UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MUUJIZA MKUBWA WA BUIBUI NA MPANGILIO WA SURA NA AYA YA BUIBUI KATIKA KURUANI TUKUFU
Sura Ya Al-Ankabuwt Ina habari za Buibui na Mwenyeezi Mungu amejaalia Sura iitwe kwa jina lake na hiyo siyo bure bure bali kwa hekima mbalimbali kubwa kubwa.
Kuna baadhi ya hekima ambazo tunazijua na baadhi hatuzijui kwani Elimu tuliyopewa na Mwenyeezi Mungu ni ndogo sana.
Hebu tuchunguze Aya Ifuatayo: Aya Namba 41 Sura Namba 29 (Al-Ankabut)
مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّـهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا ۖ وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ ۖ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ 41.
TAFSIRI
Mfano wa wale waliofanya waungu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ni kama mfano wa buibui ajitandiaye nyumba (yake ili imhifadhi, nayo haimhifadhi na lolote); na bila shaka nyumba iliyo dhaifu kuliko zote ni nyumba ya buibui; laiti wangalijua!
SHEREHE NA MUUJIZA
Mwenyeezi Mungu anafananisha Makafiri ambao hawamuabudu Mwenyeezi Mungu na Utando wa Buibui ambao ni dhaifu sana.
Makafiri hawawezi kuwafaa wafuasi wao na pia hawawezi kuwalinda kwa dhara yeyote.
Kuna Aina Mbili ya Udhaifu:
Kwanza Udhaifu huu ni wa Nyumba ya Utando wa Buibui au Nyuzi za Utando wa Buibui Na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akasema katika Aya hii ya 41 Sura namba 29 kwamba Udhaifu wa Nyumba tu. Iwapo Mwenyeezi Mungu angelisema Udhaifu wa Nyuzi za Utando wa Buibui basi ingelikosolewa na Utafiti wa Kisayansi wa Kisasa ambao umetuhakikishia kwamba Nyuzi za Utando wa Buibui una sifa za pekee na Mojawapo ya sifa hizo ni Ugumu wa Nyuzi za Utando wa Buibui kwamba Unazidi Chuma karibu mara tano. Yaani ungelipata Nyuzi za Buibui kwa wingi na kufikia uzito na Kipimo sawa na Chuma kisha ulinganishe ugumu baina yake na Chuma basi utakuta Nyuzi za utando wa Buibui una Ugumu zaidi ya chuma karibu mara 5. Angalia Maajabu. Ijapokuwa Nyuzi za Buibui ni Ngumu lakini zinapojengewa Nyuma basi Nyumba hiyo ni Dhaifu sana. Kwanza hizo Nyuzi ni nyembamba sana na Nyuma inaweza kuanguka kwa kupulizwa na upepo au mdudu yeyote mwenye nguvu kuivunja. Kwa hiyo Nyumba ya Buibui ni dhaifu sana ijapokuwa Buibui anafikiri ni Nyumba madhubuti na haitavunjika. Buibui anajidanganya.
Pili kuna Udhaifu wa Uhusiano baina ya Buibui katika Familia yake. Kuna wakati Buibui wa kike humuua Buibui mwenziwe wa Kiume. (Uhusiano wa Mume na Mke).
Kwa hiyo Udhaifu katika Aya hii unaweza kuwa ni Utando wa Buibui, na pia Unaweza kuwa Uhusiano baina ya Buibui wa Kike na Mwenziwe wa kiume kama inavyothibitishwa na Wataalamu wa Elimu ya Vijidudu. Mume kumuua Mkewe baada tu ya Maingiliano (Muashara) Na baadaye Mauti hiyo inatumika kwa chakula. Kwa kiingereza inajulikana kama Cannibalism. Na watoto wanapozaliwa kutoka katika mayai kwa ajili ya wingi na msongamano husababisha vurugu baina yako kwani nafasi ni ndogo na pia wanahitaji chakula kwa hiyo wale ambao wana nguvu huwaangamiza walio dhaifu na kuwala na hivyo hivyo wanapokua wataanza kufanya kama walivyofanya wazazi wao kazi za kudhulumiana baina yao na hata kufikia kulana. kwanza Mke atamuua Mume kisha watoto watauana basi hivyo hivyo maisha yao. Buibui hawaishi vizuri bali huuana na kutafunana hovyo hovyo Na ndiyo maana Kuruani ikasema Nyumba ya Buibui ni dhaifu kwa maana kwamba nyumba ya buibui ina udhaifu wa utulivu yaani hakuna usalama. Hii Tafsiri inakubaliana na utafiti kwani Nyuzi za utando wa Buibui ni ngumu sana ijapokuwa tunafikiri ni Dhaifu. Nyuzi hizi zinajulikana kama Hariri (Silk) zinatumika katika matumizi ya kuunda vifaa mbalimbali ya maisha mfano wa Shati wanazovaa Askari au wanajeshi Vitani ili Kuzuia Risasi isipenye mwilini. Wataalamu wanasema kwamba Nyuzi hizi zina ugumu kuliko Chuma karibu mara Tano yaani ukizikusanya nyuzi hizi kwa kiasi na uzito kama vile Chuma basi zitaishinda Chuma kwa ugumu karibu mara 5. Habari hii inathibitishwa na Utafiti wa Wataalamu duniani. Nimenukulu hapa chini Kauli kutoka katika Mtandao
