UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MLANGO HUU BADO UPO KATIKA MAANDALIZI
MAZUNGUMZO (DIALOGUE)KATIKA KURUANI
17/April/2022 = Islamic Calendar 16/Ramadhan/1443
Nimeona bora katika siku ya leo ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan nifungue mlango mpya ambao utakusanya Mazungumzo au Dialogue zilizopo katika kuruani na Kisha kusherehesha angalau kwa ufupisho. Dialogue ni Mazungumzo baina ya Wawili. Katika Mlango huu Ningependelea Kukusanya Mazungumzo Katika Kuruni Tukufu Baina Ya Mwenyeezi Mungu na Nabii Musa, Nabii Isa , Sheitan Na Mazungumzo Mengineyo. Nitaorodhesha Aya Za DIalogue au Mazungumzo na kisha Nitashetehesha Mwenyeezi Mungu akipenda.
MAZUNGUMZO/DIALOGUE BAINA YA MWENYEEZI MUNGU NA NABII IBRAHIM
سُوۡرَةُ البَقَرَة
Kuruani: Sura Ya Al-Bakarah Namba 2
وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ رَبِّ أَرِنِى ڪَيۡفَ تُحۡىِ ٱلۡمَوۡتَىٰۖ قَالَ أَوَلَمۡ تُؤۡمِنۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَـٰكِن لِّيَطۡمَٮِٕنَّ قَلۡبِىۖ قَالَ فَخُذۡ أَرۡبَعَةً۬ مِّنَ ٱلطَّيۡرِ فَصُرۡهُنَّ إِلَيۡكَ ثُمَّ ٱجۡعَلۡ عَلَىٰ كُلِّ جَبَلٍ۬ مِّنۡہُنَّ جُزۡءً۬ا ثُمَّ ٱدۡعُهُنَّ يَأۡتِينَكَ سَعۡيً۬اۚ وَٱعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ۬ (٢٦٠)
TAFSIRI
260. Na (kumbuka) lbrahimu aliposema: “Mola wangu! Nionyeshe jinsi utakavyofufua wafu.” (Mwenyezi Mungu) akasema: “Huamini?” Akasema: “La, (naamini), lakini (nataka kuona hayo) ili moyo wangu utulie (zaidi). ‘.’ Akasema: “Basi chukua ndege wanne na uwazoeshe kwako (uwadhibiti vizuri sura zao hata wasikuputee po pole unapowaona), kisha ( wachinje) uweke juu ya kila jabali sehemu katika wao. Kisha waite, watakujia mbio; Na ujue ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye Hekima.”
SHEREHE
Nabii Ibrahim alikuwa na imani kamili lakini alitaka Yakini. Alitaka uhakika aone kwa macho namna Mwenyeezi Mungu anvyohuisha vilivyokufa. Haya ndiyo mazungumzo baina ya Mwenyeezi Mungu na Nabii Isa. Nabii Isa anamwomba Mwenyeezi Mungu aonyeshwe Namna ya Kuumba na Mwenyeezi Mungu akamkubalia. Hakuonyeshwa kila kitu bali aliwaua Ndege wake na kuwasambaza kisha akawaita na Wakaumbwa Na Mola na Kuitikia Mwito huo.
MAZUNGUMZO/DIALOGUE BAINA YA MWENYEEZI MUNGU NA NABII MUSA
سُوۡرَةُ طٰه
KURUANI:SURA YA TWAHA NAMBA 20
وَهَلۡ أَتَٮٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ (٩) إِذۡ رَءَا نَارً۬ا فَقَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّىٓ ءَانَسۡتُ نَارً۬ا لَّعَلِّىٓ ءَاتِيكُم مِّنۡہَا بِقَبَسٍ أَوۡ أَجِدُ عَلَى ٱلنَّارِ هُدً۬ى (١٠) فَلَمَّآ أَتَٮٰهَا نُودِىَ يَـٰمُوسَىٰٓ (١١) إِنِّىٓ أَنَا۟ رَبُّكَ فَٱخۡلَعۡ نَعۡلَيۡكَۖ إِنَّكَ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوً۬ى (١٢) وَأَنَا ٱخۡتَرۡتُكَ فَٱسۡتَمِعۡ لِمَا يُوحَىٰٓ (١٣) إِنَّنِىٓ أَنَا ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنَا۟ فَٱعۡبُدۡنِى وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِذِڪۡرِىٓ (١٤) إِنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ أَكَادُ أُخۡفِيہَا لِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا تَسۡعَىٰ (١٥) فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنۡہَا مَن لَّا يُؤۡمِنُ بِہَا وَٱتَّبَعَ هَوَٮٰهُ فَتَرۡدَىٰ (١٦) وَمَا تِلۡكَ بِيَمِينِكَ يَـٰمُوسَىٰ (١٧) قَالَ هِىَ عَصَاىَ أَتَوَڪَّؤُاْ عَلَيۡہَا وَأَهُشُّ بِہَا عَلَىٰ غَنَمِى وَلِىَ فِيہَا مَـَٔارِبُ أُخۡرَىٰ (١٨) قَالَ أَلۡقِهَا يَـٰمُوسَىٰ (١٩) فَأَلۡقَٮٰهَا فَإِذَا هِىَ حَيَّةٌ۬ تَسۡعَىٰ (٢٠) قَالَ خُذۡهَا وَلَا تَخَفۡۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا ٱلۡأُولَىٰ (٢١) وَٱضۡمُمۡ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٍ ءَايَةً أُخۡرَىٰ (٢٢) لِنُرِيَكَ مِنۡ ءَايَـٰتِنَا ٱلۡكُبۡرَى (٢٣) ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُ ۥ طَغَىٰ (٢٤) قَالَ رَبِّ ٱشۡرَحۡ لِى صَدۡرِى (٢٥) وَيَسِّرۡ لِىٓ أَمۡرِى (٢٦) وَٱحۡلُلۡ عُقۡدَةً۬ مِّن لِّسَانِى (٢٧) يَفۡقَهُواْ قَوۡلِى (٢٨) وَٱجۡعَل لِّى وَزِيرً۬ا مِّنۡ أَهۡلِى (٢٩) هَـٰرُونَ أَخِى (٣٠) ٱشۡدُدۡ بِهِۦۤ أَزۡرِى (٣١) وَأَشۡرِكۡهُ فِىٓ أَمۡرِى (٣٢) كَىۡ نُسَبِّحَكَ كَثِيرً۬ا (٣٣) وَنَذۡكُرَكَ كَثِيرًا (٣٤) إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرً۬ا (٣٥) قَالَ قَدۡ أُوتِيتَ سُؤۡلَكَ يَـٰمُوسَىٰ (٣٦) وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَيۡكَ مَرَّةً أُخۡرَىٰٓ (٣٧) إِذۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰٓ (٣٨) أَنِ ٱقۡذِفِيهِ فِى ٱلتَّابُوتِ فَٱقۡذِفِيهِ فِى ٱلۡيَمِّ فَلۡيُلۡقِهِ ٱلۡيَمُّ بِٱلسَّاحِلِ يَأۡخُذۡهُ عَدُوٌّ۬ لِّى وَعَدُوٌّ۬ لَّهُ ۥۚ وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةً۬ مِّنِّى وَلِتُصۡنَعَ عَلَىٰ عَيۡنِىٓ (٣٩) إِذۡ تَمۡشِىٓ أُخۡتُكَ فَتَقُولُ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ مَن يَكۡفُلُهُ ۥۖ فَرَجَعۡنَـٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَىۡ تَقَرَّ عَيۡنُہَا وَلَا تَحۡزَنَۚ وَقَتَلۡتَ نَفۡسً۬ا فَنَجَّيۡنَـٰكَ مِنَ ٱلۡغَمِّ وَفَتَنَّـٰكَ فُتُونً۬اۚ فَلَبِثۡتَ سِنِينَ فِىٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ ثُمَّ جِئۡتَ عَلَىٰ قَدَرٍ۬ يَـٰمُوسَىٰ (٤٠) وَٱصۡطَنَعۡتُكَ لِنَفۡسِى (٤١) ٱذۡهَبۡ أَنتَ وَأَخُوكَ بِـَٔايَـٰتِى وَلَا تَنِيَا فِى ذِكۡرِى (٤٢) ٱذۡهَبَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُ ۥ طَغَىٰ (٤٣) فَقُولَا لَهُ ۥ قَوۡلاً۬ لَّيِّنً۬ا لَّعَلَّهُ ۥ يَتَذَكَّرُ أَوۡ يَخۡشَىٰ (٤٤) قَالَا رَبَّنَآ إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفۡرُطَ عَلَيۡنَآ أَوۡ أَن يَطۡغَىٰ (٤٥) قَالَ لَا تَخَافَآۖ إِنَّنِى مَعَڪُمَآ أَسۡمَعُ وَأَرَىٰ (٤٦) فَأۡتِيَاهُ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَا بَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ وَلَا تُعَذِّبۡہُمۡۖ قَدۡ جِئۡنَـٰكَ بِـَٔايَةٍ۬ مِّن رَّبِّكَۖ وَٱلسَّلَـٰمُ عَلَىٰ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلۡهُدَىٰٓ (٤٧)
TAFSIRI
9. Na je! Imekujia hadithi ya Musa? 10. Alipouona moto, akawaambia watu wake (aliokuwa nao) “Ngojeni, hakika nimeona moto, huenda nikakuleteeni kijinga katika huo au nitapata mwongozaji katika moto huo (wa kutuonyesha njia).,11. Basi alipoflka akaitwa: “Ewe Musa!” “Bila shaka Mimi ndiye Mola wako. Basi vua viatu vyako. Hakika wewe uko katika bonde takatifu Ia Tuwa.” 13. “Nami Nimekuchagua (kuwa Mtume). Basi yasikilize unayoletewa (yanayofunuliwa kwako) Wahyi.” I4. “Kwa yakini Mimi ndiye Mwcnyezi Mungu, Hakuna aabudiwaye kwa haki ila Mimi, Basi niabudu na usimamishe Sala kwa kunitaja.” 15. “Bila shaka Kiama kitakuja. Nataka kusudi kukificha (nisiseme lini kitakuja) ill kila nafsi ilipwe kwa yale iliyoyafanya., I6. Basi wasikuzuie na (kuyaamini) hayo wale wasioyaamini na wafuatao matamanio ya nafsi zao. Usije ukaangamia. I7. Na ni nini hicho kilichomo mkononi mwako wa kuume (kulia), ewe Musa? 18. (Musa) Akasema: “Hii ni f1mbo yangu, ninaiegemea na ninaangushia (ninapukutishia) majani kwa ajili ya wanyama wangu. Tena ninatumia kwa matumizi mengine.” I9. Mungu akasema: “ltupe, ewe Musa.20. Akaitupa. Mara ikawa nyoka anayekwenda mbio. 2I. (Mungu) Akasema: “lkamate wala usiogope, sasa hivi Tutairudisha hali yake ya kwanza.” 22. “Na uambatishe mkono wako katika kwapa lako; utatoka mweupe sana pasipo ubaya wowote. (Chkua na huu kuwa) muujiza mwengine.” 23 “lli Tukuonyeshe miujiza yetu (mingine) mikubwa mikubwa.” 14. “Nenda kwa Firauni. Bila shaka yeye amepindukia mipaka.” 25. (Musa) Akasema: “Ewe Mola wangu! Nipanulie, (nikunjulie) kifua changu (niweze kustahamili balaa zitakazonifika) ” 26. “Na Unifanyie sahali kazi yangu (hii uliyonipa) ” 27. “Na Ufungue fundo lililo katika ulimi wangu” 28. “Wapate kufahamu maneno yangu (nitakayowaambia).” 29. “Na Unifanyie waziri, (msaidizi) katika jamaa zangu-” · 30. “Ndugu yangu Haruni (mfanye awe ndiye waziri wangu) ” 31 • “Nitie nguvu kwa (ndugu yangu) huyu ” 32 . “Na umshirikishe katika kazi yangu (hii) ” 33· “Ili Tukutukuze sana” 34· “Na tukutaje kwa wingi.” 35· “Hakika Wewe Unatuona.”36. (Mungu) Akasema: “Hakika umepewa maombi yako (yote haya uliyoyataka), ewe Musa! 37. “Na hakika Tulikufanyia ihisani mara nyingine (nyingi; kama vile)”: 38. Tulipomfunulia mama yako yaliyofunuliwa (kwake. Tulimfahamisha kufanya haya):- 39. Ya kwamba mtie (mwanao, ambaye ndiye wewe Musa) sandukuni, kisha litie mtoni, na mto. utamtupa ufukoni ill amchukue adui Yangu na adui yake (amlee kwa uzuri. Naye ni Firauni). Na nimekutilia mapenzi yanayotokana kwangu (ili upendwe na watu wote), na ill ulelewe machoni mwangu (nimekurejesha kwa mama yako). 40. (Kumbuka) dada yako alipokwenda (kwa watu wake Firauni) na akasema: “Je! Nikujulisheni mtu wa (kuweza) kumlea?” Na Tukakurudisha kwa mama yako ill macho yake yaburudike wala asihuzunike. Na ulimuua mtu na Tukakuokoa katika huzuni na Tukakujaribu kwa majaribio mengi. Na ukakaa miaka mingi pamoja na watu wa Madyan kisha umekuja (hapa) kama ilivyokadiriwa, ewe Musa. 41. Na Nimekuchagua kwa ajili Yangu, (Uwe Mtume wangu).42. “Nenda wewe na ndugu yako pamoja na Hoja Zangu wala msichoke (msiache) · kunikumbuka., 43. “Nendeni kwa Firauni, bila shaka amepindukia mipaka. ” 44· “Kamwambieni maneno laini huenda atashika mawaidha au ataogopa.” 45. Wakasema: “Ewe Mola wetu! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mpaka juu yetu au kututakabaria.” 46. (Mungu) Akasema: “Msiogope, bila shaka Mimi ni pamoja nanyi: Nasikia na naona!’ 4 7. “Basi mwendeeni na mwambieni: Kwa yakini sisi ni Mitume wa Mola wako. Basi waachie wana wa Israili watoke pamoja nasi na usiwaadhibu. Hakika Tumekuletea Ishara zitokazo kwa Mola wako. Na amani itakuwa juu ya wale wanaofuata uwongofu.”
