UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
KISA CHA ASHAB AU WATU WA AL-UKHDUD KATIKA SURA YA AL-Buruj
Sura Ya Al-Buruj 85 Aya Namba 4 Mpaka 9
قُتِلَ أَصۡحَـٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ (٤) ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ (٥) إِذۡ هُمۡ عَلَيۡہَا قُعُودٌ۬ (٦) وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُہُودٌ۬ (٧) وَمَا نَقَمُواْ مِنۡہُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ (٨) ٱلَّذِى لَهُ ۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ شَہِيدٌ (٩)
TAFSIRI
4. (Kuwa) wameangamizwa watu waliowaadhibu Waislamu katika mahandaki.
5. Yenye Moto wenye kuni (nyingi)
6. Walipokuwa wamekaa hapo
7. (Waliangamizwa makafiri hao pale wakati walipokuwa) wanatazama yale wanayowafanyia hao Waislamu (walipokuwa wakiwaadhibu).
8. Nao hawajaona baya lolote kwao (Waislamu) ila kumuamini Mwenyezi Mungu Mwenye kushinda (na) Mwenye kusifiwa
9. Ambaye ni Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuona kila kitu.
HADITHI YA MTUME (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)
Reference : Sahih Muslim 3005 in-book reference :
حَدَّثَنَا هَدَّابُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا ثَابِتٌ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ، أَبِي لَيْلَى عَنْ صُهَيْبٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ “ كَانَ مَلِكٌ فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ وَكَانَ لَهُ سَاحِرٌ فَلَمَّا كَبِرَ قَالَ لِلْمَلِكِ إِنِّي قَدْ كَبِرْتُ فَابْعَثْ إِلَىَّ غُلاَمًا أُعَلِّمْهُ السِّحْرَ . فَبَعَثَ إِلَيْهِ غُلاَمًا يُعَلِّمُهُ فَكَانَ فِي طَرِيقِهِ إِذَا سَلَكَ رَاهِبٌ فَقَعَدَ إِلَيْهِ وَسَمِعَ كَلاَمَهُ فَأَعْجَبَهُ فَكَانَ إِذَا أَتَى السَّاحِرَ مَرَّ بِالرَّاهِبِ وَقَعَدَ إِلَيْهِ فَإِذَا أَتَى السَّاحِرَ ضَرَبَهُ فَشَكَا ذَلِكَ إِلَى الرَّاهِبِ فَقَالَ إِذَا خَشِيتَ السَّاحِرَ فَقُلْ حَبَسَنِي أَهْلِي . وَإِذَا خَشِيتَ أَهْلَكَ فَقُلْ حَبَسَنِي السَّاحِرُ . فَبَيْنَمَا هُوَ كَذَلِكَ إِذْ أَتَى عَلَى دَابَّةٍ عَظِيمَةٍ قَدْ حَبَسَتِ النَّاسَ فَقَالَ الْيَوْمَ أَعْلَمُ آلسَّاحِرُ أَفْضَلُ أَمِ الرَّاهِبُ أَفْضَلُ فَأَخَذَ حَجَرًا فَقَالَ اللَّهُمَّ إِنْ كَانَ أَمْرُ الرَّاهِبِ أَحَبَّ إِلَيْكَ مِنْ أَمْرِ السَّاحِرِ فَاقْتُلْ هَذِهِ الدَّابَّةَ حَتَّى يَمْضِيَ النَّاسُ . فَرَمَاهَا فَقَتَلَهَا وَمَضَى النَّاسُ فَأَتَى الرَّاهِبَ فَأَخْبَرَهُ فَقَالَ لَهُ الرَّاهِبُ أَىْ بُنَىَّ أَنْتَ الْيَوْمَ أَفْضَلُ مِنِّي . قَدْ بَلَغَ مِنْ أَمْرِكَ مَا أَرَى وَإِنَّكَ سَتُبْتَلَى فَإِنِ ابْتُلِيتَ فَلاَ تَدُلَّ عَلَىَّ . وَكَانَ الْغُلاَمُ يُبْرِئُ الأَكْمَهَ وَالأَبْرَصَ وَيُدَاوِي النَّاسَ مِنْ سَائِرِ الأَدْوَاءِ فَسَمِعَ جَلِيسٌ لِلْمَلِكِ كَانَ قَدْ عَمِيَ فَأَتَاهُ بِهَدَايَا كَثِيرَةٍ فَقَالَ مَا هَا هُنَا لَكَ أَجْمَعُ إِنْ أَنْتَ شَفَيْتَنِي فَقَالَ إِنِّي لاَ أَشْفِي أَحَدًا إِنَّمَا يَشْفِي اللَّهُ فَإِنْ أَنْتَ آمَنْتَ بِاللَّهِ دَعَوْتُ اللَّهَ فَشَفَاكَ . فَآمَنَ بِاللَّهِ فَشَفَاهُ اللَّهُ فَأَتَى الْمَلِكَ فَجَلَسَ إِلَيْهِ كَمَا كَانَ يَجْلِسُ فَقَالَ لَهُ الْمَلِكُ مَنْ رَدَّ عَلَيْكَ بَصَرَكَ قَالَ رَبِّي . قَالَ وَلَكَ رَبٌّ غَيْرِي قَالَ رَبِّي وَرَبُّكَ اللَّهُ . فَأَخَذَهُ فَلَمْ يَزَلْ يُعَذِّبُهُ حَتَّى دَلَّ عَلَى الْغُلاَمِ فَجِيءَ بِالْغُلاَمِ فَقَالَ لَهُ الْمَلِكُ أَىْ بُنَىَّ قَدْ بَلَغَ مِنْ سِحْرِكَ مَا تُبْرِئُ الأَكْمَهَ وَالأَبْرَصَ وَتَفْعَلُ وَتَفْعَلُ . فَقَالَ إِنِّي لاَ أَشْفِي أَحَدًا إِنَّمَا يَشْفِي اللَّهُ . فَأَخَذَهُ فَلَمْ يَزَلْ يُعَذِّبُهُ حَتَّى دَلَّ عَلَى الرَّاهِبِ فَجِيءَ بِالرَّاهِبِ فَقِيلَ لَهُ ارْجِعْ عَنْ دِينِكَ . فَأَبَى فَدَعَا بِالْمِئْشَارِ فَوَضَعَ الْمِئْشَارَ فِي مَفْرِقِ رَأْسِهِ فَشَقَّهُ حَتَّى وَقَعَ شِقَّاهُ ثُمَّ جِيءَ بِجَلِيسِ الْمَلِكِ فَقِيلَ لَهُ ارْجِعْ عَنْ دِينِكَ . فَأَبَى فَوَضَعَ الْمِئْشَارَ فِي مَفْرِقِ رَأْسِهِ فَشَقَّهُ بِهِ حَتَّى وَقَعَ شِقَّاهُ ثُمَّ جِيءَ بِالْغُلاَمِ فَقِيلَ لَهُ ارْجِعْ عَنْ دِينِكَ . فَأَبَى فَدَفَعَهُ إِلَى نَفَرٍ مِنْ أَصْحَابِهِ فَقَالَ اذْهَبُوا بِهِ إِلَى جَبَلِ كَذَا وَكَذَا فَاصْعَدُوا بِهِ الْجَبَلَ فَإِذَا بَلَغْتُمْ ذُرْوَتَهُ فَإِنْ رَجَعَ عَنْ دِينِهِ وَإِلاَّ فَاطْرَحُوهُ فَذَهَبُوا بِهِ فَصَعِدُوا بِهِ الْجَبَلَ فَقَالَ اللَّهُمَّ اكْفِنِيهِمْ بِمَا شِئْتَ . فَرَجَفَ بِهِمُ الْجَبَلُ فَسَقَطُوا وَجَاءَ يَمْشِي إِلَى الْمَلِكِ فَقَالَ لَهُ الْمَلِكُ مَا فَعَلَ أَصْحَابُكَ قَالَ كَفَانِيهِمُ اللَّهُ . فَدَفَعَهُ إِلَى نَفَرٍ مِنْ أَصْحَابِهِ فَقَالَ اذْهَبُوا بِهِ فَاحْمِلُوهُ فِي قُرْقُورٍ فَتَوَسَّطُوا بِهِ الْبَحْرَ فَإِنْ رَجَعَ عَنْ دِينِهِ وَإِلاَّ فَاقْذِفُوهُ . فَذَهَبُوا بِهِ فَقَالَ اللَّهُمَّ اكْفِنِيهِمْ بِمَا شِئْتَ . فَانْكَفَأَتْ بِهِمُ السَّفِينَةُ فَغَرِقُوا وَجَاءَ يَمْشِي إِلَى الْمَلِكِ فَقَالَ لَهُ الْمَلِكُ مَا فَعَلَ أَصْحَابُكَ قَالَ كَفَانِيهِمُ اللَّهُ . فَقَالَ لِلْمَلِكِ إِنَّكَ لَسْتَ بِقَاتِلِي حَتَّى تَفْعَلَ مَا آمُرُكَ بِهِ . قَالَ وَمَا هُوَ قَالَ تَجْمَعُ النَّاسَ فِي صَعِيدٍ وَاحِدٍ وَتَصْلُبُنِي عَلَى جِذْعٍ ثُمَّ خُذْ سَهْمًا مِنْ كِنَانَتِي ثُمَّ ضَعِ السَّهْمَ فِي كَبِدِ الْقَوْسِ ثُمَّ قُلْ بِاسْمِ اللَّهِ رَبِّ الْغُلاَمِ . ثُمَّ ارْمِنِي فَإِنَّكَ إِذَا فَعَلْتَ ذَلِكَ قَتَلْتَنِي . فَجَمَعَ النَّاسَ فِي صَعِيدٍ وَاحِدٍ وَصَلَبَهُ عَلَى جِذْعٍ ثُمَّ أَخَذَ سَهْمًا مِنْ كِنَانَتِهِ ثُمَّ وَضَعَ السَّهْمَ فِي كَبِدِ الْقَوْسِ ثُمَّ قَالَ بِاسْمِ اللَّهِ رَبِّ الْغُلاَمِ . ثُمَّ رَمَاهُ فَوَقَعَ السَّهْمُ فِي صُدْغِهِ فَوَضَعَ يَدَهُ فِي صُدْغِهِ فِي مَوْضِعِ السَّهْمِ فَمَاتَ فَقَالَ النَّاسُ آمَنَّا بِرَبِّ الْغُلاَمِ آمَنَّا بِرَبِّ الْغُلاَمِ آمَنَّا بِرَبِّ الْغُلاَمِ . فَأُتِيَ الْمَلِكُ فَقِيلَ لَهُ أَرَأَيْتَ مَا كُنْتَ تَحْذَرُ قَدْ وَاللَّهِ نَزَلَ بِكَ حَذَرُكَ قَدْ آمَنَ النَّاسُ . فَأَمَرَ بِالأُخْدُودِ فِي أَفْوَاهِ السِّكَكِ فَخُدَّتْ وَأَضْرَمَ النِّيرَانَ وَقَالَ مَنْ لَمْ يَرْجِعْ عَنْ دِينِهِ فَأَحْمُوهُ فِيهَا . أَوْ قِيلَ لَهُ اقْتَحِمْ . فَفَعَلُوا حَتَّى جَاءَتِ امْرَأَةٌ وَمَعَهَا صَبِيٌّ لَهَا فَتَقَاعَسَتْ أَنْ تَقَعَ فِيهَا فَقَالَ لَهَا الْغُلاَمُ يَا أُمَّهِ اصْبِرِي فَإِنَّكِ عَلَى الْحَقِّ ”
KISA CHA WATU WA MASHIMO YA MITARO YA MOTO
KUTOKA KATIKA KURUANI NA HADITHI YA MTUME HAPA JUU (Amani na Sala Zake Mwenyeezi Mungu Zimfikie)
Nimeelezea Kisa Hiki kufuatana na Aya za Kuruani na Hadithi Ya Mtume Hapa Juu. Pia Nimeongeza Habari Inayohusiana na Jina La Mfalme Dhu-Nuwas Kutoka Katika Vitabu Vinginevyo. Nimejitahidi Kurahisisha maelezo ili ipate kueleweka.