UGUMU WA NYUZI ZA MTANDO WA BUIBUI
FRENCH LANGUAGE
Soie d’araignée est connue comme l’un des matériaux naturels les plus solides au monde : elle serait jusqu’à cinq fois plus résistante qu’un câble d’acier du même poids. D’où tire-t-elle cette impressionnante solidité ? Grâce à un microscope particulièrement puissant,”Il s’avère que la fibre est constituée d’une multitude de nano-brins
SWAHILI TRANSLATION
Hariri ya buibui inajulikana kuwa mojawapo ya vitu au malighafi za asili zenye nguvu zaidi duniani: inasemekana kuwa na nguvu hadi mara tano kuliko Waya (Cable) za chuma.. Je, unatoka wapi uimara huu wa kushangaza? Kwa bahati kubwa Darubini zenye nguvu sana zinatufunulia kwamba “Nyuzi zina Muundo wa safu za Hariri nyingi zilizopangwa kwa ufundi wa hali ya juu. (Nano Structure)
UHUSIANO WA BUIBUI KATIKA FAMILIA ZAO
“In many spider species, females eat the males after sex. Studies have suggested various complex evolutionary reasons involving costs and benefits to the species, sperm competition and esoteric sexual selection schemes. Turns out the motivation for this creepy cannibalism is much simpler.It’s all about size. If males are small, they’re easier to catch and therefore more likely to be prey. Big females eat their puny mates simply because a) they’re hungry and b) they can.(Miami University in Ohio)”
SWAHILI TRANSLATION
Niliyozungumza hapo juu kutoka katika chuo kikuu cha Miami huko America ndiyo haya yaliyozungumzwa katika maandishi haya. kwamba Uadui baina ya vijidudu hivi ni mkubwa sana. Wanauana hovyo hovyo na kulana wakati wa njaa na pia hawana huruma. Kwa kweli wanyama wengine duniani huhurumiana lakini Buibui sivyo walivyo. Na Mwenyeezi Mungu amejaalia Sura katika Kuruani kwa jina la Buibui siyo bure bure bali kwa hekima kubwa.
MPANGILIO WA SURA NA AYA YA BUIBUI
Hebu tufanye utafiti wa Mfumo wa Sura ya Al-Ankabut tuone maajabu ya kushangaza sana.
1/Sura Ya Al-Ankabut imeanziwa na Herufi Ya Muqataa Alif, Lam Na Min.
Herufi hizi zinajulikana kama Muqataa (The mysterious letters, muqaṭṭaʿāt, Arabic: حُرُوف مُقَطَّعَات ḥurūf muqaṭṭaʿāt, “disjoined letters” or “disconnected letters) katika Kuruani.
Jumla ya Herufi hizi ni 14 nazo ni (ʾalif أ, hā هـ, ḥā ح, ṭā ط, yā ي, kāf ك, lām ل, mīm م, nūn ن, sīn س, ʿain ع, ṣād ص, qāf ق, rā ر.)
Vipande vya herufi hizi (zaidi ya herufi moja) visivyokariri ni 14 Pia na ukujumlisha na vilivyokariri vinakuwa jumla ni 29 kwa hiyo Herufi Hizi zimetumika mwanzoni mwa Sura 29 za Kuruani Tukufu. Nazo ni
Al-Baqarah ʾAlif Lām Mīm الم
Āl Imrān ʾAlif Lām Mīm الم
Al-Aʿrāf ʾAlif Lām Mīm
Ṣād المص
Yūnus ʾAlif Lām Rā الر
Hūd ʾAlif Lām Rā الر
Yūsuf ʾAlif Lām Rā الر
Ar-Raʿd ʾAlif Lām Mīm Rā المر
Ibrāhīm ʾAlif Lām Rā الر
Al-Ḥijr ʾAlif Lām Rā الر
Maryam Kāf Hā Yā ʿAin Ṣād كهيعص
Ṭā Hā Ṭā Hā طه
Ash-Shuʿārāʾ Ṭā Sīn Mīm طسم
An-Naml Ṭā Sīn طس
Al-Qaṣaṣ Ṭā Sīn Mīm طسم
Al-ʿAnkabūt ʾAlif Lām Mīm الم
Ar-Rūm ʾAlif Lām Mīm الم
Luqmān ʾAlif Lām Mīm الم
As-Sajdah ʾAlif Lām Mīm الم
Yā Sīn Yā Sīn يس
Ṣād Ṣād ص
Ghāfir Ḥā Mīm حم
Fuṣṣilat Ḥā Mīm حم
Ash-Shūrā Ḥā Mīm; ʿAin Sīn Qāf حم عسق
Az-Zukhruf Ḥā Mīm حم
Al Dukhān Ḥā Mīm حم
Al-Jāthiya Ḥā Mīm حم
Al-Aḥqāf Ḥā Mīm حم
Qāf Qāf ق
Al-Qalam Nūn ن
Jumla ya Sura hizi ni 29 na namba hii inalingana na Namba ya Sura ya Al-Ankabut ambayo ni ya 29.Angalia Maajabu..
