UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
NAMBA ZA KUSHANGAZA
Engineering Ya Mpangilio wa Sura, Aya, Maneno na Herufi Katika Kuruani ni wa hali ya Juu sana hakuna Mfano wa kitabu chochote Duniani. Katika Mlango huu tutaona Maajabu Makubwa ya Namba 19, 16, 7 na Nyinginezo katika Kuruani. Allahu Akbar. Kwa kweli Inatisha Na Kusisimua. Hii ni Saini yake Mwenyeezi Mungu Mtukufu na hakuna Mwingine. Kwa kweli hii ni hotuba yake Ulimwenguni.
Niligusia katika sehemu nyingineo za Mtandao (Website) hii kuhusu Namba 19, 7.
Alhamdulilah Ningependelea kuendelea na maelezo yanayohusiana na Maajabu ya namba hizi na pia nyinginezo kama vile Namba 16.
NAMBA 19 NA MAAJABU MAKUBWA
Al-Mudathir ni Sura ya Nne kushuka Kwa Mtume Mohamad ﷺ. Na ni Sura Ya Kwanza Kutajwa Namba. . Na Namba ya Kwanza kutajwa katika Kuruani ni katika Sura Hii Aya Namba 30. Namba iliyotajwa hapa ni 19. Hii Namba ina Maajabu sana. Mwenyeezi Mungu ameitaja Namba hii katika Sura Hii siyo bure bure bali kwa hekima kubwa. Kama alivyosema katika Aya Namba 31 ya Sura Hii.
Kabla Ya kuelezea Miujiza inayoambatana na namba hii Ninaona bora kwanza Tufasiri Baadhi Ya Aya za Sura Hii na kisha Tutasherehesha Namba 19 na Maajabu Yake.
سُوۡرَةُ المدَّثِّر
يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡمُدَّثِّرُ (١) قُمۡ فَأَنذِرۡ (٢) وَرَبَّكَ فَكَبِّرۡ (٣) وَثِيَابَكَ فَطَهِّرۡ (٤) وَٱلرُّجۡزَ فَٱهۡجُرۡ (٥) وَلَا تَمۡنُن تَسۡتَكۡثِرُ (٦) وَلِرَبِّكَ فَٱصۡبِرۡ (٧) فَإِذَا نُقِرَ فِى ٱلنَّاقُورِ (٨) فَذَٲلِكَ يَوۡمَٮِٕذٍ۬ يَوۡمٌ عَسِيرٌ (٩) عَلَى ٱلۡكَـٰفِرِينَ غَيۡرُ يَسِيرٍ۬ (١٠) ذَرۡنِى وَمَنۡ خَلَقۡتُ وَحِيدً۬ا (١١) وَجَعَلۡتُ لَهُ ۥ مَالاً۬ مَّمۡدُودً۬ا (١٢) وَبَنِينَ شُہُودً۬ا (١٣) وَمَهَّدتُّ لَهُ ۥ تَمۡهِيدً۬ا (١٤) ثُمَّ يَطۡمَعُ أَنۡ أَزِيدَ (١٥) كَلَّآۖ إِنَّهُ ۥ كَانَ لِأَيَـٰتِنَا عَنِيدً۬ا (١٦) سَأُرۡهِقُهُ ۥ صَعُودًا (١٧) إِنَّهُ ۥ فَكَّرَ وَقَدَّرَ (١٨) فَقُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ (١٩) ثُمَّ قُتِلَ كَيۡفَ قَدَّرَ (٢٠) ثُمَّ نَظَرَ (٢١) ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ (٢٢) ثُمَّ أَدۡبَرَ وَٱسۡتَكۡبَرَ (٢٣) فَقَالَ إِنۡ هَـٰذَآ إِلَّا سِحۡرٌ۬ يُؤۡثَرُ (٢٤) إِنۡ هَـٰذَآ إِلَّا قَوۡلُ ٱلۡبَشَرِ (٢٥) سَأُصۡلِيهِ سَقَرَ (٢٦) وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا سَقَرُ (٢٧) لَا تُبۡقِى وَلَا تَذَرُ (٢٨) لَوَّاحَةٌ۬ لِّلۡبَشَرِ (٢٩) عَلَيۡہَا تِسۡعَةَ عَشَرَ (٣٠) وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَـٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَـٰٓٮِٕكَةً۬ۙ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَہُمۡ إِلَّا