UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
HISTORIA FUPI YA UISLAMU
Siyo rahisi kuandika Historia Ya Uislamu yote katika Website ndogo kama hii lakini kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu nitajitahidi kuelezea kwa ufupi sana Matukio na Miujiza mbali mbali na Miaka ya Matukio hayo kuanzia Mwanzo wa Uislamu Mpaka Leo. Kazi Hii itatusaidia Kuelewa Uislamu Vizuri Zaidi. Maandishi haya yatachukua muda mrefu kwani Ni Muda wa Karne (Miaka 1400) ni mrefu sana.
Ninapopata Uhakika au Muujiza ninarudi tena katika Maandishi na Kurekibisha, Kupunguza au Kuzidisha. Naomba Msamaha kwani Nia Yangu niwape Ukweli baada ya Utafiti Mzuri Kutoka Sehemu Mbalimblai. Naomba Mola Atakabali Kazi hii Ya Mja wake Dhaifu. Allahu Akbar.
Nimepanga MWAKA Katika Kipindi Cha Ukristo (Gregorian Calendar) Upande wa Kushoto na TUKIO Upande wa Kulia Kama Ifuatavyo:
MWAKA / TUKIO
KARNE YA 6 NA 7
570/ Kuzaliwa Kwa Mtume Mohammad ﷺ
610/ Wahyi (Kushuka) kwa Aya za Mwanzo za Kuruani. Ali ibn Abu Talib رضي الله عنه na Abu Bakr As Siddiq رضي الله عنه Waliingia Katika Uislamu . Sura Iliyoshuka Mwanzo ni Al-Alaq Namba 96. Nayo ni kama ifuatayo. Alishishiwa Mtume alipokuwa katika Pango la HIraa kuko Mecca. Neno la kwanza aliambiwa Aseme ni
ٱقۡرَأۡ lenye maana Ya “Soma”. Je unaona Umuhimu wa Kusoma? Tunahimizwa tusome ili tupate kumjua Mwenyeezi Mungu. Allahu Akbar.
سُوۡرَةُ العَلق
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ (١) خَلَقَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مِنۡ عَلَقٍ (٢) ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ (٣) ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ (٤) عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ (٥) كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَـٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ (٦) أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ (٧) إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ (٨) أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِى يَنۡهَىٰ (٩) عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ (١٠) أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ (١١) أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ (١٢) أَرَءَيۡتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ (١٣) أَلَمۡ يَعۡلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ (١٤) كَلَّا لَٮِٕن لَّمۡ يَنتَهِ لَنَسۡفَعَۢا بِٱلنَّاصِيَةِ (١٥) نَاصِيَةٍ۬ كَـٰذِبَةٍ خَاطِئَةٍ۬ (١٦) فَلۡيَدۡعُ نَادِيَهُ ۥ (١٧) سَنَدۡعُ ٱلزَّبَانِيَةَ (١٨) كَلَّا لَا تُطِعۡهُ وَٱسۡجُدۡ وَٱقۡتَرِب ۩ (١٩)
615/ Kuingia Katika Uislamu kwa Omar ibn al Khattab رضي الله عنه . Kuingia kwa Uislamu Ni Baada ya Dua Aliyoomba Mtume ﷺ Amruzuku Omar au Abu Al-Hakim (Abu Jahl) kwa Uislamu kwani hawa wawili walikuwa na Uwezo na watu nyuma yao. Mtume ﷺ alitamani mmojawapo kati ya hawa wawili akubali Uislamu na Kuwa Msaidizi katika Kueneza Dini. Hadihi katika Vitabu Vya Tirmidhiy inasema
حَدَّثَنَا أَبُو كُرَيْبٍ، قَالَ حَدَّثَنَا يُونُسُ بْنُ بُكَيْرٍ، عَنِ النَّضْرِ أَبِي عُمَرَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ “ اللَّهُمَّ أَعِزَّ الإِسْلاَمَ بِأَبِي جَهْلِ بْنِ هِشَامٍ أَوْ بِعُمَرَ ” . قَالَ فَأَصْبَحَ فَغَدَا عُمَرُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَأَسْلَمَ . قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ غَرِيبٌ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ . وَقَدْ تَكَلَّمَ بَعْضُهُمْ فِي النَّضْرِ أَبِي عُمَرَ وَهُوَ يَرْوِي مَنَاكِيرَ مِنْ قِبَلِ حِفْظِهِ
Jami` at-Tirmidhi Hadithi Namba 3683
TAFSIRI
That the Prophet (ﷺ) said: “O Allah honor Islam through Abu Jahl bin Hisham or through ‘Umar bin Al-Khattab.” He said: “So it happened that ‘Umar came the next day to the Messenger of Allah (ﷺ) and accepted Islam.”
Mtume ﷺ Alisema “Ewe Allah Utukuze (Uupe Utukufu) Uislamu kwa njia ya Abu Jahl bin Hisham au ‘Umar bin Al-Khattab. Mtume ﷺ Akasema “Ikatokea kwamba Umar Akaja Siku ya pili Kwa Mtume ﷺ na Kukubali Uislamu”
KIsa Cha Kuingia Uislamu kwa Omar Ibn Al-Khatab ni Muujiza baada ya Dua aliyoiomba Mtume.
Baada ya Mjomba wake Mtume Mohamadﷺ
Hamzah ibn Abdul-Muttalib kusilimu, Bwana huyu Hamzah hakupendana na Bwana Abu Jahl aliyekuwa adui yake Mtume ﷺ Na Omar Ibn Khatab alitaka Kulipiza kisasi kwa Kumuua Mtume ﷺ Kwani hakufurahi Kuona Sababu za Kuangushwa Heshima ya Mjomba wake Bwana Abu Jahl na Bwana Hamzah ibn Abdul-Muttalib zinatokana na Mafundisho ya Mtume Mohamad ﷺ ambaye ameleta dini ya Uislamu. Aliamua kuchukua Upanga na Kuelekea kwa Mtume ﷺ na katika Safari hiyo akakutana na Na’im ibn Abdullah Al-Adawai Al-Qurayshi ambaye alisilimu lakini alificha siri na Omar alikuwa hakujua. Na’im Alimuuliza Omar anakwenda wapi. Omar akamjibu kwamba Anakwenda kumuua Mtume. Lakini Bwana Na’im akatafuta njia Nyingine ya kuepusha hatari hiyo na akamwambia afadhali aende kwa dada yake Fatima kwani huyo pamoja na shemeji yake Said ibn Zayd aliyekuwa Mtoto wa Mjomba wake Omar Ibn Al-Khatab wote wawili wamesilimu na kwa hiyo kwanza aende akatengeneze na kusahihisha familia yake kwanza kabla ya kuelelkea kwa mtume na pia akamtahadharisha kwamba akimuua mtume ﷺ kutafanyika kisasi kutoka kwa ukoo wa Banu Abd-Manaf. Omar akaona bora kwanza aende Kwa dada yake apate ukweli. Alipofika akasikia Kuruani Inasomwa. Hapo kwa dada yake kulikuwa na mwalimu kwa jina Khabbab ibn Al-Aratt ambaye alikuwa akiwasomesha Kuruani na Dini. Bwana huyu aliposikia sauti ya Omar akajificha Hapo Nyumbani. Omar akauliza ni nini kinasomwa na walipokataa kwamba siyo kuruani akawaambia kwamba pia amesikia kwamba wote wawili wamesilimu. Baada ya vurugu na mapigano baina ya Omar na Shemeji Yake na wakati huo Dada yake Omar alikuwa katikati yupo katika Kuamua ugomvi huo basi waliumizwa na Omar na hata kumtoa Damu dada yake. Omar alioona Damu ya Dada yake akamhurumia na akaendelea kumuomba amuonyeshe hicho kipande cha kuruani (Maandishi katika Ngozi) apewe na asome. Baada ya Kupewa na Kusoma Yule Mwalimu Bwana Khabbab ibn Al-Arat akatoka Mafichoni na Kumpa habari Omar kuhusu Hadithi tuliyosoma hapa Juu.