Sura ya Al-Ankabut ni ya kati kati baina ya Sura hizi 29 tulizozitaja hapa juu Yaani ni Sura ya 15. Kuna Sura 14 kabla ya Sura hii na Sura 14 baada ya Sura hii, na kwa hiyo Jumla Ya Vipande vya herufi vya Muqataa zilizotumika kuanzia mwanzo wa Msahafu yaani kabla ya Sura Ya Al-Ankabut ni 14 na Jumla Ya vipande vya Herufi Hizi baada ya Sura Ya Al-Ankabut mpaka mwisho wa Msahafu ni 14 pia. Angalia Maajabu.
Sura ya Ankabut ipo katikati baina ya Sura 29 Yenye Vipande vya herufi Hizi.
2/Jina la Mwenyeezi Mungu Allah katika Sura hii limekariri (tumika) mara 42 na namba hii unaweza kuigawa katika mafungu matatu ya namba 14 yaani 14 + 14 + 14
3/Jumla ya Sura za Kuruani ni 114 Yaani 57 X 2 yaani Mafungu mawili ya Sura 57 Sura ya Al-Ankabut ni ya 29 katika katika Fungu la kwanza la Sura 57. Ukiichunguza utaona Kuna Sura 28 kabla ya Sura Hii na Kuna Sura 28 baada ya sura hii. Na namba 28 ni sawa na 14 X 2. Kwa hiyo Sura hii ipo katikati ya Jumla za Sura 57 Angalia Namba 14 inavyokariri kiajabu. Yaani Sura hii imezungukwa kwa Namba 14 kwa upande wa kushoto na kulia kiajabu sana Na Namba 28 ni sawa na jumla ya jumla ya Herufi za Lugha ya Kiarabu.(Arabic letters)
4/Tukichunguza Sura 14 za ODD Numbers zilizopo kabla ya Sura Hii na kujumlisha Namba za Sura hizo utapata namba 196 na namba hii unaweza kuigawa katika mafungu 14 pia. Kwa hiyo 14 x 14=196 Angalia namba 14 inavyojitokeza
5/Tukichunguza Sura 14 za EVEN Number zilizopo Kabla ya Sura Hii utapata Jumla ya Namba za Sura hii ni 210 pia na namba hii unaweza kugawanya katika mafungu 14 pia. Kwa hiyo 14 x 14 + 14 =210 Angalia namba 14 inavyojitokeza.
6/Tukichunguza Sura 14 za ODD Number zilizopo Baada ya Sura Hii mpaka mwisho wa Sura 57 za Nusu ya kwanza na kujumlisha Namba za Sura hizo utapata namba 588 na namba hii unaweza kugawanya katika mafungu 42 ya 14 Kwa hiyo 42 x 14=588 Angalia namba 14 inavyojitokeza.
7/Tukichunguza Sura 14 za EVEN Number zilizopo Baada ya Sura Hii mpaka mwisho wa Sura 57 za Nusu ya kwanza utapata Jumla ya Namba za Sura hii ni 602 pia namba hii unaweza kuigawa katika mafungu 43 ya 14 .Kwa hiyo 43 X 14=602 Angalia namba 14 inavyojitokeza.
Na La kushangaza zaidi ni kwamba katika Elimu ya Hesabu namba 43 ni Prime Number ya 14
Tumeona namba 14 inavyojitokeza katika Sura Hii kiajabu ajabu sana. Kila hesabu tulizofanya tunapata namba ambayo inatupa namba 14. Njia zote zinaashiria namba 14. Je huoni kwamba Kuruani siyo maneno ya Binaadamu. Angalia Mpangilio wake unaoshagaza. Kila herufu, maneno na Aya zimehesabiwa. Siyo bure bure bali kwa Hekima ambayo hakuna anyejua isipokuwa Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Kuna ambayo tumefundishwa na pia kuna yale ambayo hatukufundishwa. Allahu Akbar.
