UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MIUJIZA MBALIMBALI
14/10/2022
Alhamdulilah. Leo ni Siku kubwa na pia ni Siku nzuri kuliko Siku zote za Wiki. Ni Siku ya Ijumaa Allahu Akbar. Kuna Hadithi Mbalimbali za Mtume ﷺ ambazo zinaelezea utukufu wa Siku ya Ijumaa. Hapa nitataja hadithi Moja tu ambayo imekusanywa katika Sahih Ya Muslim.
وَحَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا الْمُغِيرَةُ، – يَعْنِي الْحِزَامِيَّ – عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنِ الأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ “ خَيْرُ يَوْمٍ طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ يَوْمُ الْجُمُعَةِ فِيهِ خُلِقَ آدَمُ وَفِيهِ أُدْخِلَ الْجَنَّةَ وَفِيهِ أُخْرِجَ مِنْهَا وَلاَ تَقُومُ السَّاعَةُ إِلاَّ فِي يَوْمِ الْجُمُعَةِ ” .
SHEREHE
Abu Huraira anasimulia kwamba Mtume ﷺ alisema “Siku iliyo bora ni Siku ya Ijumaa kwani ni Siku hiyo ambayo Nabii Adam aliumbwa, Kuingizwa peponi, Kutolewa Peponi na Hakitakuwa Kiyama isipikuwa ni Siku Ya Ijumaa”
TRANSLATION
Abu Huraira reported the Messenger of Allah (ﷺ) as saying: The best day on which the sun has risen is Friday; on it Adam was created. on it he was made to enter Paradise, on it he was expelled from it. And the last hour will take place on no day other than Friday.
MAAJABU MAKUBWA
AJABU YA KWANZA
Na Katika Siku Kubwa kama hii nimeona bora niwaletee baadhi ya Miujiza niliyosoma kutoka kwa Wanavyuoni mbalimbali. na nitafanya hivyo kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu Mtukufu kwani Sisi Binaadamu ni wapungufu na bila ya Uwezo wa Mwenyeezi Mungu haitawezekana.
Ninaanza na “BIsmillah Arahmani Arahim”
Kuna siku nilishangaa sana kusoma Utafiti wa Vijana Wachamungu ambao Unashangaza.
Utafiti wa kwanza unahusu Sura Namba 21 Aya Namba 30
سُوۡرَةُ الاٴنبیَاء Sura Ya Al-Ambiya
أَوَلَمۡ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ ڪَانَتَا رَتۡقً۬ا فَفَتَقۡنَـٰهُمَاۖ وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَىۡءٍ حَىٍّۖ أَفَلَا يُؤۡمِنُونَ (٣٠)
Nilikwisha zungumzia Aya Hii katika sehemu nyingine ya Website hii lakini kipande ڪَانَتَا رَتۡقً۬ا فَفَتَقۡنَـٰهُمَاۖ hiki kina Mengineyo makubwa ambayo sikuyajua hapo mwanzo.
Aya Hii inasema kwamba Mbingu na Ardhi zilikuwa Moja au kwa lugha nyingine zilikuwa kitu kimoja zimeungana na kugandana na kisha Mwenyeezi Mungu anaendelea kusema kwamba akaleta Mfunuo au Mpasuo au Mchanuo kwa kifupi akasababisha kupasuka, kusambaa na ikafuatia kuumba kila kitu. Na anatuambia kwamba katika kuumba akajaalia kila kitu kutokana na Maji kuwa Hai na Mwishoni mwa Aya anasema “Je Hawaamini” yaani Je sisi Hatuamini baada ya yote haya.
