UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
AKILI YA MTU MKUBWA ALIYOPEWA MTOTO MDOGO NI NEEMA MOJAWAPO YA “KARAMAAT”KUTOKANA NA “KARAMAAT”NYINGINEZO MBALIMBALI
VIDEO MBALIMBALI HAPA CHINI ZA VIJANA (MUNGU AWABARIKI)
Kwa Kiingereza Neno “Genius” ni Mtoto mwenye Akili Kubwa. Lakini Wataalamu Bado kufahamu Kwa yakini Kinachosababisha Jambo Hili la kushangaza. Neno La Kitaalamu Katika Elimu ya Saikologia (Psychlogy) ni “Prodigy” Neno Hili linatumika kuitwa mtoto ambaye ni chini ya miaka kumi ambaye anakuwa na akili ya mtu mzima mfano wa Mtaalamu wa hali ya Juu. Wataalamu waliofanya utafiti wanasema akili hizi zinatokana na muingiliano kati ya Jeni (Genes) za Maumbile na Mazingara yaliyomzunguka huyu mtoto. Na wanadai kwamba hakuna Mtu yetyote anayezaliwa hivyo. Na kuna Wataalamu wengine ambao wanadai kwamba Akili Kubwa za Watoto wa aina hizi hazitokani na mazingara bali Genes za maumbile peke yake. Yaani Mtoto anazaliwa na Akili ya Asili. Soma hapa chini Habari hizi kwa Kiingereza.
(A child genius is born with brains, but there might be more than grey matter behind their incredible intelligence. A child prodigy is defined in psychology research literature as a person under the age of ten who produces meaningful output in some domain to the level of an adult expert. The term is also applied more broadly to young persons who are extraordinarily talented in some field. Many experts agree that prodigies are made as a result of calibration between a person’s genetic legacy and the environment in which the person grows. They argue that no one is born a prodigy. Others highlight prodigies’ innate abilities: for example, a 2014 study assessed 18 child prodigies and found that what they all had in common was a heightened attention to detail and exceptional working memory)
Mwenyeezi Mungu ndiye aliyetuumba na Kujaalia haya. Anasema katika Kuruani Tukufu kwamba
۞ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسۡتَحۡىِۦۤ أَن يَضۡرِبَ مَثَلاً۬ مَّا بَعُوضَةً۬ فَمَا فَوۡقَهَاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ڪَفَرُواْ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَـٰذَا مَثَلاً۬ۘ يُضِلُّ بِهِۦ ڪَثِيرً۬ا وَيَهۡدِى بِهِۦ كَثِيرً۬اۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِۦۤ إِلَّا ٱلۡفَـٰسِقِينَ (٢٦)
TAFSIRI
Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano wowote wa mbu na ulio wa zaidi yake (au chini yake kama hicho ni kijidudu kingine juu ya mgongo wa mbu kama wanasayansi wanvyotuambia). Ama wale wanaoamini, wao hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wao; lakini wale waliokufuru husema: “Ni nini analotaka Mwenyezi Mungu kwa mfano huu?” (Mwenyezi Mungu)huwawachia wengi kupotea .kwa mfano huo na huwaongoza wengi kwa mfano huo pia; lakini hamwachii yo yote kupotea kwa mfano huo (na mwingineo) isipokuwa wale wavunjao amri (Zake)
وَمَن نُّعَمِّرۡهُ نُنَڪِّسۡهُ فِى ٱلۡخَلۡقِۖ أَفَلَا يَعۡقِلُونَ (٦٨)
TAFSIRI
Na tunayempa umri (mrefu) tunamrejeza nyuma katika umbo (Jake). (Anakuwa kama mtoto).Basi je, hawayatii akilini (haya)?
وَٱللَّهُ خَلَقَكُمۡ ثُمَّ يَتَوَفَّٮٰكُمۡۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرۡذَلِ ٱلۡعُمُرِ لِكَىۡ لَا يَعۡلَمَ بَعۡدَ عِلۡمٍ۬ شَيۡـًٔاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ۬ قَدِيرٌ۬ (٧٠)
TAFSIRI
Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni kisha anakufisheni; na miongoni mwenu wako wanaorudishwa katika umri mbaya (wa uzee kabisa). Akawa hajui chochote (tena) baada ya (ule) ujuzi(aliokuwa nao). Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Muweza.