فِتۡنَةً۬ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَـٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَـٰنً۬اۙ وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَـٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۙ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِہِم مَّرَضٌ۬ وَٱلۡكَـٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِہَـٰذَا مَثَلاً۬ۚكَذَٲلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَہۡدِى مَن يَشَآءُۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَۚ وَمَا هِىَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ (٣١) كَلَّا وَٱلۡقَمَرِ (٣٢) وَٱلَّيۡلِ إِذۡ أَدۡبَرَ (٣٣) وَٱلصُّبۡحِ إِذَآ أَسۡفَرَ (٣٤) إِنَّہَا لَإِحۡدَى ٱلۡكُبَرِ (٣٥) نَذِيرً۬ا لِّلۡبَشَرِ (٣٦) لِمَن شَآءَ مِنكُمۡ أَن يَتَقَدَّمَ أَوۡ يَتَأَخَّرَ (٣٧) كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا كَسَبَتۡ رَهِينَةٌ (٣٨) إِلَّآ أَصۡحَـٰبَ ٱلۡيَمِينِ (٣٩) فِى جَنَّـٰتٍ۬ يَتَسَآءَلُونَ (٤٠) عَنِ ٱلۡمُجۡرِمِينَ (٤١) مَا سَلَڪَكُمۡ فِى سَقَرَ (٤٢) قَالُواْ لَمۡ نَكُ مِنَ ٱلۡمُصَلِّينَ (٤٣) وَلَمۡ نَكُ نُطۡعِمُ ٱلۡمِسۡكِينَ (٤٤) وَڪُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلۡخَآٮِٕضِينَ (٤٥) وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ (٤٦) حَتَّىٰٓ أَتَٮٰنَا ٱلۡيَقِينُ (٤٧) فَمَا تَنفَعُهُمۡ شَفَـٰعَةُ ٱلشَّـٰفِعِينَ (٤٨) فَمَا لَهُمۡ عَنِ ٱلتَّذۡكِرَةِ مُعۡرِضِينَ (٤٩) كَأَنَّهُمۡ حُمُرٌ۬ مُّسۡتَنفِرَةٌ۬ (٥٠) فَرَّتۡ مِن قَسۡوَرَةِۭ (٥١) بَلۡ يُرِيدُ كُلُّ ٱمۡرِىٍٕ۬ مِّنۡہُمۡ أَن يُؤۡتَىٰ صُحُفً۬ا مُّنَشَّرَةً۬ (٥٢) كَلَّاۖ بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلۡأَخِرَةَ (٥٣) ڪَلَّآ إِنَّهُ ۥ تَذۡكِرَةٌ۬ (٥٤) فَمَن شَآءَ ذَڪَرَهُ ۥ (٥٥) وَمَا يَذۡكُرُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُۚ هُوَ أَهۡلُ ٱلتَّقۡوَىٰ وَأَهۡلُ ٱلۡمَغۡفِرَةِ (٥٦)
TAFSIRI KUANZIA AYA NAMBA 27 MPAKA 31
27. Na ni nini kitakachokujulisha Moto huo?
28. Haubakishi wala hausazi.
29. Unababua ngozi mara moja.
30. Juu yake wako (walinzi) kumi na tisa.
31.Na hatukuweka walinzi wa huo Moto ila Malaika, wala hatukuifanya idadi yao (hiyo ya kumi na tisa)ila kuwa mtihani kwa wale waliokufuru; ili wawe na yakini waliopewa Vitabu (kabla yenu), na walioamini wazidi katika imani yao,wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu (kabla yenu) wala Waislamu, na ili walio na ugonjwa katika nyoyo zao na waliokufuru waseme: “Apendelea nini Mwenyezi Mungu kwa mfano huu?” Namna hii Mwenyezi Mungu humuacha kupotea amtakaye na humuongoza amtakaye. Wala hapana yoyote ajuaye majeshi ya Mola wako ila Yeye tu; na wala haikuwa (kutaja Moto na mambo yake) ila ni ukumbusho kwa viumbe.
