UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MUUJIZA WA NAMBA ZENYE VIPEO AMBAZO INAJULIKANA KWA ALAMA YA ‘√ ‘KATIKA KURUANI
NAMBA KATIKA KURUANI TUKUFU
Namba zifuatazo zimetumika katika Aya za kuruani. Kuna Namba Nne tu kati ya Hizi ambazo zina Vipezo na zote hizo pamoja na Vipezo vyake vimetajika Katika Namba hizi.
NAMBA 1/ NAMBA 2/ NAMBA 3/ NAMBA 4/NAMBA 5/NAMBA 6/NAMBA 7 /NAMBA 8/ NAMBA 9/ NAMBA 10/ NAMBA 11/NAMBA12/ NAMBA 19/ NAMBA 20/ NAMBA 30/ NAMBA 40/ NAMBA 50/ NAMBA 60/ NAMBA 70/ NAMBA 80/NAMBA 99/ NAMBA 100/ NAMBA 200/ NAMBA 300/ NAMBA 1000/NAMBA 2000/ NAMBA 3000/ NAMBA 5000/NAMBA 50000/NAMBA 100000
MUUJIZA WA KIPEO ‘√ ‘
Muujiza ni kwamba kati ya hizi namba zote zilizotajika katika kuruani kuna namba 4 tu peke yake ambazo zina Vipeo.
Maana ya Vipeo ni kama ifuatavyo:
It is a number which is the value of power 1/2 of that number. In other words, it is the number that we multiply by itself to get the original number. It is represented using the symbol ‘√ ‘.
Vipeo katika Kuruani kutoka katika Orodha ya Namba tulizozitaja hapa juu ni kama ifuatavyo:
1 (Kipeo cha Namba 1 ni 1)
4 (Kipeo cha Namba 4 ni 2)
9 (Kipeo cha Namba 9 ni 3)
100 (Kipeo cha Namba 100 ni 10)
Je unaona Muujiza
Hizi namba 4 ni pekee ambazo pia zina Vipeo pia. Na Namba hizi pamoja na Vipeo vyake pia zimetajika Katika Orodha ya Namba hapa Juu. Yaani Namba 1, 4, 9,100,2,3,na 10 zote zimatajika hapa Juu.
Ukijuumlisha Namba hizi ambazo zenye Vipeo
Yaani ukijumlisha Namba 1 + 4 + 9 + 100= 114
Huu Ndiyo Muujiza wa kushangaza. Tukijumlisha namba hizi Nne tunapata Jumla ni 114 na hizi ndizo Idadi ya Sura Za Kuruani katika Msahafu.
Je unaona Muujiza? Yaani Vipeo katika Kuruani?
Yaani Namba zinazungumza. Allahu Akbar. Allahu Akbar
AYA YENYE MIUJIZA MIWILI MIKUBWA
Sura Ya Yunus Namba 10 Aya namba 20
وَيَقُولُونَ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٌ۬ مِّن رَّبِّهِۦۖ فَقُلۡ إِنَّمَا ٱلۡغَيۡبُ لِلَّهِ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ (٢٠)
TAFSIRI
Na wanasema: “Kwa nini haikuteremshwa juu yake kutoka kwa Mola wake Miujiza (tunayoitaKa)?” Basi sema: “ilimu ya mambo yasiyoonekana yapo kwa Mwenyeezi Mungu. Basi ngojeni; na mimi ni paamoja nanyi katika wanaongoja.”
SHEREHE
Aya Hii Ina Miujiza Miwili Mikubwa
Muujiza Wa Kwanza
Sura Namba 10
Aya Namba 20
Maneno 16
Herufi 68
Ukijumlisha namba hizi utapata jawabu la kushangaza. 10 + 20 + 16 + 68=114
Na Hii Namba 114 Inaashiria Jumla Ya Sura Zote za Kuruani
Muujiza Wa Pili
Hapo zamani Waarabu na Mataifa mengine yalikuwa yakitumia Herufi kuwakilisha namba. Na Kwa hiyo ukitumia Thamani ya herufi hizo na kufasiri Aya hii tunapata Jawabu la Kushangaza sana.
Kabla Ya Kuanza Utafiti Ningependelea kusema kwamba
(Katika Muujiza Huu Herufi Ndogo ya Hamza haina Thamani kwani Haikutumika wakati wa Mtume, iliongezwa baadaye kusaidia Wageni katika Matamshi ya kuruani.Na Al-Taa Iliyofungika yaani Al-Taa Marbutta ina Thamani ya 400 sawa na Al-Taa iliyo wazi yaani Taa ya Kawaida)
Sasa Tuanze na Hesabu.
Al-llam=10 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 30=300
Al-Alif=10 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 1 =10
Al-Nun=9 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 50=450
Al-Yaa=6 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 10=60
Al-Mim=6 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 40=240
Al-Waw=5 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 6=30
Al-Haa=3 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 5=15
Ta Marbutta=1 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 400=400
Al-Raa=3 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 200=600
Al-Qaf=2 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 100=200
Al-Faa=2 80 x Thamani Ya Herufi hapo zamani ni 2=160
Al-Ain=2 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 70=140
Al-Dha=2 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 900=1800
Al-Taa=2 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 400=800
Al-Baa=2 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 2=4
Al-Kaf=1 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 1=20
Al-Ghain=1 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 1000=1000
Al-Zaa=1 x Thamani Ya Herufi moja hapo zamani ni 7=7
Sasa Tujumlishe Majawabu tuliyopata Hapa Juu na tuone Muujiza wa kushangaza.
300 + 10 + 450 + 60 + 240 + 30 + 15 + 400 + 600 + 200 + 160 + 140 + 1800 + 800 + 4 + 20 + 1000 + 7=6236
Namba hii 6236 inaashiria Jumla ya Aya Zote za Kuruani ambazo ni 6236. Allahu Akbar.
Aya Moja inatupa Miujiza Miwili; Sura Za Kuruani na Aya zake Zote.
Na Ukiangalia Tafsiri Ya Aya Hii utaona Maajabu sana kwani Makafiri walikanusha hii Kuruani na Kumuomba Mtume (Sala Na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Imfikie).awape Muujiza Mwingine waone kwa macho yao wenyewe Na Mwenyeezi Mungu anawajibu katika Aya Hii Kwamba Siri ya Miujiza yake anaijua yeye peke yake Mwenyeezi Mungu na akamwambia Mtume na Waumini wasubiri kwani Yeye Mola yupo pamoja na wale wenye kusubiri. Sasa Aya hii inatupa Miujiza Mingine yenye kushangaza katika hilo hilo jibu la Suala lao.
Hesabu tulizoona hapa Ni Majibu kwa wakafiri wa leo wanapotaka Muujiza wauone kwa macho yao basi tuwaonyeshe muujiza huu katika Aya hii.
Aya inatuelezea yaliyotokea lakini kuna habari Nyinginezo za kushangaza zilizobebwa na Aya Hii na ambazo zinataka Hesabu ili kuchambua Siri Hiyo.
Allahu Akbar. Je unaona Ya Kushangaza? Allahu Akbar.
