UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
LINGUISTICS YA KURUANI
MFUMO (STRUCTURE)WA LUGHA YA KURUANI NA VIPENGELE VYAKE
Elimu inayojulikana kama Linguistics imekusanya Elimu Ya Lugha. Katika Mlango huu Nitatumia Elimu hii ili tuelewe Kuruani vizuri zaidi. Elimu hii ilitumika Tangu kushuka Kuruani na Ndiyo iliyosababisha Makafiri kukubali Uislamu. Waarabu walikuwa Hodari sana katika Ufundi wa Lugha Yao na walikuwa waandishi wakubwa wa Mashairi katika wakati huo wa Enzi Ya Mtume huko Mecca lakini Kuruani iliwashangaza sana kwani haikuwa Mashairi (Poetry) wala Nathari (Prose) bali ni Lugha ya pekee ya hali ya juu. Na hiyo peke yake iliwasababisha Makafiri wengi kuingia katika Uislamu. Leo tupo katika Enzi ya Sayansi na Kuruani Inaendelea kutoa Miujiza isiyo na Mwisho katika Nyanja mbali mbali za kisayansi. Kuruani ni Muujiza Mkubwa Sana. Inatupa Mapya kila siku na itaendelea kufanya hivyo mpaka Mwenyeezi Mungu atakapopenda. Allahu Akbar
(Lingusitics is The scientific study of language and its structure, including the study of grammar, syntax, and phonetics. Specific branches of linguistics include sociolinguistics, dialectology, psycholinguistics, computational linguistics, comparative linguistics, and structural linguistics.)
“Katika Lugha Ya Kiarabu (Arabic) Elimu ya Sarufi (Grammar) Imekusanya Sehemu Mbili:(SYNTAX NA MORPHOLOGY)”
Na Phonetics au Elimu Ya Sauti (Al-Ilm Attaswiyt)) tunaweza kuipa Jina TAJWIYD lakini tuelewe kwamba ni Tofauti na Phonetics zinazohusiana na Elimu Ya herufi peke yake.
SUALA LA KWANZA
SURA NAMBA 11 AYA NAMBA 69
وَلَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٲهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُواْ سَلَـٰمً۬اۖ قَالَ سَلَـٰمٌ۬ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجۡلٍ حَنِيذٍ۬ (٦٩)
TAFSIRI
69. Na wajumbe wetu .(Malaika kwa sura za kibinadamu) walimwendea lbrahimu kwa bishara (khabari njema kuwa atazaa na kujukuu na mengine na) wakasema: “Salam (alaykum – amani juu yenu)” Akasema (lbrahimu) “Juu yenu pia iwe · amani.” Na hakukaa (lbrahimu) ila mara alileta ndama (aliyechomwa vizuri juu ya mawe ya moto)
SHEREHE YA AYA
Kisa hiki kinahusu Nabii Ibrahim alipojiwa na Malaika watatu ambao walikuja na ujumbe kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Alibashiriwa kwamba atapata Mtoto hali kwamba walikuwa wakongwe na pia walipewa habari ya kuangamizwa kwa watu wa nabii Lut kwani watu wake walikuwa wamezama katika Maasi makubwa.