Jambo jipya ni kipande hiki ڪَانَتَا رَتۡقً۬ا فَفَتَقۡنَـٰهُمَاۖ chenye maana ya Mbingu na Ardhi zilikuwa kitu kimoja na kisha akavitenganisha kwa kupasuka au kusambaa kwa njia na hekima azijuayo yeye mwenyewe. Kipande hiki ukigeuza Herufi zake katika Namba Zilizotumiwa na Waarabu hapo zamani katika kuwakilisha Herufi na kisha ukazijumlisha kama nilivyofanya hapa chini
ك 20 + ا 1 + ن 50 + ت 400 + ا 1 + ر 200 + ت 400 + ق 100 + ا 1 + ف 80 + ف 80 = ت 400 + ق 100 +ن 50 +ه 5 م 40 ا1
Total 1929
utashangaa kuona kwamba Namba tutakayoipata ni 1929 na kwa kweli ndiyo Mwaka ambao Ushahidi wa Kithibitisho wa Nadharia kwamba Mpasuko wa Mbingu na Ardhi ni wa ukweli ulifanyika. Ni siku ambayo Mwanasayansi Maarufu kwa kutumia Darubini kwa jina la Hubble aligundua kwamba Nyota na Kila kitu angani zipo katika Kutengana na hii ilithibitisha kwamba Nguvu za Mpasuko wa Mwanzo bado unaendelea kusambaza Kila kitu angani na hii inathibitisha kwamba Hapo mwanzo kila kitu kilikuwa Kimoja na kisha kukatokea Mpasuko. Habari hii haikuwa ikiaminika kwani Wataalamu Wakubwa Duniani walikuwa hawaamini Mtanuko wa Mbingu. Waliamini kwamba Kila kitu kipo STATIC (Kimetulia) na Hawakuamini kwamba kila kitu ni DYNAMIC (Harakati) na kwa hiyo Mwaka huu wa 1929 ulikuwa mwaka Mkubwa sana. Ni mwaka ambao Experiment au Tajruba ilifanyika na kuthibitisha Asili ya Maumbile. Habari hii siyo ndogo ni Sayansi ambayo bado inawatatanisha Wataalamu Duniani Mpaka leo. Kwa hiyo huu ni Muujiza mkubwa sana katika Kuruani ambayo inatuelezea Mpasuko huu na pia Mwaka ambao Kithibitisho kitatokea.
Yaani Kuruani Imetabiri mpaka Mwaka. Je huoni Maajabu. Uislamu ulikuja katika karne ya 6 na Ugunduzi Karne ya 20 yaani mwaka 1929. Kwa kweli Muujiza Siyo mdogo kwa mtu atakayetaka Kufikiri. Yaani Mwenyeezi Mungu anakua yote yaliyopita na yatakayokuja na ameweka habari hizi katika Kuruani kwa njia ya Namba. Allahu Akbar.
Nadharia ya Mpasuko wa Mbingu na Ardhi ilianzishwa mwaka 1927 lakini Kithibitisho chake kilikuwa Mwaka 1929 na Mtaalamu Anayejulikana kama Edwin Hubble na baadaye Darubini aliyotumia Mtaalamu huyu ilitiwa Jina Lake na kuitwa HUBBLE..
Hapa chini ninawaletea habari hizi kwa Lugha ya Kiingereza. Nimebadili rangi katika Ile habari ya Utafiti wetu wa leo.
Georges LeMaitre (1894-1966) showed that religion and science — or at least physics — did not have to be incompatible. LeMaitre, born in Belgium, was a monsignor in the Catholic church. He was fascinated by physics and studied Einstein’s laws of gravitation, published in 1915. He deduced that if Einstein’s theory were true (and there had been good evidence for it since 1919), it meant the universe must be expanding. In 1927, the year he got his PhD from MIT, LeMaitre proposed this theory, in which he stated that the expanding universe was the same in all directions — the same laws applied, and its composition was the same — but it was not static. He had no data to prove this, so many scientists ignored it. (Another scientist, Soviet Aleksandr Friedmann, had come to the same conclusion independently, a few years earlier.) Even Einstein was reluctant to endorse this extension of his theory of general relativity. In 1929 at the Mt. Wilson Observatory in California, Edwin Hubble discovered that galaxies were moving away at high speeds. He was, like most people, unaware of LeMaitre’s 1927 theory. But LeMaitre used Hubble’s dramatic discovery as evidence for his theory. It was easy. If you imagined the galaxies rushing away from us as a movie, just run the movie backwards. After a certain time, all those galaxies will rush together. LeMaitre put forth the idea that there was once a primordial atom which had contained all the matter in the universe.
AJABU YA PILI
kwa kweli kila Muujiza katika Kuruani unashangaza. Kuna Miujiza Mingine inabidi Utafiti wa hali ya Juu. Inabidi Kutumia Vifaa Mbalimbali vya utafiti. Na hii inaonyesha Kwamba Haya siyo maneno ya Mtume peke yake bali ni Ya Muumba aliyeumba kila kitu. Allahu Akbar.
Sasa tufanye uchambuzi wa Aya Ya Kwanza katika Sura Ya “A-Qalam” Utafiti huu unaonyesha Maajabu ya Mpangilio wa Herufi za Kuruani. Hebu fikiri Muujiza mpaka katika Herufi. Sasa tuchunguze Herufi Ya “NUN” katika Sura Hii namba 68 Aya Ya Kwanza.
