UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
NAKUKARIBISHENI KATIKA MADARASA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN MWAKA 2022. TUSOME KWA PAMOJA ELIMU YA FIQH
Naomba Mwenyeezi Mungu atupe uhai Mwezi Huu Mtukufu Tuufunge katika hali ya Uzima na afya nzuri. Pia Namuomba Mwenyeezi Mungu aniwezeshe Kuwaletea Habari mbalimbali zinazohusu Kuruani na Hadithi za Mtume Mohamad ﷺ
Je Kuna Mazungumzo mengine yaliyo bora kuliko Maneno Ya Muumbaji? Kwa kweli Hakuna.
Nia yangu kila siku nilete habari angalau moja na iwe fupi ili nisiwachokeshe wasomaji. Kwa hiyo Mlango huu utakuwa na Maudhui (Topics) mbalimbali kuanzia mwanzo wa Ramadhan mpaka mwisho.
02/April/2022 = Islamic Calendar 01/Ramadhan/1443
Mwenyeezi Mungu akipenda mwezi huu nitaanza na Sherehe ya Kitabu kilichoandikwa na Sheikh Imam Abu Shuja’ Al-Isfahan. Kitabu hiki ni ufupisho wa Elimu ya Fiqh kwa njia iliyo rahisi kusoma, kufahamu na kukumbuka. Kitabu kinajulikana kwa jina kama Mukhtasar Abi Shuja’ or Ghayat Al-Ikhtisar na pia Ghayat At-Taqrib (Na pia kinaitwa kwa jina la Matn of Abi Shuja’).
Elimu ya Fiqh inahusiana na Masuala mbalimbali ya dini kama vile Tohara, Sala, Zakat, Saumu, Hija, Harakati za Biashara, Usia, Ndoa, Mawindo, Mauaji yanapotokea, Sherehe za Kuzaliwa Kwa Mtoto, Kwa Kifupi Kila Elimu inayohusiana na Jamii. (Social Sciences)
Na njia ya uandishi wa Shekhe Abi Shujaa ni ufupisho na mgawanyiko wa milango mbalimbali ili kurahisisha kueleweka.
Mojawapo ya Juhudi kubwa za Mwandishi huyu ni Kitabu hiki.
Inasemekana kwamba aliishi miaka 160. Alikuwa Kadhi (Hakimu -Judge), Imam na alikuwa miongoni mwa Wanavyuoni waliokuwa wamebobea katika Elimu ya Fiqh.
Maisha Ya Sheikh Abi Shujaa Kwa ufupi.
Al-Hafith Abu Tahir As-Silafi once reported a hadith from him in his Mu’jam As-Safr up to Uthman ibn Affan (radiya Allahu Anhu) that the Prophet Muhammad said,
“Whomsoever builds a masjid for Allah the mighty and majestic Allah will build something like it for him in Jannah!”
Abu Tahir As-Silafi [died 576 A.H] said after reporting this narration.
“This Qadi Abi Shuja is from the most impeccable men of his time! He studied and taught the school of Imam Ash-Shafi’i for 40 years in Basrah. He mentioned this [hadith] to me around 500 AH and he lived for an extremely long time after that. I asked him about when he was born and he told me 434 A.H. in Basrah (Iraq) and that his father was born in Abadaan and his grandfather was from Asbahan.”
(Some resources mentions that he was born in the year 433 in Basrah (Iraq) and passed away in 593 A.H. (Islamic Calendar After Hijrah) in Madina)
His biographers mention that when he was the Wazir (Minister)he was just and cared for justice for all. While being a wazir (Minister) he would not leave his house until he prayed and recited much of the Qur’an. After retiring from his position of wazir, he travelled to Madinah and became an ascetic, divorcing the needs of this world. He became the custodian, cleaning and arranging the Masjid of the Prophet Muhammad (Peace Be Upon Him) until he died.
Other Sources such as Imam Al-Bayjuri in his Hashiyah states that Imam Abi Shuja died in 488 A.H. and that his grave is near the grave of the Ibrahim, the son of the Prophet Muhammad (P.B.U.H) at Al-Baqi.
Kitabu hiki ni ufupisho wa Shule au Madhehebu ya Shafii yaliyoanzishwa na Imamu Abū ʿAbdillāh Muḥammad ibn Idrīs al-Shāfiʿī.
Waislamu wa East Africa wanafuata Mafundisho ya Imamu Shafii katika Masuala Mbalimbali ya Dini ya Kiislamu na kwa hiyo nimeona vizuri mwezi huu wa Ramadhan tusome pamoja kitabu hiki angalau baadhi ya Milango.
Katika kusoma Nitaandika na pia ikiwezekana nitafanya Video.
Na pia nikipata nafasi nitakuwa nikidokeza kidogo kidogo miujiza ya kisayansi katika Mlango huu.
Kwa hiyo moja kwa moja leo Nitaanza na Mlango wa Kwanza la FIQH.
MLANGO WA KWANZA-TOHARA (PURIFICATION)
MAJI
“AINA YA MAJI
Maji ambayo yanafaa (yanajuzu) kutumia katika kujitoharisha (katika kufanya udhu) ni ya aina saba.
1.Maji ya Mvua
2.Maji ya Bahari
3.Maji ya Mto
4.Maji ya kisima
5.Maji ya Chemchem (kama vile zamzam huko Mecca) au Chemchem ya Mjini Kondoa Irangi (Tanzania)
6.Maji ya Theluji (Katika Nchi zenye Theluj)-Snow
7.Maji ya Mvua ya Mawe (Hail)”
Kuna ushahidi wa Kuruani na Hadithi za Mtume zinazothibitisha Tulivyovitaja hapa lakini siwezi kuorodhesha kwa ajili ya wakati.
Lengo ni kufupisha Elimu hii na kwa hiyo nitafasiri kitabu cha Abi Shujaa MATN peke yake na Kujiepusha na Maelezo ili nisichokeshe wasomaji.