Inasemekana kwamba Kisa hiki kilitokea Wakati Mayahudi wa Najrani walipoingia katika Umasihia (Baada ya Ukristo na kabla ya kuja Uislamu na ilikuwa kabla ya Umasihia kuharibiwa), alipata habari mfalme wao, Dhu-Nuwas; akaja Najrani na jeshi kubwa, akawalazimisha watu wa Nairani warudi katika Uyahudi; nao wakakataa. Dhu-Nuwas akachimba handaki kubwa akatia kuni, akawasha moto. Akawa humshika mmoja mmoja katika wale Wamasihia wa Najrani akiwatupa katika handaki lile, na yeye na watu wake wamekaa pambizoni mwa handaki watafaraji.
Kisa hiki kinatoa Mafundisho ya Kushikana na Mwenyeezi Mungu na Kufanya Uvumilivu. Na pia Umuhimu wa Dua.
MFALME ALIYEJULIKANA KWA JINA Dhu-Nuwas, MSHAURI WA MFALME MCHAWI, KIJANA MRITHI WA MCHAWI NA MTAWA (Mcha Mungu)
Mfalme anasemekana ni Dhu-Nuwas aliyeishi wakati huo alikuwa na Mshauri Mchawi Katika Mahakama Yake (Yaani Alipewa kazi na Mfalme).
Alipozeeka (mchawi) akamwambia mfalme: “Mimi Nimezeeka, nitumie kijana mdogo ili nimfundishe uchawi”. (Mfalme) alimtumia kijana ili afundishwe Uchawi na arithi Elimu hiyo.
Na katika njia yake (Njia Ya kila siku Kwenda kwa yule mchawi) alimkuta mtawa (Mchamungu) ameketi.
kijana alisikiliza mazungumzo ya mtawa na akavutiwa nayo.
Ikawa ni kawaida yake kwamba akiwa njiani kwenda kwa mchawi alikutana na mtawa na kukaa (Naye kwa muda na kumsikiliza mafundisho yake)
Siku Moja Mchawi Akampiga Kijana Yule kwa sababu ya kuchelewa. Na Kijana Akalalamika kwa mtawa na Mtawa akamshauri kwamba
“Unapoulizwa na Mchawi sababu ya Kuchelewa sema: “Jamaa zangu (Familia Yangu) wamenichelewesha”.
Na Jamaa zako (Familia Yako) Wanapokuuliza Sababu ya Kuchelewa Waambie:
“Mchawi ndiye amenichelewesha”.
Ikawa kijana yule anapotoka Nyumbani kuelekea kwa Mchawi basi kwanza anamzuru rafiki yake Mtawa na Kumsikiliza Mafundisho ya Mungu na Pia anapokuwa akirudi Nyumbani kutoka kwa Mchawi anamtembelea Rafiki yake Mtawa na Kusoma mambo ya Dini na Kisha kuelekea Nyumbani.