SHEREHE YA SARUFI -Grammar(YA AYA)
قَالُواْ سَلَـٰمً۬اۖ قَالَ سَلَـٰمٌ۬ۖ
Katika kipande hiki Malaika wakasema سَلَـٰمً۬اۖ SALAMAN
Nabii Ibrahim akawajibu سَلَـٰمٌ۬ۖ SALAMUN
neno SALAMUN na SALAMAN lina maana moja lakini Katika Lugha ya Kiarabu kuna Tofauti ya Lugha na Sarufi (Grammar). Malaika Waliposema SALAMAN Nabii Ibrahim hakujibu SALAMAN pia bali aliwajibu SALAMUN kwa sababu Malaika wametoa salamu ya Mara moja katika Ziara waliyoifanya na kwa hiyo Salamu zao zilikuwa za muda. Salamu yaani Amani ya Mwenyeezi Mungu iwe juu ya Nabii Ibrahim katika muda wa ziara yao hapo nyumbani kwake. Nabii Ibrahim akawajibu SALAMUN kwa maana Ya Salamu ya Daima isiyo mwisho. na hii ndiyo tofauti baina ya maneno haya mawili kilugha. Na pia tuelewe kwamba Nabii Ibrahim amesifiwa kwamba ni Mtu wa Amani na Salamu zake alizozitoa zilikuwa za Daima. Aliwapa Salamu Malaika ya Daima mpaka Mungu atakapopenda. Na Elimu ya Sarufi (Grammar) inatufahamisha zaidi habari hii
قَالُواْ سَلَـٰمً۬اۖ قَالَ سَلَـٰمٌ۬ۖ
Sarufi ya Kipande hiki ni kama ifuatavyo
سَلَـٰمً۬اۖ Neno hili katika Grammar lipo katika position inyojulikana kama Al Maf’ool al Mutlaq (Cognate Accusative Case) na kwa hiyo linathibitisha Maneno yaliyokadiriwa kabla yake na ambayo hayakutajwa kiwaziwazi katika Aya Hii nayo ni “NUSALIMU SALAMAN” yaani “TUNAKUSALIMIA SALAMAN” na kwa hiyo kipande NUSALIMU SALAMAN ni VERBAL TENSE.(Al-Jumla Alfiiliya) na Verbal Tense ni MTENDAJI + KITENDO + KITENDWA na Grammar inasema kwamba KITENDWA lazima kitiwe FATHA na ndiyo maana hapa Neno SALAMAN limetiwa TANWEEN FATIHA na siyo DHUMMA
Na Neno la pili سَلَـٰمٌ۬ۖ lipo katika NOMINAL TENSE.(Jumla Ismiya) Kwani Ni Predicate (Al-Khabar) ya Subject (Al-Mubtadaa) iliyokadiriwa na hiyo ni SALAMIY SALAMUN Yaani “Salamu yangu ni Salamun” SALAMIY Ni Subject ya kukadiria na SALAMUN Ni Predicate iliyotajwa. Na Katika Sheria Ya Grammar, Subject (Al-Mubtadaa) na Predicate (Al-Khabar) zinatiwa DHUMMAH zote mbili na ndiyo maana hapa neno SALAMUN limetumika na nabii Ibrahim hakujibu SALAMAN. Kwa hiyo Lugha na Sheria za Elimu ya Sarufi (Grammar)ni muhimu ili tupate kufahamu maana kama hizi.
Kuruani imejaa Elimu kubwa sana bali Elimu zetu ndogo. Na tutaendelea kupata Mapya katika Kuruani mpaka Mwenyeezi Mungu atakapopenda. Ni Muujiza mkubwa sana. Allahu Akbar
SUALA LA PILI
SURA Ya-Siin NAMBA 36 AYA NAMBA 58
سَلَـٰمٌ۬ قَوۡلاً۬ مِّن رَّبٍّ۬ رَّحِيمٍ۬ (٥٨)
TAFSIRI
58. Salama (tu juu yao), ndilo neno litokalo kwa Mola (wao) Mwenye rehema.
SHEREHE
Maneno haya ni Ahadi kutoka kwa Mwenyeezi Mungu kwa Wanaotenda mema kwamba Hao watakuwa katika Salama.