SHEREHE
Nabii Musa alipoona Moto mbali juu ya mlima wa Sinai unang’ara akawaambia watu wake wamsubiri. inaonyesha kwamba yeye peke yake ndiye aliyeuona moto huo. Na akawambia kwamba ameamua kwenda juu ya Mlima huo kwa lengo la kuchukua Kijinga cha moto na pia Huenda Moto huo utawasaidia kuwaongoza katika safari yao hapo Jangwani. Yaani huenda Moto huo ukawapa Dalili nyinginezo wasizojua. Nabii Musa alipofika Juu ya Mlima huo yaani Sinai mara akasikia Sauti Inamwita kwa Jina Lake. Anaambiwa “Ewe Musa” “Mimi ni Mungu wako” ” Vua Viatu Vyako” ” Kwa hakika upo katika Bonde Takatifu” Sehemu ya ibada ni sehemu Takatifu. Msikiti ni sehemu Takatifu na ndiyo maana Waislamu tunavua Viatu tunapoingia Msikitini. Kwani Hiyo ni Nyumba Ya Mwenyeezi Mungu. Kisha Mwenyeezi Mungu Anampa Habari Nzuri kwamba Amechaguliwa kuwakilisha kazi yake. Kuchaguliwa huko ni Utukufu mkubwa sana. Kisha Mwenyeezi Mungu anasema “kwa hakika Mimi, Mimi ni Allah. Hakuna Mungu isipokuwa Mimi. Niabudu, Na usimamishe Sala Kwa Kunitaja Mimi” Hebu fikiri maneno haya. Kwa kweli yanatisha. Mwenyeezi Mungu anaendelea kusema kwamba Kiyama Kinakuja, ameificha Siku hiyo ili iwe Mtihani, Siku hiyo Itakuja Ghafla. Na kila Nafsi italipwa kwa kila ilichochuma duniani. Na anaendelea kumwambia Nabii Musa kwamba Asiyekuwa na imani asikuzuie katika kuamini siku ya Kiama, yaani asimfuate yule ambaye anayefuata Matamanio ya nafsi yake. Na Ukienda Kinyume na haya utajikuta miongoni mwa Walioangamia. Mwenyeezi Mungu anamwuliza Nabii Musa alichobeba katika Mkono wa Kulia na akajibu ni Fimbo amabayo anaitumia katika Kujiegemea Mwili wake, Na kupurutushia Majani Ya Miti kwa ajili ya chakula cha mifugo yake, na Pia Katika Matumizi Mengineyo. Hapa Nabii Musa anaanza kuhisi urafiki na Anazungumza kwa utulivu na kuelezea vizuri bila ya wasiwasi. Suala moja tu na yeye kalijibu kwa urefu. Amelijibu kwa urefu na kwa utulivu kwani hivi sasa anajihisi anazungumza na Mwenyeezi Mungu ambaye ana huruma. Lakini Hakujua kwamba Kuna Mtihani ambao Unafuata mazungumzo hayo. Na ni Mtihani Sio Mdogo. Kabla Ya Mwenyeezi Mungu kumpa Mtihani huo alimpa Silaha mbili. Mojawapo ilimtoa Jasho Nabii Musa na Kwa kweli ni Training ya hali ya Juu. Mwenyeezi Mungu akamwambia Nabii Musa aitupe Fimbo Chini na alipofanya hivyo mara ikageuka Joka la kutisha ambalo Joka hilo lilikuwa likitembea tembea huku na huku. Nabii Musa akaogopa sana. Hebu fikiri ungelikuwa wewe katika sehemu hiyo. Mtihani wa hali ya Juu. Kwa kweli Ni Training kabla ya Mtihani Utakaofuata. Sasa anaambiwa alishike Joka hilo na bado linatembea tembea huku na huku. Anaambiwa “Lichukue na Usiogope” Nabii Musa jasho linamtoka. Anaambiwa Usiogope na kisha Baada ya Kulishika Tutaligeuza litakuwa Fimbo”. ilimbidi afanye Mtihani huo Mgumu. Hakuna Budi isipokuwa kutii Amri. Akalishika na mara likageuka na Kuwa Fimbo. Sasa anapewa Tena Muujiza wa pili. Nao ni Mkono wake. Anaamrishwa Aingize Mkono wake katika Kwapa lake na baada ya kuutoa tu ukageuka na Kung’ara. Unang’ara Mfano wa Mwezi au Nyota. Nabii Musa sasa anatulia Roho kwani Amepewa Silaha Mbili. Na hii ni zawadi kubwa. Hakujua Mtihani Unaofuata ambao siyo mdogo hata kidogo. Sasa anaamrishwa Aende akapambane na Firauni. Arudi akalinganie Dini huko Egypt. Cairo. Huko huko alipoua Mtu hapo zamani na akakimbia kwa kuogopa kuawa Arudi huko huko. Kwa kweli siyo mtihani Mdogo. Anarudishwa kwa Adui Mkubwa. Sasa Nabii Musa anaomba Apate Msaidizi na Anatamani Msaidizi huyo awe kaka yake Harun. Mwenyeei Mungu anamruzuku aliyoyaomba. Baada ya Hapo Mwenyeezi Mungu anamtia Moyo Nabii Musa kwa kumhadithia Maisha Yake yote kuanzia Kuzaliwa kwake. Mwenyeezi Mungu anampa Nguvu kumjuulisha kwamba Yote yaliyopita aliyapanga yeye mwenyewe. Na Kwa hiyo asiogope aende kwa Nabii Musa bila Ya wasiwasi wowote na kama alivyomlinda hapo zamani basi atamsaidia na kumlinda tena kama alivyomlinda kuanzia alipozaliwa na kulelewa na Firauni ambaye alikuwa katili na Adui. Wakati ambao Firauni alikuwa akiua watoto Mwenyeezi Mungu alimhifadhi Nabii Musa asiuawe kwa hiyo analiwazwa asiogope aende akapambane na Firauni. Alinganie Dini kwa Maneno Matamu huenda Yatamfaa Firauni.
