SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Elimu Za Kiislamu

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

ELIMU MBALIMBALI

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Bismillahi Arrahmani Arrahiiim

Kwa jina la mwenyeezi mungu mwenye neema kubwa kubwa na ndogo ndogo

Baada ya kutaja jina la mwenheezi mtukufu na baada ya kutaja neema zake kubwa na ndogo nitaanza kazi ya kuelezea Elimu mbalimbali ambazo zinahitajika katika kisomo cha kuruani. Kazi hii siyo rahisi kwani uwanja wa elimu hizi ni mkubwa na inahitajia utafiti wa hali ya juu, na kwa wakati huo huo kujiepusha na makosa na pia kurahisisha maandishi yasiwe magumu kwa wasomaji wa kawaida na wanavyuoni.

TAFSIRI YA NENO  “QURAN” KILUGHA NA KATIKA DINI

Neno kuruani kilugha maana yake ni Kisomo Na katika dini ya kiislamu linatumika kwa ujumbe aliopewa mtume Mohamed (Sala na Amani zimfikie) kwa njia ya kusomewa na Malaika (Jibril) kwa naye akahifadhi na kisha akafikisha ujumbe huo kwa kusoma. Kwa hiyo neno hili lina maana ya kitendo cha kusoma.

Baada ya Mtume kufariki na Maswahaba waliohifadhi kuruani wengi wao kufariki katika vita vilivyo tokea wakati wa kulingani dini (vita vya Yamama walifariki wahifadhi wengi sana wa kuruani)Omar Ibn Alkhatab akamshauri Amiri mkuu Abu Bakar Asadik afanye juhudi ya kukusanya na kuihifadhi kuruani kwa njia ya maandishi kabla ya kupotea. Mwanzoni Abu Bakar Asadik hakukubali kufanya jambo ambalo Mtume hajalifanya lakini aliridhia  mwishoni baada ya Omar kusisitiza na kumfahamisha umuhimu wa jambo hilo. 

Kazi ikaanza kwa juhudi za bwana Zaid Ibn Thabit ya kukusanya kuruani kutokana na maandishi yalioandikwa katika vitu mbali mbali wakati huo kama vile ngozi au mifupa na pia kwa msaada wa Maswahaba ambao walijulikana sana kwa hifadhi zao nzuri.

Kuruani ilihifadhiwa na Omar Ibn Al-Khatab mwenyewe na alipofariki ilihifadhiwa na mtoto wake wa kike “Hafsa”. Ili kuepusha tatizo la visomo mbalimbali vinavyotokana na tofauti za “Quranic Dialects”  au “Lahajaat za Kuruani”  kiongozi |Amir bwana Othman akaamuamrisha Zaid bn Thabit pamoja na Swahaba watatu kutayarisha nakala moja iliyoandikwa kwa kutumia lahaja moja maarufu (kikureishi) na kuacha nyinginezo.Kisha kueneza nakala hiyo katika mikoa mbalimbali ya taifa la kiislamu katika wakati huo. Nakala ya asili ilirudishwa kwa Hafsa na nyingineyo kwa Uthman ibn Afan.

Ijapokuwa kuruani ya leo tunaisoma katika misahafu lakini asili yake ya kisomo kwa moyo bila msahafu upo hai kama vile tunapokuwa katika sala tunaisoma kuruani bila misahafu na pia katika vikao mbalimbali.

Kuruani ni muujiza mkubwa usio mfano, Herufi, maneno na Ayaat zote ni muujiza

Kwa hiyo  Kuruani ni ujumbe ulioshushwa kwa mtume Mohamed (Sala na Amani za Mola Zimfikie) Naye akauhifadhi ujumbe huo bila kubadili herufi,maneno au Aya hizo. Na ujumbe huo ukafikishwa kwetu kama alivyopewa bila badiliko lolote. Na mwenyeezi aliahidi kuutunza ujumbe huo na badiliko lolote mpaka mwisho wa ulimwengu au atakapotaka kwenyewe.

TAFSIRI YA NENO “HADITHI” KILUGHA NA KATIKA DINI YA KIISLAMU

Kilugha neno “hadithi” lina maana ya maelezo au jambo au tukio jipya. Na katika elimu ya dini ya kiislamu lina maana ya jambo au tukio linalohusiana na vitendo alivyovifanya  Mtume Mohamed (Amani na Sala za Mola zimfikie) Mazungumzo, Kukiri kwa moyo wake kwa tendo la mtu mwingine na pia mazungumzo au habari za sifa zake ambazo zilitajwa na kudawiniwa.

Mfano wa Hadithi iliyokusanywa Imam Bukhari ni

حَدَّثَنَا الْحُمَيْدِيُّ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الزُّبَيْرِ، قَالَ حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، قَالَ حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الأَنْصَارِيُّ، قَالَ أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيُّ، أَنَّهُ سَمِعَ عَلْقَمَةَ بْنَ وَقَّاصٍ اللَّيْثِيَّ، يَقُولُ سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ ـ رضى الله عنه ـ عَلَى الْمِنْبَرِ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ “‏ إِنَّمَا الأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى، فَمَنْ كَانَتْ هِجْرَتُهُ إِلَى دُنْيَا يُصِيبُهَا أَوْ إِلَى امْرَأَةٍ يَنْكِحُهَا فَهِجْرَتُهُ إِلَى مَا هَاجَرَ إِلَيْهِ ‏”‏‏.‏

Hadithi hii iliyotokana na Omar Ibn Alkhatab inasema kwamba bwana Omar alimsikia mtume (Sala na Amani zake Mola zimfikie) akisema “Vitendo vyote vinaambatana na nia, kila mtu na nia yake, Na ikiwa mtu alinuia kuhama mji au nchi kwa ajili ya dunia kama vile kutafuta riziki au kwa ajili ya kuoa mke basi ujira wake utalipwa kufuatana na nia yake”

Kwa hiyo Hadithi pia ni mafundisho kutoka kwa mwenyeezi mungu kwa njia ya vitendo vyake mtume, Au kukiri kwake kwa vitendo vya maswahaba, au maswali aliyoulizwa na maswahaba, lakini maneno yaliyotumika katika kutufikishia ujumbe huo ni yake Mtume Mohamed (Amani na Sala Za Mwenyeezi Mungu Zimfikie).

TAFSIRI YA NENO “AL-HADITH -AL-KUDSIY” KILUGHA NA KATIKA DINI YA KIISLAMU

Neno hili kilugha lina maana ya Maelezo Matakatifu na Kidini ya kiislamu lina maana ya Malezo yaliyotajwa na mwenyeezi mungu na Mtume akatufikishia maelezi hayo kwa kutumia lugha yake mwenyewe. Mfano wa Al-Hadith Alkudsiy ni;   

قَالَ اللَّهُ أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ

Mwenyeezi Mungu amesema kwamba “Nimetayarisha kwa viumbe vyangu wazuri (au maswalihina zawadi ambazo) macho hayajaona, wala masikio kusikia wala kupita katika fikra za binaadamu. 

Kwa hiyo Hadithi Alkudsiy ni habari kutoka kwa mwenyeezi mungu ambazo alipewa Mtume kutufikishia. Mtume alitumia maneno yake ya kibinadamu ili kutufikishia habari hizo bila kubadili maana ya asili kutoka kwa mwenyeezi mungu.

NENO “TARJAMA” KILUGHA NA KATIKA KURUANI

Neno Tarjama lina maana ya “Translation” au Kugeuza lugha kutoka lugha moja katika lugha nyinigneyo au nyingonezo. 

Katika dini ya kiislamu tunatumia katika kuruani tunapoiandika katika lugha nyinginezo. Kwa Mfano kuna Tarjama mbali mbali zilizoandikwa katika lugha za kiingereza kutoka katika lugha ya kiarabu kama vile

Sahih International

Yusuf Ali

Mohsin Khan

Pickthall

na katika lugha ya kiswahili

Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy (Aliyekuwa kadhi mkuu wa Kenya)

Na kuna tafsiri nyingi nyinginezo katika lugha mbalimbali za ulimwenguni

kama vile kirusi, kijerumani, kifaransa, kichina, kiyoruba, na ntyinginezo.

NENO “TAFSIRI”KILUGHA NA KATIKA DINI YA KIISLAMU

Neno Tafsiri kwa kiingereza ni Interpretation au Exegesis na kwa kiswahili ni maoni au kuelezea kinaganaga,  juu ya maandishi.  Ama kidini katika elimu ya kuruani lina maana ya maoni au kuelezea kinaganaga ya Aya za kuruani. Wafasiri wanaojulikana katika uwanja huu ni

Mfasiri wa kwanza alikuwa Mtume Mohamed (Sala na Amani zake Mola zimfikie)

Wafasiri waliofuata ni Maswahaba na Wanavyuoni Waliofuata katika karne na karne. Na wengine wa karibuni ni kama wafatao hapa chini;

Ibn Jarir Attwabriy

Azamakhshariy

Ibn Kathir

Arraziy

Tafsiri Ya Jalal Addin Asuyuttiy

Na wafasiri wengi wengineo katika karne ya kumi na tisa ambao waliifasiri kuruani kufuatana na mazingara ya kielimu ya wakati huo.

Katika karne hii ya Technologia  tunakuta tafsiri mbalimbali ambazo zinatufumbua macho katika aya za kuruani ambazo zinaashiria maendeleo ya kisayansi ulimwenguni na pia kuonyesha kwamba dini ya kiislamu inakuabaliana na sayansi.Tafsiri hizi zinasaidia kuwapa imani wachamungu na pia kuwavuta wasio waislamu. Ni mwenyeezi mungu kapanga hivyo ili kuwarudisha waliopotea na kuwapa imani waliopungukiwa na imani. Mwenyeezi mungu alijua hayo yatatokea na mfano huu ni kama katika enzi za uyahudi wakati nabii musa alipokuja na fimbo yenye muujiza iliyoshinda nguvu za firauni na nabii isa alipokuja na uwezo wa matibabu ya hali ya juu kuliko madakitari wote wa wakati huo basi mtume Mohamed pia alikuja na muujiza wa kuruani ambayo muujiza huo utadendelea kutoa miujiza mpaka mwisho wa ulimwengu.

Leo hii Kuna Tafsiri mbalimbali za kuruani katika nyanja mbalimbali za Kihistoria au Kisayansi, na nyinginezo.

1-Balagha (Rhetoric) Katika Kuruani Tukufu

UCHAGUZI WA MANENO WA HALI YA JUU KATIKA KURUANI (BALAGHA) SCIENCE OF RHETORIC

Katika aya  zifuatazo Sura Namba  7, 11, 2  na 14 Mwenyeezi Mungu kwa hekima kubwa ametumia katika kunadi neno يَـٰقَوۡمِ  kwa maana “ewe kaumu yangu”  kwani baba zao hawa Manabii Watukufu wananasibishwa na kaumu zao. Mfano katika aya zifuatazo kila nabii aliwaita watu wake kwa kusema “EnyI KAUMU YANGU”  Nabii Nuhu, Nabii Hud na Nabii Musa). Kwa kweli Kuruani haikosei kabisa. Angalia aya za sura namba 5 na 61 hapa chini Nabii Isa hana baba na kwa hiyo hana kaumu na katika kuwaita/kuwanadi  maneno yafuatayo yametumika وَقَالَ ٱلۡمَسِيحُ يَـٰبَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ Akanadi Masihi (Nabii Isa) “Enyi Watoto wa Israeli” Je  unaona hekima ya Mwenyeezi Mungu. Iwapo kungetumika “Ewe kaumu yangu” basi kungelikuweko kosa katika kuruani tukufu lakini haiwezekani kuruani kuwa na kosa lolote. Hapa chini Aya Sura namba 57  neno “Kaumu Yako” nj kaumu ya Mtume Mohamed aya hii ananadiwa mtume Mohamed na siyo Nabii Isa. Na mwishoni hapa chini Aya  Sura Namba 3 Mwenyeezi Mungu anathibitisha kwamba Nabii Isa ni kama Adam kwani wote hawana baba na kwa hiyo wote wawili hawana Kaumu. Na ndiyo maana Nabii Isa anawanadi watu wa Israeli kwa  “Ya Banni Israel” Enyi Watoto wa Israleli” na siyo “Enyi Kaumu Yangu”.   Adam hana Baba na Mama. Na wote wawili katika aya hii Mwenyeezi Mungu anasema wameumbwa kwa udongo. 

