SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Maajabu Ya Kuruani-1

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

30/10/2022

Namshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kutupa uzima na pia kutupa nyenzo mbalimbali ya kutuzidishia Imani. Kuruani  ni Maneno yake Mwenyeezi Mungu ambaye Hana mwanzo  na hana Mwisho. Na amejaalia Mwongozo huu wa Kuruani  uwe Hai pia. Ni Maneno yaliyo hai na Inatoa Mapya kila siku, kila wakati , kila saa, kila dakika na kila Sekunde. 

Kwa nini isiwe Hai na Hali tunasoma Kila Siku Maajabu yasiyo na mwisho. Ni Miujiza isiyo na Mwisho yaani huwezi  kuhesabu kwani kila siku, kila saa, kila dakika, kila sekunde anaumba  tunayoyajua na tusiyoyajua. 

Siku ya Leo nitaanza kuzungumzia  Maajabu Makubwa lakini siwezi kujigamba kwamba Nitamaliza Mlango huu leo.

Nia Yangu ni kuuandika Mlango  huu kuanzia Leo  na Nitawaletea Miujiza Mbalimbali.

Lakini  siwezi Kutoa Ahadi ya Kuumaliza kwa Siku Moja kwani Miujiza Ya Kuruani haina Mwisho lakini nitaandika kidogo kidogo kwani “Ndo Ndo Ndo  hujaza Ndoo”.

SEHEMU YA KWANZA  (Ophthalmic and vision science-Matibabu ya Macho)

Ukienda Hospitalini na Kupimwa Macho na Ukiambiwa kwamba  Macho yako ni  6/6  yaani  Unaweza kuona Umbali wa Mita 6 na Kiwango hicho ni cha kawaida kwa mtu  yeyote mwenye macho  mazuri ni kuona  umbali wa Mita 6.

(The only difference is depending if you are in the UK or America, as it is measured in either feet or metres. 6/6 vision describes being able to see at 6 metres what an average person can see at 6 metres)

Kwa kipimo hicho  huhitaji Mewani kwani macho  yako ni Mazuri.

Sasa hebu tuende katika Kuruani na Tufunue Sura Namba 6  Na Aya Namba 6

Aya Yenyewe ni kama ifuatayo:

) أَلَمۡ يَرَوۡاْ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا مِن قَبۡلِهِم مِّن قَرۡنٍ۬ مَّكَّنَّـٰهُمۡ فِى ٱلۡأَرۡضِ مَا لَمۡ نُمَكِّن لَّكُمۡ وَأَرۡسَلۡنَا ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡہِم مِّدۡرَارً۬ا وَجَعَلۡنَا ٱلۡأَنۡهَـٰرَ تَجۡرِى مِن تَحۡتِہِمۡ فَأَهۡلَكۡنَـٰهُم بِذُنُوبِہِمۡ وَأَنشَأۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِمۡ قَرۡنًا ءَاخَرِينَ (٦)

Jambo lakushangaza ni Ibara  ya Kwanza la Aya hii ambalo ni  أَلَمۡ يَرَوۡاْ  yenye maana ya  “Je hawaoni”  Kwa kweli  inashangaza kwani  Madakitari wa Macho  wanasema  6 chini  ya 6  na ukienda katika Kuruani  Sura ya 6  Aya Namba  6  Ibara ya kwanza inataja  Habari  ya Kuona.

Aya Hii haizungumzii  Macho  lakini kilugha Neno  يَرَوۡاْ  lina maana nyingine ya Kuona kwa Moyo na Katika Aya Hii lina maana ya Kufikiri kwa Moyo  au Kwa Kiingereza  Vision Hebu tusome Tafsiri ya Aya Hii na kisha Tuendelee na Maajabu ya Aya Hii:

TAFSIRI

6. Je hawaoni uma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Tuliwamakinisha katika nchi tusivyokumakinisheni (nyinyi), na tukawapelekea mvua iendeleayo, (wakastarehe kwa kila namna ya mazao), na tukaifanya mito inapita mbele yao. Kisha tukawaangamiza kwa sababu ya dhambi zao.; na tukaumba baada yao uma nyingine. 

SHEREHE

Ndugu  Msomaji sasa Hebu tuchunguze  Ajabu ifuatayo ambayo imenishagaza Sana.

Herufi za ibara أَلَمۡ يَرَوۡاْ   ukigeuza katika Namba ambazo  walikuwa wakitumia Waarabu na Mataifa Yaliyopita Utapata Namba Inayoshangaza sana.

أَلَمۡ يَرَوۡاْ  

Alif=1 / Lam=30 / Mim=40 / Yaa=10 / Raa=200 / Waw=6 / Alif=1

Ukijumlisha  1 + 30 + 40 + 10 + 200 + 6 + 1=288

Namba  288  inashangaza sana  kwani Wataalamu wa Macho  wanatuambia kwamba  Macho  ya Binaadamu yana Megapixel  576  na Inashangaza sana kwani  288 ni Megapixel ya Jicho  moja na Kwa macho  mawili ni  288  x2=576

(According to scientist and photographer Dr. Roger Clark, the resolution of the human eye is 576 megapixels. That’s huge when you compare it to the 12 megapixels of an iPhone 7’s camera)

Kwa kweli  Mwenyeezi Mungu Mkubwa sana tena sana. Je huoni Maajabu ya MEGAPIXEL  katika Muujiza huu?

Kwa mfano  Simu ya Mkono, Camera au Screen ya Computer kila moja Ina Kiwango cha PIxel zake. Na Ili  Resolution (mwono) Iwe nzuri lazima Pixel ziwe nyingi na kama wataalamu wanvyotuambia kwamba Macho ya Binaadamu yana PIXEL  Milioni  576 (576,000,000) yaani  MEGAPIXEL 576.  Je unaona Maajabu Ya kuruani?  Hii kuruani ni lugha iliyo Hai na siyo Lugha ya zamani iliyokwisha Kufa hata kidogo. Inatupa  Jawabu  tunapotafuta hapo hapo. Allahu Akbar.

SEHEMU  YA PILI    (Heliophysics-Kisomo  cha Jua na Athari yake katika Solar System)

Wataalamu wanatuambia kuhusu Jua kwamba  Joto la sehemu ya Nje ya Jua (Surface Temperature)  ni   5,778 Kelvin  (Kelvin inatumika kwa kipimo cha Joto kubwa kama vile Joto la Jua.  Wataalamu watuambia Habari hizi  katika Usemi  wao hapa chini:

(The Sun is a G2V star, with G2 indicating its surface temperature of approximately 5,778 K (5,505 °C; 9,941 °F), and V that it, like most stars, is a main-sequence star).

Na  Joto la Ndani ya Jua  ni  15  Millions Kelvin. Wanatuambia  katika Usemi wao hapa Chini  kama ifuatavyo:

(The Sun’s Core is the hottest part of the Sun and of the Solar System. It has a density of 150 g/cm3 at the center, and a temperature of 15 million kelvins (15 million degrees Celsius, 27 million degrees Fahrenheit).

Sasa  Tukumbuke Vipimo hivi viwili. Cha Kwanza ni  Joto la Gamba la Jua au Surface ya Sun ni  Kelvin 5,778  Na Ndani ya Jua au SUN’s Core  ni Kelvin Millions  15

Sasa Hebu Tushangae tena. Namba hizi  mbili zipo katika Kuruani na zimeashiriwa kiajabu sana tena sana.

Mara Ya Kwanza Kutajika Kwa neno  Jua yaani “SHAMS”  katika Kuruani ni Sura Namba  2 Aya namba  258 

الم تر الي الذي حاج ابرهم في ربه ان اتيه الله الملك اذ قال ابرهم ربي الذي يحي ويميت قال انا احي واميت قال ابرهم فان الله ياتي بالشمس من المشرق فات بها من المغرب فبهت الذي كفر والله لا يهدي القوم الظلمين

TAFSIRI

(258.Hukumsikia yule aliyehojiana na Ibrahimu juu ya Mola wake kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? lbrahimu aliposema: “Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na hufisha,” yeye akasema: “Mimi pia nahuisha na kufisha.” lbrahimu akasema: “Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi.” Akafedheheka yule aliyekufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu).

Na Mara ya Mwisho Kutajika Kwa Neno Jua Yaani  “SHAMS”  ni katika Sura Namba 91 Aya Namba 1

والشمس وضحيها

TAFSIRI

1. Naapa kwa jua na kwa muangaza wake

SHEREHE

Na Ajabu ni  kwamba Ukihesabu Aya zilizopo Baina Ya Aya Hizi  mbili  utapata Jumla Ya Aya Ni 5,778  sawa sawa na  Namba tuliyotaja hapa juu yaani  inaashiria Joto la Gamba La Jua  au Surface Heat ambayo ni 5,778 tuliyoitaja hapa Juu. 

