UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MAKALA IMEKUSANYA MAMBO MBALIMBALI
Alhamdulilah. Leo ni Jumamosi Tarehe 10 September 2022
Ni wakati wa asubuhi na ni siku mpya ambayo imeanzia na Mvua. Namshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kutupa Uhai na Afya ambayo ukiwa nayo basi unaweza kufanya mambo mengi duniani. Njia zipo nyingi lakini kuna njia zilizo nzuri na kuna zilizo mbaya. Katika wakati huu wa mapema ya asubuhi na huku mvua inapiga kwa sauti kubwa Juu ya bati za nyumba niyayokaa ningependelea kuchukua fursa hii nzuri kuchukua kalamu na kuanza kuandia makala ya Tatu ya Sayansi ambayo namuomba Mwenyeezi Mungu iwe miongoni mwa zile Njia nzuri alizozibariki. Amin.
Makala Hii ningependelea kuanza na kuzungumzia Hadithi ya Mtume ﷺ Mohamad inayohusiana na Sayansi.
Hapana Nimesahau samahani Msomaji kwanza ningependelea kudokeza Muujiza kutoka katijka Kuruani Tukufu ili iwe kama Kifunguzi cha Mlango huu wa Sayansi na Baada ya hapo nitaendelea na Hadithi ya Mtume inayohusiana na Sayansi.
Najua wasomaji wengi wanapenda Miujiza ya Kuruani. Na kwa kweli kila Mtu anapenda. Nani anayejua Huenda katika Kuruani kuna Habari ya Machimbo ya Almasi katika sehemu duniani. Hebu fikiri jambo hili.
Kama katika Kuruani kuna siri imetaja habari ya Almasi zilizopo katika sehemu mojawapo duniani na unabidi uitafute katika Kuruani? hebu jiulize Suala hili.
Kwa kweli kama ipo siri hiyo basi watu dunia njima wangelijitahidi kwa mashindano kuisoma ili kupata kujua siri hiyo.
Binaadamu tunapenda Utajiri. lakini Ndugu Binaadamu wenzangu yaliyopo katika Kuruani ni zaidi Ya Almasi. Ukisoma kuruani basi yote hayo utayapata kama siyo Duniani basi Akhera. Huu ni uhakika bila ya shaka yeyote.
Sasa kwanza nikudokeze kidogo mazungumzo baina yangu na Shekhe wangu hivi karibuni kisha tutaanza Makala Yetu ya leo ambayo ina maajabu siyo madogo. Nimekuahidini na siwezi kuwadanganya hata kidogo. Je mumekubali?
Sheikh wangu (Mwenyeezi Mungu Ambariki) akaniambia;
Sheikh: kuna Muujiza Mpya nitakupa.
Al-Amin Ali Hamad: Asante Sana natamani unijuulishe
Sheikh: Sura Ya Al-Fatiha Imekusanya Maana ya Msahafu wote
Al-Amin Ali Hamad: Naam, Nimesoma Habari hii kwamba Elimu ya Msahafu yote imekusanywa katika Sura Ya Al-Fatiha na Elimu ya Sura Ya Al-Fatiha Imekusanywa katika Aya Ya Basmala yaani “Bismi llahi Arrahmani Arrahim” Kuna Wanavyuoni wanaosema hivi. Kwa Kweli inashagaza sana.
Sheikh: Ngojea Nikupe Habari itakayokufurahisha sana kuhusu Elimu hii
Al-Amin Ali Hamad: Mwenyeezi Mungu akubariki Sheikh nieleze kwani nina hamu sana nielewe habari. Nijuulishe Haraka kwani Nina wasiwasi sana nataka nijue haraka haraka.
Sheikh: Usiwe na wasiwasi wowote nitakueleza. Tulia roho. wasiwasi unatokana na Mashetani.
Al-Amin Ali Hamad: Ngoja Nitengeneze Chai kisha tuzungumze
Sheikh: hakuna tatizo tengeneza Chai na mimi uniletee na kisha ukae na kinisikiliza kwa makini.
Al-Amin Ali Hamad: Asante Sheikh Mwenyeezi Mungu akuzidishie Elimu.