Akamsomea Kauli Ya Mtume ﷺ aliyosema kwamba
اللَّهُمَّ أَعِزَّ الإِسْلاَمَ بِأَبِي جَهْلِ بْنِ هِشَامٍ أَوْ بِعُمَرَ
“Ewe Mola Utie Uislamu Nguvu kwa Mmojawapo wa wawili; Abiy Jahl au Omar”
Baada ya Omar kusoma Kuruani hiyo (Sura Ya Twaha) na Baada ya Kuelezewa Habari ya Dua Hii inaonyesha alibadilika roho kwani
Akauliza Wapi yupo Mtume Mohamad ﷺ
Alichukua Upanga wake na kuelekea kwa Mtume ﷺ
Alipofika Maswahaba walitaka kumzuia asimkaribie Mtume ﷺ kwani alikuwa amebeba silaha mbaya na alikuwa adui mkubwa wa Uislamu. Lakini Mtume ﷺ akawakataza na akawaomba wamwachie aje karibu yake. Omar alipofika alibadilisha nia yake na Kusema “Allahu Akbar” Na Maswahaba wakaelewa kwamba Amesilimu. Hiki ndicho kisa cha Omar Ibn Alkhatab cha Kusilimu Yaani kuingia katika Uislamu.
620/ Kikundi cha Waislamu kilihamia (Wakimbizi Wa Kidini) kwenda Abyssinia (Ethiopia) Kukimbia Mateso Yanayofanya na Makafiri Hapo Mecca. Mfalme Mkristo wa Eithopia aliyejulikana kwa Jina Najashiy aliwapokea Waislamu wakimbizi hawa kwa Vizuri sana na Kwa wema mkubwa. Inasemekana kwamba Mfalme huyu alisilimu.
The migration to Abyssinia (Arabic: الهجرة إلى الحبشة, romanized: al-hijra ʾilā al-habaša), also known as the First Hijra (الهجرة الأولى, al-hijrat al’uwlaa), was an episode in the early history of Islam, where the first followers of the Islamic prophet Muhammad (known as the Sahabah) fled from Arabia due to their persecution by the Quraysh, the ruling Arab tribal confederation of Mecca. They sought and were granted refuge in the Kingdom of Aksum, an ancient Christian state that was situated in modern-day Ethiopia and Eritrea (formerly referred to as Abyssinia),[1] in 9 BH (613 CE) or 7 BH (615 CE). The ruling Aksumite monarch who received them is known in Islamic sources as Najashi (نجاشي, najāšī), the Negus of the kingdom; modern historians have alternatively identified him with the Aksumite king Armah and Ella Tsaham.[2] Some of the Sahabah exiles returned to Mecca and made the migration to Medina with Muhammad, while others remained in Aksum and arrived in Medina in 628
622/ Mtume Mohammad ﷺ Alihama Kwa ajili ya kutafuta Usalama Kutoka Mecca Kwenda Yathrib (Madinna) baada ya Mateso Makubwa na Pia Njama za Makafiri Kutaka Kumuua. Mwaka Huo aliohama Mtume ﷺ Ndio Mwaka Wa Kuanzishwa Kwa Calendar Ya Kiislamu. Hijri au Hijrah Calendar. Aya Ya Kushangaza Ilishuka Wakati huu wa Hijra (Migration) Kukimbia Mecca Kuelekea Madinna. Aya kutoka katika Sura Namba 47 Aya Namba 13 inasema
وَكَأَيِّن مِّن قَرۡيَةٍ هِىَ أَشَدُّ قُوَّةً۬ مِّن قَرۡيَتِكَ ٱلَّتِىٓ أَخۡرَجَتۡكَ أَهۡلَكۡنَـٰهُمۡ فَلَا نَاصِرَ لَهُمۡ (١٣)
TAFSIRI
l3. Na (watu wa) miji mingapi iliyokuwa yenye nguvu zaidi kuliko (watu wa) mji wako uliokutoa: Tuliwaangamiza wala hawakuwa na msaidizi.
Mwenyeezi Mungu aliishusha Aya Hii Kumliwaza Mtume ﷺ Baada ya Mateso yaliyosababisha kukimbia Mji wake aliozaliwa ambao ni Mecca. Mwenyeezi Mungu anamwambia asihizunike kwani Hao Makafiri hawana Nguvu yeyote. Na anamjuulisha kwamba kuna Miji mingine Mikubwa iliyokuwa na Mataifa Yenye Majeshi yenye nguvu kubwa kuliko hao Makafiri wa Mecca nao Waliangamizwa na Mola.
Muujiza mwingine unaojitokeza kuhusiana na Aya hii ni mpangilio wake katika Kuruani. Ni Aya Namba 13. Namba hii inalingana na Mwaka wa 13 wa Kushuka kwa Kuruani Tukufu. (Kuruani ilianza kushuka katika mwaka 610 na Mwaka wa Kuhama Kwa Mtume ﷺ ni 622.) Aya hii ilishuka Mwaka wa 13 kutoka mwanzo wa Kushuka Kuruani na Ajabu ni kwamba mpangilio wake ni Namba 13 katika Msahafu. Mpangilio wa kimiujiza kwani Wakati huo Aya za Kuruani zilikuwa bado kutiwa Namba Yeyote. Je unaona Muujiza ambao sio mdogo?
Makafiri wa Mecca walifanya Njama Mbalimbali ili kumzuia Mtume (ﷺ) asiendelee na Kueneza Dini ya Kiislamu. Na hata ikafikia kufanya Njama mbalimbali za kutaka kumuua.
Muujiza wa Kwanza Uliotokea ni Kwamba Malaika Jibril alimfunulia Mtume ﷺ Njama za Mpango wa Makafiri kuja Nyumbani Kwa Mtume ﷺ ili kumuua anapokuwa amelala usiku. Na kwa hiyo alimuomba Ali Ibn Abi Twalib رضي الله عنه alale katika kitanda chake badala yake. Na yeye Mtume ﷺ akapata nafasi kutoka usiku huo kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu bila kuonekana na kuelekea Madinna. Alikuwa pamoja na Abu Bakr رضي الله عنه na katika safari hiyo waliamua Kujificha katika Pango lililojulikana kwa Jina kama Al-Thawr. Makafiri walipokuja Nyumbani kwake wakamkuta aliyekuwa kitandani mwa Mtume ﷺ ni Ali Ibn Abi Twalib رضي الله عنه na Siyo Mtume ﷺ kama walivyotarajia. Baada ya Hapo waliamua Kumfuata Kwani walijua Kwamba Mtume ﷺ alikuwa ameelekea Upande wa Mji wa Madinna. Na Mtume ﷺ aliyekuwa safarini kuelekea Madinna akamwambia Ali Ibn Abi Twalib رضي الله عنه wajifiche katika Pango hili la Al-Thawr.
Muujiza wa Pili uliotokea katika Pango hilo ni Nyoka aliyemuuma Abu Bakr رضي الله عنه na Mtume ﷺ akampaka Mate katika sehemu hiyo aliyoumwa na Akapona.
Muujiza wa Tatu ni Utando wa Buibui na Njiwa Kutaga Mayai katika Mlango wa Pango la _Al-Thawr. Makafiri walipofika hapo Pangoni wakasema kwamba haiwezekani Mtume kujificha Ndani ya pango wakati ambapo kuna Utando wa Buibui ambao unachukua muda mrefu kuujenga na Pia Nyumba ya Njiwa na Mayai Ndani yake na kwa hiyo haiwezekani Mtume ﷺ kujificha humo. Abu Bakr رضي الله عنه alimwogopea sana Mtume ﷺ asionekane. Alipata wasiwasi mkubwa wakati Makafiri walikuwa Karibu na Mdomo wa Pango hilo. Hadithi Namba 3653 Kutoka katika Kitabu Cha Bukhari inasema kwamba Abu Bakr رضي الله عنه alimwambia Mtume ﷺ kwamba hao Makafiri Wangetizama Chini ya Miguu Yao tu basi tuneonekana ndani ya Pango. Na Mtume ﷺ akamjibu kwamba Tupo wawili lakini wa tatu ni Mwenyeezi Mungu kwa hiyo usiwe na wasi wasi wowote kwani Mwenyeezi Mungu atatulinda”
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سِنَانٍ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسٍ، عَنْ أَبِي بَكْرٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قُلْتُ لِلنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم وَأَنَا فِي الْغَارِ لَوْ أَنَّ أَحَدَهُمْ نَظَرَ تَحْتَ قَدَمَيْهِ لأَبْصَرَنَا. فَقَالَ “ مَا ظَنُّكَ يَا أَبَا بَكْرٍ بِاثْنَيْنِ اللَّهُ ثَالِثُهُمَا ”.
ENGLISH TRANSLATION
I said to the Prophet (ﷺ) while I was in the Cave. “If any of them should look under his feet, he would see us.” He said, “O Abu Bakr! What do you think of two (persons) the third of whom is Allah?”