MAFUNGU MANNE YA MAJI
1/”Maji yaliyo tohara, yenye kutoharisha na yasiyo na Karaha”
SHEREHE
haya ni maji yaliyo masafi ambayo ya asili kama alivyoyaumba mwenyeezi mungu mtukufu.
2/”Maji yaliyo tohara, yenye kutoharisha lakini yana karaha”
SHEREHE
Mfano wa maji ya aina hii ni yale ambayo umeyapasha moto kwa njia ya jua. Kwa mfano umeweka maji katika sufuria na kisha kuyaweka Juani na kuyatumia. Maji ya aina hii ni Tohara na pia yanaweza kutoharisha lakini yana Udhia au Karaha. Nadhani sababu ya karaha kama anavyosema Sheikh Abi Shujaa ni Chombo unachotumia kupashia maji hayo Juani ambacho Jua huweza kusababisha kuyayuka kwa asilimia ndogo sana ya Chombo hicho na kuchanganyika na maji na kwa hiyo yatabadilikia asili yake na kuwa na karaha au Maudhi. Na pia ikiwa chombo ni Plastic inaweza kusababisha kuzalisha maudhi mengineyo katika maji hayo.
3/”Maji yaliyo Tohara lakini hayawezi kutoharisha”
SHEREHE
Maji Yaliyo Tohara lakini hayawezi kutoharisha atakayeyatumia katika udhu ni yale ambayo yameshatumika. maji yaliyotumika na kuchanganyikana na Sabuni au Marashi na takataka haya kwa asili ni Tohara lakini hayafai kwa kutoharisha.(Udhu)
4/”Maji yenye Najisi (Impurities)”
SHEREHE
Maji Yalichanganyikana na Najisi (Uchafu wa aina yeyote) Mchanganyiko huu unaweza kuzalisha maradhi mbalimbali. Anasema Shekhe kwamba Kiwango cha maji ya aina hii ni chini ya litre 200 za maji au Zaidi ya Litre 200 lakini sharti yabadilike rangi au harufu au vyote viwili. lakini maji hayo yakizidi litre 200 na ikiwa harufu au rangi haikubadilika basi haya maji siyo Najisi.
NGOZI
Tumemaliza kuelezea Aina Za Maji Yaliyo Tohara na sasa tutaelezea habari ya Tohara ya Ngozi. Anasema Sheikh Abu Shujaa Kwamba
“Ngozi ya Maiti inatoharika kwa Kuichuna isipokuwa Ngozi ya Mbwa na Nguruwe na kizaliwa cha wanyama hawa au baina ya wanyama hawa na wengineo waliokuwa wanyama Tohara. na Mifupa Ya Maiti ya wanyama wa aina yeyote na Manyoya yao ni Najisi isipikuwa Binaadamu Mifupa na Manyoya siyo Najisi kwani Mwenyeezi Mungu amemkirimu na kumpa utukufu”
SHEREHE
Sheikh Abi Shujaa anasema katika Matn Yake kwamba Ngozi za wanyama wa aina yeyote inatoharika utakapo ichuna isipokuwa ngozi ya Nguruwe au Mbwa. Na pia wazaliwa wa wanyama hawa wawili au vizaliwa baina ya wanyama hawa wawili na wengineo walikuwa wanyama Tohara.
Lakini Mifupa na Manyoya ya Binaadamu siyo Najisi kwani Mwenyeezi Mungu amemtukuza Binaadamu.
VYOMBO
Tumemaliza Maudhui ya Ngozi na tutaelezea Aina Ya Vyombo. Sheikh anasema:
“Haifai au Haijuzu kutumia Vyombo vilivyotokana na madini ya Dhahabu na Fedha lakini inajuzu kutumia vyombo vya madini nyinginezo kwa sharti viwe Tohara”
SHEREHE
Hairuhusiwi kutumia vyombo kama vile vijiko, sahani, na vinginevyo ikiwa vyombo hivo vinatokana na madini ya Dhahabu na Fedha. Kuna Matajiri wakubwa duniani ambao wanatumia Vyombo vya aina hii kwa kweli haifai. Wakati duniani kumejaa Masikini siyo jambo zuri kutumia vyombo vya gharama kama hivi (Mfano vijiko , uma, visu, sahani au sufuria na vinginevyo) Lakini inaruhusiwa iwapo vyombo hivi vimetokana na madini ya kawaida isiyo na gharama kubwa.
03/April/2022 = Islamic Calendar 02/Ramadhan/1443
MSWAKI
Sehemu hii inazungumzia Kupiga Mswaki. Sheikh Anasema kwamba Kupiga Mswaki ni Mustahab (Jambo zuri kulifanya) katika wakati wowote unapohitaji isipokuwa baada ya Dhuhuri katika mwezi wa Ramadhan. Na Mustahab (Jambo zuri) Katika Mazingara Matatu yafuatayo:
1/Unapohisi Mabadiliko katika Harufu au Taste (Utamu) wa Mdomo baada ya Kukaa kimya kwa muda mrefu. Na Pia baada ya Kutokula au Kunywa kwa muda mrefu.
2/Unapotoka Usingizini. Unapokuwa Usingizini kunakuwa hakuna Kuzungumza, Kula au kunywa.
3/Wakati wa Kutawadha. (Ablution au Purification) Ili kujiandaa na Sala.
UDHU
Baada ya Maudhui ya Mswaki Sheikh anaendelea kutuelezea Faradhi za Udhu. Anasema kwamba
Faradhi za Udhu ni Sita.
1/Nia kabla ya kuosha uso
2/Kuosha Uso
3/Kuosha mikono mpaka viwiko (Elbows)
4/Kuosha Sehemu ya Mbele Ya Kichwa
5/Kuosha Miguu Mpaka Vifundoni
6/Kufuatilia Utaratibu Huu.
Na baada ya Kutufahamisha Faradhi za Udhu Sheikh anaendelea kutufundisha Sunnah Za Udhu.
Sunnah Za Udhu Ni Mambo Kumi.
1/Kutaja Basmala Kabla ya Kuanza kufanya UDHU, Yaani kusema “Bismillahi Arrahmani Arrahiym”
2/Kusafisha Viganja Vya Mikono Kabla Ya kuchota Maji.
