SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Masuala Na Majibu

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

KULINGANIA DINI KWA HEKIMA NA MAWAIDHA YALIYO BORA

MASUALI YA WATU NA NAMNA NILIVYOYAJIBU LEO TAREHE  09/MAY/2022

katika You Tube Na sehemu nyinginezo za Mtandao kuna Video Nyingi zinazotangaza Uongo kuhusu Kuruani Tukufu na Uislamu  kwa mfano kuna Video Mojawapo iliyoandaliwa kwa lugha ya kiingereza yenye Kichwa cha habari

“43 Scientific Mistakes in the Quran” 

(Makosa 43 katika Kuruani Tukufu)

Video Hii ilinisababisha  Niijibu kwa lengo la kunusuru Dini ya Mwenyeezi Mungu. Kwa hiyo Nikatuma  Message ifuatayo katika Video hiyo ya Youtube:

FROM AL-AMIN ALI HAMAD 8 days ago

I am 100% confident that Quran has not a single error. The Knowledge of the Quran is far Superior and higher than all the Sciences. Science has Failed to answer many Questions. Science is just a small Brick from the Pyramid of Islam .

katika Kujibu huko Mara Nikajibiwa na mtu ambaye simjui lakini ni washabiki wa Video hiyo inayopuuza Dini ya Kiislamu kama ifuatavyo:

REPLY TO AL-AMIN ALI HAMAD-11 hours ago

Can quran prove ANYTHING? can it prove that there even is such thing as a soul? And that we are not just products of milion years of evolution?

Suala Nililoulizwa ni Kuhusu Uwezo wa Kuruani kuweza kuthibitisha ni nini Roho?

Na Je sisi Binaadamu ni Tokeo la Evolution?

Yaani fikra hizi zinatokana na Imani potofu kwamba kila kitu duniani kilizuka peke yake na kubadilika badilika kufuatana na mazingara na kwa hiyo Mwenyeezi Mungu hakutuumba. Na katika kulijibu suala hilo nimeona Bora sana Nilijibu kwa kutumia Kuruani Tukufu kama alivyojibu Mwenyeezi Mungu.

Alhamdulilahi Leo Nimejibu Masuala Haya na Huenda Mtu huyu atafaidika na Kujiepusha ya aliyoambiwa katika Video hiyo ya Youtube.

Majibu yangu kwa mtu huyo anayejiita ni kama yafuatalo:

REPLY FROM AL-AMIN ALI HAMAD AL-AMIN ALI HAMAD 2 hours ago (edited)

Many Thanks for your questions. The answer to your first question is from the Quran. Chapter 17 Ayat Number 85 where Allah replied to the same question which Prophet Mohamad was asked.

The Ayat Says. ( And they ask you, [O Muhammad], about the soul. Say, “The soul is of the affair of my Lord. And mankind have not been given of knowledge except a little.”)

And Concerning the second Question which deals with Evolution  I will give you an answer from the Quran itself. Allah Says In Chapter Number 71 Ayat Number 40-41 .

(What is [the matter] with you that you do not attribute to Allah [due] grandeur. While He has created you in stages?)

From the second Ayat we learn that everything is created in Stages. and that is Evolution. Not Evolution as Darwin (The Biologist Amateur)  thought but Allah Created everything in Stages. I hope my reply helps. All Great Scientists Understand that Quran is one of the Greatest Miracles in all Centuries. Yes I agree in Evolution but It’s the Creator who has created everything in Stages and not on it’s own. The Theory of Darwin was put into the Historical Bin a while ago after the Discovery of DNA. After it’s  Failure other Theories came along as a replacement such as Neo-Evolution but all failed too. Please be careful. Don’t listen to uneducated people. believe me that Quran is the word of Allah. If you want success then follow it’s teachings. No one force you as it’s your choice. Either To advance yourself or stay behind.

Na hii ndiyo Daawa nilyoifanya leo hii Alhamdulilah. Wasomaji wa Video hiyo ni karibu 575,583 (Watu milioni mia Tano na Sabini na tano Elfu na Mia Tano na Thamanini na Tatu). Ninasubiri Jibu la Mtu huyu na Mwenyeezi Mungu akipenda akinijibu tu basi Nitampa Mwanga zaidi kwa Kumfahamisha baada ya hapo ni juu yake kukubali au kukataa. Hakuna Kulazimishana. 

Sasa je tusipojibu Masuala kama haya je Inafaa? Kuruani Inatukanwa Duniani mbele ya Macho yetu na watu wapumbavu wasio na Elimu.

Kwa hiyo lazima tuinusuru Dini ya Mwenyeezi Mungu kwa Hekima. Jibu nililotoa sio langu bali Kutoka katika Kuruani.

Jawabu safi aliloliandaa Mwenyeezi Mungu kwa yule atakayeuliza. Na hii ndiyo namna ya Jawabu liwe. Tujiepushe kujibu hovyo hovyo wakati majawabu yapo katika Kuruani.

Kwa hiyo Jibu hilo Mwenyeezi Mungu akipenda litasomwa na wengi ambao pia huenda litawafaa na kuwaokoa kwani aliyeandaa Video hiyo ni kwa msaada wa Mashetani.

Usisahau Mwenyeezi Mungu Atatusaidia tukiinusuru Dini yake lakini kwa hekima na Elimu siyo Nguvu na magomabano.

Usitumie Maneno Mabaya au matusi bali kwa hekima na Kielimu kwani kazi yako nikuelimisha na siyo kulazimisha.

Mwenyeezi Mungu amesema katika kuruani kwamba Dini siyo lazima kwani Uongofu umebainika na Upotevu umebainika na kwa hiyo kazi yako ni kukumbusha tu na siyo kulazimisha.

Kwa keo naishia hapa na Mwenyeezi Mungu akipenda nitawaletea tena katika Mlango huu Vipande kama hivi Vya Kulingania Dini. Yaani Maswali na Majibu ili tupate kusoma njia mbalimbali za kuhojiana na Binaadamu wenzetu.