Siku Moja Kulikuja mnyama mkubwa wa Pori na akazuia njia ya watu, Akasema (yule kijana):
“Nitajua leo kama mchawi ni mkweli au mtawa ni ndiyo Mkweli”
Akainua jiwe na kusema:
“Ewe Mwenyezi Mungu, ikiwa jambo la mtawa ni Kubwa Kwako kuliko jambo la mchawi, mfishe mnyama huyu ili watu waweze kutembea Njiani kwa uhuru”
Akalitupa jiwe lile na kumuua Mnyama Yule na watu wakaanza kutembea katika njia kwa uhuru bila tatizo. Yule kijana akaja kwa Rafiki Yake mtawa na Akamjulisha Yaliyotokea Kuhusu Yule Mnyama Mkubwa wa Pori na yule mtawa akamnasihi:
“Mwanangu, Umekuwa Na Elimu bora kuliko mimi. Vitendo Vyako vimefikia hatua ambapo naona kwamba utafikishwa mahakamani hivi karibuni, na iwapo utafikishwa mahakamani usinitaje kabisa”
Kijana huyo aliendelea kuwatibu vipofu na wale waliokuwa na ukoma na kwa kweli alianza kuwaponya watu (wa kila aina) wenye maradhi mbalimbali.
Mshauri wa mfalme aliyekuwa kipofu aliposikia habari za huyo Kijana, alimwendea akiwa na zawadi nyingi na kusema:
“Ukiniponyesha Upofu wangu basi haya mali yote niliyokusanya hapa yatakuwa yako”.
Kijana akasema
“Mimi mwenyewe simtibu mtu yeyote. Mwenyezi Mungu ndiye anayetibu, na ikiwa wewe unamwamini Mwenyezi Mungu, basi nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye”.
Na Mshauri wa Mfalme Alikiri imani yake kwa Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akamponya na akaenda kwa mfalme na kukaa karibu yake kama alivyokuwa akikaa hapo awali.
Mfalme akamuuliza.
“Ni nani aliyekuponyesha macho yako?”
Akasema:
“Mwenyeezi Mungu Ndiye aliyeniponyesha” .
Mfalme akauliza:
“Mwenyeezi Mungu badala yangu?”(Mfalme aliamini kwamba yeye ndiye Mungu).
Mshauri wake Akamjibu :
“Mwenyeezi Mungu Wangu na Wako”
Basi Mfalme akamuadhibu Mshauri mpaka akatoa Siri ya kijana huyo aliyemtibu.
Yule kijana aliitwa na mfalme akaulizwa: “
Ewe kijana, imefikishwa habari kwangu kwamba umekuwa hodari sana katika uchawi wako Mpaka umefikia kunawaponya vipofu na wenye ukoma na unaponyesha Maradhi Mnegineyo Mbalimbali. Kijana akamjibu mfalme:
“Mimi Simponyeshi mtu bali Mwenyezi Mungu ndiye anaye ponyesha”.
Mfalme akaanza Kumuadhibisha Kijana huyu sana mpaka akatoa siri ya habari za mtawa aliyemfundisha Dini ya Mungu Mmoja.
Basi yule mtawa aliitwa na kuamrishwa Aache Dini ya Kumuabudu Mungu Mmoja. Mtawa alikataa kufanya hivyo.
Mfalme Akaamrishwa msumeno uletwe na Ulipoletwa Akampasua Yule Mtawa kichwa chake na kuupasua vipande vipande mpaka sehemu ikaanguka.
Kisha akaletwa Mshauri wa mfalme, akalazimishwa Aache Imani ya Mungu Mmoja na alikataa kufanya hivyo, na msumeno ukawekwa katikati ya kichwa chake na ukapasuliwa mpaka sehemu ikaanguka chini. Kisha akaletwa yule kijana na akaambiwa:
“Geuka katika dini yako (Acha Imani ya Mungu Mmoja) . Alikataa kufanya hivyo na Mfalme akaamrisha Watumishi wake . Akawaambia: “
Mpelekeni Kijana Huyu Katika Kilele cha Mlima Na ukifika juu yake (mwambie Aikane imani yake) na akikataa basi mtupe (chini ya mlima).
