UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
01/10/2022
Nashukuru Mwenyeezi Mungu kwa kunipa Uzima na Kuendelea na Miujiza Mipya. Siku ya leo nimeweka nia kuandika Mlango huu ambao utakusanya Miujiza Mbalimbali. Kwa hiyo Kwa siku la leo hautaona Miujiza yote lakini Mwenyeezi Mungu akipenda baadhi yake itakamilika Usiku au kesho. Usishangae unaposoma kwani otaona maudhui na sherehe zinabadilika badilika kwani bado upo katika maandalizi.
Miujiza Hii imenipa faida na nimeona tugawane faida hizi baina yangu na nyinyi wasomaji.
1/MUUJIZA KATIKA SURA YA AL-KAHF
Moja kwa moja Nitaanza na Maajabu Katika Sura Ya Al-Kahf Namba 18. Nimekwisha Elezea Miujiza Mbalimbali Ya Sura Hii Katika Sehemu mbalimbali za Website hii na Leo kuna Nyongeza. Kwa kweli Miujiza ya Kuruani haina Mwisho.
Sasa Nitapeleka Darubini katika Sura Hii ya Al-Kahf namba 18 Kuanzia Aya Namba 9 Mpaka 26
Kwanza Nitazinukulu Aya Hizo kisha Tupeleke Darubini yetu katika Aya Mbili inayotuhusu. Aya Namba 22 na 25
(Aya hizi Mbili nimebadili Rangi)
سُوۡرَةُ الکهف
أَمۡ حَسِبۡتَ أَنَّ أَصۡحَـٰبَ ٱلۡكَهۡفِ وَٱلرَّقِيمِ كَانُواْ مِنۡ ءَايَـٰتِنَا عَجَبًا (٩)
إِذۡ أَوَى ٱلۡفِتۡيَةُ إِلَى ٱلۡكَهۡفِ فَقَالُواْ رَبَّنَآ ءَاتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحۡمَةً۬ وَهَيِّئۡ لَنَا مِنۡ أَمۡرِنَا رَشَدً۬ا (١٠)
فَضَرَبۡنَا عَلَىٰٓ ءَاذَانِهِمۡ فِى ٱلۡكَهۡفِ سِنِينَ عَدَدً۬ا (١١)
ثُمَّ بَعَثۡنَـٰهُمۡ لِنَعۡلَمَ أَىُّ ٱلۡحِزۡبَيۡنِ أَحۡصَىٰ لِمَا لَبِثُوٓاْ أَمَدً۬ا (١٢)
نَّحۡنُ نَقُصُّ عَلَيۡكَ نَبَأَهُم بِٱلۡحَقِّۚ إِنَّہُمۡ فِتۡيَةٌ ءَامَنُواْ بِرَبِّهِمۡ وَزِدۡنَـٰهُمۡ هُدً۬ى (١٣)
وَرَبَطۡنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ إِذۡ قَامُواْ فَقَالُواْ رَبُّنَا رَبُّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ لَن نَّدۡعُوَاْ مِن دُونِهِۦۤ إِلَـٰهً۬اۖ لَّقَدۡ قُلۡنَآ إِذً۬ا شَطَطًا (١٤)
هَـٰٓؤُلَآءِ قَوۡمُنَا ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦۤ ءَالِهَةً۬ۖ لَّوۡلَا يَأۡتُونَ عَلَيۡهِم بِسُلۡطَـٰنِۭ بَيِّنٍ۬ۖ فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبً۬ا (١٥)
وَإِذِ ٱعۡتَزَلۡتُمُوهُمۡ وَمَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ فَأۡوُ ۥۤاْ إِلَى ٱلۡكَهۡفِ يَنشُرۡ لَكُمۡ رَبُّكُم مِّن رَّحۡمَتِهِۦ وَيُهَيِّئۡ لَكُم مِّنۡ أَمۡرِكُم مِّرۡفَقً۬ا (١٦)
۞ وَتَرَى ٱلشَّمۡسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَٲوَرُ عَن كَهۡفِهِمۡ ذَاتَ ٱلۡيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقۡرِضُہُمۡ ذَاتَ ٱلشِّمَالِ وَهُمۡ فِى فَجۡوَةٍ۬ مِّنۡهُۚ ذَٲلِكَ مِنۡ ءَايَـٰتِ ٱللَّهِۗ مَن يَہۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَلَن تَجِدَ لَهُ ۥ وَلِيًّ۬ا مُّرۡشِدً۬ا (١٧)
وَتَحۡسَبُہُمۡ أَيۡقَاظً۬ا وَهُمۡ رُقُودٌ۬ۚ وَنُقَلِّبُهُمۡ ذَاتَ ٱلۡيَمِينِ وَذَاتَ ٱلشِّمَالِۖ وَكَلۡبُهُم بَـٰسِطٌ۬ ذِرَاعَيۡهِ بِٱلۡوَصِيدِۚ لَوِ ٱطَّلَعۡتَ عَلَيۡہِمۡ لَوَلَّيۡتَ مِنۡهُمۡ فِرَارً۬ا وَلَمُلِئۡتَ مِنۡہُمۡ رُعۡبً۬ا (١٨)
وَڪَذَٲلِكَ بَعَثۡنَـٰهُمۡ لِيَتَسَآءَلُواْ بَيۡنَہُمۡۚ قَالَ قَآٮِٕلٌ۬ مِّنۡہُمۡ ڪَمۡ لَبِثۡتُمۡۖ قَالُواْ لَبِثۡنَا يَوۡمًا أَوۡ بَعۡضَ يَوۡمٍ۬ۚ قَالُواْ رَبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِمَا لَبِثۡتُمۡ فَٱبۡعَثُوٓاْ أَحَدَڪُم بِوَرِقِكُمۡ هَـٰذِهِۦۤ إِلَى ٱلۡمَدِينَةِ فَلۡيَنظُرۡ أَيُّہَآ أَزۡكَىٰ طَعَامً۬ا فَلۡيَأۡتِڪُم بِرِزۡقٍ۬ مِّنۡهُ وَلۡيَتَلَطَّفۡ وَلَا يُشۡعِرَنَّ بِڪُمۡ أَحَدًا (١٩)
