SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Herufi/Maneno/Aya

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

TAFSIRI YA NENO ٱلۡفَلَقِ KUTOKA KATIKA SURA YA AL-FALAQ (MAANA ZAIDI YA MOJA)

Neno ٱلۡفَلَقِ kutoka katika Sura Ya AL-FALAQ Lina maana kubwa iliyokusanya Maumbile ya Viumbe vyote Ulimwenguni.

Tafsiri za kuruani zinatupa maana zaidi katika kulifasiri Neno ٱلۡفَلَقِ.

Kuna Tafsiri yenye kusema kwamba Neno hili mana yake ni Ulimwengu na Kuna Nyingine inayosema kwamba Ni  “Kupasuka”. Tusibabaike kwani Tafsiri zote Mbili ni Sahihi. Kuna Ushahidi mbalimbali kutoka katika kuruani zinazothibitisha Tafsiri hizi mbili. Kupasuka ndiyo chanzo cha maumbile ulimwenguni. Sherehe hapa chini inafafanua zaidi habari hii.

TAFSIRI AYA YA KWANZA NA YA PILI YA SURA YA AL-FALAQ

سُوۡرَةُ الفَلَق

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ

ٱلرَّحِيمِ قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ (١) مِن شَرِّ مَا خَلَقَ (٢) وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا

وَقَبَ (٣) وَمِن شَرِّ ٱلنَّفَّـٰثَـٰتِ فِى ٱلۡعُقَدِ (٤) وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ (٥)

USHAHIDI WA KWANZA

1/Kuja kwa Asubuhi baada ya Kupasuliwa kwa Giza la Usiku Na Mwanga Wa Jua. (Pambazuka)

Ushahidi Wa Kwanza Kutoka Sura Namba 6 Aya Namba 96

Inafasiri Neno Hili kwa maana Ya Kupambazuka. yaani Kupasuka kwa Asubuhi

فَالِقُ ٱلۡإِصۡبَاحِ وَجَعَلَ ٱلَّيۡلَ سَكَنً۬ا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ حُسۡبَانً۬ا‌ۚ ذَٲلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ

(٩٦)

TAFSIRI

96.Ndiye anayepambazua (Kuupasua Usiku kwa Mwanga wa Jua) mwangaza wa asubuhi;na ameufanya usiku kuwa mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Huo ndio mpimo (mtengenezo) wa Mwenye nguvu(na)ajuaye.

USHAHIDI WA PILI.

Tafsiri Kutoka Katika Sura Ya Al-Anaam inafasiri Neno Hili kwa maana ya Kupasuka yaani kupasuka kwa Mbegu

TAFSIRI

۞ إِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلۡحَبِّ وَٱلنَّوَىٰ‌ۖ

Sura Namba 6 Aya Namba 95

95.Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji (mwoteshaji) wa mbegu na kokwa (zikawa miti).

Kupasuka kwa Mbegu katika Ardhi wakati wa Germination (Angalia Video Hapa Chini uone Namba Mbegu inapopasuka ardhini na kisha inapopasua udongo juu yake na kukua).

USHAHIDI WA TATU

3/Katika Reproduction (Elimu ya Kizazi)Mbegu ya Baba na Mama zinapokutana Zinaungana na Kusababisha Cell Moja Kubwa inayojulikana kwa jina ZYGOTE na Hii inapasuka na kisha zinagawanyika na kuwa Cells Mbili. Na baada ya hapo zitagawanyika tena na kuwa Cells 4 na hivyo hivyo ndivyo kila kiungo cha mwili kitaendelea kuwa kikubwa kwa njia hiyo na hatimaye kuzaliwa mtoto. Viungo vya mtoto vitaendelea kukua kwani Cells za viungo hivyo zitaendelea kupasuka na kugawanyika hatimaye atakuwa mtu mkubwa. Mgawanyiko (Mpasuko) wa aina hii unajulikana kama MITOSIS AND MEIOSIS. MITOSIS hufanyika katika Maumbile ya Binaadamu isipokuwa VIRUSI (VIRUS) na MEIOSIS hufanyika katika maumbile Ya Mimea, Wanyama na Fungi (Angalia Picha hapa Chini zinazoelezea habari hizi)

Katika Sura Namba 39 Aya Namba 6 Mwenyeezi Mungu anatufahamisha kwamba amemuumba binaadamu katika Stages mbalimbali. (Stages hizi zinahusu kugawanyika kwa Cells na kukua kwa Viungo vya mwili). Maana Tunayopata katika Aya hii ni kwamba Viungo vya Binaadamu vitakua kwa njia tuliyozungumzia hapa Juu yaani MITOSIS. Cells zitagawanyika na Kukua. Stages hizi ndizo zinazozungumziwa katika Aya hapa chini. Yaani HATUA za Maumbile katika kukua inabidi Cells Zipasuke na kugawanyika. Mgawanyiko huu ndiyo asili yetu na viumbe vyote vyenye uhai duniani kama vile Binaadamu, Miti, Wanyama, vijidudu, na vinginevyo.

