SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Makala/Fedha & Benki

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

Alhamdulilah leo ni Jumamosi Tarehe 03/09/2022.  Nashukuru Mwenyeezi Mungu kwa kutupa Uhai na Afya ya kuweza kuandika machache ambayo lengo ni  Kumtukuza na Kufuata anayotaka yeye na siyo tunayotaka sisi.

Kwa furaha na hamu kubwa leo hii ninapendelea kutumia kila Dakika na Sekunde katika kuandika Makala hii.

Ninashika Kalamu na kuanza  Kuandika Yafuatayo:

Watalamu wa hali ya hewa wanasema kwamba leo kutakuwa na Mvua lakini katika wakati huu wa Saa Tano Asubuhi naona bado Jua Limechomoza na Ni Zuri Mno na kwa hiyo Huenda Wataalamu hao wamepotea na hakutakuwa na mvua. Kwa kweli Wataalamu  ni Hodari wa kukisia lakini si hodari wa kusababisha. Mwenyeezi Mungu peke yake ndiye anayejua Kushuka kwa mvua kwani yeye ndiye anayepeleka Mawingu sehemu atakazo mvua ishuke. Na Kuruani Imethibitisha Hayo.

Katika Mlango huu nitagusia Habari ya Fedha na Mabenki ili  kukumbushana Maamrisho ya kuruani kuhusiana na Riba.

Jina la Website hii ni  UISLAMUNASAYANSI  na  Kwa hiyo  pia Tunaweza kusema kwamba  Tutakachozumzia hapa ni  Sayansi ya Harakati za Mabenki na Mizunguko ya Fedha.

Katika  Kiingereza na Kiarabu  tunaweza pia kusema ni

Islamic banking, Islamic finance (Arabic: مصرفية إسلامية), or Sharia-compliant finance.

Uislamu  haukubakiza Elimu yeyote inayohusiana na Maisha. Kila Chenye Uhusiano na Maisha kimefundishwa na Kuruani na Pia Kufafanuliwa na Hadithi a Mtume Mohamad.ﷺ

Uislamu unatufundisha uhusiano  wa Binaadamu katika mishughuliko ya Biashara, Mizunguko ya Fedha baina ya  Binaadamu kwa njia ya Halali.Kuruani na hadithi za Mtume Mohamad zimekuja na Misingi ya Maingiliano ya binaadamu katika Harakati za Maisha ya kila siku.

Uislamu haukuachia watu wauziane vitu bila mpango wowote, au kukopeshana bila ya mpango wowote bali kuna sheria ambazo lazima kuzifuata.

Kwa mfano Ukiuza kitu chochote basi uhakikishe  kumfahamisha anayenunua sifa zote za kile unachokiuza. Usiuze kitu kwa kukisifia kwamba kizuri sana lakini umeficha mengineyo. Kwa mfano siuze Gari ukalisifia kwamba ni zuri sana lakini kuna Tatizo lingine ambalo umelificha. Kwa kifupi usidanganye. Mfano mwingine mzuri usiuze Maziwa na huku umechanganya na maji na hali kwamba mnunuzi hajui uliyoficha. Ndugu Waislamu  tuwe macho sana jambo hili kwani ni aina Ya Wizi mbaya. Katika Maingiliano ya kibiashara lazima Tuwe wakweli na Riziki itakayopatikana inakuwa na Baraka. Tusile vya haramu kwani Vinaleta Maradhi.

Ndugu  Waislamu wamezungumzia Elimu hizi  kwa muda mrefu. Majadiliano na Mabishano mengi yamefanyika kuhusu RIBA.  Tatizo kubwa ni Tafsiri ya neno RIBA.  Waislamu wengi  Waliosomea Elimu hizi za Fedha wamekubaliana kwamba neno RIBA ni  INTEREST na kwa hiyo  yaliyokatazwa katika Kuruani ni  INTEREST  yaani hii ndiyo  RIBA.

Kwa lugha Rahisi  imekatazwa na kuharimishwa kukopesha au kukopeshwa Fedha  kwa njia ya RIBA. Hebi nitoe  mfano  hapa Chini ili  RIBA  ieleweke vizuri.

MFANYA BIASHARA=HABARI BWANA

BENKI=NZURI

MFANYA BIASHARA=NATAKA MKOPO WA FEDHA

BENKI=HAKUNA TATIZO JE KIASI GANI?

MFANYA BIASHARA=LAKI  36

BENKI=HAKUNA TATIZO. WEWE NI MTU MUAMINIFU NA UNAJULIKANA  NA KWA HIYO HAKUNA TATIZO TUTAKUPA

MFANYA BIASHARA=ASANTE SANA BWANA

BENKI=UNGEPENDELEA KULIPA DENI HILI KWA MUDA GANI?