SHEREHE
Mwenyeezi Mungu anatufahamisha umuhimu wa Idadi ya Malaika wa Motoni. Kwamba amewachagua Jumla yao ni 19. Na anatuelezea Sababu Tatu Muhimu za Kuchagua idadi yao kuwa 19 kwa kusema;
1/ili kuwa mtihani kwa wale waliokufuru;
2/ili wawe na yakini waliopewa Vitabu (kabla yenu),
3/na walioamini wazidi katika imani yao
Kwa hiyo Hii Namba ina Umuhimu kama Mwenyeezi Mungu anavyosema katika Aya Hizi.
Mojawapo ya Umuhimu wa Idadi ya Malaika hao kuwa 19 ni Kuwapa Yakini au Imani zaidi wale waliopewa Vitabu kabla Ya Uislamu.
Kwa hiyo Wakristo watakapojua Siri ya Namba hii 19 basi watapata Imani zaidi (Yakini) na Kuukubali Uiskamu na Mafundisho ya Uislamu.
Kazi ya Kwanza Nitakayofanya ni Kufanya Utafiti wa Namba 19 katika Sura Ya Mudathir.
Hebu Tuhesabu Herufi kuanzia Mwanzo wa Sura Ya al-Mudathir Aya Namba 1 mpaka neno عَلَيۡہَا Mwanzoni mwa Aya Namba 30 yaani Kabla Ya Maneno تِسۡعَةَ عَشَرَ Yenye Maana ya “Kumi Na Tisa”
Ukihesabu kwa kutumia Maandishi yaliyotumika wakati wa Amir Othman Ibn Afan (Othman Script) . Tutapata Jumla ya Herufi ni 361 na namba Hii ni sawa na 19 X 19 yaani (19 x 19=361).
Je unaona ya Kushangaza. Kabla ya Maneno تِسۡعَةَ عَشَرَ “Kumi na Tisa” tunapata Jumla ya herufi ni 361 ambayo inagawanyika katika Mafungu 19 ya 19. Je unaona Maajabu?
Hebu tuende katika Sura Ya Maryam ambaye ndiye Mama yake Nabii Isa (Jesus) kwani Katika Sura ya Al-Mudathir kumetajwa Watu wa Vitabu na Waksristo ni Mojawapo.
Hebu tuchunguze Sura Hii.
Kwanza, La kushangaza ni kwamba Sura Ya Maryam ni ya 19 Pia!!!
Yaani Ni Sura Namba 19 Angalia Maajabu. Unaona Mpangilio unavyoshangaza? Je Mtume Mohamad ﷺ alikuwa anatumia Super Computer katika Kuandaa Kuruani?
Sasa Mbona Namba zimepangwa Kiajabu kiasi ambacho Binaadamu inamshangaza na yeyote hawezi Kufanya Hivi? (Kuruani iliposhuka Aya na Sura zilikuwa hazina Namba wala TASHKIL (Diactritical Marks kama vile Fatha, Kasrah na Nyinginezo) HIzi zote ziliongezwa baadaye ili kuwasaidia wageni wa lugha ya Kiarabu. Baada ya Kuongezwa Namba na Alama za Tashkil sasa tunagundua Maajabu Haya. Allahu Akbar
Unaona Muujiza. Mungu Mkubwa.
Hebu Tuendelee Mbele na Uchunguzi Zaidi.
Kisa Cha Mama Matryam Na Mwanawe Kimetajwa katika Sura Hii Ya Maryam Kuanzia Aya Namba 16 mpaka Aya Namba 34 tu na Hizi pekee zinazungumzia Habari Ya Maryam na Mwanawe.