Katika Kuruani Aya Namba 40 Sura Namba 9 (Al-Tawbah) inaelezea Kisa hiki kama ifuatavyo:
إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدۡ نَصَرَهُ ٱللَّهُ إِذۡ أَخۡرَجَهُ ٱلَّذِينَ ڪَفَرُواْ ثَانِىَ ٱثۡنَيۡنِ إِذۡ هُمَا فِى ٱلۡغَارِ إِذۡ يَقُولُ لِصَـٰحِبِهِۦ لَا تَحۡزَنۡ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَنَاۖ فَأَنزَلَ ٱللَّهُ سَڪِينَتَهُ ۥ عَلَيۡهِ وَأَيَّدَهُ ۥ بِجُنُودٍ۬ لَّمۡ تَرَوۡهَا وَجَعَلَ ڪَلِمَةَ ٱلَّذِينَ ڪَفَرُواْ ٱلسُّفۡلَىٰۗ وَڪَلِمَةُ ٱللَّهِ هِىَ ٱلۡعُلۡيَاۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (٤٠)
TAFSIRI
40. Kama hamtamnusuru (Mtume), basi Mwenyezi Mungu alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru; alipokuwa (mmoja tu na mwenziwe) wa pili wake, (peke yao); walipokuwa wote wawili katika pango; (Mtume) alipomwambia sahibu yake: “Usihuzunike, kwa yakini Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.” Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona, na akafanya neno Ia wale waliokufuru kuwa chini; na neno Ia M wenyezi Mungu ndilo Ia juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayeshinda na ndiye Mwenye hekima.
Baada ya Siku 3 Mtume akaendelea na safari yake kwenda Yathrib (Madinna).
624/ Vita Vya Badr Vilifanyika Mwaka 624. Kuruani Imezungumzia Vita Hii ambayo ni Ya Mwanzo Kufanyika Baina Ya Waislamu Na Makafiri. Kuruani Halitaji Jambo lisilo na Muhimu. Kwa hiyo Hili Ni Jambo Kubwa. Huu Ni Mojawapo ya Miujiza kwani Jeshi la kiislamu lilikuwa dogo lenye Silaha Chache (Maswahaba Karibu 300) na Jeshi la Maadui lilikuwa Kubwa lenye Silaha Nyingi Mara Tatu Ya Jeshi la Kiislamu. (Makafiri Karibu 1000). Kuna Aya Katika Kuruani zinazoelezea Vita Hivi kwamba Mwenyeezi Mungu alijaalia Jeshi la Kiislamu kusaidiwa na Malaika 1000 Kuna Hadithi Za Mtume zinazoelezea Habari hizi kwa urefu. Tafsiri ya Aya zinatufahamisha vizuri Msaada wa Mweyeezi Mungu katika Vita hivi. Allahu Akbar. Katika Sura Namba 8 Aya Namba 9 Mwenyeezi Mungu anasema
إِذۡ تَسۡتَغِيثُونَ رَبَّكُمۡ فَٱسۡتَجَابَ لَڪُمۡ أَنِّى مُمِدُّكُم بِأَلۡفٍ۬ مِّنَ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ مُرۡدِفِينَ (٩)
TAFSIRI
9. (Kumbukeni) mlipokuwa mkiomba msaada kwa Mota wenu, naye akakujibuni kuwa: “Kwa yakini Mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu moja watakaofuatana mfululizo (wanaongezeka tu).”
Na Katika Sura Namba 8 Aya Namba 17
فَلَمۡ تَقۡتُلُوهُمۡ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ قَتَلَهُمۡۚ وَمَا رَمَيۡتَ إِذۡ رَمَيۡتَ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ رَمَىٰۚ وَلِيُبۡلِىَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ مِنۡهُ بَلَآءً حَسَنًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ۬ (١٧)
TAFSIRI
17. Hamkuwaua nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua; na hukutupa wewe (Mtume ule mchanga wa katika gao Ia mkono wako), ulipotupa (ukawaingia wote machoni · mwao); (hukufanya wewe haya) walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyeutupa, (yaani ndiye aliyeufikisha katika macho yao wote yakawa yanawawasha kuliko pilipili, wakenda mbio)
Alifanya haya Mwenyezi Mungu ili awape walioamini hidaya nzuri itokayo kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye. (Aya Hii Inatufahamisha Kuwa Mtume ﷺ aliokota mchanga akawatupa hewani kuelekea kwa wale Wanajeshi wa kikafiri. Mchanga huo ulikuwa Silaha kubwa kutoka kwa Mweneyeezi Mungu. Soma Tafsiri hapa Juu)
Hadithi kutoka kwa Imam Muslim ( Sahih Muslim 1763) inafafanua Mazingara ya vita hii na Misaada ya Malaika.
حَدَّثَنَا هَنَّادُ بْنُ السَّرِيِّ، حَدَّثَنَا ابْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ عِكْرِمَةَ بْنِ عَمَّارٍ، حَدَّثَنِي سِمَاكٌ، الْحَنَفِيُّ قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ، يَقُولُ حَدَّثَنِي عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ، قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمُ بَدْرٍ ح وَحَدَّثَنَا زُهَيْرُ بْنُ حَرْبٍ – وَاللَّفْظُ لَهُ – حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ يُونُسَ الْحَنَفِيُّ حَدَّثَنَا عِكْرِمَةُ بْنُ عَمَّارٍ حَدَّثَنِي أَبُو زُمَيْلٍ – هُوَ سِمَاكٌ الْحَنَفِيُّ – حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَبَّاسٍ قَالَ حَدَّثَنِي عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ قَالَ لَمَّا كَانَ يَوْمُ بَدْرٍ نَظَرَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِلَى الْمُشْرِكِينَ وَهُمْ أَلْفٌ وَأَصْحَابُهُ ثَلاَثُمِائَةٍ وَتِسْعَةَ عَشَرَ رَجُلاً فَاسْتَقْبَلَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم الْقِبْلَةَ ثُمَّ مَدَّ يَدَيْهِ فَجَعَلَ يَهْتِفُ بِرَبِّهِ ” اللَّهُمَّ أَنْجِزْ لِي مَا وَعَدْتَنِي اللَّهُمَّ آتِ مَا وَعَدْتَنِي اللَّهُمَّ إِنْ تَهْلِكْ هَذِهِ الْعِصَابَةُ مِنْ أَهْلِ الإِسْلاَمِ لاَ تُعْبَدْ فِي الأَرْضِ ” . فَمَازَالَ يَهْتِفُ بِرَبِّهِ مَادًّا يَدَيْهِ مُسْتَقْبِلَ الْقِبْلَةِ حَتَّى سَقَطَ رِدَاؤُهُ عَنْ مَنْكِبَيْهِ فَأَتَاهُ أَبُو بَكْرٍ فَأَخَذَ رِدَاءَهُ فَأَلْقَاهُ عَلَى مَنْكِبَيْهِ ثُمَّ الْتَزَمَهُ مِنْ وَرَائِهِ . وَقَالَ يَا نَبِيَّ اللَّهِ كَذَاكَ مُنَاشَدَتُكَ رَبَّكَ فَإِنَّهُ سَيُنْجِزُ لَكَ مَا وَعَدَكَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ { إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُمْ بِأَلْفٍ مِنَ الْمَلاَئِكَةِ مُرْدِفِينَ} فَأَمَدَّهُ اللَّهُ بِالْمَلاَئِكَةِ . قَالَ أَبُو زُمَيْلٍ فَحَدَّثَنِي ابْنُ عَبَّاسٍ قَالَ بَيْنَمَا رَجُلٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ يَوْمَئِذٍ يَشْتَدُّ فِي أَثَرِ رَجُلٍ مِنَ الْمُشْرِكِينَ أَمَامَهُ إِذْ سَمِعَ ضَرْبَةً بِالسَّوْطِ فَوْقَهُ وَصَوْتَ الْفَارِسِ يَقُولُ أَقْدِمْ حَيْزُومُ . فَنَظَرَ إِلَى الْمُشْرِكِ أَمَامَهُ فَخَرَّ مُسْتَلْقِيًا فَنَظَرَ إِلَيْهِ فَإِذَا هُوَ قَدْ خُطِمَ أَنْفُهُ وَشُقَّ وَجْهُهُ كَضَرْبَةِ السَّوْطِ فَاخْضَرَّ ذَلِكَ أَجْمَعُ . فَجَاءَ الأَنْصَارِيُّ فَحَدَّثَ بِذَلِكَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ ” صَدَقْتَ ذَلِكَ مِنْ مَدَدِ السَّمَاءِ الثَّالِثَةِ ” . فَقَتَلُوا يَوْمَئِذٍ سَبْعِينَ وَأَسَرُوا سَبْعِينَ . قَالَ أَبُو زُمَيْلٍ قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ فَلَمَّا أَسَرُوا الأُسَارَى قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لأَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ ” مَا تَرَوْنَ فِي هَؤُلاَءِ الأُسَارَى ” . فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ يَا نَبِيَّ اللَّهِ هُمْ بَنُو الْعَمِّ وَالْعَشِيرَةِ أَرَى أَنْ تَأْخُذَ مِنْهُمْ فِدْيَةً فَتَكُونُ لَنَا قُوَّةً عَلَى الْكُفَّارِ فَعَسَى اللَّهُ أَنْ يَهْدِيَهُمْ لِلإِسْلاَمِ . فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ” مَا تَرَى يَا ابْنَ الْخَطَّابِ ” . قُلْتُ لاَ وَاللَّهِ يَا رَسُولَ اللَّهِ مَا أَرَى الَّذِي رَأَى أَبُو بَكْرٍ وَلَكِنِّي أَرَى أَنْ تُمَكِّنَّا فَنَضْرِبَ أَعْنَاقَهُمْ فَتُمَكِّنَ عَلِيًّا مِنْ عَقِيلٍ فَيَضْرِبَ عُنُقَهُ وَتُمَكِّنِّي مِنْ فُلاَنٍ – نَسِيبًا لِعُمَرَ – فَأَضْرِبَ عُنُقَهُ فَإِنَّ هَؤُلاَءِ أَئِمَّةُ الْكُفْرِ وَصَنَادِيدُهَا فَهَوِيَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مَا قَالَ أَبُو بَكْرٍ وَلَمْ يَهْوَ مَا قُلْتُ فَلَمَّا كَانَ مِنَ الْغَدِ جِئْتُ فَإِذَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَبُو بَكْرٍ قَاعِدَيْنِ يَبْكِيَانِ قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَخْبِرْنِي مِنْ أَىِّ شَىْءٍ تَبْكِي أَنْتَ وَصَاحِبُكَ فَإِنْ وَجَدْتُ بُكَاءً بَكَيْتُ وَإِنْ لَمْ أَجِدْ بُكَاءً تَبَاكَيْتُ لِبُكَائِكُمَا . فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ” أَبْكِي لِلَّذِي عَرَضَ عَلَىَّ أَصْحَابُكَ مِنْ أَخْذِهِمُ الْفِدَاءَ لَقَدْ عُرِضَ عَلَىَّ عَذَابُهُمْ أَدْنَى مِنْ هَذِهِ الشَّجَرَةِ ” . شَجَرَةٍ قَرِيبَةٍ مِنْ نَبِيِّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم . وَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ { مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَنْ يَكُونَ لَهُ أَسْرَى حَتَّى يُثْخِنَ فِي الأَرْضِ} إِلَى قَوْلِهِ { فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلاَلاً طَيِّبًا} فَأَحَلَّ اللَّهُ الْغَنِيمَةَ لَ
Hapa chini Tafsiri baadhi tu Ya Sehemu ya Hadithi hapa Juu ambayo nimeitia Rangi Nyekundu nayo Ina uhusiano na Muujiza Wa Msaada wa Malaika. (Sikufasiri Hadithi Yote)
TAFSIRI
Siku hiyo Muislamu (Askari)alikuwa akimfukuza (Hapo Vitani) Kafiri aliyekuwa Mbele yake. Akasikia Kipigo Juu ya yule Kafiri na Akasikia Pia Sauti Nyingine Ya Kiumbe Juu ya Farasi Kikisema kumwambia yule kafiri “Nenda Mbele” Haizum” Na Kutahamaki Yule Muislamu akamuona Yule Kafiri ameanguka Chini kifudifudi. Alipomchunguza akamuona Ana alama Juu ya Pua Yake na Uso umepasuliwa kama vile umepigwa na Kiboko na wote umekuwa Rangi ya Kijani . Huyu Askari Muumini akamjia Mtume ﷺ na kumhadithia habari hii na Mtume ﷺ akamjibu kwamba “Umesema Ukweli Huu ulikuwa Msaada Kutoka katika Mbingu ya Tatu” (Yaani Misaada wa Malaika miongoni mwa Malaika waliokuja Kusaidia katika Vita Hivi)
625/ Vita Vya Uhud Vilifanyika Mwaka Huu. Kulifanyika Makosa Kwani Maswahaba Walivunja Amri Ya Mtume Mohammad ﷺ Walizihama zile sehemu walizoamrishwa Kukaa na Kukimbilia Ngawira (Spoils of War). Kabla Ya Hao Maswahaba Kuhama zile Sehemu walikuwa Wamepiga Hatua Kubwa Sana na Walijiona Wameisha Shinda na Baada ya hapo wakafanya Makosa na Kuacha hizo Sehemu zao kwa Ajili ya kwenda kukusanya Ngawira za Vita. Makafiri wa Mecca walipoziona zile sehemu hazina Mlinzi basi wakawavamia Waislamu kwa kuja nyuma yao na Kusababisha Waislamu Wengi kupoteza maisha na Hata Mtume Pia Aliumizwa. Maswahaba wengi walikimbia na Kumwacha Mtume ﷺ na Wengine wachache.
Mtume ﷺ na Baadhi ya Maswahaba waliobakia Hapo Walihamia Juu ya Mlima Wa Uhud. Na Makafiri walishindwa Kuupanda Mlima huo na kuendelea na vita. Makafiri waliamua kurudi Mecca na Huku wanafikiri Wameshinda vita. Wakawatangazia Makafiri Wenzao kwamba Wameshinda Vita.
627/ Vita Vya Mitaro au Khandaq (Battle of the Trench).Vilifanyika Mwaka Huu. Waislamu Hapo Madinna Waliwafukuza Mayahudi (Banu Nadeer )Waliokuwa Wanafiki na Wakahamia Mji wa Khyber. Na huko Wakaungana na Maadui (Makafiri) wa sehemu hiyo na Wengineo Wa huko Mecca. Na Kuna Aya Za Kuruani zenye kuzungumzia Historia Hii katika Sura Ya Al-Ahzab. Na ndiyo maana Sura Hii Ikaitwa kwa Jina Hili Lenye maana Ya “Makundi”, au “Vyama” au Kwa Kiingereza “Groups”. Sura Hii Inazungumzia Wanafiki Hawa walioshirikiana Kwenda huko Madinna katika Makundi mbalimbali Ili Kuuzingira Mji huo. (Kwa Kiingreza “Siege”). Waliuzingira Mji huo wa Madinna.
Hatua Ya Kwanza ilikuwa kuuzingira Mji huo na Kisha Kuuvamia. Swahaba aliyejulikana kwa jina kama Salman Al-Farsiy yaani alikuwa Mfarsi (Leo ni Iran)) رَضِىَ اللّٰـەُ عَـنْهُ akamshauri Mtume achimbe Mahandaki (Trenches) kuuzunguka Mji wa Madina ili kuwazuia Maadui wasiwavamie. Maadui 10,000 na Waislamu walikuwa 3000. Muujiza Mkubwa Ni Dua aliyoomba Mtume kama ilivyopokelewa katika Vitabu Vya Bukhari Na Muslim. Hadithi ifuatayo kutoka katika kitabu cha Bukhari
حَدَّثَنَا ابْنُ سَلاَمٍ، أَخْبَرَنَا وَكِيعٌ، عَنِ ابْنِ أَبِي خَالِدٍ، قَالَ سَمِعْتُ ابْنَ أَبِي أَوْفَى ـ رضى الله عنهما ـ قَالَ دَعَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم عَلَى الأَحْزَابِ فَقَالَ “ اللَّهُمَّ مُنْزِلَ الْكِتَابِ، سَرِيعَ الْحِسَابِ، اهْزِمِ الأَحْزَابَ، اهْزِمْهُمْ وَزَلْزِلْهُمْ ”.
TAFSIRI
Ibn Aufa alielezea kwamba Mtume alimuomba Mwenyeezi Mungu kwa kusema ” Ewe Allah Ambaye Mshushaji wa Kitabu na pia Mwingi wa Kuhesabu, Washinde hawa Makundi na Watetemeshe (Watingishe).
SHEREHE
Baada Ya dua Dua Hii kubwa Ilifuatiwa na Kimbunga Kikali na Ilisababisha Hao Maaskari wa Kikafiri Kuingia khofu Kubwa. Upepo mkali ulivamia Kila walichonacho. Mifugo yao Kukimbia HovyoMahema yao kuangushwa na Vinginevyo kuondolewa na upepo, Na hawakuona la kufanya isipokuwa kuancha Njama hizo za uvamizi na kuondoka. Waislamu hawakuvamiwa. Ni Ushindi Mkubwa waliopata. Fikra ya Mahandaki (Mifereji) ilisaidia Kuwazuia Maadui wasiingie Madina na Kuwavamia Waislamu. Allahu Akbar. Na hivi ndivyo Uislamu Ulivyoendelea na unavyoendelea na hakuna aliyeweza au atakayeweza kuuzuia mpaka siku ya kiyama.
