SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Elimu Ya Tawhiyd

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

ELIMU YA TAWHIYD التوحيد

Wanavtyuoni Wamegawa Elimu ya Tawhiyd التوحيد katika Mafungu Matatu.

1/ توحيد الربوبية   Yaani “Tawhiyd  Arububiyya” Maana yake Ni Kuamini  Vitendo Vya Mwenyeezi Mungu Peke Yake kama vile  Kuwa yeye peke yake ndiye aliyeumba ulimwengu au malimwengu, Yeye Peke yake ndiye aliyeumba. Yeye Peke yake ndiye anayeruzuku, Yeye peke yake ndiye anayefisha, Yeye peke yake ndiye anayeshusha Mvua na Mwengineyo ambayo Binaadamu au Kiumbe chochote kingine haliwezi kufanya. Kwa Kifupi Neno Rabi lina maana ya Mlezi. Mwenyeezi Mungu ndiyo Mlezi wetu na Ndiye anayeshughulikia maisha yetu.

2/توحيد الالوهية   Yaani “Tawhiyd Al-Uluhiyya”  Maana Yake Ni  Kuamini Kwamba Yeye Tu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa. Kuwa Na Imani Kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mmoja na Hana Mshirika. Vitendo Vyetu Vyote ni Kwa Ajili Yake. Neno Tawhiyd maana yake Kupwekesha yaani Kumpwekesha Mwenyeezi Mungu. Asili Ya Neno  TAWHIYD  kimaana ni maneno mawili  “Kitendo na Jina”.  Neno Tawhiyd Linatokana Na Kitendo  “Wahada” na Ukiligeuza na kilifanya TAWHIYD basi linakuwa Infinitive (Masdar) na Verb  Kwa Hiyo ni Kitendo na Jina Pamoja Yaani Noun and Verb (Infinitive word)

3/ توحيد الاسماء والصفات  Yaani “Attawhiyd Alasmaa Wa Swifaat.  Kumpwekesha Mwenyeezi Mungu katika Imani Ya Majina Na Sifa Zake. Hakuna Mwingine anayeitwa kwa  Majina au Sifa Hizo. 

Sura Ya Alfatiha

سُوۡرَةُ الفَاتِحَة

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (١) ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٢) ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (٣) مَـٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ (٤) إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ (٥) ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٲطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ (٦) صِرَٲطَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِمۡ غَيۡرِ ٱلۡمَغۡضُوبِ عَلَيۡهِمۡ وَلَا ٱلضَّآلِّينَ (٧)

Tafsiri

1-Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu Mwenye kuneemesh~ neema kubwa kubwa na M wenye kuneemesha neema ndogo ndogo.

2-Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mota wa walimwengu wote

3-Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo

4-Mwenye kumiliki siku ya malipo.

5-Wewe tu ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunayekuomba msaada.

6-Tuongoze njia iliyonyoka.

7-Njia ya wale uliowaneemesha; siyo (ya wale) waliokasirikiwa, wala (ya) wale waliopotea.

Kuna Hadithi na Aya Za Kuruani ambazo zinatumia ainaTatu Za Tawhiyd. Kwa Mfano Sura Ya Al-Fatiha Tutakuta Aina Tatu za Mgawanyiko huu  katika Sura Ya Al-Fatiha. Kama ifuatavyo:

katika Sura Ya Al-Fatiha tunakuta mfano Huu wa Kushangaza katika Aya 4  Zifuatazo.

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٢)

ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (٣)

مَـٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ (٤)

إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ (٥)

Aya Inayosema  

1: توحيد الربوبية:

لقوله تعالى: “الحمدلله رب العالمين”

3-توحيد الالوهية

: لقوله تعالى: “اياك نعبد واياك نستعين

توحيد الاسماء والصفات: لقوله تعالى: “الرحمن الرحيم”.

na مَـٰلِكِ يَوۡمِ ٱلدِّينِ (٤)

Katika Sura Ya Al-Fatiha Neno  “Mlezi” Yaani  Al-Rabbi limetumika Katika Aya Ya 2 Sura Ya Al-Fatiha Kama Neno “Mlezi” Yaani Tafsiri yake ni  “Mlezi wa Ulimwengu ambaye hana Shirika”.

Na Katika Aya Ya Pili Neno  “AL-Uluhiya” Limetumika Katika Aya Namba 5 Kwa Maana Ya Kuabudiwa Peke Yake. Yaani Ibada ifanyike kwa ajili Ya Mwenyeezi Mungu Peke yake kwani hana Mshirika. Yaani Neno Hili limetumika kwa Kusema  “Wewe Peke yako Ndiye Tunakuabudu na Tuna Kutegemea” Hapa Anastahiki Kupwekeshwa katika Ibada.

Katika Aya Namba 3 Sifa Zake Mwenyeezi Mungu Zinatajika Kwa Maana Ya “Ni Mwenye Rehema Kubwa Kubwa na Ndogo Ndogo”  Yaani Mwenyeezi Mungu peke yake ndiye Anastahiki kuwa na Sifa Kama Hizi na hakuna Mwingine. Na Katika Aya Namba 4 Imetumika Sifa ya Tatu ambayo ni  “Maliki” Yaani “Mfalme Wa Siku Ya Kiama” Na hizi sifa 3 Ni Miongoni mwa sifa Nyinginezo zinayojulikana kama Asmaa Al-husna na Ambayo Hastahiki kupewa Mwingine isipokuwa Peke Yake  Mwenyewe Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Na  Jumla Ya Sifa Zake ni 99

Mfano Wa Pili ambao tunakuta Sehemu Tatu Za Elimu Ya Al-Tawhiyd Yaani  Al-Rububiya, Al-Uluhiya Na Al-Asmaa Al-husna ni Katika Aya Ifuatayo Kutoka katika Sura Namba 19 Aya Namba 65

رَّبُّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَہُمَا فَٱعۡبُدۡهُ وَٱصۡطَبِرۡ لِعِبَـٰدَتِهِۦ‌ۚ هَلۡ تَعۡلَمُ لَهُ ۥ سَمِيًّ۬ا

Tafsiri

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu yeye tu na udumu katika ibada Yake. Je, unamjua (mwingine) mwenye jina lake(Mwenyezi Mungu, aliye kama yeye)?

Neno  رَّبُّ  Yaani limetumika kwa maana ya Al-Rububiya kwa maana ya Mlezi,  Ibara  فَٱعۡبُدۡهُ وَٱصۡطَبِرۡ لِعِبَـٰدَتِهِ limetumika kama  Al-Ulihiyya Yenye Maana ya Kumpwekesha katika ibada na Uvumilivu na  Na Ibara هَلۡ تَعۡلَمُ لَهُ ۥ سَمِيًّ۬ا  Linahusu  Sifa Zake Mwenyeezi Mungu. Yaani Majina Yake 99 ambayo hakuna Mwingine anyestahiku kuitwa kwa Majina au Sifa Hizi

MUUJIZA KATIKA TAWHIYD AL-ULUHIYA توحيد الالوهية

NABII ISA (YESU) NI KAMA  NABII ADAM

Kama tulivyosema kwamba توحيد الالوهية “Tawhiyd Al-Uluhiyya” Maana Yake Ni Kuamini Kwamba Yeye Tu peke yake ndiye anayestahiki kuabudiwa. Tutatoa Mfano wa Wale ambao wanakwenda kinyume na Imani Ya Mungu mmoja. Kwa Mfano Wanaodai kwamba Nabii Isa (Yesu) ni Mtoto wa Mwenyeezi Mungu au Mungu Mwenyewe. Uislamu unakataa itikadi hiyo ambayo inajulikana katika dini ya kikristo kama Trinity. (Jina la baba na la mwana na la Roho Mtakatifu). Kuruani inatuthibitishia kwa Miujiza na Maelezo yenye mifano mbalimbali kuhusiana na itikadi zisizo sahihi.Kuna Miujiza  mbalimbali katika kuruani ambayo inathibitisha kwamba Mwenyeezi Mungu ni pekee na hana mshirika, Hakuzaa wala hakuzaliwa na wala hakuna anayefanana naye. Katika mlango huu nitazungumzia muujiza wa Ajabu sana. Kuruani inatuonyesha tena Maajabu yake katika kupambana na itikadi zisizo sahihi.