Sura Namba 39 Aya Namba 6

يَخۡلُقُكُمۡ فِى بُطُونِ أُمَّهَـٰتِڪُمۡ خَلۡقً۬ا مِّنۢ بَعۡدِ خَلۡقٍ۬ فِى ظُلُمَـٰتٍ۬ ثَلَـٰثٍ۬‌ۚ

TAFSIRI

Amekuumbeni Katika Matumbo ya Mama Zenu Umbile baada ya Umbile katika Giza Tatu (Giza laTumbo,  Giza la Tumbo la kizazi na Amniotic Sac)

The three zones within the mother’s womb protect the fetus against all sorts of dangers. These are: 1- The abdominal wall, 2- The uterine wall, and 3- The amniotic sac.

USHAHIDI WA NNE

Katika Sura Ya Al-Muuminun Namba 23 Aya Namba 12 mpaka Aya namba 14 tunaelezwa kuhusu Stages za Kukua Mtoto katika Tumbo la mama na kukua huku kunategemea Mpasuko na mgawanyiko wa Cells kama tulivyoelezea hapa juu. Stages zote hapa chini katika Aya hii zinategemea Sayansi hii ya Kugawanyika kwa Cells (Mitosis). Na huwezi kugawanya kitu bila ya kukipasua.

Sura Ya Al-Muuminun Namba 23 Aya Namba 12 mpaka Aya namba 14

وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن سُلَـٰلَةٍ۬ مِّن طِينٍ۬ (١٢) ثُمَّ جَعَلۡنَـٰهُ نُطۡفَةً۬ فِى قَرَارٍ۬ مَّكِينٍ۬ (١٣) ثُمَّ خَلَقۡنَا ٱلنُّطۡفَةَ عَلَقَةً۬ فَخَلَقۡنَا ٱلۡعَلَقَةَ مُضۡغَةً۬ فَخَلَقۡنَا ٱلۡمُضۡغَةَ عِظَـٰمً۬ا فَكَسَوۡنَا ٱلۡعِظَـٰمَ لَحۡمً۬ا ثُمَّ أَنشَأۡنَـٰهُ خَلۡقًا ءَاخَرَ‌ۚ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ أَحۡسَنُ ٱلۡخَـٰلِقِينَ (١٤)

TAFSIRI 

12.Na kwa yakini tulimuumba mwanadamu kwa udongo ulio safi.

13.Kisha tukamuumba kwa tone Ia manii,(mbegu ya uzazi) lililowekwa katika makao yaliyohifadhika.

14·Kisha tukalifanya tone hilo kuwa pande Ia damu, na tukalifanya pande Ia damu hilo kuwa pande Ia nyama, kisha tukalifanya pande Ia nyama hilo kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama, kisha tukamfanya kiumbe kingine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.

USHAHIDI WA TANO

Mbingu na Ardhi zilikuwa kitu kimoja na Kama Mwenyeezi Mungu anavyosema katika Kuruani kwamba Huo Mgando ulioshikamana wa Mbingu na Ardhi ulipasuka na kisha mpasuko ukafanyika na baada ya hapo ikafuatilia kuumbwa Dunia, Nyota Na Mengineyo katika Mbingu na Ardhi. Process hii ya Kupasuka inajulikana katika Sayansi za Anga kama “BIG BANG” (Nilizungumzia habari hizi za BIG BANG Kwa Urefu katika sehemu nyinginezo na Video za Mwandalizi za Website Hii) Katika Kuruani Sura Namba 21 Aya Namba 30 Inatupa uhusiano wa Neno FALAQ na FATAQ kwa kiswahili tunaweza kufasiri kwa neno moja la “KUPASUA” lakini Katika Kiarabu kuna tofauti ndogo ndogo kati ya Maneno haya mawili.

