SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Elimu Ya Mirathi

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

ELIMU YA URITHI

UTANGULIZI

Mwenyeezi Mungu Ameelezea Sheria Za Urithi Katika Kuruani Tukufu ili Kutusaidia Katika Kugawanya Urithi na Pia Kuzuia Matatizo Yanayotokea Baada Ya Mtu Kufariki. Ili Kuondoa Ugomvi Na Kuleta Uadilifu Baina Ya Viumbe Vyake Inatubidi Tufate Sheria Hii. Mtume Mohamed (Sala na Amani Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Amehimiza Tuisome Elimu Hii. Hadithi Iliyokusanywa Katika Kitabu Cha Ibn Majjah Inasema Kwamba:

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ تَعَلَّمُوا الْفَرَائِضَ وَعَلِّمُوهَا فَإِنَّهُ نِصْفُ الْعِلْمِ وَهُوَ يُنْسَى وَهُوَ أَوَّلُ شَىْءٍ يُنْتَزَعُ مِنْ أُمَّتِي ‏”‏ ‏.‏

TAFSIRI YA HADITHI

Abu Hurayra Alisema “Mtume (Sala na Amani Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Amesema Ewe Abu Hurayra Soma Faradhi (Yaani Elimu Ya Urithi) Na Ufundishe Kwani Ni Nusu Ya Elimu. Kwani Itasahauliwa. Na Ndiyo Ya Kwanza Itakayoondolewa Katika Uma (Taifa) Langu (Yaani Taifa La Waislamu)

Kitabu: Sunan Ibn Majah  (Sunnah Ibn Majjah Ni Moja Ya Vitabu Sita Mashuhuri Vya Hadithi Za Mtume) Hii Ni Hadithi Inajyokadiriwa Kama Dhaifu. Mungu Najua Zaidi.

HATUA ZA KWANZA KABLA YA KUGAWA MALI YA URITHI

1/ Kwanza Kutaondolewa Gharama Za Mazishi na Hali Hii Inategemea Kama Aliyefariki aliacha Chochote na Kama Hakuacha Mali yoyote basi Ndugu Kama Wapo au Jamaa Watasaidia.

2/Pili Kutaangaliwa Gharama Za Madeni Ya Huyo Maiti na Hizi Zitaondolewa katika Mali Yake

3/Tatu Kutachunguzwa Iwapo Aliyefariki Kama Aliacha Wasia Wowote Katika Mali Yake Lakini isizidi Kiwango Cha 1/3 Na hii ni sawa na Mali Iliyogawanywa katika Mafungu Matatu Na Huo Wasiya Usizidi Fungu Moja Katika Haya Mafungu Matatu. Kwa Mfano Aliyefariki kama aliacha Shilingi 1500 basi Usia Usizidi Shilingi 500

Na Kitakachobaki Katika Mali Ya Aliyefariki Ndiyo Kitagawanywa Kwa Warithi Kufuatana Na Maamrisho Ya Mwenyeezi Mungu Kutoka Katika Kuruani Tukufu.

MASUALA YA ELIMU YA URITHI

1/SUALA LA KWANZA

Mume amefariki na ameacha Mke na Mtoto Mmoja wa Kiume Je Dini Ya Kiislamu Inatoa Fundisho Gani Katika Kugawanya Mali Kufuatana na Elimu Ya Urithi?

JAWABU

HESABU YA KWANZA KWA KUTUMIA UWIANO Kufuatana Na Kuruani Urithi Wa Mke Utakuwa 1/8 na Mtoto Wa Kiume atapata 7/8 Kwa Mfano Utagawa Mali katika Mafungu Manane Kisha Mke atapata Fungu Moja na Mafungu Mengine Saba Yaliyobaki atapewa Mtoto Wa Kiume. Kwa Mfano Wa Fedha tulioutaja Hapa Juu yaani Kama Maiti Aliacha Shilingi 1500 na Baada ya Kuondoa Gharama Za Usia, Madeni Na Mazishi Itabaki Shilingi 1000 basi Urithi Utakuwa Kama ifuatavyo. Utagawa Shilingi 1000 katika Mafungu 8 = 1000 Kugawa Kwa 8=125 Kwa Hiyo Mke Atapata Shilingi 125 na Mtoto Atapata Shilingi 875