Sasa Tuangalia Sura Ya Mwisho ambayo  ni Sura Iliyoitwa kwa jina la  “Al-SHAMS”  Sura Hii  inaanza na Kuzungumzia Jua na Mwanga wake (Brightness). Jambo la Kushangaza ni Kwamba Wataalamu wanatumia Mwanga katika Kupima Joto  la CORE  au Ndani ya Nyota Yeyote. Na Kipimo cha Jua itakuwa hivyo hivyo kwa kutumia Mwanga wake. Na kama tulivyosema Kwamba Ndani ya Jua Joto au Temperature ni Kelvins Milions  15. Basi  Utashangaa  sana nikikuambia tena kwamba Sura Hii ina Jumla za Aya  15 tu!!”!!  kama kwamba inaashiria  Joto  la Ndani ya Jua  au Kelvins  15!!!!!   Sura Hii  inashangaza. Kwanza  Aya Ya kwanza Inataja kiapio cha Mwenyeezi Mungu kwa Jua na Mwanga wake. Linganisha Uhusiano baina ya Mwanga na Joto katika Kazi za Wanasayansi katika kutafuta Temperature ya Core au Ndani ya Jua. Kisha Linganisha na  Aya za Sura Hii ambazo ni 15 tu  na Namba hii ni sawa sawa na Joto  au Temperarure ya Core au Ndani ya Jua.

Haya Mambo  siyo madogo. Yanatisha sana. mwenyeezi Mungu ameweka katika Kuruani Viashirio au Alama Alama ili kuwapa waja wake imani na Pia Kutupa Tahadhari. Ukitumia  Akili utaona siyo bure bure bali  ni viashirio. Sasa  huoni Hizi Namba zilivyopangwa? 

Kabla  Tuishusha Kuruani mwenyeezi Mungu aliiandaa Vizuri sana na Kisha akajaza Miujiza Mutupu. Haya siyo madogo  hata kidogo. Je huoni kila kitu  kimepimwa? kila kitu. 

Haya  tuliyoyaelezea hapa juu ni kutoka Kwa Mwenyeezi Mungu na Siyo Mtume ﷺ Hakuna Aliyejua haya Wakati huo wa karne  ya 7 hata kidogo. Hivi ni vipimo  vya Kisasa ambavyo vinatugundulia haya. Je unaona Muujiza? Kazi ya Mtume ﷺ ni Kufikisha Ujumbe tu aliopewa na alifanya hayo na akafundisha  yaliyowahusu  wakati huo. Hata yeye Mtume  ﷺ hakujua haya tunayoyasoma leo kwani  haya tumewekewa sisi wakati huu wa Sayansi ili iwe muujiza kwetu. ili kutupa Imani na pia Kuwavutia wasiokuwa Waislamu. Kuruani ni Muujiza wa kila Siku mpaka Dunia Kwisa na siyo  wakati wa Mtume  ﷺ tu.  Allahu Akbar.  

Nimeweka Picha hapa Chini ya Jua na Jicho

Miujiza Bado Inaendelea katika Mlango  huu huu…………..

Jicho na Kipimo cha Megapixel ambacho nimeelezea hapa juu.

Jua Nje na Ndani. Vipimo Vya Joto la Jua Nimeelezea Hapa Juu katika Sherehe

MAAJABU YA AYA NAMBA 68 KUTOKA KATIKA SURA NAMBA 16

وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ } [النحل:68].    

Alhamdulilah Leo Tarehe 20/11/2022. Kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu nitaanza na Kudokeza Muujiza unaohusiana na Aya Hii.  Nilikwisha zungumzia katika Milango ya Website hii kuhusu Miujiza inyohusiana na Aya Hii kwa hiyo Leo Nia Yangu ni Kufanya Nyongeza. Aya Hii inazungumzia Habari za nyuki. Kwa hiyo Tafsiri ya Aya  ni kama ifuatayo:

68.Na Mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba “Jitengenezee majumba (yako) katika milima na katika miti na katika yale (majumba) wanayojenga ( watu).”