Sheikh: Nilikuelezea hapo zamani kwamba Hapo zamani Waarabu na Makabika Mengineyo ya wakati huo kama vile Mayahudi katika Enzi ya Mtume Mohamad ﷺ walikuwa wakitumia herufi kama Namba. Yaani wakati huo kulikuwa hakuna Namba. Kwa Mfano Alif ilitumika kama Namba 1, Herufi ya Baa ilitumika kama Namba 2 na hivyo hivyo namba zote ziliwakilishwa kwa Herufi. Kwa hiyo Angalia Namba zifuatazo zinavyoshangaza:
383 + 525=114 + 794
Al-Amin Ali Hamad: Sheikh wangu mimi sijaelewa chochote naona Namba tu.
Sheikh: Ngojea nifafanue zaidi.
Namba 383 Ni Jumla Ya Herufi za neno “KURUANI” unapoligeuza katika Namba walizotumia Waarabu wakati huo.
Namba 525 Ni Jumla Ya Herufi za neno “ALFATIHA” unapoligeuza katika Namba walizotumia Waarabu wakati huo. Kwa Mfano Herufi ا, ل.ف na nyinginezo zote.
Namba 114 ni idadi ya Sura za Kuruani.
Na Namba 794 ni Majina Ya neno ALFATIHA unapoligeuza katika Namba walizotumia Waarabu wakati huo. Yaani Majina Ya Herufi kama vile أَلِف ina Herufi Tatu na لاَم ina herufi Mbili
Mgozea nipange vizuri;
383 + 525=114 + 794 ni sawa na kusema
383 + 525=908 na 114 + 794=908
Je unaona Muiwano wa kushagaza.
Yaani
Kuruani ambayo ni 383 + Alfatiha ambayo ni 525 ni sawa na Sura za Kuruani ambazo ni 114 + Majina Ya Herufi za neno Al-FATIHA
Ngojea nikupangie tena vizuri ili ieleweke:
383 + 525=114 + 794
Neno Kuruani + Neno Al-Fatiha= Sura za Kuruani + Majina Ya Sura Ya Al-Fatiha
yaani
Kuruani + Al-Fatiha= Sura za Kuruani + Majina Ya Herufi za neno Al-Fatiha
Al-Amin Ali Hamad= Naanza Kufahamu kiidogo
Mbona Muiano huu unashangaza. Ni Kama nilivyosoma katika Chemistry. Nilisoma kuhusu Balance Equations.
Ni kama vile kusema Ukichanganya Majani ya miti ya aina hii na Majani ya Miti ya aina hiyo unapata Dawa ya aina fulani.
Sasa hapa Je ina Maana kwamba Elimu ya Msahafu wote imekusanyanywa katika Sura ya Al-Fatiha? je ni hivyo?
Sheikh; Tafadhali Acha Kujibabaisha kabisa. Je unaamini Elimu ya Yaliyo wazi na yaliyo fichika? yaani Dhwahira Na Batina? basi soma Hii miujiza ikuzidishie imani lakini usiichambue kwa kuzidisha au kupunguza kwani utapotea. yaani ni hatari usichikonoe chokonoe.
Al-Amin Ali Hamad: Unasema kweli kwani Inashangaza lakini hatuwezi kujua siri ya Miujiza Mikubwa kama hii lakini huenda watu wa baadaye wakagundua lakini sisi tusijihangaishe. Mwenyeezi Mungu anasema katika sura Namba 17 Aya namba 46
َلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِۦ عِلْمٌ ۚ إِنَّ ٱلسَّمْعَ وَٱلْبَصَرَ وَٱلْفُؤَادَ كُلُّ أُو۟لَـٰٓئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْـُٔولًۭ
Aya ina maana kwamba Usifuate yasiyo na Uhakika. Yaani jiepushe na Kubuni. Yaani Guess Work. Usifasiri Aya za Kuruani kwa kubuni bali kwa uhakika. Hii ndoyo maana ya Aya hii. Huenda kuna siri. Inashangaza sana angalia tena Muiano wa kiajabu
383 + 525=114 + 794
Neno Kuruani + Neno Al-Fatiha= Sura za Kuruani + Majina Ya Sura Ya Al-Fatiha.
Yaani kila upande tunapata jawabu 908
Allahu Akbar.