Sura/Chapter (7) sūrat l-aʿrāf (The Heights)

لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَقَالَ يَـٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَـٰهٍ غَيۡرُهُ ۥۤ إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٍ۬ (٥٩) وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦۤ أَتَأۡتُونَ ٱلۡفَـٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِہَا مِنۡ أَحَدٍ۬ مِّنَ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٨٠)

Sura/Chapter (11) sūrat hūd (Hud)

وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودً۬ا‌ۚ قَالَ يَـٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَڪُم مِّنۡ إِلَـٰهٍ غَيۡرُهُ ۥۤ‌ۖ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا مُفۡتَرُونَ (٥٠) ۞ وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَـٰلِحً۬ا‌ۚ قَالَ يَـٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَـٰهٍ غَيۡرُهُ ۥ‌ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَٱسۡتَعۡمَرَكُمۡ فِيہَا فَٱسۡتَغۡفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِ‌ۚ إِنَّ رَبِّى قَرِيبٌ۬ مُّجِيبٌ۬ (٦١)

Sura/Chapter (2) sūrat l-baqarah (The Cow)

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَـٰقَوۡمِ إِنَّكُمۡ ظَلَمۡتُمۡ أَنفُسَڪُم بِٱتِّخَاذِكُمُ ٱلۡعِجۡلَ فَتُوبُوٓاْ إِلَىٰ بَارِٮِٕكُمۡ فَٱقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ ذَٲلِكُمۡ خَيۡرٌ۬ لَّكُمۡ عِندَ بَارِٮِٕكُمۡ فَتَابَ عَلَيۡكُمۡ‌ۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ (٥٤) 

Sura/Chapter (14) sūrat ib’rāhīm (Abraham)

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱذۡڪُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡڪُمۡ إِذۡ أَنجَٮٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ وَيُذَبِّحُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَڪُمۡ‌ۚ وَفِى ذَٲلِڪُم بَلَآءٌ۬ مِّن رَّبِّڪُمۡ عَظِيمٌ۬ (٦) 

Sura/Chapter (5) sūrat l-māidah (The Table spread with Food)

لَقَدۡ ڪَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ مَرۡيَمَ‌ۖ وَقَالَ ٱلۡمَسِيحُ يَـٰبَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ رَبِّى وَرَبَّڪُمۡ‌ۖ إِنَّهُ ۥ مَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ ٱلۡجَنَّةَ وَمَأۡوَٮٰهُ ٱلنَّارُ‌ۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنۡ أَنصَارٍ۬ (٧٢)

Sura/Chapter (61) sūrat l-ṣaf (The Row)

وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَـٰبَنِىٓ إِسۡرَٲٓءِيلَ إِنِّى رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقً۬ا لِّمَا بَيۡنَ يَدَىَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَٮٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٍ۬ يَأۡتِى مِنۢ بَعۡدِى ٱسۡمُهُ ۥۤ أَحۡمَدُ‌ۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَـٰتِ قَالُواْ هَـٰذَا سِحۡرٌ۬ مُّبِينٌ۬ (٦)

Sura/Chapter (43) sūrat l-zukh’ruf (The Gold Adornment)

وَلَمَّا ضُرِبَ ٱبۡنُ مَرۡيَمَ مَثَلاً إِذَا قَوۡمُكَ مِنۡهُ يَصِدُّونَ (٥٧)

Sura/Chapter (3) sūrat āl ʿim’rān (The Family of Imrān)

إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ ٱللَّهِ كَمَثَلِ ءَادَمَ‌ۖ خَلَقَهُ ۥ مِن تُرَابٍ۬ ثُمَّ قَالَ لَهُ ۥ كُن فَيَكُونُ (٥٩)

2-Sarufi na Balagha (Grammar and Rhetoric) Katika Kuruani Tukufu

Chapter (9) sūrat l-tawbah (The Repentance) Aya Namba 40

إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدۡ نَصَرَهُ ٱللَّهُ إِذۡ أَخۡرَجَهُ ٱلَّذِينَ ڪَفَرُواْ ثَانِىَ ٱثۡنَيۡنِ إِذۡ هُمَا فِى ٱلۡغَارِ إِذۡ يَقُولُ لِصَـٰحِبِهِۦ لَا تَحۡزَنۡ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَنَا‌ۖ فَأَنزَلَ ٱللَّهُ سَڪِينَتَهُ ۥ عَلَيۡهِ وَأَيَّدَهُ ۥ بِجُنُودٍ۬ لَّمۡ تَرَوۡهَا وَجَعَلَ ڪَلِمَةَ ٱلَّذِينَ ڪَفَرُواْ ٱلسُّفۡلَىٰ‌ۗ وَڪَلِمَةُ ٱللَّهِ هِىَ ٱلۡعُلۡيَا‌ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (٤٠)

Tafsiri Ya Aya (Tuliyopigia Mstari) 40.

Kama hamtamnusuru (Mtume), basi Mwenyezi Mungu alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru; alipokuwa (mmoja tu na mwenziwe) wa pili wake, (peke yao); walipokuwa wote wawili katika pango; (Mtume) alipomwambia sahibu yake: “Usihuzunike, kwa yakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.” Mwenyezi · Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona, na akafanya neno Ia wale waliokufuru kuwa chini; na neno Ia Mwenyezi Mungu ndilo Ia juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayeshinda na ndiye Mwenye hikima.

Sherehe Ya Lugha Katia Aya Tuliyopigia Mstari

Kitendoجَعَل  Kinaonyesha mabadiliko (تحويل/Mabadiliko/Transformation) yanayofanywa na Mwenyeezi Mungu kuinua na kushusha na hapa limekuja kwa maana ya Kushushwa, na ڪَلِمَةَ ya kwanza lipo katika Accusative Case (Object)Ya Mtendaji ambaye ni Mwenyeezi Mungu Na ndiyo maana Limekuwa na Fatiha (manṣūb-منصوب) Na ڪَلِمَةُ ya pili Neno hili ni Ia Mwenyezi Mungu ambalo Ni la juu daima na maana hii inatokana na kuwa ni Subject-Nominative Case Na ndiyo maana lina Dhumma (Marfuu-مرفوع) kwani ni المبتدأ ambayo Nominal Tense lenye maana ya Madhubuti na Daima. na هِىَ ٱلۡعُلۡيَا‌ۗ Ni Ibara inayoonyesha kuwa Neno la mwenyeezi Mungu ni la juu daima. Halikuwa chini wala Halitakuwa Chini na litakuwa Juu Daima. Kwa Hiyo Neno ڪَلِمَةُ la pili siyo Atfu -Yaani Conjuctive kutoka katika neno جَعَلَ lililotajwa hapo mwanzo kwani ingekuwa hivyo basi Neno la pili lingehitaji kitendo kile kile cha mwanzo yaani جَعَل Kinaonyesha mabadiliko(تحويل /Mabadiliko/Transformation na hivyo lingeleta maana kwamba neno la Mungu lilikuwa chini kisha akaliinua lakini nahau inatupa maana iliyo sahihi yaani Maneno ya mwenyeezi Mungu ni ya juu daima na yale ya Makafiri Atayafanya chini daima.

Maajabu Ya Kuruani

Kila Herufi, Neno, au Aya Katika Kuruani limepangwa kwa hekima kubwa. Katika Aya Hapa Juu tofauti ya Harakati tu imeleta mabadiliko katika maana kama tulivyoona Fatiha katika neno ڪَلِمَةَ Na Dhumma Katika Neno وَڪَلِمَةُ. Kuruani Ni Kitabu Kimekusanya Mengi ambayo yanataka utafiti mkubwa sana. Kuruani Ni Mabahari Yasiyokauka na kila ukisoma unasoma Jipya. Na kwa kweli Ni Muujiza Mkubwa sana tena sana.

3-Sarufi na Balagha (Grammar and Rhetoric) Katika Kuruani Tukufu

Chapter (35) sūrat fāṭir (The Originator)Aya Namba 37

وَهُمۡ يَصۡطَرِخُونَ فِيہَا رَبَّنَآ أَخۡرِجۡنَا نَعۡمَلۡ صَـٰلِحًا غَيۡرَ ٱلَّذِى ڪُنَّا نَعۡمَلُۚ أَوَلَمۡ نُعَمِّرۡكُم مَّا يَتَذَڪَّرُ فِيهِ مَن تَذَكَّرَ وَجَآءَكُمُ ٱلنَّذِيرُۖ فَذُوقُواْ فَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِن نَّصِيرٍ (٣٧)

Tafsiri Ya Aya

Nao humo watapiga makelele, ( watalia wanasema): “Mola wetu! Tutoe (Motoni uturejeze duniani), tutafanya vitendo vizuri visivyokuwa vile tulivyokuwa tukifanya.” (Mwenyezi Mungu awaambie): “Hatukukupeni umri wa (kuweza) kukumbuka mwenye kukumbuka? Na akakujieni Muonyaji. Basi onjeni (adhabu) madhalimu hawana wa kuwanusuru.

Sherehe Ya Aya

Neno يَصۡطَرِخُونَ na Neno يَصۡرِخُونَ Yanatofautiana kwa ajili ya nyongeza ya Herufi “Atwaa طَ” Peke Yake. Kwani herufi hii inazidisha ukubwa wa Ukelele wa Binaadamu anapokuwa katika adhabu ya Akhera na Ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akalichagua hili lenye herufi طَ Katika Aya Hii ili Kuleta maana ya Makele makubwa ya Binaadamu watakapokuwa katika adhabu huko Akhera. Neno يَصۡرِخُونَ lisilo na herufi “Twaa” lina maana ya Ukelele wa muda usio moja kwa moja bali mara kwa mara lakini neno يَصۡطَرِخُونَ ni ukelele mkubwa sana usiosimama.

Na Maneno machache sana katika Lugha ya Kiarabu ambayo yamekusanya herufi zinazojulikana kama (Mufakhama) Na herufi hizi zina ugumu wa matamshi zinapokutana katika Neno kama hIli lililopo hapa juu nazo ni Herufi tatu ص، ط ،خ hizi zina ugumu katika matamshi na hasa zinapokutana katika neno moja kama hapa. Na ukifikiri sana utaona zinaashiria ukubwa wa adhabu ya Mwenyeezi Mungu.

Herufi ي inaonyesha kukariri kwa adhabu kila wakati, (Herufi ي lina maana ya kuendelea bila kusimama), Kimatamshi Herufi Raa ر ambayo inakariri katika matamshi inaashiria kukariri kwa adhabu kwa muda mrefu, Herufi Waw; و inaonyesha Muda mrefu watakaokuwa katika adhabu Ya Mwenyeezi Mungu, na Herufi Nun inaonyesha Uchungu wa maumivu wa Adhabu Hiyo.

Kwa hiyo tunaona Kila Herufi Inaashiria maana mojawapo.

Na katika kipande cha Aya:

رَبَّنَآ أَخۡرِجۡنَا نَعۡمَلۡ صَـٰلِحًا غَيۡرَ ٱلَّذِى ڪُنَّا نَعۡمَلُۚ

Tunagundua ufupisho wa maneno ya mwenyeezi Mungu kwani hapa ombi la wanayeadhibiwa ni “Mola wetu! Tutoe (Motoni uturejeze duniani), tutafanya vitendo vizuri visivyokuwa vile tulivyokuwa tukifanya. Lakini havikutajwa vitendo hivyo kwani Quruani ina fupisha na ina refusha sherehe ya Kuruani pale inapohitajika lakini siyo kienyeji. Kuruani Ingetaja kila kitu basi kungekuwa na maandishi mengi (vitabu vingi) ambayo siyo rahisi kwetu kusoma vyote.

Kuruani Ni Mabahari Yasiyokauka na kila ukisoma unasoma Jipya. Na kwa kweli Ni Muujiza Mkubwa sana tena sana.