سُوۡرَةُ القَلَم
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ (١)
TAFSIRI
(Naapa Kwa Herufi ya )NUN. Na Kalamu yenye Kuandika.
SHEREHE
Mwenyeezi Mungu anaapia Herufi hii na Pia Kalamu ambayo kazi yake ni kuandika. Kwa hiyo kila kinachotusaidia katika Kuandika asili yake ni Kalamu na hata Computer pia msingi wake ni Maandishi.
Ukichunguza Aya zote zilizotumia Herufi Hii ya NUN نٓۚ kuanzia Aya ifuatayo mpaka Mwisho wa Kuruani. Yaani Kuanzia Aya Namba 2 mpaka mwisho wa Kuruani utakuta Jumla Aya ambazo zimetumia Herufi hii ni 681 sasa angalia maajabu. Namba hii siyo ya kawaida kwani inaashiria Herufi ya NUN ambayo ipo katika Aya Namba Moja ya Sura Ya Al-Qalam. Namba Ya Sura na Aya ni 68 Aya namba 1 au 68:1 hebu angalia maajabu. Tulipofanya utafiti wa herufi hii tukapata Jumla za Aya zilizotumia herufi hii ni 681 je huoni maajabu? Allahu Akbar. Angalia Muujiza hata katika Herufi. Utafiti Huu huwezi kuufanya kirahisi bila ya Programs . Na hii inaonyesha kwamba Kuruani siyo maneno ya kibinaadamu kwani katika Enzi za Mtume ﷺ kulikuwa hakuna Ufundi wa utafiti kama nyakati hizi za kisasa. kwani haiwezekani Mtume ﷺ ajiandikie hii kuruani na kisha apange herufi mpangilio kama huu ili aonyeshe watu. mwenye Kufikiri hivyo basi ni Mjinga au Mwongo hakuna lingine.
AJABU YA TATU
Hesabu zinazungumza. Hebu tufanye hesabu na kisha tujadili maana ya Baadhi ya Aya za Kuruani.
Mwaka wa Ardhi kuzunguka Jua kwa siku 365 unajulikana kama SOLAR YEAR
Mwaka wa Mwezi Kuzunguka Ardhi kwa siku 354 unajulikana kama “LUNAR YEAR” na huu ndio mwaka wa Kiislamu.
Hebu tugawe namba hizi Mbili
365/354=1.03
Sasa tuchunguze Idadi ya Miaka ya watu waliolazwa katika Pango. (Ashaab Alkahf). Sura Ya Al-Kahf.
Mwenyeezi Mungu alisema walilazwa kwa muda wa miaka 300 na wakazidisha miaka 9 yaani Miaka 309 Kauli hii isitubabaishe kwani Miaka waliyolazwa ya Solar Year ni 300 na Miaka hii ni sawa na ya Lunar Year (Miaka ya Kiislamu) ambayo ni 309. Kwa hiyo Sherehe itakuwa
“Watu hawa walilazwa kwa muda wa miaka 300 lakini Waislamu katika hesabu zao inabidi wazidishe Miaka 9 kwani wanatumia Mzunguko wa Mwezi katika Ardhi.. Kwa lugha Rahisi unaweza kusema kwamba Walilazwa kwa Muda wa Ardhi Kuzunguka Jua (Miaka 300) na miaka hii ni sawa na Mwezi Kuzunguka Ardhi (Miaka 309)
Na ili kuthibitisha Vizuri kama kauli hii ni sahihi hebu tugawe Miaka hii.
309/300=1.03
Je unona namba Hii ni sawa na Namba tuliyopata hapa juu ya Mgawanyo wa miaka ya Solar na Lunar
Sasa Tuchunguze Maana na Uhusiano baina ya maneno mawili عام na سنة haya maneno mawili yametumika katika Kuruani kwa maana mbili. عام ni Miaka ya Neema na سنة kwa maana ya Miaka ya Shida.(Nimezungumzia Habari Hizi katika Website Hii na Nimechambua Baadhi ya Aya) Lakini katika Hesabu nitakazofanya hapa chini inaonyesha pia kwamba neno عام na سنة Ukigeuza Herufi zake katika Namba walizokuwa wakitumia Waarabu hapo zamani utapata Neno عام Jumla ya Herufi zake ni 111 na neno سنة Jumla ya Herufi zake ni 115
عام=
ع 70 + ا 1 + م 40= 111
سنة=
س 60 + ن 50 + ة 5=115
Hebu tuchunguze kihesabu kwa kugawanya kama tulivyofanya hapa juu.