HESABU YA PILI KWA KUTUMIA ASILIMIA (%)

Unaweza Pia Kugawa Kwa Kutunia Hesabu Ya Asilimia Kwa Mfano 1 Kugawa Kwa 8 Mara Asilimia 100 Ni sawa na 12.5% (1/8 X 100=12.5%) na 7 Kugawa Kwa 8 Mara Asilimia 100 Ni sawa Na 87.5 (7/8 X 100=87.5%) Na Ukitafuta Katika Fedha Shilingi 1000 Utapata 12.5/100 X 1000=125 na 87.5/1000 X 1000=875 Uchaguzi Ni wako Wa Hesabu Unayoona Rahisi. Ya Kwanza Kwa Kutumia Uwiyano au Ya Au Ya Pili Kwa Kutumia Asilimia Yaani %

Je Unaona Urithi Unavyogawiwa Katika Uislamu? Mwenyeezi Mungu Amejaalia Hivi Kwa Hekima Kubwa. Kwani Mtoto Wa Kiume Ndiye Anahitaji Mali Zaidi kwani Atakuwa Ana Familia Yake na Pia Atamwangalia Mama Yake.

USHAHIDI WA VIPIMO VYA HESABU ZA URITHI KUTOKA KATIKA KURUANI TUKUFU

Sura Ya Al-Nisaa Namba 4 Aya Namba 12

وَلَـكُمۡ نِصۡفُ مَا تَرَكَ اَزۡوَاجُكُمۡ اِنۡ لَّمۡ يَكُنۡ لَّهُنَّ وَلَدٌ ۚ فَاِنۡ كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَـكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡنَ​ مِنۡۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٍ يُّوۡصِيۡنَ بِهَاۤ اَوۡ دَ يۡنٍ​ ؕ وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡتُمۡ اِنۡ لَّمۡ يَكُنۡ لَّكُمۡ وَلَدٌ ۚ فَاِنۡ كَانَ لَـكُمۡ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكۡتُمۡ​ مِّنۡۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٍ تُوۡصُوۡنَ بِهَاۤ اَوۡ دَ يۡنٍ​ ؕ وَاِنۡ كَانَ رَجُلٌ يُّوۡرَثُ كَلٰلَةً اَوِ امۡرَاَةٌ وَّلَهٗۤ اَخٌ اَوۡ اُخۡتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنۡهُمَا السُّدُسُ​ ۚ فَاِنۡ كَانُوۡۤا اَكۡثَرَ مِنۡ ذٰ لِكَ فَهُمۡ شُرَكَآءُ فِى الثُّلُثِ مِنۡۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٍ يُّوۡصٰى بِهَاۤ اَوۡ دَ يۡنٍ ۙ غَيۡرَ مُضَآرٍّ​ ۚ وَصِيَّةً مِّنَ اللّٰهِ​ ؕ وَاللّٰهُ عَلِيۡمٌ حَلِيۡمٌ ؕ‏

TAFSIRI YA AYA 12.

Na nyinyi mtapata nusu ya (mali) walizoacha wake zenu, kama wao hawana mtoto (wala mjukuu). Na ikiwa wana mtoto (au mjukuu), nyinyi mtapata robo ya walivyoacha. Baada ya kutoa walivyousia au kulipa deni. Nao (wake zenu) watapata robo ya mlivyoacha, ikiwa hamna mtoto, ( wala mjukuu). Lakini ikiwa mnaye mtoto (au mjukuu), basi wao (hao wanawake) watapata thumni (sehemu ya nane) ya vile mlivyoacha. Baada ya kutoa mlivyousia au kulipa deni. Na kama mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto (wala mjukuu) wala wazazi, lakini anaye kaka (wa kwa mama) au dada (wa kwa mama pia), basi kila mmoja katika hawa atapata sudusi (sehemu ya sita). Na wakiwa zaidi kuliko hivyo basi watashirikiana katika thuluthi (sehemu ya tatu). Baada ya kutoa vilivyousiwa au kulipa deni, pasipo kuleta dhara. (Huu) ndio wasia uliotoka kwa Mwenyezi Mungu. na Mwenyezi Mungu Ni Mjuzi (na) Mwenye Upole.

USHAHIDI WA HADITHI YA MTUME (Sala na Amani Zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)

Hadithi kutoka katika Sahih al-Bukhari

 عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ “‏ أَلْحِقُوا الْفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا، فَمَا بَقِيَ فَهْوَ لأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ ‏”‏‏.‏

TAFSIRI

Hadithi Hii ameelezea  Ibn Abbas kwamba Mtume alisema “Wapeni Faradhi (Ni Vipimo (shares) Vya Urithi ambavyo vipo katika Kuruani Tukufu) Kwa wale ambao wanastahiki.(Entitled) Na chochote kitakachobaki apewe yoyote wa Kiume (male) ambaye ni karibu na aliyefariki dunia.

Kufuatana na Suala La Kwanza Nimepigia Msitari Jawabu lake. Mwenyeezi Mungu anasema Katika Aya Hii Kwamba Mtu Akifariki na Akamwacha Mke na Mtoto basi Mke atapata Sehemu Moja Ya Mafungu 8. Na kwa Vile Mtoto Ndiye Aliyebaki Pekee basi Atapata Urithi Wote Uliobakia Yaani Mafungu 7 kutoka Katika Mafungu 8. Nimefanya Hesabu Hapa Juu Na Natumai Imeeleweka. Allahu Akbar.

—————————

2/SUALA LA PILI

Mtu amefariki na ameacha Mtoto wa Kiume Mmoja na Watoto Wawili Wa Kike. Je Dini Ya Kiislamu Inatoa Fundisho Gani katika Kugawanya Mali Kufuatana na Elimu Ya Urithi?

JAWABU

HESABU YA KWANZA KWA KUTUMIA UWIANO

Kufuatana na Kuruani Urithi Wa Mtoto wa Kiume utakuwa 1/2 (Yaani Nusu Ya Urithi) na Watoto Wawili Wa Kike watapata Kila Mmoja 1/4 (Yaani robo ya Mali) Yaani Mtoto wa Kiume ambaye atakuwa na Jukumu Kubwa zaidi ya Watoto wa Kike atapata Mara Mbili ya Kila Ndugu zake Wa Kike Wawili.Kwa Mfano Wa Fedha tulioutaja Hapa Juu yaani Kama Maiti Aliacha Shilingi 1500 na Baada ya Kuondoa Gharama Za Usia, Madeni Na Mazishi Itabaki Shilingi 1000 basi Urithi Utakuwa Kama ifuatavyo. Utagawa Shilingi 1000 katika Mafungu 4 = 1000 Kugawa Kwa 4=250 Kwa Hiyo Mtoto Wa Kiume Atapata Shilingi 500 na Kila Mtoto Wa Kike atapata Shilingi 250. (Kufuatana na Kuruani Tukufu Mtoto wa Kiume atapata Mara Mbili Ya Kila mmoja wa Dada Zake Wawili.)

HESABU YA PILI KWA KUTUMIA ASILIMIA (%)

Unaweza Pia Kugawa Kwa Kutunia Hesabu Ya Asilimia Kwa Mfano 1 Kugawa Kwa 4 Mara Asilimia 100 Ni sawa na 25% (1/4 X 100=25%) na 1 Kugawa Kwa 2 Mara Asilimia 100 Ni sawa Na 50% (1/2 X 100=50%) Na Ukitafuta Katika Fedha Shilingi 1000 Utapata 25/100 X 1000=250 (Yaani Kila Mtoto Wa Kike atapata shilingi 250) na 50/100 X 1000=500 (Mtoto wa Kiume atapata Shilingi 500. Mara Mbili ya Kila Dada Katika Dada zake wawili) Uchaguzi Ni wako Wa Hesabu Unayoona Rahisi. Ya Kwanza Kwa Kutumia Uwiyano au Ya Au Ya Pili Kwa Kutumia Asilimia Yaani % Je Unaona Urithi Unavyogawiwa Katika Uislamu? Mwenyeezi Mungu Amejaalia Hivi Kwa Hekima Kubwa. Kwani Mtoto Wa Kiume Ndiye Anahitaji Mali Zaidi kwani Atakuwa ana Jukumu Zaidi.