MFANYA BIASHARA=IKIWEZEAKANA MIAKA MITATU

BENKI= SAFI. SASA TUFANYE HISABU.

1/KWANZA KUNA INTEREST YA ASILIMIA 2 YA HIZO  LAKI 36 KWA HIYO  INTEREST ITAKUWA SHILINGI ELFU  72 KILA MWEZI.

2/NA CAPITAL YA PESA UNAZOKOPA NI MALIPO YALAKI MOJA KILA MWEZI

3/KWA HIYO  UTALIPA  KILA MWEZI NI LAKI MOJA NA ELFU  72

KWA HIYO  LAKI MOJA NI  DENI NA ELFU 72 NI INTEREST YAANI GHARAMA YA MKOPO WAKO. JE UNAKUBALI?

MFANYA BIASHARA=ASANTE SANA BWANA. KWA KWELI SINA BUDI  BALI KUCHUKUA KWANI NINA SHIDA NA NINAHITAJI SANA FEDHA.

BENKI=KWA HIYO  NDUGU  MWISHO  WA MWAKA WA TATU DENI LAKO LITAKUWA LIMEKWISHA NA WEWE UTAKUWA UMELIPA JUMLA YA FEDHA NI LAKI 61 NA ELFU 92  JE MAMBO  SAFI

MFANYA BIASHARA=SAFI SANA BWANA. 

BENKI=LAKINI KUNA MASHARTI. LAZIMA ULIPE KILA MWEZI KWANI USIPOLIPA BASI UNAWEZA KUNYANGANYWA BIASHARA AU NYUMBA YAKO AU CHOCHOTE KILE KISHA KIUZWE NA ITUMIKA KATIKA KULIPA DENI LETU.

MFANYA  BIASHARA=NIMEFAHAMU. ASANTE SANA HAYO YOTE NINAYAELEWA.

——————–

Kama tulivyoona INTEREST hapa juu ilivyokuwa kubwa. Yaani mkopaji anataka laki  36  na baada ya miaka Mitatu atakuwa amelilipia deni hilo Asilimia 2 ya pesa hizo yaani  2%  ya Laki  36  na jumla atakuwa amelilipa deni hilo na gharama zake zote ni  Laki 61 na  Elfu 92

yaani  RIBA  ambayo  inajulikana kama Interest ni  karibu nusu ya Deni hili. Mfanya Biashara amekopa Laki  36  na atalilipa deni hili mara mbili yake.  Hebu fikiri kidogo. 

Mfanyi biashara amekopeshwa pesa na anapofeli kulilipa basi atanyang’anywa alichonacho kama vile biashara yake au nyumba au cochote  alichonacho na kisha alipie gharama hizo.kwa kweli hii  hatari kubwa. Yaani hakuna ubinaadamu wowote. Benki haiangalii matatizo yako kama umepata faida au hasara katika biashara yako na kwa hiyo kutaweza kulipa deni hilo bali Benki wanataka deni lao na faida tu yaani hakuna ubinaadamu au udugu au huruma yeyote. Yaani  Benki haiangalii yaliyokupata katika Biashara yako bali  wanaangalia fedha zao tu. 

Sasa  umeona  Hatari za RIBA  au Interest  na ndiyo maana Mwenyeezi Mungu akakataza RIBA ili kumsaidia Kiumbe chake. Imeharimishwa kabisa hakuna utani na mwenyeezi Mungu  amesisitiza kwamba atampiga vita yule atakayechukua RIBA.

Wataalamu wa Kiislamu wamekuja na Mbinu mbalimbali ili kujiepusha na Bidhaa za Mabenki duniani. Wametafuta mbinu ili  Mabenki pia washiriki katika Hasara.  Yaani Mkopaji na Mkopeshaji washiriki katika  Heri na Shari au katika Faida na Hasara. Na hii inajulikana katika Elimu ya Fedha kama  “Profit and Loss Sharing”.

Huu  Mfano  wa Mazungumzo baina ya Mfanya Biashara na Benki pia katika Manunuzi ya Kila kitu. Kwa mfano  Ukinunua Gari na Kulipa hapo hapo bila ya Deni inakuwa hakuna Tatizo kwani umenuua kaka kawaida na umelilipia Bila ya Kuongeza Riba yeyote lakini ukilipia kidogo kidogo yaani  Installements kila mwenzi kwa muda mtakaowafikiana basi kutakuwa na RIBA  kwani Muuzaji anakuwa amekukopesha na Anaongeza gharama za Interest katika Bei ya gari hilo. Ukishindwa kulilipia Gari hilo basi litataifishwa na Muuzaji.  Ukinunua Gari kwa mkopo basi utalilipia zaid ya Bei ya gari hilo. Kama ni Milioni  10 basi mwisho  wa Installement utakuwa umelilipia Milioni 15. MIlioni 5 hapa ni  RIBA. kwa hiyo tuwe macho sana katika Maisha na tusione kwamba mambo haya ni mazuri.