115/111=1.03
Lakini Huu ni utafiti wa Kihesabu wakati mwingine unababaisha. Namba zinafanana lakini tumeona katika Kuruani Maana ya Maneno mawili. Yaani neno “AAM” maana ya Miaka ya Neema na Neno “SANA” Lina maana Ya Miaka Ya Shida.
Katika Utafiti Huu wa leo Tunapata Pia kwamba neno “AAM” linaleta maana ya Miaka ya Lunar na Neno “SANA” Lina maana Ya Miaka Ya Solar kwani Ratio ni sawa na Mgawanyo tuliofanya hapa juu yaani 1.03
Kwa hiyo Maneno haya mawili huenda yanabadilika maana ya matumizi yake kufuatana na Matumizi yake. Yaani kuna wakati huweza kutumika kwa maana ya Neema na Shida na wakati mwingine Solar au Lunar Year. Na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi iwapo tumepata au tumekosea. Allahu Akbar.
AJABU YA NNE
Kwa kweli Kuruani ni Muujiza Usio na Mwisho. Na Mtume Mohamad ﷺ ametimiza amri ya Mwenyeezi mungu kama ipasavyo. Ujumbe aliouleta haukubadilishwa hata kidogo. Huu sio muujiza mdogo. Herufi, Maneno, Aya, Sura, Majina Ya Sura Na Mpangilio wake Yote Ni Muujiza Mkubwa ambao bado mengi hatuyajui. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Kwa kweli wakati umefika tuamke na tusilale usingizi kwani inatisha na ni hatari sana kwani ulimwengu siyo wetu. Miaka inapita haraka, Nyumba zetu ni Makaburi na yanatusubiri na wadudu humo Makaburini wana Njaa na wanatusubiri kwa hamu sana watutafune. Kwa kweli haya ninayosema kwanza najiambia mwenewe na kisha kila atakayepata bahati kusoma nasiha hizi. Allahu Akbar.
Sasa tusome Katika Muujiza Huu wa nne maneno mawili tu na tuone maajabu mengine.
Neno الإيمان “IMANI” na neno الكفر “KUFURU”
Haya Maneno mawili yametumika katika Kuruani Katika Aya na Mifumo mbalimbali lakini maana yake ni ile ile.
Imani kinyume chake ni Kutokuwa na imani na Ndiyo Kufuru. Na Kufuru kinyume chake ni Imani na Imani maana yake Kuwa na Imani. Haya maneno mawili yanapingana. Neno na Kinyume chake. Kufuru Kinyume chake ni Imani na Imani kinyume chake ni Kufuru.
Hebu tugeuze maneno haya mawili katika Namba kwa kutumia namba za hapo zamani kama nilivyofanya katika Miujiza mingineyo hapa juu.
Ukigeuza Herufi hizi katika Namba Utapata Namba na Kinyume chake kiajabu sana hebu tuone hapa chini:
الإيمان=133
الكفر=331
الإيمان=
ا 1 + ل 30 + إ 1 + ي 10 + م 40 + ا 1 + ن 50 = 133
الكفر=
ا 1 + ل 30 + ك 20 + ف 80 + ر 200=331
Je unaona namba na Kinyume chake? Unaona ya kushangaza? Namba 133 kinyume chake ni namba 331
Yaani Imani na kinyume chake ni Kufuru. Hebu ziangalie namba hizi mbili kisha uzilinganishe:
133
331
Namba na Kinyume chake. Angalia maajabu. Imani ni namba 133 na kafiri 331. Allahu Akbar. Allahu Akbar.
Hebu tujumlishe Namba Hizi Mbili:
133 + 331=464
sasa tuchunguze katika Kuruani Aya Ya 464 kuanzia mwanzo wa Msahafu tuone Aya gani tutakayoipata.
يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّهِ وَ فَضْلٍ وَ أَنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ
Hii ni aya ya 464 kuanzia Mwanzo wa Msahafu nayo inasema
Katika Aya Hii Mwenyeezi Mungu anaelezea Neema watakazopata waliofariki kwa ajili yake yaani Mashuadaa wake. Katika Aya Hii Mwenyeei Mungu anasema kwamba Hao Mashahidi wanabashiri habari nzuri za Neema kutoka kwa Allah na Fadhila Na Mwenyeezi Mungu hatampotezea Ujira Muumini yeyote.
Angalia neno MUUMINI yaani mwenye Imani.
Hebu tufikiri. Tulipojumlisha Namba 133 na 331 tukapata 464 na namba hii imetupeleka katika Aya yenye neno MUUMINI yaani mwenye Imani na pia habari nzuri ya zawadi watakazopewa na Mwenyeezi Mungu.