AYA TATU AMBAZO ZIMENISHANGAZA SANA. NI MUUJIZA MKUBWA
سُوۡرَةُ البَقَرَة Namba 2 Aya Namba 51
وَإِذۡ وَٲعَدۡنَا مُوسَىٰٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةً۬ ثُمَّ ٱتَّخَذۡتُمُ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِهِۦ وَأَنتُمۡ ظَـٰلِمُونَ (٥١)
TAFSIRI
51.Na (kumbukeni) tulipomwahidi Musa siku arubaini, (afanye ibada mfululizo, kisha tumpe Taurati). Mkamfanya ndama (kuwa mungu) baada yake, na mkawa madhalimu (wa nafsi zenu).
SHEREHE YA AYA
Aya inazungumzia Kisa cha Nabii Musa na siku Arubaini za Ibada
MUUJIZA WA HESABU
Jambo la kushangaza ni Muujiza Mwingine unajitokeza unaohusu Idadi za Herufi kuanzia neno أَرۡبَعِينَ lenye maana ya 40 mpaka mwisho wa Aya. Yaani Ukihesabu Herufi za kipande hiki utapata 40 sawa sawa na neno أَرۡبَعِينَ Allahu Akbar.
——————————-
سُوۡرَةُ المجَادلة Namba 58 Aya Namba 4
فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَہۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ مِن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۖ فَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ فَإِطۡعَامُ سِتِّينَ مِسۡكِينً۬اۚ ذَٲلِكَ لِتُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۗ وَلِلۡكَـٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ
(٤) TAFSIRI
4·Na asiyepata (uwezo huo)basi afunge saumu ya miezi miwili mfululizo kabla ya kugusana; na asiyeweza, basi awalishe maskini sitini (kila masikini kibaba kimoja cha chakula kinacholiwa sana katika mahala hapo). (Mumeambiwa) haya i1i mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake; na hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, (msipindukie); na kwa makafui iko adhabu iumizayo.
SHEREHE YA AYA
Aya Hii Inazungumzia Hukumu inayohusu Matusi anayotamka Mume kwa Mke kumtukana Na kumwambia “wewe ni kama mama yangu” au Tusi lolote lile kubwa la kumuumiza na kumtesa Mkewe basi adhabu yake kwa wakati tulionao ni Kufunga miezi miwili mfululizo au kulisha Maskini sitini. Aya Hii ilishuka ili kuvunja Itikadi iliyokuwa ikifuatwa wakati huo ya kutengana na Mke na kumnyima Haki zake kama vile kuolewa na Mtu mwingine.
MUUJIZA WA HESABU
Jambo la kushangaza ni kwamba Ukihesabu Herufi kuanzia Neno سِتِّينَ lenye maana ya 60 mpaka mwisho wa Aya utapata Herufi 60. Allahu Akbar
————————————
سُوۡرَةُ التّوبَة Namba 9 Aya Namba 80
ٱسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ أَوۡ لَا تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ إِن تَسۡتَغۡفِرۡ لَهُمۡ سَبۡعِينَ مَرَّةً۬ فَلَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡۚ ذَٲلِكَ بِأَنَّہُمۡ ڪَفَرُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ لَا يَہۡدِى ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَـٰسِقِينَ (٨٠)
TAFSIRI
8o.(Ewe Mtume)! Waombee msamaha (hao wanafiki) au usiwaombee; (yote sawa sawa). Hata ukiwaombea msamaha mara sabiini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao wamemkataa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu wavunjao amri (Zake).
SHEREHE YA AYA
Aya hii inahusu Ahadi aliyotoa Mwenyeezi Mungu kwamba Yeye hawaongozi wanaovunja amri zake na hata wakiombewa dua haitasaidia chochote.
MUUJIZA WA HESABU
Jambo la kushangaza kuna Muujiza Mwingine wa hesabu ambao unajitokeza katika Aya Hii. Ukihesabu Herufi kuanzia Neno سَبۡعِينَ Lenye maana ya 70 mpaka mwisho wa Aya utapata Herufi 70
MUUJIZA WA NENO مُدۡهَآمَّتَانِ NA NAMBA 8 INAYOASHIRIA MILANGO YA PEPO
فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (٦٣) مُدۡهَآمَّتَانِ (٦٤) فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (٦٥)
TAFSIRI
63.Basi ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha, (kuwa si neema yake)? 64.Yenye rangi nzuri ya kijani kilichowiva (bara bara). 65.Basi ipi katika neema za Mola wenu mnayoikanusha, (kuwa si neema yake)?
SHEREHE YA AYA
Aya Namba 64 ni Neno la pekee katikati ya sura za kuruani tukufu. kwani Kuna Aya zenye neno moja mwanzoni mwa kuruani lakini katikati ya sura za kuruani hakuna Aya Yenye neno moja isipokuwa hili tu peke yake. Neno Hili ni sifa za Mabustani mawili huko peponi na maana yake ni Rangi Iliyowiva ya Kijani. Yaani hayo mabustani rangi yake ni Green Iliyowiva. Jambo la kushangaza ni kwamba neno hili linatupa Namba 8 kwa njia mbalimbali. Angalia Utafiti Hapa chini wa kushangaza.
Namba Hii Inathibitisha Hadithi Ya Mtume (Sala na Amani za Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Inayosema kwamba Milango ya Pepo ni Minane. Hadithi hii ipo katika Vitabu vya Bukhari Na Muslim
وَعَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ” فِي الْجَنَّةِ ثَمَانِيَةُ أَبْوَابٍ مِنْهَا: بَابٌ يُسَمَّى الرَّيَّانَ لَا يدْخلهُ إِلَّا الصائمون “
Sahl b. Sa’d reported God’s messenger as saying, “In paradise there are eight gates among which is a gate called Ar-Rayyan which only those who fast will enter.” (Bukhari and Muslim.)
MUUJIZA WA NAMBA 8
Angalia Utafiti Wa kushangaza hapa Chini
1/Neno La Aya hii lina herufi 8
2/Namba Ya Aya Ni 64 na Namba hii ni sawa na 8 X 8
3/Ukihesabu Maneno Kuanzia mwanzo wa kuruani tukufu mpaka Aya namba 63 kabla Ya Neno hili مُدۡهَآمَّتَانِ utapata maneno 77312 na namba hii ni sawa na 8 X 8 X 8 x 151
4/Herufi za neno مُدۡهَآمَّتَانِ zimetumika katika Sura Ya Al-Rahman mara 1152 na namba hii ni sawa na 8 x 8 x 18 Namba 18 hapa inaashiria Herufi za Aya َبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ yaani Aya hii ina herufi 18 Na Ni Aya ambayo ipo kabla na baada ya Aya namba 64.
5/Aya zinazozungumzia Pepo Mbili katika Sura Ya Al-Rahman ni 16 Namba hii ni sawa na 8 X 2 (Aya hizi ni kuanzia Aya Namba 46 mpaka Aya namba 61 na Aya ya mwisho namba 61 inasema َبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ Na Aya ambazo zinazungumzia Mabustani mengine mawili Ni 16 pia Namba hii ni sawa na 8 X 2 (Aya Hizi kuanzia Aya Namba 62 mpaka Aya namba 77 na Aya Ya Mwisho namba 77 inasema َبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ)
Katika Aya hizi 16 zinazozungumzia Mabustani Mawili huko Peponi ni 8 mara mbili na inakubaliana na Hadithi ya Mtume iliyosema kwamba kila Bustani lina Milango 8.
Mabustani Mawili ya kwanza yana milango 16 na Mabistani mawili ya pili yana Milango 16 pia. Angalia Mpanglio Huu wa Kiajabu. Je kuna Mtu gani anayeweza Kuandika Kitabu kama hiki Ulimwenguni? Ni Nani anayeweza kupanga Mpangilio wa Ajabu Kama huu.
