UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MAISHA YA MTUME MOHAMAD
Mwenyeezi Mungu akipenda katika mlango huu nitazungumzia kwa ufupi Maisha Ya Mtume Mohamad ﷺ Kuanzia Kuzaliwa mpaka Kufariki.
Haiwezekani Kuelezea Biography (Maisha au Sira) ya mtu yeyote aliyeishi muda wa miaka 63 katika Mlango wa Mtandao (Website) mdogo kama huu lakini kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu nitajitahidi kufupisha na Kutaja kila tukio lililo muhimu katika kipindi cha maisha yake.
Na ili tuelewe maisha ya Mtume Mohamad ﷺ kwa vizuri zaidi itabidi nielezee kwa ufupi Mji Wa Mecca na mazingara yake katika wakati huo, Kaabah, Ibada za Masanamu, Sababu zilizofanya kwa Kisima cha maji ya Zam Zam kugunduliwa na kuchimbuliwa, Miujiza iliyohusiana na Kuja kwa Mtume ﷺ, Habari zinazohusu Ukoo na Familia yake, Wake na watoto wake, Sifa Zake, Miujiza Aliyoitenda Mtume Mohamad ﷺ, Utabiri mbalimbali wa Wa mtume ﷺ Watu wa Mecca katika wakati huo na Imani zao, Dini waliozoamini na kufuata, Kushushiwa Uhai (Revelation) alipokuwa katika Pango la Hiraa, Mateso waliyoyapata Waumini wa Kwanza hapo Mecca, Wakimbizi Waumini wa Kidini wa kwanza Kuelekea Ethiopia, Kuhajiri Kwa Mtume ﷺ, Kwenda Madinna na Kujenga Taifa la Waumini, Kurudi Kwa Mtume ﷺ Mecca na Wapiganaji Elfu Kumi, Kuikomboa na Kuiteka Mecca na Miji Ya Karibu, Hotuba Ya Mwisho, Kufariki Kwa Mtume.ﷺ Haya ndiyo machache ninayotarajia kuyaelezea kwa ufupi katika Mlango huu.
Kwa hiyo nitajitahidi kuelezea kwa njia ya miaka kama nilivyofanya katika mlango wa “Historia Ya Uislamu” Kwa kutaja kila yaliyo muhimu na kujiepusha na yale ambayo nimeshaelezea katika Historia Ya Kiislamu.
Kuna wakati mwingine Nitapunguza, Nitazidisha na Nitageuza Vidondoo nilivyovitaja hapa juu ili Sira iwe katika mpangilio mzuri na kukubaliana na Ushahidi wa Kuruani na Sunnah za Mtume ﷺ.