SHEREHE- KARAMAAT کرامات
Mwenyeezi Mungu ambaye ana hekima kubwa sana tena sana. Anachagua wakati na sehemu kisha anazalisha viumbe vyake kama hawa, kisha anawapa Neema za Kushangaza ili zisaidie katika kuongoza waja wake, ziwarudishe waja wake waliopotea. Na pia kuwazidishia imani waumini. Hizi ni dalili za Kukaribia kwa Kiyama. Kama vile Nabii Nuhu alivyojenga Meli yake na kuwahimiza watu wapande meli hiyo kabla ya kuja kwa Tufani. Mfano ule ule. Na leo tunaletewa maajabu haya ili turudi katika Meli Ya Mtume Mohamed (Sala na Amani Zake Mola Zimfikie)
Kutokana na Aya tulizozitaja tunasoma kwamba Mwenyeezi Mungu ametoa mifano mingi ambayo inathibitisha kwamba yeye ndiye aliyeumba ulimwengu. Na akampa binaadamu elimu kubwa na kisha anapozeeka anapoteza Elimu hiyo kwa ajili ya uzee. Na uzee unapozidi binaadamu anarudi tena na kuwa kama mtoto. Haya Tunayoyaona Leo kuhusu hawa watoto wenye Elimu kama watu wakubwa ni mifano ya Neema anazotoa Mwenyeezi Mungu zinazojulikana kama “KARMAAT” کرامات Kuna Vikundi vingine vya Kiislamu vilivyopo huko Saudi Arabia kama vile Wahabi au Salafi ambavyo vinapinga Habari hizi. Na Kuna Vikundi Vingine ambavyo Vinakubaliana na Zawadi hizi kwa mfano “SUFISM” wanasema kwamba kuna Miujiza ambayo walipewa Mitume tu peke yao ili kuthibitisha Ujumbe waliokuja nao lakini Kuna KARAMAAT ambazo Mawalii na Wachamungu wamepewa. Wanaendelea kusema kwamba Wachamungu ambao wanafanya Ibada sana na pia DHIKR za hali ya juu wanaweza kupata KARAMAAT.Kuna wengine siyo MAWALII peke yao ambao wanapewa KARAMAAT bali hata watu wa kawaida ambao wanamcha mungu. HADITHI YA MTUME NA KURUANI KARAMAAT ni neema mbalimbali kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Kwa Mfano Akili wanazopewa Watoto Wadogo ambazo ni za hali ya juu utafikiri wataalamu wenye umri mkubwa. Nitaweka Video Mbali Mbali za Watoto wa aina Hii ambao kwa kweli inashangaza na huenda Elimu walizonazo ni aina mojawapo ya KARAMAAT. na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi. Kuna Hadithi za Mtume ambazo Zinathibitisha” KARAMAAT kama hizi na pia katika Kuruani kuna Kisa kama kile cha Watu wa pango (Ashab Al-Kahf) katika Sura Ya Al-Kahf ambao walikuwa watu wa kawaida na kwa uchamungu wao walibarikiwa kuenda katika pango hilo walilolazwa kwa miaka 300 kwa Calendar za kileo au Miaka 309 kwa Calendar za Kiislamu. Kisa hiki kinatufahamisha Imani yao ilikuwa Kubwa na kwa usalama wao waliamua kuukimbia Mji walioishi ambao ulizama katika ibada za kikafiri na kuelekea katika Pango mbali na mji huo ili kujificha. Na Mwenyeezi Mungu akawahifadhi hapo. Neema hiyo waliyopata ni aina Za KARAMAAT kutoka kwa Mwenyeezi Mungu kwa waja wake. Hadithi ya Mtume ifuatayo pia ni mfano mzuri wa KARAMAAT.