3/Kusafisha Midomo kwa kusukutua Maji
4/Kusafisha Ndani ya Pua kwa Maji
5/Kupaka Maji Kichwa Chote kwa kukisafisha.
6/Kusafisha Masikio Nje na Ndani
7/Kusafisha Ndevu kama Nyingi kwa kuzichambua kwa maji
8/Kusafisha Vidole Vya Mikono na Miguu kwa Kuvichambua Baina Yake.
9/Kutanguliza Viungo Tulivyovitaka Vya Kulia kwanza na kisha Vya Kushoto.
10/Kila Hatua Tuliyoitaja ifanyIke Mara Tatu Tatu. Kwa mfano Uoshe Midomo mara tatu, Mikono mara Tatu na hivyo hivyo viungo vyote tulivyovitaja hapa. Na Katika Kuosha Viungo hivi ufuate Utaratibu.Kwa Mfano uanze na Nia Kisha Uso na hivyo hivyo mpaka Mwisho.
SHEREHE
Haya mafundisho yanatokana na Imamu Shafii. Sheikh Abi Shujaa anatuelezea mafundisho haya katika kitabu chake cha “MATN Abi SHUJAA”. Kama anavyosema kwamba tukifanya UDHU basi tufuate utaratibu huu tulioutaja hapa. Tumeona Faradhi za Udhu na Pia Sunna. Ukifuata Faradhi hizi Sita, Udhu unakuwa Umefanyika bila Tatizo na Ukitaka Kuzidisha kwa Kufuata Sunna inakuwa Safi zaidi kwa hiyo ni uchaguzi wako na sio lazima. Ukitaka Excellent basi fuata Sunna Zote na Usipofanya Utapata Very Good.
Dini ya Kiislamu haina Ugumu. Kuna Uchaguzi Mkubwa katika Kila kitu ili kurahisishia Waumini.
Ninarudia tena kuelezea kwamba Katika Faradhi ukiosha Uso mara Moja basi ni Faradhi na hii ni lazima lakini ukiosha Mara Tatu ni Sunnah na hii siyo lazima bali ni Nzuri. Kila Kiungo tulichokitaja hapa ukitaka unaweza kukisafisha Mara Tatu Tatu na hii ni Sunnah. Kuna sehemu nyingine duniani ambazo maji siyo Rahisi kupatikana na katika hali hiyo tunaona Faida ya Kutumia maji kwa kuosha Kiungo mara moja tu badala ya mara tatu. Na ikiwa Maji hakuna kabisa basi Kuna sheria nyingine ambayo injulikana kama TAYAMUM. ambayo tutaizungumzia baadaye katika MATN ya Abi Shujaa.
KUSAFISHA HAJA (Al-istinjaa)
Anasema Sheikh Abi Shujaa Kuhusu Usafishaji wa Kinachotoka Mwilini. Yaani Uchafu unaotoka Mwilini kama vile Mikojo na Choo Kikubwa, Kwamba Ni Wajibu (Lazima) Kusafisha.
Na ni Bora mtu ajisafishe kwa kutumia Mawe kama unaishi Jangwani na Kisha Ufuatilie kwa Maji. Na inajuzu Kufupisha kwa kutumia kimojawapo baina ya vitu viwili. Mawe Matatu au Maji tu Pekee.
Na Mtu akitaka Uchaguzi ulio mzuri basi Maji ni Bora zaidi kuliko chochote kingine.
Na ajipushe anapokuwa katika kujisafisha asielekee Kibla au kuupa Mgongo. Yaani asielekee Msikiti wa mecca au Kuupa Mgongo bali aufanye Msikiti huo uwe upande wake wa kulia au kushoto.
Pia Mtu yeyote anapokuwa katika Shughuli hiyo ya kusisafisha basi asifanye hivyo katika Maji yaliyotulia kama vile Mabwawa ambayo maji yake yametulia.
Na asifanye pia chini ya Miti yenye kuzalisha Matunda. Na katika zile Njia na sehemu ambazo zina Vivuli, na iwapo mtu atafanya haja katika sehemu hizi anawajibika kupata Laana ya Mwenyeezi Mungu.
Na ajiepushe pia kufanya Haja katika Matundu ardhini ili kujiepushia hatari za kuwaudhi wadudu ambao huweza kutoka na kumdhuru mtu huyo. Na pia ajiepushe na Kuzungumza anapokuwa katika Haja.
Sheikh anaendelea kusema kwamba Mtu anapokuwa katika Haja asielekee na kuupa mgongo Mwezi au Jua bali ajaalie Jua Na Mwezi ziwe katika upande wake wa kulia na kushoto.
SHEREHE
Sheikh Abi Shujaa anaelezea mafundisho Ya Imam Shafii ambayo pia yanatokana na hadithi za Mtume ﷺ na Aya za Kuruani na siyo bure bure.
Katika website hii nimeepusha kurikodi kila kitu kwani nikifanya hivyo itachukua maandishi mengi na haiwezekani. Kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba tutatumia njia ya ufupisho kama alivyofanya Abu Shujaa. Yaani tunafasiri MATN peke yake bila kurikodi ushahidi wa Hadithi za Mtume ﷺ au Aya za Kuruani.
Sheikh ametaja Kujisafisha kwa kutumia Mawe. Siku hizo ilikuwa mawe na siku za leo kuna Toillet Paper ambayo ni sawa na mawe. Ukitumia Toilet Paper na kisha maji basi inakuwa safi. Na ikiwa utatumia maji tu peke yake pia ni safi kwani si sehemu zote kuna Toilet Paper. Tumekatazwa kuzungumza wakati upo chooni. Na tumekatazwa kufanya haja katika sehemu za vivuli kwani sehemu hizo ni za watu kupumzika na sio vizuri kuacha uchafu katika sehemu kama hizi. Na pia kufanya haja katika maji yaliyotulia kwani uchafu unaweza kuzalisha Maradhi mbalimbali ya hatari kubwa. Kwa hiyo Sheikh anatuusia tujiepushe na sehemu hizo. Tumekatazwa kuuelekea au kuuoa mgongo Msikiti mkubwa wa Mecca. kwani Ni Nyumba tukufu. Na pia Maumbile Mawili makubwa tusielekee kwa mbele au nyuma (Mgongo). Haya ndiyo mafundisho ya Immu Shafii katika Habari za Kwenda HAJA.
