UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
Alhamdulilah Namshukuru Mwenyeezi Mungu kuweza kuandika Makala/Fedha na Benki kama nilivyopanga. Kwa kweli sijaimaliza na itachukua muda lakini niliyoandika yanatosha kumpa msingi mtu yeyote.
Leo Ni Jumapili Jioni ya Tarehe 04/09/2022. Baada ya Kumaliza Kuandika Makala ya RIBA katika Mlango wa Fedha na Benki nimeona nisimame hapo kwani nilichoka kuendelea na Habari za Noti na Benki. Nimeona bora siku ya leo nigeuze Juhudi zilizobaki ziende katika Sayansi.
Ni Wakati wa Jioni ambao mzuri sana kwa kazi hii na hasa kazi ya Mwenyeezi Mungu. hakuna Lililo zuri kama Kuzungumza habari ya Kuruani ambayo ni Hotuba ya Muumba. Kwani mazungumzo ya kidunia yana Porojo nyingi na kwa hiyo nimekimbilia katika Kuruani ili kujiepusha na Porojo.
Makala hii itahusu mchanganyiko wa Elimu mbalimbali na kwa hiyo usibabaike kwani nitakuwa nikirekibisha Darubini Yangu katika kila kona, au kila Angle ya Kuruani na Viumbe vyake Mwenyeezi Mungu.
Katika Makala hii tutaanza kwa kuelekeza Darubini yetu katika Sura namba 75 Aya ya 26 mpaka 30
سُوۡرَةُ القِیَامَة كَلَّآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلتَّرَاقِىَ (٢٦) وَقِيلَ مَنۡۜ رَاقٍ۬ (٢٧) وَظَنَّ أَنَّهُ ٱلۡفِرَاقُ (٢٨) وَٱلۡتَفَّتِ ٱلسَّاقُ بِٱلسَّاقِ (٢٩) إِلَىٰ رَبِّكَ يَوۡمَٮِٕذٍ ٱلۡمَسَاقُ (٣٠)
Hebu kwanza Tufasiri Aya hizi kisha tushereheshe.
TAFSIRI
26.Sivyo (hivi mnavyofanya)!· (Roho) itakapoflkia katika mitulinga (mifupa ya mabega)
27. Na kukasemwa: “Ni nani wa kumzingua (na kumpoza mgonjwa huyu)?”
28. Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa hiyo ni (saa ya) kufariki (dunia)
29. Na utakapoambatanishwa muundi kwa muundi
30. Siku hiyo ni kucbungwa (tu). kupelekwa kwa Mola wako.
SHEREHE
Aya hizi zinatupa picha ya mtu anapofariki dunia. Kwa kweli inatisha. Yaani sisi wote tutayapata haya na siyo uwongo na hata Mitume pia walikutwa na Kifo na huu ndiyo mwisho wa kila kiumbe. Lengo la Kupeleka Darubini yangu katika Aya hizi ni neno ٱلتَّرَاقِىَ “ATARAQIY” lenye maana ya Mfupa wa Mabega. na kabla ya kilielezea neno hili kwanza ningependelea kuelezea Aya za mwisho wa Sura hii.
Inaishia na Aya zinazozungumzia asili ya Binaadamu kwanza alikuwa Tonye la Manii yaliyotoka kwa Nguvu, Kisha Kipande cha Nyama kinachonin’ginia katika Tumbo la uzazi la mama na baadaye akazaliwa na kuwa Kiumbe cha kike au kiume na Mwenyeezi Mungu anamalizia kusema kwamba Je anayefanya haya bila shaka yeyote ana uwezo wa kumpa kiumbe uhai tena baada ya kufariki dunia. Yaani ikiwa amekuumba kisha akakufisha basi pia atakufufua. Hebu tuone Tafsiri inavyosema hapa chini:
أَلَمۡ يَكُ نُطۡفَةً۬ مِّن مَّنِىٍّ۬ يُمۡنَىٰ (٣٧) ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً۬ فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ (٣٨) فَجَعَلَ مِنۡهُ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ (٣٩) أَلَيۡسَ ذَٲلِكَ بِقَـٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يُحۡـِۧىَ ٱلۡمَوۡتَىٰ (٤٠)
TAFSIRI
37.Je! Hakuwa tone Ia manii lilotonwa?
38. Kisha akawa kidonge cha damu, kisha akamuumba na akamsawazisha (mwanaadamu kamili)?
39· Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
40. Je! Hakuwa Huyo ni Muweza wa kuhuisha wafu?
SHEREHE
Hebu tufikiri. Aya hizi za mwishowa Sura hii zinazungumzia asili ya Binaadamu na kuzaliwa kwake.