Sasa Angalia Kuanzia Aya Namba 16 Mpaka 34 kuna Aya 19 Pia!!!!!
Allahu Akbar. Tunapata tena Namba 19 Je unaona Mpangilio wa kiajabu usio wa Kibinaadamu?
Sasa Namba 19 inashangaza sana. Ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akasema katika Aya namba 31 Ya Sura Ya Al-Mudathir Kwamba Watu wa Vitabu watakapojua habari hii watapata yakini,
Huenda Labda Hivi ndivyo Mwenyeezi Mungu ana vyotuambia? Mungu anajua zaidi.
Aya hizi 19 kutoka katika Sura Ya Maryam ni kama zifuatazo:
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَٰبِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا (16) فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا (17) قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا (18) قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَٰمًا زَكِيًّا (19) قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَٰمٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا (20) قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَلِنَجْعَلَهُ ءَايَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا (21) فَحَمَلَتْهُ فَانتَبَذَتْ بِهِ مَكَانًا قَصِيًّا (22) فَأَجَاءَهَا الْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَٰلَيْتَنِي مِتُّ قَبْلَ هَٰذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا (23) فَنَادَىٰهَا مِن تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا (24) وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَٰقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا (25) فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنسِيًّا (26) فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ قَالُوا يَٰمَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْءًا فَرِيًّا (27) يَٰأُخْتَ هَٰرُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا (28) فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا (29) قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللَّهِ ءَاتَىٰنِيَ الْكِتَٰبَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا (30) وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَٰنِي بِالصَّلَوٰةِ وَالزَّكَوٰةِ مَا دُمْتُ حَيًّا (31) وَبَرًّا بِوَٰلِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا (32) وَالسَّلَٰمُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا (33) ذَٰلِكَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ قَوْلَ الْحَقِّ الَّذِي فِيهِ يَمْتَرُونَ (34) [مريم:16-34].
Hatujamaliza, Bado tuendelee na Utafiti.
Ukihesabu Kuanzia Aya Namba 16 Ya Sura Hii Ya Maryam Lenye Jina Maryam Mpaka Mwisho wa Kuruani (Msahafu) utapata Jumla Ya Aya ni 3971
وَ اذْكُرْ فِي الْكِتَٰبِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا (16)
Sasa Angalia Maajabu mengineyo. Namba 3971 ni sawa na 19 X 19 X 11
Yaani 19 imekariri mara mbili. Je unaona Maajabu. Sasa namba 11 ni nini? La kushangaza ni kwamba ukihesabu Maneno ya Aya Hii utapata jumla ni maneno 11 Pia!!! Allahu Akbar. Unaona Muujiza Mbele ya macho yako. (Herufi WAW hapa inahesabiwa kama Neno).
Na Pia Ukihesabu Kukariri kwa Jina la Maryam katika Kuruani utapata Mara 11 Pia!!!!
Je Unaona Muujiza wa Kushangaza.
Na Pia Huenda (Mungu anajua Zaidi) Namba hii 11 inaashiria Jina La Maryam mama yake Nabii Isa. kwani Ukihesabu Jina la Maryam (Uhesabu Jina Lake Pekee. Usihesabu Jina Lake lililoambatanishwa na Mtoto wake Nabii Isa Kama vile: Isa Ibn Maryam, Masih Ibn Maryam, Ibn Maryam Wa Umuhu au Ibn Maryam. Bali Jina Lake Pekee) kama nilivyofanya Hapa Chini utapata Jumla ya Kutajika Kwa Jina lake katika Kuruani Tukufu ni Mara 11 Tu.
{ فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَٰنِ الرَّجِيمِ } [آل عمران:36].
{ فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا قَالَ يَٰمَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَٰذَا قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ } [آل عمران:37].
{ وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَٰئِكَةُ يَٰمَرْيَمُ إِنَّ اللَّهَ اصْطَفَىٰكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَىٰكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَٰلَمِينَ } [آل عمران:42].
{ يَٰمَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّٰكِعِينَ } [آل عمران:43].
{ ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَٰمَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ } [آل عمران:44].
{ إِذْ قَالَتِ الْمَلَٰئِكَةُ يَٰمَرْيَمُ إِنَّ اللَّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْءَاخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ } [آل عمران:45].
{ وَبِكُفْرِهِمْ وَقَوْلِهِمْ عَلَىٰ مَرْيَمَ بُهْتَٰنًا عَظِيمًا } [النساء:156].
{ يَٰأَهْلَ الْكِتَٰبِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَىٰهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ فَءَامِنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ وَلَا تَقُولُوا ثَلَٰثَةٌ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ إِنَّمَا اللَّهُ إِلَٰهٌ وَٰحِدٌ سُبْحَٰنَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ لَّهُ مَا فِي السَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ وَكِيلًا } [النساء:171].
{ وَاذْكُرْ فِي الْكِتَٰبِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا } [مريم:16].
{ فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ قَالُوا يَٰمَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْءًا فَرِيًّا } [مريم:27].
{ وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَٰنَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَٰتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَٰنِتِينَ } [التحريم:12].
Maajabu Yasiyo Na Mwisho. Allahu Akbar. Je Katika karne ya 7, yaani katika Enzi ya Mtume ﷺ Iliwezekana Vipi Kupanga yote haya.
Haiwezekani Hata Kwa Kutumia Super Compurer za Kisasa.
Haiwezekani Hata Ma Profesa wote wa Duniani na Majini wote kusaidiana ili Kutoa Mfano wa Hii Kuruani. Wengi wamejitahidi na Wameshidwa vibaya sana.
Na Leo Hii hata Makafiri wanaelewa haya.
Nilimsikia Kwa masikio Yangu Mjerumani aliyekuwa Shabiki wa NAZI. Kama tunavyoelewa Kiongozi wa NAZI (Chama Kilichotawala Ugerumani 1920-1945 na kusababisha Vita Vikubwa Vya Dunia) ni Hitler. Basi Shabiki huyu amesilimu na ameamua Kulingania Dini ya Kiislamu na anasema kwamba “
Kuruani ni Maneno Yake Mwenyeezi Mungu na haiwezekani kwa Mtu kuzua haya. Kuruani Unapoisoma inakuzungumza” na akaendelea kusema kwamba “Mtume Mohammad ﷺ ni Mkweli na Omar Ibn Alkhatab alipoamua Kwenda Kumuua Mtume ﷺ na Huku amebeba Upanga na Kisha Akatoa Shahada na Kuingia katika Uislamu Mbele ya Mtume na hali amebeba Upanga mkononi ni Muujiza Mkubwa”
Bado Hatujamaliza Muujiza wa namba 19. Ni Muujiza Mkubwa sana ambao Mungu akipenda nitaelezea Mengi Mengineyo. Inshaallah. Kwa leo Naishia Hapa.
MUUJIZA WA KIHESABU WA KUSHANGAZA KATIKA SURA YA AL-NAHL
SURA YA AL-NAHL NAMBA 16
سُوۡرَةُ النّحل
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨) ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ فَٱسۡلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلاً۬ۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌ۬ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٲنُهُ ۥ فِيهِ شِفَآءٌ۬ لِّلنَّاسِۗ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَةً۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ (٦٩)
TAFSIRI
68.Na Mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba “Jitengenezee majumba (yako) katika milima na katika miti na katika yale (majumba) wanayojenga ( watu).”