SHEREHE YA SARUFI -Grammar(YA AYA)
سَلَـٰمٌ۬ قَوۡلاً۬ مِّن رَّبٍّ۬ رَّحِيمٍ۬ (٥٨)
Neno سَلَـٰمٌ۬ limetiwa TANWEEN DHUMMA na neno la Pili قَوۡلاً۬ limetiwa TANWEEN FATIHA kwa nini yote mawili yasifanane kwa kutiwa Harakati zenye kufanana. Sababu gani iliyofanya La kwanza likatiwa TANWEEN DHUMMA na la Pili limetiwa TANWEEN FATIHA
Jawabu ni kwamba Neno SALAMUN ni ahadi anayotoa Mwenyeezi Mungu ambayo ni ya Daima. Yeye Mwenyeezi Mungu moja ya Jina lake ni SALAM yaani ni moja ya sifa zake na kwa hiyo Anapotoa Salamu basi itakuwa ya Daima na ndiyo maana hapa imetiwa TANWEEN DHUMMAH na Neno la Pili ni QAWLAN ambalo ni kauli yake ambayo haina mwisho. Kwa mfano Elimu ya Kuruani haina mwisho na kila siku tunasoma Mapya na kwa hiyo Kauli yake MUTAJADID daima yaani Haina mwisho au wakati au sehemu hatuwezi kuyapimia. “You can’t limit Allah’s words or his knowledge” Kuruani ni Muujiza ambao unazalisha kila siku mapya na ni maneno au kauli yake Mwenyeezi Mungu. Na ndiyo maana Neno QAWLAN limetiwa katika Aya Hii TANWEEN FATIHA yaani QAWLAN na siyo QAWLUN. Je imeeleweka? huu ni muujiza siyo mdogo.
Sasa tuje kwenye Elimu ya Grammar (Sarufi) ili tuelewe zaidi Aya Hii
سَلَـٰمٌ۬ قَوۡلاً۬ مِّن رَّبٍّ۬ رَّحِيمٍ۬ (٥٨)
NENO سَلَـٰمٌ۬ Ni Predicate (Al-khabar) ya Subject (Al-Mubtadaa) inayokadiriwa lakini haikutajwa waziwazi nayo ni ” SALAMU-ALLAHI” maana yake “Salaam Za Mwenyeezi Mungu” Kwa hiyo Tukiunga maneno haya itakuwa “SALAMU-ALLAHI SALAMUN” maana yake “Salaamu Za Mwenyeezi Mungu ni Salaam” Na yapo katika NOMINATIVE CASE au (Jumlah Ismiya) ambayo ina maana ya DAIMA Na Sheria ya Sarufi (Grammar) inasema Subject na Predicate lazima zitiwe DHUMMAH na ndiyo maana Neno la kwanza limekuwa SALAMUN na siyo SALAMAN. Na kwa ajili hiyo Menyeezi Mungu ametaka Aya hii itaje SALAMU ziwe daima huko Peponi. Na Neno la Pili قَوۡلاً۬ Katika Sentensi lipo katika position inyojulikana kama Al Maf’ool al Mutlaq (cognate accusative case) na kwa hiyo linathibitisha Maneno yaliyokadiriwa kabla yake na ambayo hayakutajwa waziwazi katika Aya Hii nayo ni “QALA ALLAHU QAWLAN” maana yake ni “Alisema Mwenyeezi Mungu Kauli” Kipande hiki ni “VERBAL TENSE” (Al-Jumla Alfiiliya) na kwa hiyo Neno “QAWLAN” limetiwa TANWEEN FATIHA na siyo QAWLUN kutiwa Dhummah. kama Tulivyosema hapo awali kwamba VERBAL TENSE inaonyesha RENEWAL au mabadiliko. Ni Sentensi inayoonyesha Mabadiliko. Kuruani inatoa kila siku mapya na Kauli au maneno yake Mwenyeezi Mungu hayana mwisho na tunapata kila siku mapya. Huwezi kuweka LIMIT au kumpangia Mwenyeezi Mungu Kauli yake. Anavyosema atakavyo na itaendelea hivyo mpaka mwisho wa Ulimwengu. Allahu Akbar. Je Imeeleweka? Aya Hii ni sawa na Aya Iliyopita kwani zote zinahusiana na Subject na Predicate Tenses katika Arabic Language. Subject Tense inaonyesha Stability au Kuthibiti na Verbal Tense inaonyesha Mabadiliko ya Vitendo kutegemea Wakati. Alhamdulilahi. Allahu Akbar.