Basi wakamchukua na wakampandisha mlimani na yule kijana akaomba dua na huku akasema:
“Ewe Mwenyezi Mungu niokoe (kwa namna yoyote) Upendayo”
Mlima ukaanza kutetemeka na watumishi wote wakaanguka chini na kufa. Kijana Huyo akarudi akitembea kwa mfalme.
Mfalme akamwambia:
“Nini kimewapata wenzako? Alisema:
“Mwenyezi Mungu ameniokoa kutoka kwao. Akawaamrisha watumishi wake na akasema:
“Mchukueni katika merikebu ndogo na mkifika katikati ya bahari mwambieni aikane Dini yake, lakini asipoiacha dini yake mtupeni. ndani ya maji”.
Basi wakamchukua na Kijana akaomba Mungu na kusema
“Ewe Mwenyezi Mungu niokoe na wao na wanachotaka kufanya”.
Upesi sana mashua ikageuka na wakazama na akarudi kwa mfalme, na mfalme akamuuliza:
“Nini kimewapata wenzako?”
Akasema:
“Mwenyezi Mungu ameniokoa kutoka kwao”,
na Kijana Yule akamwambia mfalme:
“Huwezi kuniua mpaka ufanye ninachokuomba”
Na Mfalme akasema: “
“Ni nini hicho?” Akasema:
“Uwakusanye watu kwenye uwanja na unitundike kwenye shina (la mti). Kisha shika mshale na Useme”: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa kijana”.
Piga mshale na ukifanya hivyo (Uombe dua hiyo) na ndiyo utaweza kuniua.
Basi (Mfalme) akawaita watu kwenye uwanja ulio wazi na watu wote walikuwa wakitizama hayo. Akamfunga (Yule kijana) kwenye shina la mti, kisha akashika mshale na kuuweka kwenye upinde kisha akasema:
“Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa kijana” kisha akapiga mshale na akafa.
Na watu wakasema: “
Tunaamni imani yetu kwa Mola wa kijana huyu”. (Watu wakawa na Imani ile ile ya huyu Kijana aliyeuawa)
Wakuu wakamjia mfalme, akaambiwa: “
Je! unaona kwamba Mwenyezi Mungu amefanya yale uliyokusudia kuyaepuka”
“Wao (watu) wameamini na kuthibitisha imani yao kwa Mola”
Mfalme hakufurahi habari hii ya watu wengi kuingia katika imani ya Mungu Mmoja na aliamuru mitaro kuchimbwa kwenye sehemu ya Mji huo.
Ilipochimbwa mitaro hiyo, moto mkubwa sana ukawashwa ndani yake ikasemwa (kwa watu): “Asiyeiacha dini ya huyu kijana atatupwa motoni au wataambiwa ruka ndani yake”
Watu walikufa wengi kwani walikhiari Kufa katika Moto kuliko kutupa imani ya Dini Ya Mungu Mmoja. Inasemekana Kulikuwa Na Mwanamke alyekuwa na Mtoto wa Kubeba (Kunyonya) ambaye alikuwa na Imani Ya Mungu mmoja na alipoambiwa achague kutupwa motoni au kutupa Imani ya Dini hiyo.
Huyu Mama alisita sana kwani alimhurumia Mtoto wake mchanga aliyekuwa Amebebwa lakini Muujiza Ulitokea Na Mtoto akasema
“Mama, Vumilia (hili) kwani Upo katika Haki”
Maneno haya yakampa Moyo huyu mama na Akajitupa Motoni.
Hiki ndicho kisa cha ASHAB ALUKHDUD katika Sura Ya Al-Buruj.