Nimefikiri sana Muujiza Wa Maneno haya mawili na nikajiuliza Kwa nini tukijumlisha namba hizi mbili tunapata namba ambayo inahusu IMANI.
Ninasema Huenda Kwani Mwenyeezi Mungu anajua zaidi. Huenda Maana tunayopata ni kama ifuatavyo:
Batili na Imani inaposhindana basi Imani itashinda bika shaka yeyote na ndiyo maana namba 133 tukijumlisha na namba 331 tunapata aya inayohusu Imani.
133 + 331= 463 ni sawa na kusema
Imani + Kufuru=Imani
Je unaona maajabu? Na fikira hii inatibitishwa na Aya ya kuruani inayosema
وَقُلْ جَآءَ ٱلْحَقُّ وَزَهَقَ ٱلْبَـٰطِلُ ۚ إِنَّ ٱلْبَـٰطِلَ كَانَ زَهُوقًۭا
“Sema Haki Imekuja Na Ubatili Umeondoka Kwa Hakika Ubatili ni wa kuondoka”
(The truth has come and falsehood has vanished. Indeed, falsehood is bound to vanish)
Kwa hiyo huu ni Utafiti lakini mwenyeezi mungu anajua zaidi. Ni Juhudi ndogo za Mja lakini huenda tunakosea. Tunamuomba Mwenyeezi Mungu atakabalie kazi hizi ndogo ndogo. Allahu Akbar.
MUUJIZA WA TANO
Muujiza Huu ni wa Kisayansi. Kwa kweli unashangaza na Inaonyesha Kuwa kuruani siyo maneno ya Kibinaadamu hata kidogo., Haiwezekani hata chembe. Ni wachache wajinga wasiolewa ndiyo wanaota ndoto na kufikiri kuruani iliandikwa na Mtume. Kwa kweli Haiwezekani kabisa. Hebu tupeleke Darubini katika Aya Ifuatayo kutoka Katika Sura Ya Al-Anaam Namba 6 Aya Namba 35 kisha tuone Maajabu mengine katika maajabu yasiyo na Mwisho. Allahu Akbar.
سُوۡرَةُ الاٴنعَام
وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكَ إِعۡرَاضُہُمۡ فَإِنِ ٱسۡتَطَعۡتَ أَن تَبۡتَغِىَ نَفَقً۬ا فِى ٱلۡأَرۡضِ أَوۡ سُلَّمً۬ا فِى ٱلسَّمَآءِ فَتَأۡتِيَہُم بِـَٔايَةٍ۬ۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَمَعَهُمۡ عَلَى ٱلۡهُدَىٰۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡجَـٰهِلِينَ (٣٥)
TAFSIRI
35. Na ikiwa ni makubwa Kwako huku kujitenga kwao (na haya unayowaambia kwa kuwa wanataka waonyeshwe hiyo miujiza wanayoitaka; ukawa unataka sharti waonyeshwe miujiza hiyo, na Mimi sitaki), basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini. katika ardhi (kwenda kutafuta miujiza hiyo) au :(unaweza kupata) ngazi ukapanda mbinguni na kuwaletea miujiza (wanayoitaka, fanya). Na kama Mwenyezi Mungu angependa bila shaka angewakusanya katika uwongozi (huu kwa miujiza hiyo; lakini hataki). Basi usiwe miongoni mwa wasiojua.
ENGLISH TRANSLATION
And if their turning away is hard on you, then if you can seek an opening (to go down) into the earth or a ladder (to ascend up) to heaven so that you should bring them a sign and if Allah had pleased He would certainly have gathered them all on guidance, therefore be not of the ignorant.
SHEREHE
Nabii Muhammad ﷺ alikuwa na hamu kubwa kabisa ya kutaka watu wote wasilimu upesi upesi. Wapewe hiyo miujiza wanayoitaka udhia uishe Lakini Mwenyezi Mungu alikuwa hapendi Uislamu huo. Anapenda wasilimu baada ya kuyafahamu vyema hayo wanayoambiwa. Siyo wanasilimu kwa nguvu za miujiza. Kwa hiyo Mwenyeezi Mungu anamwambia Mtume ﷺ kwamba ikiwa anaona kwamba Miujiza ni muhimu sana basi atafute Mwenyewe ndani ya ardhi yaani atafute njia aende akatafute Miujiza hiyo ardhini au Atafute Ngazi na aitumie kwenda Mbinguni ili kutafuta Miujiza Hiyo.