إِنَّہُمۡ إِن يَظۡهَرُواْ عَلَيۡكُمۡ يَرۡجُمُوكُمۡ أَوۡ يُعِيدُوڪُمۡ فِى مِلَّتِهِمۡ وَلَن تُفۡلِحُوٓاْ إِذًا أَبَدً۬ا (٢٠)
وَڪَذَٲلِكَ أَعۡثَرۡنَا عَلَيۡہِمۡ لِيَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقٌّ۬ وَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ لَا رَيۡبَ فِيهَآ إِذۡ يَتَنَـٰزَعُونَ بَيۡنَہُمۡ أَمۡرَهُمۡۖ فَقَالُواْ ٱبۡنُواْ عَلَيۡہِم بُنۡيَـٰنً۬اۖ رَّبُّهُمۡ أَعۡلَمُ بِهِمۡۚ قَالَ ٱلَّذِينَ غَلَبُواْ عَلَىٰٓ أَمۡرِهِمۡ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيۡہِم مَّسۡجِدً۬ا (٢١)
سَيَقُولُونَ ثَلَـٰثَةٌ۬ رَّابِعُهُمۡ كَلۡبُهُمۡ وَيَقُولُونَ خَمۡسَةٌ۬ سَادِسُہُمۡ كَلۡبُہُمۡ رَجۡمَۢا بِٱلۡغَيۡبِۖ وَيَقُولُونَ سَبۡعَةٌ۬ وَثَامِنُہُمۡ ڪَلۡبُہُمۡۚ قُل رَّبِّىٓ أَعۡلَمُ بِعِدَّتِہِم مَّا يَعۡلَمُهُمۡ إِلَّا قَلِيلٌ۬ۗ فَلَا تُمَارِ فِيہِمۡ إِلَّا مِرَآءً۬ ظَـٰهِرً۬ا وَلَاتَسۡتَفۡتِ فِيهِم مِّنۡهُمۡ أَحَدً۬ا (٢٢)
وَلَا تَقُولَنَّ لِشَاْىۡءٍ إِنِّى فَاعِلٌ۬ ذَٲلِكَ غَدًا (٢٣)
إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ وَٱذۡكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلۡ عَسَىٰٓ أَن يَهۡدِيَنِ رَبِّى لِأَقۡرَبَ مِنۡ هَـٰذَا رَشَدً۬ا (٢٤)
وَلَبِثُواْ فِى كَهۡفِهِمۡ ثَلَـٰثَ مِاْئَةٍ۬ سِنِينَ وَٱزۡدَادُواْ تِسۡعً۬ا (٢٥)
قُلِ ٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا لَبِثُواْۖ لَهُ ۥ غَيۡبُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ أَبۡصِرۡ بِهِۦ وَأَسۡمِعۡۚ مَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِىٍّ۬ وَلَا يُشۡرِكُ فِى حُكۡمِهِۦۤ أَحَدً۬ا (٢٦)
TAFSIRI
Aya Namba 22 na 25.
22. (Wengine) wanasema: “Walikuwa watu watatu wa nne wao ni mbwa wao., Na (wengine) wanasema, “Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao.” (Wanasema) kwa kuvurumiza (tu) kwa wasioyajuwa. Na (wengine) wanasema, “Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao.” Sema: “Mola wangu ndiye ajuaye sawasawa hisabu yao., Hakuna anayewajua (hakika yao) isipokuwa wachache tu. Basi usibishane (usishindane) juu yao ila kwa mabishano ya juu juu tu hivi (kwani hapana faida juu ya mabishano ya kuwa walikuwa wangapi). Wala usiulize khabari zao kwa yoyote yule. (M wenyezi Mungu ameshakutajia. Basi hivi alivyokutajia ndio ndivyo).
25.Na walikaa katika pango yao myaka mia tatu, na wakazidisha (myaka) tisa.
SHEREHE
Aya hizi zinahusu wachamungu ambao walikuwa wakimbizi wa Siasa ya Ukafiri katika Enzi Hizo. Kulikuwa na Mfalme Kafiri Katika Mamlaka hiyo na Watu hawa Wakaondoka mji huo kwa Siri na kukimbilia katika Pango. Ni Wachamungu walikuwa na Imani Kubwa sana Kama Mwenyeezi Mungu alivyowasifu katika Aya Hizi. Na Muujiza Mkubwa ukazuka. Mwenyeezi Mungu akawalaza usingizi mkali kwa muda wa miaka 309. Angalia Muujizahuu ambao siyo Mdogo. Miujiza mingine katika Sura Hii inathibitisha kwamba Kisa hikini cha ukweli. Kama nilivyoelezea katika Sehemu ntyinginezo za Website hii.
Kwanza Maneno Ya Kisa Hiki ni 309 Pia kama Miaka waliyolazwa.!!!!!
Pili Ukihesabu Kurasa za Msahafu kuanzia Pale palipotajwa miaka 309 mpaka mwisho wa Msahafu utapata Jumla ya Kurasa ni 309 Pia. Angalia Maajabu!!!!!.
Kisa hiki kimetajika Kwa Jumla ya Aya 18 na Sura Hii ambayo imetiwa Jina Hili la Al-Kahf ni ya 18 Pia. Je unaona Maajabu?!!!!!
Alhamdulilah Leo Nitapeleka Darubini katika Aya Mbili tu za Aya zilizopo hapa juu ili tuone Muujiza Mwingine wa Kushangaza. Yaani Miujiza ya kuruani Haina Mwisho. Allahu Akbar.