MAZUNGUMZO BAINA YA NABII IBRAHIM NA BABA YAKE KATIKA SURA YA MARYAM
سُوۡرَةُ مَریَم
KURUANI:SURA YA MARYAM NAMBA 19
وَٱذۡكُرۡ فِى ٱلۡكِتَـٰبِ إِبۡرَٲهِيمَۚ إِنَّهُ ۥ كَانَ صِدِّيقً۬ا نَّبِيًّا (٤١) إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ يَـٰٓأَبَتِ لِمَ تَعۡبُدُ مَا لَا يَسۡمَعُ وَلَا يُبۡصِرُ وَلَا يُغۡنِى عَنكَ شَيۡـًٔ۬ا (٤٢) يَـٰٓأَبَتِ إِنِّى قَدۡ جَآءَنِى مِنَ ٱلۡعِلۡمِ مَا لَمۡ يَأۡتِكَ فَٱتَّبِعۡنِىٓ أَهۡدِكَ صِرَٲطً۬ا سَوِيًّ۬ا (٤٣) يَـٰٓأَبَتِ لَا تَعۡبُدِ ٱلشَّيۡطَـٰنَۖ إِنَّ ٱلشَّيۡطَـٰنَ كَانَ لِلرَّحۡمَـٰنِ عَصِيًّ۬ا (٤٤) يَـٰٓأَبَتِ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ۬ مِّنَ ٱلرَّحۡمَـٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيۡطَـٰنِ وَلِيًّ۬ا (٤٥) قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنۡ ءَالِهَتِى يَـٰٓإِبۡرَٲهِيمُۖ لَٮِٕن لَّمۡ تَنتَهِ لَأَرۡجُمَنَّكَۖ وَٱهۡجُرۡنِى مَلِيًّ۬ا (٤٦) قَالَ سَلَـٰمٌ عَلَيۡكَۖ سَأَسۡتَغۡفِرُ لَكَ رَبِّىٓۖ إِنَّهُ ۥ كَانَ بِى حَفِيًّ۬ا (٤٧) وَأَعۡتَزِلُكُمۡ وَمَا تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَأَدۡعُواْ رَبِّى عَسَىٰٓ أَلَّآ أَكُونَ بِدُعَآءِ رَبِّى شَقِيًّ۬ا (٤٨)
TAFSIRI
41.Na mtaje lbrahimu katika Kitabu (hiki). Bila shaka yeye alikuwa mkweli sana na Nabii.42. (Wakumbushe) alipomwambia baba yake: “Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyosikia na visivyoona na visivyokufaa chochote?” 43· “Ewe baba yangu! Kwa yakini imenijia ilimu isiyokujia. Basi nifuate nitakuongoza njia iliyo saw a.” 44· “Ewe baba yangu! Usimuabudu Shetani, hakika Shetani ni mwenye kumuasi (Mwenyezi Mungu) Mwenye wingi wa rehema., 45. “Ewe baba yangu! Hakika naogopa kupatwa na adhabu inayotoka kwa Mwingi wa rehema (Mwenyezi Mungu),· (ukifanya hivyo) utakuwa mwenziwe Shetani. 46. Akasema (Yule baba yake) “Je! unaichukia miungu yangu, ewe lbrahimu? Kama huachi (hayo unayoyasema) lazima nitakupiga mawe. Na niondokelee mbali, kwa muda mchache (huu).” 47· (lbrahimu) akasema: “Amani iwe juu yako! Nitakuombea msamaha kwa Mola wangu, bila shaka Yeye ananihurumia sana.” 48. “Na mimi nakuondokeeni (na kujiepusha) na mnayoyaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu. Na nitamuomba Mola wangu: hakika sitakuwa mwenye kukhibu (kukosa ninalolitaka) kwa kumuomba Mola wangu.”
SHEREHE
Haya Ni Mazungumzo baina ya nabii Ibrahim na baba Yake.Nabii Ibrahim Anamnasihi aache ibada ya Masanamu na Baba Yake anamfukuza amuache katika Ibada yake hiyo. Nabii Ibrahim Anamuombea Baba Yake Usalama na Amani Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu. Baba Yake alikuwa amezama katika itikadi zao za Kuabudu Masanamu na Hakukubali Kumsikiliza Mwanawe.