Sura Namba 21 Aya Namba 30

أَوَلَمۡ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ ڪَانَتَا رَتۡقً۬ا فَفَتَقۡنَـٰهُمَا‌ۖ وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَىۡءٍ حَىٍّ‌ۖ أَفَلَا يُؤۡمِنُونَ (٣٠)

TAFSIRI

30. je! hawakuona wale waliokufuru ya kwamba mbingu na ardhi vilikuwa vimeambatana, kisha tukaviambua, (tukavipambanua au kuvipasua): Na tukafanya kwa maji kila kitu kilicho hai. Basi jee hawaamini?

Kwa kuzingatia Aya za Kuruani Hapa Juu Tunaweza kufasiri Aya za kwanza na ya pili Ya Sura Ya Al-Falaq kama ifuatavyo:

Tafsiri Ya Aya ya kwanza na ya pili ya Sura Ya Al-FALAQ itakuwa kama ifuatavyo

قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلۡفَلَقِ (١) مِن شَرِّ مَا خَلَقَ (٢)

TAFSIRI

1.Sema, Najikinga Kwa Mola wa Ulimwengu (au Malimwengu) Wote (kwani yeye ndiye aliyeumba Mipasuko ambayo imezalisha na inazalisha vinginevyo ulimwenguni kwa hiyo Yeye ndiye anamiliki vyote ulimwenguni) Na Kwa Shari ya Alivyoviumba

2.Aya ya Pili inathibitisha haya tuliyosema kwani tunafundishwa na Mwenyeezi Mungu tumuombe atulinde na Shari zinazotokana na Viumbe Vyake).

VIDEO  na Picha hapa Chini zinaonyesha

-Kupasuka na Kugawanyika kwa Cells za Viumbe venye uhai

-Kupasuka kwa Mbegu na kuota. Usiharakishe fanya Subira na Uiangalie. Mizizi Inaota polepole na Pia Mengineyo. Udongo unapasuliwa na na kuendelea kuota. Fanya Subira katika Kuangalia. 

-Nadharia ya BIG BANG  yaani Mpasuko wa Mbingu na Ardhi na kisha Mwenyeezi Mungu akaumba kila kitu baina ya Mbingu na Ardhi.  Allahu Akbar.

PICHA

Kupasuka, na Kugawanyika kwa Cells (Celi). Viumbe Vyote Vyenye Uhai Vinapitia katika Stages Hizi. Mbegu ya Kiume na Kike hugawanyika kwa njia ya kupasuka. Na huendelea hivyo katika maisha ya Viumbe vyote. Na hii ndiyo njia inayosababisha Kukua kwa Viungo Vyetu. Na Tunaelewa vizuri zaidi Maana ya neno AL-Falaq Katika Kuruani.Allahu Akbar. Akbar

VIDEO 1

Ukuangalia VIDEO usiharakishe. Subiri na Uangalie mpaka mwisho.
Angalia Mbegu Inavyopasuka na kuota na Kisha Inapasua Udongo na kuendelea Kuota. Allahu Akbar. Je tafsiri Ya neno FALQ imefahamika? Allahu Akbar. Kwa Kweli Mwenyeezi Mungu ni Mola wa Vyenye KUPASUKA.

VIDEO 2

BIG BANG imeelezwa vizuri. Inathibitisha Aya Ya Kuruani katika Maelezo yetu hapa Juu. Mpasuko uliotokea ukafuatwa na Kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi na kila kilichomo baina yake. Je unaona Maana Ya FALAQ inavyoeleweka vizuri zaidi
Na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akasema “Mola wa Vyenye Kupasuka”

SURA YA AL-KAFIRUN NA HEKIMA KATIKA MATUMIZI YA MANENO YAKE

Sura Ya Al-Kafirun  Namba 109  Aya 1 Mpaka 6

سُوۡرَةُ الکافِرون

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

قُلۡ يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡڪَـٰفِرُونَ (١) لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ (٢) وَلَآ أَنتُمۡ عَـٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ (٣) وَلَآ أَنَا۟ عَابِدٌ۬ مَّا عَبَدتُّمۡ (٤) وَلَآ أَنتُمۡ عَـٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ (٥) لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِىَ دِينِ (٦)

TAFSIRI

1. Serna:Enyi makafIri

2. Siabudu mnachoabudu.

3·Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu.