TUKIO LA KUPOTEZA NURU YA MACHO KATIKA MAISHA YA IMAMU BUKHARI
Imamu Bukhari alizaliwa Katika Mji wa Bukhara (Nchi iliyojulikana kwa jina kama Khorasan Na hivi sasa Jina Limebadilishwa na kuwa Uzbekistan). katika Mwaka 196 Baada Ya Hijra (A.H.) Mwaka 810 katika Miaka ya Kikristo (Chritian Era).
Baba Yake alifariki alipokuwa Imamu Bukhari bado kijana mdogo.
Alipoteza Macho yake alipokuwa Mtoto mdogo. Mama Yake alikuwa Mcha Mungu. Baada ya Kufiwa na Mumewe akabaki na watoto wawili na mmojawapo ndiyo Huyu Bukhari. Jina lake kamili ni Muḥammad ibn Ismā’īl al-Bukhārī.
Mama Yake Muḥammad ibn Ismā’īl al-Bukhārī. alipatwa na huzuni kubwa baada ya Misiba hiyo ya kufiwa na Mumewe na Mtoto wake Kupoteza Nuru ya Macho. Na akatumia wakati wake Usiku na Mchana kumuombea Dua Mtoto wake.
Siku Moja Akaota Ndoto Nabii Ibrahim anamuahidi Kurudisha Macho ya Mtoto wake. Alipoamka Asubuhi akaenda kumwamsha Mtoto Wake na Alishangaa sana Kukuta Mtoto wake anaweza kuona tena. Dua Ya Mama Yake ilikubaliwa.
Inasemekana Macho yake baada ya Kuyapoteza yalikuwa na nguvu sana kiasi ambacho aliweza kusoma vitabu kwa kutumia Nuru ya Mwezi.
Na pia Nguvu za Ubongo katika Kuhifadhi Ilikuwa Na Nguvu zaidi kuliko kabla ya kupoteza Nguvu za Kuona.
Aliweza Kuhifadhi Kuruani Yote alipokuwa na Umri wa Miaka 9
Na Baada ya Hapo akaanza kusoma Hadithi za Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie).
Alipokuwa na Umri wa Miaka 18 alikwenda Saudi Arabia Na akaishi huko kwa muda wa Miaka 16. Alikaa huko kwa lengo la kukusanya Hadithi Za Mtume Mohamad. ((Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie).
Inasemekana kwamba Alisoma karibu Hadithi 600,000 za Mtume kutoka kwa Wanavyuoni karibu1000.
Katika Maisha Yake aliandika Vitabu kama vile Tarikh Al-Kabeer, Adab Al-Mufrad na Sahih Al-Bukhari.
Sahih Al-Bukhari Ni Volumes (Vitabu) Vilivyokusanya Hadithi za Mtume. Ni Vitabu Vinavyoaminiwa (Authentic) sana na Waislamu Duniani baada tu Ya Kuruani.

Picha Ya Imamu Bukhari
KISA CHA KUCHOMWA MOTO MSIKITI UNAOJULIKANA KWA JINA KAMA مسجد الضرار
KISA KUTOKANA NA WANVYUONI WAFUATAO
At-Tabari, Al-Jalalayn na Ibn Kathir
Sura Ya Al-Tawba Aya Namba 107-108
وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مَسۡجِدً۬ا ضِرَارً۬ا وَڪُفۡرً۬ا وَتَفۡرِيقَۢا بَيۡنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَإِرۡصَادً۬ا لِّمَنۡ حَارَبَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُ ۥ مِن قَبۡلُۚ وَلَيَحۡلِفُنَّ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّا ٱلۡحُسۡنَىٰۖ وَٱللَّهُ يَشۡہَدُ إِنَّہُمۡ لَكَـٰذِبُونَ (١٠٧)
TAFSIRI
107. Na wako (wanafiki wengine) waliojenga msikiti wa (kuleta) udhia na kutia nguvu ukafiri na kuwafarikisha walioamini na kuufanya mahali pa kuwangojea wale waliomfanyia vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake zamani. Na bila shaka wataapa (waseme): “Hatukukusudia ila wema.” Lakini Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao ni waongo.