04/April/2022 = Islamic Calendar 03/Ramadhan/1443
VITENGUA UDHU
Sheikh Abu Shujaa anaendelea kuelezea katika MATN yake kwamba vitu venye kutengua Udhu ni Sita:
1/Chochote kitakachotoka kutoka katika sehemu za Haja
2/Kulala Usingizi isipokuwa mtu huyo akilala kwa njia ambayo itazuia chochote kutoka katika sehemu za haja.
3/Kupotea Akili kwa Kulewa au Maradhi
4/Kugusana na Mwanamke ambaye siye katika MAHARIM na ikiwa imetokea hivyo bila ya kinga yeyote.
5/Kujigusa katika sehemu za Mwili za Siri (Sehemu za Haja Ndogo) kwa njia kiganja cha mkono wako. (Palm)
6/Kujigusa Sehemu Ya Haja Kubwa
SHEREHE
Vitendo Sita alivyovitaja Sheikh ndivyo ambavyo ukivifanya basi Udhu utakuwa umeharibika na itabidi ufanye Udhu Tena mara nyingine. Chochote kitakachotoka kutoka katika sehemu za Utupu yaani sehemu za Haja basi Udhu utakuwa umeharibika. Ukipitiwa na usingizi kwa njia ambayo una uhakika kwamba hakuna chochote kimetoka kutoka katika sehemu za haja kama vile Upepo au chochote kingine na hali hii inakuwa unaposinzia au kulala kwa Kukaa basi Udhu bado safi na hakuna tatizo isipokuwa ukihisi labda ulipitiwa na usingizi na hali kwamba umelala upande mmoja wa mwili na huenda labda kuna upepo ulikutoka basi Udhu unakua umevunjika.
Na Ukijikuta labda umemgusa Mwanamke kwa bahati mbaya yaani bila kukusudia kwa mfano ulikuwa katika Basi la usafiri au popote pale na Mwanamke huyo siyo katika wale MAHARIM (Maharim ni wanawake ambao Huruhusiwi Kuwaoa) yaani Mwanamke ambaye unaweza kumuoa basi Udhu wako utakuwa umetenguka na inabidi ufanye Udhu upya mara nyingine. Na hii ndiyo Shule ya Imamu Shafii inavyofundisha.
KUWAJIBIKA KUOGA
Yanayolazimu kuoga ni mambo sita:
Mambo Matatu Yanahusu Wanawake na Wanaume na Mambo Matatu Yanmhusu Mwanamke Peke Yake. Mambo Matatu Yanayolazimisha Mwanamke na Mwanamume Kuoga ni Yafuatayo:
1/Mume Na Mke wanapokuwa wamekutana au neno zuri Ni JImaa au Mwingiliano wa Kibinaadamu.
2/Kutoka kwa Manii (The male gamete, or sperm, and the female gamete, the egg or ovum)
3/Maiti
Na Mambo Matatu Yanamhusu Mwanamke Peke Yake na hayo ni kama yafuatayo:
1/Hedhi (Damu Ya Uke).
2/Nifasi (Damu Itokayo wakati wa Kuzaa na baada ya siku zifuatazo)
3/Kuzaa
SHEREHE
Mambo Sita aliyoyataja Sheikh Abi Shujaa ni lazima kuoga. Kwani mwili huwezi kuwa Tohara bila kuoga. Ili Uswali inabidi uwe na Tohara.
Hedhi Ni Damu Ya Uke katika kila Mwezi. (Menstruation, or period, is normal vaginal bleeding that occurs as part of a woman’s monthly cycle) Na NIfasi ni Damu inayotokana na Kuzaa. (bleeding that occurs from the obstetrician’s body up to forty days after giving birth). Kwa hiyo haya ndiyo mambo sita ambayo lazima uyazingatie katika maisha ya kila siku.
FARADHI ZA KUOGA NA SUNNA ZAKE
Faradhi za kuoga ni mambo matatu:
1/Kufanya Nia (Intention)
2/Kuondoa Najasi (Uchafu) katika Mwili iwapo kuna Uchafu wowote ule
3/Kufikisha Maji katika Nwele zote na Ngozi
Na Sunna Ni Mambo Matano:
1/Kutaja Basmala (Yaani Bismillahi Arahmani Arrahiym)
2/Kufanya Udhu kabla ya Kuoga.
3/Kujisafisha mwili mzima kwa kuutembeza mkono wako (katika viungo vyote ambavyo unaweza kuvifikia)
4/Ufuatilie Utraratibu Huu tukioutaja Kuanzia Namba 1 mpaka mwisho na usigeuze
5/Na unapooga utangulize Kulia na kisha Kushoto.
SHEREHE
Faradhi za Kuoga na Sunna Zake zinahusu Baada ya kutengua Udhu katika vile Vitengua Udhu tulivyovitaja hapa Juu. Na kwa hiyo ufuate hatua hizi tano tulizozitaja hapa juu na usigeuze mpangilio wake. Katika Kuoga Kila kiungo utangulize cha kulia kwanza kisha kushoto. Kwa mfano mkono wa kulia kwanza kisha wa kushoto na hata kama ukishindwa jitahidi angalau nia yako iwe hivyo.
05/April/2022 = Islamic Calendar 04/Ramadhan/1443
GHUSL-(UDHU MKUBWA) AU KUOGA
Sheikh Abi Shujaa anaendelea kusema katika MATNI yake kwamba Jumla Ya Sunnah za Kuoga kama zifuatazo:
1/Kuoga kabla ya Sala ya Ijumaa
2/Kuoga katika siku za EID Al-Fitr
3/Kuoga katika siku za EID Al-Adhha
4/Kuoga kabla ya Sala ya Al-Istisqaa
5/Kuoga kabla Ya Sala Ya Kusuf
6/Kuoga kabla Ya Sala Ya Khusuf
7/Kuoga baada ya Kuosha Maiti
8/Kafiri Anaposilimu
9/Mtu akizimia au Kupoteza Akili (Famamu)
10/Kuoga Kwa sababu ya Ihram Katika Sehemu zilizopo karibu na Mecca kabla Ya kufanya Hija au Umrah.