4·Wala sitaabudu mnachoabudu.

5.Wala nyinyi hamtaabudu ninayemuabudu.

6.Nyinyi mna dini yenu nami nina dini yangu

SABABU YA KUSHUKA  SURA HII       

Makafiri wa Makka walipojiona wamechoka, hawawezi kuzima nuru ya Uislamu, na wakamuona Mtume (s.a.w.) kila siku anizidi hima katika kazi yake, na dini kila siku inaendelea mbele, walimwendea Mtume wakamtaka washirikiane naye katika ibada, wao wamuabudu Mwenyezi Mungu mwaka mmoja pamoja naye, na Waislamu  waabudu Miungu Yao Mwaka Mmoja vile vile; yaani mwaka mmoja Makafiri na Waislamu waabudu Mungu wote Kwa pamoja na mwaka Unaofuatia Makafiri na Waislamu waabudu masanamu wote kwa pamoja Ndipo iliposhuka Sura hii.

Na makusudio yake ni haya: Nyinyi muna Mungu wenu na namna ya ibada zenu muabudiazo, na mimi nina Mungu wangu  na namna ·ya ibada nimuabudiayo.

Haiwezekani kuchanganya baina ya Mungu Wangu wa kweli na Miungu yenu ya uwongo, wala baina ya ibada yangu ya haki na ibada zenu za batili. Nyjnyi muna dini yenu na itikadi yenu; na mimi nina dini yangu na itikadi yangu.                                                                                        

HEKIMA YA LUGHA ILIVYOTUMIKA KATIKA AYA HIZI 

قُلۡ يَـٰٓأَيُّہَا ٱلۡڪَـٰفِرُونَ (١)

لَآ أَعۡبُدُ مَا تَعۡبُدُونَ (٢)

وَلَآ أَنتُمۡ عَـٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ (٣)

وَلَآ أَنَا۟ عَابِدٌ۬ مَّا عَبَدتُّمۡ (٤)

وَلَآ أَنتُمۡ عَـٰبِدُونَ مَآ أَعۡبُدُ (٥)

لَكُمۡ دِينُكُمۡ وَلِىَ دِينِ (٦)    

Tukichunguza Aya Katika Sura Hii Utaona  Kitendo Neno   أَعۡبُدُ   katika Aya Namba 3 na 5  ni Kitendo chenye maana ya “Wala nyinyi hamtaabudu ninayemuabudu”  Neno Hili  halikubadilika katika Matumizi kama tunavyoona. Aya zote mbili zimetumia Neno  hili bila mabadiliko.

Katika Aya namba 2 Neno تَعۡبُدُونَ  limetumika na Katika Aya namba 4 Neno عَبَدتُّمۡ  Limetumika. Tafsiri ya maneno haya mawili ni  “Mnayemuabudu” na “Mliyemuabudu” yaani Maneno haya mawili yana maana moja lakini tunaona yote mawili hayalingani kufuatana na wakati. kwanza ni katika wakati huo Mtume alipokuwa akihojiana na hao Makafiri na Pili ni Wakati Uliopita.  La kwanza ni TAABUDUNA  na la pili ni  ABADTUM.

Katika Kutofautiana maneno haya Kuna Hekima kubwa.

Neno أَعۡبُدُ   Lina maana ya Ninayemuabudu. na Kwa hiyo  Katika Aya namba 3 na 5  Neno hili  halikubadilika kwani Mwenyeezi Mungu ni Mmoja tu. Ni Yule yule habadiliki.

Lakini katika Aya namba 2 na 4  Maneno mawili Yametumika na  ijapokuwa yana maana moja lakini yametofautiana kufuatana na Wakati “MNAYEMUABUDU” na “MLIYEABUDU” (Yaani Kuyaabudu yale Masanamu) Maneno haya mawili  yaani  TAABUDUNA  na ABADTUM yametofautiana. La kwanza ni Present Tense na La Pili Past Tense. Hii inaonyesha Miungu ya Masanamu yanavyobadilika badilika. Hapo zamani waliabudu masanamu na baadaye pia Masanamu Mengineyo. Kubadilika Kwa Maneno hapa kuna maana Ya Kubadilika Kwa Miungu ya Bandia.

