UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
Jumamosi Tarrehe 27/08/2022
NINAWATUMIA SALAAM NYINGI KWA WASOMAJI WOTE WA WEBSITE HII. “Assalaam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh” Salaam Kwenu, Rahma na Baraka Zake Mwenyeezi Mungu Ziwafikie.
Alhamdulilah. Leo Jua Zuri limechomoza na Ni Wakati Mzuri wa kuwaletea Habari Nzuri kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu Mtukufu.
Ninachukua Kalamu na Kuwaandikia Habari nzuri Sana ambayo inatuliza Roho.
Kwanza Ningependelea kuwajuulisha Kuwa Katika Maandishi Yangu huenda utakuta Makosa Madogo madogo ya Herufi katika Maneno. Makosa haya yanatokana na Uchapishaji wa haraka haraka. Nikipata nafasi nitajitahidi kusoma tena makala zangu na kuzisahihisha. Nina hakika kuna makosa makosa ya aina hii lakini ukisoma vizuri utaelewa maana niliyokusudia na hilo ndilo lengo.
MUUJIZA WA KWANZA (POLISI WATATU)
Sasa Tuelekeze Darubini Yetu katika Habari Nzuri katika Sura Tatu za Kuruani. Sura Ya “GHAFIR”, “AL-SWAF” na “AL-SHAMS”
Tusiende mbali bali Ninaelekeza Darubini katika Sura Hizi tatu tu.
Kabla Ya kuchunguza Sura Hizi ningependelea Kuwajuulisha kwamba Kuruani Imekusanya Sura 114 na Ina Jumla za Aya 6236 na Mara ya Kwanza Kutajika neno Kuruani Tukufu kuanzia Mwanzo wa Msahafu ni katika Sura Ya Al-Bakarah Aya Namba 185. Yaani Ukihesabu Kuanzia Mwanzo wa Msahafu Kuanzia Sura Ya Al-Fatiha ambayo Ina Aya 7 mpaka katika Aya namba 185 utapata Jumla za Aya ni 192.
Aya namba 185 katika Sura ya Al-Bakarah ni kama ifuatayo
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْءَانُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَٰتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُوا الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Kwa hiyo Aya hii ni ya 192 kuanzia Mwanzo wa Msahafu ambayo inataja neno “KURUANI”
Kwa Kifupi
Kuruani Ina Sura 114
Kuruani Ina Aya 6236
Neno الْقُرْءَانُ “KURUANI” ni la 192 kuanzia Sura Ya Al-Fatiha.
Katika Utafiti huu Kumbuka Namba Hizi Tatu.
Sasa Tuelekeze Darubini katika Hizo Sura Tatu Tulizozitaja Hapa Juu Uone Muujiza. Allahu Akbar. Muujiza sio Mdogo. Unathibitisha Kwamba Kuruani Imepangwa. Mpangilio wake wa Kimaneno, Kiherufi na Aya zake zote ni Muujiza Mtupu.
Sasa Tuanze Utafiti:
1/SURA YA GHAFIR NAMBA 40 INA JUMLA ZA AYA 85 NA JUMLA YA HERUFI 5041
2/SURA YA AL-SWAF NAMBA 61 INA JUMLA ZA AYA 14 NA JUMLA YA HERUFI 945
3/SURA YA AL-SHAMS NAMBA 91 INA JUMLA ZA AYA 15 NA JUMLA YA HERUFI 250
Hebu Tujumlishe namba za Sura, Aya na Maneno.
Jumla Za Sura=40 + 61 + 91=192
Jumla Za Aya=85 + 14 + 15=114
Jumla Za Herufi=5041 + 945 + 250=6236
Je Unaona Maajabu. Hizi Sura Tatu zimetupa habari za kushangaza. Kwanza namba 192 Inashiria Jina la Kuruani ni Aya ya 192 kuanzia mwanzo wa Msahafu. Kisha Namba 114 inashiria Jumla Ya Sura za Kuruani na Namba 6236 inaashiria Jumla ya Aya za Kuruani yote.