Kama tulivyosema kuna mbinu  mbalimbali za kutatua tatizo hili. Kuna Benki mbalimbali za Kiislamu na hata ambazo siyo za Kiislamu hivi sasa wameanza kujiepusha na RIBA  ili kuwavutia Waislamu na pia wameona Ukweli kwamba RIBA siyo kitu kizuri na hivyo hata wasiokuwa waislamu wanapendelea  kujiepusha na RIBA. 

Hebu  nitoe mfano  wa Benki ya Kiislamu na Mnunuzi  ili tupate  kufahamishana vizuri.

MNUNUZI=Habari Bwana

MUUZAJI AU BENKI YAKIISLAMU=Nzuri. Karibu

MNUNUZI=Ningependelea kununua Gari lakini  sina Fedha za kutosha. Nimekuja kuwaomba mnisaidie  Mkopo  wa milioni  36

MUUZAJI AU BENKI YAKIISLAMU=Hakuna Tatizo. Benki  yetu inafuata Sheria Ya Kiislamu na kwa hiyo tunajiepusha na RIBA.  Na ili  tuweze kukusaidia sisi pia tuna Gharama zetu. kwa hiyo  Tutanunua Gari lako na kisha tutakuuzia kwa kukukodishia wewe kwa Milioni 38 yaani  Milioni mbili ni faida yetu na ndiyo itatuwezesha kulipa Gharama zetu pia.Tutakukodishia ulipe kidogo kidogo kufuatana na muda ambao tutakubaliana baina yetu. Je unakubali  Biashara hii? Yaani  Sisi tutanunua  Gari hilo kutoka katika Kiwanda na kisha Tutakuuzia kwa Kukukodishia  kwa faida. Na kisha  Utatulipa Kwa muda tutakaokubaliana baina yetu na wewe. Na siku utakapomaliza Deni basi Gari litakuwa lako. Yaani Wewe utakuwa Mnunuzi na Sisi Wauzaji. Angalia Bwana. Tunafanya hivi ili kujiepusha na RIBA  yaani Interest. Kama ukilinganisha na Mabenki yasiyokuwa ya Kiislamu utaona Watakukopesha na kisha Wataongeza Asilimia Ya Pesa katika Mkopo wako.

Sisi tutakuwa Wauzaji na kwa hiyo ukiwa na Tatizo kulipa deni tutatafuta Njia ya Usalama kwani tunajua Maisha yalivyo. Ukitaka kulilipa lote au baadaye au kila mwezi basi tunaweza tukapanga baina yetu, Tupange ili wewe na sisi tusiwe katika tatizo. Ukipata  Hasara au Faida basi ni sisi sote na siyo  wewe tu au sisi tu pekee. Je umefahamu

MNUNUZI=Ahsante sana. Sasa je Mpangilio huu au  System hii inaitwa kwa jina gani?

BENKI YA KIISLAMU=Inaitwa  “IJARAH  Hii ni mbinu moya ya kujiepusha na RIBA kwani  Tumeamrishwa katika Dini ya kiislamu (Kuruani na Hadithi za Mtume) tujiepushe na RIBA lakini  Biashara ni Halali na ndiyo maana hatuongezi Gharama zetu kwa njia ya RIBA Yaani Interest bali tunakuuzia kwa Faida ili tupate faida sote wewe upate Gari na sisi tupate hizo Milioni   Mbili. Na iwapo Gari lako limeharibika lenyewe bila ya kosa lako basi wakati ule bado lipo katika matengenezo hutatakiwa ulipe malipo yoyote. Na ikiwa una matatizo Mengineyo na huwezi kulipa Deni lako kwa muda maalum kama tulivyoahidiana  basi utasamehewa wakati huo mpaka upate fedha na kisha ulipe lakini kuna masharti ambayo tutakufahamisha.

Je umefahamu?

MNUNUZI= Ahasante  sana nimefahamu. Kwa kweli kuna Misamiati mingi ambayo inatatanisha. MURABAHA, MUSHARAKAH  AU MUDARABAH. NA mingineyo chungu  nzima.

BENKI YA KIISLAMU=Ndugu kwa kweli  Kuruani imeshusha Aya Chache zenye kutukataza tusichukue au kulipa  RIBA na pia kuna Hadithi  za Mtume  pia Chache lakini karne hii ya leo imekuja na mambo mbalimbali ambayo hayakuweko wakati huo wa Mtume na kwa hiyo  Waislamu  wamejitahidi kuja na Mbinu mbali mbali za kujiepusha na RIBA  na ndiyo maana Misamiati imekuwa mingi. MIsamiati au Mbinu hizi  hazikuweko wakati wa Mtume bali  imeundwa hivi karibuni.