Kwa kifupi hapo mwanzo wa Sura Hii Aya zimetaja Kifo na Mwisho wa Sura kuzaliwa.
Baada ya Kuzielezea Aya za Mwisho wa Sura hii Ningepnedelea kurudi Mwanzo wa Sura Hii.
Hebu tulichunguzae Neno ٱلتَّرَاقِىَ “ATARAQIY” lenye maana ya Mfupa wa Mabega.
Sayansi ya leo inatuthibitishia kwamba Mtoto anapokuwa katika Tumbo la mama mfupa wa kwanza kukua au kutokea ni huu wa mabega yaani ٱلتَّرَاقِىَ “ATARAQIY” na Mfupa wa mwisho kukua kwa binaadamu anapokamilika yaani Ujanani ni huu huu ٱلتَّرَاقِىَ “ATARAQIY”
hebu tujiulize swali. Je huu siyo Muujiza? hebu fikiri. Binaadamu ana mifupa 206 mwilini lakini huu ndiyo alioutaja katika Sura hii na ndiyo wa kwanza kukua katika tumbo la mama Na ndiyo huu huu alioutaja wakati Roho ya Binaadamu inapotoka na huu mfupa ndiyo wa mwisho kukua katika mwili wa binaadamu. Je unaona Ya kushangaza. Kuna maajabu makubwa katika Sura hii na nyinginezo pia.
katika National Library of Medicine (National centre of Biotechnical Information) tunasoma habari hizi kama ifuatavyo yaani baada ya utafiti wa Wataalamu.
The clavicle has the honor of being the first bone to start the ossification process and the last to finish it. It has also been described as the most frequently injured bone in children less than 10 years of age
Na hii clavicle ndiyo ٱلتَّرَاقِىَ “ATARAQIY” Kwa hiyo utafiti mbalimbali umefanywa na kutupa habari kama hizi kwamba huu ndiyo mfupa wa kwanza kukua katika Tumbo la uzazi wa mama na ndiyo mfupa wa mwisho kukua katika ujanani.
Wataalamu wanaendelea kutufahamisha zaidi kwamba Mifupa ya kitoto katika tumbo la mama ndiyo ya kwanza kuonekana au kukua kabla ya Misuli. Na Kuruani haikukosea kabisa. Utafiti wa Wataalamu mbalimbali wanatuthibitishia Mpangilio huu ambao ni wa kisasa baada ya Uchunguzi kwa machine za kisasa. Hakuna aliyejua hapo zamani. Kauli zao ni kama zifuatazo:
(The Signaling For Bone Formation is Present Earlier Than The Signaling For Muscle Formation. Cartilage is Present Before Muscle Formation)
Nishati ya Alama za Kukua kwa mifupa huonekana kabla ya Nishati ya Alama za kukua kwa Misuli. Cartilage au Kwa Kiswahili Gegedu inakuwapo kabla ya Misuli. Na hii Gegedu ndiyo inayogeuka na kuwa Mifupa. Sasa hebu tuzilete zile Aya zinazoelezea mpangilio huu wa Kiajabu ili tuzione. Allahu Akbar.
Sura Namba 23 Aya namba 12 mpaka 14
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن سُلَـٰلَةٍ۬ مِّن طِينٍ۬ (١٢)
ثُمَّ جَعَلۡنَـٰهُ نُطۡفَةً۬ فِى قَرَارٍ۬ مَّكِينٍ۬ (١٣)
ثُمَّ خَلَقۡنَا ٱلنُّطۡفَةَ عَلَقَةً۬ فَخَلَقۡنَا ٱلۡعَلَقَةَ مُضۡغَةً۬ فَخَلَقۡنَا ٱلۡمُضۡغَةَ عِظَـٰمً۬ا فَكَسَوۡنَا ٱلۡعِظَـٰمَ لَحۡمً۬ا ثُمَّ أَنشَأۡنَـٰهُ خَلۡقًا ءَاخَرَۚ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ أَحۡسَنُ ٱلۡخَـٰلِقِينَ (١٤)
TAFSIRI
12. Na kwa yakini tulimuumba mwanadamu kwa udongo ulio safi.
13. Kisha tukamuumba kwa tone Ia manii, (mbegu ya uzazi) lililowekwa katika makao yaliyohifadhika.
14·Kisha tukalifanya tone hilo kuwa pande Ia damu, na tukalifanya pande Ia damu hilo kuwa pande Ia nyama, kisha tukalifanya pande Ia nyama hilo kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama, kisha tukamfanya kiumbe kingine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji.