Allahu Akbar. Kuruani Imapimwa kila kitu. Yaani Baadhi ya Sura Zinathibitisha Ukweli wa Kuruani yote. Sura Hizi Tatu ni kama Polisi wanailinda kuruani isigeuzwe. Ni baadhi ya Mapolisi Watatu wa kitabu hiki.
Hebu Fikiri mwenyewe uone haya maajabu makubwa. Mapolisi watatu wanailinda Kuruani Tukufu. Yaani Kuruani inajilinda yenyewe.
Hakuna Upuuzi. Hakuna Atakayeibadili kwa kuongeza au Kuipunguza. Allahu Akbar. Ingegeuzwa au kupunguzwa basi Tusingepata Miujiza kama hii..
Ufundi huu tunaweza kuuita kwa ibara inayosema
“Iterlocking Mathematical Values” (Thamani za Kihesabu zilizofungamana au Makufuli yaliyofungamana.)
Allahu Akbar. Allahu Akbar. Kwa kweli Nimeivulia Kofia Kuruani. Ukubwa wa Kuruani unathibitisha ukubwa wa Mwenyeezi Mungu. Ni Hotuba Yake. Na Ikiwa ni Hotuba yake basi je Aliyeiandaa atakuwa vipi?
MUUJIZA WA PILI (NAMBA ZA AYA NA IDADI ZA AYA)
Sasa nitawaletea Muujiza wa pili. Kwa kweli inafurahisha Nafsi.
Nilipokuwa bado kijana wa umri mdogo Rafiki yangu alikuwa akiniambia kwama Pesa ndiyo “SABUNI YA ROHO” kila akiniona ninashika Pesa mkononi basi ananiambia hiyo Bwana ndiyo Sabuni ya Roho. Rafiki huyu alikuwa hakukosea. Kwa kweli Pesa ni Sabuni ya Roho kweli sio kosa hata kidogo.
Usemi huu ningependelea kuutumia leo pia na kusema
“KURUANI NDIYO SABUNI YA ROHO KUBWA KULIKO PESA AU
CHOCHOTE KILE TUNACHOKIJUA NA TUSICHOKIJUA”
Hebu tujifurahishe kwa Muujiza Mtamu wa Kuruani. Sasa tuelekeze Darubini katika Aya Hizi Nne tuone Ya Kushangaza. Allahu Akbar.
Jina La Mtume ﷺ Yaani Mohamad ﷺ Limetajika katika Kuruani Mara 4 tu katika Aya Zifuatazo Nne.
Kabla Ya kuendelea na Muujiza huu ningekushauri Utengeneze Chai iwe karibu yako na ikiwezekana Mandazi au Vitumbua Pia.
Huku unakunywa na kula kwa Raha yako bila wasiwasi soma Muujiza unaofuata Wenye Utamu zaidi Ya Asali
Umetengenezwa na Muumbaji wa kila kitu. Ni zawadi aliyotengeneza kwa ajili ya Viumbe vyake.
1/SURA YA AL_IMRAN NAMBA 3 AYA NAMBA 144
وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ أَفَإِين مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَٰبِكُمْ وَمَن يَنقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَن يَضُرَّ اللَّهَ شَيْءًا وَسَيَجْزِي اللَّهُ الشَّٰكِرِينَ
2/SURA YA AL-AHZAB NAMBA 33 AYA NAMBA 40
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَٰكِن رَّسُولَ اللَّهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّنَ وَكَانَ اللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا
3/SURA YA SURA YA MOHAMAD NAMBA 47 AYA NAMBA 2
وَالَّذِينَ ءَامَنُوا وَعَمِلُوا الصَّٰلِحَٰتِ وَءَامَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّءَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ
4/SURA YA AL-FATH NAMBA 48 AYA NAMBA 29
مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ تَرَىٰهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَٰنًا سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَىٰةِ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْءَهُ فَءَازَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ ءَامَنُوا وَعَمِلُوا الصَّٰلِحَٰتِ مِنْهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا
Hizi ndizo Aya nne ambazo zimetaja Jila Mohamad ﷺ katika Kuruani yote.