3-Sarufi (Grammar)Katika Kuruani Tukufu

Matumizi Ya Sarufi Kwa Hekima Kubwa

Chapter (7) sūrat l-aʿrāf (The Heights) Ayat Number 59-61

لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَقَالَ يَـٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَـٰهٍ غَيۡرُهُ ۥۤ إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٍ۬ (٥٩) قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِهِۦۤ إِنَّا لَنَرَٮٰكَ فِى ضَلَـٰلٍ۬ مُّبِينٍ۬ (٦٠) قَالَ يَـٰقَوۡمِ لَيۡسَ بِى ضَلَـٰلَةٌ۬ وَلَـٰكِنِّى رَسُولٌ۬ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَـٰلَمِينَ (٦١)

Tafsiri Ya Kuruani

59· Tulimpeleka Nuhu kwa watu wake, naye akasema: “Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya siku (hiyo) iliyo kuu.” 6o. Wakuu wa watu wake wakasema: “Sisi tunakuona umo katika upotofu (upotevu) ulio dhahiri (kwa kutukataza haya tuliyowakuta nayo wazee wetu).” 6 I. Akasema: “Enyi kaumu yangu! Mimi simo katika upotofu (upotevu) lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola wa walimwengu wote.”

Sherehe Za Aya

Kisa cha Nabii Nuhu na Kaumu Yake alipowanasihi wamuabudu Mwenyeezi Mungu na waache ibada potovu lakini wakamuona onyo lake halina maana yeyote na wakamjibu kwamba

“Kwa hakika Tunakuona umezama katika upotevu ulio waziwazi”

Nabii Nuhu akajibu “Ewe kaumu yangu mimi sina uhusiano na upotevu hata moja na kwa hakika ni Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu ambaye ni Mlezi wa Malimwengu Yote”

Katika Sherehe hii kuna nyongeza ambayo inatokana na Sarufi (Grammar) kwani Kilugha ibara hii  إِنَّا لَنَرَٮٰكَ فِى ضَلَـٰلٍ۬ مُّبِينٍ۬  utaona Neno Fiiy فِى lina maana ya “kuzama” na Neno Dhalal ضَلَـٰلٍ۬  Ni Gerund (Masdar) Na kwa kawaida Masdar (kwa Kiingereza Gerund) Ni Neno la asili ambalo linazalisha maneno mengineyo kwa mfano Upotevu imezalisha kupotea, alipotea tutapotea na maneno mengineyo. Ni Neno la kitendo na pia lina maana ya Wingi na Uchache na hapa tunaweza kufasiri kama “Upotevu mwingi uliokuwa waziwazi” yaani kila mtu anaona upotevu huu.

Nabii Nuhu hakujibu kwa kusema “mimi sikuzama katika Upotevu mwingi waziwazi” kwani angejibu hivi basi angethibitisha kujiepusha na upotevu wa wingi lakini kujithibitishia mwenyewe upotevu wa uchache.

Lakini Kuruani haikosei kabisa kwani huyu alikuwa Mtume na Mwenyeezi Mungu hakuchaguliwa burebure ashindwe kuwajibu watu wake na kwa hiyo Nabii Nuhu akajibu vizuri sana akasema.

“Enyi watu wangi mimi sina uhusiano wowote hata na Upotevu Mmoja”

Kwa jibu hili alijikanushia Upotevu wowote ule. Mkubwa au Mdogo. Kwa Uchache au Kwa Wingi.

Je unaona Jibu la hekima hilo ambalo linatokana na Matumizi ya hali ya juu ya Sarufi (Grammar) Yaani Hapa Nabii Nuhu katumia Neno ضَلَـٰلَةٌ۬ ambalo linajulikana katika Sarufi Ya kiarabu اسم مرة Ni aina ya Masdar Maalum inayohusika na Hesabu. kwa mfano katika Aya hii “Upotevu Mmoja Tu” ni Aina Ya Masdar Au Gerund ambayo inahusika na hesabu ya kitendo. Na ajabu ni kwamba katika Jibu alilotoa Nabii Nuhu alikanusha kuwa na uhusiano wowote angalau kosa moja.

Na jambo lingine  Neno Hili  ضَلَـٰلَةٌ۬ ni Indefinite Noun au Jina lisilojulikana au Kwa kiarabu ni jina  نكرة na hapa litaleta maana ya “wowote” katika ibara “Enyi kaumu yangu Mimi sina uhusiano na upotevu wowote hata Mmoja”

Ama katika Maneno Ya Kaumu Yake wametumia Neno ضَلَـٰلٍ۬ kwani ni Definite Noun “Jina Maalum” Na katika Aya Hii ni  Neno “Maalum” katika Aya “Potevu mbalimbali Maalum ambazo kila mtu katika kaumu yake anazijua”.

Neno بِى lina maana mbalimbali lakini katika Aya Hii lina maana ya Uhusiano alipojibu Nuhu “Sina Uhusiano na Upotovu Wowote”

Je unaona Maana Mbalimbali katika Aya Hizi chache? Kuruani Ni bahari Ya Elimu Kubwa Kubwa..

Angalia Sarufi (Grammar) Ya Hali Ya juu ambayo ni miongoni mwa Sarufi mbalimbali ambazo ziliwatingisha Waarabu waliokuwa mahodari wa lugha yao katika wakati huo wa karne ya 7 na wakaingia katika Uislamu baada tu ya Kuona Muujiza wa Kilugha.

Na leo hii tunaona Muujiza Mwingine wa Sayansi.

Kwa Kweli Kuruani Ni Muujiza Mkubwa sana tena Sana.

Allahu Akbar Mungu Mkubwa sana Ndugu zangu Waislamu.

ELIMU YA SARUFI (GRAMMAR) NA BALAGHA(RHETORIC) INATUPA SIRI MBALI MBALI KATIKA AYA ZIFUATAZO.

TAFSIRI YA BAADHI YA AYAAT NA HEKIMA ZAKE

I. Chapter (23) sūrat l-mu’minūn (The Believers) Ayat Namba 61

أُوْلَـٰٓٮِٕكَ يُسَـٰرِعُونَ فِى ٱلۡخَيۡرَٲتِ وَهُمۡ لَهَا سَـٰبِقُونَ (٦١)

Tafsiri Ya Aya 61.

Basi wote hao ndio wafanyao haraka katika mambo ya kheri, na ndio wendao mbele katika hayo.

Sherehe Ya Aya

Wanashindana katika Kufanya kheri. Neno في “Fiy” lina maana kwamba binaadamu wako ndani ya kheri. Na tafsiri safi hapa ni “Wanashindana katika kufanya kheri” na Ni rehema zake Mwenyeezi Mungu ametujaalia kuzungukwa na kheri.Ingelikuwa Kheri ipo mbali basi kilugha Mwenyeezi Mungu angelisema katika Aya hii يسارعون إلى الخيرات  lakini hakusema hivi.

Kwa hiyo angalia maajabu kila neno katika Kuruani na kila Herufi zimechaguliwa na kupangwa kwa maana maalum.

————-

Chapter (1) sūrat l-fātiḥah (The Opening) Ayat Number 6

ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٲطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ (٦)

Tafsiri Ya Aya 6.

Tuongoze njia iliyonyoka.

Sherehe Ya Aya

Mwenyeezi mungu anasema “Tuongoze Katika Njia Iliyonyooka” hapa maana siyo tuongoze kwa kutuonyesha tu bali tuongoze na tunataka msaada wako utuongoze na kutusaidia mpaka mwisho wa njia. Na ingelikuwa kuomba msaada tu wa uongofu na kisha tuelekee wenyewe kuelekea katika njia iliyonyooka bila ya msaada wake basi Mwenyeezi Mungu angelisema;

“اهدنا إلى الصراط”

Na tungefasiri kama ifuatavyo:

“Tuongoze kwa kutuonyesha njia iliyonyooka lakini tutafuata wenyewe bila msaada wako” Je unaona tofauti Ya kilugha. Mwenyeezi Mungu amechagua Maneno Yake na akayapanga kwa hekima kubwa na kila mojawapo ina maana maalum.

—————-

Chapter (35) sūrat fāṭir (The Originator) Ayat Number 10

مَن كَانَ يُرِيدُ ٱلۡعِزَّةَ فَلِلَّهِ ٱلۡعِزَّةُ جَمِيعًاۚ إِلَيۡهِ يَصۡعَدُ ٱلۡكَلِمُ ٱلطَّيِّبُ وَٱلۡعَمَلُ ٱلصَّـٰلِحُ يَرۡفَعُهُۚ ۥ وَٱلَّذِينَ يَمۡكُرُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ لَهُمۡ عَذَابٌ۬ شَدِيدٌ۬ۖ وَمَكۡرُ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُوَ يَبُورُ (١٠)

Tafsiri Ya Aya

I-Anayetaka ukubwa (naamtii Mwenyezi Mungu) kwani ukubwa wote ni wa Mwenyezi Mungu tu. Kwake hupanda maneno mazuri; na · kitendo kizuri huyapandisha (hayo maneno mazuri.Maneno mazuri peke yake hayana maana kubwa) Na wale wanaofanya hila ya maovu, hao watapata adhabu kali. Na hila za hao zitaangamia (zitaondoka patupu).

Sherehe Y a Aya

Herufi ه “Haa” katika neno يرفعه inaashiria uhusiano baina ya maneno  katika Aya hii kufuatana na maoni matatu ambayo kila moja ni Muujiza.

1-Inaashiria Mwenyeezi Mungu ndiye anayeinua Vitendo vizuri “Neno zuri hupandishwa Kwake Na Mwenyeezi Mungu Mwenyewe” Na hapa Mwenyeezi Mungu anainua mwenyewe vitendo vizuri kwa ajili ya utukufu wa Neno hilo.(Hapa Mtendaji ni Mwenyeezi Mungu Mwenyewe)

2-kitendo kizuri “العمل الصالح” kinainua neno zuri “الكلم الطيب” (Hapa Mtendaji ni Vitendo Vizuri). Kwa maana kwamba Maneno Mazuri hayatoshi bila ya vitendo vizuri

3-Neno zuri ndilo linainua Kitendo kizuri, Kitendo Kizuri hakitoshi bila ya maneno mazuri (Mtendaji hapa Ni Neno Zuri).

Maana Ya Maneno Katika Aya 

1-Neno يصعد Maana Yake Kupanda kutoka chini mpaka juu (movement au haraka tu na siyo sehemu  مكان ). Neno zuri kujipandia lenyewe na hakuna anayelibeba baina ya ardhi na mbingu. Yaani tuwe macho sana tunapozungumza kwani neno linapanda lenyewe moja kwa moja kwa haraka bila kuchelewa kwa hiyo tunapewa usia tusizungumze ya hovyo.

2-Na neno إليه limetangulia katika Aya hii kuonyesha umuhimu wa sehemu au destination wa sehemu inayopandishwa neno la mwenyeezi Mungu.Na kibalagha linaleta pia maana ya Takhswis- تخصيص  yaani Sehemu hiyo yake Mwenyeezi Mungu Na siyo sehemu nyingine.

3-Neno يرفعه Maana Ya Neno hili ni Kupanda kutoka chini mpaka juu (Harakati au Movement na Sehemu) Yaani Daraja kwa daraja au stage by stage na inahitaji Atakayelipandisha (Naye Ni Mwenyeezi Mungu) katika kupandishwa. kama vile kupanda daraja kazini mfano huo huo unataka wakubwa wakubaliane na kisha wasaini makaratasi maalum kabla kupewa cheo na Huwezi Kujiinua mwenyewe.

4-Neno الكلم Elimu ya Sarufi inasema neno hili lina maana ya ibara isiyokamilika maana, na kwa rehema ya menyeezi mungu kachagua neno hili lenye maana ya kutokukamilika kwani litapanda tu ikiwa nia yako nzuri. Ingelikuwa sivyo hivyo kama vile angetumia neno الكلام “Alkalam” lenye maana ya Ibara isiyokamilika na ingekuwa kila neno tunalotamka lingechujwa yaani lile ambalo halikukamilika halipandi juu hata likiwa neno hilo lina nia nzuri. Yaani Yale tu yaliyokamilika maana ndiyo yangepanda kwake, lakini kwa rehema zake Mola wetu hapa anatusaidia katika lugha zetu za maisha yetu ya haraka haraka hata tusipokamilisha maneno Mola wetu anaelewa nia zetu na anatukamilishia na kuyapandisha maneno yetu ambayo pungufu.