Katika kupinga itikadi hii Mwenyeezi Mungu amemsawazisha Nabii Isa (Yesu) Na Nabii Adam. Katika Aya Ifuatayo:

(إِنَّ مَثَلَ عِيسَى عِنْدَ اللَّهِ كَمَثَلِ آَدَمَ خَلَقَهُ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ)

[آل عمران: 59].  Sura Ya Imran Aya Namba  59

Mwenyeezi Mungu anasema katika Aya Hii Kwamba Kwa hakika Mfano wa Nabii Isa Kwa Mwenyeezi Mungu Ni Mfano wa Nabii Adam ambaye amemuumba kutokana na Udongo kisha akamwambia “Kuwa na Akawa” 

Mwenyeezi Mungu anapinga itikadi za binaadamu ambazo ni potovu zenye kudai kwamba Nabii Isa ni Mtoto wa Mungu au Mungu Mwenyewe kwa kusema katika Aya Hii kwamba Mfano wa Kuumbwa kwa  Nabii Isa ni sawa sawa na kuumbwa kwa  Nabii Adam ambao wote waliumbwa kwa udongo. Wenye kudai kwamba Nabii Isa anastahiki kuwa Mungu au Mtoto wa Mungu kwa sababu alikuwa hana baba basi  Nabii Adam atastahiki zaidi kuwa na sifa hizo kwani aliumbwa bila kuwa na Baba na Mama. Kwa hiyo tunakatazwa tusifuate Itikadi hii ambayo ni ya upotovu mkubwa. Ni Kumpa Mwenyeezi Mungu sifa asiyostahiki.  

MUUJIZA KATIKA MATUMIZI YA JINA LA NABII ISA NA ADAM KATIKA KURUANI TUKUFU

Aya zinazofuata zinashangaza sana na Muujiza mkubwa. 

Jina la Nabii Isa (Yesu) Limetajika katika Kuruani Mara 25  na Jina La Nabii Adam limetajika katika Kuruani mara 25 Pia!!! Hebu tuone haya maajabu. Katika Mpangilio huu Mwenyeezi Mungu anamsawazisha Nabii Isa (Yesu) Na Nabii Adam kwa njia ya Namba pia. Yaani kututhibitishia kwamba wote wawili ni sawa kwani wote ni binaadamu na wote waliumbwa kwa udongo na haiwezekani nabii Isa (Yesu) Kustahiki sifa ya kuwa Mtoto wa Mungu au Mungu Mwenyewe.  Na kwa hivyo hata kutajika kwao katika kuruani ni sawa pia yaani Jina Isa limetajika mara 25 na Jina Adam limetajika mara 25 pia!!!  Allahu Akbar.  Nimekusanya Aya hizo hapa chini.

Aya Zifuatazo zimetaja Jina La Nabii Adam mara 25

1- وَعَلَّمَ آَدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا

2- قَالَ يَا آَدَمُ أَنْبِئْهُمْ بِأَسْمَائِهِمْ

3- وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآَدَمَ

4- وَقُلْنَا يَا آَدَمُ اسْكُنْ أَنْتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ

5- فَتَلَقَّى آَدَمُ مِنْ رَبِّهِ كَلِمَاتٍ

6- إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَى آَدَمَ

7- إِنَّ مَثَلَ عِيسَى عِنْدَ اللَّهِ كَمَثَلِ آَدَمَ

8- وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ ابْنَيْ آَدَمَ بِالْحَقِّ

9- ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآَدَمَ

10- وَيَا آَدَمُ اسْكُنْ أَنْتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ

11- يَا بَنِي آَدَمَ قَدْ أَنْزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا

12- يَا بَنِي آَدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ

13- يَا بَنِي آَدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِنْدَ كُلِّ مَسْجِدٍ

14- يَا بَنِي آَدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِنْكُمْ

15- وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِنْ بَنِي آَدَمَ

16- وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآَدَمَ

17- وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آَدَمَ

18- وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآَدَمَ

19- مِنْ ذُرِّيَّةِ آَدَمَ

20- وَلَقَدْ عَهِدْنَا إِلَى آَدَمَ

21- وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآَدَمَ

22- فَقُلْنَا يَا آَدَمُ إِنَّ هَذَا عَدُوٌّ لَكَ

23- فَوَسْوَسَ إِلَيْهِ الشَّيْطَانُ قَالَ يَا آَدَمُ

24- وَعَصَى آَدَمُ رَبَّهُ فَغَوَى

25- يَا بَنِي آَدَمَ أَنْ لَا تَعْبُدُوا الشَّيْطَانَ

Aya Zifuatazo zimetaja Jina La Nabii Isa (Yesu) mara 25 Pia!!!

1- وَآَتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ

2- وَمَا أُوتِيَ مُوسَى وَعِيسَى

3- وَآَتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَاتِ

4- اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ

5- فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَى مِنْهُمُ الْكُفْرَ

6- يَا عِيسَى إِنِّي مُتَوَفِّيكَ

7- إِنَّ مَثَلَ عِيسَى عِنْدَ اللَّهِ كَمَثَلِ آَدَمَ

8- وَمَا أُوتِيَ مُوسَى وَعِيسَى

9- وَقَوْلِهِمْ إِنَّا قَتَلْنَا الْمَسِيحَ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ

10- وَعِيسَى وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ

11- إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّهِ

12- وَقَفَّيْنَا عَلَى آَثَارِهِمْ بِعِيسَى

13- عَلَى لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ

14- إِذْ قَالَ اللَّهُ يَا عِيسَى

15- إِذْ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ يَا عِيسَى

16- قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ

17- وَإِذْ قَالَ اللَّهُ يَا عِيسَى

18- وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَى وَعِيسَى

19- ذَلِكَ عيسَى ابْنُ مَرْيَمَ

20- وَمُوسَى وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ

21- إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَى وَعِيسَى

22- وَلَمَّا جَاءَ عِيسَى بِالْبَيِّنَاتِ

23- وَقَفَّيْنَا بِعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ

24- وَإِذْ قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ

25- كَمَا قَالَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ

Kutokana na Aya Hizi tunaona Miujiza Ifuatayo yenye kushangaza sana.

1-Muujiza wa Kwanza

Jina la Nabii Isa limetumika katika Kuruani mara 25 na Nabii Adam Pia mara 25 yaani Usawa wa kutajika unaonyesha usawa wa kuwa wote wawili ni Binaadamu yaani wote wawili wameumbwa kwa udongo na haiwezekani Nabii Isa kuwa Mwenyeezi Mungu au mtoto wa Mwenyeezi Mungu.

2-Muujiza wa Pili

katika kutajika kwa majina yote mawili Nabii Isa  na Nabii Adam  katika Aya Namba 7 ( Angalia Aya Namba 7 Hapa Juu Katika Mafungu yote mawili ya Nabii Isa na Adam) Kwa kweli hii ni Muujiza Mkubwa. Hii Inathibitisha Kwamba Kuruani siyo maneno ya Binaadamu. Mwenyeezi Mungu ameumba mbingu kwa siku 7 kama alivyosema katika kuruani Tukufu na kama alivyosema kwamba Kuumbwa kwa  Ulimwengu ni Jambo kubwa zaidi kuliko Binaadamu. Ukichunguza Aya Hizi utaona  Mwenyeezi Mungu anatuambia kwamba ameweza kuumba  mbingu na ardhi kwa siku 7 na ambazo kubwa zaidi na kwa hiyo hatashindwa kuwaumba Nabii Isa na Adam kwa udongo kwa kusema  “Kun Fa Ya Kun”

كُنْ فَيَكُونُ Yaani  “Kuwa na Itakuwa” na Kwa hiyo haiwezekani yeye kuwa na Mshirika yeyote. Na Nabii Isa na Adam ni Watu kama kawaida isipokuwa walizaliwa kwa njia aliyotaka Mwenyeezi Mungu Mwenyewe. Nabii Isa alikuwa hana Baba na Nabii Adam alikuwa hana Baba na Mama. Mwenyeezi Mungu anafanya atakavyo. Allahu Akbar.