11/Kuoga kabla ya Kuingia Mecca
12/Kuoga katika Kusimama Arafah (Hija)
13/Usiku unapokuwa Muzdalifah (Hija)
14/Kuoga kabla ya Kutupia Vijiwe 7 Jamrah 3 katika Hija
15/Kuoga kabla ya Kutembea baina ya Safwa na Marwa mara 7 (Katika Hijaau Umrah)
16/Kuoga kabla ya Kuingia Mji wa Madina Munawara
SHEREHE
Ningependelea Kuelezea vipengele alivyovitaja Sheikh katika MATNI yake. Kwanza Kuoga kabla ya Sala ya Istisqaa ni Sunnah. Hii ni Sala inayofanywa ili kuomba Mwenyeezi Mungu ashushe Mvua. Ndugu Waislamu huswali sala hii kumuomba Mwenyeezi Mungu alete mvua. Sala ya Kusuf ni Wakati Jua limepatwa na Sala Ya Khusuf ni wakati Mwezi Umepatwa. Kwa kiingereza inajulikana kama. Solar Eclipse na Lunar Eclipse
(Salat ul-Kusuf (Arabic: صلاة الكسوف) is a prayer offered during a solar eclipse; Salat ul-Khusuf (Arabic: صلاة الخسوف) is performed during a lunar eclipse. They are both Nafl (non-obligatory) with two rakat prayers that should be performed by the Muslim).
Mtu anapopoteza fahamu kwa kuzimia au kuchanganyika akili kwa sababu yeyote ile kama vile maradhi basi atakapotoka katika hali hiyo tu Udhu Mpya wa Sala unabidi ufanywe tena.
Kabla ya Kuingia Mecca kwa hija kuna zile sehemu ambazo zinajulikana kama Miqaat na hapo ndipo Mahujaji na Wenye kufanya Umrah wanajiandaa kwa Kuoga na mengineyo ya kufanya Usafi kabla kuingia Mecca.
06/April/2022 = Islamic Calendar 05/Ramadhan/1443
KUSAFISHA KHUFAYNI(SOKSI AU VIATU)
Khufayni ni Soksi au aina ya viatu vya ngozi isiyokuwa haramu. Tutafanya sherehe baadaye na hivi sasa ningependelea kunakili maneno ya Shekhe wetu Bwana Abu Shujaa kuhusu Khufayni.
Kusafisha Miguu ambayo umevalisha Khufayni (Soksi au Viatu) inabidi usafishe Juu ya Soksi au Kiatu bila ya kuvivua kutoka katika miguu yako na baada ya hapo unaweza kuswali navyo bila tatizo maadamu umevisavisha vizuri.
Ufanye kama unavyofanya katika Udhu wa kawaida lakini itakuwa juu ya Soksi au Viatu na utatembea navyo ndani ya msikiti kama kawaida.
Maadamu umeondoa Najisi na ni safi basi hakuna tatizo lolote.
Lakini Sheikh anasema kwamba kuna Masharti matatu.
1/Uwe umevaa Soksi au Viatu baada ya Kuchukuwa Udhu kama kawaida.
2/Uhakikishe Soksi au Viatu zote mbili zimefunika zile sehemu za Miguu unazozifanyia Udhu kila siku. Yaani miguu mpaka Fundoni.
3/Uhakikishe Viatu na Soksi hizo unaweza kutembea nazo bila kizuizi.
Muda wa Kutumia Soksi na Viatu kwa Asiyekuwa Msafiri ni Mchana na Usiku mmoja. Na Mtu akiwa Safarini ni Siku Tatu na Usiku zake Tatu.
Muda huu utahesabika mara tu mtu anapovunja Udhu. Baada ya Muda huu kwisha itabidi avue Soksi au Viatu na Kufanya tena Udhu kama kawaida na baadaye avae tena Soksi au Viatu.
Ataanza kuhesabu muda huo tuliouelezea hapa juu. Yaani siku Moja na usiku wake kwa mkazi na siku tatu na usiku wake kwa msafiri.
Sheikh Abi Jahl anaendelea kusema kwamba Mtu akiosha miguu na hali kwamba ni Mkazi kisha akaamua kusafiri basi muda wa Udhu wake kama haukuvunjika katika muda wa Kuvaa Soksi au Viatu ni Siku moja na Usiku wake. Na hali kadhalika Hivyo hivyo akiwa Safarini kisha akaamua kukaa basi muda wa udhu wake utakuwa kama Mkazi yaani siku moja na usiku wake.
Vinavyobatilisha Khufayni ni mambi matatu:
1/Kuvua Khufayni
2/Muda wa Siku Moja na Usiku wake kwa Mkazi na Muda wa Siku Tatu na Usiku wake kwa Msafiri unapokwisha.
3/Na kila kinachoharibu Udhu na ikabidi Kuoga.
SHEREHE
Ukifikiri utaona kwamba hapo zamani Misikiti ilikuwa haina Mazulia ya kisasa(Carpets) na watu walikuwa wakivaa viatu hata Msikitini lakini viatu hivyo vilikuwa vikisafishwa vizuri kama tulivyotaja hapo juu yaani waislamu hawakuwa wakivaa viatu kama vile wakristo wa leo wanvyokwenda makanisani bali walikuwa waichukuwa Udhu juu ya viatu au soksi. Na pia hata leo kuna watu wengine bado wanatumia aina ya viatu au Soksi kwa ajili ya maradhi. Kwa hiyo dini ya kiislamu ni pana sana. Tumepewa Uchaguzi mbalimbali ili kurahisisha maisha. Wenye kujikuta hawana budi isipokuwa kuvaa viatu au soksi basi wanaruhusiwa lakini kwa masharti tuliyoyataja hapa juu. Usije ukaenda chooni na viatu kisha ukaenda msikitini kwa swala au kuswaki nyumbali na viatu au soksi ambazo umetembelea sehemu chafu. Kama Sheikh alivyosema lazima viatu au soksi ziwe safi na ufanye udhu vizuri kama vile ungekuwa hukuvaa yaani kama unavyofanya udhu mwilini.