MNUNUZI=Kwa nini Waislamu wameunda na kuja na mambo mapya ambayo hayakuwako wakati huo. kwa kweli  Tunababaika

BENKI YA KIISLAMU-=Usibabaike Ndugu. Maendeleo ya kileo yamesababisha Wanavyuoni wa Kiislamu kuja na Mbinu mbalimbali ili Sheria za Kuruani  zifuatwe. Usibabaike na Misamiati. Sheria Ni Moja nayo ni kujiepusha na RIBA na Pia kuna aina za RIBA  mbalimbali. Hadithi  za Mtume  zimeelezea vizuri  sana Tofauti  zote hizi.  na pia Biashara na Maingiliano ya Binaadamu na Fedha zimesababisha Kuweko kwa MISAMIATI  mbalimbali ili tupate kuelewa tofauti ya Vipengele vya Elimu hii. kwa hiyo  usibabaike. Mabenki yamekuja na bidhaa au  Mikopo pia ya aina mbalimbali na kwa hiyo  Wataalamu wa Kiislamu wamekuja na Elimu mbalimbali zenye MISAMIATI  mbalimbali ili kuwianisha na Bidhaa au Mikopo ya aina hizo. Kwa hiyo ukitaka kununua Bidhaa yeyote ambayo ipo katika Njia ya RIBA  basi  ujue kwamba Wanavyuoni Waislamu  wameshatafuta Alternative au Bidhaa Ya kiislamu isiyo na RIBA na ambayo ingependelea ununue Bidhaa hiyo kwa njia ya Kiislamu yaani ujiepushe na ile ya RIBA na usije  ukasema nimenunua bidhaa hii yenye RIBA kwa sababu Waislamu hawana au bado  hawana.

MNUNUZI=Ahsane sana bwana kwa maelezo na msaada wako mzuri. Mwenyeezi Mungu akubariki.

BENKI YA KIISLAMU=Amin

Katika Mfano nilioutoa hapa juu ni Mkopo wa Kununua Kitu  unachohitaji kama vile  Gari.  Kuna Mikopo ya aina Nyingi.  Kwa mfano Ukitaka Pesa kwa mahitaji ya haraka kama vile unaumwa na unataka pesa ili umlipe dakitari au chochote kile basi Benki ya kiislamu pia wanafuata Sheria ya kiislamu katika kukukopesha. Utakopeshwa lakini hutatakiwa kulipa  RIBA yoyote.

Katika Benki  isiyokuwa ya Kiislamu pia wanakopesha lakini wanahitaji ulipe RIBA  yaani Interest. kwa mfano ukihitaji Laki 5  basi kwa muda mtakaowafikiana kulipa itabidi uongeze pesa  za Interest juu ya hizo laki 5 yaani mwishowe utakapomaliza deni utakuwa umelipa zaidi ya laki 5.

Benki ya kiislamu  hawataki ulipe  ziyada yeyote lakini lazima uweke Rehani ambayo utakaposhindwa kulipa deni lako na baada ya kupewa muda wa kuhurumiwa kwisha basi watakujuulisha kwamba hakuna budi isipokuwa watauza Rehani uliyoweka na kisha watachukukua deni la Benki na wewe utapewa masalia  yaani kitakachobaki.  Kwa hiyo kuna Utu katika maingiliano baina ya mkopaji na Benki ya kiislamu. Kuna Huruma na kukusaidia bila ya malipo yeyote. Lakini uwe macho kwani ukishindwa kulipa deni lako basi unaweza kupoteza Rehani yako pia.

Mikopo  ipo mbalimbali. Ukitaka mkopo wa kununua nyumba pia Benki ya kiislamu inaweza kukupa mkopo unaojulikana kama  Musharaka Al-Mutanaqisa au kwa kiingereza inajulikana kama DIMINISHING MUSHARAKA na aina hii pia ina maelewano baina ya mkopa na mkopwa. Watashirikiana kununua nyumba. Kwa mfano  Mnunuzi atatoa aslimia  30  na Benki ya kiislamu itatoa asilimia  zilizobakia yaani   70 na kisha baada ya hapo mnunuzi  ataendelea kuilipa Benki Installements (Gharama za Kodi + Gharama za Kununua hiyo Asilimia 70) kwa muda  watakayowafikiana bila ya Benki kuongeza  RIBA  na baada ya muda kwisha Nyumba itakuwa ya mnunuzi.

Wataalamu wa kiislamu wametafuta mbinu mbalimbali katika kutatua  Tatizo la RIBA  katika  Mataifa ya kileo na Uchumi  wa kisasa. Yaani  Uislamu unakwenda na wakati. Hakuna Tatizo. Uislamu ni dini Dynamic  yaani yenye  Uhai. Dini hii  Inakubaliana na Mazingara na Wakati wowote  Tangu  karne ya 7, Kuja kwa Uislamu  mpaka Mwisho  wa Dunia. 