3-Muujiza wa Tatu 

Aya ya 7  katika mfululizo wa Aya 25  zinazozungumzia Nabii Isa na Nabii Adam ni Aya Namba 59  Sura Namba 3  Inayoitwa  Al-Imran. Huyu alikuwa baba yake  Maryam Na Maryam ni mama yake Nabii Isa (Yesu). Aya Ya 19 katika Aya 25 zinazozungumzia Nabii Isa ni Aya Namba 34 Ya Sura Ya Maryam  na Aya ya 19 katika Aya 25 zinazozungumzia Nabii Adam ni Aya Namba 58 katika Sura Ya Maryam. Na Ajabu Ni Kwamba Sura Ya Maryam ni Ya 19. Je unaona Maajabu. Kama Nilivyozumgumzia kuhusu Muujiza wa namba 19. Mwenyeezi Mungu alisema katika Sura Ya Al-Mudathir kwamba namba 19 Ni Muujiza Mkubwa. Hii Namba Ni Muujiza wa kuwazidishia  imani Waumini, kuwarudisha waliopotea na Kuwavutia Makafiri wakubali Uislamu. Kama tunavyoona hapa Aya ya 19  inazungumzia Nabii Isa na Nabii Adam na Sura hiyo ni Namba 19 Pia!! Na La Kushangaza zaidi ni Kwamba Katika Sura Ya Maryam KIsa Cha Nabii Isa na Mama Yake kimetajwa katika Jumla Ya Aya 19 Tu!!! yaani kuanzia Aya Namba 16 mpaka Aya namba 34 ya Sutra Ya Maryam.  Allahu Akbar. Kwa kweli hii inathibitisha kwamba kuruani siyo maneno ya Binaadamu hata kidogo. Tusijidanganye. Haya ni maneno ya Mola Mtukufu aliyeumba Ulimwengu. Kwa kifupi. Ukihesabu Majina Ya Nabii Isa na Nabii Adam kuanzia Mwanzo wa Kuruani Tukufu Yaani Kuanzia Al-Fatiha mpaka Sura Ya Maryam Utakuta Nabii Isa Ametajika mara 19  kuanzia Mwanzo wa kuruani mpaka Aya namba 34 Ya Sura Ya Maryam. Na Nabii Adam pia Ametajika Mara 19 Kuanzia Mwanzo wa Kuruani Mpaka Aya namba  58 Sura Ya Maryam. Na la Kushangaza ni kwamba Sura Ya Maryam ni Namba 19  na Aya zenye kuzungumzia Maisha Ya Nabii Isa na Mama Yake Yaani Maryam ni Aya 19 Tu peke yake. Sasa tunaona Muujiza wa namba 19. Na Kama Ilivyoelezwa katika Sura Ya Al-Mudathir kwamba Namba 19 ni Namba iliyojaaliwa na Mwenyeezi Mungu ili iwe Muujiza Mkubwa kwa Binaadamu. Kuwarudisha waliopotea, Kuwaongoza katika Uislamu wasiokuwa Waislamu na Kuwazidishia Imani Waumini.