Miujiza Mikubwa Mingineyo katika Vita hivi kabla ya Kimbunga tulichotaja hapa juu kuna Miujiza Ifuatayo:
Muujiza-1
Jabir Bin Adlillah ( رضي الله عنه ) aliandaa chakula ili kumkaribisha Mtume Mohamad ﷺ. Alikubali mwaliko huo na yeye akawakaribisha Maswahaba wote (karibu 1000). Alipofika (Mtume Mohamad ﷺ )na Maswahaba (Jeshi lote) alikiombea chakula hicho Dua. Muujiza ni kwamba Maswahaba wote wakala na kushiba na isitoshe kukabaki chakula kingi ambacho kiliwafaa Jabir na Familia yake. Angalia Muujiza. Chungu Kimoja kililisha Wanajeshi karibu 1000 au zaidi .
Huu siyo Muujiza Mdogo. Hadithi Ifuatayo Kutoka katika Vitabu Vya Imamu Bukhari (Sahih al-Bukhari Hadithi Namba 4101) Inathibitisha Muujiza Huu Wa Chakula.
حَدَّثَنَا خَلاَّدُ بْنُ يَحْيَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَاحِدِ بْنُ أَيْمَنَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ أَتَيْتُ جَابِرًا ـ رضى الله عنه ـ فَقَالَ إِنَّا يَوْمَ الْخَنْدَقِ نَحْفِرُ فَعَرَضَتْ كُدْيَةٌ شَدِيدَةٌ، فَجَاءُوا النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالُوا هَذِهِ كُدْيَةٌ عَرَضَتْ فِي الْخَنْدَقِ، فَقَالَ ” أَنَا نَازِلٌ ”. ثُمَّ قَامَ وَبَطْنُهُ مَعْصُوبٌ بِحَجَرٍ، وَلَبِثْنَا ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ لاَ نَذُوقُ ذَوَاقًا، فَأَخَذَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم الْمِعْوَلَ فَضَرَبَ، فَعَادَ كَثِيبًا أَهْيَلَ أَوْ أَهْيَمَ، فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ ائْذَنْ لِي إِلَى الْبَيْتِ. فَقُلْتُ لاِمْرَأَتِي رَأَيْتُ بِالنَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم شَيْئًا، مَا كَانَ فِي ذَلِكَ صَبْرٌ، فَعِنْدَكِ شَىْءٌ قَالَتْ عِنْدِي شَعِيرٌ وَعَنَاقٌ. فَذَبَحْتُ الْعَنَاقَ وَطَحَنَتِ الشَّعِيرَ، حَتَّى جَعَلْنَا اللَّحْمَ فِي الْبُرْمَةِ، ثُمَّ جِئْتُ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم وَالْعَجِينُ قَدِ انْكَسَرَ، وَالْبُرْمَةُ بَيْنَ الأَثَافِيِّ قَدْ كَادَتْ أَنْ تَنْضَجَ فَقُلْتُ طُعَيِّمٌ لِي، فَقُمْ أَنْتَ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَرَجُلٌ أَوْ رَجُلاَنِ. قَالَ ” كَمْ هُوَ ”. فَذَكَرْتُ لَهُ، قَالَ ” كَثِيرٌ طَيِّبٌ ”. قَالَ ” قُلْ لَهَا لاَ تَنْزِعُ الْبُرْمَةَ وَلاَ الْخُبْزَ مِنَ التَّنُّورِ حَتَّى آتِيَ ”. فَقَالَ ” قُومُوا ”. فَقَامَ الْمُهَاجِرُونَ وَالأَنْصَارُ، فَلَمَّا دَخَلَ عَلَى امْرَأَتِهِ قَالَ وَيْحَكِ جَاءَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِالْمُهَاجِرِينَ وَالأَنْصَارِ وَمَنْ مَعَهُمْ. قَالَتْ هَلْ سَأَلَكَ قُلْتُ نَعَمْ. فَقَالَ ” ادْخُلُوا وَلاَ تَضَاغَطُوا ”. فَجَعَلَ يَكْسِرُ الْخُبْزَ وَيَجْعَلُ عَلَيْهِ اللَّحْمَ، وَيُخَمِّرُ الْبُرْمَةَ وَالتَّنُّورَ إِذَا أَخَذَ مِنْهُ، وَيُقَرِّبُ إِلَى أَصْحَابِهِ ثُمَّ يَنْزِعُ، فَلَمْ يَزَلْ يَكْسِرُ الْخُبْزَ وَيَغْرِفُ حَتَّى شَبِعُوا وَبَقِيَ بَقِيَّةٌ قَالَ ” كُلِي هَذَا وَأَهْدِي، فَإِنَّ النَّاسَ أَصَابَتْهُمْ مَجَاعَةٌ ”.
SHEREHE YA HADITHI
Hadithi inayotokana na Jabir inaelezea Kisa cha Kazi ya Kuchimba Mitaro/Trernch ya kuihami Mji wa Madinna na Jabir aliyekuwa katika kazi hiyo alimhurumia sana Mtume ﷺ alipomuona ana Njaa na hali amefunga jiwe tumboni katika njia za kujikinga na Njaa. Akamuomba Mtume ﷺ ruhusa ili aende nyumbali kwake na alipofika nyumbanikwake alizungumza na Mkewe aandae Chakula kwa ajili ya kumkaribisha Mtume na Baadhi ya Waumini.(Moja au wawili). Kisha Jabir akarudi Kazini (Kuchimba Mtaro)na akamwalika Mtume ﷺ lakini Haikuwa kama alivyopanga Jabir kwa kumualika Mtume ﷺ na Waumini Wawili au Watatu lakini Mtume ﷺ alialika Waumini wote yaani jeshi lote lililokusanya Wananchi wa Madinna (Ansari) na Wakimbizi waliokuja Madina Kutoka Mecca (Muhajirin). Mtume ﷺ akawanasihi waingine katika Nyumba ya Jabir bila ya Fujo bali mmoja mmoja na kisha akawapa kila mmoja Mkate na nyama. Alitayarisha Kwa kukata Vipande Vya Mkate na kuweka Nyama Juu yake na kisha kuwapa Wageni kila mmoja. Akafanya hivyo moaka wageni wote wakapata kula na kushiba. Muujiza sio Mdogo kwani Chungu kilikuwa Kimoja na kila akitoa Nyama anafunika Chungu hicho kwa Hekima tusiyoijua isipokuwa yeye peke yake. Allahu Akbar. Waliokuja Kwa Jabir walikuwa Wengi. Na wote wakala na wakashiba. Na Chakula kingine kikabaki kwa wenye Nyuma yaani Jabir na Mkewe. La kushangaza ni kwamba Chungu kimoja lakini Wageni Wengi. Jabir aliandaa chakula kufuatana na uwezo wake na kilikuwa cha watu wachache na hakujua kwamba Mtume ﷺ atawakaribisha Ansari na Muhajirin Wote. lakini Dua za Mtume ﷺ zilikubaliwa na Chakula kidogo kikawa kinatoka kutoka katika Chungu bila kwisha.
Muujiza-2
Wakati wanachimba Mtaro/Handaki kubwa kuuzunguka Mji wa Madinna walikuta Jiwe kubwa ambalo hawakuweza kulivunja basi wakamuomba Mtume ﷺ awasaidie. Mtume ﷺ akaomba Dua na kulivunja Jiwe hilo baada ya Mapigo Matatu. Na kutokana na Habari zinazotokana na Imam Ahmad An-Nasa’i (Rahimahullah) Zinasema Kwamba kila pigo kulisababisha Mwanga unaotokana na Mapigo ya Nguvu. Kila Pigo alisema “Allahu Akbar” na Katika Pigo la kwanza Akasema “Nimeahidiwa Funguo za Nchi Ya Syria” na Katika Pigo la Pili akasema “Nimeahidiwa Funguo za Persia” na Katika Pigo la Tatu akasema “Nimeahidiwa Funguo za Yemen” Habari hizi ni Ahadi alizopewa Mtume ﷺ alipokuwa akipasua jiwe hilo.
628/ Mwaka huu kulifanyika “Mkataba (Treaty) Wa Hudaybiyyah. (Jina La Sehemu huko Saudi Arabia) Ni Tukio Kubwa ambalo lilifanyika katika kipindi cha uhai wa Mtume Mohamad ﷺ .
