UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
HISTORIA FUPI YA KURUANI TUKUFU
Salaam Nyingi kwa Wasomaji wa Website hii.
Alhamdulilah Nashukuru Mwenyeezi Mungu kwa kunipa uwezo siku ya leo Tarehe 11 September 2022 Jumapili Jioni kuweza kuandika machache kuhusu Historia Fupi Ya Kuruani. Kuna Habari nyingi na Mbalimbali za Kuzungumza lakini nimeona bora Nigusie machache kuhusu Historia Fupi ya Kuruani Tukufu. Lengo langu siyo kuelezea Tarehe kwa Tarehe kuanzia Kushuka kwa Aya za Kuruani mpaka mwisho kwani hiyo Mwenyeezi Mungu akinipa uzima ningependelea kuandika katika Mlango wa “HISTORIA YA UISLAMU” ambao bado sijaumaliza na hapo ndipo ningependelea kuandika Historia Ya Kuruani kwa njia hii lakini siku ya leo ningependelea kuelezea tu tofauti ya Maneno kama vile “Versions”, “ManualScript” ,”Quran Recitations” na “Quran Huruf” kwani nimeona tofauti ya Maneno haya yatasadia kutupa mwanga zaidi katika kuelewa Historia ya Kuruani Tukufu. Maneno haya siyo madogo bali yameleta Utatanishi Mkubwa katika Uislamu na Pia kuwapa wale wasiojua Uislamu njia ya Kupitisha Uongo na hila katika kuuvuruga Uisamu. Kwani Ukweli ni Ukweli na Huwezi Kudanganya watu kwa Uongo.
Versions au Toleo kwa Kiswahili katika Maandishi lina maana yake ni Kitabu kilichoandikwa na Mwandishi na kisha akakiandika Tena baada ya Masahihisho kwa kuzidisha au kupunguza na kwa hiyo Versions hazifanani. Na iwapo mwandishi huyo ataandika kitabu chake hicho mara kumi basi Versions zake zote zitakuwa tofauti kwani kila version au Toleo litakuwa limekuja na ziyada au upungufu wa alichoandika.
Manuscript maana yake ni Maandishi ya Mkono. Kwa hiyo unaweza kukuta Manuscript mbalimbali za Toleo au Version Moja. Neno Manu ni kifupi cha neno Manual na maana yake ni Kwa mkono na Neno Script ni Herufi zilizotumika katika Kuandika na kwa hiyo ManuScript maana yake Maandishi Ya Mkono au Mashine ya kuandikia kwa kutumia Herufi. ManuScript inaweza kuwa kwa lugha yeyote. Kwa mfano Manuscript ya Kiswahili au Kiarabu au Kiingereza au Kifaransa au Kijerumani au Kihindi au Kiyahudi au Lugha yeyote Duniani.
Biblia za zamani sana zipo Versions Mbalimbali na ningependelea kuzipanga kufuatana na Miaka. Biblia hizi siyo zote ambazo zimekamilika bali nyinginezo ni badhi tu ya Vitabu au Kurasa na Kwa hiyo zote zimetofautiana na hivi ndivyo Wakristo wanavyotufundisha na siyo Waislamu. Siwezi kuzitaja Versions zote bali chache tu. kwa mfano:
Wanatufundisha kwamba Hivi karibuni walivumbua SCROLLS kama vile
1/VERSION YA KETEF HINNOM SCROLLS. Wanadai kwamba haya ndiyo maandishi ya BIBLIA ya zamani sana yaani katika karne ya 600 kabla ya Ukristo na kwa hiyo ni maandishi ya Nabii Musa au Agano la Kale.
2/VERSION YA DEAD SEA SCROLLS ambayo inadaiwa kwamba iliandikwa mwaka c. 150 BCE – 70 CE
Herufi C yaani Century “Karne” na BCE yaani Kabla Ya Ukristo na CE yaani Kipindi cha Ukristo. Sasa ngojea nikupangie Versions zilizofuata yaani Baada Ya SCROLLS hizi mbili.
3/Version ya Septuagint Nitazitaja mbili hapa chini
1/Codex Vaticanus 2nd century BCE (Vipande Vya Makaratasi)
na 2/ Version ya Codex Sinaiticus 4th century CE (Iliyokamilika)
Huu ni mfano tu wa Baadhi ya Vitabu Vya Toleo Mbalimbali za Biblia za Zamani kwani kuna zaidi ya hizi nilizozitaja.
Tusichanganye na Kuruani kwani Kuruani ni Version au Toleo Moja tu. Hakuna Versions katika Kuruani. Huu ndio ukweli. Kuruani ya Leo ni ile ile ya Karne ya 7 hakuna Tofauti.
Lakini kuna Maandishi ya mkono mbalimbali yaani Manual Script na Haya maandishi ukichunguza utakuta hakuna tofauti na Kuruani ya Mwanzo.
Wasiojua wanachanganya na kudhani Script mbalimbali zilizopo ni Versions na kwa hiyo Kuruani zinatofautiana ukisema hivyo basi unapotosha.