Mwenyeezi Mungu akubariki Sheikh. Siku ya leo umenipa habari ya majabu makubwa. Neno Kuruani kujumlisha neno Al-fatiha jawabu ni 908 na Jumla ya Sura za kuruani 114 kujumlisha Majina Ya hefufi ya Neno Al-Fatiha unapata jawabu ni 908 pia. Allahu Akbar. Sheikh haya kweli ni maajabu. Nadhani siwezi kulala leo hii. Nitakuwa nikifikiri hizi namba tu usiku wote. Nitakuwa nikifikiri siri gani imefichwa katika Muiano huu.
Sheikh namuomba Mwenyeezi Mungu anionyeshe siri ya Muiano huu wa kiajabu. Allahu Akbar
Najua kwamba wasomaji wa Website hii bado wana hamu sana ya kusoma ahadi niliyotoa hapo juu ya kwamba Nitazungumzia katika Mlango huu habari za Sayansi. Naona Sasa wakati umefika na Nitaanza. Nitaacha Yasiyohusu Website hii na kwa haraka Nitaanza na mapya. Haya Tuanze:
KUZIMA MOTO
Miaka mingi wanasayansi wametafuta njia mbalimbali za ufundi wa kuzima moto kwa njia safi kwani Kutumia Vyombo vya kisasa yenye kutumia madawa pia yana hatari nyinginezo kwa mimea na kuharibu hali ya hewa. madawa haya yana “Toxic Chemicals”
Hivi karibuni Wataalamu wamegundua Ufundi mpya ambao huenda ukawa Mfundi wa hali ya juu na wa siku za mbeleni.
Wataalamu Huko Marekani kutoka George Mason University wamegundua njia mpya kuzima moto kwa kutumia Sauti. Habari zinasema:
(Two former U.S. electrical engineering students have discovered a cutting-edge and unconventional way to fight fires: with sound. Specifically, bass frequencies between 30 and 60 Hz)
KIla siku Wataalamu wanatafuta Njia mbalimbali za kuleta Maendeleo katika Uzimaji a Moto na hasa wakati huu ambao Mashamba Makubwa makubwa yanaungua kama tunavyoona katika News au Habari za Dunia.
Je uamini au usiamini Mtume Mohamad alidokeza habari hizi katika Hadithi yake hapa chini:
س/ صحة حديث اذا رأيتم الحريق فكبروا ؟
ج/ يُروَى حديث في ذلك عن عبد الله بن عمرو بن العاص أن النبي صلى الله عليه وسلم قال : ( إِذَا رأيْتُمُ الحَرِيقَ فَكَبِّرُوا فَإِنَّ التَّكْبِيرَ يُطْفئُهُ ) أخرجه ابن السني في “عمل اليوم والليلة” (295) ، والطبراني في “الدعاء” (1/307) ، ولكنه حديث ضعيف لا يصح, لكن استحب بعض العلماء التكبير عند الحريق. يقول ابن القيم رحمه الله في “زاد المعاد” (4/194) : ” لما كان الحريق سببه النار ، وهي مادة الشيطان التي خلق منها ، وكان فيه من الفساد العام ما يناسب الشيطان بمادته وفعله ، كان للشيطان إعانة عليه وتنفيذ له ، وكانت النار تطلب بطبعها العلو والفساد ، وهذان الأمران – وهما العلو في الأرض والفساد – هما هدي الشيطان ، وإليهما يدعو ، وبهما يُهلِك بني آدم ، فالنار والشيطان كل منهما يريد العلو في الأرض والفساد ، وكبرياء الرب عز وجل تقمع الشيطان وفعله ، ولهذا كان تكبير الله عز وجل له أثر في إطفاء الحريق ؛ فإن كبرياء الله عز وجل لا يقوم لها شئ ، فإذا كبر المسلم ربه أثَّر تكبيره في خمود النار وخمود الشيطان التي هي مادته ، فيطفئ الحريق ، وقد جربنا نحن وغيرنا هذا فوجدناه كذلك ، والله أعلم #الكلام_دا_صح؟
Katika Mazungumzo yaliyopo katika Habari nilizonukulu hapa. Yaani Suali na Jibu kuhusu Hadithi Ya Mtume ambayo insemekana kwamba ni Hadithi Dhaifu. Kwa kweli kuna Hadithi ambazo zilikusanywa na Kupewa sifa za Udhaifu lakini huenda zikawa Hadithi sahihi kwani baadhi yake zinakubaliana na Mambo mengi katika maisha yetu.
