UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MAAJABU
1/ Herufi Tatu za Mwanzo wa Sura ya ABASA (A’in, Baa na Sin)Namba 80. Jumla ya Kutumika kwake katika Sura hii ni Sawa na namba ya Aya Zake?
Herufi A’in Imetumika katika Sura ya Abasa mara 13
Herufi Baa Imetumika katika Sura Ya Abasa mara 19
Herufi Sin Imetumika Katika Sura Ya Abasa mara 10
Jumla ni 13 + 19 + 10=42
Ajabu kubwa ni kwamba Sura hii ya Abasa ina Jumla za Aya 42. Allahu Akbar. Angalia Mpangilio wa Kiajabu. Hata Super Computer haifikii ufundi wa aina hii.
—————————-
2/Sura Ya Yasin Ni Namba 36 na Idadi ya Aya zake ni 83. Ukifanya hesabu 36 x 83 utapata namba 2988. La kushangaza ni kwamba Idadi ya Herufi za Sura hii ni 2988. Allahu Akbar.
Unaona Mpangilio wa kiajabu. Leo hii kuna kitabu gani Duniani kinachohesabu Herufi mfano huu. Hebu Fikiri. Kila herufi katika Kuruani Imhesabiwa kimuujiza sana tena sana. Allahu Akbar.
—————————————————-
3/Herufi za Mwanzo wa Sura Ya Bakarah ambayo ni namba 2 ni Alif, Lam na Mim. Ajabu ni kwamba Herufi ya Kwanza kutajika kwa wingi katika Sura hii ni Alif, na Ya Pili kutajika kwa wingi ni Lam na ya Tatu kutajika kwa wingi ni Mim. Hebu angalia Mpangilio huu wa kimuujiza. Sura inanziwa na الم Yaani Alif, Kisha Lam na kisha Mim.
ِKatika Sura ya Bakarah Kuna Herufi Alif 4213
Inayofuatia ni Herufi Lam 3198
Na ya mwisho ni Mim 2192
Unaona Mpangilio wa kiajabu. Siyo bure bure bali kwa Hekima kubwa. Hata Super Computer haiwezi kupanga maneno na habaro zote na hukukuhesabu Herufi kwa mfano huu. Allahu Akbar.
—————————————-
3/Sura Ya Ashura Namba 42 imetanguliwa na Herufi zifuatazo
حم عسق كذلك يوحي اليك والي الذين من قبلك
Na Sura Ya Qaf namba 50 imetanguliwa na Herufi َQaf
ق والقران المجيد
ٍMwanzoni mwa Sura Hizi Mbili zinazungumzia Kuruani Tukufu. Yaani Wahyi au Revelation.
Sasa la kushangaza ni kwamba Katika Sura ya Ashura Herufi QAF imetumika mara 57
Na katika Sura Ya Qaf Pia Herufi Qaf imetumika mara 57
Jumla la Herufi hizi mbili ni 57 + 57=114
Je unaona Muujiza? Sura mbili zinazungumzia Kuruani na Ukijumlisha Herufi QAF ambayo pia ni ya kwanza katika Neno Quran yaani Kuruani unapata idadi ya Sura za Kuruani tukufu ambazo no 114. Allahu Akbar. Unaona Muujiza ambao sio mdogo. Kwa kweli haya yanatosha kutuzidishia imani. Na pia wasio Waislamu. Muujiza mbele yetu. Allahu Akbar. Hizi Herufi zimehesabiwa na Mwenyeezi Mungu. Hakuna Binaadamu anayewweza kufanya hivi hata kidogo asikudanganye mtu yeyote. Tufumbue macho na Tusilale. Allahu Akbar.