USHAHIDI WA VIPIMO VYA HESABU ZA URITHI KUTOKA KATIKA KURUANI TUKUFU

Ushahidi Wa Kuruani Aya Namba 11 Sura Ya Al-Nisaa Namba 4

Hii Ni Sehemu Ya Aya Na siyo Kamili ambayo inahusika na Suala La pili

يُوصِيكُمُ ٱللَّهُ فِىٓ أَوۡلَـٰدِڪُمۡ‌ۖ لِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ‌ۚ

Tafsiri

Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu;mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili

USHAHIDI WA HADITHI YA MTUME (Sala na Amani Zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)

Hadithi Ya Mtume kutoka katika Vitabu va Jami` at-Tirmidhi vilivyokusanya hadithi za Mtume. Aliyeshughulikia kazi hii ni Imam Abu `Isa Muhammad at-Tirmidhi (Rehema Za Mwenyeezi Mungu Zimfikie).

حَدَّثَنَا عَبْدُ بْنُ حُمَيْدٍ، قال حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ سَعْدٍ، أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ أَبِي قَيْسٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْمُنْكَدِرِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ جَاءَنِي رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَعُودُنِي وَأَنَا مَرِيضٌ فِي بَنِي سَلِمَةَ فَقُلْتُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ كَيْفَ أَقْسِمُ مَالِي بَيْنَ وَلَدِي فَلَمْ يَرُدَّ عَلَىَّ شَيْئًا فَنَزَلَتْ ‏:‏ ‏(‏يُوصِيكُمُ اللَّهُ فِي أَوْلاَدِكُمْ لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الأُنْثَيَيْنِ ‏)‏ الآيَةَ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ ‏.‏ وَقَدْ رَوَاهُ شُعْبَةُ وَابْنُ عُيَيْنَةَ وَغَيْرُهُ عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْمُنْكَدِرِ عَنْ جَابِرٍ.‏

Tafsiri

Jabir bin ‘Abdullah alisema kwamba Mtume (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Imfikie) alinizuru wakati nilipokuwa naumwa katika Ukoo wa Banu Salamah. Nikasema; “Ewe Mtume wa Mwenyeezi Mungu (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Imfikie) Nitagawanya vipi mali yangu kwa watoto wangu? Hakunijibu mpaka Aya ifuatayo iliposhuka Aya Inayosema:

يُوصِيكُمُ ٱللَّهُ فِىٓ أَوۡلَـٰدِڪُمۡ‌ۖ لِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ

Tafsiri

Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu;mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili

IDADI YA WATOTO  WA KIUME AU KIKE INAPOBADILIKA

Hesabu tuliyotaja hapa Juu inahusu Mtoto mmoja wa kiume na watoto wawili wa kike. Lakini idadi yao inapozidi kama vile watoto wa kiume wawili na zaidi au wa kike watatu na zaidi basi Sheria ya Kuruani haibadiliki itakuwa vile vile kama tulivyoona katika suali la pili. Lakini Hesabu zitafanyika tofauti. Kwa mfano wakiwa watoto wa kiume wawili na wa kike watatu basi utagawa mali katika mafungu 7 kisha kila mtoto wa kiume atapata mafungu mawili na kila mtoto wa kike atapata fungu moja. Sheria ile ile ya kuruani kwani watoto wa kiume watapata mara mbili ya watoto wa kike. Kwa hiyo hesabu itakuwa kama ifuatavyo:

Kila mtoto wa kiume atapata mafungu mawili na kwa asilimia atapata 2/7 x100= 28.57%   kwa hiyo Jumla ya watoto wawili itakuwa 57.14%

Kila mtoto wa kike atapata fungu moja na kwa hesabu ya asilimia atapata 1/7 x 100=14.29 kwa hiyo Jumla ya mali ya  watoto watatu wa kike itakuwa 42.86%

na urithi wa shilingi 1000 utakuwa kila mtoto wa kiume atapata shilingi 285.7  

na kila mtoto wa kike  atapata shilingi 142.9

kwa hiyo  watoto wa kiume wawili itakuwa shilingi 285.7 x2 =571.4

na watoto wa kike watatu itakuwa shilingi  142.9 x3=428.6

na ukijumlisha shilingi  571.4 + 428.6=  shilingi 1000

Hivi ndivyo utakavyofanya namba ya watoto wa kiume au kike inapozidi.