Huenda inaashiria aina Ya Buibui wenye Kanda
za Uzazi 14 (Chromosomes 14) kama vile speshi (Species) Araneae: Gnaphosidae, Miturgidae and Philodromidae.
Au huenda kuna mengine tusiyajua. Lililo muhimu ni mpangilio ambao unshangaza. Mpangilio wa kiajabu. Sura imepimiwa Sehemu yake kwa namba 14.
IBLIS NA KIBURI (Istikbar) CHAKE, MUUJIZA WA SIJIDA (SUJUDU)
Kabla ya Kusherehesha Aya zinazozungumzia Ablis ni ngependelea kutaja mambo mawili.
Jambo la kwanza Katika Maasi Makubwa ni Kiburi. Na Iblis ni miongoni mwa Majini ammbaye alikataa kumsujusia Binaadamu kama alivyoamrishwa na Mwenyeezi Mungu.
Jambo la pili ambalo muhimu kulielewa ni kwamba Jumla ya Sala za Faradhi Tano zina Jumla ya Sujudu 34 Na Katika Kuruani tukufu kuna Aya ambazo zinazungumzia Kusujudu na unapokuwa ukisoma kuruani na kufikia katika Aya hiyo basi inabidi ufanye Sujuda. Jumla Ya Sujuda za aina hii ni 15
Katika Aya zifuatazo Namba 34 na 15 zimerikodiwa kiajabu sana. Ukaidi wa Iblis unadhihirika katika Aya hizi. Alikatata kumsujudia Binaaamu kama alivyoamrishwa na Mwenyeezi Mungu. Aliambiwa Amsujudie Sijida Moja tu akakataa. Mwenyeezi Mungu amejaalia Aya hizi zinazotaja Habari za Iblis kubeba Idadi ya Sijida za Sala za Faradhi na Pia Sijida 15 za Kisomo cha Kuruani (Tilwaat Al-Quran) Hebu angalia Maajabu. Maajabu yasiyo na mwisho.
Aya Namba 34 Sura Ya Al-Bakarah Namba 2
وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأَدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ وَٱسۡتَكۡبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلۡكَـٰفِرِينَ (٣٤)
TAFSIRI
34·Na (wakumbushe watu khabari hii): Tulipowaambia Malaika: “Msujudieni Adam” (yaani mwadhimisheni kwa ile ilimu yake aliyopewa). Wakamsujudia wote isipokuwa lblis; akakataa na akajivuna; na (tokea hapo) alikuwa katika makafiri; (ila alichanganyika tu na Malaika).
SHEREHE ZA HESABU
Jambo la kushangaza ni kwamba kuna Kuna Herufi 34 kuanzia mwanzo wa Aya hii mpaka kabla ya Neno “Iblis” Neno “Aba” yaani Kukataa au kukana ni neno la 510 kuanzia mwanzo wa Sura ya Bakarah na namba hii ni sawa na 34 x 15 namba 34 inaashiria Jumla ya Sujudu za Sala na namba 15 Ni Jumla ya Sujudu za Kisomo cha Kuruani (Sujudu za Tilawat Al-Quran).
Na ajabu nyingine ni kwamba Neno وَٱسۡتَكۡبَرَ “Wastakbarah” (Na Akafanya Kiburi) herufi zake zimetumika na kukariri katika Aya hii mara 34 kama ifuatavyo:
WAW mara 5
Alif Mara 15
SIN mara 4
Taa mara 1
Kaf mara 4
Baa mara 3
Ra mara 2
Kwa hiyo Namba 34 inaashiria Sujudu za Sala ambazo Iblis alikana. Mwenyeezi Mungu anatoa Muujiza katika Aya hii.
Na katika mfululizo wa Aya zinazotaja Iblis katika Kuruani Tukufu hebu tuchunguze Aya ya Mwisho ambayo inazungumza habari Iblis katika kuruani ambayo ipo katika Sura ya Swad namba 38 Aya namba 75
قَالَ يَـٰٓإِبۡلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسۡجُدَ لِمَا خَلَقۡتُ بِيَدَىَّۖ أَسۡتَكۡبَرۡتَ أَمۡ كُنتَ مِنَ ٱلۡعَالِينَ (٧٥)
TAFSIRI
15·(Mwenyezi Mungu) akamwambia:- ”Ewe Ibilisi Kipi kilichokuzuia kumtii yule niliyemuumba kwa mikono yangu? Je! umetakabari, (wala huna ukubwa) au umo miongoni mwa wakubwa (kweli)?”