Ngojea nizinukulu zile Aya Mbili Nilizobadili rangi hapa Juu ili tuone Vizuri:
سَيَقُولُونَ ثَلَـٰثَةٌ۬ رَّابِعُهُمۡ كَلۡبُهُمۡ وَيَقُولُونَ خَمۡسَةٌ۬ سَادِسُہُمۡ كَلۡبُہُمۡ رَجۡمَۢا بِٱلۡغَيۡبِۖ وَيَقُولُونَ سَبۡعَةٌ۬ وَثَامِنُہُمۡ ڪَلۡبُہُمۡۚ قُل رَّبِّىٓ أَعۡلَمُ بِعِدَّتِہِم مَّا يَعۡلَمُهُمۡ إِلَّا قَلِيلٌ۬ۗ فَلَا تُمَارِ فِيہِمۡ إِلَّا مِرَآءً۬ ظَـٰهِرً۬ا وَلَاتَسۡتَفۡتِ فِيهِم مِّنۡهُمۡ أَحَدً۬ا (٢٢)
وَلَبِثُواْ فِى كَهۡفِهِمۡ ثَلَـٰثَ مِاْئَةٍ۬ سِنِينَ وَٱزۡدَادُواْ تِسۡعً۬ا (٢٥)
TAFSIRI
22. (Wengine) wanasema: “Walikuwa watu watatu wa nne wao ni mbwa wao., Na (wengine) wanasema, “Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao.” (Wanasema) kwa kuvurumiza (tu) kwa wasioyajuwa. Na (wengine) wanasema, “Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao.” Sema: “Mola wangu ndiye ajuaye sawasawa hisabu yao., Hakuna anayewajua (hakika yao) isipokuwa wachache tu. Basi usibishane (usishindane) juu yao ila kwa mabishano ya juu juu tu hivi (kwani hapana faida juu ya mabishano ya kuwa walikuwa wangapi). Wala usiulize khabari zao kwa yoyote yule. (M wenyezi Mungu ameshakutajia. Basi hivi alivyokutajia ndio ndivyo).
25. Na walikaa katika pango yao miaka mia tatu, na wakazidisha (myaka) tisa.
NAMBA ZA KUSHANGAZA
Muujiza ni kwamba Namba zilizotajika katika Aya hizi ukizipanga vizuri unapata Jina la Mwenyeezi Mungu Allah Akbar.
Usibabiske kwani Nitaambatanisha Video hapa Chini ieleweke na uone ya Maajabu.
Namba hizi ni Idadi ya Hao wachamungu na Mbwa wao. KIsa kiantuelezea kwamba Watu wanabuni buni idadi yao Na Mwenyeezi Mungu anatusimulia habari za mazungumzo hayo.
Namba Hizi kama nilizozitia Rangi katika Aya hizi ni
3, 4, 5, 6,7.8,3, na 9
Sasa Nitaambatanisha Video Namba 1 hapa chini uzione kwa macho yako kwa vizuri. Tafadhali Angalia Namba Hizi unapozipanga na Kuziunga unapata Jina La Mola. Kwa kweli Inashangaza. Ukiangalia VIzuri Utafahamu. KIla Namba Nimetia DOA Kwa mfano Namba 3 Nimetia Doa
. . .
Namba 4
. . . .
Namba 5
. . . . .
Kwa kiarabu Maandishi yanakuwa kuanzia Kulia na kwenda kushoto. Kwa kiingereza ni Kinyume Maandishi yanakuwa Kushoto kwenda Kulia na hivyo hivyo Lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo Namba pia za Kiarabu Pia zitakuwa Kuanzia Kulia na Kwenda Kushoto.
Kwa Mfano Namba 15 Kwa kiarabu Namba 1 itakuwa Kulia na Namba 5 itakuwa kushoto yaani kinyume na Kiswahili. Kwa hiyo Madoa Haya Yatakuwa kwa Kufuata nidhamu ya lugha ya Kiarabu Kama ilivyo Kuruani ilivyo yaani Siyo Tafsiri ya Lugha Nyingine bali Kwa Kiarabu.
Sasa Naishia Hapa. Angalia Video Hapa Chini. Ni Fupi sana karibu Dakika 5.
Ukiangalia Utafahamu Vizuri habari hii. Kwa Kweli Kuruani ina maajabu yasiyo na mwisho. Allahu Akbar.
Video-1
MAAJABU YA KURUANI HAYANA MWISHO. NAMBA TULIZOZIONA KATIKA AYA MBILI YA 22 NA 25 KATIKA SURA YA AL-KAHF ZINASHANGAZA SANA. TUKIZIGEUZA KATIKA MADOA NA KISHA KUZIPANGA NA KUZIUNGA PAMOJA TUNAPATA JINA LA MWENYEEZI MUNGU “ALLAH” KWA KWELI MUUJIZA SOYO MDOGO HATA KIDOGO.
2/MUUJIZA WA MZUNGUKO WA MWEZI NA JUA (LUNAR MOON CYCLE) NA AYA ZA KURUANI TUKUFU
Alhamdulilah Nilizungumzia Kuhusu Metonic Cycle katika Mlango wa “BLOGS ZA KURUANI” wa website hii nikaelezea kwa picha kwamba Metonic Cycle ni Uhusiano unaosababishwa na Mwezi Na Jua. Harakati za Mwezi katika kuizunguka Ardhi na wakati huo huo Mwezi na Ardhi kuzunguka Jua. Kila baada ya Miaka 19 Mwezi Na Jua zinakutana na kukaribiana tena katika Positions au sehemu zake za asili.
Kuruani imetaja majina mawili katika Aya 19 na Kila Aya inaambatanisha Jua na Mwezi.
الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ
“Jua na Mwezi”
Nimeorodhesha katika Mlango huo Aya zote 19 ambazo kila Aya inatumia ibara hii.
الشَّمْسَ وَ الْقَمَرَ
yaani “Jua na Mwezi”.