Hii Ndiyo hekima ya  Kutokubadilika kwa neno أَعۡبُدُ  katika Aya Mbili (3 na 5) 

Na Kubadilika kwa Maneno تَعۡبُدُونَ   na عَبَدتُّمۡ  katika Aya Mbili (2 na 4)

Na Mwenyeezi Mungu anajua Zaidi. Kuna Mengi Mengineyo ambayo hatuyajui. Allahu Akbar.                                                                                                                                                                                                       

SURA YA AL-ANFAL NAMBA 8 AYA NAMBA 33

Hekima ya Matumizi ya Maneno لِيُعَذِّبَهُمۡ na مُعَذِّبَهُمۡ katika Sura Namba 8 Aya Namba 33

Sura Ya Al-Anfal Namba 8 Aya Namba 33

Kila Herufi, Neno au Aya limewekwa mahali pake katika Kuruani Tukufu na kwa hekima kubwa sana.

Katika Aya Ifuatayo Maneno mawili  لِيُعَذِّبَهُمۡ na مُعَذِّبَهُمۡ yaana maana moja ya “Kuadhibisha“. lakini kuna Tofauti ya  Makusudio.

وَمَا ڪَانَ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمۡ وَأَنتَ فِيہِمۡ‌ۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمۡ وَهُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ (٣٣)

TAFSIRI

33.Lakini Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu maadamu wewe (Nabii Muhammad) umo pamoja nao hapa Makka), wala Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu pia bali ya kuwa (baadhi yao wamesilimu) wanaomba msamaha.

SHEREHE

وَمَا ڪَانَ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمۡ وَأَنتَ فِيہِمۡ‌ۚ 

Katika Kipande hiki cha kwanza Mwenyeezi Mungu ametumia Neno  لِيُعَذِّبَهُمۡ   lenye maana ya kuadhibisha

وَمَا كَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمۡ وَهُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ

Na katika Kipande hiki cha pili Mwenyeezi Mungu ametumia Neno مُعَذِّبَهُمۡ  lenye maana ya Kuadhibisha pia

Ukijiuliza Suali Kwa nini Mwenyeezi Mungu asitumie neno Muadhibuhum katika Kipande cha kwanza 

وَمَا ڪَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمۡ وَأَنتَ فِيہِمۡ‌ۚ

na ingekuwa hivyo basi Aya ingekuwa na Maneno mawili yenye kufanana na Pia Maana itakuwa  ile ile ya “Kuadhibisha

Mfano kama ifuatavyo.

وَمَا ڪَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمۡ وَأَنتَ فِيہِمۡ‌ۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمۡ وَهُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ (٣٣)

Kilugha hakuna Tatizo katika kutumia Neno مُعَذِّبَهُمۡ  katika Vipande hivi viwili.

Lakini Kuna Hekima Kubwa ya Mwenyeezi Mungu  Kutumia haya maneno Mawili .لِيُعَذِّبَهُمۡ   na مُعَذِّبَهُمۡ  na siyo bure bure.

وَمَا ڪَانَ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمۡ وَأَنتَ فِيہِمۡ‌ۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمۡ وَهُمۡ يَسۡتَغۡفِرُونَ (٣٣)

GRAMMAR (SARUFI)

Neno لِيُعَذِّبَهُمۡ  ni Kitendo  (VERB)  الفعل )(Al-Fi’l)

Na neno مُعَذِّبَهُمۡ  ni  Nomino Mtendaji (Doer Noun) اسم الفاعل

(Ismu  Fail)

لِيُعَذِّبَهُمۡ  Neno Hili katika Aya Hii lina maana kwamba Mwenyeezi Mungu hatawaadhibu Hao Makafiri wa Mecca Maadamu Mtume Mohamed (Sala Na Amani Ya mwenyeezi Mungu Zimfikie) yupo pamoja nao. (Yaani Mtume alikuwa akiwaombea Dua wasiadhibiwe) Na kwa hiyo Kitendo hiki ni kwa muda tu ule ambao Mtume alikuwa Hai.

 مُعَذِّبَهُمۡ Lakini Neno Hili la pili katika Aya Hii lina maana kwamba Mwenyeezi Mungu hatawaadhibu Hao Makafiri wa Mecca Milele maadamu wanaomba Msamaha (Maghfira)yaani Wanatubia kila mara.  