Jambo la kushangaza ni kioande cha Aya ambacho nimekitia Rangi katika Aya hii.
أَوۡ سُلَّمً۬ا فِى ٱلسَّمَآءِ
Kipande hiki kinasema au atafute ngazi na kwenda Mbinguni. Hebu tupeleke Darubini yetu katika Kipande hiki. Inayozungumzia Ngazi ya Kwenda Angani.
Je unajua hivi sasa Wanasayansi wapo mwanzoni katika Utafiti Mpya ambao mchanga sana wa kutengeneza Ngazi au Elevator ambayo kazi yake ni kwenda Katika Mwezi au katika Satelites huko Angani. Fikira Hii ilizaliwa hapo zamani mwishoni mwa karne ya 19 (Mwaka 1895) lakini mpaka leo bado inafanyiwa utafiti. Angalia Hapa Chini Video na Picha Kuhusu Habari hizi za Kushangaza. Kwa kweli unaweza kufikiria Upuzi lakini la kushangaza zaidi ni Aya Ya Kuruani ambayo imetaja Fikra hizi kuanzia Karne ya 6 sasa Mtume Mohamad ﷺ alijua vipi Habari hizi? kwa vipi Kuruani imeweza kuja na fikra na kutaja Ngazi? katika wakati huo wa zamani wakati kulikuwa hakuna Sayansi kama leo.
Hii inaonyesha Kwamba maneno ya Kuruani ni Yake Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Ni yule yule aliyeumba ulimwengu na ni yule yule ndiye aliyeshusha kuruani hii. Allahu Akbar. Alijua ya Baadaye na Tutakayoyafanya yote.
Hapa Chini Habari Nimenukulu kutoka katika Utafiti wa Wataalamu Duniani:
The Penn State University researchers had a hunch that these diamond nanothreads, which are remarkably light and strong at the same time — could prove to be an ideal material for a space elevator, a long cable anchored on Earth and reaching into space to attach to a satellite in orbit.
Just recently, a team from the Queensland University of Technology in Australia modeled the diamond nanothreads using large-scale molecular dynamics simulations and concluded that the material is far more versatile than previously thought and has great promise for aerospace properties. The simulation was published in early November.
LIft au Elevator ya Anga Inathibitisha Maajabu Ya Meneno ya Kuruanu Tukufu. Allahu Akbar
VIdeo-1
Video-2
Ngazi za Anga. Kuruani Imataja Habari ya Ngazi za Angani. Maajabu siyo Madogo. Kuruani imetaja haya Tangu karne ya 6 na Sayansi imekuja na fikra hizi hivi karibuni katika Karne ya 19 je unaona Maajabu?
MUUJIZA WA MIAKA 23 YA KUSHUKA KWA KURUANI-(MIAKA 23 YA UJUMBE WA MTUME MOHAMAD ﷺ)
Hebu tuchunguze Herufi za Sura Ya Kwanza na Kisha Sura Ya Mwisho katika Msahafu. Yaani Sura Namba 1 na Namba 114.
SURA YA ALFATIHA-SURA NAMBA 1
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (١) ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٢) ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (٣) مَـٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ (٤) إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ (٥) ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٲطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ (٦) صِرَٲطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ (٧)
SURA YA AL-NAS -SURA NAMBA 114
قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ (١) مَلِكِ النَّاسِ (٢) إِلَـٰهِ ٱلنَّاسِ (٣) مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ (٤) ٱلَّذِى يُوَسۡوِسُ فِى صُدُورِ ٱلنَّاسِ (٥) مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ (٦)
Maajabu ni kwamba Katika Herufi 28 za Lugha ya Kiarabu tunakuta Herufi 23 tu ambazo zimetumika katika Sura Ya Kwanza (Al-Fatiha) na 23 Katika Sura Ya Mwisho (Al-Nas).