5-Na ibara والعمل الصالح  imegawanyika katika sehemu mbili:

a-Vitendo Vya Moyo na

b-Vitendo Vya Viungo

Na Vitendo Vingi Ni Vile Vya Moyo.Kwani ndiyo sehemu ya Usafi (الإخلاص “Alikhlas”) wa moyo ni sehemu muhimu kwani Mwenyeezi Mungu hakubali Vitendo Vya Viungo Vyetu bila ya Kuwa na Nia Nzuri Yaani Moyo Mzuri, lazima Mioyo yetu iwe safi ili Mwenyeezi Mungu akubali vitendo vyetu. Kwa Mfano Huwezi Kumsaidia Masikini na hali unamsimanga au unamchukia kwa hiyo ni lazima kusafisha Moyo kabla ya kitendo cha Mwili.

—————————————–

Chapter (18) sūrat l-kahf (The Cave) Ayat Namba 63

قَالَ أَرَءَيۡتَ إِذۡ أَوَيۡنَآ إِلَى ٱلصَّخۡرَةِ فَإِنِّى نَسِيتُ ٱلۡحُوتَ وَمَآ أَنسَٮٰنِيهُ إِلَّا ٱلشَّيۡطَـٰنُ أَنۡ أَذۡكُرَهُ ۥ‌ۚ وَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُ ۥ فِى ٱلۡبَحۡرِ عَجَبً۬ا (٦٣) 

Tafsiri Ya Aya 63.

Akasema: “Unaona! Pale tulipopumzika katika mlima basi hapo nimesahau (kukupa habari ya) yule samaki. Na hakuna aliyenisahaulisha isipokuwa Shetani, nisikumbuke. Naye akashika njia yake baharini kwa namna ya ajabu.”

Sherehe Ya Aya

Kisa hiki kinatuelezea kisa cha Nabii Musa nacho kina mafundisho makubwa. Hatutazungumzia kisa chote bali neno moja katika Aya namba 63 nalo ni أَنسَٮٰنِيهُ ambalo limetiwa alama ya Dhumma mwishoni.

Neno hili lina Kitendo, Mtendaji na Kilichotendwa. (Verb, Subject and Object). Katika Sheria (Sarufi) ya Lugha ya Kiarabu Neno lolote ambacho linakuwa “Object” basi litatiwa alama ya Fatiha. Na katika neno hili أَنسَٮٰنِيهُ kuna Object Mbili (Dhamiri za Yaa na Hu) dhamiri Zote mbili asili yake ni (Yaa na Haa) lakini dhamiri  “Hu” haikufata sheria ya Sarufi kwani imetiwa Dhumma badala ya Fatiha. (Yaani “Hu” badala ya “Ha”) Kwani Alama ya dhumma ina maana ya Jambo lolote lililo kubwa na ndiyo maana unapolitumia unaona lina uzito katika ulimi kuliko alama nyinignezo kama vile Kasira, au Fatiha au Sukun.

Na huu ndiyo muujiza wa Kuruani. Sababu ya kutiwa Dhumma hapa ni Habari ya ajabu inaoelezewa katika Aya hii na Alama Ya Dhumma ina nguvu zaidi katika Mshangao wa habari inayozungumziwa, kwani  aliponena kijana kumwambia Nabii Musa kwamba kitoweo cha samaki ambaye alishapikwa na tayari kuliwa ameshatoweka Baharini kwani kijana alisahau kumwambia nabii Musa baada ya kumwona yule samaki ametoka katika kikapu na kuelekea baharini.(Muujiza ni samaki aliyekuwa tayari kuliwa mara akawa na uzima na kwenda baharini)

Ajabu ya kuruani ni kwamba kila herufi bali kila neno na aya lina maana.

Hapa alama ya Dhumma imetumika kwa maana ya Jambo kubwa la kushangaza na ndiyo maana sheria ya Sarufi (Grammar) Haikufuatwa!!!!. na iwapo ingelifuatwa basi neno  lingetamkwa أَنسَٮٰنِيهَ kwa kutumia Fatiha mwishoni na siyo أَنسَٮٰنِيهُ kwa kutumia Dhumma mwishoni.

Mwenyeezi Mungu amechagua na kupanga maneno ya kuruani  kiajabu na huu ndiyo Muujiza wa Kulugha katika Kuruani Takatifu.

—————————————

Chapter (3) sūrat āl ʿim’rān (The Family of Imrān) Aya Namba 31

قُلۡ إِن كُنتُمۡ تُحِبُّونَ ٱللَّهَ فَٱتَّبِعُونِى يُحۡبِبۡكُمُ ٱللَّهُ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡ‌ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬ (٣١)

Tafsiri Ya Aya 3 1.

Sema: “lkiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni; (hapo) Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufurieni madhambi yenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira (na) Mwenye rehema.”

Sherehe Ya Aya

Herufi Baa Katika Maneno تُحِبُّونَ ٱللَّهَ limetiwa Shadda kwa maana ya Tafkhiym (Tukuza) kulingana na Mapenzi Yetu ya Mwenyeezi Mungu nayo yanaonyesha Utukufu wake Mwenyeezi Mungu.

Na Maneno يُحۡبِبۡكُمُ ٱللَّهُ Alama ya Shadda Hapa Imeondolewa ili ilingane na Upole wake Mwenyeezi Mungu na mapenzi yake kwetu sisi binaadamu. Katika maneno يُحۡبِبۡكُمُ ٱللَّهُ Herufi Baa Imechambuliwa (Yaani asili yake zilikuwa zimeungana katika maneno ( تُحِبُّونَ ٱللَّهَ) Na sababu ya kuchambuliwa ni sheria za Sarufi ambayo limefanya neno يُحۡبِبۡكُمُ liwe Majzum. Kwa kawaida neno likiwa Majzum basi linatiwa Sukuwn na katika kutiwa Sukuwn imebidi Herufi Baa ambazo asili yake zilikuwa  zimeungana kuchambuliwa na mojawapo kuwa na Sukuun. Na katika kuchambuliwa maana pia inabadilika kuonyesha Mapenzi Ya Mwenyeezi Mungu kwetu sisi ni Makubwa sana kuliko sisi tunavyompenda. Kwa kifupi. Maneno yaliyochambuliwa nyaani يُحۡبِبۡكُمُ ٱللَّهُ yanaonyesha Mapenzi Makubwa sana yanayotoka kwa Mwenyeezi Mungu kuliko yetu kama inavyoonyesha maneno Yaliyogandamana. Yaani تُحِبُّونَ ٱللَّهَ

——————————————-

Chapter (75) sūrat l-qiyāmah (The Resurrection) Ayat Number 34-35

أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰ (٣٤)ثُمَّ أَوۡلَىٰ لَكَ فَأَوۡلَىٰٓ (٣٥)

Tafsiri Ya Aya 34·

(Ataambiwa): “lmekwisha kukufika (adhabu, ya Mwenyezi Mungu); imekwisha kukufika” 35. Kisha “lmekwisha kukufika (adhabu ya Mwenyezi Mungu); imekwisha kukufika.,

Shrehe Ya Aya

Mwenyeezi Mungu katika Aya Hizi anatoa Onyo la Adhabu mara nne. (Mwenyeezi Mungu anaelewa zaidi kuhusu Aya hizi)

Mwenyeezi Mungu anatupa onyo la adhabu za duniani  na adhabu ya pili itakuwa baada ya kuingia kaburini Na neno Thumma yaani baada ya wakati mpaka kufufuliwa kisha adhabu itakayofuata ni baada ya kufufuliwa na adhabu ya nne ni Motoni.

Hapa wanavyotuambia wafasiri Hizi onyo nne ni kwa maana ya Adhabu Duniani, Kaburini, Siku Ya kiama Na Motoni.

MUIYANO WA KUSHANGAZA BAINA YA NAMBA ZA AYA NA MAFUNDISHO YAKE (CONTENTS)

Chapter (20) sūrat ṭā hā Aya Namba 114

فَتَعَـٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّ‌ۗ وَلَا تَعۡجَلۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مِن قَبۡلِ أَن يُقۡضَىٰٓ إِلَيۡكَ وَحۡيُهُ ۥ‌ۖ وَقُل رَّبِّ زِدۡنِى عِلۡمً۬ا (١١٤)

TAFSIRI YA AYA I14.

Ametukuka Mwenyezi Mungu. Mfalme wa haki. Wala usiifanyie haraka (hii) Qurani (kwa kusoma), kabla haujamalizika Wahyi (ufunuo) wake. Na (uombe) useme: “Mola wangu, nizidishie ilimu.”

SHEREHE YA AYA

Mwenyeezi Mungu anamfundisha Mtume asiharakishe katika kuhifadhi kuruani na pia katika kusoma bali afanye subira na amuombe Mwenyeezi Mungu. Aya Hii Inawiana na idadi za sura za kuruani ambazo idadi yake ni 114 na ajabu ni kwamba Namba Ya Aya Hii pia Ni 114 katika Sura Ya Twaha.

——————————

Chapter (47) sūrat muḥammad Aya Namba 13

وَكَأَيِّن مِّن قَرۡيَةٍ هِىَ أَشَدُّ قُوَّةً۬ مِّن قَرۡيَتِكَ ٱلَّتِىٓ أَخۡرَجَتۡكَ أَهۡلَكۡنَـٰهُمۡ فَلَا نَاصِرَ لَهُمۡ (١٣)

TAFSIRI YA AYA l3.

Na (watu wa) miji mingapi iliyokuwa yenye nguvu zaidi kuliko (watu wa) mji wako uliokutoa: Tuliwaangamiza wala hawakuwa na msaidizi.

SHEREHE YA AYA

Mwenyeezi Mungu anamliwaza Mtume na kumtia moyo alipokuwa akiwakimbia maaadui wa Mecca. Namba Ya Aya Ni 13 nayo inawiana na mwaka wa 13 ambao mtume Alipohajiri (kuhama) kwenda Madina alipofukuzwa na makafiri wa Mji wa Mecca.

————–

Chapter (14) sūrat ib’rāhīm (Abraham)

وَلَنُسۡڪِنَنَّكُمُ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ‌ۚ ذَٲلِكَ لِمَنۡ خَافَ مَقَامِى وَخَافَ وَعِيدِ (١٤) I4·

TAFSIRI YA AYA 14

“Na tutakukalisheni (nyinyi) katika nchi (hizi) baada yao.” Watapata haya wale . waliogopa kusimamishwa mbele yangu na wakaogopa maonyo yangu (Kwa hivyo wakafanya mema na wakajiepusha na mabaya).

SHEREHE YA AYA

Aya namba 14 sura ya Ibrahim inahusu ahadi ya ardhi watakayoishi katika mji wa Basra ambao ulikuwa mji wa kwanza kujengwa na waislamu katika mwaka 14 A.H. lakini kwa sharti wamche Mungu. namba ya Aya Ni 14 na inawiana na tarehe hiyo ya 14c  Baada Ya Hijra.

——————————-

Chapter (8) sūrat l-anfāl Ayat Namba 15(The Spoils of War)

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ زَحۡفً۬ا فَلَا تُوَلُّوهُمُ ٱلۡأَدۡبَارَ (١٥)

TAFSIRI YA AYA 15

15-Enyi Mlioamini! Mkutanapo vitani na wale waliokufuru basi msiwageuzie mgongo (mkakimbia).

SHEREHE YA AYA

Vita Vya Badr vilifanyika mwaka wa 15 Baada ya Wahyi kushuka yaani mwaka wa 2 A.H. Na Ajabu ni kwamba Aya ya Sura hii ni namba 15 pia kama tarehe iliyofanyika vita hivyo ni  Miaka 15  Baada Ya Wahyi yaani mwaka 2 Baada Ya Hijra.