إِنَّ مَثَلَ عِيسَى عِنْدَ اللَّهِ كَمَثَلِ آَدَمَ خَلَقَهُ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ

Huenda Kuna hekima nyingine kwa Mwenyeezi Mungu kutumia Jina La Nabii Isa katika Aya Hii na halikutumika Jina lingine kama vile Masihi ibn Maryam, au Isa Ibn Maryam ni Muujiza wa Kuzaliwa kwake. Fertilisation ilikuwa bado kufanyika na Sperms (Tonye la baba) Haikuweko. Kwa hiyo Aya Hii Imetumia Isa peke yake kwani Inazungumzia Kuumbwa kwa Nabii Isa na Nabii Adam. Kabla Ya Fertilisation kufanyika ilikuwa bado hajawa mtoto wa  Maryam. 

4-Mjuujiza Wa Nne.

Hesabu ya Kushangaza ni kwamba Katika Sura Ya Maryam kuanzia Jina Nabii Isa Katika Aya Namba 34 mpaka Jina Adam Aya namba 58 Kuna maneno 268 (Maneno yaliyohesabiwa na Wanavyuoni ni 268 na kuna wengine wanatupa hesabu nyinginezo. Hii inatokana na Visomo mbali mbali vya kuruani na Misahafu tuliyonayo maandishi yake yanatofautiana na Msahafu wa Mwanzo katika Karne ya 7) Ikiwa Hesabu hii Ni  sahihi na ni 268 basi namba hii ni sawa na  22 X 13.  Na Ajabu ya kushangaza ni Kwamba Manabii waliotajwa katika Sura Ya Maryam ni  13 na Kukariri kwa majina Yao katika Sura Ya Maryam ni mara 22. Kwa kweli inashangaza. Majina Ya Manabii hawa 13 ni kama yafuatavyo

(Zakaria, Yahya , Maryam, Isa, Ibrahim Ishaaq, Yaakub, Musa, Harun, Ismail, Idris, Adam Na Noah)

Na Kukariri katika matumizi ni kama ifuatavyo:

(Zakaria Mara 2, Yahya Mara 2, Maryam Mara 3, Isa Mara 1, Ibrahim Mara 3, Ishaaq Mara 1, Yaakub Mara 3, Musa Mara 1,Harun Mara 2, Ismail Mara 1,Idris Mara 1,Adam Mara 1,Na Noah Mara 1)

Idadi ya Majina na Kukariri Kwao kunalingana na namba  13 X 22 ambayo ni maneno baina na Nabii Isa na Adam.

5-Muujiza Wa Tano

Baina Ya Jina Nabii Isa katika Aya Namba 34 na Jina Nabii Adam katika Aya Namba 58  kuna Aya  25.  Na ajabu ni Kwamba Namba  25  Inaasshiria Mara 25 kutajwa kwa Nabii Isa na Mara 25 Kutajwa kwa Nabii Adam.  Allahu Akbar.  Muujiza Mbele ya Macho yetu. Allahu Akbar. Yaani Wote wawili ni sawa katika Kuumbwa kwa Udongo. Na wala haiwezekani Nabii Isa kuwa Mtoto wa Mungu au Mungu Mwenyewe. Allahu Akbar. Namba Zinazungumza. Allahu Akbar. Muujiza Siyo Mdogo.

6-Muujiza Wa Sita

إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ ٱللَّهِ كَمَثَلِ ءَادَمَ‌ۖ  

Kipande cha Aya Hii Inayosema Kwamba Mfano wa Nabii Isa ni Sawa na Mfano wa Adam  Ni kutoka katika Aya Namba 59  Sura Ya Maryam. Na ni kipande cha Aya Ya  7 kuanzia Mwanzo wa Kuruani. (Ni Aya Ya Saba katika Zile Aya 25 Zinazowataja Nabii Musa na Isa). La kushangaza zaidi ni Kwamba Kipande cha Aya kina Idadi ya Maneno 7 pia kama nilivyopanga hapa chini. Allahu Akbar. Mpangilio wa Ajabu. Allahu Akbar.