SHEREHE ZA HESABU
Angalia Maajabu Jumla ya Maneno ya Aya hii ni 15 na Nuqta zilizopo katika aya hii ni 34 na kama nilivyosema hapo awali kwamba namba 15 ni idadi ya Sijida za Kisomo cha Kuruani na 34 ni idadi ya sujudu za sala za Faradhi. Angalia ya Kushangaza. Muujiza siyo mdogo. Muujiza mpaka Katika Nuqta ambazo ziliongezwa katika kuruani baada ya kufariki ka Mtume Mohamad ﷺ yaani baada ya Miaka. Nuqta hizi zilionqezwa ili kuwasaidia Wasomaji wa Kuruani. Mwenyeezi Mungu ameitunza kuruani mpaka katika Nuqta. Hakuna kilichoongezwa au kupunguzwa ila kwa muongozo wa Mwenyeezi Mungu kama alivyoahidi kwamba Ataihifadhi Kuruani Tukufu. Allahu Akbar. Maajabu yasiyo na Mwisho. Allahu Akbar.
Neno ISTAKBARA limetumika katika Kuruani mara 4 Katika Sura zifuatazo
Sura Ya Qasas Aya namba 39
Sura Ya Baqarah Aya Namba 34
Sura Ya Swad Aya Namba 74
Sura Ya Mudathir Aya namba 23
Jumla ya Maneno ya Aya hizi Nne ni 34 na Jumla ya Namba za Aya za Sura Hizi ni 170 na Namba hii ni sawa na 5 X 34 Je unaona Ya Kushangaza? Allahu Akbar. Huu siyo Muujiza mdogo hata kidogo.
Aya Namba 11 katika sura ya Al-Araaf Namba 7
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَـٰڪُمۡ ثُمَّ صَوَّرۡنَـٰكُمۡ ثُمَّ قُلۡنَا لِلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأَدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ لَمۡ يَكُن مِّنَ ٱلسَّـٰجِدِينَ (١١)
TAFSIRI 11.
Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: “Msujudieni Adamu.” Basi wakasujudu isipokuwa lbilisi hakuwa miongoni mwa waliosujudu.
SHEREHE ZA HESABU
Aya Hii ina jumla ya Nuqta 32 je onaona Muujiza usiyo na mwisho?
Na Herufi za Neno إِبۡلِيسَ “Iblis” zimetumika katika Aya hii mara 32 pia kama ifuatavyo.
Alif=13
Baa=1
Lam=11
Ya=3
Sin=4
Namba 32 Inaashiria Sura Ya Sijdah ambayo ni namba 32 na Ukilinganisha Aya hii ya 11 katika Sura ya Al-Araaf na Aya ya mwisho ya Sura Ya Sajida utakuta kukingana kwa neno la mwisho katika Aya hizi mbili na neno hili ni ٱلسَّـٰجِدِينَ “Asajidin” lenye maana ya “Wenye Kusujudu”
Na Namba 11 Ya Aya hii ya Al-Araaf inaashiria Kutumika kwa Jina Iblis katika Kuruani mara 11. (Iblis ametajika katika Kuruani katika Aya 11)
Aya ya kwanza kuzungumzia habari za Iblis katika Kuruani ni ya 34 katika Sura Ya Al-Bakarah na ajabu ni kwamba Namba 34 Ni Idadi ya Sijida za Faridha. Namba Ya Aya pia Muujiza.
Kama tulivyoona kwamba Namba 34 Ni Idadi ya Sijida za Faridha na 15 Ni Idadi ya Sijida za Tilawat za Kuruani. Hebu tujumlishe Jumla ya Namba hizi mbili.
15 + 34=49 na 49 ni sawa na 7 x7 angalia ya kushangaza Namba 7 ni idadi ya Viungo vinavyotumika katika Kusujudu.
Paji la uso
Viganja vya mikono miwili
Magoti mawili
Na vidole vya miguu miwil
Jumla ni viungo 7 je unaona Maajabu yasiyo na mwisho. Muujiza mpaka katika Viungo vya mwili.
Hebu tuendelee na Uchunguzi tuone ya kushangaza.
Aya namba 206 Sura ya Al-Araaf namba 7
إِنَّ ٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَيُسَبِّحُونَهُ ۥ وَلَهُ ۥ يَسۡجُدُونَ ۩ (٢٠٦)
206. Wale walioko kwa Mola wako (Nao ni Malaika) hawajivuni (wakaacha) kumuabudu (Mola wao kwa kuwa ni wakubwa la; bali) na wanamtukuza na kumsujudia.
SHEREHE YA HESABU
Aya hii ina Sijida Tilawat ya kwanza katika Kuruani tukufu.Yaani Aya hii ndiyo ya kwanza katika Kuruani ambayo inatubidi tunapoisoma tufanye Sujudu moja na hii inajulikana kama Sijida Al-Tilwat ya Kuruani. Aya hii ina maneno 11 Na Ajabu ni kwamba Kukariri kwa Jina la Iblis ambaye aliyekuwa wa kwanza kufanya kiburi na kukataa kusujudu ametajika katika kuruani mara 11 pia Angalia namba 11 inavyoshangaza. Ukaidi wa Iblis unadhihirika mpaka katika Namba.