69.Kisha ”Kula katika kila matunda, na upite katika niia za Mota wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita).” Kinatoka katika matumbo yao kinywaji (asali) chenye rangi mbali mbali; ndani yake kuna matibabu (dawa) kwa wanaadamu. Hakika katika hayo muna mazingatio kwa watu wenye fikra
SHEREHE SAYANSI
Kabla ya utafiti wa kihesabu hebu tugusie kidogo Engineering Ya Kilugha inayohusiana na maneno mawili katika Aya Namba 69 kutoka Katika Sura Ya Al-Nahl
ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ فَٱسۡلُكِى
Katika Lugha ya Kiarabu, Kitendo كُلِى (KULIY)yaani Kula na فَٱسۡلُكِى (FASLUKIY) yaani “Upite” au “Ufuate” ni Vitendo Vinachomhusu Nyuki wa Kike kwani Herufi ي “Ya” mwishoni mwa vitendo hivi ni ya Kike (Feminine) kama ingekuwa Nyuki wa Kiume basi Maneno yangelikuwa كل (KUL)na فاسلك (FASLUK) bila ya Herufi ya ي (YA) mwishoni mwa vitendo hivi.
Na leo Sayansi inathibitisha haya kwamba nyuki wa Kike ndiye mwenye kufanya Kazi (Worker Bee) ya kutafuta Asali. Nyuki wa kiume ana kazi Nyinginezo na mojawapo ni Kumlinda Nyuki Malkia na kumtia Mbolea.
A drone is a male honey bee. Unlike the female worker bee, drones do not have stingers. They gather neither nectar nor pollen and are unable to feed without assistance from worker bees. A drone’s only role is to mate with an unfertilized queen.
Kuruani Inasema Nyuki wa Kike ndiye anayefanya Kazi hiyo ya Kutafuta Chakula na Kwa hiyo inafundisha Habari hii kabla ya Uvumbuzi huu wa Kisayansi wa siku hizi za Mandeleo ya Kisayansi na Teknologia. Allahu Akbar. Mtume ﷺ alisoma wapi na alitumia vyombo gani vya utafiti katika kuchunguza Elimu kubwa kama hii.
ELIMU YA UZAZI WA NYUKI
Kabla ya kufanya Utafiti wa Kihesabu ningependelea pia kugusia Chromosomes za Nyuki. Chromosomes ni Kanda ambazo zinabeba Mbegu (Genes). Kwa hiyo Nyuki wa Kiume ana Kanda 16 na wa kike ana kanda 32 na hizi zinabeba “Mbegu” au Sifa Mbali Mbali za Maumbile ya Nyuki.
Kanda hizi zipo katika Kiini (Nucleus) ya Seli (Cells).
Kila Kiumbe kina Chromosomes na Genes (Kanda na Mbegu za Sifa Za Kizazi) na ndiyo maana Kila kiumbe kinatofautiana. Mwenyeezi Mungu amejaalia Kila kiumbe kitofautiane na Kingine kwa njia hiyo. Na ndiyo maana Kila kiumne kina Idadi ya Kanda (Chromosomes) Tofauti na Kingine. kwa Mfano Binaadamu ana Chromosomes 46 (Baba 23 na Mama 23)
Nyuki wa Kike ana Kanda 16 na wa kiume 32. Tofauti hii inatokana na Namna ya Kuzaliwa kwa Nyuki kutokana na Yai lililokuwa Fertilized na Unfertilized. Nyuki wa Kike anazaliwa kutoka katika Yai Fertilized na Mbegu ya Kiume na kwa hiyo Yai litakusanya mbegu za kiume na kike na Jumla itakuwa mbegu 32 yaani Mbegu 16 Mara 2 (16 X 2=32).
Na Nyuki Wa Kiume atazaliwa kutokana na Yai Unferilized katika Process (Mchakato) i=unaojulikana kama parthenogenesis na kwa hiyo Kanda zitakuwa 16 tu.
Na hii Ndiyo sababu Nyuki wa kiume anakuwa na Kanda 16 na wa Kike Kanda 32.
Habari hizi kwa kiingereza pia Nimeweka hapa chini.