Ukichunguza Aya Hii kwa makini utaona Herufi za Lugha ya kiarabu zilizotumika katika Aya Hii (zisizokariri) ni 16 tu yaani zimeunda Aya Hii kutoka katika Herufi za Kiarabu  28.

Ukichunguza tena utaona Jumla ya Maneno (Ukihesabu Herufi WAW  kama neno) ni 16  Pia.

Namba ya Sura Hii ni 16. Habari hizi nilizungumzia hapo zamani lakini leo nitadokeza Ajabu nyingine katika Aya Hii ni kwamba Jumla ya NUQTA  au DOTS  zilizopo  juu na chini ya herufi hizi  ni  32       

Katika Kuruani ya hapo mwanzo yaani wakati wa Mtume ﷺ na baadaye kidogo NUQTA na Alama Nyinginezo kama vile  FATHA, KASRAH na DHUMMA  na Namba za Aya ziliongezwa na Wanavyuoni ili kuwasaidia  Wasomaji wa Kuruani watamke na pia kuisoma kuruani  bila ya Kosa. Lakini Kuongezwa huku hakubadilishi maana ya Aya. Muujiza mkubwa ni kwamba Kila kilichoongezwa  kilikuwa chini ya Uongozi wa Mwenyeezi Mungu.

Sayansi  Inatuambia kwamba Chembe za Uzazi (Chromosomes) za nyuki wa Kiume ni 16 na Nyuki wa kike ni 32  Angalia Maajabu.

Hizi  NUQTA  pia zinatupa Muujiza wa Chromosomes za Kike. Yaani Kuruani kila kitu kinaashiria Saini ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu. 

Allahu Akbar. Katika Kuruani kila Alama za Matamshi na Namba zote zilizoongezwa  Zinatupa Miujiza ambayo hakuna aliyejua wakati huo wa zamani. Hivi leo Baada ya Maendeleo ya Computer hivi sasa tunagundua mambo yasiyo na Mwisho. Allahu Akbar. Miujiza isiyo na Mwisho.

“Diploid females have16 pairs, or 32, chromosomes, and haploid males have only 16 single chromosomes”.

MAAJABU YA SURA YA  LAYLATU AL-QADR. SURA NAMBA 97

{ إِنَّا أَنزَلْنَٰهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ (1) وَ مَا أَدْرَىٰكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ (2) لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ (3) تَنَزَّلُ الْمَلَٰئِكَةُ وَ الرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ (4) سَلَٰمٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ (5) } [القدر:1-5].

TAFSIRI YA SURA LAYLATU AL-QADR

SURATUL QADR (Imeteremka Macca)


1. Hakika Tumeiteremsha (Qurani) katika
Laylatul-Qadr (usiku wenye heshima kubwa), (usiku wa mwezi wa Ramadhani).
2. Na jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini huo usiku wa Laylatul-Qadr?
3· Huo usiku wa hishima (huo) ni bora kuliko miezi elfu.
4· Huteremka Malaika na roho (za viumbe watakatifu) katika (usiku) huo kwa idhini ya Mola
wao kwa kila jambo
5· Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.

SHEREHE YA SURA HII

1 . Qurani-kama iJulikanavyo – ilikuwa ikiteremshwa kidogo kidogo, basi siku ile iliyoanza kuteremshwa ilikuwa katika Usiku wa Laylatu Al-Qadr (usiku wenye hishima kubwa). Ndio ikaambiwa kuwa Qurani imeteremshwa katika
Laylatu Al-Qadr , ni usiku mmoja mtukufu umo katika mwezi wa Ramadhani, ambao umebarikiwa kuliko miezi elfu;
yaani mtu akifanya amali njema katika usiku huo hupata thawabu kama za mwenye kufanya amali ile kwa zaidi ya miezi elfu : na mwenye kufanya maovu naye hupata dhambi za mwenye kufanya maovu kama yale kwa zaidi ya miezi elfu. Na Mwenyezi Mungu ameuficha usiku huu haujulikani ni upi, ili watu wajitahidi kufanya ibada katika
mwezi mzima wa Ramadhani; lakini unatarajiwa zaidi kuwa katika kumi Ia mwisho na Hasa usiku wa kuamkia mwezi 23,25,27 na 29. Basi atakaye kujua yakini kuwa ameupata usiku huu, bila ya shaka, inamlazimu ajipinde na kufanya ibada mwezi mzima. Wala si lazima kwa mwenye kuupata usiku huu kuona alama yoyote.