3/SUALA LA TATU

Mtu amefariki na ameacha Mtoto wa Kike Mmoja na Dada Wawili Wa Kwa Baba na Mama. Je Dini Ya Kiislamu Inatoa Fundisho Gani katika Kugawanya Mali Kufuatana na Elimu Ya Urithi?

JAWABU

Kufuatana na Kuruani Urithi Wa Mtoto wa Kike utakuwa 1/2 au 2/3 (Yaani Nusu Ya Urithi), Yaani Mtoto wa Kike Urithi wake umedhibitiwa na Kuruani kuwa Nusu 1/2 au 2/3 lakini kuna masharti:

1/Mtoto Wa Kike atapata kipimo cha Nusu 1/2 iwapo atakuwa peke yake na maiti hakuacha watoto wa kiume. 2/Na atapata 2/3 iwapo kutakuwa na watoto wa kike zaidi ya mmoja. Na pia iwapo maiti hakuacha watoto wa kiume.

Kufuatana na Kuruani Urithi Wa Dada(Baba na Mama Mmoja) utakuwa 1/2 lakini kwa masharti:

1/Iwapo Aliyefariki ameacha Mtoto wa Kike Pekee. 2/Aliyefariki hana watoto na 3/Aliyefariki hana Kaka (Baba na Mama Mmoja). Na Urithi wake utakuwa 2.3 lakini kwa masharti:

1/Aliyefariki ameacha Zaidi ya Dada Mmoja    2/Aliyefariki hana watoto                                        3/Aliyefariki hana Kaka (Baba na Mama Mmoja)

HESABU YA KWANZA KWA KUTUMIA UWIANO Kufuatana na Shera ya Kuruani Urithi wa Mtoto wa kike utakuwa 1/2 Ya mali. Na Dada kufuatana na Sheria Hatakuwa Na kipimo chochote kwani Kuna Mtoto wa Kike wa Aliyefiwa. Kwa Hiyo atalachokipata na Masalia baada ya Mtoto wa Kike Kupewa sehemu yake.Kwa Hiyo 1/2 atapewa Mtoto wa Kike na Nusu Itakayobaki 1/2 watagaiana Madada Wawili yaani kila mmoja atapata Robo 1/4 ya mali.Kwa Mfano Wa Fedha Kama Maiti Aliacha Shilingi 1500 na Baada ya Kuondoa Gharama Za Usia, Madeni Na Mazishi Itabaki Shilingi 1000 basi Urithi Utakuwa Kama ifuatavyo. Utagawa Shilingi 1000 katika Mafungu Mawili. Mtoto wa Kike atachukuwa Fungu moja. Yaani Nusu 1/2 na Dada wawili wataiana Fungu lililobaki la Nusu 1/2 yaani kila mmoja atapata Robo 1/4.

HESABU YA PILI KWA KUTUMIA ASILIMIA (%)

Unaweza Pia Kugawa Kwa Kutunia Hesabu Ya Asilimia Kwa Mfano 1 Kugawa Kwa 4 Mara Asilimia 100 Ni sawa na 25% (1/4 X 100=25%) na 1 Kugawa Kwa 2 Mara Asilimia 100 Ni sawa Na 50% (1/2 X 100=50%) Na Ukitafuta Katika Fedha Shilingi 1000 Utapata 25/100 X 1000=250 (Yaani Kila Dada atapata shilingi 250 na Jumla ya Dada Wawili ni 250 X 2=500) na 50/100 X 1000=500 (Mtoto wa Kike atapata Shilingi 500).

Uchaguzi Ni wako Wa Hesabu Unayoona Rahisi. Ya Kwanza Kwa Kutumia Uwiyano au Ya Au Ya Pili Kwa Kutumia Asilimia Yaani % Je Unaona Urithi Unavyogawiwa Katika Uislamu? Mwenyeezi Mungu Amejaalia Hivi Kwa Hekima Kubwa.

