UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MIUJIZA ISIYO NA MWISHO
Baada ya kufikiri sana Maajabu ya Kuruani nikakumbuka Usemi au Methali walizoniambia Rafiki zangu miaka Mingi iliyopita (Zaidi ya miaka Arubaini) tulipokuwa wanafunzi katika Chuo Kikuu.
Rafiki wa Kwanza ni Sheikh (Ndugu) kutoka Mwanza na wa pili ni Sheikh (Ndugu) kutoka Zanzibar.
Katika mazungumzo Rafiki wa Mwanza aliniambia Usemi Mzuri sana wa Kiswahili unaosema
“KULIKOUNGUA SHOKA KUKABAKI MPINI”
Kwa hiyo ningependelea kuutumia usemi huu katika Mlango huu kwa kusema
“ELIMU ILIYOPO KATIKA KURUANU TUKUFU NI NYINGI MNO NA KWA KWELI KATIKA KITABU HIKI NDIPO PALIPOUNGUA SHOKA KUKABAKI MPINI”
Na Rafiki wa pili kutoka Zanzibar alikuwa akiniambia kila tukikutana.
SHEIKH AL-AMIN JE TUTAFIKA HUKO?
Kwa usemi huu alikuwa ana maana kwamba
KAZI YA HAPO SHULENI YAANI MASOMO SIYO RAHISI NA INABIDI JUHUDI KUBWA NA KWA HIYO JE TUTAYAWEZA?
Leo hii Usemi huu ninaukumbuka mpaka leo na kila ninapofikiri Aya za Kuruani. Kwa kweli ninajiuliza Suala hili kwa kusema.
“JE TUTAFIKA HUKO? JE TUTAFIKIA LINI KUMALIZA KUSOMA MIUJIZA YA KURUANI YOTE? JE INAWEZEKANA?”
Kwa usemi huu ninaona “HATUTAFIKA KABISA” Kwani hakuna Mwisho. Kuruani imejaa Elimu isiyo na Mwisho.
Mwenyeezi Mungu amefanya hivyo ili watu wauukubali Uislamu na waingie katika Dini hii ili Mwisho wa Dunia kusiwe na Hoja. Tusije tukabisha na kusema hatukuletewa Ujumbe wowote.
Katika Mlango huu nitajitahidi kuweka Miujiza mbali mbali. Kwa kweli Inashangaza sana. Inathibitisha kwamba Kuruani siyo maneno ya Binaadamu hata kidogo.
Allahu Akbar. Kama huamini basi endelea kufuatilia habari za mlango huu kwani Mwenyeezi Mungu akipenda kila nitakapo pata nafasi nitakuwa nikiongeza mapya yaani kila mara kama bado nipo hai katika dunia hii. Afya au Uzima ni muhimu sana. Na pia Usinisahau katika Dua zeni kwani ni muhimu sana. Mimi sina uwezo isipokuwa Uwezo unatoka kwa Mwenyeezi Mungu.
Pia Nawashukuru wale ambao nasoma kwao. Kila anayenifundisha Mwenyeezi Mungu ampe kila la kheri katika Dunia na Akhera. Mengine ni yangu na Mengine ni ya Walimu zangu. Namuomba Meenyeezi Mungu awape kila la kheri kwa Juhudi zao kubwa.
Sasa Tuanze kazi.
MUUJIZA WA KWANZA
Hebu Tupeleke Darubini yetu katika Sura Ya Al-Fatiha ambayo pia ina majina Mbalimbali. Na katika majina hayo mojawapo ni “UMMU AL_KITAAB” yaani MAMA WA KITABU. (The Mother of The Book) au “ASABAA ALMATHANI” yaani AYA SABA ZINAZOKARIRI. (The seven repeatedly recited) yaani Ni Aya Saba ambazo zinatumika katika Kila Sala na kwa hiyo matumizi yake yana kariri kariri kila wakati. Na Mwenyeezi Mungu anathibitisha Jina hili katika Sura Ya Al-HIjr namba 15 Aya namba 87
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَـٰكَ سَبۡعً۬ا مِّنَ ٱلۡمَثَانِى وَٱلۡقُرۡءَانَ ٱلۡعَظِيمَ (٨٧)
Mwenyeezi Mungu anamwambia Mtume Mohamad ﷺ
Kwa hakika Tumekupa Aya Saba zenye kukariri na pia Kuruani Tukufu. yaani Sura ya Alfatiha na pia Sura nyinginezo 113 za kuruani Tukufu.
سُوۡرَةُ الفَاتِحَة
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (١) ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٢) ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (٣) مَـٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ (٤) إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ (٥) ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٲطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ (٦) صِرَٲطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ (٧)
SHEREHE
Hebu tuchunguze idadi ya Herufi za Jina lake Mwenyeezi Mungu katika Sura Hii. Yaani Jina lake la
الله (ALLAH)
ALIF= imetumika mara 22
Alam= imetumika mara 22
Ha= imetumika mara 5
Jumla ni 22 + 22 + 5=49
Je unaona maajabu. Namba 49 ni sawa na kusema
7 x7 ambayo ni 49
Je unaona Namba 7. Yaani Sura imepewa Jina na Mwenyeezi Mungu “Aya Saba Zinazokariri” na herufi za Jina lake Yaani الله (ALLAH) pia zimakariri mara 49 ambayo ni sawa na 7 x 7. Hapa Namba 7 ni Muujiza na siyo bure bure. Mpangilio wa hekima kubwa.
MUUJIZA WA PILI
Sura ya Mohamad namba 47 Ina Jumla za Aya 38
Hebu Tuelekeze Darubini Katika Sura Ya Mohamad.
Tuchunguze Herufi za Jina Mohamad katika Sura hii ambayo imepewa Jina lake.
MIM=Imetumika mara 223
HAA=Imetumika mara 23
MIM=Imetumika mara 223
DAL=Imetumika mara 35
Jumla ya Herufi katika Sura hii ni
223 + 23 + 223 + 35=504
Kwa hiyo 504 kihesabu ni sawa na kusema 63 X 8
yaani 63 x 8=504
Unaona Muujiza katika Jina la Mtume?
Aliishi miaka 63 tu. kwa hiyo Umri wake ulikuwa umefichika katika Idadi ya Herufi ya Jina lake. Allahu Akbar. Yaani Hata yeye mwenyewe alikua hakujua kwani hakuna anayejua siku atakayofariki dunia. Angalia Maajabu haya. Siyo mambo madogo.
MIUJIZA INAENDELEA….