A male honeybee has 16 chromosomes whereas its female has 32 chromosomes. … It is because of Haploid which is a sex determination system in which males develop from unfertilized eggs and are haploid, and females develop from fertilized eggs and are diploid. Male honeybees are born from unfertilised eggs by the process known as parthenogenesis where as female honeybees are born from fertilised eggs. As unfertilised eggs carries only half number of chromosome as compared to fertilised eggs, therefore male honeybee has 16 chromosomes whereas female has 32 chromosomes.
UTAFITI MKUBWA WA ENFGINEERING YA MPANGILIO WA MANENO KIAJABU
Sayansi hizi za kisasa zinatufahamisha kwamba Nyuki wa Kike ana Chromosomes 32 na Nyuki wa Kiume ana Chromosomes 16.
Hebu sasa tuchunguze Kuruani Tukufu tuone Maajabu Yasiyo Na Mwisho. Tumsikilize Mwenyeezi Mungu aliyeumba yote haya ijapokuwa makafiri na wajinga wengi hawaamini.
Sasa Mimi Pamoja Na Nyinyi Ndugu wasomaji hebu tuichambue Kuruani. Maneno ya Allah.
Nakukaribisheni hapa chini wote katika Sura Ya Al-Nahl yaani Sura Ya Nyuki.
MUUJIZA WA KWANZA
Tukienda katika Sura Ya Al-Nahl jambo la kwanza au Muujiza wa Kwanza utaona Sura Hii ni Namba 16. Je onaona ya kushangaza? Haya ndiyo tuliyoyasoma hapo juu.
Tumekwisha ona kwamba Kanda za Nyuki wa kiume ni 16 na wa kike ni 16 X 2 yaani 32. Je unaona.
Sasa tunedelee na maajabu yasiyo na mwisho. Allahu Akbar.
MUUJIZA WA PILI
Aya Ya Pekee inayomtaja na kumzungumzia Nyuki katika kuruani yote ni hii moja tu peke yake ambayo ipo katika Sura Hii ya Nyuki, Aya namba 68. Tumeifasiri hapa Juu.
Sasa Muujiza Mwingine unajitokeza je unauona? Tukihesabu Maneno ya Aya hii tutakuta ni 16 Pia!!!! Je unaona Maajabu yasiyo na Mwisho. (Tafadhali Hesabu Herufi وَ WAW kama neno na siyo Herufi) utapata Jumla ya meneno ni 16)
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨)
MUUJIZA WA TATU
Ndugu zanguni wasomaji bado tunaendelea na utafiti na hatujamaliza kwani Maneno ya Allah yana Mengi. Haya tunayoyajua ni Tonye katika Bahari. Kuna mengi mengoineyo katika Aya hizi chache ambayo hatuyajui bado na huenda watakokuja baadaye karibuni na pia karne zijazo watagundua. Allahu Akbar.
Idadi ya Aya za Sura Ya Al-Nahl ni 128 na utashagaa sana ukiambiwa kwamba Namba hii ni sawa na kusema 16 X 8 . Ukihesabu unaweza kuigawa namba hii 128 katika mafungu manane ya namba 16. Kwa hiyo nyuki wa kiume ana Kanda 16 na wa kike ana kanda 32. Ukifanya hesabu utapata pia Muujiza wa Nyuki wa Kike. Kwani namba 128 ni sawa na 32 mara 4 (32 X 4=128) Yaani Hata Nyuki wa kike hesabu hii inakubaliana na kanda zake pia. Allahu Akbar. Unaona Muujiza mbele ya Macho yako. Je Unaonaje Haya?
MUUJIZA WA NNE
Hebu tuchunguze idadi ya Maneno ya Sura Hii na tutakuta Muujiza wa kushangaza. Jumla ya Maneno ya Sura hii ni 2080. (Ukihesabu Herufi وَ WAW kama Herufi) na namba hii ni sawa na 130 Mara 16 (130 X 16=2080). Namba 16 ni Kanda za Kiume na hata Kanda za kike pia tunapata Muujiza. 2080 ni sawa na 32 Mara 65 (32 X 65=2080). Hapa 32 ni Kanda za Kike. Je unaona Muujiza wa Kushangaza. Allahu Akbar. Ndugu Yangu Binaadamu Mwenzangu Unaonaje namba hizi?