Hapa Mwenyeezi Mungu Anatuhakikishia Kuwepo kwa Pepo. Kwamba sio Uongo.
Fikiri jinsi Namba 8 Ilivyokariri.
Angalia Maajabu Haya yasiyo na Mwisho. Neno Hili halipo sehemu hiyo bure bure. Bali limepangwa na yule yule aliyeumba ulimwengu. Ameliweka hapo kiajabu sana na Limehesabiwa na huwezi kulibadili sehemu nyingine.
Angalia Muujiza katika neno moja tu.
Neno Hili linasifu Mabustani huko Peponi kwamba Yana Rangi ya Kijani iliyowiva lakini angalia Miujiza mingine iliyoambatana na Aya Hii. Allahu Akbar.
Miujiza Mingine ni Hesabu ya Milango ya pepo ambayo ni Minane kama alivyosema Mtume katika Hadithi iliyopokelewa na Bukhari na Muslim
Msomi yeyote aliyesomea Elimu Ya Hesabu kwa ujumla na Pia kusomea Hesabu za Probabilities atakubaliana kwamba Haiwezekani namba Kukariri kiasi hiki na iwe Bahati Nasibu. Haiwezekani kabisa. Hizi namba zimepangwa kwa makusudi na Mwenyeezi Mungu Mtukufu.
Tumeona Namba 8 Imekariri hapa kwa njia mbalimbali na hii inathibitisha Ukubwa wa Elimu ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Allahu Akbar.
Kuna wale wanaodharau Kuruani. Kama wana uwezo basi nao waandike kitabu kama hiki na waonyeshe miujiza kama hii. Hakuna awezaye.
Mfano huu mdogo ni neno moja tu. Na Katika Kuruani kila Herufi, Neno au Aya zina Maajabu mbalimbali yasiyo na Mwisho.
MUUJIZA WA RANGI (أَلْوَانُهُ) NA MILANGO YA PEPONI NA MOTONI
1/MUUJIZA WA RANGI (أَلْوَانُهُ)
Sura Namba 16 Al-Nahl Aya Namba 13
وَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ
TAFSIRI
13.Na (akakuumbieni) hivi alivyovitawanya katika ardhi vya rangi mbali mbali. Hakika katika hayo imo Ishara kwa watu wanaosikia mauidha.
SHEREHE
1/Neno La Saba ni أَلْوَانُهُ (Rangi Zake)Ukihesabu Kuanzia mwanzo wa Aya Na Ni neno la 7 ukihesabu kuanzia Mwisho wa Aya kuelekea mwanzo wa Aya (Reverse) Mpaka Neno أَلْوَانُهُ
2/Herufi Za Aya hii ni 49 Na Namba hii ni sawa na 7 X 7
3/Aya Namba 13 inalingana na jumla ya Maneno Ya Aya ambayo ni 13
4/Namba 7 (Namba 7 Ni Position ya Neno أَلْوَانُهُ)X Namba 13 (Jumla Ya Maneno ya Aya Hii) =91
Ukijumlisha Kuanzia Aya namba 1 ya Sura Ya Al-Nahl mpaka Aya Namba 13 Unapata Jawabu Namba 91 Pia (1+2 +3+4+5+6+7+8+9+10+11+12+13=91)
5/Ukihesabu Maneno Kuanzia Mwanzo wa Sura Mpaka mwisho wa Aya hii utapata Maneno=147
Na namba hii ni sawa na 7 X 7 X 3
Namba hizi Tatu zinaashiria Maajabu Yafuatayo:
Namba 7 Ya Kwanza Inaashiria Namba 7 ya kukariri kwa Neno أَلْوَانُهُ katika Kuruani
Namba 7 Ya Pili inaashiria Namba za Rangi 7 Tunazozijua Duniani (Visible Spectrum Colours)na hizi ndizo zinafanya Mwanga Tunaoujua. (White Light). Ukichambua Mwanga huu utapata Rangi 7.
(Visible light travels at a speed of 300,000 km per second and can be broken down into seven colors. From longest to shortest wavelength, they are: red, orange, yellow, green, blue, indigo, and violet. To be clear, color is the eye’s perception of different wavelengths of electromagnetic light)
Namba 3 Inaashiria Namba 3 ambazo ni Msingi wa Rangi zote. Yaani Rangi zote duaniani zinatokana na Rangi Tatu, Nazo ni Nyekundu, Buluu na Manjano. Michanganyiko Mbalimbali wa Rangi Hizi tatu inazalisha Rangi nyinginezo tunazozijua.
(The three additive primary colours are red, green, and blue; this means that, by additively mixing the colours red, green, and blue in varying amounts, almost all other colours can be produced, and, when the three primaries are added together in equal amounts, white is produced).
6/Maneno 6 yametajika kabla na baada ya neno أَلْوَانُهُ na tunaelewa kwamba Neno hili ni la 7 Jambo la kushangaza ni kwamba Katika Kuruani neno أَلْوَانُهُ limetajika mara 7 katika Aya 6 tu peke yake.
Kuna Aya Moja katika hizi sita ambayo imelitumia neno أَلْوَانُهُ mara 2. Angalia Namba zinavyolingana na kushangaza.
7/Jumla ya Maneno ya Aya hii ni 13 Ajabu ni kwamba Prime Number ya 6 ni 13 (2,3,5,7,11,na 13)
(Prime Number ni Mlango katika Elimu Ya Hesabu)
Angalia Mlinganisho wa Kihesabu unavyoshangaza baina ya Namba 13 na 6.
Tumeona Jumla ya Maneno ya Aya ni 13 Yaani kila Upande wa Neno أَلْوَانُهُ ni maneno 6 Ukijumlisha Jumla ya Maneno 6 ya kushoto na 6 ya Kulia na Neno أَلْوَانُهُ utapata 13
8/Ukijumlisha Jumla ya Aya za Sura 6 katika Kuruani ambazo zimetaja neno أَلْوَانُهُ utapata Jumla ya Aya zote ni 180
Aya hizi ni kama zufuatazo
Sura Namba 16 Aya Namba 13
Sura Namba 16 Aya Namba 69
Sura Namba 30 Aya Namba 22
Sura Namba 35 Aya Namba 27
Sura Namba 35 Aya Namba 28
Sura Namba 39 Aya Namba 21
13 + 69 + 22 + 27 +28 + 21=180
Na Namba 180 ni sawa na 66 + 114
Neno أَلْوَانُهُ limetajika Mara Sita katika Sura 4 kwani kuna Sura Mbili ambazo Neno hili limetajika mara mbili. Tukijumlisha Namba za Hizi Sura Nne
16 + 30 + 35 + 39=120
Na Namba 120 ni sawa na 6 + 114
Jumla ya Maneno Ya Aya Zote 6 ni 120
Na Namba Hii ni sawa na 6 + 114
Angalia Namba 6 ilivyokariri na Namba 114 inaashiria Jumla ya Idadi za Sura Za Kuruani
9/Katika Aya Hizi 6 zimetumika herufi za Kiarabu 27 na ya 28 ambayo haikutumika ni “Herufi ظ DHA”
ا ب ت ث ج ح خ د ذ ر ز س ش ص ض ط ظ ع غ ف ق ك ل م ن هـ و ي
Hii ni Herufi ya 17 katika mpangilio wa herufi 28 za lugha ya Kiarabu. Na Jambo la kushangaza ni kwamba namba 17 Ni Prime Number ya 7.