MAZUNGUMZO/DIALOGUE BAINA YA NABII IBRAHIM NA KAUMU (TAIFA) YAKE, PAMOJA NA BABA YAKE
سُوۡرَةُ الاٴنبیَاء
KURUANI:SURA YA AL-AMBIYAA NAMBA 21
۞ وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَآ إِبۡرَٲهِيمَ رُشۡدَهُ ۥ مِن قَبۡلُ وَكُنَّا بِهِۦ عَـٰلِمِينَ (٥١) إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَا هَـٰذِهِ ٱلتَّمَاثِيلُ ٱلَّتِىٓ أَنتُمۡ لَهَا عَـٰكِفُونَ (٥٢) قَالُواْ وَجَدۡنَآ ءَابَآءَنَا لَهَا عَـٰبِدِينَ (٥٣) قَالَ لَقَدۡ كُنتُمۡ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُڪُمۡ فِى ضَلَـٰلٍ۬ مُّبِينٍ۬ (٥٤) قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا بِٱلۡحَقِّ أَمۡ أَنتَ مِنَ ٱللَّـٰعِبِينَ (٥٥) قَالَ بَل رَّبُّكُمۡ رَبُّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ ٱلَّذِى فَطَرَهُنَّ وَأَنَا۟ عَلَىٰ ذَٲلِكُم مِّنَ ٱلشَّـٰهِدِينَ (٥٦) وَتَٱللَّهِ لَأَڪِيدَنَّ أَصۡنَـٰمَكُم بَعۡدَ أَن تُوَلُّواْ مُدۡبِرِينَ (٥٧) فَجَعَلَهُمۡ جُذَٲذًا إِلَّا ڪَبِيرً۬ا لَّهُمۡ لَعَلَّهُمۡ إِلَيۡهِ يَرۡجِعُونَ (٥٨) قَالُواْ مَن فَعَلَ هَـٰذَا بِـَٔالِهَتِنَآ إِنَّهُ ۥ لَمِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٥٩) قَالُواْ سَمِعۡنَا فَتً۬ى يَذۡكُرُهُمۡ يُقَالُ لَهُ ۥۤ إِبۡرَٲهِيمُ (٦٠) قَالُواْ فَأۡتُواْ بِهِۦ عَلَىٰٓ أَعۡيُنِ ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَشۡهَدُونَ (٦١) قَالُوٓاْ ءَأَنتَ فَعَلۡتَ هَـٰذَا بِـَٔالِهَتِنَا يَـٰٓإِبۡرَٲهِيمُ (٦٢) قَالَ بَلۡ فَعَلَهُ ۥ ڪَبِيرُهُمۡ هَـٰذَا فَسۡـَٔلُوهُمۡ إِن ڪَانُواْ يَنطِقُونَ (٦٣) فَرَجَعُوٓاْ إِلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ فَقَالُوٓاْ إِنَّكُمۡ أَنتُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ (٦٤) ثُمَّ نُكِسُواْ عَلَىٰ رُءُوسِهِمۡ لَقَدۡ عَلِمۡتَ مَا هَـٰٓؤُلَآءِ يَنطِقُونَ (٦٥) قَالَ أَفَتَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُڪُمۡ شَيۡـًٔ۬ا وَلَا يَضُرُّكُمۡ (٦٦) أُفٍّ۬ لَّكُمۡ وَلِمَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ (٦٧) قَالُواْ حَرِّقُوهُ وَٱنصُرُوٓاْ ءَالِهَتَكُمۡ إِن ڪُنتُمۡ فَـٰعِلِينَ (٦٨) قُلۡنَا يَـٰنَارُ كُونِى بَرۡدً۬ا وَسَلَـٰمًا عَلَىٰٓ إِبۡرَٲهِيمَ (٦٩) وَأَرَادُواْ بِهِۦ كَيۡدً۬ا فَجَعَلۡنَـٰهُمُ ٱلۡأَخۡسَرِينَ (٧٠) وَنَجَّيۡنَـٰهُ وَلُوطًا إِلَى ٱلۡأَرۡضِ ٱلَّتِى بَـٰرَكۡنَا فِيہَا لِلۡعَـٰلَمِينَ (٧١)
TAFSIRI
51.Na hakika tulimpa lbrahimu uwongofu wake zamani na tulikuwa tukimjua ( vizuri). 52. (Wakumbushe watu) alipomwambia baba yake na watu wake: “Ni nini masanamu haya mnayakalia wakati wote (kuya-abudu)?” 53. Wakasema, “Tuliwakuta babu zetu wakiyaabudu, (basi na sisi tunayaabudu).” 54· Akasema: “Bila shaka nyinyi na baba zenu mlikuwa katika upotofu (upotevu) ulio dhahiri.” 55.Wakasema: “Je! Umetujia kwa (maneno ya) haki au umo miongoni mwa wachezaji?” 56. Akasema: “(Siyo! mimi si mchezaji) Bali Mola wenu ni yule Mola wa mbingu na ardhi ambaye ndiye aliyeziumba. Nami ni miongoni mwa wenye kuyashuhudia haya.” 57. “Na Wallahi (Kwa haki ya Mungu) nitayafanyia mabaya masanamu yenu haya baada ya kunipa mgongo mkenda zenu.” 58. Basi akayavunja (masanamu yote yale) vipande vipande isipokuwa lile kubwa lao (aliliacha), ili wao (hao makafiri) walirudie. 59· Wakasema: “Nani aliyeifanya hivi miungu yetu? Hakika huyo yu miongoni mwa madhalimu (wakubwa)”. 6o. Wakasema: “Tulimsikia kijana mmoja akiwataja anayeitwa lbrahimu.” 61. Wakasema: “Basi mleteni mbele ya macho ya watu. wamshuhudie (kwa ubaya wake huo).” 62. Wakasema: “Je! Wewe umeifanya hivi miungu yetu, Ewe lbrahimu?” 63.Akasema: “Siyo, Bali amefanya (hayo) huyu mkubwa wao, basi (muulizeni na) waulizeni (pia hao waliovunjwa) kama wanaweza kunena!”64. Basi wakajirudi nafsi zao, (wakafikiri udhalilifu wa waungu hao walio nao, wasioweza kujipigania) na wakasema: “Hakika nyinyi mlikuwa madalimu (wa nafsi zenu kwenda kuwaabudu wasiokuwa na maana).” 65.Kisha wakainamishwa vichwa vyao, (wakarejea ujingani, ukafirini, wakasema): “Hakika umekwishajua . ya kwamba hawasemi, (kwa nini unatucheza shere? ). ” 66. Akasema: “Je! Mnaabudu badala ya Mwenyeezi Mungu (miungu) isiyokufaeni chochote (mnapowaabudu) wala kukudhuruni (chochote mnapowacha kuwaabudu)?” 67.Kefule (udhalilifu) yenu na ya hivyo mnavyoviabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu. Je! hamfikiri? 68. Wakasema: “mteketezeni kwa moto na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi ni watendao jambo (basi tendeni hili)., 69. Tukasema: “Ewe moto! Kuwa baridi na salama juu ya lbrahimu ” 70.Na walimtakia ubaya, lakini tukawafanya wao ndiyo wenye kupata hasara. 71.Na tulimuokoa yeye na Luti (tukawapeleka katika ardhi tuliyoibarikia kwa ajili ya walimwengu. (Ardhi ya Shamu).
SHEREHE
Nabii Ibrahim alitumia Hekima katika kulingania Jina la Mwenyeezi Mungu. Kwanza aliwaeleza kaumu hiyo akiwamo Baba yake mzazi ukweli kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mwenye Kumiliki Mbingu na Ardhi na ibada ya hayo Masanamu ni Upotovu ulio Wazi. Hatua ya Pili aliyochukua ni Kuyavunja masanamu hayo na kubakiza Sanamu Moja Kubwa. Walipomuuliza kwa nini ameyavunja Masanamu Yao akawashauri wamuulize yule Sanamu Mkubwa na Pia yale yaliyovunjika. Hekima hii ikawatatanisha Watu wa Kaumu yake.
Kwanza wakalaumiana wenyewe kwa wenyewe kwa Kuabudu Masanamu yasiyo na uwezo wowote lakini haikuchukua muda wakajidanganya tena kwa ujinga wao na kurudisha fikra zao katika ukafiri.. Wakamwona Ibrahim ndiye aliyepotea na siyo wao.