Kuna Tafsiri au Translations za kuruani mbalimbali. Zile za Kiarabu kwa kiarabu ni Tafsiri ya Kufafanua Aya za kuruani na Zile za Kugha Nyinginezo kama vile Tafsiri ya Kuruani iliyoandikwa na Yusuf Ali kwa kiingereza ni Kuwasaidia wasiojua Kiarabu waielewe Kuruani na hivyo hivyo lugha nyinginezo. Kwa hiyo Tafsiri siyo Version hata kidogo bali ni Tafsiri ya Kutoka Lugha moja na kwenda lugha nyingine.
Kuna Visomo vya kuruani mbalimbali. Kuna Visomo Saba na kuna Wanavyuoni wanaosema kwamba Kuna Visomo ni Kumi. Na kila kisomo kinatofautiana na Kingine katika Matamshi ya maneno. Katika Upande wa linguistic, lexical, phonetic, morphological and syntactical forms. Tofauti ya visomo hivi kumi ni ndogo na inakusanya tofauti ya sheria zinazohusiana na prolongation, intonation, and matamshi ya maneno lakini tofauti katika vituo “stops”, vowels, na consonants (Na kusababisha tofauti ya pronouns na verb forms), na siyo kubadili Maana ya Maneno au Aya. Yaani tofauti ya Visomo hivi ni Matamshi tu na haibadili maana ya Maneno, Aya au Sura. Na hili ni jambo zuri kwani Tofauti hii inatusaidia sisi wageni katika Matamshi ya Lugha hii kwani siyo wote tunaozungumza Lugha Kiarabu.
Kuruani hakuna Versions au toleo mbalimbali. na hakuna kilichofichwa. Kwa vile Kuruani ilishushwa katika mifumo Saba za makabila ya Kiarabu (saba) katika Enzi ya Mtume Mohamad hapo baadaye ilibidi uchaguliwe mfumo mmoja tu yaani Standard Language ili iwe inawakilisha Kuruani iliyokuja kwa lugha saba. Lugha ilityochaguliwa ni ile ya Kabila la Mtume yaani Kikureish. Na ilimbidi Amiri au Khalifa Othmani Ibn Affan afanye hivyo kwani Kuwepo kwa Kuruani katika lugha saba ingeleta matatizo na hivi ndivyo ilivyoanza kwani kila kabila lingesema Kuruani ya kabila langu ni bora kuliko Kuruani ya kabila nyingineyo.
Kuruani ni Version Moja tu lakini visomo vipo mbalimbali vilivyozaliwa kutokana na Mifumo (Ahruf) ile saba na Kuwepo kwa visomo mbalimbali inasaidia watu duniani kwani lugha za dunia zipo mbalimbali pia na matamshi ya lugha za dunia yanatofautiana na kwa hiyo inakuwa rahisi kwa wageni kuchagua Kisomo kilicho Rahisi kufuatana na Matamshi aliyozoea katika Lugha yake ya Asili lakini visomo au mifumo hiyo lazima zisipingane na Kuruani ya Standard iliyopitishwa na Kiongozi Othman Ibn Afan ambaye alifanya juhudi kubwa ya kuandaa Kurfuani moja na kuziodoa nyinginezo ambazo ijapokuwa zilikuwa sahihi na zilipokelewa na Mtume lakini ilikuwa bora wachague Kuruani moja tu ambayo itawakilisha nyinginezo. Lakini hapo baadaye miaka ikiyofuata kulizuka Visomo (Qiraat) nyinginezo 10 ambazo baadhi yake zinatumika mpaka leo katika baadhi ya mataifa ya kiislamu duniani.
Katika Mlango Huu ningependelea kutaja Vile Visomo Kumi Vya Kuruani, Walimu wake na Waliotangaza Visomo Hivi.Yaani QARI au Reader na RAWI au Tramsmitter. Na Kisha Pia kuzitaja Zile Manuscript za Kuruani ambazo Zilivumbuliwa na Kwa hivi sasa zimehifadhiwa katika Sehemu Mbalimbali za Dunia. Ningependelea pia Kuwaletea Picha za Manuscript Hizi.
Jambo muhimu la kuelewa ni kwamba Kuruani ni Ujumbe aliopewa Mtume Mohamad kama vile Taurati aliyopewa Nabii Musa.
Mafundishi ya Nabii Isa yaliandikwa na Wengine na Siyo Revelation au Wahyi kama vile Kuruani au Tourati na Pia hakuandika Nabii Isa Mwenyewe. Yaani Nabii Isa Hakuwa Messenger bali alikuwa Mtume.
Musa na Mohamad walikuwa Messengers na Watume pia.
Maandishi kuhusu Nabii Isa Yamepewa Jina katika kuruani “Injili” na Kitabu cha Asili cha Injili tunakiamini hakuna Tatizo kwani Hata Kuruani imekitaja.
Tatizo ni kwamba Baada ya Kupita Muda Maandishi haya Yaliharibiwa kwa kubadilishwa, Kuongeza na Kupunguza na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akashusha Kuruani ili kuwarudisha watu katika ukweli na wasipotee. kwa hiyo tuwe macho. Na huu ndiyo ukweli
INAENDELEA HIVI KARIBUNI…………………………..