AYA  ZA KURUANI NA HADITHI  ZA MTUME MOHAMAD ZINAZOHUSU RIBA

Jumapili Tarehe 04/09/2022. Alhamdulilah leo nitaendelea na kazi niliyoianza jana. Je tutafika huko? Sijui kwani kuna mengi na siyo rahisi. Hebu nijaribu…..

Sasa  Nitakusanya hapa  chini Aya za Kuruani na hadithi  za Mtume na  Tafsiri zake na Kisha  tutaekdelea na Sherehe kuhusiana na Elimu hii  ambayo ni Kubwa.

Mwenyeezi Mungu anaelewa kwamba binaadamu anapenda  Mali na kwa hiyo Aya zilizoshuka kukataza RIBA zilishushwa kwa hekima kubwa yaani  kukatazwa kidogo kidogo. Hatua kwa hatua. Hazikushushwa Mara Moja bali  Step By Step.  Kwani watu wakati huo  walizama katika biashara hii na walijitajirisha kwa njia hii. Siyo  Rahisi  kumuamrisha mtu aache kitu haraka haraka na ndiyo maana Ilikuwa Step By Step. Aya za mwanzo hazikuwa na Maamrisho makali ya kukataza RIBA baadaye Kila Aya ifuatayo ilikuwa ikihimiza kwa nguvu zaid  Kujiepusha na RIBA na ukiangalia Aya ya mwisho utaona Amrisho ni Kali zaidi. Katika Aya ya mwisho Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Yeye mwenyewe atampiga Vita mwenye kujishirikisha na RIBA.

1/Sura Namba 30  Aya Namba 39

وَمَآ ءَاتَيۡتُم مِّن رِّبً۬ا لِّيَرۡبُوَاْ فِىٓ أَمۡوَٲلِ ٱلنَّاسِ فَلَا يَرۡبُواْ عِندَ ٱللَّهِ‌ۖ وَمَآ ءَاتَيۡتُم مِّن زَكَوٰةٍ۬ تُرِيدُونَ وَجۡهَ ٱللَّهِ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلۡمُضۡعِفُونَ (٣٩)

TAFSIRI

39.Na zile (pesa za kukopeshea) riba mtoazo (katika kuwakopesha watu) ili zizidi katika mali ya watu, mbele ya Mwenyezi Mungu hazizidi (pesa hizo; bali zinaingia nuhusi na shakawa); lakini (mali). mnayoyatoa kwa ajili ya Zaka kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi hao (wenye kufanya haya) ndio wazidishao (mali zao).

2/Sura Namba 4 Aya  Namba 161

وَأَخۡذِهِمُ ٱلرِّبَوٰاْ وَقَدۡ نُہُواْ عَنۡهُ وَأَكۡلِهِمۡ أَمۡوَٲلَ ٱلنَّاسِ بِٱلۡبَـٰطِلِ‌ۚ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَـٰفِرِينَ مِنۡہُمۡ عَذَابًا أَلِيمً۬ا (١٦١)

TAFSIRI

16 Na kwa (sababu ya) kula kwao riba, na hali wamekatazwa wasile, na (kadhalika) kwa kula kwao mali za watu kwa batili. Basi tumewaandalia makafiri-nao ndio wao–adhabu iumizayo.

3/Sura Namba 3  Aya Namba 130-132

3/يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡڪُلُواْ ٱلرِّبَوٰٓاْ أَضۡعَـٰفً۬ا مُّضَـٰعَفَةً۬‌ۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ (١٣٠) وَٱتَّقُواْ ٱلنَّارَ ٱلَّتِىٓ أُعِدَّتۡ لِلۡكَـٰفِرِينَ (١٣١) وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ لَعَلَّڪُمۡ تُرۡحَمُونَ (١٣٢) 

TAFSIRI

130. Enyi mlioamini! Msile riba, mkizidishazidisha; na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kutengenekewa.

131. Na ogopeni moto ambao umewekewa wenye kukanusha amri za Mwenyezi Mungu. (Na katika hizo ni huku kutokula riba).

132.Na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume ili mpate kurehemewa

