SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Fatwa Na Rai

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

MADA MBALIMBALI. (FATWA, NA RAI MBALI MBALI ZA NCHI NA WANAVYUONI)

MAWLID

Leo Tutaanza Na Suala Linalohusu  Sherehe za Mawlidi.

Swali Namba 1

Je Sherehe Ya Mawlid Inakubalika Katika Dini Ya Kiislamu?

Katika Mlango Huu Nitazungumzia Fatwa na Rai au Fikra Za Wanavyuoni Mbalimbali . Na Nimeona Bora Nikusanye Mazungumzo Yao Yaliyorikodiwa Yaani Katika Video zao na Tuwasikilize Tunapopata Nafasi. Kama Huna Nafasi hakuna Tatizo kwani Mimi Nimewasikiliza Kila Mmoja Kisha Nimefupisha Rai Zao Katika kila Video Hizi. Na Mwisho Nitaelezea Fatwa Zilizotolewa na  Nchi Kama Vile Egypt, Saudi Arabia na Jordan. Kila waliotoa Fatwa na Rai wana Sababu Zao. Sisi Tuwasikilize kisha wewe Msomaji Utachagua Mwenyewe. Hakuna Kulazimishana. Na Tusisahau Kuhitilafiana Umma Ni  Rehema kama alivyosema Mtume (Amani na Sala Zimfikie).

RAI ZA WANAVYUONI NA FATWA ZA SERIKALI ZA MISRI, SAUDI ARABIA NA JORDAN

FATWA

Serikali Ya Misri (Egypt) inakubaliana na Sherehe Za Mawlidi Ya Mtume Na Wanazo Aya Za Kuruani pamoja Na hadithi za Mtume kuthibitisha Rai Zao.

Serikali Ya Saudi Arabia Inapinga kuweko kwa Sherehe Za Mawlidi Ya Mtume Na Wanazo Aya Za Kuruani pamoja Na hadithi za Mtume kuthibitisha Rai Zao.

Serikali Ya Jordan  Inakubaliana Sherehe Za Mawlidi Ya Mtume.

RAI

Video Hizi Zina Rai (Opinion) Mbalimbali. Kuna wanaopendelea na wanaokataa kuwepo kwa Sherehe Za Mawlid Ya Mtume. Kwa Hiyo Wewe pia Msomaji Ufanye uchaguzi Mwenyewe. Mimi Rai Yangu ninakubaliana Na Sheikh wetu wa Tanzania Bwana Othman Maalim, Marehemu Sheikh Shaarawi na Sheikh Deedat. Ninakubaliana na Rai zao. Kwa Kweli Nimezipenda. Na wewe msomaji Ufanye Uchaguzi Unaopendelea kwani Kila Mmoja ana Fikra zake. Na huu ndio uzuri wa Dini Ya Kiislamu. Kuna Uhuru katika Suala hili. Hakuna Aliyekufuru katika Kufanya Mawlid. Na Mungu Anajua Zaidi. 

Video-1

Mwanachuoni Maarufu Hapo Tanzania Sheikh Othman Maalim. Ni Hotuba Nzuri Sana ambayo ina Mazungumzo Ya Kielimu. Mungu Ambariki na Ampe Kila La Kheri. Amezungumza Maneno Ya Maana Na Kielimu. Anakubaliana Na Sherehe za Mawlid. Sina Zaidi Ya Kuongeza. Kwa Kifupi Video Nzuri Sana. Allahu Akbar

Video-2

Mwanachuoni Maarufu Marehemu Sheikh Deedat Kutoka South Aftica. Mungu Amrehemu. Rai Yake anakubaliana Na Rai Ya wenye kupendelea Kufanya Sherehe Za Mawlid.

Video-3

Mwanachuoni Zakir Naik Rai Yake Anakataa Kuwepo na Sherehe za Mawlid. Anasema Katika Video Hii kwamba Ni Bida’a

Video-4

Mwanachuoni Yasir Kadhi Rai yake ni kwamba Sherehe za mawlid Ni Bidaa iliyo Mustahab. Yaani Siyo Haramu Kuifanya. Kwa Hiyo Inategemea Nia. Na anaona kwamba Mawlid siyo Bid’aa Kubwa Bali Ni ndogo. Bora Kutokufanya Mawlid lakini Tusipingane wala kulaumiana au kuiata makafiri. Ni Makosa kufanya hivyo.

Video-5

Mwanachuoni Sheikh Bilal Philips anakataa na Kupinga kuweko kwa Sherehe za Mawlid Ya Mtume

Video-6

Marehemu Sheikh Shaarawi ambaye alikuwa Mwanachuoni Mkubwa Huko Misri. Ni Mfasiri Wa Kuruani Tukufu. Ni Maarufu sana Kwa Elimu kubwa liyotoa kufuandisha Watu. Anakubaliana na Sherehe za Mawlidi na Anapendelea Ifanyike.Amezungumza hapa kwa lugha ya Kiarabu.

Video-7

Marehemu Sheikh Shaarawi anajibu Swala linalohusiana na Sherehe ya Mawlid Huko Misri (Egypt) Kama tulivyosema Katika Video namba 6 kwamba Sheikh Huyu alibarikiwa kwa Elimu ya Tafsiri Ya Kuruani Na Ni Maarufu Sana mpaka Leo.

Video-8

Marehemu Mwanachuoni Maarufu Anayejulikana Kwa Jina Sheikh Kishk. Ni mwananchi wa Misri (Egypt) anasema hapa kwa Lugha Ya Kiarabu kwamba Siku zote ni Mawlid Ya Mtume na Tusichague Siku kwani Abu Bakr au Omar Ibn Khatab ambao walikuwa Viongozi hawakufanya hivyo. Kwa Hiro Rai Yake Mawlid ni Bid’aa

Video-9

Mufti Menk na Assim anakataa kufanya Sherehe za Mawlidi Ya Mtume kama anavyotueleza Katika Video Hii

Video-10

Assim Al-Hakeem anakataa kufanya Sherehe zaMawlidi Ya Mtume kama anavyotueleza Katika Video Hii

Video-11

Marehemu Sheikh Ibn Baz Mwenyeezi Mungu Amrehemu alikuwa Maarufu Huko Saudi Arabia anakataa kuwepo kwa Sherehe za Mawlid Ya Mtume. (S.A.W.)

MADA YA PILI IPO KATIKA MAANDALIZI. INSHAALLAH MUNGU AKIPENDA NITACHAPISHA HIVI KARIBUNI