Ukifikiri utaona Maneno Haya Hayakupangika bure bure bali kimiujiza. Hizi ni Aya Pekee katika Kuruani yote. Huu Sio Muujiza Mdogo.
Alhamdulilah Leo Mwenyeezi Mungu akipenda Nitaelezea Muujiza Mwingine wa Kila Miaka 33 na pia Kila Miaka 11.
Kuhusu Miaka Tunasoma katika Elimu ya Astronomy kwamba Mwezi Unazunguka Ardhi kwa siku 354 na Ardhi linazunguka Jua kwa siku 365 kwa hiyo tofauti ni siku 11. Calendar ya Mwezi Kuzunguka Jua inajulikana kama Lunar Calendar na Calendar ya Ardhi Kuzunguka Jua inajulikana kama Solar Calendar.
Calendar zote mbili ni zake Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Kwa hiyo Baina Ya Calendar hizi Mbili kuna Tofauti ya Siku 11.
Ukijumlisha Tofauti hii ya siku 11. Katika Kila Miaka 33 inatimia Siku 363 (11 x 33=363) Na siku hizi 363 ni karibu Mwaka. Yaani Baada ya Miaka 33 Jua, Mwezi na Kila kitu kitarudi katika Sehemu (Position) zake ya Asili.
Na Tarehe zitajirakibisha na Kuanza tena. Yaani Tuaanza kuhesabu tofauti ya siku 11 na baada ya Mwaka ufuatao itakuwa 22 na baada ya Mwaka Ufuatao itakuwa 33 na hivyo hivyo mpaka Utakuwa mwaka tena na baada ya hapo kila kitu kitakuwa mahala pake pa asili na Hesabu Itaanza upya.
Ni sawa na Saa ya Mkono. Inaanza na 1 mpaka 12 na baada ya hapo inaanza 1 tena. Inazunguka hivyo 1 mpaka 12 na tena 1 mpaka 12. Nadhani imeeleweka. Na kwa hivyo Jua na Mwezi na kila kitu baada ya Muda huo wa miaka 33 kila Tofauti ya Masiku hujirekibisha na Kuanza tena Upya. Na Mwenyeezi Mungu anaelewa vizuri zaidi ikiwa sivyo. Allahu Aliym.
Na Kuhusu Smaku (Magnetic) ya Jua Pia inalizunguka Jua na hii Inajulikana kama “Solar Cycle” Yaani kila baada ya Miaka 11 Kunakuwa na mzunguko wa Smaku na Mzunguko huo unasababisha North Pole na South Pole ya Jua Kubadilika. North inakuwa South na South inakuwa Pole.
(The Sun’s magnetic field goes through a cycle, called the solar cycle. Every 11 years or so, the Sun’s magnetic field completely flips. This means that the Sun’s north and south poles switch places. Then it takes about another 11 years for the Sun’s north and south poles to flip back again).
Kwa kifupi:
1/Miaka 33 Ni Miaka ya Jua Na Ardhi Kujirekibisha Tofauti zake za Masiku
2/Masiku 11 ni Tofauti Ya Calendar ya Lunar (Calendar Ya Kiislamu) Na Solar (Calendar za Gregorian au za Kisasa)
3/Miaka 11 ni Mzunguko wa Smaku juu ya Jua na Kubadilika Kwa South na North Pole. au Kwa kiingereza. “Flip”
Sasa umefika wakati wa Kupeleka Darubini yetu katika Kuruani Tukufu Tuone Maajabu Yasiyo Na Mwisho na Pia Maajabu Makubwa. Allahu Akbar.
Sasa Umefika wakati wa Kupeleka Darubini yetu katika Aya Ya Kuruani tuone hizi namba tulizotaja hapa juu. Yaani namba 33, na 11
Aya Ifuatayo Moja tu Itatupa namba hizi mbili. Sasa tujiulize Swali Kwa vipi?
Jawabu linafuata hebu tufanye Utafiti. Tizama vizuri linalofuata. Alhamdulilah. Allahu Akbar. Fumbua macho katika Aya ifuatayo Sura Ya Al-Ambiyaa Namba 21 Aya namba 33
وَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّہَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلٌّ۬ فِى فَلَكٍ۬ يَسۡبَحُونَ (٣٣)
TAFSIRI
33.Na yeye ndiye aliyeumba usiku na mchana . na jua na mwezi; vyote vinaogelea katika duara (zao).
SHEREHE YA MAAJABU YA KURUANI
Kila Mtu ataona namba 33 ni namba ya Aya kwa hiyo mtasema naam ni Namba ya Aya. Kwa kweli mmepata. Ni Namba Ya Aya na Jawabu ni sahihi lakini kuna Namba 33 iliyofichika Hebu tuitafute.
Ukiangalia vizuri utaiona na pia Namba 11 imefichika.
Tuichunguze Aya tena kwa pamoja:
وَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّہَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلٌّ۬ فِى فَلَكٍ۬ يَسۡبَحُونَ (٣٣)
Angalia Vipande Nilivyotia Rangi
Kipande Chekundu cha Aya kinasema:
“Yeye Ndiye aliyeumba Mchana na Usiku na Jua Na Mwezi”
Ndugu Msomaji Jumla ya Herufi za Kipande hiki ni 33 pia!!!!!! na ndicho kinachotuhusu kwani Kinazungumzia Jua na Mwezi Na kama tulivyoona Kwamba Jua na Mwezi zinazunguka kwa muda wa miaka 33 na baada ya hapo Tarehe inajisawazisha. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Angalia Maajabu. Mara ya kwanza tumepata Namba Ya Aya na Sasa Tumepata Jumla ya Herufi ni 33. Je huoni Maajabu? Huoni Kukariri kariri huku siyo Bure bure tu.
Sasa Tuchunguze namba 11 Katika Aya Hii. Ngojea Niinukulu tena hapa chini.
وَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّہَارَ وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلٌّ۬ فِى فَلَكٍ۬ يَسۡبَحُونَ (٣٣)
Hebu tusogeze darubini tena katika Aya hii.
Je unaione namba 11?
Ngojea Niinukulu tena Aya Hii:
وَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلَّيۡلَ وَ ٱلنَّہَارَ وَ ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ كُلٌّ۬ فِى فَلَكٍ۬ يَسۡبَحُونَ (٣٣)
Tumesema Kuzunguka kwa Smaku ya Jua katika Jua Inachukua Miaka 11 na Pia Tofauti ya Siku 11 ni Mzunguko wa Mwezi katika Ardhi na Ardhi katika Jua.
Kwa hiyo Angalia kipande cha aya katika Aya Hii
ٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَۖ
Maneno Haya Mawili yana maana ya Jua Na Mwezi. Na Jumla Ya herufi zake ni 11 pia!!!!!
Kwa kweli Inashangaza sana. Allahu Akbar. Angalia Ukubwa wa Kuruani Ulivyo. Kwa kweli Inatisha na siyo Uwongo. Kuruani imejaa Ulimwengu au Malimwengu wote. Unajionea kwa Macho yako Mwenyewe Maajabu Yasiyo na Mwisho. Allahu Akbar.
Na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi ikiwa siyo hivyo. Lakini sisi binadamu tunashangaa sana na Maajabu Haya. Je unaonaje? Namuomba Mola Anisamehe iwapo sivyo. Kitu muhimu Tumefanya Jitihada kuinua Jina lake. Allahu Akbar.
Inaendelea kwani kuna Miujiza Mingine katika Mlango huu. Ukirudi tena utaikuta Mwenyeezi Mungu akipenda.
02/10/2022
Alhamdulilah Mwenyeezi Mungu Akipenda Siku ya Leo Nitaanza na Kuendelea Kuelezea Miujiza Mingineyo katika Mlango huu.
3/MUUJIZA WA HERUFI ZA MAAJABU KATIKA KURUANI (Muqaṭṭaʿāt, Arabic: حُرُوف مُقَطَّعَات ḥurūf muqaṭṭaʿāt, “disjoined letters” or “disconnected letters)
Herufi Tutakazozichunguza ni Tatu. Nun, Qaf na Swad. Na Tutakapoziunga Pamoja Tutapata Neno نَقُصُّ “NAQUSU” lenye maana ya “Tunakuhadithia” au “Tunakusimulia” Tuanze Utafiti katika Kuruani wa neno Hili نَقُصُّ “NAQUSU” na kisha Tuangalie Sura Ambazo zimetumia Mwanzoni mwake Herufi hizi Tatu. Kwanza Ningependelea kuelezea Herufi hizi kwamba Herufi za Muqataa zimetumika mwanzoni mwa Sura 29 kati ya Sura 114 za Kuruani Tukufu. Jumla ya Herufi ni 79 lakini tukiondoa zilizokariri zinabaki 14 tu. Ni Herufi ambazo ni Muujiza Mkubwa Hakuna ajuaye isipokuwa Mwenyeezi Mungu Tu peke yake. Lakini kuna Miujiza ambayo imepatika hivi karibuni kutokana na matumizi ya Herufi hizi. Katika Sehemu Hii tutachunguza Herufi Tatu ambazo zimetumika Mwanzoni mwa Sura Tatu kati ya hizo Sura 29.
Sasa Tuzitaje zile Sura Zilizotumia neno نَقُصُّ au “NAQUSU”
Sura Namba 7 Al-Arraf Aya Namba 101
تِلْكَ الْقُرَى نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنْبَائِهَا وَ لَقَدْ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا مِنْ قَبْلُ كَذَلِكَ يَطْبَعُ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِ الْكَافِرِينَ
Sura Namba 11 Hud Aya Namba 120
وَ كُلًّا نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنْبَاءِ الرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِ فُؤَادَكَ وَ جَاءَكَ فِي هَذِهِ الْحَقُّ وَ مَوْعِظَةٌ وَ ذِكْرَى لِلْمُؤْمِنِينَ
Sura Namba 12 Yusuf Aya Namba 12
نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَذَا الْقُرْآنَ وَ إِنْ كُنْتَ مِنْ قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ
Sura Namba 18 Al-Kahf Aya Namba 13
نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُمْ بِالْحَقِّ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَ زِدْنَاهُمْ هُدًى
Sura Namba 20 Twaha Aya Namba 99
كَذَلِكَ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنْبَاءِ مَا قَدْ سَبَقَ وَ قَدْ آتَيْنَاكَ مِنْ لَدُنَّا ذِكْرًا
Neno نَقُصُّ Lina maana ya “Kuhadithia” au “Kukuelezea Kisa” Neno hili نَقُصُّ kwa matamshi ni “NAQUSU” Katika Kuruani Neno Hili limetumika katika Aya Nilizonukulu hapa juu yaani Hizi tu na hakuna Nyingineo. Yaani neno hili limetumika mara 5 Tu katika Kuruani Tukufu.
Mara Ya Kwanza Kutumika ni katika Sura Namba 7 Al-Arraf Aya Namba 101 katika Msahafu ni Kurasa namba 163
Na Mara Ya Mwisho Kutajika ni katika Sura Namba 20 Twaha Aya Namba 99 katika Msahafu ni Kurasa namba 319
Neno Hili نَقُصُّ limetumia herufi Tatu NUN, QAF na SWAD na ambazo ni katika Herufi za Maajabu.
Kuna Sura Tatu Katika Kuruani Ambazo zimenziwa na Herufi hizi Tatu nazo ni Sura ZIfuatazo:
Sura Ya Qalam Namba 68 Imeanziwa na Herufi ya Nun Sura Ya QAF Namba 50 Imenziwa na Herufi QAF Sura Ya Swad Namba 38 Imeanziwa na Herufi SWAD
Sasa Ttuendelee na Utafiti. Hebu tupeleke Darubini katika Kuruani.