إِنَّ / مَثَلَ /عِيسَىٰ /عِند  /ٱللَّهِ  /كَمَثَلِ  /ءَادَمَ‌ۖ 

Herufi Pia Zipo saba katika Ibara 3 za Kipande hiki kama ifuatavyo

إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ  =  Herufi  7 nazo ni Alif, Nun, Mim, Tha, Lam, A’in, Sin (Tafsiri  “Kwa Hakika Mfano wa Isa)

عِندَ ٱللَّهِ= Herufi 7 Nazo ni A’in, Nun, Dal, Alif, Lam Zipo mbili ba Haa (Tafsiri  “Kwa Mwenyeezi Mungu”)

كَمَثَلِ ءَادَمَ‌ۖ= Herufi 7 nazo ni  Kaf, Mim, Tha, Lam, Hamza, Dal na Mim (Tafsiri “Ni Mfano wa Adam”).

ثُمَّ قَالَ لَهُ= Herufi 7  Nazo Ni   Tha, Mim, Qaf, Alif, Lam, Lam Ya Pili Na Ha(Tafsiri “Kisha Akamwambia)

كُنْ فَيَكُونُ= Herufi 7  Nazo ni  Kaf, Nun, Fa, Ya, Kaf, Waw, na Nun (Tafsiri  ” Kuwa na Ikawa”

—————————————–

7-Muujiza Wa 7

إِنَّ مَثَلَ عِيسَى عِنْدَ اللَّهِ كَمَثَلِ آَدَمَ خَلَقَهُ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ

-Katika Aya Hii Jumla Ya Idadi Ya Herufi za Neno مَثَلَ  na Neno كَمَثَلِ  ni 7 

-Aya Hii Ipo katika Sura Ya Al-Imran ambayo Herufi zake ni 7 (آل عمران  Ina herufi  7  Alif + Lam + A’in + Mim + Ra + Alif + Nun) 

-Neno la Kwanza katika Aya Hii ni إِنَّ na lina herufi 2 na Neno la Mwisho katika Aya Hii ni  فَيَكُونُ  lina herufi 5 Na ukijumlisha unapata 7

-Mwenyeezi Mungu amemuumba Adam kwa udongo na ukihesabu Jina la Adam na Udongo utapata Jumla 7 kama ifuatavyo; Adam  آدم  +    Udongo   تراب    Jumla ya Herufi ya haya maneno mawili ni 7 (Alif + Dal + Mim + Ta + Ra + Alif + Ba)

-Jina آدم  lina herufi  3  na Neno خَلَقَهُ  Lina herufi 4. Jumla Ni Herufi 7

-Aliyeamrisha Kuumbwa kwa Adamu Ni Mwenyeezi Mungu kwa Hiyo ni  الله  na neno  قال  yaani Alisema Kutoka katika Aya hapa Juu. Jumla ya  Herfufi za Haya maneno mawili ni 7

Angalia Mpangilio wa kiajabu. Namba 7 Mwenyeezi Mungu ameipa utukufu sana. Mbingu ameziumba 7, Matabaka Ya Ardhi yameumbwa 7, Hija Tawaf ni mara 7, Safwa wal Marwa ni mara 7, Vijiwe vinavyotumika kumpigia \Sheitani huko Hijja Jumla yake ni 7 Kwa kweli haina mwisho. Namba 7 katika Aya hii imekariri kiajabu sana. Allahu Akbar.

Na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akasema katika Sura Ya Al-Bakarah Aya 23-24 kwamba

وَإِنْ كُنْتُمْ فِي رَيْبٍ مِمَّا نَزَّلْنَا عَلَى عَبْدِنَا فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِنْ مِثْلِهِ وَادْعُوا شُهَدَاءَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ * فَإِنْ لَمْ تَفْعَلُوا وَلَنْ تَفْعَلُوا فَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ) [البقرة: 23-24].

Kwamba sisi binaadamu hatuwezi kamwe kuandika kitabu mfano wa kuruani Tukufu na hata Tukikusanyika wote hatutaweza.

Na Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) amesema pia kwamba Kuruani haiishi kutoa ya kushangaza.  ولا تنقضي عجائبه

IPO KATIKA MAANDALIZI. NITAENDELEA BAADAYE MUNGU AKIPENDA. ALHAMDULILAH. ALLAHU AKBAR.