Angalia Tunapata tena namba 7 ambayo ina uhusiano na neno أَلْوَانُهُ ambalo pia limetajika mara 7 katika Aya 6 na pia ni neno la 7 katika Aya ifuatayo:
وَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ
10/Tukijumlisha Positions za Herufi za Kiarabu zote kuanzia 1 mpaka ya mwisho 28 (Yaani 1 + 2 + 3 + 4 + 5 mpaka 28)
ا ب ت ث ج ح خ د ذ ر ز س ش ص ض ط ظ ع غ ف ق ك ل م ن هـ و ي
utapata jawabu 406 na kisha tukitoa ile Herufi Ya ظ DHA ambayo haikutajika (Herufi ya 17) utapata Jawabu 389 (406-17=389) na la kushangaza Namba 389 ni Prime Number Ya 77!!!
Angalia Maajabu tunapata Namba ya Maajabu yaani 77 ambayo ni sawa na Jumla ya Positions za herufi za neno أَلْوَانُهُ katika mpangilio wa Herufi za Lugha Ya Kiarabu.
Yaani Alif 1 + Al-Lam 23 + Al-Waw 27 + Al-Alif 1 + Al-Nun 25=77
na Namba 77 Mara Sura 4 ambazo zimetaja neno أَلْوَانُهُ unapata 308 (77 x 4=308) na ajabu ni kwamba tukijumlisha Aya Zote za Sura Nne utapata 308 pia kama nilivyofanya hapa chini.
Neno أَلْوَانُهُ limetajika Mara 7 katika Sura Zifuatazo.
Sura Namba 16 – Ina Jumla za Aya 128
Sura Namba 30 -Ina Jumla za Aya 60
Sura Namba 35 -Ina Jumla za Aya 45
Sura Namba 39 -Ina Jumla za Aya 75
Ukijumlisha Idadi za Aya zote Utapata 128 + 60 + 45 + 75=308
Angalia Mlinganisho wa Kiajabu. Tunapata Namba 308 mara mbili. Kwa kweli inashangaza sana. na hii ndiyo Kuruani Tukufu ambaye imejaa Miujza isiyo na Mwisho. Allahu Akbar.
11/Katika Kuruani Neno أَلْوَانُهُ (Plural Ya Neno Rangi) limetajika Katika Aya 6 ambazo zipo katika Sura 4 tu. Jambo la kushangaza ni kwamba Herufi ث THA imetumika na kukariri katika Aya Hizi 6 Mara 6 na pia Imetumika katika Sura Nne mara 114 na Ajabu kubwa ni kwamba Namba 114 Inaashiria Jumla ya Sura zote za Kuruani ambazo ni 114
Na Herufi ض DHWAD ni pekee ambayo imetumika katika Aya Hizi 6 mara 4 Na pia Imetumika katika Sura Nne mara 114 na Ajabu kubwa ni kwamba namba hii ni Idadi ya Sura zote za Kuruani ambazo ni 114
Sura Namba 16 Herufi THA Imekariri mara 45 na DHWAD mara 32
Sura Namba 16 Herufi THA Imekariri mara 27 na DHWAD mara 30
Sura Namba 16 Herufi THA Imekariri mara 13 na DHWAD mara 20
Sura Namba 16 Herufi THA Imekariri mara 29 na DWAD mara 32
Jumla ya Herufi THA= 45 + 27 + 13 + 29=114
Jumla ya Herufi DWAD=32 + 30 + 20 + 32=114
Angalia Muujiza. Allahu Akbar. Namba 114 ni Jumla Ya Sura Za Kuruani Tukufu.
Unaona Muujiza usio na Mwisho? Je unaona Maajabu. Allahu Akbar.Ufundi wa Hali Ya Juu. Haya ndiyo Maneno ya Kuruani. Ni Maneno ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu aliyeumba Ulimwengu/Malimwengu ni Yule aliye na Elimu kubwa isiyo Mfano. Ni yule aliyetuumba kwa udongo. Na marejeo yetu ni kwake. Allahu Akbar.
12/Hebu tuchunguze Rangi ya Kijani (Green) Katika Sura Namba 18 Aya Namba 31
Mwenyeezi Mungu anasema kwamba watu watakaobarikiwa kuingia Peponi watavaa Nguo za rangi ya Kijani (Green)
أُوْلَـٰٓٮِٕكَ لَهُمۡ جَنَّـٰتُ عَدۡنٍ۬ تَجۡرِى مِن تَحۡتِہِمُ ٱلۡأَنۡہَـٰرُ يُحَلَّوۡنَ فِيہَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ۬ وَيَلۡبَسُونَ ثِيَابًا خُضۡرً۬ا مِّن سُندُسٍ۬ وَإِسۡتَبۡرَقٍ۬ مُّتَّكِـِٔينَ فِيہَا عَلَى ٱلۡأَرَآٮِٕكِۚ نِعۡمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتۡ مُرۡتَفَقً۬ا (٣١)
TAFSIRI
31.Hao watapata mabustani ya milele yanayopita mito (ya maji) mbele yake. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu na watavaa nguo za kijani za hariri laini na za hariri nzito; wanaengemea humo juu ya vitanda vilivyopambwa (makochi). Ni malipo mazuri yaliyoje hayo! Na mahali bora palioje hapo (pa kupumzikia).
SHEREHE
Rangi ya Kijani (Green) imetajika katika Kuruani Mara 8 katika Sura Na Aya Zifuatazo:
Sura Namba 6 Aya Namba 99,
Sura Namba 12 Aya Namba 43 na 46,
Sura Namba 18 Aya Namba 31,
Sura Namba 22 Aya Namba 63,
Sura Namba 36 Aya Namba 80,
Sura Namba 55 Aya Namba 76
na Sura Namba 76 Aya Namba 21
Jambo la kushangaza ni kwamba Rangi ya Kijani خُضۡرً۬ا imetajika katika kuruani mara 8 kulingana na Milango ya Pepo. Na kama tulivyosoma katika Kuruani kwamba Nguo watakazovaa watu wa Peponi zitakuwa na Rangi ya Kijani.
Na Kuna Hadithi Ya Mtume Kutoka katika Sahih Al-Bukhari Inayosema kwamba Milango ya Peponi ni 8.
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي مَرْيَمَ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ مُطَرِّفٍ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو حَازِمٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ “ فِي الْجَنَّةِ ثَمَانِيَةُ أَبْوَابٍ، فِيهَا باب يُسَمَّى الرَّيَّانَ لاَ يَدْخُلُهُ إِلاَّ الصَّائِمُونَ ”.
TAFSIRI
Alielezea Sahl bin Sa`d: Mtume (ﷺ) Alisema, “Pepo ina milango minane, na Mojawapo (Ya Milango Hii Minane) Unaitwa Ar-Raiyan Hakuna atakayeingia Pepo kwa kutumia Mlango huu isipokuwa Wale wenye Kufunga (Saumu) Reference-Sahih al-Bukhari 3257
2/NYONGEZA KUHUSU MILANGO YA MOTONI NA PEPONI
Nilizungumzia siku zilizopita katika mlango wa kwanza wa “ELIMU” ya website hii kuhusu Milango ya Motoni na tukaona Muujiza unaohusiana na Idadi ya Milango 7 leo ningependelea kufanya nyongeza ya Muujiza huu. Kwanza ningependelea tukumbushane Muujiza na kisha tuzungumze Mapya.