HEKIMA YA NENO لِصَـٰحِبِهِۦ na صَاحِبُهُ KATIKA AYA SURA YA AL-KAHF Sura Ya Al-Kahf Namba 18 Aya Kuanzia Namba 32 Mpaka Namba 44
HEKIMA YA NENO لِصَـٰحِبِهِۦ na صَاحِبُهُ KATIKA AYA SURA YA AL-KAHF
Sura Ya Al-Kahf Namba 18 Aya Kuanzia Namba 32 Mpaka Namba 44
وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلاً۬ رَّجُلَيۡنِ جَعَلۡنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيۡنِ مِنۡ أَعۡنَـٰبٍ۬ وَحَفَفۡنَـٰهُمَا بِنَخۡلٍ۬ وَجَعَلۡنَا بَيۡنَہُمَا زَرۡعً۬ا (٣٢)
كِلۡتَا ٱلۡجَنَّتَيۡنِ ءَاتَتۡ أُكُلَهَا وَلَمۡ تَظۡلِم مِّنۡهُ شَيۡـًٔ۬اۚ وَفَجَّرۡنَا خِلَـٰلَهُمَا نَہَرً۬ا (٣٣)
وَكَانَ لَهُ ۥ ثَمَرٌ۬ فَقَالَ لِصَـٰحِبِهِۦ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ ۥۤ أَنَا۟ أَكۡثَرُ مِنكَ مَالاً۬ وَأَعَزُّ نَفَرً۬ا (٣٤)
وَدَخَلَ جَنَّتَهُ ۥ وَهُوَ ظَالِمٌ۬ لِّنَفۡسِهِۦ قَالَ مَآ أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَـٰذِهِۦۤ أَبَدً۬ا (٣٥)
وَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآٮِٕمَةً۬ وَلَٮِٕن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّى لَأَجِدَنَّ خَيۡرً۬ا مِّنۡهَا مُنقَلَبً۬ا (٣٦)
قَالَ لَهُ ۥ صَاحِبُهُ ۥ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ ۥۤ أَكَفَرۡتَ بِٱلَّذِى خَلَقَكَ مِن تُرَابٍ۬ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٍ۬ ثُمَّ سَوَّٮٰكَ رَجُلاً۬ (٣٧)
لَّـٰكِنَّا۟ هُوَ ٱللَّهُ رَبِّى وَلَآ أُشۡرِكُ بِرَبِّىٓ أَحَدً۬ا (٣٨)
وَلَوۡلَآ إِذۡ دَخَلۡتَ جَنَّتَكَ قُلۡتَ مَا شَآءَ ٱللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِٱللَّهِۚ إِن تَرَنِ أَنَا۟ أَقَلَّ مِنكَ مَالاً۬ وَوَلَدً۬ا (٣٩)
فَعَسَىٰ رَبِّىٓ أَن يُؤۡتِيَنِ خَيۡرً۬ا مِّن جَنَّتِكَ وَيُرۡسِلَ عَلَيۡہَا حُسۡبَانً۬ا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَتُصۡبِحَ صَعِيدً۬ا زَلَقًا (٤٠)
أَوۡ يُصۡبِحَ مَآؤُهَا غَوۡرً۬ا فَلَن تَسۡتَطِيعَ لَهُ ۥ طَلَبً۬ا (٤١)
وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِۦ فَأَصۡبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيۡهِ عَلَىٰ مَآ أَنفَقَ فِيہَا وَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِہَا وَيَقُولُ يَـٰلَيۡتَنِى لَمۡ أُشۡرِكۡ بِرَبِّىٓ أَحَدً۬ا (٤٢)
وَلَمۡ تَكُن لَّهُ ۥ فِئَةٌ۬ يَنصُرُونَهُ ۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِرًا (٤٣)
هُنَالِكَ ٱلۡوَلَـٰيَةُ لِلَّهِ ٱلۡحَقِّۚ هُوَ خَيۡرٌ۬ ثَوَابً۬ا وَخَيۡرٌ عُقۡبً۬ا (٤٤)
32. Na wapigie mfano wa watu wawili: mmoja wao tulimfanyia (tulimpa) mabustani mawili ya mizabibu, na tukaizungushia mitende, na pia katikati yake tukatia miti ya nafaka (nyingine).
33. Haya mabustani mawili yote yalijaa matunda yake wala hayakupunguza chochote (katika uzazi wake); na ndani yake tukapitisha mito
34. Na akawa na mali mengine (pia). Basi akamwambia mwenzake na hali ya kuwa akibishana naye, “Mimi nina mali nyingi kuliko wewe na (nina) nguvu zaidi kwa ajili ya wafuasi (nilio nao).”
35· Na akaingia katika bustani yake na hali ya kuwa anajidhulumu nafsi yake (kwa maasia) akasema: “Sidhani abadan kuwa (bustani) hili litaharibika “
36. “Wala sidhani kuwa Kiama kitatokea. Na kama (kitatokea hicho Kiama) nikarudishwa kwa. Mola wangu, bila shaka nitakuta kikao chema kuliko hiki (alichonipa ulimwenguni. Siku njema huonekana asubuhi. Kama nilivyopata huku, na huko nitapata)
37. Mwenzake akamwambia na hali ya kuwa anamjibu: “Je! Unamkufuru (na unakanusha neema za) yule aliyekuumba kwa udongo, tena kwa tone Ia manii, kisha akakufanya mtu kamili?”
38. “Lakini (mimi namuamini) yeye Mwenyezi Mungu (tu kuwa) ndiye Mola wangu, wala simshirikishi Mola wangu na yoyote.”
39. “Na lau ulipoingia katika bustani yako (hii) ulisema “Hivi nilivyonavyo amenitakia Mwenyezi Mungu. Nguvu hazipatikani ila kwa (kupewa na) Mwenyezi Mungu. (Ungesema hivi ingekuwa bora). Kama unaniona mimi nina mali kidogo na watoto wachache kuliko wewe.”
40. “Basi huenda Mola wangu akanipa kilicho bora kuliko bustani yako na kuipelekea (hiyo bustani yako) mapigo ya radi kutoka mbinguni na ikawa ardhi tupu inayotelezesha (isiyokuwa na mmea) “
41. “Au maji yake yakawa yenye kuzama hata usiweze kuyapata.”
42. Basi matunda (mali) yake yakabambwa (yakaangamizwa) na akawa anapinduapindua viganja vyake (anasikitika) kwa ajili ya alichokigharimia (yale mabustani). Ikawa miti yake imeanguka juu ya chanja zake, na akawa anasema: “Laiti nisingalimshirikisha Mola wangu na yoyote!”
43. Wala hakuwa na watu wa kumsaidia baada ya (kumkosa) Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe kujisaidia.
44·Huko (akhera) ufalme ni wa Mwenyezi Mungu tu aliyoko daima. Yeye ndiye bora kwa malipo na (ndiye) bora wa (kuleta) matokeo mazuri.
SHEREHE YA AYA
Kwa kifupi kisa hiki kinahusu Marafiki wawili. Mmoja wa Marafiki hawa alikuwa na Mabustani mawili na Mitende na pia Miti ya Nafaka nyinginezo na Neema ilikuwa kubwa kwani Kila Mti ulizaa sana na Mazao yaliyo mazuri sana. alijigamba na kubishana na Rafiki yake aliyekuwa siyo Tajiri na kumwambia kwamba ana utajiri na wafuasi wengi zaidi kuliko mwenziwe na akaendelea kumwambia kwamba Haamini siku ya Kiyama na hata kama kitatokea kweli yeye ataruzukiwa yaliyo mazuri kama alivyoruzukiwa duniani. Alikuwa ana imani kwamba “Dalili ya Mvua Mawingu” Maadamu Duniani amepewa Neema kubwa kama hii basi Baada ya Kiama atapewa Neema pia. Kwa hiyo Mtu huyu alifanya Kiburi na Kujisifu sana na Akaamini kwamba Neema Hiyo haitaondoka Kamwe. Na Huyu mwenziwe (Rafiki Yake) akamnasihi Tajiri Huyu asijivune na kumsahau Mwenyeezi Mungu. Kwani ameumbwa kwa tone la Manii linalotokana na Udongo na lazima amuogope muumbaji. Maneno haya ya Kujigamba yalimwuudhi sana Rafiki yake na hasa kule kujiona Bora kwa kukana kwa siku ya kiyama. Mwenyeezi Mungu akatoa Mtihani na Mara Shamba likaangamizwa na baada ya hapo yakafuatilia Majuto Makubwa. Akasema Laiti asingelimshirikisha Mwenyeezi Mungu na Yeyote. Lakini Maziwa yanapomwagika huwezi kuyazoa. Hiki ndichi kisa kwa ufupi.