SHEREHE
Aya hizi zipo wazi wazi. Aya namba 14 inasema Kwanza ilikuwa mifupa na kisha nyama. Yaani kitoto katika tumbo la mama kwanza alianza kuwa na mifupa na baadaye nyama. Na hii ndiyo Sayansi ya leo inavyotuhakikishia. Utafiti mbalimbali umefanywa na Jawabu linawafikiana na Kuruani kama vile Soksi unavyoivalisha Miguuni. Je Mtume Alisoma wapi wakati huo ambao hakukuwako na vyombo vya hali ya juu vya kuchunguza mambo yanayopita Matumboni. Hebu fikiri. Huoni Maajabu. Allahu Akbar. Hii inathibitisha kwamba Kuruani ni Muujiza mkubwa sana. Allahu Akbar.
Kwa Kweli hakuna mwisho. Hebu tuendelee na Uchunguzi wa kushangaza. Tupeleke Darubini katika Sura Ya Zumar na hapo Kuna Aya inayohusiana na Elimu ya Kizazi. Tuchunguze zaidi Maajabu na Mishangao.
Sura Namba 39 Aya Namba 6
خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٍ۬ وَٲحِدَةٍ۬ ثُمَّ جَعَلَ مِنۡہَا زَوۡجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ ٱلۡأَنۡعَـٰمِ ثَمَـٰنِيَةَ أَزۡوَٲجٍ۬ۚ يَخۡلُقُكُمۡ فِى بُطُونِ أُمَّهَـٰتِڪُمۡ خَلۡقً۬ا مِّنۢ بَعۡدِ خَلۡقٍ۬ فِى ظُلُمَـٰتٍ۬ ثَلَـٰثٍ۬ۚ ذَٲلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمۡ لَهُ ٱلۡمُلۡكُۖ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَۖ فَأَنَّىٰ تُصۡرَفُونَ (٦)
TAFSIRI
6.Amekuumbeni katika nafsi moja, kisha kamfanya mwenziwe (mkewe) katika jinsi ile ile, na akakuteremshieni (akakuumbieni) wanyama wanane (hawa wenye nafuu kubwa kwenu) madume na majike. (Ngamia, Ng’ombe, Kondoo na Mbuzi).Hukuumbeni matumboni mwa mama zenu- umbo baada ya umbo – katika viza vitatu. Huyu ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu: Ufalme ni wake; hakuna aabudiwaye kwa haki ila yeye. Basi nyinyi mnageuzwa wapi?
SHEREHE
Tutaielekeza darubini katika kipande cha Aya hapa juu
فِى ظُلُمَـٰتٍ۬ ثَلَـٰثٍ۬ۚ Yaani Viza au Kiza Tatu. Hebu tufikiri Ajabu ya maneno haya. Je Mtume ﷺ amepata wapi habari kama hizi. haiwezekani mtu ajisemee hovyo hovyo kisha baada ya miaka iwe sio kweli. Kutoa kauli kama hii inathibitisha haya siyo maneno yake Mtume ﷺ peke yake hata kidogo. Heiwezekani. Haya ni maneno makubwa kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Hebu tufikiri. Wataalamu wa siku hizi za Teknologia na Sayansi wamefanya uchunguzi yanayopita katika tumbo la uzazi kwa kutumia Mashine za hali ya juu na kutueleza habari hizi za kushangaza. Allahu Akbar.
Sayansi inasema kwamba Giza Tatu ni:
1- The darkness of the anterior abdominal wall (Abdomen)
Giza la Ndani ya ngozi ya Tumbo
2- The darkness of the uterine wall
Giza la ndani ya Tumbo la Kizazi (Uterus)
3- The darkness of amniochorionic membrane
Giza la Mfuko unaomfunika Kijitoto
Wanatuambia tena kwamba maisha katika Tumbo la uzazi unapitia Hatua Tatu kama zifuatazo:
1- Pre-embryonic stage; (first two and a half weeks).
2- Embryonic stage; (up to the end of the eighth week).
3- And the Fetal stage; (from the eighth week to the birth).
Na Hata Ngozi ya Embryo yaani Inayomfunika katoto pia imegawanyika katika Matabaka matatu yaani Ngozi moja lakini ina Matandiko au Matabaka (layers) ya Ngozi nyembamba tatu kufanya ngozi moja Wanasema kwamba
The layers of Embryo are also Three as follows:
1/Ectoderm will give rise to the skin and nervous system
2/Mesoderm Specifies the development of bones, muscles and connective tissues and
3/Endoderm becomes the lining of respiratory and digestive system as well as other organs
Je unaona Kuruani inavyotufundisha? Allahu Akbar.