USHAHIDI WA VIPIMO VYA HESABU ZA URITHI KUTOKA KATIKA KURUANI TUKUFU

Sura Ya Al-Nisaa Namba 4 Aya Namba 11

يُوصِيكُمُ ٱللَّهُ فِىٓ أَوۡلَـٰدِڪُمۡ‌ۖ لِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِ‌ۚ فَإِن كُنَّ نِسَآءً۬ فَوۡقَ ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَ‌ۖ وَإِن كَانَتۡ وَٲحِدَةً۬ فَلَهَا ٱلنِّصۡفُ‌ۚ وَلِأَبَوَيۡهِ لِكُلِّ وَٲحِدٍ۬ مِّنۡہُمَا ٱلسُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُ ۥ وَلَدٌ۬‌ۚ فَإِن لَّمۡ يَكُن لَّهُ ۥ وَلَدٌ۬ وَوَرِثَهُ ۥۤ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ ٱلثُّلُثُ‌ۚ فَإِن كَانَ لَهُ ۥۤ إِخۡوَةٌ۬ فَلِأُمِّهِ ٱلسُّدُسُ‌ۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٍ۬ يُوصِى بِہَآ أَوۡ دَيۡنٍ‌ۗ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ لَا تَدۡرُونَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ لَكُمۡ نَفۡعً۬ا‌ۚ فَرِيضَةً۬ مِّنَ ٱللَّهِ‌ۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمً۬ا (١١)

TAFSIRI

Mwenyeezi Mungu anakuusieni Juu ya watoto wenu; Mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili. Na ikiwa wanawake ni (wawili au)zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za (mali) aliyoiacha (maiti). Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi apewe nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi (sehemu ya sita) ya (mali) aliyoiacha (maiti), akiwa (maiti hiyo) anaye mtoto (au mjukuu). Lakini kama hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndiyo warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja (na baba thuluthi mbili). Na kama (Huyu Maiti) anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi (sehemu ya sita). Na huku kurithi kunakuwa baada ya kutoa aliyoyausia na kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu; Nyinyi hamjui ni nani miongoni mwao aliye karibu zaidi kukunufaisheni.(Hiyo) ni Sharia iliyotoka kwa Mwemyeezi Mungu. Bila shaka Mwenyeezi Mungu ni Mjuzi (na) Mwenye Hekima.

USHAHIDI WA HADITHI YA MTUME (Sala na Amani Zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)

Hadithi iliyopo kutoka Katika Vitabu Vya Sahih Al-Bukhari حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ خَالِدٍ،

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنِ الأَسْوَدِ، قَالَ قَضَى فِينَا مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم النِّصْفُ لِلاِبْنَةِ وَالنِّصْفُ لِلأُخْتِ‏.‏ ثُمَّ قَالَ سُلَيْمَانُ قَضَى فِينَا‏.‏ وَلَمْ يَذْكُرْ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏.‏

TAFSIRI

Mu’Adh bin Jabal alitupa Hukumu hii wakati Mtume (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikiye) alipokuwa hai. Nusu ya Urithi apewe Mtoto wa Kike na Nusu Kwa Dada.Suleiman Akasema: “Mu’Adh alitupatia Hukumu hii lakini hakutaja (matumizi) ya hukumu hii wakati wa uhai wa Mtume (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikiye” Mu`adh bin Jabal gave this verdict for us in the lifetime of Allah’s Messenger (ﷺ). One-half of the inheritance is to be given to the daughter and the other half to the sister. Sulaiman said: Mu`adh gave a verdict for us, but he did not mention that it was so in the lifetime of Allah’s Messenger (ﷺ).

SUALA LA NNE

Nitaendelea na Swala La Nne Hivi Karibuni Mungu Akipenda.

4/SUALA LA NNE

Mtu amefariki na ameacha Baba Mzazi na Kaka Wa Kwa Baba na Mama.Je Dini Ya Kiislamu Inatoa Fundisho Gani katika Kugawanya Mali Kufuatana na Elimu Ya Urithi?

JAWABU

Kufuatana na Kuruani Urithi Wa Baba atapewa Mali yote na Kaka yake yule Aliyefariki hatapata chochote.