Tuhesabu Namba za Sura Hizi Tatu 68 + 50 + 38=156
Tumepata 156 Hebu Tuchunguze Zile Kurasa Tulizozipata hapo juu 319 na 163
Hebu tutoe namba 163 (Namba Ya Ukurasa wa mara ya Mwanzo kutumika neno نَقُصُّ) kutoka katika Namba 319 (Mara ya Mwisho kutumika neno نَقُصُّ)
(319-163=156)
Kwa kweli inashangaza hebu angalia Maajabu yasiyo na Mwisho.
ukijumlisha Namba za Sura Tatu (Qalam Iliyoanziwa na herufi NUN + Qaf + Swad) tumepata namba 156 Tulipotoa Aya Ya Mwisho kutoka katika Aya Ya Kwanza ambazo zimetumia neno نَقُصُّ NAQUSU tumepata namba 156 Mbona Namba hizi zinalingana.
Huu ndiyo Muujiza. Maajabu Makubwa. Huu siyo Uchawi bali Muujiza. hii ni Lugha Ya Muumbaji. Ni Lugha ya Mwenyeezi Mungu aliyetukuka sana tena sana. Lugha ya Kiajabu Tupu. Allahu Akbar.
Kwa kweli tumeshindwa. Hatuwezi chochote mbele ya Maandishi yaliyopangika Kiajabu. Kuna siri Kubwa ambazo hatuzijui. Labda inawahusu Majini au Viumbe vya Baadaye au Sisi. Ukifanya hiki unapata hiki, Ukifanya hiki unapata hiki. Ajabu Kubwa. Hebu fikiri. Tumeangalia Herufi na kisha herufi katika Neno na mara Jawabu Limefanana. Allahu Akbar.
MUUJIZA WA KIPANDE CHA AYA ان الدين عند الله الاسلم KATIKA KURUANI RUKUFU
Tutafanya Utafiti wa Kipande cha Aya ان الدين عند الله الاسلم katika Sura Zifuatazo:
Sura Ya Al-Imran Namba 3 Aya Namba 19
ان الدين عند الله الاسلم و ما اختلف الذين اوتوا الكتب الا من بعد ما جاهم العلم بغيا بينهم و من يكفر بايت الله فان الله سريع الحساب
TAFSIRI
19.Bila shaka dini (ya haki) mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manasara) hawakukhitalitiana ila baada ya kuwajia ilimu. (Walikhitalifiana) kwa sababu ya uhasidi uliokuwa baina yao. Na anayezikataa Aya za Mwenyezi Mung’u (mara moja Mwenyezi Mungu atamuadhibu huko Akhera), na Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
Sura Namba 3 Al-Imran Aya Namba 85
وَمَن يَبۡتَغِ غَيۡرَ ٱلۡإِسۡلَـٰمِ دِينً۬ا فَلَن يُقۡبَلَ مِنۡهُ وَهُوَ فِى ٱلۡأَخِرَةِ مِنَ ٱلۡخَـٰسِرِينَ (٨٥)
TAFSIRI
85.Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa).
Sura Namba 5 Al-Maidah Aya Namba 3
حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةُ وَٱلدَّمُ وَلَحۡمُ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦ وَٱلۡمُنۡخَنِقَةُ وَٱلۡمَوۡقُوذَةُ وَٱلۡمُتَرَدِّيَةُ وَٱلنَّطِيحَةُ وَمَآ أَكَلَ ٱلسَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيۡتُمۡ وَمَا ذُبِحَ عَلَى ٱلنُّصُبِ وَأَن تَسۡتَقۡسِمُواْ بِٱلۡأَزۡلَـٰمِۚ ذَٲلِكُمۡ فِسۡقٌۗ ٱلۡيَوۡمَ يَٮِٕسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن دِينِكُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِۚ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِى وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَـٰمَ دِينً۬اۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِى مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٍ۬ لِّإِثۡمٍ۬ۙ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬ (٣)
TAFSIRI
3. Mmeharimishiwa nyamafu na damu na nyama ya nguruwe, na kinyama kilichochinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kilichokufa kwa kusongeka koo, na kilichokufa kwa kupigwa, na kilichokufa kwa kuanguka, na kilichokufa kwa kupigwa pembe (na mwengine), na alichokila mnyama (kikafa), ila mkiwahi kukichinja (kabla hakijafa). Na (pia mmeharimishiwa) kilichochinjwa panapofanyiwa ibada isiyokuwa ya Mungu (kama mizimuni). Na ni (haramu kwenu) kutaka kujua siri kwa kuagua kwa mabao (na yaliyo kama hayo). Hayo yote ni maasiya. Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu. Na mwenye kushurutishwa na njaa, pasipo kuelekea kwenye dbambi, (akala hivi vilivyoharimishwa, basi hapana kitu); hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha (na) Mwingi wa rehema.
Sura Namba 61 As-Saf Aya Namba 7
وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُوَ يُدۡعَىٰٓ إِلَى ٱلۡإِسۡلَـٰمِۚ وَٱللَّهُ لَا يَہۡدِى ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٧)
TAFSIRI
7. Na ni nani dhalimu mkubwa wa nafsi yake kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uwongo, na hali anaitwa katika Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhalimu (wa nafsi zao).
SHEREHE
Maana Ya Kipande cha Aya Katika Aya Ya Kwanza Hapa Juu ان الدين عند الله الاسلم Imekariri katika Aya Tatu nyinginezo hapa Juu. Yaani Ukichunguza Utaona Maana Iliyokariri ni “Uislamu Ndiyo Dini Inayokubalika Mbele ya Mwenyeezi Mungu.
Nimetia Rangi Nyingine Hapa Juu Vile vipande vyenye Kuleta maana hii katika Aya zote Nne ili ieleweke vizuri. Ijapokuwa Maana za Aya ni Tofauti lakini kila Aya Imeelezea Umuhimu wa Dini ya Kiislamu.