Ni Mkataba uliofanywa Mwezi wa January Mwaka 628 (Inayowiana na Mwezi wa Kiislamu wa Dhul-Q’adah Mwaka wa 6 Baada Ya Hijrah) baina ya Mtume ﷺ ambaye aliwakilisha Taifa la Kiislamu la Madinna na Makureishi ambao waliwakilisha Taifa la Makafiri wa Mecca.
Mkataba huu ulipunguza Mvutano baina ya Waislamu wa Madinna Na Makafiri wa Mecca.
Kuweka amani na Usalama kwa muda wa miaka 10, na Kuruhusiwa Waislamu kwenda Hija Mwaka Ufuatao.
Kabla ya Kufanyika Kwa Mkataba huu Mtume ﷺ Alipewa Wahyi (Revelation Kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu) kwamba yeye pamoja na Waislamu wa Madinna waende Mecca wakafanye Umrah (Hija Ndogo). Jambo hili halikuwa dogo kwani Ni Mpango wake Mola.
Kwa kweli ni Muujiza. Hawakuogopa kwenda huko Mecca. Tusisahau Vita Vya Handaq (Trench au Mitaro) vilivyofanyika Mwaka uliopita wa 627 (Christian Era). Maswahaba Hawakuogopa Kwenda huko Mecca na kukutana na maadui wa Kiislamu.
Maswahaba walifurahi sana kwenda Mecca na kufanya Umrah.
Historia inasema kwamba Waislamu walikuwa karibu 1400 na wakasafiri bila ya Silaha yeyote kwani nia yao ilikuwa ibada. Nguo walizovaa na wanyama waliowachukua kwa ajili ya machinjo inathibitisha kwamba nia yao ilikuwa ibada na sio vita.
Walipofika Karibu na Mecca Walipiga Kambi katika Sehemu inayoitwa Hudaybiya ambayo ni Karibu na Mecca.
Wajumbe wa Mecca waliwazuia Waislamu waingie Mecca kwa Ajili ya Ibada.
Na baada Ya Majadiliano Marefu yaliyochukua zaidi ya siku moja Mtume ﷺ akaamua Kufanya Mkataba na Makafiri wa Mecca.
Mkataba Huo ulipingwa sana na Omar Ibn Al-khatab na Pia Baadhi wa Maswahaba, lakini Mtume ﷺ alishikilia msimamo wake ambao ulipendekeza Mkataba ufanyike..
Dondoo za Mkataba huo ni kama ufuatao:
1/Pande zote mbili zitazingatia usitishaji (Ceasefire) wa vita kwa miaka kumi (10).
2/Waislamu warudi Madinna bila kufanya Umra mwaka huu.
3/Waje kufanya Umra mwaka ujao na wataruhusiwa kukaa Makka siku tatu.
4/Waislamu wasibebe silaha yeyote isipokuwa panga tu na panga hizo ziwe ndani ya ala.
5/Mtu akihama kwenda Madina kutoka Makka atarudishwa; lakini mtu akihama kwenda Makka kutoka Madina hatarudishwa.
6/Makabila ya Uarabuni yatakuwa na mamlaka (Madaraka yaani Wataruhusiwa) ya kuingia upande wowote wanaotaka. (Yaani Upande wa Waislamu au Makafiri)
Ukiuchunguza Mkataba Huu utaona Waislamu wamedhulumiwa. Kwanza Hawakuruhusiwa Kuingia Mecca siku hiyo na Kwamba warudi walikotoka yaani Madinna. Na pia Dondoo Namba 5 (Mtu akihama kwenda Madina kutoka Makka atarudishwa; lakini mtu akihama kwenda Makka kutoka Madina hatarudishwa) linaonyesha Dhuluma.
Mkataba huu unaonyesha Hila za Makafiri. Kama wanavyosema katika Kiswahili “Mwamba Ngoma Ngozi huvutia Kwake”. Hapa Makafiri walivutia upande wao kwa kusema Mtu akihama kutoka Mecca kwenda Madinna yaani akikubali Uislamu basi Waislamu wa Madinna Wamrudishe huko Mecca. Lakini Mwenyeezi Mungu ana hekima Kubwa. Kheri Dhuluma hiyo ndogo kuliko Vita.
Maswahaba walitamani Kuingia Macca kwa nguvu na waliona uchungu kukataliwa kuingia Mecca kwa Umrah. Hawakuogopa kutakuwa na Vita kwani walikuwa tayari ikiwa itazuka Vita yeyote na Makafiri Walikuwa tayari kumwaga Damu.
Kuna Hekima Nyingine kubwa aliyokadiria Mwenyeezi Mungu. Kuna methali inayosema kwamba “Kheri Nusu ya Shari Kuliko Shari Zima”. Hivi ndivyo kiswahili kinavyosema. Mkataba Uliofanywa na Mtume ﷺ ni mipango yake Mwenyeezi Mungu.
Sisi Binaadamu tunaona Karibu na Mwenyeezi Mungu anaona mbali. Mola ndiye aliyepanga haya.
Ijapokuwa Baadhi ya Mwaswahaba hawakufurahi kwa Mtume ﷺ kukubali Mkataba ufanyike lakini baada tu ya Kushuka Aya Ya Kuruani Sura Namba 48 Aya Namba 1 inayosema;
إِنَّا فَتَحۡنَا لَكَ فَتۡحً۬ا مُّبِينً۬ا
TAFSIRI
umekufunulia Mfunuo ulio Wazi.
SHEREHE
Aya hii inamliwaza Mtume ﷺ na Maswahaba. Aya ilijibu suala lao. Na inaonyesha faida kubwa ya Mkataba huo.
Baada ya Aya hii kushuka Omar Ibn Alkhatab alisikitika Kuhusu mabishano aliyoyafanya na Mtume ﷺ baada ya Mkataba huu.
Aya Iliyoshuka iliwapa Waislamu Moyo na Imani kwamba Mwenyeezi Mungu yupo pamoja nao.
Na Hadithi Ifuatayo Ya Mtume ﷺ Namba 1786a iliyokusanywa katika Kitabu Miongoni mwa Vitabu Vya Sahih Muslim Inatufafanulia zaidi Kisa Hiki inasema:
وَحَدَّثَنَا نَصْرُ بْنُ عَلِيٍّ الْجَهْضَمِيُّ، حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ الْحَارِثِ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي، عَرُوبَةَ عَنْ قَتَادَةَ، أَنَّ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ، حَدَّثَهُمْ قَالَ لَمَّا نَزَلَتْ { إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا * لِيَغْفِرَ لَكَ اللَّهُ} إِلَى قَوْلِهِ { فَوْزًا عَظِيمًا} مَرْجِعَهُ مِنَ الْحُدَيْبِيَةِ وَهُمْ يُخَالِطُهُمُ الْحُزْنُ وَالْكَآبَةُ وَقَدْ نَحَرَ الْهَدْىَ بِالْحُدَيْبِيَةِ فَقَالَ ” لَقَدْ أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آيَةٌ هِيَ أَحَبُّ إِلَىَّ مِنَ الدُّنْيَا جَمِيعًا ”
SHEREHE YA HADITHI
Baada ya Mtume ﷺ Kurudi Madina kutoka Hudaybiya wakati ambapo walikuwa wamejaa Huzuni kubwa na Dhiki Ya Nafsi kwa ajili ya Huo Mkataba walioufanya na lawama za Maswahaba kwani walimuona Mtume ﷺ amefanya kosa kwa kukubali Mkataba huo. Basi Aya Za Mwanzo za Sura Ya Al-Fath zikashuka. Na Mtume na Maswahaba wakafutahi sana. Mtume akasema
“Nimeshushiwa Aya Ambazo Ni Adhimu (Bora) Kuliko Dunia (Ulimwengu Wote) Yote”
Nazo ni kama zifuatazo:
Sura Ya Al-Fath Namba 48 Aya 1 Mpaka 5
إِنَّا فَتَحۡنَا لَكَ فَتۡحً۬ا مُّبِينً۬ا (١) لِّيَغۡفِرَ لَكَ ٱللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنۢبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعۡمَتَهُ ۥ عَلَيۡكَ وَيَہۡدِيَكَ صِرَٲطً۬ا مُّسۡتَقِيمً۬ا (٢) وَيَنصُرَكَ ٱللَّهُ نَصۡرًا عَزِيزًا (٣) هُوَ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ ٱلسَّكِينَةَ فِى قُلُوبِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ لِيَزۡدَادُوٓاْ إِيمَـٰنً۬ا مَّعَ إِيمَـٰنِہِمۡۗ وَلِلَّهِ جُنُودُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمً۬ا (٤) لِّيُدۡخِلَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَـٰتِ جَنَّـٰتٍ۬ تَجۡرِى مِن تَحۡتِہَا ٱلۡأَنۡہَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيہَا وَيُڪَفِّرَ عَنۡهُمۡ سَيِّـَٔاتِہِمۡۚ وَكَانَ ذَٲلِكَ عِندَ ٱللَّهِ فَوۡزًا عَظِيمً۬ا (٥)
TAFSIRI
1 .Bila shaka tumekwishakupa kushinda kuliko dhahiri
2.Ili Mwenyezi Mungu akusamehe makosa yako yaliyotangulia na yanayokuja, na kukutimizia neema zake na kukuongoa katika njia iliyonyoka
3.Na akunusuru Mwenyezi Mungu nusura yenye nguvu kabisa.