MASIKU, MIEZI NA MWAKA KATIKA KURUANI TUKUFU-SAYANSI YA ASTRONOMY YA HALI YA JUU

Nyongeza Ya Elimu hii nimeizungumzia katika Video yangu iliyopo katika Mlango wa “Sauti za Mwandalizi” ya Website hii.Na katika Video hiyo kuna maelezo juu ya tofauti baina ya Sidereal na Sinodical Months. Kuna maajabu makubwa katika Aya zifuatazo kutoka katika Sura Ya A-Mudathir.

عَلَيۡہَا تِسۡعَةَ عَشَرَ (٣٠) وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَـٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَـٰٓٮِٕكَةً۬‌ۙ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَہُمۡ إِلَّا فِتۡنَةً۬ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَـٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَـٰنً۬ا‌ۙ وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَـٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ‌ۙ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِہِم مَّرَضٌ۬ وَٱلۡكَـٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِہَـٰذَا مَثَلاً۬‌ۚ كَذَـٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَہۡدِى مَن يَشَآءُ‌ۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ‌ۚ وَمَا هِىَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ (٣١) كَلَّا وَٱلۡقَمَرِ (٣٢)

وَٱلَّيۡلِ إِذۡ أَدۡبَرَ (٣٣) وَٱلصُّبۡحِ إِذَآ أَسۡفَرَ (٣٤) إِنَّہَا لَإِحۡدَى ٱلۡكُبَرِ (٣٥)

Tafsiri Ya Aya Namba 30-32 Sura Ya Almudathir Namba 74

30-Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa.

31-Na hatukuweka walinzi wa huo Moto ila Malaika, wala hatukuifanya idadi yao (hiyo ya kumi na tisa) i1a kuwa mtihani kwa wale waliokufuru; ill wawe na yakini waliopewa Vitabu (kabla yenu), na walioamini wazidi katika imani yao, wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu (kabla yenu) wala Waislamu, na ill walio na ugonjwa katika nyoyo zao na waliokufuru waseme: “Apendea nini Mwenyezi Mungu kwa mfano huu?” Namna hii Mwenyezi Mungu humuacha kupotea amtakaye na humuongoza amtakaye. Wala hapana yoyote ajuaye majeshi ya Mola wako ila Yeye tu; na wala hakuwa (kutaja Moto na mambo yake) ila ni ukumbusho kwa viumbe.

32-Sivyo! Naapa kwa mwezi.

33- Na kwa usiku unapokucha.

34. Na kwa asubuhi inapopambazuka

35. Hakika huo (Moto) ni moja katika (balaa) kubwa (kabisa)

MUUJIZA WA KUSHANGAZA KATIKA AYA KUANZIA  30 mpaka 32 ZA SURA YA AL-MUDATHIR

Jumla ya herufi katika Aya namba 30, 31 na 32 ni 266 (Herufi za Aya Namba 30 ni 12 + Herufi Za Aya Namba 31 ni 245 +  Herufi za Aya Namba 32 ni 9 tutapata jumla herufi 266) ukigawa na herufi za Aya namba 32 ambazo ni 9 tutapata 29.5(266/9=29.5) Na  namba hii inalingana/inaashiria siku za Mwezi unaojulikana kama Sinodical. Mwezi wa Sinodical (Sinodical Month) una siku 29 na masaa 12 yaani siku 29.5 na Kisayansi ni mzunguko wa Mwezi kuizunguka Ardhi kwa mzunguko uliokamilika (Full Moon to Full Moon). Yaani baada ya 360 degrees ya mzunguko wa kwanza uliochukua siku 27.3 kwa muda wa siku 2.2 na kukamilisha siku 29.5 ambayo ni siku 29 na masaa 12.

Jumla ya herufi za Aya namba 31 ni 245 na ukijuumlisha herufi ndogo au nusu (herufi ambazo maneno yake nimepigia mstari katika Aya hapa juu) utapata jumla herufi 245 + 0.9=245.9 Na ukigawa namba hii na herufi za Aya namba 32 ambayo ina herufi 9 utapata 27.3 (245.9/9=27.3) na namba hii inalingana/inaashiria masiku yanayojulikana kama Sidereal (Sidereal Month). Mwezi wa Sidereal una siku 27.3 nao ni Mzunguko wa Mwezi kuizunguka Ardhi na husimama kabla ya mzunguko kamili kisha utaondoka tena kwa muda wa siku 2.2 ili kukamilisha msafara wake mpaka kufikia mwisho wa safari yake na Mwezi unafanya safari hii ya pili kutokana na Mzunguko wa ardhi ambao unajizungukia yenyewe (on its axis) kwa wakati ule ule ambao mwezi unapoizunguka ardhi na Muda utakuwa ni siku 29.5 au siku 29 na masaa 12 (sikiliza video yangu yenye habari hizi kwa urefu katika “sauti za mwandalizi” wa website hii).

Calendar ya kiislamu inatumia Mzunguko wa Mwezi kuizunguka ardhi kwa siku 29.5 kila mwezi na katika mwaka tunapata masiku 254 (29.5 X 12=254) .

Tofauti na Calendar za kizungu ambazo zinatumia Ardhi kulizunguka Jua kwa muda wa siku 365. Mwaka wa Kiislamu unatumia mwezi kuzunguka ardhi na una siku 11 pungufu ukilinganisha na Mwaka wenye kutumia Ardhi kulizunguka Jua kwa muda wa siku 365 (Miezi Minne Ya Mwaka kila mmoja una siku 30 + Mwezi wa February una Siku 28 + Miezi 7 ina Siku 31).

Aya namba 30 inaashiria masiku 30 ya mwezi (miezi yenye siku 30) na Herufi zake ni 12 ambazo zinaashiria miezi 12 ya Mwaka. Jambo lingine la kushangaza ni kwamba Aya Hii inazungumzia Malaika wanaosimamia Moto wa Jahanam ambao idadi yao ni 19

Na Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba Katika kila baada ya Miaka 19, Mwezi , Jua, Ardhi  hurudi zote  katika sehemu zao za asili zilizoondokea (starting points) katika mzunguko yao na hii kila baada ya  miaka 19 . Na mzunguko huu unajulikana katika Elimu ya Astronomy kama Metonic Cycle iliyoanzishwa na Meton (The cycle was discovered by Meton katika mwaka 432 kabla ya Ukristo kuja na Mgiriki aliyekuwa Astronomer).Na ajabu ni kwamba katika miaka hii 19 Mwezi utakuwa umeizunguka ardhi mara 254 (ni Sidereal Months yenye masiku 6,939.702 na siyo Sinodical ambayo ni mizunguko yake ni mara 235 yenye masiku 6,939.688) na ajabu zaidi ni kwamba Aya ifuatayo namba 31 ina herufi 254.

Aya zifuatazo mbili (Namba 33 na 34) baada tu ya Aya namba 32 zina maajabu mengine. Ukihesabu maneno yake utapata ni manane (Herufi Waw  وَ huhesabiwa kama Neno linapokuwa na maneno yenye kuleta maana na huhesabiwa kama herufi linapokuwa na herufi nyinginezo zisizokuwa na maana). Na jumla ya herufi za Aya hizi mbili (Namba 33 na 34) ni 24 (Aya namba 33 ina herufi 11 + Na Aya namba 34 ina herufi 13=24) Hapa huenda namba hizi zinaashiria hayo tuliyoyataja hapa Juu. Yaani 24 inaashiria tarehe na 8 inaashiria Mwezi. Kama tukivyosema kila miaka 19 Jua, Mwezi na Ardhi kurudi katika sehemu zao za awali yaani za asili na hiyo huenda ikawa kila tarehe 24 mwezi wa 8 katika kila miaka 19. Na pia huenda 24 hapa inaashiria Masaa ya siku moja. (Yaani Mwenyeezi Mungu kajaalia Siku Moja ina Masaa 24) Kwa kweli hizi ni Jitihada zetu katika utafiti lakini Mwenyeezi Mungu anajua zaidi. Na maana inayokusudiwa katika Aya hizi ni Tafsiri Tuliyoweka hapa Juu na haya ya Sayansi ni Vifaa au Elimu nyinginezo ambazo zimewekwa katika kuruani ili ije iwe hoja kwa wale wanaokataa na kutoamini hii kuruani. Elimu hizi ni Vifaa mbalimbali vya hali ya Juu vya kuwasaidia waliokuwa wamepotea na wale wasioamini na pia kuwazidishia imani wacha mungu. Kwani Yule Yule aliyeumba Ulimwengu au Malimwengu basi ndiye yule yule aliyeshusha Ujumne huu wa Kuruani Tukufu.

Je unaona Maajabu ya Kuruani? Aya hizi zina ujumbe na pia hapo hapo zinaashiria Elimu nyinginezo za kisasa. Na hii inathibitisha kwamba yule yule aliyeumba ulimwengu ndiyo yule yule aliyeshusha Kuruani hii.

Je Unajua kwamba:

-Neno Month (Ashahr) الشهر limekariri/limetumika katika kuruani mara 12 Na huu ni muujiza mkubwa kwani kama alivyosema Mwenyeezi Mungu katika kuruani kwamba idadi ya Miezi katika mwaka ni 12 (From January to December)

-Neno Moon (Alkamar) القمر limetajika na kukariri katika kuruani mara 27 nalo linaashiria siku 27 za Mwezi unaojulikana kama Sidereal Month (mzunguko wa mwezi kwa kipimo cha 360 degrees kufuatana na Nyota Angani

-Neno Ayaam (plural) ايام Limetajika na kukariri katika Kuruani mara 27 Nalo linaashiria masiku ya Mwezi kuzunguka ardhi na kusimama kabla ya kuondoka tena na kukamilisha siku 29.5.Na Masiku haya 27 ni ya Calendar za Kiislamu zinazofuata Sidereal Month.Sinodical na Sidereal nimezielezea vizuri katika Video za “Sauti za Mwandalizi” katika Website hii. Yaani Miezi ya Kiislamu yenye siku 27 (siku 11 pungufu kufuatana na Calendar za kizungu katika kila Mwaka). Kwa kifupi Sinodical ni pale Mwezi Unapochomoza. Au Full moon to Full Moon yaani Ukipima Kuanzia Mwezi unapokua umetimia na baada ya muda utaanza kuwa mdogo mpaka kupotea na kuchomoza na kukua tena mpaka unapotimia tena na hii ndiyo full moon to full moon. Sinodical inahusiana na Phases of the moon bali sidereal inahusiana na Mzunguko wa degrees 360 mwezi kuizunguka ardhi mara moja kwa kipimo cha nyota angani. Nyota ndiyo kingozi wa kutujuulisha kwamba mwezi umetimiza degrees 360 (circle moja)

-Neno Yaum (Singular) يَوْمٌ limetajika na kukariri katika kuruani mara 365 na linaashiria ardhi kulizunguka Jua kwa muda wa masiku 365 na ni tarehe zinazojukana kama Gregorian Calendar (aliyeanzisha tarehe hii alijukana kama Pope Gregory XIII)

MUUJIZA WA SIKU 365 NA 354 KUTAJIKA KATIKA AYA ZA KURUANI KIAJABU

Kuna pia Hesabu nyinginezo katika kuruani zinazoshangaza sana ambazo zinazotupa Masiku 365 ya Mwaka wa Gregorian na Masiku 354 ya Mwaka wa Kiislamu. Hesabu hizi nitaelezea hapa kama ifuatavyo:

Neno Shahr الشهر limekariri/limetumika katika kuruani tukufu mara 12 na ajabu ni kwamba mwaka una miezi 12 pia. Mweyeezi Mungu pia amesema katika kuruani tukufu kwamba mwaka una miezi 12.