Kwa Hiyo Tafsiri  itakuwa kama ifuatavyo

33.Lakini Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu maadamu wewe (Nabii Muhammad yumo pamoja nao hapo Makka. Yaani Adhabu ni ya muda ule ambao Mtume yupo Hai pamoja nao), wala Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu pia bali ya kuwa (baadhi yao wamesilimu) wanaomba msamaha. (Adhabu Wataepushiwa maadamu Wanaomba Msamaha au Maghfira mpaka mwisho wa maisha yao)

Kwa hiyo hii ndiyo hekima ya Tofauti ya haya maneno mawili. La kwanza Mwenyeezi Mungu katumia  VERB  yaani Kitendo cha Muda (Verb ni Kitendo chochote chenye  maana ya Muda uliopita, tulionao na kinachokuja kwa hiyo ni cha muda  na siyo milele)   na Neno la pili ni  Doer Noun (Nomino Mtendaji)ambalo lina maana ya Kitendo kisichokuwa na Kipimo (Yaani Timeless).

Je unaona Hekima?  Kila Neno Katika Kuruani Limepimwa.  Allahu Akbar. Na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi Iwapo siyo hivyo. Allahu Akbar.

HEKIMA YA KUTANGULIA KWA ألخبر AL-KHABAR (Predicate) Kabla Ya ألمبتدأ Al-Mubtadaa (Sublect) Katika Aya Za Kuruani Tukufu

Katika Lugha ya Kiarabu Kuna Sababu mbalimbali za Kilugha au Kibalagha (Linguistically and Rhetorically) ambazo zinasababisha Kutangulia Kwa Predicate kabla ya Subject katika Sentensi.

Nitaelezea Sababu Mojawapo kwa kutumia Mifano ya Aya Mbili Zifuatazo ili tupate kuielewa Kuruani Vizuri zaidi.

Sura Al-Fatia Namba 1 Aya Namba 5

إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ

TAFSIRI

Wewe tu ndiyo tunakuabudu na Wewe tu ndiye tunakutegemea

Sura Al-Bakarah Namba 2 Aya Namba 2

ذَٲلِكَ ٱلۡڪِتَـٰبُ لَا رَيۡبَ‌ۛ فِيهِ‌ۛ هُدً۬ى لِّلۡمُتَّقِينَ (٢)

TAFSIRI

Kitabu Kile hakina Shaka yeyote na ni Uongofu kwa Wachamungu

SHEREHE AYA YA KWANZA

Kuruani imepanga na kutumia maneno kwa Hekima ya hali ya juu sana.

Kwa kawaida Elimu ya Sarufi inasema kwamba Sentensi yeyote ya kawaida kwanza Subject Inatangulia na Kisha Predicate lakini Ukichunguza Aya Ya Kwanza kutoka katika Sura Ya Al-Fatiha utaona neno إِيَّاكَ ni Predicate na neno نَعۡبُدُ ni Subject.

Hapa maneno haya mawili yametumika kinyume na Sheria za Kisarufi.

Kuna Hekima Gani katika Mageuzo haya?

Katika Lugha ya Kiarabu kuna Sababu Mbalimbali ambazo zinasababisha Mabadiliko kama haya lakini katika Aya hii kuna sababu moja tu. kuna hekima kubwa.

Mwenyeezi Mungu ametumia Neno إِيَّاكَ lenye maana ya “Wewe Tu” kwanza na kisha neno نَعۡبُدُ (Kitendo na Mtendaji) lenye maana ya “Tunakuabudu”

Hapa Elimu ya Balagha (Rhetorics) Inatufahamisha kwamba Kwa kutumia Mpangilio huu Maana ya Aya hii  inakuwa “wewe tu ndiye tunakuabudu” na hii inaleta faida ya تخصيص au Kukhusisha. Yaani unamkhusisha na Kumpa Mwenyeezi Mungu sifa peke yake na siye mwingine. Yaani hakuna Mwingine anayestahiki sifa hiyo ya kuabudiwa na kutegemewa isipokuwa yeye tu.

Na iwapo Maneno yangelifuata sheria za Sarufi (Grammar) na kugeuza Maneno katika  Aya yaani

نَعۡبُدُ إِيَّاكَ وَ نَسۡتَعِينُ إِيَّاكَ

kwa kubadilisha Maneno Yaani kwa kutumia Subject Kwanza na Kisha Predicate basi Aya isingelileta maana iliyokusudiwa bali Tafsiri ingekuwa (Tunakuabudu wewe na tunakutegemea wewe na Pia Tunaabudu na Tunategemea Wengineo au Miungu Mingineyo)

Kwa hiyo Mwenyeezi Mungu amejaalia Aya hii ipangike hivi إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ ili ilete maana kwamba yeye tu peke yake ndiye anastahiki kuabudiwa na kutegemewa Kwa Hiyo Tafsiri Safi itakuwa kama ifuatavyo

“Wewe tu ndiye tunakuabudu (Na hakuna miungu au mwingine ambaye anastahiki kuabudiwa) na wewe tu ndiye tunakutegemea (Na hakuna Mwingine ambaye anastahiki kutegemewa).