وعن أنس رضي الله عنه أن رجلين من أصحاب النبي صلى الله عليه وسلم خرجا من عند النبي صلى الله عليه وسلم، في ليلة مظلمة ومعهما مثل المصباحين بين أيديهما، فلما افترقا، صار مع كل واحد منهما واحد حتى أتى أهله. ((رواه البخاري)) من طرق، وفي بعضها أن الرجلين أسيد بن حضير، وعباد بن بشر رضي الله عنهما.
TAFSIRI
Hadithi hii pia ipo katika Riyadh Aswalihiyn ambayo inahusu KARAMAAT inayosema kwamba Bwana Anas (Radhi Za Mwenyeezi Mungu Zimfikie) alisema kwamba: Mawahaba wawili wa Mtume ambao waliondoka kutoka katika nyumba ya Mtume katika Usiku uliokuwa na Giza Kubwa sana walikuwa wana mwanga mbele yao na walipotengana kila mmoja alikuwa na mwanga mbele yake (na huku kila mmoja akiongozwa na mwanga huu) mpaka waliporejea kwao (Katika Nyumba zao) Hebu Tusikilize Video Mbalimbali za kushangaza. Watoto hawa Wanazungumza na kufundisha mambo makubwa ambayo Kuna wengi watu wakubwa ambao hawawezi. Yaani Elimu za kushangaza sana. Allahu Akbar. Mwenyeezi Mungu awahifadhi na KUwazidishia Elimu.
NASIHA YANGU
Ninawaomba wazazi na mashekhe popote pale walipo wawaelekeze watoto hawa (Katika Video Hizi) na wengineo katika yaliyo bora. Kwani Wanasifa za Kuhifadhi na kuelewa kwa haraka na kwa hiyo kwanza wafundisheni Kuruani na Hadithi za Mtume hali bado wadogo. Kisha wafundisheni kila yenye faida katika dini na dunia wasije wakapoteza wakati kusoma Elimu zisizo na maana kama vile kupiga Bao. Pia Muwatunze sana wasifuatane na Marafiki wahuni wasije wakawapoteza. Mazoezi ya Kimwili pia ni muhimu kwa kulinda afya zao. Wafundisheni Maisha Ya Kawaida “Simple Means Of Life” na wajiepushe na Kutamani Maisha Ya Hali Ya Juu. Kutafuta elimu na kulingania dini siyo kazi rahisi na kwa hiyo muwafundishe subira, uvumilivu na kutosheka.
Nitaweka hapa chini Video Mbalimbali za Kushangaza Sana. Kuna Watoto wengi kama mfano huu lakini nimechagua wachache katika hawa kwa ajili na Nafasi katika Website hii. Mungu awahifadhi na Kuwapa Baraka katika Maisha Yao Yote. Alhamdulilah.
Video-1-MWANACHUONI MTOTO MDOGO-HAITHAM KHAMIS-TANZANIA
Msichana Haytham Khamis anafundisha Sayansi na Kuruani. Kwa kweli Haya ndiyo niliyoelezea katika Sherehe hapa juu. Hizi Ni KARAMAAT kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Ni Neema Mojawapo Kubwa. Alhamdulilah Mungu amzidishiye na awape kila la kheri wazazi wake. Allahu Akbar
Video-2-MAISHA YA MWANACHUONI MTOTO MDOGO-HAITHAM KHAMIS-TANZANIA
Namuomba Mwenyeezi Mungu amlinde na ampe kila la kheri Msichana Huyu Kwa Jina Haytham Khamis Na Pia Wazazi Wake. Ampe Elimu Kubwa Yenye Manufaa. Dua Yangu Na Sala Zangu Nitazifanya Kumuombea Kila la Kheri Duniani Na Akhera. Ninafurahi sana anapoichambua Sayansi, Tawhiyd na Dini. Alhamdulilah.