MAAJABU YA SURA HII

Swahaba wa Mtume  

aliyejulikana kwa jina kama Ibn Abbas alijaribu kukisia siku hiyo kwa kuhesabu maneno Ya Sura Hii mpaka Neno  هِيَ  ambalo ni Neno La 27   lenye maana ya “Huo”  yaani Siku Hiyo na akasema huenda  Neno Hili linaashiria Siku hiyo ya Tarehe 27. Na Huyu ndiyo wa kwanza katika Uislamu kutumia Hesabu katika Utafiti. Kwa hiyo siyo jambo Geni. Vipimo vya hesabu vilianzwa na Swahaba huyu. Na Angalia  Maajabu Ya Sura Hii ambayo Inazungumzia Kushushwa kwa Kuruani. Sura Ina Maneno  30  sawa sawa na Siku za Mwezi  wa Ramadhan. Na Neno  “HIYA”  ni neno  la 27. Allahu Akbar.

Hivi karibuni Watafiti  wamefanya Juhudi kubwa ya Utafiti  wa Sura Hii na wakagundua Tarehe hiyo ya 27 ambayo imetajika pia  katika Sura hii kiajabu sana.

Hebu Tuichunguze Sura Hii tuone Maajabu Yasiyo na Mwisho:

{ إِنَّا أَنزَلْنَٰهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ (1) وَ مَا أَدْرَىٰكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ (2) لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ (3) تَنَزَّلُ الْمَلَٰئِكَةُ وَ الرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ (4) سَلَٰمٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ (5) } [القدر:1-5].

1/Ibara لَيْلَةُ الْقَدْرِ Imetajika katika Sura Hii mara 3  na Herufi  za Ibara hii ni 9  kwa hiyo ukijumlisha  9 + 9 +9=27  Angalia Maajabu  tunapata Tarehe 27

2/Neno الْقَدْرِ Limetajika Katika Sura Hii katika Aya  ya Kwanza Neno la  5 

Na limetajika tena katika Aya ya Pili Neno  la 10   na Mara ya Mwisho katika Aya Ya 3 Neno  la 12

Hebu tujumlishe Positions au Sehemu hizi

5 + 10 + 12=27

Angalia Maajabu   tunapata Tena Tarehe 27  Je unaona  Maajabu. Allahu Akbar. Kwa hiyo muashirio ni Tarehe  27. Lakini Ingelikuwa bora tufanye Ibada Kila siku ili tusije Tukaikosa kwani Hizi ni Juhudi za kibinaadamu lakini Huenda sivyo. Kwa kweli Inashagaza sana.  Kuruani Ni Muujiza mkubwa sana. Allahu Akbar.

MAAJABU YA  AYA NAMBA  76  KUTOKA KATIKA SURA NAMBA 6

{ فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ الَّيْلُ رَءَا كَوْكَبًا قَالَ هَٰذَا رَبِّي فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْءَافِلِينَ } [الأنعام:76].

TAFSIRI YA AYA

76. Na usiku ulipomwingilia (lbrahimu na hali kakaa na makafiri), akaona nyota, alinena (makusudi
kutaka kuwavuta watumie fikira zao): ‘(Nyota) hii ni Mola wangu.” Ilipotua (ikapotea), alisema (kuwaambia wale makaftri kama kwamba yu pamoja nao katika ibada ile): “Sipendi Mola  wanaopotea (hawawepo ila wakati makhsusi tu).”

SHEREHE YA AYA

Nabii Ibrahim  akatumia  Hekima kubwa katika kulingania Dini. Hii ni Falsafa ya hali ya Juu sana. TRunafundishwa namna ya kujibizana na Makafiri yaani kwa kutumia hekima na siyo  kutukanana.

MAAJABU YA KIPANDE CHA AYA KUTOKA KATIKA AYA HAPA JUU

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ الَّيْلُ رَءَا كَوْكَبًا

Sura Namba 6  Ayan Namba  76

Kwanza Ningependelea kuelezez Neno  كَوْكَبًا

Neno Hili lina maana Mbalimbali lakini maana zote zinakubaliana kwamba كَوْكَبًا  katika Aya Hii  ni Sayari ambayo inategemea Mwanga wa Nyota Nyingineyo inayowaka. Kwa hiyo neno hili  lina maana ya Sayari, Kometi, Asteroidi, Meteors, Kila Umbile Angani ambalo Halina mwanga wa peke yake bali kwa kutengemea  mwanga kutoka katika Nyota inayowaka  (Reflected Light).