Kwa kifupi Aya hii inathibitisha Kuabudiwa kwa Mwenyeezi Mungu na Kukanusha Kuabudiwa kwa Mwingine Na Tunathibitisha Kumtegemea yeye tu na Kukanusha kutegemea wenngineo. Kwa kifupi Aya Inaleta Kuthibitisha na Kukanusha.

SHEREHE AYA YA PILI

ذَٲلِكَ ٱلۡڪِتَـٰبُ لَا رَيۡبَ‌ۛ فِيهِ‌ۛ هُدً۬ى لِّلۡمُتَّقِينَ (٢) 2.

Kile ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu

Katika Aya Hii tutaelezea kipande cha Aya 

ذَٲلِكَ ٱلۡڪِتَـٰبُ لَا رَيۡبَ‌ۛ فِيهِ‌ۛ

ambacho kinafuata Mpangilio wa Sarufi (Grammar) Yaani Subject Kwanza na Kisha Predicate.

Neno ذَٲلِكَ Ni Subject Na maana yake ni “Kile” yaani Kile Kitabu (Kuruani) na Ibara لَا رَيۡبَ‌ۛ فِيهِ‌ۛ ni Predicate ya neno ذَٲلِكَ Maana Yake ni “Hakina Shaka Ndani Yake” Tafsiri safi ya Kipande hiki ni Kitabu Kile hakina shaka yeyote ndani yake (Na vitabu Vinginevyo vilivyotangulia kama vile Injili na Tawrati pia havina shaka yeyote)

Kutangulia kwa Subject kunaleta maana ya Kuthibitisha kwamba Kuruani haina Shaka Yeyote na Kufuatiliwa kwa Predicate Kunaleta maana ya Kuthibitisha Pia kwamba Kuruani Haina Shaka Yeyote na Pia Vitabu vilivyopita vya Mwenyeezi Mungu vyote havina Shaka yeyote.

MLINGANISHO BAINA YA AYA HIZI MBILI

AYA YA SURA YA AL-FATIHA

1 / إِيَّاكَ نَعۡبُدُ وَإِيَّاكَ نَسۡتَعِينُ

Aya hii kuna Predicate kwanza na Kisha Subject (Mpangilio uliogeuzwa kwa makusudio kwa Hekima)

2/Aya Hii Inathibitisha kumuabudu na kumtegemea Mwenyeezi Mungu na inaleta maana ya Kukanusha kuabudu na kutegemea Miungu Mingineyo au chochote kingine

3/Aya Hii kuna إثبات ITHBAAT na نفي NAFIYUN (Kuthibitisha sifa hizi kwa Mwenyeezi Mungu peke yake Na kukanusha Sifa hizi kwa Miungu Mingineyo)

AYA YA SURA YA AL-BAKARAH

ذَٲلِكَ ٱلۡڪِتَـٰبُ لَا رَيۡبَ‌ۛ فِيهِ‌ۛ هُدً۬ى لِّلۡمُتَّقِينَ (٢)

1/Aya hii kuna Subject Kwanza na kisha Predicate (Huu ndio mpangilio wa kawaida)

2/Aya hii inathibitisha Kwamba Kuruani ni kitabu ambacho hakina Shaka Yeyote. Na inaleta maana ya kuthibitisha kwamba Vitabu vinginevyo vya Mwenyeezi Mungu havina Shaka Pia

3/Aya hii Kuna إثبات ITHBAAT ya kwanza na إثبات ITHBAAT ya pili (Kuthibitisha Kwamba kuruani haina Shaka yeyote na Kuthibitisha kwamba Vitabu Vyote Vya Mwenyeezi Mungu havina Shaka Yeyote)

Je Unaona Elimu ya Grammar (Sarufi) na Balagha (Rhetoric) zilivyotumika katika kuleta maana?

Je unaona Mageuzi ya Maneno ambayo yanaleta maana Inayokusudiwa? Allahu Akbar.