Neno يَسۡتَكۡبِرُونَ yaani “Wanafanya Kiburi” yaani “Yastakbituwna” limekariri na kutumika katika kuruani mara 7 katika Sura zifuatazo:
Sura ya Al-Araf Aya namba 206
Sura ya Al-Anbiyaa Aya namba 19
Sura Ya Aswafaat Aya Namba 35
Sura Ya Al-maidah Aya namba 82
Sura ya Al-Nahl Aya Namba 49
Sura Ya Asajdah Aya Namba 15
Sura Ya Ghafir Aya Namba 60
Jumla ya Maneno ya Aya hizi ni 102. Na namba hii ni sawa na 34 x 3 .
Je unaona namba 34 inavyokariri kiajabu?
Huu siyo Muujiza mdogo. Kuruani haina Mfano wowote. Ni maneno ya aliyeumba kila kitu. Heiwezekani kuwa maneno ya binaadamu hata kidogo. wewe huoni haya tuliyoyasherehesha? Allahu Akbar.
NYONGEZA YA MUUJIZA WA CHROMOSOMES ZA NYUKI AU KANDA ZA UZAZI
Wataalamu wa Elimu ya Uzazi au Genetics wanatuambia kwamba Nyuki wa Kiume ana Chromosomes 16 na Nyuki wa Kike ana Chromosome 32 yaani Pair mbili za Chromosomes.
Na Wataalamu wa Elimu za Vijidudu wanasema kwamba Muda unaotakikana wa kukua kwa Nyuki wa kike na hatimaye kuwa Malkia ni siku 16
(A queen bee can be produced in only 16 days! She has the shortest development time of any bee in the colony).
Nimekwisha Elezea Utafiti mbalimbali unaohusu Nyuki katika Sehemu nyinginezo za Website hii na Al-hamdulilah leo nitafanya nyongeza. Kama tulivyoona kwamba Elimu ya Kuruani haina mwisho na ndoyo maana ninawaletea habari hizi za nyuki mara kwa mara. kwani mapya yanagunduliwa kila siku. Allahu Akbar.
Sura Ya Annahl ni ya 16 yaani Namba 16 katika Kuruani (Unaona Maajabu kwani inaashirIa Chromosomes 16 za Nyuki) hebu tuendelee na uchunguzi:
Jumla Aya za Sura ya Nyuki ni 128 na namba hii ni sawa na 16 x8 (Angalia Namba 16 inavyojitokeza)
Aya ambayo fupi sana katika sura hii ni Aya namba 16 Katika Aya hii kuna Herufi 16 za Lugha ya Kiarabu ambazo hazikutumika yaani kutoka katika Jumla ya herufi 28 za lugha ya kiarabu. (Angalia Namba 16 inavyojitokeza)
Aya ya mwisho yaani Aya namba 128
إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحۡسِنُونَ (١٢٨)
TAFSIRI
128.Kwa hakika Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wale wanaomcha, na wale wafanyao wema
SHEREHE
Idadi ya herufi zake ni 32 ambazo ni sawa na 16 + 16 NA Idadi ya maneno ya Aya hii ni 8 8 x 16=128 (Angalia Namba 16 inavyojitokeza)
Aya namba 68 kutoka katika Sura Ya Al-Nahl ni Aya pekee inayozungumzia Asali katika kuruani yote.
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨)
TAFSIRI
68.Na Mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba “Jitengenezee majumba (yako) katika milima na katika miti na katika yale (majumba) wanayojenga ( watu).”