MAZUNGUMZO/DIALOGUE BAINA YA NABII IBRAHIM NA KAUMU (TAIFA) YAKE, PAMOJA NA BABA YAKE
سُوۡرَةُ الصَّافات
KURUANI:SURA YA AL-SWAFAAT NAMBA 37
۞ وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبۡرَٲهِيمَ (٨٣) إِذۡ جَآءَ رَبَّهُ ۥ بِقَلۡبٍ۬ سَلِيمٍ (٨٤) إِذۡ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوۡمِهِۦ مَاذَا تَعۡبُدُونَ (٨٥) أَٮِٕفۡكًا ءَالِهَةً۬ دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ (٨٦) فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٨٧) فَنَظَرَ نَظۡرَةً۬ فِى ٱلنُّجُومِ (٨٨) فَقَالَ إِنِّى سَقِيمٌ۬ (٨٩) فَتَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ مُدۡبِرِينَ (٩٠) فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِہِمۡ فَقَالَ أَلَا تَأۡكُلُونَ (٩١) مَا لَكُمۡ لَا تَنطِقُونَ (٩٢) فَرَاغَ عَلَيۡہِمۡ ضَرۡبَۢا بِٱلۡيَمِينِ (٩٣) فَأَقۡبَلُوٓاْ إِلَيۡهِ يَزِفُّونَ (٩٤) قَالَ أَتَعۡبُدُونَ مَا تَنۡحِتُونَ (٩٥) وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ وَمَا تَعۡمَلُونَ (٩٦) قَالُواْ ٱبۡنُواْ لَهُ ۥ بُنۡيَـٰنً۬ا فَأَلۡقُوهُ فِى ٱلۡجَحِيمِ (٩٧) فَأَرَادُواْ بِهِۦ كَيۡدً۬ا فَجَعَلۡنَـٰهُمُ ٱلۡأَسۡفَلِينَ (٩٨)
TAFSIRI
83.Na hakika lbrahimu alikuwa katika kundi lake, (akenda mwendo wake). · 84. Aliiendea (dini ya) Mola wake kwa moyo safi. 85· Alimwambia baba yake na watu wake, “Mnaabudu nini?” 86. “Oh! Kwa uzushi tu, miungu badala ya Mwenyezi Mungu-ndiyo mnayoitaka?” 87.”Basi nini flkira yenu juu ya Mola wa walimwengu wote? (Mnamuona hatoshelezii ndio mnatafuta Waungu wengine?)” 88. Kisha akatazama mtazamo (mkubwa) katika nyota (akasema “Nitachukua fursa ya kuwajulisba uwongo wa dini yao· kwa kuwaonyesha kuchomoza kwake hizo nyota wanazoziabudu na kuchwa kwake).” 89. Akasema: “Hakika mimi ni mgonjwa.” 90.Nao wakamuacha, wakampa kisogo (wakenda zao viungani katika mandari zao). 91 ; Basi alikwenda kwa siri kwa miungu yao akaiambia (kwa stihzai): “Muna nini? Mbona hamuli? (Vyakula hivi vya mihanga mlivyowekewa?)” 92. “Mumekuwaje! Hamsemi?” 9 3. Kisha akawageukia kuwapiga kwa mkono wa kulia, (kwa mwisho wa nguvu zake). 94· (Basi waliposikia wenyewe) wakamjia upesi upesi (wakamwambia kwa nini kuwavunja waungu wao). 95· Akasema: “Oh! Mnaviabudu mnavyovichonga (wenyewe kwa mikono yenu)?” 96. “Hali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekuumbeni nyinyi na mnavyovifanya.” 97. Wakasema: Mjengeeni jengo (mlitie makuni mliwashe moto), kisha mtupeni motoni humo.” 98.Basi walitaka kumfanyia vitimbi _(yya kumua) lakini tukawafanya wao kuwa wadhalilifu. (Moto ute haukumuunguza hata chembe Nabii Ibrahimu.)
SHEREHE
Kisa Kile kile tulichokitaja hapo awali, Mazungumzo baina ya Nabii Musa na Kaumu yake. Habari ile ile inayohusu kuvunja kwa Masanamu. Mwishoni walipomuona ameshilia Imani Yake barabara wakaamua wamuue kwa kumchoma Moto. Muujiza Mkubwa uliofanyika ni kwamba Baada ya Kutupwa Motoni na Moto Huo Kuzimika Wakamkuta Nabii Ibrahim yupo Mzima na Afya Nzuri. Hakuathirika Kwa Moto mkubwa uliondaliwa kwa lengo la kumuua na Huu ni Muujiza siyo Mdogo.
MAZUNGUMZO/DIALOGUE BAINA YA NABII IBRAHIM NA MFALME ALIYEJULIKANA KAMA NAMRUD AU NAMROD ALIYEKUWA MFALME WA BABYLON ALIYEKUWA HAAMINI KUWEKO KWA MWENYEEZI MUNGU
سُوۡرَةُ البَقَرَة
KURUANI:SURA YA AL-BAKARAH NAMBA 2
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِى حَآجَّ إِبۡرَٲهِـۧمَ فِى رَبِّهِۦۤ أَنۡ ءَاتَٮٰهُ ٱللَّهُ ٱلۡمُلۡكَ إِذۡ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ رَبِّىَ ٱلَّذِى يُحۡىِۦ وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا۟ أُحۡىِۦ وَأُمِيتُۖ قَالَ إِبۡرَٲهِـۧمُ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَأۡتِى بِٱلشَّمۡسِ مِنَ ٱلۡمَشۡرِقِ فَأۡتِ بِہَا مِنَ ٱلۡمَغۡرِبِ فَبُهِتَ ٱلَّذِى كَفَرَۗ وَٱللَّهُ لَا يَہۡدِى ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٢٥٨)
TAFSIRI
258. Hukumsikia yule aliyehojiana na Ibrahimu juu ya Mola wake kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? lbrahimu aliposema: “Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na hufisha,” yeye akasema: “Mimi pia nahuisha na kufisha.” lbrahimu akasema: “Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi.” Akafedheheka yule aliyekufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu
SHEREHE
Mazungumzo baina Ya Nabii Ibrahim na Mfalme Namrud au Namrod wa Babylon ambayo leo ni Iraq. Habari zilifika Kwa Mfalme wa Dola Hiyo. Historia Insema kwamba Mfalme huyu alikuwa jabari ambaye alidai Uungu, na raia zake wakamwabudu. Alipokuja Nabii lbrahimu kufundisha dini ya haki Yenye Kukataa Miungu. Alimuuliza Nabii lbnbimu “Kwani huyo Mungu wa haki hufanya nini?” Nabii Ibrahim akamjibu “Huhuisha na kufishaa” Akajifanya kama kwamba hakufahamu muradi wa Nabii lbrahimu. Mfalme akamwambia Nabii Ibrahim ‘Na mimi pia nafanya kazi hii. Nitazame ninavyoifanya.’ Pale pale akaamrisha waletwe watu wawili waliostahiki kuuawa, akaamrisha auawe mmoja katika hao wawili na mwingine asamehewe. Akamwambia Nabii lbrahimu ‘Umeonaje? Nimehuisha na Kufisha?’ Nabii lbrahimu alipomwona anajitia Ujanja alimpa Mfalme jambo ambalo hawezi kulitilia Kulifanya.akamwambia habari hii ya kutolesha Mwenyezi Mungu jua Mashariki akamwambia Mfalme alitoleshe Magharibi kama yeye ni Mungu pia. Hapo akatahadari asijue Ia kutenda wala Ia kunena.