Sasa Tuelekeze Darubini Yetu katika Namba Za Aya na Sura tuone Muujiza wa Kiajabu usio na Mwisho. Allahu Akbar.
Kufuatana na Mpangilio wa Sura Za Msahafu (Yaani Mpangilio wa Sura za Msahafu ni tofauti na Mpangilio wa Kushushwa kwa Kuruani) Kama Misahafu tuliyonayo leo hii. Haikupangwa bure bure bali Muujiza.
Kufuatana na Mpangilo wa Sura katika Msahafu Mara ya Kwanza Kutajwa kwa Jina La Mtume ﷺ ni Katika,
SURA YA AL_IMRAN NAMBA 3 AYA NAMBA 144
na mara ya Mwisho kutajwa Jina La Mtume Mohamad ﷺ ni katika,
SURA YA AL-FATH NAMBA 48 AYA NAMBA 29
Angalia Vizuri Namba za Aya.
Aya namba 144 na Aya namba 29
Kumbuka vizuri namba hizi mbili.
Sasa ukihesabu Aya zote kuanzia Aya namba 144 mpaka Aya Namba 29 utapata Jumla ya Aya ni 4176
yaani Elfu Nne Mia Moja na Sabini na Sita.
Je unajua Kwamba Namba hii kihesabu ni sawa na
144 mara 29
yaani 144 X 29=4176
Ebwe, Hebu angalia Maajabu haya.
Namba 4176 ni sawa na 144 x 29 sasa mbona tunapata Namba ya Aya ya kwanza kutajwa kwa Mtume ni 144?
na Aya Namba 29 ni mara ya mwisho kutajwa kwa Mtume?
Unaona Maajabu.
Unaona Muujiza.
Mjomba Usibabaike. Fumbua Macho. Hii ndiyo Kuruani Tukufu.
Muujiza unaopita miujiza yote.
Tumehesabu Idadi ya Aya kisha tumepata namba 144 na 29 ambazo ni namba ya Aya ya kwanza kutajika kwa mtume na pia Aya ya Mwisho.
Je onaona Ukubwa wa Mwenyeezi Mungu Alivyo?
Nani anayeweza kuandika Kitabu na kafanya hivi?
Ndugu zanguni ni nani Mfalme?
Ni Nani Mfalme?
Jawabu ni moja tu. Ni Muumba
“Lilahi Alwahid AlQahar”
Ni Yule Yule Mkubwa Mwenye Nguvu aliyeumba kila kitu.
Allahu Akbar. Allahu Akbar.
Kabla Ya kuendelea na Miujiza ningependelea Kukuletea Msemo wa Mshairi wa Kifarsi (Persian) Maarufu Jalal ad-Din Muhammad Rumi Alizaliwa Mwaka 1207 (CE) yaani miaka ya kikristo.
Mshairi Huyu alisema kwamba
“Lazima Uendelee Kuuvunja Moyo wako mpaka Ufunguke”
Katika Usemi huu ana maana kwamba Moyo huwa imefungika na kwa hiyo ufanye juhudi kuufungua kwa juhudi zako zote. Yaani Uufungue kwa kusoma kila cha faida katika maisha yako. Usijifungie na fikra zako mbaya bali uufungue moyo wako katika kila la kheri na faida.
Aliulizwa pia Suala lifuatalo
“Je Unapata Faida Gani katika Sala?”
Akajibu “Sipati Faida Yeyote bali Nimepoteza”.
“Nimepoteza Majivuno”
“Nimpoteza Hasira”
“Nimepoteza Maradji ya nafsi”
“Nimepoteza Ulafi”
“Nimepoteza Hamu ya Udanganyifu”
“Nimepoteza Hamu ya Kufanya Maasi”
“Nimepoteza Kukata Tamaa”
Haya ndiyo majibu ya Bwana Rumi. Alikuwa Philosopher na Mshairi mkubwa katika wakati wake na alikuwa mashuhuri sana. Mwenyeezi Mungu ambariki.