4.Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za Waislamu ili waongezeke imani juu ya imani yao. Na majeshi ya mbingu na ardhi ni ya Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi (wa kila jambo) na Mwenye hikima
5-(Ameyafanya haya) ili awaingize Waislamu wanaume na Waislamu wanawake katika Mabustani yapitayo mito mbele yake, wakadumu huko milele, na awafutie makosa yao. Na huku ndiko kufaulu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu
FAIDA ZA MKATABA
Sasa Tuendelee na Kuelezea Baadhi Ya Faida za Mkataba Huu.
Kwanza Ulisababisha Taifa La Kiiislamu huko Madinna litambuliwe na Taifa La Makafiri huko Mecca.
Kwa hiyo Waislamu walitambulikana kwa mara ya kwanza kwamba wana Taifa lao. Kwani hapo mwanzo walikuwa wakihesabiwa kama Wapiganaji Magaidi wa Kidini.
Sura Iliyoshuka Aya Hii inajulikana kwa jina Kama Al-Fath yaani maana yake ni Ushindi au kwa kiingereza Victory.
Haikuchukua Muda Mrefu watu wengi walianza kuingia katika Uislamu. Miji ya Khyber, Fidak, and Tabuk ilitekwa na Waislamu. Na baada ya Muda Mfupi wakaingia Mecca na Kuuteka Mji huo bila ya Kumwaga Damu. Mateka Wote hapo Mecca waliachiwa Huru bila Adhabu yeyote. Allahu Akbar.
630/ Mwaka Huu ndiyo Mecca ilitekwa na Waislamu. Na miongoni mwa sababu zilizofanya Waislamu waamue kuuteka Mji huu ni makosa yaliyofanywa na Kabila la Ukoo wa (Bani) Bakr ambao walikuwa na Uhusiano mzuri na Makafiri wa Mecca kwa kuvamia Kabila la Ukoo wa (Bani) Khuza’s ambao walikuwa na Uhusiano mzuri na Waislamu wa Madinna. (kabila la Khuza’s lilimkubali Mtume ﷺ na Kuingia katika dini ya Kiislamu) .
Kabila la Banu Bakr (Ambao ni washiriki wa Makafiri) lilisababisha kuvunjika kwa Kipengele cha Mkataba wa Hudaybiyah ambao ulifanyika katika mwaka wa 638, Kipengele hicho kilikuwa ni “Kudhibiti Amani pamoja na Usalama baina ya Makafiri wa Mecca na Waislamu wa Madinna kwa muda wa miaka 10”
Baada ya Makafiri Kufanya kosa hilo la kutokuiheshimu Mkataba walioufanya na Waislamu waliamua kutuma mjumbe kwa jina ni Abu Sufyan kwa Mtume Mohamad ﷺ huko Madinna lengo lilikuwa ni kuomba msamaha na pia kufanya Mkataba mwingine mpya lakini Mtume ﷺ hakukubali ombi hilo kwani lilikuwa siyo kosa dogo na pia upuzi mtupu.
Kama tulivyoelezea hapo juu Mkataba ulikuwa umeelemea upande mmoja yaani ulikuwa umefanywa kwa lengo la kuwapa faida zaidi Makafiri kuliko Waislamu na juu ya hivyo hawakuuheshimu.
Mtume Mohamad ﷺ aliazimia kuusimamisha utawala wa dhulma na uadui wa Makafiri ambao ulikuwa umedumu kwa muda mrefu sana pale Makka. Baada ya Hapo Hakupoteza Muda bali aliamua kukusanya Wapiganaji Elfu Kumi na kuelekea huko Mecca Tarehe 1 Januari, 630.
Na baada ya siku Nane wakafika na kupiga Kambi katika sehemu inayojulikana kwa jina kama “Marr Az-Zahran”. Kwa Nyenzo za Usafiri wakati huo Ni Safari ya muda wa Siku Moja kutoka sehemu hiyo mpaka Mecca. Mtume Mohamad ﷺ aliwapa amri wapiganaji waumini wote wabebe vijinga vya moto mikononi mwao ili Makafiri wapate kuona idadi kubwa ya wapiganaji waliouzunguka mji wa Mecca.
Jaribu kufikiri Namna Makafiri wa Mecca walivyogopa waliopoona wamezungukwa na Jeshi kubwa la Wapiganaji Wa Kiislamu karibu 10,000. Ni Jambo ambalo hawakutegemea hata kidogo kwamba Waislamu wengi kiasi hicho. Walipoona wamezungukwa na idadi kubwa kama hiyo hawakuwa na budi isipokuwa kukata tamaa na kukubali Mji wa Mecca uchukuliwe. Hawakuthubutu kujilinda kwa njia yeyote bali kujiachia wafanywe chochote. Allahu Akbar. Angalia Maajabu. Ikabidi Abu Sufyan ambaye alikuwa Miongini mwa wakubwa wa Mecca aje hapo Kambini sehemu inayojulikana kama Marr Az-Zahran na kuzungumza Na mtume ﷺ na kumuomba asiivamie Mecca kwa vita. Kwa kweli Mtume ﷺ hakuja Mecca kuvamia na kuua bali nia yake ilikuwa nzuri kwani alitaka kusimamisha Dhuluma na Ukandamizaji wa haki usimamishwe na Hao Makafiri wa Mji wa Mecca. Maombi yake yalipokelewa vizuri sana kwani hilo ndolo lengo la Mtume ﷺ.
Miaka Michache iliyopita waliwatesa sana Waislamu na Kuwaua na hata kuwafukuza Hapo Mecca. Lakini baada ya Miaka Michache kupita mambo yakageuka na Makafiri Wamekuwa Hawana la kufanya. Waislamu walikuwa wachache na sasa Mtume Mohamad ﷺ amerudi na Jeshi la wapiganaji 10,000 (Elfu Kumi!!!!) Angalia Maajabu. Huu ni Muujiza Mkubwa usio Mfano.
Inathibitisha ile Aya iliyoshuka baada ya Mkataba wa Hudaybiyah inayosema. kumwambia Mtume Mohamad ﷺ kwamba “Tumekupa au Tumekufunulia Ushindi ulio Wazi au Bainifu”. Aya Hii inaashiria Ushindi huu wa Kuiteka Mecca. Allahu Akbar.
Kwa kweli waliuteka Mji wa Mecca bila kumwaga damu. Makafiri wa kikundi kilichoandaliwa na Ikrimah na Sufwan walianzisha Mapigano na Waislamu katika Upande mmoja aliokuwako Al-Khaliyd na Wapiganaji wake. Makafiri walitumia silaha kama vile Mapanga na Upinde katika pambano dogo la upande mmoja Walikufa wapiganaji wachache sana. (Wapiganaji Makafiri waliofariki Dunia ni 10 na Waislamu Wawili).
Mtume Mohamad ﷺ aliwanasihi Waislamu wasiwavamie wapiganaji wa Mecca isipokuwa wakivamiwa.
Na pia kama kawaida ya Vita vyote vilivyopita Mtume Mohamad ﷺ aliwanasihi wapiganaji waislamu wajiepushe na kuuwa Wananchi wasiokuwa Wapiganaji wa Vita kama vile Wazee, Wanawake, Watoto, Wanyama na Pia kukata Miti hovyo hovyo.
Mtume Mohamad ﷺ na Maswahaba wakaingia mji wa Mecca.
Bilali aliyekuwa Swahaba akafanya Adhana ya Kwanza katika Kaaba.