HEKIMA YA MANENO MAWILI
Kuna mengi katika Aya Hizi lakini Leo Alhamdulilahi nitazungumzia Neno Moja tu ambalo linashangaza sana. Yaani neno Moja Lenye Maana Ya Ajabu Kubwa. Katika Kuruani Kila Herufi ina maajabu. Neno hili katika Aya 34 na 37 hapa juu.
Neno Katika Aya namba 34 ni لِصَـٰحِبِهِۦ
Na Neno katika Aya Namba 37 ni صَاحِبُهُ
Tafsiri Ya Neno hili ni “Mwenziwe” au “Rafiki” au “Swahibu” maana ni moja lakini ukiangalia vizuri utaona Tofauti katika Maandishi.
SHEREHE YA NENO لِصَـٰحِبِهِۦ na صَاحِبُهُ
Katika Aya Namba 34 لِصَـٰحِبِهِۦ Kuna Alif Ndogo sana baina ya Herufi SWAD na HAA na Alif hii inajulikana kama The dagger alif or superscript alif (Arabic: ألف خنجري alif khanjarīyah) (Hii siyo Alif ya kawaida bali Alif ya Ishara kuashiria kwamba kulikuwa na Alif na kwamba Kufuatana Na Visomo vya Kuruani kuna uwezekano kuirudisha mahali pake. Yaani QIRAAT za Kuruani zipo zaidi ya Moja na Kufuatana na Sheria kuna uwezekano kuirudisha katika Kisomo, Hivi ndivyo Historia Inavyosema)
Na Katika Aya Namba 37 صَاحِبُهُ Kuna Alif kubwa baina ya Herufi SWAD na HAA na Alif hii inajulikana kama MEDIAL VOWEL ALIF Nayo ipo katikati Ya Neno.
Hebu tuzilete zile Ibara mbili kutoka katika Aya namba 34 na 37 na kisha tuzichambue.
Aya Namba 34 – فَقَالَ لِصَـٰحِبِهِۦ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ ۥۤ
Tafsiri=Basi akamwambia mwenzake na hali ya kuwa akibishana naye
Haya ndiyo maneno ya Yule Tajiri
Aya Namba 37- قَالَ لَهُ ۥ صَاحِبُهُ ۥ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ
Tafsiri=Mwenzake akamwambia na hali ya kuwa anamjibu:
Na Haya Ndiyo Majibu aliyotoa Yule Rafiki yake asiyekuwa Tajiri
SUALA LA KUJIULIZA
Mbona neno katika Aya namba 34 Lina Alif ndogo sana. Na katika Aya Namba 37 kuna Alif Kubwa ya Kawaida? Je kuna Hekima gani ya Matumizi kama haya?
JAWABU LA SUALA
Wataalamu wa Lugha wanatuambia Hekima Kubwa ya Maneno na Herufi za Kuruani Kufuatana na Kisa katika Aya Tulizosoma Hapa Juu.
Katika Aya namba 34 Hawa Marafiki wawili walikuwa bado Urafiki wao Mzuri na kwa hiyo Neno لِصَـٰحِبِهِۦ lilikuwa Kamili bila Ya Alif inayojulikana kama ALIF AL-FASL yaani ALIF ya Kutenganisha. (Separation) Kufuatana na Urafiki wa watu hawa wawili Neno hili lilikuwa Moja na Liliungana kama vile marafiki wa kweli wanavyoungana kirafiki.