Sura Ya Atawbah Namba 9 Aya Namba 36

إِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّہُورِ عِندَ ٱللَّهِ ٱثۡنَا عَشَرَ شَہۡرً۬ا فِى ڪِتَـٰبِ ٱللَّهِ يَوۡمَ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ مِنۡہَآ أَرۡبَعَةٌ حُرُمٌ۬‌ۚ ذَٲلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُ‌ۚ فَلَا تَظۡلِمُواْ فِيہِنَّ أَنفُسَڪُمۡ‌ۚ وَقَـٰتِلُواْ ٱلۡمُشۡرِڪِينَ كَآفَّةً۬ ڪَمَا يُقَـٰتِلُونَكُمۡ ڪَآفَّةً۬‌ۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ (٣٦)

Tafsiri Ya Aya 36.

ldadi ya miezi (ya mwaka mmoja) mbele ya Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika ilimu ya Mwenyezi Mungu (Mwenyewe tangu) siku alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo imo minne iliyo mitukufu kabisa (nayo ni Rajabu, Mfunguo Pili, Mfunguo Tatu, na Mfunguo Nne). (Kufanya) hivi ndiyo dini iliyo swa. Basi msijidhulumu nafsi zenu (kwa kufanya maasi) katika (miezi) hiyo. Na nyote piganeni na washirikina kama wao wote wanavyopigana nanyi; na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaomuogopa.

Aya ya mwanzo kutaja Neno Mwezi (Shahr au Month) ni Sura namba 2 Aya namba 185 Na sura Ya mwisho kutaja Neno Mwezi (Shahr au month)ni Sura Namba 97 Aya Namba 3

Neno Yawm (Day) limekariri katika kuruani tukufu mara 365 na huu ni muujiza baina ya miujiza mikubwa. Na kama ilivyo mwaka wa Gregorian-Tarehe zetu za leo-una masiku 365.

Ukipanga Aya za kuruani ambazo zimetaja jina Yawm (day) kuanzia mwanzo wa kutajika neno hili katika kuruani Sura Ya Alfatiha Aya Namba 4 mpaka mwisho wa kutajika neno hili katika sura namba 101 Aya namba 4 utakuta limekariri mara 365! ambayo ni masiku ya mwaka wa leo hii (Gregorian Calendar) na Ukipima au ukipachika namba za sura na aya zilizotajika Mwezi (Shahr au Month)katika kuruani kuanzia mara ya kwanza kutajika katika Sura Namba 2 Aya namba 185 na mwisho wa kutajika Sura namba 97 Aya namba 3 katika Namba za Aya ambazo neno Yawm limekariri mara 365 basi utakuta Aya zilizopo baina ya Sura hizi mbili ni masiku (Yawm au Day) 354 na hizi zinaashiria masiku ya mwaka wa Kiislamu.

Kwa kifupi Kuruani imetupa masiku 365 ya Ardhi kuzunguka Jua kwa muda wa siku 365 kwa njia ya kukariri neno Yawm na idadi hii inalingana na Masiku ya Ardhi kuzunguka Jua kwa Muda wa Masiku 365

Na imetupa pia Masiku 354 ya Mwezi kuzunguka ardhi kwa siku 29.5 na hizi katika mwaka (29.5 x 12=354) utapata siku 354 ambazo ni Calendar inayohusiana na Calendar Ya Waislamu.

Calendar hizi mbili zimeshiriwa katika kuruani kama tulivyoona na inatuthibitishia kwamba Calendar zote mbili ni sahihi nazo ni zake Mwenyeezi Mungu ambaye ameumba kila kitu.

Haya yote yanatuthibitishia kwamba yule yule aliyeumba malimwengu/ulimwengu ndiye yule yule aliyetutumia ujumbe wa Kuruani na Mtume Mohamed ni Mtume wake bila ya shaka yeyote. Ni mjinga pekee atakayekataa na kupinga. Je hatuoni haya tuliyoyataja hapa juu kwamba yanashangaza? Ni muujiza usio mfano. Allahu Akbar, Allahu Akbar.

NAMBA ZA AYA, SURA, IDADI ZA HERUFI, MANENO NA SURA NA MPANGILIO NI MUUJIZA WA HALI YA JUU.

BAADHI YA AYA ZA KURUANI NA MAAJABU YAKE

Sura Namba 2 Aya Namba 34

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأَدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ وَٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَـٰفِرِينَ (٣٤)

Tafsiri Ya Aya

34-Na (wakumbushe watu khabari hii): Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Adam” (yaani mwadhimisheni kwa ile ilimu yake aliyopewa). Wakamsujudia wote isipokuwa lblis; akakataa na akajivuna; na (tokea hapo) alikuwa katika makafiri; (ila alichanganyika tu na Malaika).

Namba Ya Aya hii katika Kuruani ni ya 34 na ukihesabu herufi za Aya kuanzia mwanzo mpaka kabla ya neno Iblis pia ni 34. Namba hii inashangaza kwani ukihesabu Jumla ya Sujudu za sala tulizoamrishwa 5  pia ni 34 Na hii ndiyo maajabu ya kuruani. kama kama Mwenyeezi Mungu anatuambia kwamba ikiwa Iblis alikataa kumsujusia Mwenyeezi Mungu basi Binaadamu anamsujudia mara 34 Je unaona namba zinavyozungumza na kushangaza?

Sura Namba 38 Aya Namba 70

قَالَ أَنَا۟ خَيۡرٌ۬ مِّنۡهُ‌ۖ خَلَقۡتَنِى مِن نَّارٍ۬ وَخَلَقۡتَهُ ۥ مِن طِينٍ۬ (٧٦)

Aya Hii pia ina herufi 34 kama hapo Juu tulivyoona.

Tafsiri Ya Aya 

76-Akasema: “Mimi ni bora kuliko yeye; kwani mimi umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo.

Sura Namba 15 Aya Namba 34

قَالَ فَٱخۡرُجۡ مِنۡہَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ۬ (٣٤)

Namba Ya Aya hii ni ya 34.

Tafsiri Ya Aya

34-Akasema (Mungu): “Basi toka humo, na bali ya kuwa wewe (sasa) ni mwenye kufukuzwa na kubaidishwa na rehema “

Baada ya Shetani  kujiona bora na kujivuna akafukuzwa. Angalia Aya hizi mbili ya 38 na 15. Ya kwanza Alijivuna nayo ina herufi 34 na ya pili akafukuzwa na namba ya Aya hii ni 34. Angalia muiyano wa kihesabu. Hesabu Za Aya, Herufi na Sura zinaonyesha maajabu matupu na pia zinathibitisha kwamba kuruani ni yake Mwenyeezi Mtukufu. Namba 34 katika Aya hapa juu zimewekwa katika Sura tofauti na kiajabu. Allahu Akbar.

SURA YA YASIN NA NAMBA 2988

Sura Ya Yasin Namba 36 Ina Aya 83 Ukizidisha 36 X 83 utapata Jawabu namba 2988 Jambo la kushangaza ni kwamba Jumla ya Herufi za Sura Ya Yasin ni 2988. Hii Inaonyesha kwamba mpangilio wa herufi, maneno, na sura katika kuruani ni katika haki ya juu sana, na kila kimojawapo kimehesabiwa. havikutungwa hovyo, hovyo bali kuna Mwenyeezi Mungu aliyeamrisha haya.

HADITHI INAYOHUSIANA NA BARUA YA MTUME MOHAMED KWA MFALME HERACLIUS WA DOLA YA ROMA ILIYOPO KATIKA SAHIH AL-BUKHARI

Barua Ya Mtume aliyompelekea Heraclius aliyekuwa Emperor (Mfalme) wa Dola Ya Byzantine (Dola Ya Roma) inashangaza sana kwani Mfalme huyu alikubali kwamba Kudhihirika Kwa Mtume ni Kweli kama ilivyotajwa katika Biblia. Alijua kwamba ni Mtume wa kweli na kama alivyosema mwenyewe kwamba anampa heshima kubwa Mtume huyu na alingekuwa karibu naye basi angemwosha Miguu yake kwa utukufu wake. Yaani Mfalme huyu alikuwa tayari kumwosha muguu mtume Mohamed.Pia jambo hili alilitilia umuhimu sana na mpaka kufikia kuota ndoto ya utawala wake unakaribia kuondoka na utachukuliwa na wenye kwenda Jando (Yaani Waislamu). Ajabu ni kwamba hapo baadaye kweli Waislamu walipigana na Utawala wa Roma ambao walikuwa watawala wa nchi zaidi ya moja. Waislamu chini ya Makhalifa yaani baada ya kufariki kwa Mtume Mohamed, walipigana na Heraclius katika Vita Vya Yarmouk (August 636) na kushinda vita hivyo ambavyo vilimaliza utawala wa Byzantine (Roma) huko Syria.

Hadithi Ya Mtume Mohamed (Sala na Amani Zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) hapa chini kutoka katika Kitabu cha Sahih Al-Bukhariy inatufahamisha vizuri Barua ya Mtume Kwa Mfalme Mkubwa wa Dola Ya Byzantine (Roma) na yaliyopita baadaye.

Hadithi Inasema:

Alisimulia ‘Abdullah bin’ Abbas:Abu Sufyan bin Harb alinijulisha kuwa Heraclius alikuwa amemtumia mjumbe kwake wakati alikuwa akiandamana na msafara kutoka kwa(watu wa kabila la) Quraish. Walikuwa wafanyabiashara wanaofanya biashara huko Sham (Syria, Palestina, Lebanoni na Yordani), wakati ambapo Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alikuwa na maafikiano ya amani na makafiri (Abu Sufyan na Waquraishi).Kwa hivyo Abu Sufyan na wenzake walikwenda kwa Heraclius huko Ilya (Jerusalem). Heraclius aliwaita kortini na alikuwa na waheshimiwa wote wakuu wa Kirumi karibu naye. Alimwita mtafsiri wake ambaye, akitafsiri swali la Heraclius aliwaambia, “Ni nani kati yenu aliye na uhusiano wa karibu na yule mtu anayedai kuwa Nabii?” Abu Sufyan alijibu, “Mimi ndiye jamaa wa karibu naye (miongoni mwa kikundi).”

Heraclius alisema, “Mlete karibu yangu (Abu Sufyan) na uwapange wenzake wasimame nyuma yake.” Abu Sufyan aliongeza, Heraclius alimwambia mtafsiri wake awaambie wenzangu kwamba anataka kuniuliza maswali juu ya mtu huyo (Mtume) na kwamba ikiwa nitasema uwongo wao (wenzangu) wanapaswa kunipinga. “Abu Sufyan aliongeza,” Wallahi! Laiti nisingeogopa wenzangu kunipa sifa za kuwa mwongo, nisingesema ukweli juu ya Mtume. Swali la kwanza aliniuliza juu yake lilikuwa:

‘”Je! Ana hadhi gani ya familia kati yenu?” Nikajibu, “Yeye ni wa familia nzuri(yenye utukufu) kati yetu.”

Heraclius aliuliza tena, “Je! Kuna mtu yeyote kati yenu aliyewahi kudai hivyo (yaani kuwa Nabii) kabla yake?” Nilijibu, “Hapana.”

Alisema, “Je! Kulikuwa na mtu yeyote katika ukoo wake kuwa mfalme?” Nilijibu, “Hapana.”

Heraclius aliuliza, “Je! matajiri au masikini wanamfuata?” Nilijibu, “Ni masikini wanaomfuata.”

Akasema, “Je! Wafuasi wake wanazidi au kupungua (siku hadi siku)?” Nilijibu, “Wanaongezeka.” Kisha akauliza, ‘

Je! Kuna mtu yeyote kati ya wale wanaokubali dini yake kuichukia na kuachana na dini baadaye?’ Nilijibu, “Hapana.”

Heraclius alisema, “Je! Umewahi kumshtaki kwa kusema uwongo kabla ya madai yake (kuwa Nabii)?” Nilijibu, ‘Hapana. ‘

Heraclius alisema, “Je! Yeye huvunja ahadi zake?” Nilijibu, ‘Hapana. Tuko kwenye maafikiano ya amani naye lakini hatujui atafanya nini katika kipindi cha maafikiano hayo. ‘ Sikuweza kupata nafasi ya kusema chochote dhidi yake isipokuwa hiyo.

Heraclius aliuliza, ‘Je! Umewahi kupigana naye?’ Nilijibu, ‘Ndio.’ Kisha akasema, “Je! Matokeo ya vita yalikuwa nini?” Nilijibu, “Wakati mwingine alikuwa mshindi na wakati mwingine sisi.”