Ukihesabu Herufi Zote utakuta Herufi za Sura Ya Al-Fatiha ni 139 Na herufi za Sura Ya Al-Nas ni 80 lakini hapa ninazungumzia ni Herufi zisizokariri. Katika Herufi za Sura Ya Al-Fatiha ambazo ni 139 kuna 23 tu peke ambazo zimejenga Sura hii lakini kuna zaidi ya moja Kwa mfano Herufi ya LAM zipo 22, Herufi ya Alif zipo 19 Na hivyo hivyo nyinginezo. Kwa hiyo ukichukua Herufi Moja ya LAM na Herufi Moja ya Alif na Ukifanya hivi katika Sura Hii ya Al-Fatiha na Pia Sura Ya Al-Nas utapata kila Sura katika hizi mbili zimetumia Herufi 23 tu katika Herufi 28 za Lugha ya Kiarabu. Lwa kweli inashangaza. Kwa nini Namba 23. Namba hii siyo Bure Bure. Namba 23 inaashiria Muda wa Ujumbe wa Mtume Mohamad ﷺ Ujumbe au Wahyi (Revelation) ilichukua muda wa Maiaka 23 tu. Ujumbe ulianza Mtume ﷺ alipokuwa na miaka 40 na kwa muda wa miaka 23 ujumbe alikuwa akiletewa Aya za Kuruani mpaka alipofikia Miaka 63 akafariki dunia. Je unaona Maajabu. Yaani Kuruani aliyepewa Ujumbe alikuwa yeye mwenyewe hajui Ghaib. Yaani hakujua kwamba Muda wa Wahyi utakuwa miaka 23. Kuruani ilificha habari hizi mpaka hivi leo mimi na wewe tunagundua haya maajabu. Je huoni Muujiza wa kushagaza. Allahu Akbar.
Katika Maandishi ya Hapo Mwanzoni ukihesabu Herufi utapata 20 lakini ukihesabu Herufi Maandishi Ya Herufi za Othman au Rasm Othman Utapata Herufi 23 kwa sababu Kuliongezwa Herufi ya Hamza mojawapo ni Ya Hamza yenye Fatha na ya pili yenye Kasra na Imetumika juu na chini ya Alif. Iliyopo juu ya Alif
inatamkwa “a” kama katika neno أَعُوذُ na Iliyopo chini ya Alif inatamkwa “i” kama katika Jina إِلَٰهِ
Na Pia Kulionegezwa Taa Marbouta kama vile katika neno الْجِنَّةِ inatamkwa “ti”
Hizi ziada ziliongezwa kuwasaidia watu watamke maneno haya bila makosa.
Jambo la kushangaza ni kwamba Namba 23 ambayo inaashiria miaka ya WAHYI tunaipata tena katika Aya Ifuatayo ambayo ni Aya inayowajibu Makafiri hapo zamani walipomuuliza Mtume ﷺ kwa nini Kuruani isishushwe mara moja yaani Kwa kiswahili kizuri Kwa Mpigo mmoja. Yaani Kwa nini ilichukua Muda wa Miaka 23? Hebu tuichunguza Aya Hiyo iliyoshuka Kuwajibu Makafiri Na Muujiza Mungine wa Kushangaza.
Sura Ya Al-Furqan Namba 25 Aya Namba 32
وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡلَا نُزِّلَ عَلَيۡهِ ٱلۡقُرۡءَانُ جُمۡلَةً۬ وَٲحِدَةً۬ۚ ڪَذَٲلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِۦ فُؤَادَكَۖ وَرَتَّلۡنَـٰهُ تَرۡتِيلاً۬ (٣٢)
TAFSIRI
32.Na wakasema wale waliokufuru: “Mbona hakuteremshiwa Qurani yote mara moja?” Kama hivi (unavyoona tumeiteremsha kidogo kidogo kwa mpango mzuri ) ill tuuthubutishe, (tuutilie nguvu) moyo wako (kwa hizo Aya mpya mpya zinazoteremka wakati baada . ya wakati), na tumeipanga kwa uzuri.
SHEREHE
Kuruani ina miujiza isiyo na Mwisho Allahu Akbar. Hebu angalia Aya Hii. Kwa kweli utashangaa sana nikikuambia kwamba Aya hii pia ina Herufi 23!!!!
Yaani Mwenyeezi Mungu aliwajibu makafiri lakini hata Namba zinathibitisha kwamba Wahyi (Revelation) ni Miaka 23.
Makafiri Walikuwa wanamuuliza Mtume ﷺ kwa nini WAHYI Unashuka Kidogo kidogo Na jibu likatolewa kwa kushuka Aya hii lakini Mtume ﷺ pia Hakujua Habari za Miaka 23 kwani ni Ghayb. Hizi tumegundua leo hii yaani Mimi na wewe ili iwe Muujiza. Mwenyeezi Mungu hakutaka Kumfunulia Mtume ﷺ Muda wa WAHYI au Revelation. na Yeye Mtume ﷺ wakati huo hakujua Muda utakaochukua wa Ujumbe huo kwani ni Siri yake Mwenyeezi Mungu. Mwenyeezi Mungu hawezi kutuambia Siku ya Kufariki Dunia na hivyo hivyo hakumwambia Mtume Mwisho wa WAHYI na Baadaye atafariki haiwezekani kuwa hivyo lakini Katika Aya Hii imebeba Muujiza ambao Ulifichwa kwa hekima kubwa. Leo ndiyo tunagundua iwe Muujiza Kwetu . Allahu Akbar. Allahu Akbar. Angalia Muujiza ambao Unatupita Kipimo. Allahu Akbar.