Baada ya Kujiburudisha na Mashairi ya Bwana Rumi Sasa tuendelee na Miujiza Yetu.
MUUJIZA WA TATU (SURA YA AL-IKHLAS)
Nimekwisha Kuzungumzia Miujiza mbalimbali ya Sura Hii katika Milango mingineyo ya Website hii.
Kama nilivyosema Kuruani ina miujiza isiyo na mwisho. Kwa hiyo leo nitaelezea Nyongeza ya Muujiza kutoka katika Sura Ya A-lIkhlas.
Sasa Tuelekeze Darubini yetu katika Sura Hii tuone Maajabu yasiyo na Mwisho.
Sura Ya Al-Ikhlas Namba 112 Aya 4
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ/ اللَّهُ الصَّمَدُ/ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ/ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
Kwanza Tuelewe kwamba Katika Lugha ya Kiarabu Hapo zamani kulikuwa na Herufi ambazo zilijulikana kama ABJAD na baadaye Herufi zikageuzwa na kuitwa HIJAI
herufi za ABJAD zimepangika kama ifuatavyo
Alif
Ba
Jim
Daj
…. Na zote Nyinginezo Mpaka mwisho yaani Hamzah
Na Herufi Za Hijai za kisasa ni kama ifuatavyo:
Alif
Baa
Taa
Thaa
………Na zote Nyinginezo Mpaka mwisho yaani Hamzah.
kwa hiyo mipangilio ya aina ya herufi hizi mbili inatofautiana.
Muujiza wa leo tutafanya utafiti kwa kutumia Herufi za hapo zamani yaani Herufi za ABJAD
Ukizipanga herufi hizi kwa kutumia Namba kama ifuatavyo
Alif Ni Namba 1
Ba Ni Namba 2
Jim ni Namba 3
Dal ni Namba 4
Ufanye hivyo mpaka mwisho wa herufi zote.
Sasa tuanze Utafiti wetu. Tuje na Darubini na tuanze uchunguzi katika Aya hizi 4 za Sura hii ya Al-Ikhlas.
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ/ اللَّهُ الصَّمَدُ/ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ/ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
Ukichunguza Aya hizi nne utaona Kuna Alama Ya Haraka moja tu ya Kisrah nayo ipo chini ya Herufi Ya LAMU nayo imegawanya Aya hii katika Herufi 23 kwa upande wa kushoto na 23 kwa upande wa Kulia.
Ngoja nigawe Upate kuona kwa macho:
قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ/ اللَّهُ الصَّمَدُ/ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ/ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ
Herufi ya Lamu yenye Kasrah chijni yake ipo katika Neno يَلِدْ “YALID”
Sasa tukigeuza Herufi 23 za upande wa kushoto katika Namba kwa kufuata sehemu (Positions) za Herufi za ABJAD tulizozitaja hapa juu na kuzijumlisha utapata Jumla ya herufi hizi 23 ni = 198
Ajabu Ni Kwamba Ukifanya hivyo hivyo na Herufi 23 za Upande wa Kushoto utapata Jumla ya Herufi hizo 23 ni 198 Pia
Sasa tuelekeze Darubini kuanzia Sura Hii namba 112 mpaka mwisho yaani katika Sura Ya Al-Nas.
Angalia Muujiza. Ukihesabu Aya zote kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Al-Ikhlas mpaka Mwisho wa Msahafu yaani katika Sura ya Al-Nas basi Jumla Ya Aya zote ni 198 Pia!!!!!
Angalia Mpangilio wa Kushangaza. Je unaona Maajabu yasiyo na Mwisho.
Namba 198 Ilivyokariri mara 3 mfululizo. Ndugu Yangu, Mjomba wangu huoni Muujiza huu? Kwa nini imepangika hivi?
Jawabu ni “HII NDIYO KURUANI TUKUFU ILIVYO”
Hakuna Mfano wowote wa kitabu chochote ulimwenguni kama hiki. Je unaona?
Allahu Akbar. Allahu Akbar. Kwa kweli Nimeivulia Kofia. Hata Super Computer haiwezi kufua Dafu.