wake: “Nitaendelea tu kwenda mpaka nifike katika maungano ya bahari mbili, au niendelee karne na karne (mpaka nikutane na huyo ninayetaka kukatana naye).

61.Basi walipofika wote wawili (mahali) zinapoungana (hizo bahari mbili) walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake kwenda baharini, bali ya kuwa inafanya alama. (Nabii Musa alisahau kumuuliza khabari ya samaki huyo, na yule kijana alisahau kumsimulia Nabii Musa habari ya samaki huyo).

62. Na walipoftka mbele (Musa) alimwambia kiiana wake “Tupe chakula chetu cha asubuhi; maana tumepata uchofu (mkubwa) katika safari yetu hii (ya sasa).

63. Akasema: “Unaona! Pale tulipopumzika katika mlima basi hapo nimesahau (kukupa habart ya) yule samaki. Na hakuna aliyenisahaulisa isipokuwa Shetani, nisikumbuke. Naye akashika Njia yake baharini kwa namna ya ajabu.”

64. (Musa) akasema: “Hapo ndipo tulipokuwa tunapataka.” Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia yao (ile ile)

na pia Katika Sura Ya Al-Maidah Namba 5  Aya Namba 22-23

قَالُواْ يَـٰمُوسَىٰٓ إِنَّ فِيہَا قَوۡمً۬ا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدۡخُلَهَا حَتَّىٰ يَخۡرُجُواْ مِنۡهَا فَإِن يَخۡرُجُواْ مِنۡهَا فَإِنَّا دَٲخِلُونَ (٢٢) قَالَ رَجُلَانِ مِنَ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡہِمَا ٱدۡخُلُواْ عَلَيۡہِمُ ٱلۡبَابَ فَإِذَا دَخَلۡتُمُوهُ فَإِنَّكُمۡ غَـٰلِبُونَ‌ۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَتَوَكَّلُوٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ (٢٣)

TAFSIRI

22. Wakasema: “Ewe Musa! Huko kuna watu majabari. Nasi hatutaingia huko mpaka watoke humo; wakitoka humo hapo tutaingia.”

23. Watu wawili miongoni mwa wale waliomwogopa (Mungu) ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha, walisema (kuwaambia wenzao): “Waingilieni katika hilo Iango (la nchi yao); maana mtakapowaingilia hapo, kwa yakini nyinyi mtashinda. Na tegemeeni juu ya Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini

SHEREHE

Baadhi ya Wanavyuoni wanasema kwamba Aya Namba 23 hapa Juu  inaashiria Nabii Yusha Bin Nun. Yaani katika  wawili hawa  mmojawapo alikuwa Yusha.

Inasemekana kwamba Baada ya Kufariki Nabii Harun na Nabii Musa  basi  Waisraeli  waliongozwa na Nabii Yusha katika Kuikomboa  Jerusalem. 

Kwani hapo mwanzo  Waisraeli  walikuwa wakitangatanga kwa muda wa miaka 40 baada ya Kuasi maamrisho ya Nabii Musa. 

Walioasi Amri ya Mwenyeezi Mungu walipewa Mtihani mkubwa. Asi hilo ni kukataa Kuikomboa Palestina kwa hoja kwamba kuna watu wenye nguvu kwa kweli  wao waliogopa kupigana. 

Kuivunja kwa Amri ya Nabii Musa ambayo ni Ya Mwenyeezi Mungu  ni Kosa kubwa.

Baada ya hapo Waliadhibiwa kwa Kujikuta hawana Nchi na  Utulivu bali kutanga tanga katika Jangwa kwa muda mrefu. Kuruani inataja habari hizi na pia miaka  waliopoteza ilikuwa  40.

Habari Hii Imeelezewa katika Sura Hii ya Al-Maidah Aya Namba 26

قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيۡہِمۡ‌ۛ أَرۡبَعِينَ سَنَةً۬‌ۛ يَتِيهُونَ فِى ٱلۡأَرۡضِ‌ۚ فَلَا تَأۡسَ عَلَى ٱلۡقَوۡمِ ٱلۡفَـٰسِقِينَ (٢٦)

TAFSIRI

6. (Mwenyezi Mungu) akasema: “Basi wameharimishiwa (ardhi) hiyo kwa (muda wa) miaka arubaini; watatangatanga (mumu humu) ardhini (jangwani muda wote huo). Basi usihuzunike juu ya watu maasi.”

SHEREHE

Mara kwa mara  Mayahudi  walifanya Ukaidi na  Ilifikia Kutengeneza Miungu  Ya Masanamu. Kwa mfano  walitengeneza Sanamu la   “NDAMA” ambalo lilitengenezwa kwa Dhahabu.