Mtume ﷺ Akavunja Masanamu Yote yaliyokuwa katika Jengo la Kaaba. Inasemekana idadi ya Masanamu Hayo ilikuwa 360 (Mia Tatu na Sitini). Mtume Mohamad ﷺ Mwenyewe alishiriki kwa kuvunja Masanamu hayo kwa kutumia Fimbo yake. Na huku anasoma Aya Ya Kuruani Namba 81 Katika Sura Namba 17 inayosema
وَقُلۡ جَآءَ ٱلۡحَقُّ وَزَهَقَ ٱلۡبَـٰطِلُۚ إِنَّ ٱلۡبَـٰطِلَ كَانَ زَهُوقً۬ا (٨١)
TAFSIRI
Haki (Ukweli) Umekuja na Upotovu Umeondoka (Umetoweka) Kwa Kweli Upotovu ni Wenye Kuondoka
Hadithi iliyokusanywa na Bukhari ( Sahih al-Bukhari Hadithi Namba 4720) inaelezea Habari hii kama ifuatavyo:
حَدَّثَنَا الْحُمَيْدِيُّ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنِ ابْنِ أَبِي نَجِيحٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ أَبِي مَعْمَرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ دَخَلَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم مَكَّةَ وَحَوْلَ الْبَيْتِ سِتُّونَ وَثَلاَثُمِائَةِ نُصُبٍ فَجَعَلَ يَطْعُنُهَا بِعُودٍ فِي يَدِهِ وَيَقُولُ {جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا} {جَاءَ الْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ الْبَاطِلُ وَمَا يُعِيدُ}
TAFSIRI
Abdallah Bin Masuud anaelezea kwamba Mtume wa Mwenyeezi Mungu aliingia Mecca (Katika Mwaka Walipoiteka (Conquest) Mecca) na kulikuwa na Masanamu 360 (Mia Tatu na Sitini yaliyozunguka Kaabah. Akaanza Kuyavunja Vunja kwa kutumia Fimbo Kwa Mikono yake Mwenyewe na huku akisema
“Haki (Ukweli) Umekuja na Upotovu Umeondoka (Umetoweka) Kwa Kweli Upotovu ni Wenye Kuondoka” (17.81)
Ukweli Umekuja na Upotovu (Ubatili) hauwezi Kuumba au Kufufua Chochote (34.49)
SHEREHE
Hadithi inafahamisha kwamba Mtume Mohamad ﷺ alisoma Aya mbili. Ya kwanza ni Aya Namba 81 katika Sura Ya Israa namba 17 na Aya ya pili ni Namba 49 katika Sura ya Sabaa Namba 34. Maana Ya Aya zote hizi mbili inahusiana na Kuja kwa Ukweli na Kuondoka kwa Ubatili.
Baada ya Ushindi huu mkubwa Makafiri hawakuona budi isipokuwa kuukubali Uislamu.
Na katika Waliosilimu ni Abu Sufyan ambaye alihusiana na Mtume Mohamad ﷺ kwani mtoto wake kwa jina Umm Habiba Ramlah alikuwa Mke wa Mtume Mohamad ﷺ
Abu Sufyan alikuwa Miongoni mwa Viongozi wakubwa hapo Mecca yaani alikuwa na Cheo na pia Mtu Maarufu na aliposilimu Mtume Mohamad akasema maneno yafuatayo:
“Na Hata Atakayeingia nyumba ya Abu Sufyan atakuwa katika Usalama, Atakayeweka Silaha Chini atakuwa katika Usalama. Na Atakayefunga Mlango mlango wa nyuma yake atakuwa katika Usalama”
Na Pia akaendelea kusema maneno yafuatayo kama ilivyopokelewa Na Imamu Bukhari (Sahih al-Bukhari Hadithi namba 4313) katika Hadithi zake:
حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ، حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنِ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ أَخْبَرَنِي حَسَنُ بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ قَامَ يَوْمَ الْفَتْحِ فَقَالَ ” إِنَّ اللَّهَ حَرَّمَ مَكَّةَ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضَ، فَهْىَ حَرَامٌ بِحَرَامِ اللَّهِ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ، لَمْ تَحِلَّ لأَحَدٍ قَبْلِي، وَلاَ تَحِلُّ لأَحَدٍ بَعْدِي، وَلَمْ تَحْلِلْ لِي إِلاَّ سَاعَةً مِنَ الدَّهْرِ، لاَ يُنَفَّرُ صَيْدُهَا، وَلاَ يُعْضَدُ شَوْكُهَا، وَلاَ يُخْتَلَى خَلاَهَا وَلاَ تَحِلُّ لُقَطَتُهَا إِلاَّ لِمُنْشِدٍ ”. فَقَالَ الْعَبَّاسُ بْنُ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ إِلاَّ الإِذْخِرَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَإِنَّهُ لاَ بُدَّ مِنْهُ لِلْقَيْنِ وَالْبُيُوتِ، فَسَكَتَ ثُمَّ قَالَ ” إِلاَّ الإِذْخِرَ فَإِنَّهُ حَلاَلٌ ”. وَعَنِ ابْنِ جُرَيْجٍ أَخْبَرَنِي عَبْدُ الْكَرِيمِ عَنْ عِكْرِمَةَ عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ بِمِثْلِ هَذَا أَوْ نَحْوِ هَذَا. رَوَاهُ أَبُو هُرَيْرَةَ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم
SHEREHE
Imepokewa kutoka kwa Mujahid (Swalla Allaahu Alayhi wa Aalihi wa Sallam) alisema: Mtume ﷺ wa Mwenyeezi Mungu alisimama na kusema “Mwenyezi Mungu ameifanya Makka kuwa patakatifu tangu siku alipoumba mbingu na ardhi, na itabakia kuwa ni patakatifu kwa mujibu Mwenyezi Mungu alivyoijaalia mpaka Siku ya Kiyama, kupigana humo hakuhalalishiwa yeyote kabla yangu na kupigana tena haitahalalishwa kwa yeyote baada yangu. Na haikuhalalishwa kwangu isipokuwa kwa muda mfupi.Wanyama Wake Wasiwindwe, wala mimea yake na nyasi zake zising’olewe. Na Vitu Vitakavyookotwa lazima Vitangazwe Hadharani.
Imepokelewa kwamba Abbas bin Abdul Muttalib akamwuliza Mtume ﷺ “Je Al-Idhkhir, Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu k ﷺ kwani ni muhimu kwa Wahunzi na katika (Matumizi ya) Nyumba (Je ni haramu pia?) Hapo Mtume ﷺ akanyamaza kisha akasema: Isipokuwa Idhkhir kwani ni halali kukata.
Mtume Mohamad ﷺ alipoiteka Mecca baada ya Kukimbia Mateso makubwa yaliyofanywa na Makafiri, hakulipiza kisasi chochote kwa wale Mateka Makafiri waliofanya Ubaya mkubwa wa Kutesa na Kuua bali aliwasamehe wote kufuatana na Habari yafuatayo:
“Kisha Mtume Muhammad ﷺ akawageukia Mateka na akasema: “Enyi Maquraishi, mnaonaje juu ya Malipo ninayopaswa kukupeni?”
Na Suhayl ibn Amr akasema: “Rehema, ewe Mtume ﷺ wa Mwenyezi Mungu. Hatutarajii ila kheri kutoka kwako.”
Hapo Mtume Muhammad ﷺ akasema: “Nawaambieni kama Yusufu alivyowaambia ndugu zake. Leo hapana lawama juu yenu; nendeni zenu, kwa kuwa mmekuwa huru.”
Suhayl akaingia katika Uislamu na akabadilika na kuwa Mwislamu Mcha Mungu ambaye alishiriki katika vita pamoja Mtume Muhammad na pia katika Enzi za Viongozi Wanne wa Kwanza wanaojulikana kama Khulafaa Arashidun Yaani Ukhalifa wa Rashidu.
Katika Mwaka Huu wa 630 kuna Habari 3 ambazo Mwenyeezi Mungu alipenda nitazungumzia hivi karibuni nazo ni
-Mapigano (Vita) ya Hunayn.
-Mapiganio (Vita)Ya Autas na
-Matayarisho Ya Kivita Kwenda Taif na Kuuzingira Mji Huo
Mtume Mohamad ﷺ alishiriki katika Mapigano Yote Matatu.(Hunayn, Autas na Taif)
Na baada ya Hapo Nitaendelea Kuelezea Matukio mengine katika Mwaka unaofuatia 631
Na hii ndiyo Nia Yangu Mola akipenda.
631/
INSHAALLAH INAKUJA KARIBUNI
HISTORIA HII FUPI YA UISLAMU BADO INAENDELEA

Historia Fupi Kuanzia Kuzaliwa Kwa Mtume Mohammad ﷺ Katika Karne Ya 6 Mpaka Enzi Ya Dola Ya Othman Karne ya 20