ِAya Hii Ina Jumla ya Herufi 68 lakini zisizokariri ni 23 tu peke yake katika Herufi 28 za Lugh aya Kiarabu. Kukariri Kariri kwa baadhi ya herufi ndiyo inaongeza Idadi ya Herufi na Kuwa 68. Kwa Hiyo Huu ni Muujiza siyo Mdogo. Angalia Maajabu. Suala la Makafiri lilijibiwa lakini Muda wa Miaka 23 ulikuwa Umewekwa kwa njia za Namba. Hakuna aliyejua Mpaka Leo. Sisi tunagundua iwe Muujiza na Ituzidishie Imani na Kutuongoza. Hii ndiyo inaonyesha kwamba Muujiza wa kuruani hautakwisha Mpaka Mwisho wa Dunia na Ulimwengu. Mwenyeezi Mungu amefanya hivyo ili kuwapa imani watu katika siku hizi za leo na baadaye. Mitume wote wamekwisha Fariki Dunia na hakuna Miujiza ya Kuona Kwa Macho lakini Kuna Kuruani Tukufu ambayo inatupa Imani na Inashuhudia Kwamba Mwenyeezi Mungu Yupo. Allahu Akbar.
Aya Mbili zifuatazo ambazo zimeanziwa na Ibara inayosema “Bila shaka Qurani”
Aya hizi za mfano huu ni Mbili tu katika Msahafu wote. Ajabu Ni Kwamba pia zimeundwa na Herufi 23 katika Herufi 28 za Lugha ya Kiarabu.
Hii inaashiria na kuthibitisha Muda wa WAHYI wa miaka 23 kwa kweli haya siyo madogo. Kuruani Ni Muujiza Siyo Mdogo. Allahu Akbar.
Sura Ya Israa Namba 17 Aya Namba 9
إِنَّ هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ يَہۡدِى لِلَّتِى هِىَ أَقۡوَمُ وَيُبَشِّرُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ أَنَّ لَهُمۡ أَجۡرً۬ا كَبِيرً۬ا (٩)
TAFSIRI
9. Hakika hii Qurani inaongoza katika njia iliyonyoka kabisa; na inawapa habari njema Waislamu wafanyao vitendo vizuri, ya kwamba watapata malipo makubwa (kabisa).
Sura Ya Al_Naml Namba 27 Aya Namba 76
إِنَّ هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ أَڪۡثَرَ ٱلَّذِى هُمۡ فِيهِ يَخۡتَلِفُونَ (٧٦)
TAFSIRI
76. Bila shaka Qurani hii inawaeleza wana wa lsraili mengi ambayo kwayo wanahitilafiana.
SHEREHE
Aya Hizi Mbili ni pekee katika Kuruani yote yaani ni Aya Mbili tu ambazo zimeanziwa na Ibara inayosema “Bila shaka Qurani” na Ajabu Ni kwamba Pia Kila Moja ya Hizi Aya zimetumia Herufi zisizokariri 23 tu. Huu kweli siyo Muujiza Mdogo hata kidogo.
Aya Hizi Mbili zimeanziwa na Ibara inyosema “Bila shaka Qurani” yaani Kila Aya Katika Aya Hizi Mbili zimetumia Herufi 23 tu katika Maandishi yake.
Lakini ukihesabu utapata zaidi ya herufi 23 kwani kuna badhi ya Herufi ambazo zimekariri.
Unapohesabu uzihesabu tu zile zilizotumika mara moja na ukifanya hivi utapata kila Aya imetumia Herufi 23 tu.
Allahu Akbar. Ni Muashirio wa Miaka Ya Wahyi (Revelation) Tuliyozungumza Hapa Juu. Allahu Akbar.
Kwa hiyo Sura Ya Israa Namba 17 Aya Namba 9 Ina jumla ya Herufi 70 lakini zisizikariri ni 23 tu na
Sura Ya Al_Naml Namba 27 Aya Namba 76
Ina Jumla Ya Herufi 47 lakini zisizokariri ni 23 tu. Je unaona Maajabu? Allahu Akbar.