MAZUNGUMZO/DIALOGUE BAINA YA NABII IBRAHIM NA BABA YAKE
سُوۡرَةُ الاٴنعَام
KURUANI:SURA YA AL-ANAM NAMBA 6
۞ وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٲهِيمُ لِأَبِيهِ ءَازَرَ أَتَتَّخِذُ أَصۡنَامًا ءَالِهَةًۖ إِنِّىٓ أَرَٮٰكَ وَقَوۡمَكَ فِى ضَلَـٰلٍ۬ مُّبِينٍ۬ (٧٤) وَكَذَٲلِكَ نُرِىٓ إِبۡرَٲهِيمَ مَلَكُوتَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلِيَكُونَ مِنَ ٱلۡمُوقِنِينَ (٧٥) فَلَمَّا جَنَّ عَلَيۡهِ ٱلَّيۡلُ رَءَا كَوۡكَبً۬اۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّىۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلۡأَفِلِينَ (٧٦) فَلَمَّا رَءَا ٱلۡقَمَرَ بَازِغً۬ا قَالَ هَـٰذَا رَبِّىۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَٮِٕن لَّمۡ يَہۡدِنِى رَبِّى لَأَڪُونَنَّ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلضَّآلِّينَ (٧٧) فَلَمَّا رَءَا ٱلشَّمۡسَ بَازِغَةً۬ قَالَ هَـٰذَا رَبِّى هَـٰذَآ أَڪۡبَرُۖ فَلَمَّآ أَفَلَتۡ قَالَ يَـٰقَوۡمِ إِنِّى بَرِىٓءٌ۬ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ (٧٨) إِنِّى وَجَّهۡتُ وَجۡهِىَ لِلَّذِى فَطَرَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ حَنِيفً۬اۖ وَمَآ أَنَا۟ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ (٧٩) وَحَآجَّهُ ۥ قَوۡمُهُ ۥۚ قَالَ أَتُحَـٰٓجُّوٓنِّى فِى ٱللَّهِ وَقَدۡ هَدَٮٰنِۚ وَلَآ أَخَافُ مَا تُشۡرِكُونَ بِهِۦۤ إِلَّآ أَن يَشَآءَ رَبِّى شَيۡـًٔ۬اۗ وَسِعَ رَبِّى ڪُلَّ شَىۡءٍ عِلۡمًاۗ أَفَلَا تَتَذَڪَّرُونَ (٨٠) وَڪَيۡفَ أَخَافُ مَآ أَشۡرَڪۡتُمۡ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمۡ أَشۡرَكۡتُم بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ عَلَيۡڪُمۡ سُلۡطَـٰنً۬اۚ فَأَىُّ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ أَحَقُّ بِٱلۡأَمۡنِۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ (٨١) ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَمۡ يَلۡبِسُوٓاْ إِيمَـٰنَهُم بِظُلۡمٍ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ لَهُمُ ٱلۡأَمۡنُ وَهُم مُّهۡتَدُونَ (٨٢)وَتِلۡكَ حُجَّتُنَآ ءَاتَيۡنَـٰهَآ إِبۡرَٲهِيمَ عَلَىٰ قَوۡمِهِۦۚ نَرۡفَعُ دَرَجَـٰتٍ۬ مَّن نَّشَآءُۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ۬ (٨٣)
TAFASIRI
74· Na (kumbukeni) lbrahimu alipomwambia baba yake, Azar: “Unawafanya masanamu kuwa waungu? Hakika ninakuona wewe na watu wako mumo katika upotofu (upotevu) ulio dhahiri. 75. Na namna hivi tulimwonyesha lbrahimu ufalme wa mbingu na ardhi (kuwa ni wa Mungu), na ili awe miongoni mwa wenye yakini. 76. Na usiku ulipomwingilia (lbrahimu na hali kakaa na makafiri), akaona nyota, alinena (Kwa makusudi kutaka kuwavuta watumie fikira zao): “(Nyota) hii ni Mola wangu.” ilipotua (ikapotea), alisema (kuwaambia wale makaftri kama kwamba yupo pamoja nao katika ibada ile): “Sipendi waola wanaopotea (hawawepo ila wakati makhsusi tu).” 77. Na (usiku wa pili) alipouona mwezi unachomoza alisema (kuwaambia wale marafiki zake wa kikafiri): “Huu (mwezi) ndio Mola wangu.” Ulipotua alisema: “Asiponiongoza Mola wangu, bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu wapotofu (wapotevu). (Na mola huyu hawezi kuniongoza kwani anakuwa hayupo wakati mwengine).” 78. Na (siku ya tatu) alipoliona jua linachomoza alisema (kuwaambia): “Hili (jua) ndilo Mola wangu. Huyu Mola mkubwa kabisa.” Lilipotua alisema: “Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayoyashirikisha (na Mungu)., 79. “Mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimewacha dini za upotevu. Mimi (ni Mwislamu) si miongoni mwa washirikina.” 80. Na watu wake wakajadiliana naye (kwa kumwambia Unaacha ibada ya wazee! Utadhurika)! Akasema: “Je, Mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali yeye ameniongoa? Wala siogopi wale mnaowashirikisha naye. Isipokuwa Mola wangu akipenda jambo (kuwa, basi litakuwa). Mola wangu anakijua vyema kila kitu. Basi je, hamshiki mawaidha (Hamzindukani)?” 81. “Na nitawaogopaje hao mnaowashirikisha, bali nyinyi hamwogopi kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kile ambacho hakukiteremshia dalili kwenu (yo yote ya kuonyesha kuwa ni waungu)? 83. Na hizi ndizo (baadhi ya) hoja zetu tulizompa lbrahimu juu ya watu wake. Tunamyanyua katika vyeo yule tumtakaye (kwa kuwa anakwenda mwendo tunaoutaka). Hakika Mola wako ndiye Mwenye hikima(na) ndiye ajuaye
SHEREHE
Mazungumzo baina ya Nabii Ibrahim na Kaumu (Watu) yake yanatufahamisha hekima ya Kulingania Dini Ya Haki Yaani Dini ya Kumuamini Mungu Mmoja. Nabii Ibrahim Alianza Kuwauliza watu wake Maswali ya Hekima Kubwa. Kwanza Alipoona Nyota akawaambia watu wake waliokuwa Makafiri kwamba Nyota hiyo ni Mungu. Na Ilipopotea akawaambia Kwamba Haifai Nyota Kuwa Mungu kwani Imepotea na Haipo Daima. Siku ya Pili akaona Mwezi na Akawaambia Watu wake Kwamba Mwezi huo Ni Mungu na Ulipozama na Kupotea akasema Mwezi Siyo Mungu kwani haiwezekani Kuabudu Mungu alsiyekuwako Daima. Na siku ya Tatu alipoona Jua akawaambia watu wake kwamba Jua Ndiyo Mungu Mkubwa na Lilipotua na Kuzama akawaambia watu wake kwamba Haifai Jua Kuwa Mungu. Baada ya Kuwadokeza Mara Tatu na Baada ya kuwaonyesha kwamba Nyota au Mwezi au Jua hazistahiki kuwa Mungu akaona Bora awaeleze Ukweli kwamba Ameuelekeza uso wake kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa ameacha dini za upotevu. Akakiri kwamba yeye ni Mwislamu na si miongoni mwa washirikina. Na watu wake wakajadiliana naye kwa kumwambia kwamba kwa nini anaacha ibada ya wazee wake na atadhurika. Nabii Ibrahim akawajibu kwamba Haogopi chochote na Kwamba anayestahiki kuogopewa ni Mwenyeezi Mungu tu peke yake.