USHAHIDI WA VIPIMO VYA HESABU ZA URITHI KUTOKA KATIKA KURUANI TUKUFU

Sura Ya Al-Nisaa Namba 4 Aya Namba 11

فَإِن لَّمۡ يَكُن لَّهُ ۥ وَلَدٌ۬ وَوَرِثَهُ ۥۤ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ ٱلثُّلُثُ‌ۚ فَإِن كَانَ لَهُ ۥۤ إِخۡوَةٌ۬ فَلِأُمِّهِ ٱلسُّدُسُ‌ۚ

TAFSIRI

Lakini kama hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja (Baba atapata theluthi mbili)

SHEREHE YA AYA

Baba anapokuwa peke yake basi atachukua mali yote peke yake na Kaka hatapata kitu. Kufuatana na Sheria za Urithi Baba atamzuia Kaka apate Urithi. (Father blocks FullBrother from receiving any share)

USHAHIDI WA HADITHI YA MTUME (Sala na Amani Zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)

Hadithi kutoka Katika Vitabu Vya Sahih Al-Bukhari na Muslim

SAHIH BUKHARI

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا ابْنُ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏ أَلْحِقُوا الْفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا فَمَا بَقِيَ فَهْوَ لأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ ‏”‏‏.‏

TAFSIRI

Hadithi Inatokana na Ibn Abbas inasema kwamba “Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Wapatieni Urithi (Faraidh zilizoelezwa katika kuruani Tukufu) kwa wale wanaostahiki kupata, na chochote kitakachobaki basi apewe yule ndugu wa kiume wa karibu (ukaribu wa damu) na Maiti.

English Translation

Allah’s Messenger (ﷺ) said, “Give the Fara’id (shares prescribed in the Qur’an) to those who are entitled to receive it; and whatever remains, should be given to the closest male relative of the deceased.’

SAHIH MUSLIM

حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، وَمُحَمَّدُ بْنُ رَافِعٍ، وَعَبْدُ بْنُ حُمَيْدٍ، – وَاللَّفْظُ لاِبْنِ رَافِعٍ – قَالَ إِسْحَاقُ حَدَّثَنَا وَقَالَ الآخَرَانِ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، أَخْبَرَنَا مَعْمَرٌ، عَنِ ابْنِ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏ اقْسِمُوا الْمَالَ بَيْنَ أَهْلِ الْفَرَائِضِ عَلَى كِتَابِ اللَّهِ فَمَا تَرَكَتِ الْفَرَائِضُ فَلأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ ‏”

TAFSIRI

Hadithi aliyosimulia Tawus ambayo inatokana na Ibn Abbas. (Radhi za Mwenyeezi Mungu Ziwafikie) Anasema Kwamba  Mtume Alisema ” Mgawanye Mali kwa watu wa Faraidh yaani kufuatana na kitabu cha Mwenyeezi Mungu na Cochote Kitakachobaki atapewa Mrithi wa Kiume aliyekuwa wa Karibu na maiti (Kwa Damu)

English Translation

Distribute the property amongst Ahl al-Fara’id, according to the Book of Allah, and what is left out of them goes to the nearest male heir.

4/SUALA LA TANO

Mtu amefariki na ameacha Mama Mzazi na Kaka Wa Kwa baba na mama.Je Dini Ya Kiislamu Inatoa Fundisho Gani katika Kugawanya Mali Kufuatana na Elimu Ya Urithi?

JAWABU

HESABU YA KWANZA KWA KUTUMIA UWIANO

Kufuatana Na Kuruani Urithi Wa Mama Utakuwa 1/3 na Kaka wa Kwa Baba na Mama Atapata 2/3 Kwa Mfano Utagawa Mali katika Mafungu Matatu Kisha Mama atapata Fungu Moja na Mafungu Mengine Mawili Yaliyobaki atapewa Kaka wa Kwa baba na Mama. Kwa Mfano Wa Fedha tulioutaja Hapa Juu yaani Kama Maiti Aliacha Shilingi 2000 na Baada ya Kuondoa Gharama Za Usia, Madeni Na Mazishi Itabaki Shilingi 1500 basi Urithi Utakuwa Kama ifuatavyo. Utagawa Shilingi 1500 katika Mafungu 3 = 1000 Kugawa Kwa 3=500 Kwa Hiyo Mama Atapata Shilingi 500 na Kaka Atapata Shilingi 1000

HESABU YA PILI KWA KUTUMIA ASILIMIA (%)