Sasa Tufanye Utafiti WA Aya Ya Kwanza Hapa Juu ambayo maana yake ipo katika Aya Nyinginezo Tatu. Ukikigeuza Kipande hiki ان الدين عند الله الاسلم katika Hesabu au Thamani ya Namba.
(Warabu na mataifa mengineyo hapo zamani walikuwa wakitumia Herufi kuwakilisha Namba. Kwa hiyo walitumia Alif Kuwakilisha Namba 1 na Baa kuwakilisha Namba 2 na hivyo hivyo namba zote. Nimekwisha zungumzia habari hii kwa urefu katika milango ya Website hii)
tutapata namba 498 Hebu Tupange namba za Sura,
Aya Na Herufi za Aya Hizi Nne:
Sura Namba 3 Aya Namba 19 Jumla ya Herufi Za Aya Hii ni 105
Sura Namba 3 Aya Namba 51 Jumla Ya Herufi Za Aya Hii ni 51
Sura Namba 5 Aya Namba 3 Jumla Ya Herufi Za Aya Hii ni 276
Sura Namba 61 Aya Namba 66 Jumla Ya Herufi Za Aya Hii ni 66
Tumesema kwamba maana ya kipande ان الدين عند الله الاسلم katika Sura Namba 3 Aya Namba 19 imakariri katika Aya Tatu nyinginezo hapa Juu.
Na Tumesema kwamba Thamani ya Herufi ya kipande hiki ni 498
Sasa hebu tujumlishe Herufi za Aya hizi Nne tuone Jawabu. 105 + 51 + 276 + 66=498
Haya kweli ni maajabu. Thamani Ya Kipande ان الدين عند الله الاسلم na ambacho kina maana katika Aya zilizotajwa hapa juu yaani namba 498 ambayo ni sawa na Jumla ya herufi ya Aya Hizi Nne.
Hebu Nipange tena vizuri ili tuone:
Thamani Ya Kipande ان الدين عند الله الاسلم hiki ni 498
Na Jumla Ya Herufi za Aya Hii pia Ni 498
Haya Kweli Maajabu. je ni Uashirio kwamba Maana Ya Kipande Cha Aya Ya Kwanza ni sawa na Maana Iliyopo katika Aya Nyinginezo?
Labada Hivyo kwani Hesabu Ndizo zinavyotuambia.
Kwa kweli Muujiza Wa Kuruani Hauna Mwisho. Allahu Akbar.
Na Ajabu Nyingine ni kwamba Ukihesabu Namba za Aya zake Tunapata Idadi nyingine ya kushangaza: Hebu Tuone: 19 + 85 + 3 + 7=114
Angalia Maajabu Tukijumlisha Namba za Aya tunapata Idadi ya Sura za Kuruani ambazo ni 114!!!!
Yaani Kipande hiki cha Aya ان الدين عند الله الاسلم ambacho kinasema kwamba “Dini Inayokubaliwa Mbele ya Mwenyeezi Mungu” Kina Miujiza Isiyo na Mwisho. Tumepata hapa Maajabu mawili. Kwanza Kukariri kwa Namba 489 na Pili Idadi ya Sura za Kuruani 114. Kwa kweli Kuruani imekusanya Ulimwengu. Haya siyo Madogo. Allahu Akbar.
UMRI WA MTUME MOHAMAD, MUDA WA UJUMBE WA MWENYEEZI MUNGU (UISLAMU) NA KANDA ZA KIZAZI (CHROMOSOMES) NI BAADHI YA MIUJIZA MIKUBWA KATIKA KURUANI TUKUFU
Jambo la kushangaza ni kwamba Umri wa Mtume Mohamad ﷺ ambao ni miaka 63, Na Muda wa Ujumbe wake ambao ni Miaka 23 na Chromosomes 23 ambazo ni kanda za Uzazi wa Binaadamu zote zimeashiriwa katika Kuruani tukufu kiajabu sana. Na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi iwapo tunakosea.
Ajabu ya Kwanza ni Jumla ya Kanda hizi za Uzazi ni 23 na Namba hii inalingana na Muda wa Ujumbe wa Mtume Mohamad ﷺ katika Dunia. Kanda za Uzazi wa Binaadamu 23 kutoka kwa Baba na 23 Kutoka Kwa mama jumla ni 46
Kila Mwaka Mtume Mohamad ﷺ alifundishwa Kuruani Na Jibril mara Moja (Mwezi wa Ramadhan) na Katika Mwaka wa Mwisho wa Maisha Yake Yaani Mwaka wa Mwisho wa Ujumbe wake yaani ule mwaka wa 23 alisomeshwa Kuruani Mara Mbili Katika Mwezi wa Ramadhan (Revision of Quran was 2 Times)
Na katika Elimu ya Kizazi (Embryology) Mbegu ya Baba na mama ni sawa na 23 X 2 pia!!!!
Angalia Maajabu. Je Huu siyo mpangilio wa kiajabu? Je huoni Namba zinavyozungumza? Allahu Akbar.
Miaka 23 ni Miaka Ya Ujumbe aliolingania Dini Mtume Mohamad. ﷺ
Sasa tuendelee na Utafiti huu katika Kuruani Tukufu tuone Maajabu Mengineyo.
Tuchukuwe Majina Ya Sura Zote Za kuruani yaani Majina 114. Kwa mfano Jina La Kwanza ni “Al-Fatiha” La pili ni Al-Bakarah na hivyo hivyo mpaka majina yote ya Sura 114 ya Msahafu.
