UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
Alhamdulilah leo ni Ijumaa tarehe 02 September 2022. Ni siku kubwa ya Kiislamu na Kwa munasaba huu ningependelea kuanza Makala Mpya inayohusiana na Sayansi za Kidunia, Na Katika Sherehe hiyo Mwenyeezi Mungu akipenda nitakuwa Nikipeleka Darubini mara kwa mara katika Aya za Kuruani tukufu ambazo zina Uhusiano na Maelezo ya Sherehe hii.
MAKALA ZA SAYANSI KATIKA KARNE YA ISHIRINI
Hii ni Makala ya kwanza inayohusu uwanja wa Sayansi za karne ya 20.
Mwanzoni mwa karne ya 20 wanasayansi walikuwa na tumaini kubwa la maendeleo ya kisayansi katika nyanja za Sayansi Duniani na pia kujihisi na mafanikio makubwa.
Sayansi katika Karne ya 19 ilikuwa Haina Msimamo madhubuti bali Nadharia zilikuwa zikiyumba yumba.
Charles Darwin Na Richard Owen walikuja na Nadharia inayojulikana kama “Evolution” ambayo inaamini kwamba Kila kilichopo ulimwenguni kimezuka bila kuumbwa.
Mpaka leo bado Nadharia hii inafuatwa na baadhi ya watu na pia inafundishwa mashuleni. Kwa kweli Nadharia hii imekufa na imetupwa katika Madebe ya Takataka Ya Kihistoria.
Walioitupa ni Wanasayansi Na Wataalamu wa kileo ambao wamegundua Mengi yaliyo kweli.
Nadharia ya Evolution haisimami mbele ya Sayansi za kileo na Pia hazikubaliani na Dini ya Kiislamu. Mwenyeezi Mungu amekwisha tuambia katika Kuruani tukufu kwamba Yeye ndiye aliyeumba kila kitu hatua kwa hatua. Kwa hiyo Darwin na Timu yake walikosea sana waliposema kwamba Viumbe vimezuka hovyo hovyo Hatua Kwa Hatua.
Katika Wakati huo wa karne ya 19 Mtaalamu Charles Lyell Alielezea Muhtasari wa Historia ya Jiologia ya Ardhi. (Gelology).
Na Elimu ya Saikolojia (Psychology”) ilizuka na kuhesabiwa miongoni mwa Sayansi Mpya.
James Clerk Maxwell aligundua “Spectrum ya SumakuUmeme” au Electromagnetic Spectrum.
Haya ni Mawimbi (Waves) ya Nishati za Umeme katika Anga.
Vipimo vya urefu wa Mawimbi na Harakati zake ndiyo inayosababisha kuweko kwa aina mbalimbali ya Mwanga Angani kwa mfano
Kuna Mawimbi Marefu yenye Harakati ndogo ndogo na Mawimbi haya yanatumika kwa Radio na Yanajulikana kama Radio Spectrum.
Kuna Mawimbi Mafupi yenye Harakati kubwa sana na Haya yanatupa aina ya Mwanga unaojulikana kama Gamma Spectrum.
Baina Ya Mawimbi marefu na Mafupi kuna Mawimbi ya Urefu (size0mbalimbali na pia kuna aina mbalimbali ya Mianga.
X-Ray
Ultraviolet
Visible
Infrared
Microwave
Kila Aina ya Mianga au Spectrum hutumika kwa kazi maalum.
Kwa mfano Binaadamu tunatumia Visible Light ili kuona. X-Ray ni mwanga ambao unatumiwa Hospitalini. Microwave ni aina ya mwanga unotumiwa katika Majiko ya Umeme.Kuna wanyama ambao wanatumia mwanga wa Ultraviolet ili kuona.
Ukisoma Ulimwengu utamjua Mwenyeezi Mungu aliyeumba haya. Tunashangaa ya dunia lakini hatushangai Utukufu wa Mola.
Katika Karne ya 19 Louis Pasteur alituelezea Namna ya Vijidudu (Microbes) wanavyoweza kuleta Maradhi na aliweza kutengeneza Chanjo ziilizoleta faida kubwa na zikawa msingi wa Dawa za Ganzi (Anaesthetics) na Antiseptics na hizi ndizo zinazosaidia leo hii katika Kufanya Operesheni za Miili.
Wakati huo Mandeleev aliweza kuchapisha Periodic Table ya Elements au Jaduali ya Elements na kutuelezea Tabia za Chemicals.
Miaka ya mwisho wa karne ya 18 Kuligunduliwa Electron, Virusi, Antibodies, na Kuweza kutibu maradhi kama vile Diphtheria.
Namna ya Kutibu maradhi kama haya kwa kutumia ufundi wa mwanzo katika wakati huo unaonyesha mwanzo wa Muamko wa Sayansi katika karne hiyo.
Vijana ambao waliingia katika Mkondo wa Sayansi walikuwa wakijiuliza maswali mbalimbali. Walijiuliza watakachofanya na kipi kilichobaki cha Kugundua?
Binaadamu tunasahau kwamba Kuna mengi ambayo bado hatujui. Kuna wakayi mwingine tunafikiri kwamba tumekwisha maliza.