1/kama Anavyosema Mwenyeezi Mungu katika Kuruani sura Namba 15 Aya Namba 43 na 44 kuhusu Milango 7 ya Motoni (Jahannam)
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوۡعِدُهُمۡ أَجۡمَعِينَ (٤٣) لَهَا سَبۡعَةُ أَبۡوَٲبٍ۬ لِّكُلِّ بَابٍ۬ مِّنۡہُمۡ جُزۡءٌ۬ مَّقۡسُومٌ (٤٤)
TAFSIRI
43.Na bila shaka Jahanamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote.
44.Ina miJango saba; na kwa kila mlango iko sehemu yao iliyogawanywa (ya kuwa hii ya mlango fulani na hii ya mlango fulani).
2/Jambo la kushangaza ni kwamba Neno ABWAB أَبۡوَٲبٍ۬ limetajika katika Kuruani mara 15 sawasawa na Jumla Ya Milango ya Motoni na Peponi 8 + 7=15
Hebu tupange Sura zote ambazo zimetaja neno MILANGO katika Kuruani Tukufu
1.Sura Namba 2 Aya Namba 189
2.Sura Namba 6 Aya Namba 44
3.Sura Namba 7 Aya Namba 40
4.Sura Namba 12 Aya Namba 23
5.Sura Namba 12 Aya Namba 67
6.Sura Namba 15 Aya Namba 44
7.Sura Namba 16 Aya Namba 29
8.Sura Namba 38 Aya Namba 50
9.Sura Namba 39 Aya Namba 71
10.Sura Namba 39 Aya Namba 72
11.Sura Namba 39 Aya Namba 73
12.Sura Namba 40 Aya Namba 76
13.Sura Namba 43 Aya Namba 34
14.Sura Namba 54 Aya Namba 11
15.Sura Namba 78 Aya Namba 19
Tumezitaja Sura zote ambazo zimetumia neno “MILANGO” kufuatana na Mpangilio wa Msahafu kuanzia Sura ya 2 mpaka Sura Namba 78
Ningependelea kusema kwamba Katika Aya hizi 15 siyo zote zinazungumzia Milango ya Peponi na Motoni. Yaani kuna Aya Nyinginezo ambazo zimetaja Neno “MILANGO” lakini inayohusiana na Madhumuni Mengineyo na siyo Milango ya Pepo au Moto.
Sasa Angalia Ya Kushangaza; Katika Aya zote 15 Hapa Juu tukichunguza Sura ya 7 (Namba 16, Aya Namba 29) na Sura ya 8 (Sura Namba 38 Aya Namba 50) Tutakuta Aya zenye kushangaza Sana na inaonyesha Kwamba Mpangilio huu siyo bure bure bali kwa Hekima Kubwa sana.
Sura ya 7, Sura namba 16 Aya Namba 29 Inasema:
فَٱدۡخُلُوٓاْ أَبۡوَٲبَ جَهَنَّمَ خَـٰلِدِينَ فِيہَاۖ فَلَبِئۡسَ مَثۡوَى ٱلۡمُتَكَبِّرِينَ (٢٩)
TAFSIRI 19.”Kwa hivyo ingieni milango ya Jahanamu kwa kukaa humo milele. Basi ni Pabaya kabisa makazi ya wafanyao kiburi.”
Na Sura ya 8, Sura Namba 38 Aya Namba 50
Inasema: جَنَّـٰتِ عَدۡنٍ۬ مُّفَتَّحَةً۬ لَّهُمُ ٱلۡأَبۡوَٲبُ (٥٠)
TAFSIRI
50.Mabustani ya kukaa milele yatakayofunguliwa milango (yake) kwa ajili yao.
SHEREHE
Angalia Muujiza Katika Aya 15 Hapa Juu siyo zote zinazungumzia Milango ya Moto na Pepo. Lakini tulipochunguza Sura Ya 7 tukakuta Aya inazungumzia Moto wa Jahannam na Ajabu ni kwamba mpangilio wa Sura Namba 7 hapa inaashiria Milango ya Moto wa Jahannam
Na Sura Ya 8 tulipoichunguza tukakuta Aya inazungumzia Milango ya Peponi Namba 7 Inaashiria Milango ya Peponi.
Yaani Muujiza mpaka katika Namba za Sura!!!! Allahu Akbar.
Kwa kweli hakuna Mwisho. Miujiza Imetupita Elimu. Angalia Mpangilio huu wa ajabu. Hii Inathibitisha kwamba Maneno ya kuruani ni Ya Mwenyeezi Mungu kwani hakuna awezaye kuandika kwa mpangilio wa kiajabu kama huu.

Mwanga Wa Jua au Nyota ni Mweupe lakini ni mchanganyiko wa Rangi 7. Kila Rangi lina kipimo cha Wimbi (Wavelength) lililo tofauti na lingine

Rangi 7 ambazo zinafanya Mwanga Mweupe (White Light), Rangi Zote Duniani asili yake ni Rangi 3 ambazo zikichanganywa tunapata nyinginezo na hizi ni Nyekundu, Kijani na Buluu

Hizi ni Rangi 7 zinazofanya mwanga wa Jua. Na vipimo vya kila Rangi
MATUMIZI YA KIAJABU YA NENO رجل (RAJUL) YAANI MWANAUME NA امرا (IMRAA) LENYE MAANA YA MWANAMKE
NENO رجل (RAJUL) lenye maana ya “Mwanamume” Mmoja (yaani singular)(Pamoja na Derivatives (Mushtaqaat) zake zote. Limekariri katika Kuruani Mara 24 na Neno امرا (IMRAA) lenye maana ya “Mwanamke” Mmoja (yaani singular)(Pamoja na Derivatives (Mushtaqaat) zake zote. Limekariri katika Kuruani Mara 24 pia.
Nimekusanya Aya Zote ambazo zimetumia Haya Maneno mawili katika Singular tu na nimeacha Yale yenye kutaja Wawili au zaidi ya Mmoja yaani (Plural Words). Kwa hiyo katika Singular Neno Mwanaume na Mwanamke na Derivatives zake (Mushtaqaat Zake) zimetajika sawa sawa mara 24.
Huu usawa wa kutajika kwa mara 24 unaashiria usawa wa Haki baina ya Mwanamke na Mwanaume. Usawa katika Imani, Sala na Mengineyo ya Dini.
Angalia Mlinganisho uliojitokeza wa Maneno haya. Kutajika Kwa Mwanaume sawasawa na kutajika kwa Mwanamke.
Hii inaonyesha Wote wawili ni Binaadamu na wote wanabidi kufuata maagizo ya Dini. Allahu Akbar.
Angalia Kuruani Ilivyopangwa. Hii inaonyesha dalili kwamba Kuruani imepangwa kimakusudi na siyo bure bure tu.
Hapa chini nimeorodhesha Aya zote ambazo zimetaja haya maneno mawili. Hapa Chini Katika Kuruani yote Aya zenye Neno “MWANAUME” katika Singular na pia na المشتقات (Derivatives) Mushtaqaat zake.