Heraclius alisema, “Anakuamuru ufanye nini?” Nikasema, ‘Anatuambia tumwabudu Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu peke yake na tusiabudu chochote pamoja naye, na kukataa yote ambayo baba zetu walikuwa wamesema. Anatuamuru tusali, tuseme ukweli, tuwe safi na tuwe na uhusiano mzuri baina yetu, jamaa na ndugu.

Heraclius alimwuliza Mfasiri (Translator) akariri kwangu yafuatayo;

“nimekuuliza juu ya familia yake na jibu lako ni kwamba alikuwa wa familia ya utukufu sana. Kwa kweli Mitume wote wanatoka katika familia bora miongoni mwa watu wao.

Nilikuuliza ikiwa mtu mwingine yeyote kati yako alidai kitu kama hicho, jibu lako lilikuwa sivyo. Ikiwa jibu lingekuwa ndiyo basi ningefikiria kuwa mtu huyu alikuwa akifuata kauli ya mtu aliyetangulia.

Kisha nikakuuliza ikiwa yeyote wa baba zake alikuwa mfalme. Jibu lako lilikuwa hapana, na ikiwa ingekuwa ndiyo basi ningefikiria kuwa mtu huyu alitaka kurudisha ufalme wa baba yake.

Niliuliza zaidi ikiwa aliwahi kushtakiwa kusema uwongo kabla ya kusema kile alichosema, na jibu lako lilikuwa sivyo. Kwa hivyo nilijiuliza ni vipi mtu ambaye hasemi uwongo juu ya wengine anaweza kusema uongo juu ya Mwenyezi Mungu.

Mimi, kisha nikakuuliza ikiwa matajiri walimfuata au masikini. Ulijibu kwamba ni masikini aliyemfuata. Na kwa kweli Mitume yote wamefuatwa na tabaka hili la watu.

Kisha nikakuuliza ikiwa wafuasi wake walikuwa wakiongezeka au wanapungua. Ulijibu kwamba walikuwa wakiongezeka, na kwa kweli hii ndiyo njia ya imani ya kweli, mpaka iwe kamili katika mambo yote.

Nilikuuliza zaidi ikiwa kuna mtu yeyote, ambaye, baada ya kushika dini yake, aliichukia na kutupilia mbali dini yake. Jibu lako lilikuwa sivyo, na kwa kweli hii ni (ishara ya) imani ya kweli, wakati furaha yake inaingia mioyoni na kuchanganyika nayo kabisa.

Nilikuuliza ikiwa alikuwa amewahi kusaliti. Ulijibu sivyo na vivyo hivyo Mitume hawajawahi kusaliti.

Kisha nikakuuliza nini alikuamuru ufanye. Ulijibu kwamba amekuamuru umwabudu Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu peke yake na sio kuabudu kitu pamoja na Yeye na akakukataza kuabudu masanamu na akukuamuru kusali, kusema ukweli na kuwa safi. Ikiwa uliyosema ni kweli, Hivi karibuni atakaa katika kiti cha utawala wangu na nilijua (kutoka kwa maandiko) kwamba atatokea lakini sikujua kwamba atatoka kwenu, na ikiwa ningeweza kumfikia (kumwona)bila shaka basi ningeenda kukutana naye na iwapo nitakuwa naye basi kwa hakika ningemwosha miguu.

Heraclius kisha akauliza barua iliyoandikiwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu ambayo ililetwa na Dihya kwa Gavana wa Busra (Iraq), ambaye aliipeleka kwa Heraclius ili asome.

Yaliyomo katika barua hiyo yalikuwa kama ifuatavyo:

“Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu (Barua hii ni) kutoka kwa Muhammad mtumwa wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa Heraclius mtawala wa Byzantine. Amani iwe juu yake, ambaye anafuata njia iliyonyooka, ninakualika kwenye Uislam, na ikiwa utakuwa Muislamu utakuwa salama, na Mwenyezi Mungu atakuongezea thawabu mara mbili, na ikiwa utakataa mwaliko huu wa Uislamu utakuwa unatenda dhambi ya Arisiyin (wakulima yaani watu wako).

قُلۡ يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَـٰبِ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ ڪَلِمَةٍ۬ سَوَآءِۭ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمۡ أَلَّا نَعۡبُدَ إِلَّا ٱللَّهَ وَلَا نُشۡرِكَ بِهِۦ شَيۡـًٔ۬ا وَلَا يَتَّخِذَ بَعۡضُنَا بَعۡضًا أَرۡبَابً۬ا مِّن دُونِ ٱللَّهِ‌ۚ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُولُواْ ٱشۡهَدُواْ بِأَنَّا مُسۡلِمُونَ (٦٤)

Tafsiri Ya Aya:

Sema:”Enyi watu mliopewa Kitabu (cha Mwenyezi Mungu. Mayahudi na Manasara)! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu: ya kwamba tusimwabudu yo yote ila Mwenyezi Mungu wala tusimshirikishe (Mwenyezi Mungu) na chochote; wala baadhi yetu tusiwafanye wengine kuwa waungu badala ya Mwenyezi Mungu (au pamoja na Mwenyezi Mungu). Wakikengeuka, semeni: “Shuhudieni ya kwamba sisi ni Waislamu, (tumenyenyekea amri za Mwenyezi Mungu).” Sura 3:Aya 64

Abu Sufyan kisha akaongeza, “Wakati Heraclius alipomaliza hotuba yake na kusoma barua hiyo, kulikuwa na sauti kubwa na kelele za juu katika Mahakama ya Mfalme (Royal). Kwa hivyo tulifukuzwa nje ya korti.

Niliwaambia wenzangu kuwa swali la Ibn-Abi -Kabsha) ( Yaani Mtume (ﷺ) Muhammad) amekuwa maarufu sana hivi kwamba hata Mfalme wa Bani Al-Asfar (Byzantine) anamwogopa.

Ndipo nikaanza kuhakikisha kuwa yeye (Mtume) atakuwa mshindi katika siku za usoni mpaka nikasilimu (yaani Mwenyezi Mungu aliniongoza). “

Msimulizi anaongeza, “Ibn An-Natur alikuwa Gavana wa llya ‘(Jerusalem) na Heraclius alikuwa mkuu wa Wakristo wa Sham. Ibn An-Natur anasimulia kwamba wakati mmoja wakati Heraclius alikuwa akitembelea ilya’ (Jerusalem), aliamka asubuhi katika hali ya huzuni. Baadhi ya makuhani (priests/Mapadri) wake walimuuliza ni kwanini alikuwa katika hali hiyo?

Heraclius alilikuwa anafuata elimu za utabiri (foreteller and astrology). Akajibu, “Usiku wakati nikitazama nyota, niliona kuwa kiongozi wa wale watu wenye kwenda Jando (kufanya Tohara) ilikuwa imeonekana (kuwa ni mshindi).

Je! ni kina nani wanaotahiri? ‘ Watu wakajibu, “Isipokuwa Wayahudi hakuna anayetahiri, kwa hivyo haupaswi kuwaogopa (Wayahudi). ‘Toa tu amri ya kuua kila Myahudi aliyeko nchini.’ Wakati walikuwa wakijadiliana, mjumbe aliyetumwa na mfalme wa Ghassan kufikisha habari za Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) kwa Heraclius. Aliposikia habari hiyo, (Heraclius) aliwaamuru watu waende kuona kama mjumbe wa Ghassan alitahiriwa. Watu, baada ya kumwona, walimwambia Heraclius kwamba alikuwa ametahiriwa. Heraclius kisha akamwuliza juu ya Waarabu. Mjumbe akajibu, ‘Waarabu pia wanafanya tohara (Tahiriwa).’ (Baada ya kusikia hayo) Heraclius alisema kuwa enzi kuu ya Waarabu imetokea. Heraclius kisha aliandika barua kwa rafiki yake huko Roma ambaye alikuwa mzuri kama Heraclius katika maarifa. Heraclius kisha akaondoka kwenda Homs. (mji huko Syria na alikaa huko mpaka alipopata jibu la barua yake kutoka kwa rafiki yake ambaye alikubaliana naye kwa maoni yake juu ya kudhihirika kwa Mtume (s) na ukweli kwamba yeye alikuwa Nabii.

Hapo Heraclius aliwaalika wakuu wote  wa Wabyzantine kukusanyika katika kasri (Palace)lake huko Homs. Walipokusanyika, aliamuru milango yote ya ikulu yake ifungwe.

Kisha akatoka nje akasema:

“Enyi Wabyzantine! Ikiwa mafanikio ni hamu yenu na ikiwa mnatafuta mwongozo sahihi na unataka himaya yako ibaki basi mtiini na mkubalini Nabii huyu (yaani kusilimu).

Baada ya kusikia maoni ya Heraclius watu walikimbia kuelekea milango ya ikulu (State House) ya wakati huo kama wanyama wanojulikana kwa jina (orangers) lakini waligundua milango imefungwa.

Heraclius alitambua chuki yao dhidi ya Uisilamu na alipopoteza tumaini la kusilimu kwao, aliamuru warudishwe kwa mbele ya hadhara ya mkutano huo. (Waliporudi) akasema:

“Kilichosemwa ni kujaribu nguvu ya imani yenu na nimeiona.” Watu walimsujudia na kufurahishwa naye, na huu ndio ukawa mwisho wa hadithi ya Heraclius (kuhusiana na imani yake).

HAKI ZA BINAADAMU DUNIANI NA MAFUNDISHO MBALIMBALI KATIKA UISLAMU

HOTUBA YA MWISHO YA MTUME MOHAMED (Sala Na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie)

Katika Hotuba Hii nimeongezea sherehe zangu, Nimezidisha na kupunguza maneno  ili maana ieleweke kwa wasomaji. Niliyoongeza nimetia baina ya Brackets kama ( ) ili hotuba ya Mtume isichanganyikane na maneno yangu.

Ukichunguza Vifungu Vya Azimio La Haki za Binaadamu vilivyoandaliwa na Umoja Wa Mataifa: Universal Declaration of Human Rights (UDHR)  Utaona Kwamba Kuruani na Hadithi za Mtume Mohamed zilikwisha fundisha haya yote na pia Kila lilizo zuri katika maisha ya Binaadamu Na kutatua vifungu vyote vilivyozungumziwa katika Azimio hilo. Uhuru na Usawa wa Binaadamu katika Kila Pande za Maisha, Haki za Wanaume na Wanawake, Usalama Wa jamii, Afya na Elimu, Haki za Urithi na mengi mengineyo. Hotuba Aliyofanya Mtume kabla ya Kufariki Dunia inayojulikana kama “Hotuba Ya Kuaga” imekusanya pia nasiha nzuri ambazo zinahusiana na haki za Binaadamu.Hotuba hii ya Mtume pia ipo katika hadithi za Mtume zilizokusanywa na Vitabu mbalimbali vya Bukhari na Muslim.

Hotuba Ya Mwisho (Prophet Mohamed-Last Sermon):

Hotuba ya mwisho ya Mtume Muhammad ilitolewa wakati wa Hija ya mwaka wa 632 Christian Era (kipindi cha Ukristo) siku ya tisa ya Dhul Hijjah, Mwezi wa 12 Wa Miezi Ya Lunar Year (Tarehe Ya Kiislamu)huko Arafat,(Mecca) siku hiyo iliyobarikiwa katika Mwaka. Kulikuwa na Waislamu Wengi pamoja na Mtume wakati wa hija yake ya mwisho alipotoa Hotuba yake ya mwisho.

Hotuba:

Baada ya kumsifu, na kumshukuru Mungu, Mtume (Amani Na Sala za Mwenyeezi Mungu Zimfikie) alisema:

“Enyi watu, nisikilizeni kwa utulivu, kwani sijui ikiwa baada ya mwaka huu, nitakuwa kati yenu tena. Kwa hivyo, sikiliza kile ninachokuambieni kwa utulivu sana na mpeleke maneno haya kwa wale ambao hawakuweza kuwapo hapa leo.

Enyi watu, kama vile mnavyochukulia mwezi huu,(Mwezi wa Hija) leo hii(Siku ya Arafat), mji huu kama Mtakatifu,(Yaani Mecca) kwa hivyo zingatieni maisha na mali ya kila Muislamu kama amana takatifu. Rudisha bidhaa unazotunza kwa wamiliki wa hiyo amana.(yaani rudisheni mali mnapokuwa mnaaminiwa kuwatunzia wengine na msiwadhulumu baadaye).