Wanasema mashekhe katika Suali na Jibu hapa kwamba Hadihi inayosema kwamba
إذا رأيتم الحريق فكبروا؛ فإن التكبير يطفئه
Mtume ﷺ anasema kwamba Ukiona moto basi Useme
“Allahu Akbar” kwani kwa kusema hivyo unauzimisha moto.
Mashekhe wanasema kwamba ukisema Allahu Akbar unaondoa Shari ya Mashetani kwani hao ndiyo sababu ya Moto huo. Mashetani wanapenda kuleta Uharibifu na ndiyo kazi yao. Kwa hiyo ukisema “Allahu Akbar” basi hao Mashetani unawashinda na Shari inaondoka na kwa kusema hivyo itasadia kuuzimisha Moto huo.
SHEREHE YA KISANYANSI
Hebu tuifasiri Hadithi hii Kisayansi. Je huoni kwamba Kwa kusema “Allahu Akbar” Ni Kutumia Sauti katika Kuuzima Moto na hasa hizo herufi za “Allahu Akbar” . Kwa mfano Herufi HAA katika HU ya Allahu ni herufi inafuatiliwa na Upepo. Hizi ni Herufi zinazojulikana kama “bass frequencies” Yaani ni herufi za frequencies ya chini. Kwa mfano Herufi ya SIN ni herufi yenye frequencies za Juu na hakuna Herufi za aina hii katika ” “Allahu Akbar” Je huoni Muujiza wa Kisayansi uliotolewa na Mtume hapa? kwa kusema Allahu Akbar unakuwa umemtukuza Mwenyeezi Mungu na Unaondoa Shari ya Sheitani na hapo hapo unaondoa Moto Kisayansi. Kwa Kweli Sayansi ni Yake Mwenyeezi Mungu. Tunafundishwa Sayansi ya Hali ya Juu. Sisi tunadharau na tunafikiri kwamba mambo haya ya kidini yana uhusiano na Mashetani ambao hatuwajui na hatuamini lakini ukweli ni kwamba Kuna Siri nyinginezo za Kisayansi zimefichika. Tungeliamini hadithi hii na kuisoma basi tusingelingojea Mpaka Wataalamu kutoka Marekani waje kutufundisha. Na ndiyo maana Tukawa Nyuma kwani tumeipuuza Dini kwa ujinga wetu. Kuruani na Uislamu una kila kitu lakini tupo nyuma ya binaadamu wenzetu kwani tumeiacha kuruani. Wanakuja wengine kugundia mambo kisha tunasema ilikuwapo katika Kuruani au katika Hadithi za Mtume. Huu ndiyo ujinga wetu na ndiyo maana tupo nyuma. Allahu Akbar.
INAENDELEA………
NGUVU YA SAUTI NA MATUMIZI YAKE
Wengi hawajui kwamba Kuruani Imekusanya tunayoyajua na tusiyoyajua. Ulimwengu bali Malimwengu yote yapo katika Kuruani.
Hebu tusome Aya zifuatazo kutoka katika Kuruani Tukufu kisha Tuone Faida kutoka Katika Aya hizi.
لَوْ أَنْزَلْنَا هَذَا الْقُرْآنَ عَلَى جَبَلٍ لَرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُتَصَدِّعًا مِنْ خَشْيَةِ اللَّهِ وَتِلْكَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ) [الحشر: 21]
وَلَوْ أَنَّ قُرْآنًا سُيِّرَتْ بِهِ الْجِبَالُ أَوْ قُطِّعَتْ بِهِ الْأَرْضُ أَوْ كُلِّمَ بِهِ الْمَوْتَى بَلْ لِلَّهِ الْأَمْرُ جَمِيعًا) [الرعد: 31]
Aya ya kwanza kutoka katika Sura ya Al-Hashr Aya namba 21 inasema kwamba
21.Lau kama tungaliteremsha hii Qurani juu ya mlima, ungaliuona ukinyenyekea (na) kupasuka kwa sababu ya hofu ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mifano tunawapigia (tunawaeleza) watu ili wafikiri.