4/Sura Namba 2 Aya Namba 275-281

ٱلَّذِينَ يَأۡڪُلُونَ ٱلرِّبَوٰاْ لَا يَقُومُونَ إِلَّا كَمَا يَقُومُ ٱلَّذِى يَتَخَبَّطُهُ ٱلشَّيۡطَـٰنُ مِنَ ٱلۡمَسِّ‌ۚ ذَٲلِكَ بِأَنَّهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّمَا ٱلۡبَيۡعُ مِثۡلُ ٱلرِّبَوٰاْ‌ۗ وَأَحَلَّ ٱللَّهُ ٱلۡبَيۡعَ وَحَرَّمَ ٱلرِّبَوٰاْ‌ۚ فَمَن جَآءَهُ ۥ مَوۡعِظَةٌ۬ مِّن رَّبِّهِۦ فَٱنتَهَىٰ فَلَهُ ۥ مَا سَلَفَ وَأَمۡرُهُ ۥۤ إِلَى ٱللَّهِ‌ۖ وَمَنۡ عَادَ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ أَصۡحَـٰبُ ٱلنَّارِ‌ۖ هُمۡ فِيہَا خَـٰلِدُونَ (٢٧٥) يَمۡحَقُ ٱللَّهُ ٱلرِّبَوٰاْ وَيُرۡبِى ٱلصَّدَقَـٰتِ‌ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ (٢٧٦) إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُاْ ٱلزَّڪَوٰةَ لَهُمۡ أَجۡرُهُمۡ عِندَ رَبِّهِمۡ وَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ (٢٧٧) يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَذَرُواْ مَا بَقِىَ مِنَ ٱلرِّبَوٰٓاْ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ (٢٧٨) فَإِن لَّمۡ تَفۡعَلُواْ فَأۡذَنُواْ بِحَرۡبٍ۬ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ‌ۖ وَإِن تُبۡتُمۡ فَلَڪُمۡ رُءُوسُ أَمۡوَٲلِڪُمۡ لَا تَظۡلِمُونَ وَلَا تُظۡلَمُونَ (٢٧٩) وَإِن كَانَ ذُو عُسۡرَةٍ۬ فَنَظِرَةٌ إِلَىٰ مَيۡسَرَةٍ۬‌ۚ وَأَن تَصَدَّقُواْ خَيۡرٌ۬ لَّڪُمۡ‌ۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ (٢٨٠) وَٱتَّقُواْ يَوۡمً۬ا تُرۡجَعُونَ فِيهِ إِلَى ٱللَّهِ‌ۖ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفۡسٍ۬ مَّا ڪَسَبَتۡ وَهُمۡ لَا يُظۡلَمُونَ (٢٨١)

TAFSIRI

275.Wale wanaokula riba, hawasimami (kuendesha yao) ila kama anavyosimama yule ambaye Shetani kamzuga kwa kumsawaa; (wako mbioni tu, hawana kituo). (Na) haya ni kwa sababu wamesema, “Biashara ni kama Riba”, bali Mwenyezi Mungu · ameihalalisha biashara na kaiharimisha riba. Na aliyefikiwa na mauidha kutoka kwa Mola wake (ya huku kukatazwa riba), kisha akajizuia, basi yamekwisha mthibitikia yale (mali) yaliyopita (aliyokwisha yapata); na hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wanaorejea (kula riba) basi hao ndio watu wa Motoni, humo watakaa milele.

276. Mwenyezi Mungu huyafutia (baraka mali ya) Riba: na huyatia baraka (mali yanayotolewa) sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila kafiri (na) afanyae dhambi.

277. Hakika wale walioamini na kufanya vitendo vizuri na kusimamisha Sala na kutoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola wao, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.

278. Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni yaliyobakia katika riba, ikiwa mmeamini.

279. Na kama hamtafanya (hivyo), basi fahamuni mtakuwa na vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkiwa mmetubu, basi mtapata rasilimali zenu; msidhulumu wala msidhulumiwe.

280. Na kama (mkopi) ana dhiki, basi (mdai) angoje mpaka afarijike. Na kama nyinyi (mnaodai mkizisamehe deni zenu) mkazifanya sadaka, basi ni bora kwenu. Ikiwa mnajua haya (basi fanyeni).

181. Na iogopeni Siku ambayo mtarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha viumbe wote watalipwa kwa ukamilifu yote waliyoyachuma; nao hawatadhulumiwa

SHEREHE

Kufuatana na Aya tulizozinukulu hapa juu utaona kwamba Riba imeharimishwa na Mwenyeezi Mungu ameahidi kumpiga vita mwenye kuchukua au kutoa Riba. Riba maana yake  Ziyada au Kukua. Ni tamaa ya Kujitajirisha  kwa njia hii ya Kutaka ziyada kutoka kwa Mhitaji. Ni Kinyume na Sadaka.  Sadaka ni kusaidia na huku unatarajia ujira kutoka kwa Mwenyeezi Mungu lakini  Riba ni kutarajia Malipo ya Mali peke yake. Mwenyeezi Mungu amepiga vita RIBA lakini amehimiza Biashara. Amemlaani Anayejishirikisha na Biashara kama hii. Kwa hiyo tuwe macho sana kwani kama Tulivyosoma Aya hapa juu Mwenyeezi Mungu ameamua Kumpiga Vita Mwenye Kujishirikisha na Riba. Je nani anaweza kupigana vita Na Muumba?