Video-3-MWANACHUONI MTOTO MDOGO-RAMADHAN BARAKA-TANZANIA
Alhamdulilah. Maajabu Ya Mwenyeezi Mungu. Mwenyheezi Mungu anatuletea zawadi nyingine kubwa ya Kijana Sheikh Ramadhan. Namuomba Mungu na Nitamsalia Special Prayer ampe kila la kheri yeye na wazazi wake. Anazungumza maneno makubwa sana. Sina zaidi isipokuwa usikilize mwenyewe kisha umuombee dua.
Video-4-MWANACHUONI MTOTO MDOGO-RAMADHAN BARAKA-TANZANIA
Mwanachuoni Mtoto Bado Mdogo Kwa Jina Ramadhan. Katika juhudi zake za kulingania Dini. Mwenyeezi Mungu ampe kila la kheri yeye na Familia Yake.
Video-5-MAISHA YA MWANACHUONI -SH. SHARIFU MIKIDADI-TANZANIA
Huyu Kijana Mwingine Ni Maajabu mengine ambayo makubwa. Amesilimisha watu wengi sana. Allahu Akbar. Miaka Mingi imepita na sasa amekuwa kijana. Namuombea kila la kheri katika shugjuli zake zote. Alhamdulilahi Mwenyeezi Mungu ampe Baraka katika Juhudi zake zote.
Video-6-MWANACHUONI SH. SHARIFU ALIPOKUWA AKILINGANIA DINI-TANZANIA
Hii Video inassisimua kweli kweli. Juhudi za Kijana huyu zilisababisha wengi kuukubali Uislamu. Namuombe Mwenyeezi Mungu Kila la Kheri. Allahu Akbar.
Video-7 Profesa Soborno Isaac Bari-INDIA
Huyu Kijana Mwingine Mdogo Ni Mwislamu amezaliwa India. Kwa hivi sasa anaishi America. Amezaliwa na Kipaji cha Elimu ya Sayansi na Mathematics. Maajabu Makubwa kwani alianza hayo alipokuwa mdogo sana miaka 4 na hivi sasa ana miaka 9. Ameandika kitabu. Namuomba Mungu amlinde na kumbariki.
Video-8- Profesa Soborno Isaac Bari-INDIA
Professor Soborno anafundisha University. Kwa kweli inashangaza. Mtoto mdogo kuwa Professor na kufundisha watu wenye umri mkubwa.Mwenyeezi Mungu ambariki na Ampe Elimu Ya Kuruani na PIa afundishe Kuruani kama anvyofundisha Sayansi. Kijana huyiu ametunikiwa zawadi mbalimbali. Allahu Akbar
Video-9 Mwanachuoni Mtoto Omar-Mombasa-Kenya
Katika Video Hii Sheikh Nuruddin Kishk na ndugu wanavyuoni wengineo pamoja na Kijana mdogo anayejulikana kwa Jina Omar. Namuombea kila la kheri mtoto huyu.Katika maisha yake. Na pia Sala zangu Special namuomba Mwenyeezi Mungu ampe yeye na wazazi wake kila la kheri. Alhamdulilah. Allahu Akbar.
Video-10 MTOTO WA MIAKA 3 – AMEHIFADHI KURUANI-Algeria
Maajabu Mengine ya Huyu mtoto ambaye inasemekana kwamba ametiwa katika kumbukumbu la kitabu cha Gueness Record. Mwenyeezi Mungu ambariki na amhifadhi. na wazazi wake pia. Allahu Akbar
Video-11 MWANACHUONI MTOTO MDOGO-NADHANI KUTOKA EGYPT
Huyu Kijana Mdogo sana. Anazielezea Aya Za Kuruani Na kuzichmabua. Allahu Akbar. Nadhani Kutoka Egypt. Jina Lake Muslim Said. Mwenyeezi Mungu ambariki na amhifadhi na wazazi wake pia. Allahu Akbar
Video-13 MTOTO MDOGO ANASOMA KURUANI VIZURI SANA-PAKISTAN
Bonyeza “Watch on YouTube” ukipendelea kuiona Video hii na itakuruhusu uione katika YouTube.
Maajabu Mengine ya mtoto huyu anyesoma kuruani vizuri sana huko Pakistan. Mwenyeezi Mungu ambariki na Kumhifadhi. Allahu Akbar.