Na Aya Ya Pili kutoka katika Sura Ya Al-Raad Aya Namba 31 inasema kwamba:
31.Na kama ingalikuwako Qurani ambayo kwa Qurani hiyo milima ingaliondoshwa (inaposomwa). au kwa hiyo ardhi ingalipasuliwa, au wafu wangalisemeshwa kwa hiyo (basi ingekuwa Qurani hii ndiyo ya kufanya kazi hiyo, lakini hiyo siyo kazi ya Qurani). Siyo! ·Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je! Hawajajua walioamini ya kwamba Mwenyezi Mungu angalipenda bila shaka angaliwaongoza (Uislamuni) watu wote? (Akawaumba kama Malaika, hawana matamanio. Lakini amewapa akili na matamanio wapigane baina ya viwili hivi, washinde waingie Peponi). Wala msiba hautaacha kuwapata wale waliokufuru kwa sababu ya yale waliyoyafanya, au utashuka karibu na nchi zao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu (ya kuwatoa roho). Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi (yake).
SHEREHE
Hizi Aya Mbili zinaelezea Utukufu na ukubwa wa maneno ya Mwenyeezi Mungu. Maneno yake yana utukufu na ukubwa wa hali ya juu sana. Watu wengi hawajui na wanafikiri maneno ya utani kwa kucheka kwamba Je Kuruani inaweza kutingisha na kuondoa Milima? Je Kuruani Inaweza Kupasua Ardhi? Je Kuruani inaweza Kumzungumza Maiti aliyefariki Dunia? Wengi wanadharau na kuona upuzi na uongo.
Ndugu zanguni wajinga ni sisi wenyewe. Kuruani tumeiacha na ndiyo maana tumekuwa nyuma na wajinga. laiti tungeifuata na kuisoma Kuruani basi tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana katika maisha yetu yote.
Hizi Aya zimeficha mengineyo tusiyoyajua na katika yale machache tunayoyajua ni Sauti. Kwa mfano Neno “KURUANI” maana yake Kisomo yaani kwa kutumia Sauti. Aya hapa zinasema kwamba Maneno ya Mwenyeezi Mungu na siyo MSAHAFU yaani Kitabu cha Kuruani bali Yale maneno ya Kuruani yaani Kisomo cha Sauti. Lazima tuelewe hivyo. Maana ya neno Kuruani ni KISOMO na siyo makaratasi ya MSAHAFU.
Na kisomo chochote kinataka Sauti. Kwa hiyo katika Aya hizi tunapewa faida nyinginezo za ishara ya Faida ya Sauti tulizopewa na Mweenyeezi Mungu.
Jambo la kwanza Aya Zinatuelezea Muujiza na Ukubwa wa Kuruani Tukufu na Pia hapo hapo kuna Siri nyinginezo zimefichika. Na Mwenyeezi Mungu anajua Zaidi.
Hivi karibuni Wataalamu wamefanya Utafiti namna ya Kutumia SAUTI katika Kusukuma na Kuinua vitu. Habari zinasema kwamba Timu ya Watafiti wa Vyuo vikuu vya Sao Paulo huko Brazil na Huko Edinburgh Scotland (UK) wameweza Kuinua kampira kadogo cha Polysterine kwa kutumia sauti.
(Research team at University of São Paulo in Brazil and Heriot-Watt University in Edinburgh has now successfully levitated a polystyrene ball 3.6 times bigger than the wavelength lifting it)
Hapa chini nitaweka Picha ya Kapira na Pia Video yenye kuzungumzia mambo haya ya Kushangaza.
Kuruani siyo mchezo. Imekusanya Faida kubwa ambazo unaweza kugundua Mambo makubwa yenye kuleta faida duniani kwa hiyo tuwe macho tusilale. Angalia picha na Video hapa chini iliujionee mwenyewe. Allahu Akbar.
Kapira Kadogo Chekundu kinainuliwa na Sauti. Hii ni Experiment angalia Video hapa
Video-1
Video ya Utafiti. Nguvu Ya Sauti inavyoweza kuathiri Vitu. Allah Akbar
Video-2
Sauti – Experiment