Lakini katika Aya Namba 37 Baada ya Rafiki Tajiri Kubishana na Mwenziwe na Kujigamba kwa Kumtukana Mwenyeezi Mungu Urafiki wao ukawa sio Mzuri na neno صَاحِبُهُ likatumika. Hapa neno hili limetenganishwa na ALIF ya FASL (Separation Alif) Yaani Alif ambayo ipo katikati ya neno صَاحِبُهُ Inaashiria Urafiki Umevunjika.
Je unaona hekima Ya Kuruani? Yaani Kila Herufi imechaguliwa kwa Hekima Kubwa sana. Neno hili limegawanywa na Kuvunjwa katikati na Herufi Nyingine ya ALIF kama vile Urafiki unapovunjika.
Urafiki Umevujika baada ya Yule Rafiki Tajiri Kujiona Bora Ya Yule Aliyemuumba na Kumuudhi Mwenziwe. Angalia Muujiza Wa Kuruani. Allahu Akbar.
Baada ya Kusoma Habari hizi nimefahamu kwamba katika Kuruani Kila Herufi, Neno au Aya Ni Muujiza isiyo na Mwisho. Allahu Akbar.
Fikiri sana utaona Hivyo. Katika Kisa hiki neno hili limetumika mara Mbili. Mara ya kwanza walipokuwa marafiki hawa bado wanapendana na Mara ya Pili walipochukiana na neno pia limebadilika.
Na ushahidi ni kwamba mara ya kwanza Yule tajiri ndiye aliyetumia Neno لِصَـٰحِبِهِۦ lililokamilika kwani alighafilika anayoyasema na huku akidhani jambo la kawaida na Mara ya Pili alilitumia neno hili صَاحِبُهُ yule Rafiki aliyekuwa siyo Tajiri na ambaye Hakutamani urafiki na Mtu aliyekufuru na ndiyo maana Neno hili limevunjwa na ALIF ya FASL Na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi Hekima Hii iwapo tumekosea. Allahu Akbar
MAAJABU YA AYA NAMBA 68 na 69 KUTOKA KATIKA SURA NAMBA 16 (Al-Nahl)
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨)
ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ فَٱسۡلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلاً۬ۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌ۬ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٲنُهُ ۥ فِيهِ شِفَآءٌ۬ لِّلنَّاسِۗ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَةً۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ (٦٩)
TAFSIRI
68. Na Mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba “Jitengenezee majumba (yako) katika milima na katika miti na katika yale (majumba) wanayojenga ( watu).”
69. Kisha ”Kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mota wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita).” Kinatoka katika matumbo yao kinywaji (asali) chenye rangi mbali mbali; ndani yake kina ponyo (dawa) kwa wanaadamu. Hakika katika hayo muna mazingatio kwa watu wenye kufikiri.
SHEREHE.
Aya hizi mbili zimekusanya Miujiza Mbalimbali ya kushangaza. Kwani Sayansi imegundua hivi karibuni. Vitendo vilivyotumika katika Aya hii vinamuashiria Nyku wa kike (Feminine Bee). Anaambiwa Kwamba ndiye aliyeamrishwa kujijengea Nyumba zao, Na pia ni yeye ndiye anayefanya kazi ya kutafuta chakula. kuruani imetumia Vitendo vifuatavyo vyenye kumhusu Nyuki wa Kike na siyo wa Kiume. Angalia Herufi ya mwisho katika vitendki vifuatavyo vinamuashiria Nyuki Feminine. Herufi “Ya” ni ya Kike na Herufi ” Kaf” yenye Kasrah ni Ya kumuashiria Nyuki wa Kike.
ٱتَّخِذِى = Chukua au Fanya (Herufi Ya mwisho wa neno hili ى ni Ya Kike (Feminine)
كُلِى= Kula (Herufi Ya mwisho wa neno hili ى ni Ya Kike (Feminine)
فَٱسۡلُكِى= Fuata (Herufi Ya mwisho wa neno hili ى ni Ya Kike (Feminine)
رَبِّكِ= Mungu Wako (Herufi Ya كِ Yenye Alama ya Kasrah mwisho wa neno hili ni Ya Kike (Feminine)
Sayansi inatufundisha kwamba Nyuki wa Kiume ana kazi nyinginezo kama vile Kumtunza Nyuki Malkia (Queen Bee).