07/April/2022 = Islamic Calendar 06/Ramadhan/1443
Alhamdulilahi Leo Mwenyeezi Mungu akipenda Nitaendelea na Mafundisho ya Sheikh Abu Shujaa. Kwanza Nitawaelezea MATNI yake kisha Nitafanya nyongeza ya Sherehe kuhusu MATNI hii.
TAYAMUM (DRY ABLUTION) AU KUFANYA UDHU KWA UDONGO
Ningependelea kuwakumbusha kwamba bado tupo katika Mlango wa TOHARA yaani Usafi. Katika MATNI Sheikh anasema yafuatayo kuhusu Tayamum.
Shuruti za Kutayamum au kufanya Udhu kwa kutumia Udongo ni Tano.
1/Kuwa na Udhuru wa Safari au Maradhi. (Ukiwa Safarini na Hakuna Maji au Una Maradhi ambayo huwezi Kufanya Udhu kwa Maji)
2/Kuingia kwa wakati wa Sala.
3/Kunapokuwa hakuna Maji
4/Kutokuweza kuyatumia Maji kutokana na udhuru wowote ule kama vile Maradhi.
5/Lazima uwe Udongo uliochanganyikana na Vumbi la udongo na kusiweko na Mchanga au Mchanga aina ya Gypsum.
SHEREHE
Kabla ya kuendelea Na Habari ya Tayamum yaani Faridha Zake, Sunnah Zake na Vyenye kubatilisha Tayammum ningependelea kusherehesha tuliyoyataja hapa juu kuhusu Aina Ya Udongo wa Tayamum.
Katika Madhehebu Manne ya Sunni wanatofautiana kuhusu aina ya Udongo ambao unaweza kutumika katika Kujisafisha kwa kutumia Tayamum. Kwa mfano Imamu Maliki anasema inawezekana kutumia Vijiwe vidogo vidogo (Pebles) katika Kutayamamu. Hapa katika website hii tunamzungumzia Imamu Shafii. Na Kitabu cha Abi Shujaa Kinatufundisha mafundisho ya Imamu Shafii. Kwa hiyo anaposema kwamba Udongo uliochanganyikana na Vumbi la udongo na kusiweko na Mchanga au Mchanga aina ya Gypsum. Hapa Gypsum ni aina ya Minerali ambayo inatumika katika kutengenezea Chaki na Vinginevyo.
Gypsum is a soft sulfate mineral composed of calcium sulfate dihydrate, with the chemical formula CaSO₄·2H₂O. It is widely mined and is used as a fertilizer and as the main constituent in many forms of plaster, blackboard/sidewalk chalk, and drywall.
Baada ya Sherehe hii Sasa tuendelee na MATNI ya Sheikh wetu.
Sheikh anasena kwamba Fardhi za Kutayamam ni Mambo Manne:
1/Kwanza Ni Nia
2/Kisha Ujisafishe au kupaka Uso
3/Kusafisha Mikono Miwili mpaka Katika Mafundo. (Mfano kama vile unavyofanya katika Udhu)
SHEREHE
Ili kufanya Tayamam Inabidi kwanza Uweke Nia kimoyomoyo kisha Upige Viganja vya mikono yako miwili chini yaani Juu ya Udongo unaokubalika kisha Upulize kupunguza Vumbi Vumbi) na Utumie viganja vya Mikono yako miwili kwa kujisafisha Uso wako kama kawaida yako unapofanya na maji. Kisha usafishe mikono yako miwili mpaka mafundoni. Na hii ndiyo Tayamum. Ukifanya hivi utakuwa una Udhu wa kuweza kusali bila Tatizo
Sasa tuendelee na MATNI ya Shekhe Wetu.
Sheikh anaendelea kutuelezea Sunnah za Tayamamu kwa kusema kwamba Sunnah za Tayamamu ni Tatu:
1/Kwanza Utaje Basmallah (Yaani useme kimoyomoyo Bismillahi Arrahmani Arrahim)
2/Kutanguliza viungo vyako katika kufanya Tayamamu Kulia Kisha Kushoto.
3/Usiruke Utaratibu wa Kufanya Tayamamu
SHEREHE
Kila mara utangulize kulia kisha kushoto. Yaani kwanza utumi mkono wa kulia kusafisha mkono wa kushoto na kisha ufuatilie na mkono wa kushoto na kusafisha mkono wa kulia. Usigeuze au kukata utaratibu wa Tayamamu. Yaani Usianze kusafisha Mikono kisha Uso au Kusafisha Uso tu Pekee bali ufuate mpangilio tulioutaja.
Sasa tuendelee na MATNI ya Sheikh
Vinavyobatilisha Tayamum ni Mambo Matatu
1/Vyenye Kubatilisha (Kuharibu) Udhu ni hivyo hivyo ambavyo vitabatilisha Tayamum
2/Kuona au Kupata Maji kabla ya Sala.
3/Kutoka katika Uislamu.
SHEREHE
Kinachoharibu Udhu kwa kutumia maji ndiyo pia kinaweza kuharibu udhu ukifanya kwa Udongo, yaani Tayamamu Sheria ni ile ile.
Na pia Tayamum itaharibika mara tu ukipata Maji.
Kwani unafanya Tayamamu kwa sababu hakuna maji na mara tu ukiyapata kabla ya sala basi ufanye udhu tena kwa kutumia maji.
Ukitoka katika dini ya kiislamu kwa Matamko au Kitendo kinachopinga dini basi Udhu wa Tayamamu utakuwa umeharibika.