Watu hawa walikuwa wakaidi sana. Waisraeli ambao walikuwa chini ya Uongozi wa  Nabii Yusha ni Vizazi Vipya na Siyo hao waliovunja Amri ya Nabii Musa ya kuikomboa Jerusalem.

Nabii Yusha alipofika hapo Jerusalem (Palestina). Ilikuwa Jioni siku ya Ijumaa na kwa vile Mayahudi (Waisraeli) hawawezi  Kupigana Jumamosi kwani ni Siku Kuu ya Kiyahudi ambayo  inajulikana kama Sabath.

Yusha Aliinua mikono Juu na Kuomba Mwenyeezi Mungu alisimamishe Jua lisitue mpaka wamalize kazi ya Kuuteka Mji  huo wa Jerusalem.

Dua Yake Ilikubaliwa na Jua Likasimamishwa kwa uwezo wake Mola

Tusifikiri  Habari hizi za Uongo kwani Kuna Hadithi  iliyopokelewa na Bukhari na Pia Muslim ambayo Wanavyuoni wanasema  Hadithi hii inamuashiria Nabii Yusha.

الخامس‏:‏ عن أبي هريرة ، رضي الله عنه ، قال‏:‏ قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ‏:‏ ‏ “‏غزا نبي من الأنبياء صلوات الله وسلامه عليهم فقال لقومه‏:‏ لا يتبعني رجل ملك بضع امرأة‏.‏ وهو يريد أن يبني بها ولما يبن بها، ولا أحد بنى بيوتا لم يرفع سقوفها، ولا أحد اشترى غنما أو خلفات وهو ينتظر أولادها‏.‏ فغزا فدنا من القرية صلاة العصر أو قريباً من ذلك، فقال للشمس‏:‏ إنك مأمورة وأنا مأمور، اللهم احبسها علينا، فحبست حتى فتح الله عليه، فجمع الغنائم، فجائت -يعني النار- لتأكلها فلم تطعمها، فقال ‏:‏ إن فيكم غلولاً، فليبايعني من كل قبيلةٍ رجل، فلزقت يد رجل بيده فقال‏:‏ فيكم الغلول، فلتبايعني قبيلتك، فلزقت يد رجلين أو ثلاثة بيده فقال‏:‏ فيكم الغلول‏:‏ فجاؤوا برأس مثل رأس بقرة من الذهب، فوضعها فجاءت النار فأكلتها، فلم تحل الغنائم لأحد قبلنا، ثم أحل الله لنا الغنائم لما رأى ضعفنا وعجزنا فأحلها لنا‏”‏ ‏(‏‏(‏متفق عليه‏)‏‏)‏ ‏.‏

TRANSLATION  (ENGLISH)

Abu Hurairah (May Allah be pleased with him) reported that the Messenger of Allah (ﷺ) said: “One of the earlier Prophets who was out on an expedition proclaimed among his people that no man should follow him who had married a woman with whom he wished to cohabit but had not yet done so, or who had built houses on which he had not yet put the roofs, or who had bought sheep or pregnant she-camels and was expecting them to produce young. He, then, went on the expedition and approached the town at the time of the ‘Asr prayer or little before it. He then told the sun that both it and he were under command and prayed Allah to hold it back for them, so it was held back till Allah gave him victory. He collected the spoils and it (meaning fire) came to devour these, but did not. He said that among the people there was a man who stole from the booty. He told them that a man from every tribe must swear allegiance to him, and when a man’s hand stuck to his, he said: “There is thief among you and every individual of your tribe must swear allegiance to me”. (In course of swearing of allegiance,) hands of two or three persons stuck to his hand. He said: “The thief is among you”. They brought him a head of gold like a cow’s head and when he laid it down, the fire came and devoured the spoils. Spoils were not allowed to anyone before us, then Allah allowed spoils to us as He saw our weakness and incapacity and allowed them to us”.

[Al-Bukhari and Muslim].

Wengi  hatujawahi kumsikia Nabii huyu na pia  Muujiza za Kusimamisha Jua.  Tumesoma Kuhusu Muujiza wa Mtume Mohamad ﷺ wa  Kupasua Mwezi.  Allahu Akbar.

Kwa kweli kuna mengi ya Kusoma. Dunia na Ulimwengu ni wa zamani. Binaadamu  aliumbwa baadaye baada ya Muda mrefu  sana kama alivyosema Mwenyeezi Mungu katika Kuruani Tukufu.   Sura Namba 76  Aya Namba 1  

هَلۡ أَتَىٰ عَلَى ٱلۡإِنسَـٰنِ حِينٌ۬ مِّنَ ٱلدَّهۡرِ لَمۡ يَكُن شَيۡـٴً۬ـا مَّذۡكُورًا (١)

1. Hakika ulimpitia Binaadamu wakati mrefu katika dahari, hakuwa kitu kinachotajwa. (Binaadamu ndiye kiumbe cha mwisho kuletwa ulimwenguni).