Kuruani Ni Muujiza usio Mdogo.
Neno YAKHRUJU katika Aya Hii يَخۡرُجُ linatupa Maana Ya Kushangaza sana. Lina maana ya “Mwenyezi Mungu ndiye aliyejaalia Nyuki watoe Asali” Katika Lugha ya Kiarabu Herufi ya “YA” inatupa maana hii. Lakini ingelikuwa “TAKHRUJU” yaani kwa kutumia Herufi ya “TA” mwanzoni mwa Kitendo hiki basi maana ingebadilika na kuwa “Kunatoka Matumboni mwa nyuki Asali” na siyo Majaliwa yake Mwenyeezi Mungu. angalia Muujiza wa kilugha. Kuruani imetumia Kila herufi kwa mana maalumu na siyo bure bure. Herufi “Ya” na “Ta” mwanzoni mwa Kitendo hiki inasababisha Aya ibadilike maana. Herufi “Ya” ina maana ya Kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu” na “Ta” ina maana ya uwezo wake nyuki tu peke yake. Je unaona Hekima ya Kuruani na Je unaona Sayansi inavyhoashiriwa kiajabu. Allahu Akbar.
22/05/2022
Alhamdulilah Ningependelea leo kuzungumzia Aya za Mwanzo Kutoka katika Sura Ya Al-Waqia. Aya hizi zinazungumzia Siku ya Kiyama. Yaani siku ya Mwisho wa Dunia na pia Tunaweza kuita ni siku ya Malipo.
سُوۡرَةُ الواقِعَة
إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ (١) لَيۡسَ لِوَقۡعَتِہَا كَاذِبَةٌ (٢) خَافِضَةٌ۬ رَّافِعَةٌ (٣)
TAFSIRI
I. (Wakumbushe) Litakapotokea takeo (hilo li Kiyama)
2. Ambalo Kutokea kwake si uwongo.
3. Lifedheheshalo (wabaya), Litukuzalo (wazuri)
Aya Hizi zinazungumzia siku ya Kiyama. kwamba siku hiyo ni ya kweli na sio Utani au uwongo. Sayansi pia inathibitisha kwamba Dunia ina mwisho. Leo ningependelea kuelezea Aya Namba 3 ya Sura Hii. Nayo ni خَافِضَةٌ۬ رَّافِعَةٌ (٣)
Maneno Mawili Ya Aya hii yamechaguliwa kwa Ufundi wa hali ya Juu. Yana Maana ya Wabaya watafedheheshwa na Wazuri watainuliwa. Ukichunguza utaona hakuna herufi ya و “WAW” baina ya maneno haya mawili. Na Herufi ya و “WAW” ingeleta maana ya Neno “NA” ya kiungio kama tulivyofasiri hapa. Kwa nini Katika Aya hakuna Herufi ya WAW? Wataalamu wa Lugha au Grammar ya Arabic wanasema kwamba Kungetumika herufi WAW (Aya ingekuwa خافضة ورافعة ) basi maana ingebadilika na kuwa “Wabaya Watafedheheshwa katika wakati maalum na katika wakati mwingine Wazuri watainuliwa” Je unaona Maana ilivyobadilika? Herufi WAW au و inaleta maana ya MUGHAYARA au Mabadiliko ya wakati kama wanavyosema watu wa Lugha. Kutokutumika kwa Herufi ya WAW katika Aya namba 3 kumesababisha wakati usibadilike. Yaani Watakapofedheheshwa Wabaya basi na wakati huo huo wazuri watainuliwa. Kwa lugha nyingine Time ile le Vitendo viwili vitafanyika. Jed unaona Lugha invyotumika? Kwa hiyo Mwenyeezi Mungu ametumia Haya maneno mawili tu ni kwa hekima kubwa.
Kila neno limetumika kwa hekima na katika mahali pake.