KIsha Tutafute Thamani au Namba za Herufi Hizi kufuatana na Mpangilio wa Alphabet za Lugha Ya Kiarabu. (Tafadhali usichukue zile Namba walizotumia Waarabu na Mataifa mengineyo hapo zamani yaani kama nilivyosema katika sehemu nyinginezo kwamba Hapo zamani Waarabu na Mataifa mengineyo walitumia Herufi kuwakilisha Namba. Utafiti huu hutachukua Namba hizo bali namba za Mpangilio wa Herufi za Lugha ya Kiarabu. Kwa mfano katika Herufi zote 28 Alif itakuwa namba 1 na Baa 2 hivyo hivyo mpaka herufi zote 28 na kwa hiyo Herufi ya Mwisho itakuwa ya 28).
Tukifanya hivyo na kisha Tuzichunguze namba zote na kujaalia au kuzipanga Namba Kubwa iwe ya Kwanza na Hivyo hivyo itakayofuatia ndogo yake na ufanye hivyo mpaka namba ya mwisho ambayo itakuwa ndogo kabisa. Ukifanya Hivyo utapata Maajabu mengineyo ya Kushangaza. Yaani Ukiangalia Namba Ya Majina Ya Sura zote 114 utaona zile Namba 3 kubwa za kwanza zinashangaza sana.
Namba Ya Kwanza Itakuwa 176
Namba Ya Pili itakuwa 167
Na Namba ya Tatu Itakuwa 157
Sasa Tuchunguze Majina Ya Sura Ya Namba Hizi:
Namba 176 Inawakilisha Sura Namba 23
Namba 167 Inawakislisha Sura Namba 63
Namba 157 Inawakilisha Sura namba 83
Angalia Maajabu Tuliyoyapata katika Majina Ya Sura
Yaani Hizi Ndizo Sura Tatu katika Sura ambazo Thamani Ya Herufi za Majina Yake ni za Juu kuliko Zote nyinginezo.
Namba 23 hapa Ni Muda wa Ujumbe wa Mtume Mohamad.ﷺ
Namba 63 Ni Umri alioishi Mtume Mohamad
Na Namba 83 Ni Namba ya 23 katika Namba zinazojulikana kama Prime Numbers.
Na Namba hii 23 ya Tatu inaashiria Kama tulivyosema hapa Juu. Muda wa Ujumbe wake Mtume Mohamad.ﷺ
Na Kwa vile kuna namba 23 mara 2 basi huenda ni ile miaka ya Kisomo cha Kuruani alichofundishwa na Malaika Jibril katika Mwaka wa Mwisho wa Ujumbe wake yaani mwaka wa 23 alijiwa na JIbril mara Mbili.
Katika Bukhari kuna Hadithi Ya Mtume inayotokana na Fatima Inasema:
عَنْ فاطمة عَنْ النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ أَسَرَّ إِلَيَّ إِنَّ جِبْرِيلَ كَانَ يُعَارِضُنِي الْقُرْآنَ كُلَّ سَنَةٍ مَرَّةً وَإِنَّهُ عَارَضَنِي الْعَامَ مَرَّتَيْنِ وَلَا أُرَاهُ إِلَّا حَضَرَ أَجَلِي وَإِنَّكِ أَوَّلُ أَهْلِ بَيْتِي لَحَاقًا بِي فَبَكَيْتُ فَقَالَ أَمَا تَرْضَيْنَ أَنْ تَكُونِي سَيِّدَةَ نِسَاءِ أَهْلِ الْجَنَّةِ أَوْ نِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ فَضَحِكْتُ لِذَلِكَ 3376 صحيح البخاري كتاب المناقب باب علامات النبوة في الإسلام
TAFSIRI
Imepokewa kutoka kwa Fatimah: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: “Jibril alikuwa akinijia ili Kunifundisha (Revision au Marejeo ya Kisomo) Quran mara moja kila mwaka na Mwaka huu alinifundisha (Revision au Marejeo ya Kisomo)Mara Mbili . Sidhani kama ina maana yoyote (Sielewi Undani wake) bali huenda muda wangu (Wa Maisha na Ujumbe) utafikia mwisho. Hakika wewe utakuwa wa kwanza kukutana nami katika watu wa nyumba yangu. Kwa hiyo nililia na Mtume akasema: “Je, hufurahii kuwa kiongozi wa wanawake wa Peponi au Waumini wanawake? Kwa hiyo nilicheka kwa hilo.
English Translation
Fatimah reported: The Prophet, peace and blessings be upon him, said, “Gabriel would come to me to revise the Quran once every year. This year he revised with me twice. I do not think it means anything but that my term will come to an end. Verily, you will be the first of the people of my house to meet me.” So I wept and the Prophet said, “Are you not pleased with be the master of the women of Paradise or the believing women?” So I laughed at that.
Source: Ṣaḥīḥ al-Bukhārī 3376 Grade: Sahih (authentic) according to Al-Bukhari
Na Huenda Pia ni Kanda za Uzazi wa Binaadamu (Chromosoms) 23 za baba na 23 za mama na Jumla ni 46.
Au 23 ya mwanzo ni Muda wa Ujumbe na 23 ya pili ni Chromosomes za Binaadamu.
Kwa kweli Huu siyo Muujza mdogo. Hakuna Dogo hapa kwani miashirio Mingi kama hii siyo bure bure. Kuruani haina Mchezo au Upuuzi. Hizi ni Alama za kuthibitisha Ujumbe aliokuja nao Mtume Mohamad.ﷺ Hata siyo mambo ya Utani. Ni Mambo ya Kutisha sana. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Uhusiano Baina Ya Ujumbe Huu na
Chromosomes za Binaadamu yaani Kanda za Uzazi unaonyesha Ujumbe huu ni wa Binaadamu wote Duniani kwani KIla Binaadamu ana Chromosomes hizi 23. Je unaona Namba zinavyozungumza? Na pia Namba tulizopata katika Majina Ya Sura Za Kuruani pia Inaonyesha uhusiano wake na Kanda za Uzazi (Chromosomes) pia. Kwa hiyo Ujumbe Huu ni Dunia Nzima. Kuruani ni Mafundisho kwa kila Mtu Duniani. Allahu Akbar.