MUUJIZA WA TANO
Katika Lugha ya Kiarabu kuna Herufi 28 na katika hizi herufi 28 kuna herufi 16 pekee zilizounda Aya hii yenye Jina la Nyuki ambazo ni kama zifuatazo:
[ و ا ح ي ر ب ك ل ن ت خ ذ م ج ش ع ]
Hizi Ndizo herufi pekee zilizounda Aya hapa chini. Usihesabu Kukariri kwa herufi hizi bali aina ya vifaa vilivyohitajika Kuunda Aya Hapa chini ni hizi Herufi 16 peke yake. Je unaona Muujiza Wa Ajabu Usiyo na Mwisho. Angalia Haya Maajabu. Ndugu Zanguni Waislamu Lazima Tuogope haya mambo siyo Madogo. Allahu Akbar.
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨)
MUUJIZA WA SITA
Tuendelee na Miujiza isiyo na Mwisho. Allahu Akbar. Kwa kweli Mungu ni Mkubwa na Siyo Utani. Hakuna Utani hapa hata kidogo.
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ
Ibara hii inajitosheleza kimaana. Inasema “Na Mola wako akamfahamisha nyuki” Yaani Mola alimfundisha Nyuki”.
Ukihesabu Herufi za Ibara hii peke yake utapata Herufi 16 tu Je unaona Ya Maajabu. Allahu Akbar.
MUUJIZA WA SABA
Hebu Tuendelee na Utafiti. Ukihesabu maneno kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Al-Nahl mpaka Mwanzoni mwa Aya Namba 68 Katika neno إِلَى yaani kabla ya neno ٱلنَّحۡلِ utapata Jumla ya Maneno ni 992 (Tafadhali Hesabu Herufi ya و WAW kama Neno) Namba hii ni sawa na 16 Mara 62 (16 X 62=992) Yaani tumegawa Namba 16 katika Mafungu 62 na Namba hii 16 ni Kanda za Nyuki wa Kike. Allahu Akbar. Na Hesabu ya Kanda za Nyuki wa Kike pia hivi hivi. Namba 992 ni sawa na 32 Mara 31 (32 X 31=992) Yaani Tunaweza Kugawa Namba 32 katika mafungu 31 Je unaona Ya Maajabu. Allahu Akbar.
MUUJIZA WA NANE
Sasa Tuhesabu Maneno Kuanzia Neno ٱلنَّحۡلِ Al-Nahl lenye maana ya Nyuki katika Aya hii ya 68 mpaka Mwisho wa Sura Hii Ya Nyuki.
Tukihesabu tutapata Jumla ya maneno ni 1088 (Tafadhali Uhesabu Herufi ya و WAW kama Neno). Namba Hii ni sawa na 16 Mara 68 ( 16 X 68=1088) Hapa namba 16 ni nyuki wa kiume Tumeigawa namba 16 katika Mafungu 68. Na wa kike ni sawa na 32 Mara 34 (32 X 34=1088) na hapa namba 32 ni ya Nyuki wa Kike. Tumeigawa namba 32 katika mafungu 34 Allahu Akbar Unaona Ya Maajabu.
Tumeona Namba 16 X 68 ni sawa na 1088. Hapa Namba 68 pia inaashiria Aya Pekee katika Sura Hii na Ni Aya ambayo tunaifanyia Utafiti. Namba ya Aya Hii ni 68!!!
Yaani Aya Ya nyuki inayosema
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨)
Je unaona Miujiza Inayotutoa Mapovu Midomoni?
Je ni nani Aliye Mkubwa Duniani? Ni Nani Mfalme wa Kila Kitu Ulimwenguni? Ni Allah. Angalia Engineering ya Maneno Yake Yanavyoshangaza. Allahu Akbar.
Aya Moja Ya Nyuki Peke yake inatutoa Jasho sasa Je Kuruani Yote?