SHEREHE
Kipande cha Aya وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ (Wa Awha Rabuka Ila Annhl) chenye maana ya “Na Mola wako alipomfahamisha au alipomfundisha nyuki” kina Herufi 16 (Angalia Namba 16 Inavyojitokeza)
Aya Ina maneno 13 ni Aya Namba 68 hebu tu Multiply namba hizi (13 X 68=884) na Namba hii 884 inaashiria Jumla ya maneno kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Annahl mpaka Mwisho wa neno ٱلنَّحۡلِ Annahl wa Aya hii Idadi ya maneno ni 884
Aya Iliyo Ndefu katika sura ya Annahl ni Aya namba 92
وَلَا تَكُونُواْ كَٱلَّتِى نَقَضَتۡ غَزۡلَهَا مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ أَنڪَـٰثً۬ا تَتَّخِذُونَ أَيۡمَـٰنَكُمۡ دَخَلاَۢ بَيۡنَكُمۡ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِىَ أَرۡبَىٰ مِنۡ أُمَّةٍۚ إِنَّمَا يَبۡلُوڪُمُ ٱللَّهُ بِهِۦۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَـٰمَةِ مَا كُنتُمۡ فِيهِ تَخۡتَلِفُونَ (٩٢)
TAFSIRI
Wala msIwe kama yule mwanamke aliyeukata uzi wake vipande vipande banda ya (kuusokota) kuwa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu njia ya kudanganyana baina yenu. Kwa. ajili kundi moja la watu kuwa na nguvu zaidi kuliko kundi la watu wengine (ndio mnawaacha hao wasio na nguvu mliopeana ahadi nao! Msifanye hivyo). Hakika Mwenyezi Mungu anakujaribuni kwa njia hiyo. Na bila shaka atakubainishieni siku ya Kiyama mliyokuwa mkihitalifiana
SHEREHE
Ina Maneno 32 na Herufi 128 (Herufi Othmaniy) au 131 (HerufiImlaiy) Ikiwa 128 (Uthmaniy) Namba hii ni sawa na 16 x 8 (Angalia namba 16 inavyojitokeza) Ikiwa 131 basi namba hii katika Elimu ya Hesabu ni Prime Number ya 32 (Angalia namba 32 inavyojitokeza na namba hii ni sawa na 16 + 16) Katika namba hizi mbili tuanona muashirio wa Chromosomes za Nyuki zinavyojitokeza.
Sura Ya Annahl Namba 16-Aya namba 11 na Aya namba 103 kila moja ina maneno 16
يُنۢبِتُ لَكُم بِهِ ٱلزَّرۡعَ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلنَّخِيلَ وَٱلۡأَعۡنَـٰبَ وَمِن ڪُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِۗ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَةً۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَڪَّرُونَ (١١)
TAFSIRI
11.(Na kwa hayo) hukuotesheeni mimea (ya kila namna) na mizeituni na mitende na mizabibu na kila matunda. Na bila shaka katika hayo imo ishara kwa watu wenye kufikiri (kuwa yuko Mwenyezi Mungu).
وَلَقَدۡ نَعۡلَمُ أَنَّهُمۡ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ ۥ بَشَرٌ۬ۗ لِّسَانُ ٱلَّذِى يُلۡحِدُونَ إِلَيۡهِ أَعۡجَمِىٌّ۬ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِىٌّ۬ مُّبِينٌ (١٠٣)
TAFSIRI
33.Na bila shaka tunajua kwamba wanasema: “Yuko mtu anayemfundisha!’ (Lakini) lugha ya yule wanayemwelekezea (kuwa anamfundisha Mtume) ni ya kigeni, na hii (lugha inayotumika katika Qurani) ni lugha ya Kiarabu iliyo baini (wazi au clear)
SHEREHE
Ukijumlisha Namba za Aya utapata 103 + 11=114 namba 11 ni Prime Number ya 5 na namba 103 ni prime number ya 27.
27 + 5=32 na namba 32 ni sawa na 16 + 16 Na Jumla ya maneno ya Aya hizi mbili ni 32 ambayo ni 16 + 16 (Angalia namba 16 inavyojitokeza)
Huu ni Muujiza siyo mdogo. Tumeona namna Namba 16 inavyojitokeza yaani kwa kila njia. Kil anjia tulizipita zinaishia katika namba 16. Miujiza mingine kutoka katika Sura ya nyuki ambayo nimeilelezea katika website hii pia ni mikubwa sana. Kwa kweli hakuna mwisho. Jaribu kufikiri utaona huu ndiyo ukweli. Hakuna Mwisho wa Maajabu. na Hii inathibitisha kauli ya Mtume ﷺ iliyosema Maajabu ya Kuruani hayana mwisho. na Mwenyeezi Mungu amesema katiak kuruani kwamba amejaalia kila kitu kwa Hesabu. Allahu Akbar. Allahu Akbar.
MUUJIZA WA MAJINA NA SIFA ZA MTUME MOHAMAD ﷺ
Kwa kawaida watu watukufu hawaitwi kwa majina yao bali kwa kutumia sifa zao. Mtume Mohamad amepewa Heshima hii na Muumbaji. Katika Kuruani hakuitwa kwa jina lake kama walivyoitwa mitume mingine kama vile
YA ADAMU yaani Ewe Adamu
YA NUHU yaani Ewe Nuhu
YA MUSA yaani Ewe Musa
YA ISA yaani Ewe Isa
Katika Kuruani Tukufu Mtume Mohamad ﷺ hakuitwa kama walivyoitwa Mitume waliotangulia bali kwa sifa zake kama vile
YA AYUHA ARASSULU
YA AYUHA ANNABIYU
YA ِ AYUHA AL-MUZAMILU
YA AYUHA AL-MUDATHIR
ALMUZAMIL NA ALMUDATHIR NI SIFA mbili tukufu za Mtume Mohamad ﷺ
Katika Kuruani Tukufu Jina na Sifa za Mtume zimetumiwa katika Majina ya Sura Tatu zifuatazo: Sura Ya Mohamad
Sura Ya Muzamil
Sura ya Mudathir
Na baina ya Sura hizi kuna Mfungamano wa Namba unaoshangaza sana.