Wataalamu wanafichua Siri ya Nyota hii kwa kusema Ni  Kometi ambayo  inapitia karibu na Ardhi na tunaiweza kuiona katika kila baada ya miaka  76  na  Jina La Kometi linaitwa Halleys  Comet ambaye aliigundua 

Mtaalamu huyu aliyejulikana kwa jina kama  Edmond Halley na kuanzia siku hiyo  Kometi ikatiwa Jina lake “Halley’s Comet”

(Halley’s periodic returns to the inner Solar System have been observed and recorded by astronomers around the world since at least 240 BC. But it was not until 1705 that the English astronomer Edmond Halley understood that these appearances were reappearances of the same comet. As a result of this discovery, the comet is named after Halley.)

Wataalamu Wanasema Muda wa kuiona Kometi hii tukiwa Ardhini  ni Miaka  6  yaani kuanzia  Mwaka wa 74  Mpaka Mwaka wa 79

MUUJIZA KATIKA KURUANI

Sasa Tuangalie Maajabu. Aya Namba 76 inaashiria Ile miaka 76 ya kuja kwa nyota yaani kila miaka  76  na Sura Namba 6 Inaashiria Ile Miaka 6 Ya kuiona Nyota Hiyo. Allahu Akbar.

(Halley is a short-period comet visible fromEarth every 75 to 79 years)

Kuna  watafiti  wengineo ambao  wanajitahidi mpaka kutoa Jina la Mtaalamu huyu katika kipande cha Aya tuliitaja hapa Juu.

فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ الَّيْلُ رَءَا كَوْكَبًا

Wanatamka herufi  hizi kwamba Ni  Hailley ambaye aliigundia Kometi hii.  Na Ajabu ni kwamba Ukigeuza Herufi za Jina Hili Katika Namba walizokuwa wakitumia Waarabu na mataifa Mengineyo kwani Namba zilikuwa Bado kugunduliwa wakati huo tutapata  Jumla ya Herufi Hizi ni Namba ya Kushangaza  ambayo  ni  76                                            

Hebu  Tuzichambue hapa chini na kisha Tujumlishe=

Herufi Ha=5

Herufi Alif=1

Herufi  Lam=30

Herufi Lam ya pili=30

Herufi  Ya=10

Jumla hapa ni      5 + 1 + 30 + 30 + 10=76

Angalia Maajabu. Herufi za Kiarabu ambazo ukizitamka jina la Hailley ukigeuza katika Namba na kisha Kujumlisha utapata Namba  76.

Huu ndiyo Muujiza. Allahu Akbar. Yaani Mtaalamu atakayegundua Nyota Hii ametajika katika Aya Hii Kiajabu sana.

Yaani Hizi Namba zinashangaza, Unaweza Kukataa lakini ukifikiri sana unajikuta unakubaliana na Wataalamu. Allahu Akbar.


NAMBA Pi “π” NA MAAJABU YAKE KATIKA KURUANI TUKUFU

Hebu nianze na Safari hii ya kushangaza sana tena sana.
Mashuleni tunafundishwa Namba Pi ambayo inatumika katika Vipimo vya Kutafuta Eneo (Area) Na Mduara (Circumference). Kipimo Hiki kinajulikana nacho ni 3.14.

Sitaelezea Mafundisho ya Elimu ya Hesabu za Kutafuta Eneo lakini jambo ambalo la kushangaza na ambalo ningependelea wewe msomaji ufikiri sana ni kwamba katika Kuruani Kuna Sura Inayojulikana kama “AL-HAJ” yaani HIJA. Jina HIJA limetumika au Kutajika katika Kuruani mara 7 tu. Lakini kuna mara moja tu Limetajika kama Kitendo kwa hiyo Jumla ni Mara 8. Lakini kama Jina “Noun” ni mara 7 tu. Hii inalingana na Huko Mecca Mahujaji wanazunguka Kaaba Mara 7 tu ambayo ni sawa sawa na Kutajika kwa Neno “AL-HAJ” katika Kuruani Tukufu. Sasa Utashangaa zaidi Nikikuambia Kwamba Sura Ya “Al-Haj” ni Ya 22. Hebu angalia Maajabu. Mahujaji wanazunguka Kaaba Mara 7 yaani Kwa Duara au Mduara. Hebu tugawe Namba Ya Sura na Mizunguko hii 7