Sura Na Namba Ya Aya
{ يايها الذين امنوا اذا تداينتم بدين الي اجل مسمي فاكتبوه وليكتب بينكم كاتب بالعدل ولا ياب كاتب ان يكتب كما علمه الله فليكتب وليملل الذي عليه الحق وليتق الله ربه ولا يبخس منه شيا فان كان الذي عليه الحق سفيها او ضعيفا او لا يستطيع ان يمل هو فليملل وليه بالعدل واستشهدوا شهيدين من رجالكم فان لم يكونا رجلين فرجل وامراتان ممن ترضون من الشهدا ان تضل احديهما فتذكر احديهما الاخري ولا ياب الشهدا اذا ما دعوا ولا تسموا ان تكتبوه صغيرا او كبيرا الي اجله ذلكم اقسط عند الله واقوم للشهده وادني الا ترتابوا الا ان تكون تجره حاضره تديرونها بينكم فليس عليكم جناح الا تكتبوها واشهدوا اذا تبايعتم ولا يضار كاتب ولا شهيد وان تفعلوا فانه فسوق بكم واتقوا الله ويعلمكم الله والله بكل شي عليم } [البقرة:282].
{ ولكم نصف ما ترك ازوجكم ان لم يكن لهن ولد فان كان لهن ولد فلكم الربع مما تركن من بعد وصيه يوصين بها او دين ولهن الربع مما تركتم ان لم يكن لكم ولد فان كان لكم ولد فلهن الثمن مما تركتم من بعد وصيه توصون بها او دين وان كان رجل يورث كلله او امراه وله اخ او اخت فلكل وحد منهما السدس فان كانوا اكثر من ذلك فهم شركا في الثلث من بعد وصيه يوصي بها او دين غير مضار وصيه من الله والله عليم حليم } [النساء:12].
{ ولو جعلنه ملكا لجعلنه رجلا وللبسنا عليهم ما يلبسون } [الأنعام:9].
{ اوعجبتم ان جاكم ذكر من ربكم علي رجل منكم لينذركم ولتتقوا ولعلكم ترحمون } [الأعراف:63].
{ اوعجبتم ان جاكم ذكر من ربكم علي رجل منكم لينذركم واذكروا اذ جعلكم خلفا من بعد قوم نوح وزادكم في الخلق بصطه فاذكروا الا الله لعلكم تفلحون } [الأعراف:69].
{ واختار موسي قومه سبعين رجلا لميقتنا فلما اخذتهم الرجفه قال رب لو شيت اهلكتهم من قبل وايي اتهلكنا بما فعل السفها منا ان هي الا فتنتك تضل بها من تشا وتهدي من تشا انت ولينا فاغفر لنا وارحمنا وانت خير الغفرين } [الأعراف:155].
{ اكان للناس عجبا ان اوحينا الي رجل منهم ان انذر الناس وبشر الذين امنوا ان لهم قدم صدق عند ربهم قال الكفرون ان هذا لسحر مبين } [يونس:2].
{ وجاه قومه يهرعون اليه ومن قبل كانوا يعملون السيات قال يقوم هولا بناتي هن اطهر لكم فاتقوا الله ولا تخزون في ضيفي اليس منكم رجل رشيد } [هود:78].
{ نحن اعلم بما يستمعون به اذ يستمعون اليك واذ هم نجوي اذ يقول الظلمون ان تتبعون الا رجلا مسحورا } [الإسراء:47].
{ قال له صاحبه وهو يحاوره اكفرت بالذي خلقك من تراب ثم من نطفه ثم سويك رجلا } [الكهف:37].
{ ان هو الا رجل به جنه فتربصوا به حتي حين } [المؤمنون:25].
{ ان هو الا رجل افتري علي الله كذبا وما نحن له بمومنين } [المؤمنون:38].
{ او يلقي اليه كنز او تكون له جنه ياكل منها وقال الظلمون ان تتبعون الا رجلا مسحورا } [الفرقان:8].
{ وجا رجل من اقصا المدينه يسعي قال يموسي ان الملا ياتمرون بك ليقتلوك فاخرج اني لك من النصحين } [القصص:20].
{ ما جعل الله لرجل من قلبين في جوفه وما جعل ازوجكم الي تظهرون منهن امهتكم وما جعل ادعياكم ابناكم ذلكم قولكم بافوهكم والله يقول الحق وهو يهدي السبيل } [الأحزاب:4].
{ وقال الذين كفروا هل ندلكم علي رجل ينبيكم اذا مزقتم كل ممزق انكم لفي خلق جديد } [سبأ:7].
{ واذا تتلي عليهم ايتنا بينت قالوا ما هذا الا رجل يريد ان يصدكم عما كان يعبد اباوكم وقالوا ما هذا الا افك مفتري وقال الذين كفروا للحق لما جاهم ان هذا الا سحر مبين } [سبأ:43].
{ وجا من اقصا المدينه رجل يسعي قال يقوم اتبعوا المرسلين } [يس:20].
{ ضرب الله مثلا رجلا فيه شركا متشكسون ورجلا سلما لرجل هل يستويان مثلا الحمد لله بل اكثرهم لا يعلمون } [الزمر:29].
{ وقال رجل مومن من ال فرعون يكتم ايمنه اتقتلون رجلا ان يقول ربي الله وقد جاكم بالبينت من ربكم وان يك كذبا فعليه كذبه وان يك صادقا يصبكم بعض الذي يعدكم ان الله لا يهدي من هو مسرف كذاب } [غافر:28].
{ وقالوا لولا نزل هذا القران علي رجل من القريتين عظيم } [الزخرف:31].
———————————————————–
Hapa Chini Katika Kuruani yote Aya zenye Neno “MWANAMKE” katika Singular na pia na المشتقات (Derivatives) Mushtaqaat zake.
Sura na Namba Ya Aya
{ اذ قالت امرات عمرن رب اني نذرت لك ما في بطني محررا فتقبل مني انك انت السميع العليم } [آل عمران:35].
{ قال رب اني يكون لي غلم وقد بلغني الكبر وامراتي عاقر قال كذلك الله يفعل ما يشا } [آل عمران:40].
{ ولكم نصف ما ترك ازوجكم ان لم يكن لهن ولد فان كان لهن ولد فلكم الربع مما تركن من بعد وصيه يوصين بها او دين ولهن الربع مما تركتم ان لم يكن لكم ولد فان كان لكم ولد فلهن الثمن مما تركتم من بعد وصيه توصون بها او دين وان كان رجل يورث كلله او امراه وله اخ او اخت فلكل وحد منهما السدس فان كانوا اكثر من ذلك فهم شركا في الثلث من بعد وصيه يوصي بها او دين غير مضار وصيه من الله والله عليم حليم } [النساء:12].
{ وان امراه خافت من بعلها نشوزا او اعراضا فلا جناح عليهما ان يصلحا بينهما صلحا والصلح خير واحضرت الانفس الشح وان تحسنوا وتتقوا فان الله كان بما تعملون خبيرا } [النساء:128].
{ فانجينه واهله الا امراته كانت من الغبرين } [الأعراف:83].
{ وامراته قايمه فضحكت فبشرنها باسحق ومن ورا اسحق يعقوب } [هود:71].
{ قالوا يلوط انا رسل ربك لن يصلوا اليك فاسر باهلك بقطع من اليل ولا يلتفت منكم احد الا امراتك انه مصيبها ما اصابهم ان موعدهم الصبح اليس الصبح بقريب } [هود:81].