Usimdhuru mtu yeyote ili mtu yeyote asiweze kukukudhuru. Kumbuka kwamba hakika utakutana na Mola wako Mlezi, na kwamba Yeye hakika atahesabu vitendo vyako.(Vitendo vyetu vizuri na vibaya vinaandikwa na tutahukumiwa)

Mwenyeezi Mungu amekukataza kuchukua Riba (Interest) na itaondolewa. Mali yako ya Asili (Capital) ni yako na unayo haki kuitunza.(Ukijiepusha na Riba Hautasababisha kujidhulumu au kumdhulumu mwingine). Mungu amehukumu kwamba hakutakuwa na Riba, na kwamba Riba yote ya Abbas ibn Abd’al Muttalib (Mjomba wake Mtume Mohamed alikuwa pia amejishughulisha na Riba na Mtume anaanzia kuharimisha Riba katika Familia Yake Kabla Ya wengine)Itaondolewa.

Jitahadharini na Shetani, kwa usalama wa dini yenu. Amepoteza matumaini yote kwamba ataweza Kukupotezeni katika mambo makubwa, kwa hivyo tahadharini na kumfuata katika maasi madogo madogo.

Enyi watu, ni kweli kwamba mna haki fulani kwa wanawake wenu, lakini pia wana haki juu yenu. Kumbuka kwamba umewachukua kama wake zenu chini ya amana kutoka kwa Mungu na kwa idhini yake. Ikiwa wanafuata haki zenu basi ni haki zao ya kulishwa na kuvishwa wema. Watendee wanawake zenu mazuri na Muwafanie wema, kwani wao ni wenzi wenu na wasaidizi waliojitolea. Na ni haki yako kwamba hawafanyi urafiki na yeyote ambaye haumkubali, na vile vile wasiwe wanafanya maasi ya uzinifu na wengine.

Enyi watu, nisikilizeni kwa makini, mwabuduni Mungu, fanyeni sala zenu tano za kila siku, funga wakati wa mwezi wa Ramadhani, na toeni Zaka. Nenda Hija kwa ibada ikiwa una uwezo.

Wanadamu wote wametokana na Adamu na Hawa. Mwarabu hana ubora kuliko asiye Mwarabu, na asiye Mwarabu hana ubora wowote juu ya Mwarabu; mweupe hana ubora kuliko mweusi, wala mweusi hana ubora kuliko mweupe; [hakuna aliye bora kuliko mwingine] ila kwa Kumcha Mungu na vitendo vyema. Elewa kwamba kila Mwislamu ni ndugu wa kila Mwislamu (Mtu yeyote aliyejisilimisha kwa Mwenyeezi Mungu anajulikana kama Muislamu) na kwamba Waislamu wanaunda udugu mmoja.

Hakuna kitu kitakachokuwa halali kwa Muislamu ambacho ni cha Mwislamu mwenzake isipokuwa kama kilipewa bure na kwa hiari. Basi msidhulimiane.

Kumbuka, siku moja utakuwa mbele ya Mwenyeezi Mungu na kujibu Maswali kufuatana na vitendo vyako. Kwa hivyo jihadhari, usipotee kutoka kwa njia ya haki baada ya mimi kuondoka.

Enyi watu, hakuna nabii au mtume atakayenifuata, na hakuna imani mpya itakayozaliwa. fikirieni vizuri, kwa hivyo, enyi watu, muelewe maneno ninayowafikishia.

Ninaacha nyuma yangu vitu viwili, Quran na Sunnah Yangu (Mfano Wa Mwenendo Wangu),ukifuata viwili hivi hutapotea kamwe.

Wote wanaonisikiliza watapeleka maneno yangu kwa wengine na wale kwa wengine tena; na huenda ikawa wa mwisho kuelewa maneno yangu vizuri kuliko wale ambao hunisikiliza moja kwa moja.(directly).

Ewe Mwenyeezi Mungu, kuwa shahidi wangu, kwamba nimewasilisha ujumbe wako kwa watu wako.

” Enyi watu, Mwenyezi Mungu amegawanya kila mrithi apaye sehemu yake ya mali ya urithi. Ukoo wa mtoto ni ule wa [mume anayemiliki kitanda]. Yeyote anayedai kuwa ni mtoto wa mtu mwingine mbali na baba yake basi atabeba laana ya Mwenyezi Mungu na malaika na watu wote.

Kwa hivyo Mtume mpendwa alikamilisha Hotuba yake ya Mwisho karibu na kilele cha Arafat,

Na Hapo Aya Ya Kuruani ilishuka:

ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِى وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَـٰمَ دِينً۬ا‌ۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِى مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٍ۬ لِّإِثۡمٍ۬‌ۙ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬ (٣)

Tafsiri Ya Aya

Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu. (Sura Ya Al-Maidah Namba 5 Aya Namba 3)

BARUA YA MTUME MOHAMED KWA NEGUS MFALME WA ETHOPIA NA JIBU ALILOLETEWA

Barua Ya Kulingania Dini kutoka Kwa Mtume Mohamed kwa Mfalme wa Ethopia aliyejulikana kwa jina Ashama bin Al-Abjar na Jibu aliloletewa na Mfalme. Baada ya Utafiti Uliofanywa inaonyesha kwamba barua hii iliandikwa wakati wa Wakimbizi wa Kiislamu Walipokwenda Ethopia.

Nimeifasiri kwa kiswahili kwa kuhifadhi Maana na ile ile lakini baadhi ya maneno machache ya kiswahili nimechagua mwenyewe ili ipate kueleweka kwa wasomaji.

BARUA KUTOKA KWA MTUME MOHAMED KWA NEGUS (MFALME WA ETHOPIA)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Kutoka kwa Muhammad Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu Mtukufu Kwa Negus, mfalme wa Abyssinia (Ethiopia). Amani iwe juu yake anayefuata mwongozo. Salamu Kwenu. Kwanza Ningependelea kutukuza sifa za Mwenyeezi Mungu; hakuna Mungu mwingine isipokuwa Yeye peke yake, Mwenye Enzi Kuu, Mtakatifu, Chanzo cha amani, Mpaji wa amani, Mlinzi wa imani, Mlinzi wa usalama. Ninashuhudia kwamba Yesu, mwana wa Mariamu, ni roho kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Neno lake ambalo alimshushia Mariamu, aliyekuwa bikira, mzuri wa tabia, na Mtakatifu ili achukue mimba ya Yesu. Mwenyezi Mungu amemuumba kutokana na roho kama alivyomuumba Adamu kwa mkono wake. Ninakutumia Mwaliko Kumtii Mwenyezi Mungu peke yake bila mshirika na kunifuata na kuamini kile kilichonijia, kwani mimi ndiye Mtume wa Mwenyezi Mungu. Nakualika wewe na watu wako kwa Mwenyezi Mungu, Mtukufu, Mwenye nguvu. Natoa ushahidi kwamba nimewasilisha ujumbe na nasiha Nakualika usikilize na ukubali ushauri wangu. Amani iwe juu yake anayefuata uongofu. “[Za’d Al-Ma’ad 3/60]

JIBU LA BARUA KUTOKA KWA NEGUS MFALME WA ETHIOPIA KWA MTUME MOHAMED.

(Sala na Amani zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Wakati ‘Amr bin Omaiyah Ad-Damari alipowasilisha barua ya Mtume Mohamed (Amani na Sala Zimfikie) kwa Negus, Maneno Aliyotumiwa na Mtume Aliridhika nayo na akakiri imani yake katika Uislamu baada ya hapo akaandika jibu lifuatalo kwa Mtume: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwenye Rehema Kubwa Kubwa na Ndogo Ndogo Kutoka kwa Negus Ashama kwa Muhammad Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu Mtukufu Amani iwe juu yako, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Rehema na Baraka Ni Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake ambaye hakuna Mungu Mwingine. Nimepokea barua yako ambayo umetaja habari za Yesu na kwa hakika kuhusu Yesu ni kama unavyosema hakuna zaidi. Tunakubali kabisa hayo ambayo uliyotumiwa na Mwenyeezi Mungu utufikishie Na Ninaahidi Kuwakaribisha na kuwahifadhi wakimbizi waliokuja kwetu Binamu Yako na Maswahaba Waislamu na Ninashuhudia kwamba wewe ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wa kweli na anayekuja kuthibitisha (Ujumbe Uliopita kabla yako), Ninakiri kwa ushahidi mbele ya binamu yako (aliyekwenda huko Ethoipia pamoja na wakimbizi wa kidini) kwamba ninakukubali Uislamu na kujielekeza kwa Mola wa walimwengu wote. “[Za’d Al-Ma’ad 3/61]

NEGUS ALIKUBALI UISLAMU

Mtume (Sala na Amani ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) alikuwa amemwomba Negus awarudishe Ja‘far na Swahaba Na Walirudi kumwona Mtume [SAW] huko Khaibar. Negus baadaye alifariki huko Rajab 9 A.H (baada ya Hijra ya Madinna) muda mfupi baada ya vita vya Tabuk . Mtume alitangaza kifo chake na akamsalia kama ilivoelezewa katika hadithi ya Bukhari na Muslim.

Hadithi Ya Bukhari

حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ، عَنْ سَلِيمِ بْنِ حَيَّانَ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ مِينَاءَ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ ـ رضى الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم صَلَّى عَلَى أَصْحَمَةَ النَّجَاشِيِّ، فَكَبَّرَ عَلَيْهِ أَرْبَعًا‏.‏ تَابَعَهُ عَبْدُ الصَّمَدِ‏.‏

TAFSIRI YA HADITHI

Jabir b. Abdullah aliripoti kwamba Mtume (ﷺ) alisali sala ya mazishi ya Ashama, Negus, na alisoma Takbir Nne Sahih Albukhari

———————

Hadithi Ya Muslim

وَحَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، عَنْ سَلِيمِ بْنِ حَيَّانٍ، قَالَ حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ مِينَاءَ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم صَلَّى

TAFSIRI YA HADITHI

Jabir b. Abdullah aliripoti kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) alisali kwa ajili ya Ashama, Negus, na alisoma takbir nne Sahih Muslim

————-

MAKAFIRI WALIJITAHIDI KUWARUDISHA WAKIMBIZI WA KIDINI

Baada ya wakimbizi Kuenda Ethopia Makuraishi Makafiri walimtuma Amr ibn al-‘As na ‘Abdullah ibn Abi Rabi‘a (kabla ya kusilimu) na zawadi kwa Negus na maaskofu wake. Nia yao ilikuwa kuwarudisha Waislamu Makka kwa sababu ya kusababisha shida kati ya makabila na kwa kuacha dini ya baba zao huko Mecca Walishindwa kumshawishi Negus ambaye aliamua kutunza sheria za wakimbizi.(Mfalme Huyu alikuwa anafuata Maadili ya ubinaadamu ambayo ya kisasa yaliyopitishwa na UMOJA WAMATAIFA wa haki za binaadamu.

MUUJIZA WA KUSHANGAZA

Mtume alijua vipi kwamba huko Ethopia (Africa) ndiyo wakimbizi watapata usalama? hakuchagua sehemu yeyote ulimwenguni. Na mtume hafanyi wala kuzungumza bure bure bali kwa kuongozwa na Mwenyeezi Mungu Mtukufu.Na Ajabu nyingine ni kwamba Mfalme huyu akawakaribisha Waislamu wakimbizi wa mwanzo katika wakati huo na kuwahifadhi. Na walipoletewa zawadi na Makafiri wa Mecca ili warudishwe Mfalme huyu alikataa. Je Huoni mpangilio wa Mwenyeezi Mungu.

FILM IFUATAYO INAYTUELEZEA MAKAFIRI WALIPOKUJA ETHOPIA NA KUTAKA MFALME AWARUDISHE WAKIMBIZI WA KIISLAMU HUKO MECCA NA HUYU MFALME MJASIRI HAKUKUBALI ZAWADI ALIZOLETEWA NA MAKAFIRI ILI WAKAMATWE NA KURUDISHWA HUKO MECCA.