Biashara ni kununua na kuuza na kwa hiyo hii haina tatizo bali imehimizwa. Lakini RIBA haiwi hivyo bali unakopesha Pesa na kisha unasubiri  ulipwe ziyada. Pia Kuna aina za RIBA  ambazo nitazungumzia hapa chini kwa Msaada wa Hadithi za Mtume  Mohamad. ﷺ

Hadithi  Ifuatayo kutoka katika  Sahih Al-Bukhari Hadithi namba 2312  inazungumzia aina nyingine ya RIBA

حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ ـ هُوَ ابْنُ سَلاَّمٍ ـ عَنْ يَحْيَى، قَالَ سَمِعْتُ عُقْبَةَ بْنَ عَبْدِ الْغَافِرِ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ جَاءَ بِلاَلٌ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم بِتَمْرٍ بَرْنِيٍّ فَقَالَ لَهُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏”‏ مِنْ أَيْنَ هَذَا ‏”‏‏.‏ قَالَ بِلاَلٌ كَانَ عِنْدَنَا تَمْرٌ رَدِيٌّ، فَبِعْتُ مِنْهُ صَاعَيْنِ بِصَاعٍ، لِنُطْعِمَ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم فَقَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم عِنْدَ ذَلِكَ ‏”‏ أَوَّهْ أَوَّهْ عَيْنُ الرِّبَا عَيْنُ الرِّبَا، لاَ تَفْعَلْ، وَلَكِنْ إِذَا أَرَدْتَ أَنْ تَشْتَرِيَ فَبِعِ التَّمْرَ بِبَيْعٍ آخَرَ ثُمَّ اشْتَرِهِ ‏”‏‏.‏

TAFSIRI/TRANSLATION

Abu Sa`id al-Khudri alisema kwamba:

Once Bilal brought Barni (i.e. a kind of dates) to the Prophet (ﷺ) and the Prophet (ﷺ) asked him, “From where have you brought these?” Bilal replied, “I had some inferior type of dates and exchanged two Sas of it for one Sa of Barni dates in order to give it to the Prophet; to eat.” Thereupon the Prophet (ﷺ) said, “Beware! Beware! This is definitely Riba (usury)! This is definitely Riba (Usury)! Don’t do so, but if you want to buy (a superior kind of dates) sell the inferior dates for money and then buy the superior kind of dates with that money.”

SHEREHE

kwa hiyo hii ni aina nyingine ya Riba. hadithi inasema kwamba Kubadili  Tende (Kwa Wingi) za Hali ya Chini kwa tende (Kwa Uchache) za Thamani za hali ya Juu  haifai na ni aina ya RIBA  na kwa hiyo kwa njia iliyo sahihi  kwanza ni Kuuza tende iliyo na  thamani ndogo na kisha ununue kwa pesa ile iliyo na thamani kubwa.

Hadithi kutoka katika Sahih Al-Bukhariy Hadithi Namba 2174

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ مَالِكِ بْنِ أَوْسٍ، أَخْبَرَهُ أَنَّهُ الْتَمَسَ، صَرْفًا بِمِائَةِ دِينَارٍ، فَدَعَانِي طَلْحَةُ بْنُ عُبَيْدِ اللَّهِ فَتَرَاوَضْنَا، حَتَّى اصْطَرَفَ مِنِّي، فَأَخَذَ الذَّهَبَ يُقَلِّبُهَا فِي يَدِهِ، ثُمَّ قَالَ حَتَّى يَأْتِيَ خَازِنِي مِنَ الْغَابَةِ، وَعُمَرُ يَسْمَعُ ذَلِكَ، فَقَالَ وَاللَّهِ لاَ تُفَارِقُهُ حَتَّى تَأْخُذَ مِنْهُ، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏ الذَّهَبُ بِالذَّهَبِ رِبًا إِلاَّ هَاءَ وَهَاءَ، وَالْبُرُّ بِالْبُرِّ رِبًا إِلاَّ هَاءَ وَهَاءَ، وَالشَّعِيرُ بِالشَّعِيرِ رِبًا إِلاَّ هَاءَ وَهَاءَ، وَالتَّمْرُ بِالتَّمْرِ رِبًا إِلاَّ هَاءَ وَهَاءَ ‏”‏‏.‏

TAFSIRI/TRANSLATION

Narrated Ibn Shihab: that Malik bin Aus said, “I was in need of change for one-hundred Dinars. Talha bin ‘Ubaidullah called me and we discussed the matter, and he agreed to change (my Dinars). He took the gold pieces in his hands and fidgeted with them, and then said, “Wait till my storekeeper comes from the forest.” `Umar was listening to that and said, “By Allah! You should not separate from Talha till you get the money from him, for Allah’s Messenger (ﷺ) said, ‘The selling of gold for gold is Riba (usury) except if the exchange is from hand to hand and equal in amount, and similarly, the selling of wheat for wheat is Riba (usury) unless it is from hand to hand and equal in amount, and the selling of barley for barley is usury unless it is from hand to hand and equal in amount, and dates for dates, is usury unless it is from hand to hand and equal in amount”