Haya ndiyo mazungumzo baina ya Nabii Ibrahim na Watu wake yalivyokwenda.
MAZUNGUMZO/DIALOGUE BAINA YA MWENYEEZI MUNGU NA NABII ISA
سُوۡرَةُ المَائدة
KURUANI:SURA YA ALMAIDAH
وَإِذۡ قَالَ ٱللَّهُ يَـٰعِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ ءَأَنتَ قُلۡتَ لِلنَّاسِ ٱتَّخِذُونِى وَأُمِّىَ إِلَـٰهَيۡنِ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالَ سُبۡحَـٰنَكَ مَا يَكُونُ لِىٓ أَنۡ أَقُولَ مَا لَيۡسَ لِى بِحَقٍّۚ إِن كُنتُ قُلۡتُهُ ۥ فَقَدۡ عَلِمۡتَهُ ۥۚ تَعۡلَمُ مَا فِى نَفۡسِى وَلَآ أَعۡلَمُ مَا فِى نَفۡسِكَۚ إِنَّكَ أَنتَ عَلَّـٰمُ ٱلۡغُيُوبِ (١١٦) مَا قُلۡتُ لَهُمۡ إِلَّا مَآ أَمَرۡتَنِى بِهِۦۤ أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ رَبِّى وَرَبَّكُمۡۚ وَكُنتُ عَلَيۡہِمۡ شَہِيدً۬ا مَّا دُمۡتُ فِيہِمۡۖ فَلَمَّا تَوَفَّيۡتَنِى كُنتَ أَنتَ ٱلرَّقِيبَ عَلَيۡہِمۡۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ شَہِيدٌ (١١٧) إِن تُعَذِّبۡہُمۡ فَإِنَّہُمۡ عِبَادُكَۖ وَإِن تَغۡفِرۡ لَهُمۡ فَإِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ (١١٨) قَالَ ٱللَّهُ هَـٰذَا يَوۡمُ يَنفَعُ ٱلصَّـٰدِقِينَ صِدۡقُهُمۡۚ لَهُمۡ جَنَّـٰتٌ۬ تَجۡرِى مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيہَآ أَبَدً۬اۚ رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنۡہُمۡ وَرَضُواْ عَنۡهُۚ ذَٲلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ (١١
SHEREHE
Nitasherehesha hivi karibuni mwenyeezi mungu akinipa nafasi na uzima inshaallah
MAZUNGUMZO/DIALOGUE BAINA YA MWENYEEZI MUNGU NA SHEITAN RAJIM
سُوۡرَةُ الحِجر
KURUANI SURA YA AL-HIJR
وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ إِنِّى خَـٰلِقُۢ بَشَرً۬ا مِّن صَلۡصَـٰلٍ۬ مِّنۡ حَمَإٍ۬ مَّسۡنُونٍ۬ (٢٨) فَإِذَا سَوَّيۡتُهُ ۥ وَنَفَخۡتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُواْ لَهُ ۥ سَـٰجِدِينَ (٢٩) فَسَجَدَ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةُ ڪُلُّهُمۡ أَجۡمَعُونَ (٣٠) إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰٓ أَن يَكُونَ مَعَ ٱلسَّـٰجِدِينَ (٣١) قَالَ يَـٰٓإِبۡلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّـٰجِدِينَ (٣٢) قَالَ لَمۡ أَكُن لِّأَسۡجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقۡتَهُ ۥ مِن صَلۡصَـٰلٍ۬ مِّنۡ حَمَإٍ۬ مَّسۡنُونٍ۬ (٣٣) قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡہَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ۬ (٣٤) وَإِنَّ عَلَيۡكَ ٱللَّعۡنَةَ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلدِّينِ (٣٥) قَالَ رَبِّ فَأَنظِرۡنِىٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ (٣٦) قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ (٣٧) إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡوَقۡتِ ٱلۡمَعۡلُومِ (٣٨) قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغۡوَيۡتَنِى لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمۡ فِى ٱلۡأَرۡضِ وَلَأُغۡوِيَنَّہُمۡ أَجۡمَعِينَ (٣٩) إِلَّا عِبَادَكَ مِنۡہُمُ ٱلۡمُخۡلَصِينَ (٤٠) قَالَ هَـٰذَا صِرَٲطٌ عَلَىَّ مُسۡتَقِيمٌ (٤١) إِنَّ عِبَادِى لَيۡسَ لَكَ عَلَيۡہِمۡ سُلۡطَـٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ (٤٢) وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ (٤٣) لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٲبٍ۬ لِّكُلِّ بَابٍ۬ مِّنۡہُمۡ جُزۡءٌ۬ مَّقۡسُومٌ (٤٤)
SHEREHE
Nitasherehesha hivi karibuni mwenyeezi mungu akinipa nafasi na uzima inshaallah