Unaweza Pia Kugawa Kwa Kutumia Hesabu Ya Asilimia Kwa Mfano 1 Kugawa Kwa 3 Mara Asilimia 100 Ni sawa na 33.33% (1/3 X 100=33.33%) na 2 Kugawa Kwa 3 Mara Asilimia 100 Ni sawa Na 66.66 % (2/3 X 100=66.66%) Na Ukitafuta Katika Fedha Shilingi 1500 Utapata 33.33/100 X 1500= Approximation 500 na 66.66%/100 X 1500=Approximation 1000 Uchaguzi Ni wako Wa Hesabu Unayoona Rahisi. Ya Kwanza Kwa Kutumia Uwiyano au Ya Au Ya Pili Kwa Kutumia Asilimia Yaani % Je Unaona Urithi Unavyogawiwa Katika Uislamu? Mwenyeezi Mungu Amejaalia Hivi Kwa Hekima Kubwa. Kwani Mtoto Wa Kiume Ndiye Anahitaji Mali Zaidi kwani Atakuwa Ana Familia Yake na Pia Atamwangalia Mama Yake.

USHAHIDI WA VIPIMO VYA HESABU ZA URITHI KUTOKA KATIKA KURUANI TUKUFU

Sura Ya Al-Nisaa Namba 4 Aya Namba 11

فَإِن لَّمۡ يَكُن لَّهُ ۥ وَلَدٌ۬ وَوَرِثَهُ ۥۤ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ ٱلثُّلُثُ‌ۚ فَإِن كَانَ لَهُ ۥۤ إِخۡوَةٌ۬ فَلِأُمِّهِ ٱلسُّدُسُ‌ۚ

TAFSIRI

Lakini kama hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja (Yaani 1/3 na Baba atapata theluthi mbili  2/3)

SHEREHE YA AYA

Mama atapewa sehemu yake ya Thuluth yaani 1/3 kama inavyosema Aya Ya Kuruani na Kinachobaki yaani 2/3 atapewa Kaka (Wa Damu)

USHAHIDI WA HADITHI YA MTUME (Sala na Amani Zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)

Hadithi kutoka Katika Vitabu Vya Sahih Al-Bukhari na Muslim

SAHIH BUKHARI

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا ابْنُ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏ أَلْحِقُوا الْفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا فَمَا بَقِيَ فَهْوَ لأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ ‏”‏‏.‏

TAFSIRI

Hadithi Inatokana na Ibn Abbas inasema kwamba “Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Wapatieni Urithi (Faraidh zilizoelezwa katika kuruani Tukufu) kwa wale wanaostahiki kupata, na chochote kitakachobaki basi apewe yule ndugu wa kiume wa karibu (ukaribu wa damu) na Maiti. English Translation Allah’s Messenger (ﷺ) said, “Give the Fara’id (shares prescribed in the Qur’an) to those who are entitled to receive it; and whatever remains, should be given to the closest male relative of the deceased.’

SAHIH MUSLIM

حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، وَمُحَمَّدُ بْنُ رَافِعٍ، وَعَبْدُ بْنُ حُمَيْدٍ، – وَاللَّفْظُ لاِبْنِ رَافِعٍ – قَالَ إِسْحَاقُ حَدَّثَنَا وَقَالَ الآخَرَانِ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، أَخْبَرَنَا مَعْمَرٌ، عَنِ ابْنِ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏ اقْسِمُوا الْمَالَ بَيْنَ أَهْلِ الْفَرَائِضِ عَلَى كِتَابِ اللَّهِ فَمَا تَرَكَتِ الْفَرَائِضُ فَلأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ ‏”

TAFSIRI

Hadithi aliyosimulia Tawus ambayo inatokana na Ibn Abbas. (Radhi za Mwenyeezi Mungu Ziwafikie) Anasema Kwamba Mtume Alisema ” Mgawanye Mali kwa watu wa Faraidh yaani kufuatana na kitabu cha Mwenyeezi Mungu na Chochote Kitakachobaki atapewa Mrithi wa Kiume aliyekuwa wa Karibu na maiti (Kwa Damu)

SHEREHE

katika suala namba 5 Mama atapewa Haki yake ya Thuluth yaani 1/3 kufuatana na Faraidh (zilizopo katika Kuruani) na Kinachobaki atapewa Kaka kwani huyo ndiyo pekee ambaye ni karibu na Maiti.

English Translation

Distribute the property amongst Ahl al-Fara’id, according to the Book of Allah, and what is left out of them goes to the nearest male heir.

Nitaendelea na Swala La Sita Hivi Karibuni Mungu Akipenda.