Kwa kweli tunajidanganya kwani Bado tupo mwanzo Ulimwengu bado hatuujui kabisa. Uvumbuzi bado haujaisha kwani kuna mengi bado hatuyajui.
Kuruani imekusanya ulimwengu wote bali malimwengu yote pia hivyo hivyo. Tunadhani Tumekwishamaliza Kuruani na kwa hiyo hakuna mengine mapya kwa kweli tunajidanganya.
Ndugu zangu Kuruani haina mwisho. Elimu yake haina mwisho. Kuna Miujiza isiyo na Mwisho.
Ikiwa Ulimwengu ni Kuruani Tunayoiona na Kuruani ni Ulimwengu tunaousoma Basi itakuaje Temekwisha maliza kuisoma kuruani?
Haiwezekani kabisa. Tunajidanganya. Miujiza katika kuruani haina mwisho kwani Elimu ya Mwenyeezi Mungu haina mwisho kama alivyosema katika Kuruani Tukufu kwamba angejaalia Mabahari yote kuwa Wino na kujaalia Miti yote kuwa kalamu basi Wino huo ungekwisha kabla ya maneno yake kwisha.
Nakumbuka Kuna siku Nilimpa Rafiki yangu asiyekuwa Muislamu Kuruani Tukufu iliyoandikwa kwa Tafsiri ya Kiingereza. Nilipokutana naye siku ya pili nilimwuliza je umenza kusoma Kuruni? Akanijibu kwamba ameishamaliza kusoma. Nilishangaa sana. Nikamwambia Umesoma Juu Juu kama Unavyosoma Gazeti. Na hivi ni kosa. Tusisome Kuruani kama Gazeti kwani Mwenyeezi Mungu amatuambia katika Kuruani Tunapoisoma lazima tuisome kwa utulivu na tufikiri. Usisome kama vile unasoma vitabu vya Hadithi za Porojo au Michezo za Kuigiza.
Usifanye hivyo kwani Unapoteza Faida kubwa. Unaposoma ingependelea Usome na Tafsiri kama vile Ya Sheikh Abdallah Farisi au ya kiingereza kama vile Yusuf Ali. Usome kisha ufikiri. Usiharakishe bali kidogo kidogo. Kuruani siyo Nyimbo. Usione utamu wa sauti tu bali Jitahidi ueleqwe maana yake na ikiwezekana Tuifuate.
katika Mwanzoni mwa karne ya 20 kulianza kuonekana juhudi kubwa za Wanasayansi wakubwa duniani na hasa katika Uwanja wa Physics. Mwana Sayansi Maarufu Einstein alikuja na Mapinduzi makubwa ya Kisayansi ambayo yaliwashagaza weataalamu Dunia nzima. Alikuja na Nadharia ambazo ziliwatingisha WanaSayansi wengineo kama vile Newton. Kwa mfano Einstein alisema kwamba Ulimwengu Ni Dynamic na siyo Static. Kwa hiyo Ukweli huo ulipingwa na Wasasaynasi wa wakati huo lakini hesabu za Einsein zilionyesha kwamba Ulimwengu hauna utulivu bali Dynamic na Upo katika Kutanuka. “Expansion of The Universe”. Wakati huo Wanasayansi kama vile Newton walikataa Ukweli huu kwani waliamini Ulimwengu umetulia “Static” na Kwa hiyo hakuna Expansion yeyote. Ajabu ni kwamba baada ya miaka michache iligundulikana kwamba Einstein alisema kweli na hakukosea. Bwana huyu alisikitika sana kwani aligeuza Hesabu zake ili kuwiana na Fikra hizo za makoza za kina Newton za wakati huo na akasema usemi maarufu uliorikodiwa “This is a blunder of my life”
Baada ya Juhudi zote hizo na baada ya miaka kupita tunakuta Ukweli huu katika kuruani Tukufu. Je uamini au usiamini Mwenyeezi Mungu anasema katika Kuruani kwamba “Tunatanua Mbingu” Allahu Akbar. Je unaona Maajabu? Mtume Mohamad alisoma wapi Elimu hii ambayo imechukua juhudi kubwa na wakati mrefu.
Ugunduzi huu mkubwa unatuthibitishia kwamba Kuruani ni maneno ya Ukweli. Kuruani inatoka Kwa Mwenyeezi Mungu bila ya shaka yeyote. Kuna wachache wasiojua chochote na ndiyo wenye kupinga. Na pia kuna wanafiki na waongo ambao watapinga tu na hata kama huu ndiyo ukweli. Huu ni uamuzi wao ambao unatokana na ujinga wao.
Wanasayansi pia walijitahidi katika mwanzo wa karne hii kusoma Ulimwengu wa Atom na kuja kwa Nadharia inayojulikana kama Quantum Theory nayo pia ilifanyiwa utafili.
Vita vya kwanza Duniani 1918 na Maradhi ya homa ya FLU duniani (Pandemic Flu) yalikuja na Kusababisha Maharibiko ya Juhudi za Kisayansi.
Lakini ukweli ni kwamba Miaka ya mwanzo ya Karne ya 20 yaani kabla ya Vita vya Dunia ilikuwa ni miaka ya Uvumbuzi Mzuri ambao ni mwanzo wa Maendeleo makubwa yaliofuata miaka ya baadaye.