{ وقال الذي اشتريه من مصر لامراته اكرمي مثويه عسي ان ينفعنا او نتخذه ولدا وكذلك مكنا ليوسف في الارض ولنعلمه من تاويل الاحاديث والله غالب علي امره ولكن اكثر الناس لا يعلمون } [يوسف:21].
{ وقال نسوه في المدينه امرات العزيز ترود فتيها عن نفسه قد شغفها حبا انا لنريها في ضلل مبين } [يوسف:30].
{ قال ما خطبكن اذ رودتن يوسف عن نفسه قلن حش لله ما علمنا عليه من سو قالت امرات العزيز الن حصحص الحق انا رودته عن نفسه وانه لمن الصدقين } [يوسف:51]. { الا امراته قدرنا انها لمن الغبرين } [الحجر:60].
{ واني خفت المولي من وراي وكانت امراتي عاقرا فهب لي من لدنك وليا } [مريم:5].
{ قال رب اني يكون لي غلم وكانت امراتي عاقرا وقد بلغت من الكبر عتيا } [مريم:8].
{ اني وجدت امراه تملكهم واوتيت من كل شي ولها عرش عظيم } [النمل:23].
{ فانجينه واهله الا امراته قدرنها من الغبرين } [النمل:57].
{ وقالت امرات فرعون قرت عين لي ولك لا تقتلوه عسي ان ينفعنا او نتخذه ولدا وهم لا يشعرون } [القصص:9].
{ قال ان فيها لوطا قالوا نحن اعلم بمن فيها لننجينه واهله الا امراته كانت من الغبرين (32)
ولما ان جات رسلنا لوطا سي بهم وضاق بهم ذرعا وقالوا لا تخف ولا تحزن انا منجوك واهلك الا امراتك كانت من الغبرين (33) }
[العنكبوت:32-33].
{ يايها النبي انا احللنا لك ازوجك التي اتيت اجورهن وما ملكت يمينك مما افا الله عليك وبنات عمك وبنات عمتك وبنات خالك وبنات خلتك التي هاجرن معك وامراه مومنه ان وهبت نفسها للنبي ان اراد النبي ان يستنكحها خالصه لك من دون المومنين قد علمنا ما فرضنا عليهم في ازوجهم وما ملكت ايمنهم لكيلا يكون عليك حرج وكان الله غفورا رحيما } [الأحزاب:50].
{ فاقبلت امراته في صره فصكت وجهها وقالت عجوز عقيم } [الذاريات:29].
{ ضرب الله مثلا للذين كفروا امرات نوح وامرات لوط كانتا تحت عبدين من عبادنا صلحين فخانتاهما فلم يغنيا عنهما من الله شيا وقيل ادخلا النار مع الدخلين (10) وضرب الله مثلا للذين امنوا امرات فرعون اذ قالت رب ابن لي عندك بيتا في الجنه ونجني من فرعون وعمله ونجني من القوم الظلمين (11) } [التحريم:10-11].
{ وامراته حماله الحطب } [المسد:4].
UMRI WA MTUME NA IDADI YA MILANGO YA PEPO NA MOTO
Katika Mlango wa Kwanza wa “Elimu” nilizungumzia Muujiza Unaohusiana na Milango ya Peponi na Motoni na Alhamdulilahi Leo nitafanya Nyongeza katika Habari hii. Allahu Akbar.
Katika Kuruani Nzima kuna Aya Moja Ndefu ambayo inazungumzia Moto wa Jahannam katika
Sura Ya Al-Mudathir Namba 74 Aya Namba 31.
Al-Mudathir ni Jina Lingine la Mtume Mohamad ﷺ
وَمَا جَعَلۡنَآ أَصۡحَـٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَـٰٓٮِٕكَةً۬ۙ وَمَا جَعَلۡنَا عِدَّتَہُمۡ إِلَّا فِتۡنَةً۬ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ لِيَسۡتَيۡقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَـٰبَ وَيَزۡدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِيمَـٰنً۬اۙ وَلَا يَرۡتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَـٰبَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۙ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِہِم مَّرَضٌ۬ وَٱلۡكَـٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِہَـٰذَا مَثَلاً۬ۚ كَذَٲلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَہۡدِى مَن يَشَآءُۚ وَمَا يَعۡلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَۚ وَمَا هِىَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡبَشَرِ (٣١)
TAFSIRI
31.Na hatukuweka walinzi wa huo Moto ila Malaika, wala hatukuifanya idadi yao (hiyo ya kumina tisa) i1a kuwa mtihani kwa wale waliokufuru; ili wawe na yakini waliopewa Vitabu (kabla yenu), na walioamini wazidi katika imani yao, wala wasiwe na shaka wale waliopewa Kitabu (kabla yenu) wala Waislamu, na ili walio na ugonjwa katika nyoyo zao na waliokufuru waseme: “Apenddea nini Mwenyezi Mungu kwa mfano huu?” Namna hii Mwenyezi Mungu humuacha kupotea amtakaye na humuongoza amtakaye. Wala hapana yoyote ajuaye majesbi ya Mola wako ila Yeye tu; na wala haikuwa (kutaja Moto na mambo yake) ila ni ukumbusho kwa viumbe.
Na Katika Kuruani Nzima kuna Aya Moja Ndefu ambayo inazungumzia Pepo ambayo ipo katika
Sura Ya Mohamad Namba 47 Aya Namba 15
مَّثَلُ ٱلۡجَنَّةِ ٱلَّتِى وُعِدَ ٱلۡمُتَّقُونَۖ فِيہَآ أَنۡہَـٰرٌ۬ مِّن مَّآءٍ غَيۡرِ ءَاسِنٍ۬ وَأَنۡہَـٰرٌ۬ مِّن لَّبَنٍ۬ لَّمۡ يَتَغَيَّرۡ طَعۡمُهُ ۥ وَأَنۡہَـٰرٌ۬ مِّنۡ خَمۡرٍ۬ لَّذَّةٍ۬ لِّلشَّـٰرِبِينَ وَأَنۡہَـٰرٌ۬ مِّنۡ عَسَلٍ۬ مُّصَفًّ۬ىۖ وَلَهُمۡ فِيہَا مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ وَمَغۡفِرَةٌ۬ مِّن رَّبِّہِمۡۖ كَمَنۡ هُوَ خَـٰلِدٌ۬ فِى ٱلنَّارِ وَسُقُواْ مَآءً حَمِيمً۬ا فَقَطَّعَ أَمۡعَآءَهُمۡ (١٥)
TAFSIRI
I5.Mfano wa Pepo waliyoahidiwa watawa( wacha Mungu itakuwa hi vi): imo mito ya maji yasiyovunda, na mito ya miziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao,na mito ya asali iliyosafishwa; tena humo watapata matunda ya kila namna, namsamahakutoka kwa Mola wao. Je hao watakuwa sawa na wawatakaokaa Motoni na kunyweshwa maji yachemkayo yatakayokata matumbo zao?
SHEREHE
Angalia Muujiza Wa Aya Hizi Mbili ambazo zote mbili ni Aya Ndefu pekee katika kuruani nzima zenye kuzungumzia Moto na Pepo na zote mbili zipo katika Sura Zenye majina yake Mtume ﷺ Al-Mudathir na Mohamad.
Mtume ﷺ aliitwa kwa jina hili la Al-Mudathir lenye maana ya “Aliyejifunika Maguo”
Mara Ya kwanza baada ya Jibril Kukutana na Mtume Mohamad alikimbilia kwa Mkewe Bibi Khadija na kisha akafunikwa Nguo alipokuwa katika hali ya Kutetemeka baada ya kutikishwa na Malaika Jibril mara ya kwanza katika Pango la Hiraa. Kwa hiyo hili ni moja Ya jina lake aliloitwa katika Kuruani.