Sheikh Abi Jahl anamalizia Mafundisho ya Tayamamu kwa kusema kwamba:
TAYAMUM JUU YA BANDEJI
Mtu akiwa ametumia Bandeji kwa ajili ya Jeraha (Kidonda) inabidi afanye Tayamam au Udhu kwa kupaka Maji kidogo Juu ya Bandeji kama kawaida na afanye hivyo katika kila sala za Faradhi (Yaani sala 5 za Siku) lakini idadi ya Sala za Sunnah anaweza kuzifanya kama apendavyo kwa Tayamum Moja pekee. Na baada ya kufanya Udhu Aswali kama kawaida.Hivi ndivyo MATNI Ya Abi Shujaa inavyosema kufuatana na mafundishi ya Imam Shafii
SHEREHE
Yaani Tayamum Moja inatosha kwa Sala za Sunnah zote kama unavyopenda na siyo lazima kufanya Tayamamu katika kila Sala za Sunnah. Lakini Sala za Faradhi yaani sala 5 za kila siku itabidi ufanye Tayamamu kabla ya Kila sala. Na ikiwezekana na kama hakuna tatizo unaweza kufanya Udhu juu ya bandeji na kama hakuna Tatizo lolote. Sheikh hakufafanua habari hii. ikiwa Maji yataleta matatizo juu ya Bandeji kuilowanisha na kuleta Matatizo basi ufanye njia nyingine kama vile uchukuwe Plastic juu ya Kidond na kisha ufanya udhu juu ya Plastic au nguo yeyote ambayo itazuia maji kupenya ndani ya Bandeji au kama ikiwezekana kuondoa Bandeji na kufanya Udhu bila kuleta Matatizo basi unaweza pia kufanya hivyo. Kwa kifupi usilazimishe mambo katika Dini. Dini inatuonyesha njia mbalimbali za kuzuia Madhara kwa hiyo siyo kujilazimisha bure bure bila sababu. Ufanye Udhu kama inawezekana na kama haiwezekani basi tafuta njia rahisi iliyo bora. Dini ni Rahisi na siyo ngumu. Simple.
Alhamdulilahi leo tumemaliza Mafundisho ya Tayamamu.
Inshallah Bado hatujamaliza Mlango wa Tohara tutaendelea Mwenyeezi Mungu akipenda Kesho au siku zifuatazo za mwezi huu Inshaallah.
17/April/2022 = Islamic Calendar 16/Ramadhan/1443
Alhamdililah kwa kila alichotupa na kila asichotupa. Baada ya Dua hii nitaendelea na Kufasiri MATNI ya Sheikh Abi Shujaa ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiarabu kwa njia Ya ufupisho na historia inasema kwamba Shekhe huyu aliamua kuelezea Sheria za Fiqh kwa Kugawanya Milango mbali mbali. Aliitikia mwito wa wanafunzi wake kwani walipendelea Elimu hii iandikwe kwa Lugha na Mpangilio ulio Rahisi na Alhamdulilahi akafanya hivyo na Ndio Hii MATNI yake ambayo tunaisoma leo hii.
Leo Tutasoma Mlango wa NAJASA ambao kwa lugha ya kiswahili tunaweza kufasiri kama ni UCHAFU amabo lazima uusafishe au uuondoe.
Anasema Sheikh kwamba Maji Yanayotoka Kutoka katika mwili wa Binaadamu katika njia mbili yaani Njia mbili ni Utupu au zile njia za Kwenda Haja ni NAJASI au kwa kiingereza “Impure” Na hata MADHIY (MADHIY nii yale majimaji yanayotoka kutokana na Shahawa inapokuzidi kutokana na Fikra za Kibinaadamu). Yaani lazima ujisafishe vizuri. Lakini MANII ambayo yanatoka kwa Binaadamu au kwa Kiingereza SPERMS siyo NAJASI kwani Mwenyeezi Mungu amevikirimu. Huwezi Kuswaki na Najasi yeyote.lakini MANII au SPERMS siyo NAJASI. Sheikh anaendelea kusema kwamba kusafisha Mikojo na Choo (Mavi) ni Wajibu yaani Lazima isipikuwa MIKOJO ya Mtoto ambaye bado hajaanza kula chakula chochote yaani ambaye bado ananyonya. MIKOJO hiyo inatoharika au kusafishika kwa njia ya Maji. Siyo lazima Maji mengi bali kidogo kiasi cha kuondoa MIkojo hiyo na itatosha.NAJASA zote lazima zisafishwe au ziondolewe isipokuwa DAMU na USAA ambao sharti uwe Kidogo sana kwani huwezi kusafisha kama ukiwa na Kidonda. na Pia DAMU YA vijidudu ambavyo havina DAMU inayotembea katika miili yao kama vile Sisimizi au Nzi na hivi vikiangukia katika Chombo chochote Havinajisishi kwani Viumbe hivi havina NAJISI.
Sheikh anaendelea kusema kwamba Kila Mnyama aliyekuwa Hai ni TOHARA isipokuwa MBWA na NGURUWE.Na Kizaliwa cha wanyama hawa wawili pia Ni Najisi. Na kama tulivyoelezea hapo mwanzo kwamba Ngozi ya Wanyama hawa wawili pia ni NAJISI.
MAITI za Viumbe vyote ni NAJISI isipokuwa SAMAKI, NZIGE NA BINAADAMU.
Chombo chochote ambacho Mbwa au Nguruwe amevilamba basi itabidi uvisafishe kwa udongo mara Sita na Mara ya Saba iwe kwa Maji.
Na NAJISI zinginezo zote itabidi uziondowe kwa kusafisha Mara Moja lakini ukisafisha Mara Tatu ni Bora.
Pombe yeyote ikigeuka na Kuwa SIKI kwa yenyewe bila kuguswa basi SIKI hiyo ni TOHARA na hainza tatizo kuitumia lakini Pombe hiyo ikibadilishwa na Kuwa SIKI kwa Kuongezwa na kitu chochote kile basi SIKI hiyo haifai kuitumia yaani inakuwa siyo TAHARA bali NAJISI.
Haya ndiyo mafundisho ya Imamu Shafii. Hapa tunafundishwa na Hakimu bwana Abi Shujaa katika MATINI yake.