SHEREHE

Tunasoma na kufahamu katika hadithi hii kwamba RIBA  siyo pesa tu peke yake bali hata Mazao pia. Yaani mtu anapokuja na Unga wa ngano  wa aina mojawapo na kutaka kubadilishana na Unga wa ngano wa aina nyingine basi Uislamu umeweka Sheria kwamba unaweza kufanya hivyo lakini iwe mkono kwa mkono yaani Biashara ya hapo kwa hapo na pia Uzito wa Unga wa ngano uwe sawa sawa. Usije ukafikiri kwamba Thamani ya Unga wa ngano wa aina moja ni kubwa kuliko nyingine na kwa hiyo mkibadilishana basi yenye Thamani kubwa Itskuwa na Uzito zaidi ya nyingine. Kwa mfano  Kilo  Moja kwa Kilo Mbili. Yaani  Kilo Moja ya Umga wa ngano wa thamani ya chini kwa kilo Moja ya Unga wa ngano wa Thamani ya juu. Hadithi  zimekataza haya ili kuepusha RIBA  tuliyozungumza hapo  juu. Kwa hiyo RIBA siyo katika Mikopo  tu peke yake bali katika Biashara pia.

Ili kuepusha  Dhuluma na kudanganyana katika Mabadilishano  (Barter) ya Mazao au chochote kile basi Tufate Tunayofundishwa katika Dini ya Kiislamu kama ilivyoamrishwa katika Kuruani na Hadithi za Mtume Mohamad.ﷺ

Kuna Hadithi za Mtume ﷺ mbalimbali zenye kufafanua aina za RIBA.

AINA ZA RIBA

Kuna aina mbili za Riba

1. Ya kwanza Inaitwa Riba An Nasiyah, Riba Al Jahiliya au Riba al Quran

Na hii ndiyo  tuliyozungumzia katika Mifano ya mazungumzo baina ya Mnunuzi na Bani hapa juu, Ni  Ziyada au Interest zinazoongezwa katika Mikopo. na hii ndiyo RIBA  iliyotajwa katika Kuruani Tukufu.

2. Ya Pili inaitwa Riba al Fadl, Riba an Naqd, Riba Al Bai.

au Riba al Hadeeth.

Riba Hii  imeelezewa na Hadithi za Mtume na ndiyo maana imeitwa pia RIBA  ya Hadeeth. na  kama tulivyosoma hadithi  hapa juu ni aina ya RIBA inayohusiana na Mazao na vinginevyo  kama vile  Dhahabu, Fedha au Chumvi

Mazao yaliyotajwa katika Hadithi ni kama vile Ngano, Tende  au Barley.

Wanavyuoni wamehitilafiana Kuhusu  aina Nyinginezo za Mazao na Pia katika Tafsiri  ya Aina za RIBA  na pia RIBA yenyewe.  Na kwa hiyo  siyo rahisi kufahamu kwa vizuri kwani kuna Hadithi mbalimbali za Mtume ﷺ ambazo  zimeelezea kwa urefu. na Pia kuna kauli mbali mbali za wanavyuoni.  Katika Mlango huu nitajitahidi kuelezea hadithi  hizo lakini itachukua muda. Inahitaji utafiti wa hali ya juu. Njia nitakayofuata ni ya katikati na kudakua dakua fikra za wanavyuoni huku na huko mpaka tupate picha iliyo  safi na kamili. Sijigambi kwamba mimi ni Profesa wa mambo ya Benki na Fedha lakini ni Mtafiti kama watafiti wengineo. Inshaallah Mwenyeezi Mungu akipenda nitafasiri kila Hadithi katika Hadithi za Mtume zinazohusu RIBA.

Uislamu haukubakiza kitu. Kila Uwanja katika Nyanja za Kidunia umeshaelezea kwa urefu. Alhamdulilahi Neema kubwa hii. Tuna kila Kitu kilichobaki ni Kusoma na Kufuata.

Elimu ya Biashara Ni Mlango mkubwa wa FIQH  “Jurispridence”  ya Kiislamu na katika Mlango huu tumegusia  Kipengele kimoja tu cha Mlango huu wa Business. Yaani  RIBA  peke yake.

Kwa hiyo  Mwenyeezi Mungu akipenda na kupata nafasi nitaendelea na Hadithi  za Mtume  hapa chini na pia Kuzifasiri. Kisha Nitaelezea  Faida gani tunapata kwa  Kujiepusha na Aina za RIBA  tulizozitaja hapa juu.

Hebu  tuendelee na Hadthi za Mtume. ﷺ

inaendelea……………………