Aya ya Mwanzo ya Sura Ya Al-Mudathir inasema
“Ewe Unayejifunika Maguo” “Simama Kisha Uonye”
Alikuwa akiamrishwa hapa aanze kazi ya kulingania Dini. Angalia Namba Ya Sura Inavyowiana.
Sura Ya Mudathir ni Namba 74 na Sura Ya Mohamad Namba 47. Namba hizi kila moja ni kinyume ya nyingine. Namba 74 ukiigeuza unapata 47 na 47 ukiigeuza unapata 74 Angalia Maajabu ya
Mpangilio unaoshangaza. Sasa Tuhesabu Herufi za Jina المدَّثِّر zilivyotumika(Al-Mudathir) Katika Sura Hii tutashangaa kupata namba zifuatazo
Alif imetumika mara =162
Al-Lam imetumika mara=104
Al-Mim imetumika mara=71
Al-Dal imetumika mara=26
Al-Thaa imetumika mara=10
Al-Raa imetumika mara=68
Jumla ya matumizi ya herufi hizi ni
441 ( 162 + 104 + 71 + 26 + 10 + 68=441)
Na Namba hii Kihesabu unaweza kuigawa katika Mafungu 7 ya 63 kihesabu tunaandika
63 X 7
Sasa Angalia Muujiza. Namba 7 Inaashiria Milango 7 Ya Moto wa Jahannam Na Namba 63 Umri atakaoishi Mtume ﷺ
Na Kama tulivyoona Kwamba Aya Ndefu inayozungumzia Moto wa jahannam ipo katika Sura
Hii ni Ghayb kwani Mtume hakujua Umri wake umefichwa katika Kuruani Tukufu, mpaka leo hii ndiyo tunagundua Muujiza uliofichika. Allahu Akbar. Allahu Akbar.
Sasa Tuhesabu Herufi za Jina محَمَّد (Mohammad) Katika Sura Ya Mohammad na tutashangaa kupata namba zifuatazo
Al-Mim imetumika mara=223
Al-Haa imetumika mara=23
Al-Mim imetumika mara=223
Al-Dal imetumika mara=35
Jumla ya matumizi ya herufi hizi ni 504
( 223 + 23 + 223 + 35=504)
Na Namba hii Kihesabu Unaweza Kuigawa Katika Mafungu 8 ya 63 kihesabu tunaandika
63 X 8=504
Angalia Muujiza. Namba 8 Inaashiria Milango 8 Ya Pepo. Na usisahau kwamba hii ni Aya Ndefu inayozungumzia Pepo katika Sura Hii .
Namba 63 inaashiria Umri wa Mtume Mohamad.
Hii ni Ghayb kwani Mtume hakujua Umri wake.
Allahu Akbar. Allahu Akbar.
USHAHIDI WA KURUANI NA HADTHI YA MTUME
Hadithi ya Mtume Mohamed hapa chini (Amani na Sala Zake Mwenyeezi Mungu zimfikie) iliyopo katika Vitabu vya Bukhari na Muslim inasema kwamba
“Katika Pepo kuna Milango Minane Na Kuna Mlango Unaoitwa kwa jina “Ar-Raiyan” hakuna watakaoutumia katika kuingia Peponi isipokuwa Wenye Kufunga(Saumu)”
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي مَرْيَمَ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ مُطَرِّفٍ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو حَازِمٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ “ فِي الْجَنَّةِ ثَمَانِيَةُ أَبْوَابٍ، فِيهَا باب يُسَمَّى الرَّيَّانَ لاَ يَدْخُلُهُ إِلاَّ الصَّائِمُونَ ”.
Narrated Sahl bin Sa`d: The Prophet (ﷺ) said, “Paradise has eight gates, and one of them is called Ar-Raiyan through which none will enter but those who observe fasting.”
na Kuhusu Jumla ya Milango ya Motoni ni Saba kama Mwenyeezi Mungu alivyosema katika Kuruani Tukufu
Sura Ya Al-Hijr Aya Namba 43 na 44 (44)
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ (43) لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِكُلِّ بَابٍ مِنْهُمْ جُزْءٌ مَقْسُومٌ
Tafsiri
43. Na bila shaka Jahanamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote ‘
44. Ina miJango saba; na kwa kila mlango iko sehemu yao iliyogawanywa (ya kuwa hii ya mlango fulani na hii ya mlango fulani).
MUUJIZA WA UMRI WA MTUME MOHAMAD ﷺ KATIKA SURA YA AL-NASR
SURA AL-NASR NAMBA 110
إِذَا جَآءَ نَصۡرُ ٱللَّهِ وَٱلۡفَتۡحُ (١) وَرَأَيۡتَ ٱلنَّاسَ يَدۡخُلُونَ فِى دِينِ ٱللَّهِ أَفۡوَاجً۬ا (٢) فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَٱسۡتَغۡفِرۡهُۚ إِنَّهُ ۥ ڪَانَ تَوَّابَۢا (٣)
TAFSIRI
1. ltakapoflka nusura ya Mwenyezi Mungu na kushinda · :
2. Na ukawaona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi makundi
3. Basi hapo mtakase Mola wako pamoja na kumsifu, umuombe maghufira (msamaha); hakika Yeye ndiye Apokeaye toba.
SHEREHE YA SURA
Sura Hii ni Ya Mwisho kushuka kwa Mtume ﷺ alipokuwa na Umri wa Miaka 63. Maswahaba walielewa undani wa Sura Hii Kwamba hataishi muda Mrefu. Na hivi ndivyo ilivyotokea baada ya kushuka Sura Hii na baada ya siku chache Mtume ﷺ akafariki Dunia.
SAYANSI YA HESABU INTHIBITISHA UMRI WA MTUME
Sasa tuangalie Muujiza Mwingine uliokuwa umefichika na hakuna aliyejua tangu Enzi ya Mtume ﷺ Mpaka Hivi Karibuni baada ya Karne 14 kupita katika Enzi yetu hii ya Kisayansi na Technologia. Allahu Akbar.
Hebu Tuchunguze Ibara ifuatayo inyohusu Jina la Mtume ﷺ na Sifa Yake.
محمد رسول الله
Ibara hii ina Maana ya “Mohamad Ni Mjumbe wa Allah
au Kwa Kiingereza “Mohamad Is The Prophet of Allah”
محمد رسول الله
Tukihesabu Kutumika na Kukariri kwa Herufi Za Ibara Hii Katika Sur ay Al-Nasr utashangaa Kupata Idadi yake ni 63 sawa sawa na Umri wake Mtume ﷺ ambao ni miaka 63!!! . Yaani Muda atakaoishi umefichika katika Sura hii ya Mwisho.
Je Unaona Ghaybu (Kufichika) Kwa Umri wa Mtume? wakati yeye mwenyewe hakuwa akijua?
Binaadamu wote hakuna anyejua siku ya kuaga Dunia. Allahu Akbar na Mtume Pia hakujua lakini leo hii tunaona Muujiza uliofichika.
Mtume ﷺ aliipokea Sura hii na wala hakujua Muda wa maisha yake.
Je unaona Maajabu katika Kuruani? Allahu Akbar.