Katika Mlango wa TAHARA kumebakia Mlango mmoja ambao nitauelezea hapa chini na huu ndio mlango wa mwisho wa TAHARA na baadaye Mungu akipenda tutaingia katika Mlango wa SWALA.
Sheikh Abi Shujaa Anaendelea Kutufahamisha kwamba Damu Zinazotoka Kwa Mwanamke Ni Aina Tatu:
1/Damu Ya HEDHI
2/Damu Ya NIFASI
3/Damu Ya ISTIFADHA
Damu Ya Hedhi ni Damu inayotoka Kwa Mwanamke wakati anapokuwa na Afya kama kawaida
Damu Ya NIFASI Ni Damu inayotoka kwa Mwanamke baada tu ya Kuzaa
Damu Ya ISTIFADHA ni Damu ambayo inayotoka kwa Mwanamke katika zile siku zisizokuwa za HEDHI na NIFASI
SHEREHE
Sayansi za Kisasa zinatupa Misamiati ambayo ningependelea kuitaja hapa chini na pia Maelezo yanayohusiana na Habari hizi.
DAMU YA HEDHI inajulikana kama Menstrual Blood.
(The menstrual blood is partly blood and partly tissue from inside the uterus)
DAMU YA NIFASI
Hii ni damu inyofuata Kuzaa na inajulikana kama LOCHIA
(Lochia is the vaginal discharge you have after giving birth. It contains a mix of blood, mucus and uterine tissue. It has a stale, musty odor like menstrual period discharge and can last several weeks. Lochia is heavy at first but gradually subsides to a lighter flow until it goes away)
DAMU YA ISTIHADHA inajulikana kama Metrorrhagia siyo damu ya Mwezi kama inavyoelezewa hapa chini na Wataalamu.
(Metrorrhagia, now commonly called intermenstrual bleeding, is vaginal bleeding that occurs at irregular intervals not associated with the menstrual cycle. While the blood comes from the uterus as it does during menstruation, the bleeding does not represent a normal period)
Sheikh Abi Shujaa anaendelea Kuelezeas kwamba Muda Mfupi kabisa wa HEDHI ni Usiku na Mchana na Mkubwa Kabisa ni Siku Kumi na Tano.Na Muda wa Kawaida ni Siku Sita au Saba.
Na anaendelea Na Muda wa Damu ya NIFASI kwamba Muda Mfupi kabisa wa NIFASI ni Mara tu Baada ya Kuzaa yaani Mara Moja tu Pekee. Na Muda unaweza Kurefuka Kutoka Damu na Kufikia Siku Sitini. Na hii inategemea Na mtu mwenyewe kwani Binaadamu wanatofautiana. Na Kawaida Ya Muda wa Damu ya Nifasi ni siku Arubaini.
Muda Mfupi sana Baina Ya Hedhi Mbili ni siku Kumi na Tano. Na masiku haya yanaweza Kurefuka na hakuna Kipimo (Limit).
Muda Mfupi sana (Limit) wa HEDHI ni miaka Tisa. (kwa maana haiwezekani kuwa chini ya hapo) na Hakuna Kipimo baada ya Miaka tisa yaani inaendelea zaidi ya miaka tisa.
Kuhusu Mimba Sheikh anasema kwamba Muda wa Mimba ulio mdogo sana ni Miezi Sita, Na Mudas mkubwa sana ni Miaka Minne na Muda wa Kawaida ni Miezi Tisa.
Anasema Sheikh kwamba Kuna Mambo manane ambayo yameharimishwa kuyafanya kwa Mwenye HEDHI na NIFASI na mambo hayo ni kama yafuatayo:
1/Kuswali
2/Saumu
3/Kusoma Kuruani
4/Kuugusa Msahafu na Kuubeba
5/Kuingia Msikitini
6/Kufanya TAWAFU huko Hija au Umra (Mecca)
7/Makutano ya Kibinaadamu baina ya Mume na Mke (JIMAA).
8/Mume asimguse au Kumpapasa Mke kwa lengo lolote lile baina ya Kitovu na Magoti (Miguu) na hata kwa ajili ya kutafuta Raha yeyote ile.
SHEREHE
Uislamu haukubakiza kitu. Umefundisha kila kidogo na kila kikubwa hakuna kilichabakia. Kumetaja mambo mengine ambayo hakuna budi kama vile Elimu ya Biology. Fiqh imechambua hata Uchi wa Binaadamu na Uhusiano baina ya mume na Mke. Na hii ni katika Kumfundisha binaadamu. Sheikh hapa anasema kwamba Mume amwache Mke akiwa katika Hedhi na Nifasi. Asitamani kumgusa gusa au kumpapasa sehemu hizo tulizozitaja hapa juu na pia Asitamani zaidi ya hayo. Asifanye Ulafi wa kumsumbua Mke mpaka Damu hizo itakaposimama.
Na ni haramu kwa Mwenye Janaba Mambo Matano:
1/Sala
2/Kusoma Kuruani
3/Kuugusa Msahafu na Kuubeba
4/Kufanya Tawafu (Huko Mecca katika Hija ayu Umra)
5/Kukaa Msikitini
Unapoharibu Udhu kwa sababu ya Kitengua Udhu. Yaani sababu yeyote miongoni mwa Vitengua Udhu (Vitengua Udhu nimevifasiri Katika Mlango Huu hapo Mwanzoni) basi Inabidi ujiepushe na Mambo Matatu.
1/Sala
2/Kufanya TAWAF (Huko Mecca kwa Hija au Umrah)
3/Kugusa Msahafu na Kuubeba
Alhamdulilah Nimemaliza Mlango wa Tohara na Mwenyeezi Mungu Akipenda nitaanza Kesho au siku zifuatazo na Safari Ndefu Ya Mlango Mpya wa “SALA” Inshaallah. Na baada ya Hapo itafuatiwa na Milango ya Zakat kisha Saumu kisha Hija na Milango Mingineyo Mbalimbali ambayo nitaielezea katika siku za mbeleni Mwenyeezi Mungu akitupa Uhai.