22 kugawa na 7 utapata jawabu ni 3.14!!!! Yaani Tunapata Ile Namba Pi. Yaani Kuruani inatupa Elimu ya Kisasa kwa njia Ya kiajabu sana. Namba Hii ambayo inatumika katika Kutafutia Maeneno na Miduara ipo katika Kuruani kwa njia ya Muujiza. Allahu Akbar. Hebu fikiri Duara la Kaaba na Mara 7 mizunguko Ya Mahujaji na Namba Ya Sura ni 22. Ukigawa unapata Namba Pi ya Kitaalamu. Uhusiano wa kiajabu sana. Duara ni CIRCLE na namba hii 3.14 ni Ratio ya mzunguko wa Mduara katika Kipenyo (Diameter) yake. Kwa maelezo zaidi soma Namba Pi hapa chini. Allahu Akbar.


(Pi (Greek letter “π”) is the symbol used in mathematics to represent a constant —the ratio of the circumference of a circle to its diameter— which is approximately 3.14159. It is the ratio of a circle’s circumference to its diameter.

To calculate the value of π, the pi formula is used, which is:π = (Circumference/ Diameter)Or, π = 3.14159 = 22/7.

What is pi used for? In basic mathematics, pi is usedto find the area and circumference of a circle. Pi can be used to find an area by multiplying the radius of the circle squared times pi.)

MAAJABU YA IDADI ZA HERUFI KULINGANA NA IDADI ZA AYA ZA KURUANI TUKUFU

Idadi ya Aya za Kuruani ni 6236 na ukihesabu herufi zote kuanzia mwanzo wa Kuruani mpaka ikifikia Herufi ya 6236 utafikia katika Neno الْكِتَٰبَ “KITABU” katika Aya ifuatayo: Sura Namba 2 Ya Al-Bakarah Aya Namba 87


وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى الْكِتَٰبَ وَقَفَّيْنَا مِن بَعْدِهِ بِالرُّسُلِ وَءَاتَيْنَا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ الْبَيِّنَٰتِ وَأَيَّدْنَٰهُ بِرُوحِ الْقُدُسِ أَفَكُلَّمَا جَاءَكُمْ رَسُولٌ بِمَا لَا تَهْوَىٰ أَنفُسُكُمُ اسْتَكْبَرْتُمْ فَفَرِيقًا كَذَّبْتُمْ

وَفَرِيقًا تَقْتُلُونَ

TRANSLATION

We gave Moses the Book and followed him up with a succession of messengers; We gave Jesus the son of Mary Clear (Signs) and strengthened him with the holy spirit. Is it that whenever there comes to you a messenger with what ye yourselves desire not, ye are puffed up with pride?- Some ye called impostors, and others ye slay!


Kuruani imekusanya Aya zenye idadi ya Herufi 326159

Hebu fikiri Mpangilio huu wa kiajabu. Allahu Akbar. Yaani Herufi zimepangwa kihesabu. Unapohesabu Herufi kuanzia mwanzo wa kuruani mpaka Unapofikia Herufi namba 6236 ambayo idadi hii ni sawa sawa na idadi ya Jumla Ya Aya za kuruani ambazo ni 6236 pia basi utajikuta upo katika Aya namba 87 ya Sura Namba 2 na neno la 6236 ni KITABU yaani “Kuruani” je unaona Muashirio? Inaashiria kwamba Namba hii 6236 ni idadi ya Aya za Kuruani. Je unaona Maajabu ya Mpangilio wa Kimuujiza? Allahu Akbar. Mtume Hakujua Hesabu hizi ambazo leo hii tunazipata kwa Ufundi wa kutumia Program mbalimbali za Computer kama vile Excel na Nyinginezo ambazo ni za kisasa. Sasa Je Mtume alijua vipi Hesabu hizi na akapanga herufi hizi kwa njia ya ufundi wa hali ya juu kama unavyoona. Hii Ni mojawapo wa Mamilioni na Mamilioni ya Miujiza mbalimbali iliyopo katika Kuruani Tukufu.