MAAJABU MAKUBWA YA KURUANI TUKUFU
MOHAMAD AYA ZAKE NI 38
MUZAMIL AYA ZAKE NI 20
MUDATHIR AYA ZAKE NI 56
JUMLA AYA ZOTE NI 114
Je Unaona Namba 114 ni Jumla ya Sura za Kuruani Tukufu.
Utafiti wa Herufi Katika Sura zifuatazo:
SURA YA MOHAMAD
MIM IMEKARIRI MARA 223
Ha IMEKARIRI MARA 23
DAL IMEKARIRI MARA 35
223 + 23 + 35=281 JUMLA 281
KATIKA SURA A MUZAMIL
MIM IMEKARIRI MARA 52
HAA IMEKARIRI MARA 5
DAL IMEKARIRI MARA 11
52 + 5 + 11=68 JUMLA 68
KATIKA SURA YA MUDATHIR
MIM IMEKARIRI MARA 71
HAA IMEKARIRI MARA 10
DAL IMEKARIRI MARA 26
71 + 10 + 26=107 JUMLA 107
JUMLA YA HERUFI KATIKA SURA 3 HAPA JUU NI=
281 + 68 + 107 =456
NA NAMBA HII NI SAWA NA 114 X 4
Namba 114 Inaashiria Sura za KURUANI ambazo ni 114 Na Namba 4 Inaashiria Kukariri kwa Jina Mohamad ﷺ Katika Kuruani Tukufu.
JUMLA YA MANENO KATIKA SURA MBILI ZIFUATAZO:
MUZAMMIL MANENO 200
MUDATHIR MANENO 256
JUMLA 456 NA NAMBA 456 NI SAWA NA 114 X 4 Na Namba 4 Inaashiria Kukariri kwa Jina Mohamad ﷺ Katika Kuruani Tukufu. Sura Hizi Mbili za Sifa zake Mtume ﷺ pia zinatupa Namba 456 ambayo kama tulivyoona ni sawa na 114 x 4
Hebu Tuchunguze Aya ya mwisho katika Sura ya MOHAMAD
Herufi za Jina Mohamad zimekariri mara 14
Herufi za Sifa Al-Muzamil zimekariri mara 47
Herufi za Sifa Al-Mudathir zimekariri mara 53
Jumla ya Herufi Hizi ni 14 + 47 + 53=114
Namba 114 Inaashiria Sura za KURUANI ambazo ni 114
Jumla ya Idadi ya Nuqta katika Aya Hii ni 73 Na Namba hii 73 ni Namba Ya Sura ya Al-Muzamil Katika Kuruani
Katika Kuruani tunakuta Aya Ya Kwanza Yenye Nuqta 38 Ni Aya Namba 22 Katika Sura Ya Al-Bakarah.
Herufi za Jina Mohamad zimekariri katika Aya hii mara 12
Herufi za Sifa Al-Muzamil zimekariri katika Aya hii mara 48
Herufi za Sifa Al-Mudathir zimekariri katika Aya hii mara 54
Jumla 12 + 48 + 54=114
Angalia Maajabu Tunapata Namba ya Jumla ya Sura za Kuruani
Sasa Tuchunguze Aya Mbili:
Aya namba 38 Sura Ya Mohamad na Aya namba 22 Sura ya Bakarah ambayo ina Nuqta 38
Herufi za Jina Mohamad zimekariri katika Aya hizi mbili mara 26
Herufi za Jina AlMuzamil zimekariri katika Aya hizi mbili mara 95
Herufi za Jina AlMudathir zimekariri katika Aya hizi mbili mara 107
Tukijumlisha Jumla hizi tutapata 228 (26 + 95 + 107=228) na Ajabu ni kwamba Jumla ya Herufi za Aya hizi mbili ni 228
Na Namba hii ni sawa na 114 + 114
Namba 114 inaashiria Jumla Ya Sura za Kuruani.
Je unaona Maajabu. Huu siyo mpangilio wa Kibinaadamu hata kidogo. Jaribu kufikiri utaona ninayosema ni ukweli. Angalia namba zilivyojipanga na namna zinavyoashiria kuruani kiajabu ajabu. Allah Akbar. Huu siyo Muujiza mdogo hata kidogo.