لَا تَقُمۡ فِيهِ أَبَدً۬اۚ لَّمَسۡجِدٌ أُسِّسَ عَلَى ٱلتَّقۡوَىٰ مِنۡ أَوَّلِ يَوۡمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِۚ فِيهِ رِجَالٌ۬ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُواْۚ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلۡمُطَّهِّرِينَ (١٠٨)
TAFSIRI
108. Usisimame (msikitini) humo kabisa. Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa kumcha Mungu tangu siku ya kwanza (ya kufika Mtume Madina) unastahiki zaidi wewe usimame humo. Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wajitakasao. (Nao ndio ule msikiti wa Mtume unaosaliwa na Maswahaba watwahirifu).
SHEREHE
Aya hizi Mbili kutoka katika Sura Ya Al-Tawba zilishuka kwa Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Mwanzoni mwa karne ya 7 huko Madina. Sababu ya kushushiwa Mtume Aya Hizi ni Kutokana na Msikiti Wa Wanafiki uliojengwa kwa Nia Mbaya hapo Madinna. Kama tunavyosoma katika Aya Mbili hapa Juu kwamba Msikiti huo wa Wanafiki ulijengwa kwa Lengo la kuleta fitina ya Kuwaaangamiza Waislamu.
Historia inasema kwamba Msikiti huo Wa Wanafiki ambao Unajulikana kwa jina kama Masjid Al-Dhirar Ulijengwa karibu sana na Msikiti Mwingine unaojulikana kwa jina kama Masjid Al-Qubah.
Masjid Al-Qubah ni Msikiti wa kwanza Kujengwa na Mtume na ambao ni moja ya Misikiti Minne maarufu ya zamani (Msikiti wa Haram-Mecca, Msikiti wa Al-Aqsa-Old Jerusalem, Sacred Monument-Muzdalifah, Na Quba Mosque-Madinna).
Msikiti wa Wanafiki ulijengwa na Mtawa (Monk) wa Kikristo anayejulikana kwa jina kama Abu Amir na Wanafiki Wengineo ambao walishirikiana Naye katika Ujenzi huo.
Lengo la kujenga Msikiti huo ni Kuwaletea Ghasia Waislamu kwa njia ya kuwavurugia imani yao na pia Kuwatenganisha.
Baada tu ya msikiti huo kujengwa Mtume Mohamad (Sala na Amani yake Mwenyeezi Mungu zimfikie) akaalikwa alipokuwa katika mji unaojulikana kama Dhu Awan (Mji huu ni saa Moja kutoma Madina) aje asali hapo.
Walimwambia kwamba Watu wameujenga msikiti huo wa Al-Dhirar kwa ajili ya Wagonjwa, Wenye Shida, Wakati wa Mvua na Pia Usiku wa Baridi kali.
Lakini Mtume akawajibu kwamba yupo katika mishughuliko ya safari ya Kwenda Huko Tabuk. Lengo la kwenda Tabuk ni Kuulinda Mji huo baada ya Mtume kupata habari kwamba Utavamiwa na Dola Ya Kirumi (Byzantine Empire)
Mtume alishiriki Safari hiyo ambayo ilikusanya Jeshi la waislamu karibu 30,000 (Thelathini Elfu).
Warumi hawakuvamia Tabuk na kwa hiyo Vita havikufanyika.
Mtume alionyesha Ushujaa Mkubwa sana kwa Kuwa Tayari Kupigana na Dola Kubwa ya Kirumi (Romans).
Alipokuwa akirudi vitani na kusimama katika Mji wa Dhu Awan akaletewa Wahyi wa kushushiwa Aya Hizi Mbili tulizozitaja hapa Juu. Mmwenyeezi Mungu akamfunulia Mbinu na Njama za Mahaini wanaomwandalia katika Msikiti huo.
Akawaamrisha Baadhi ya Maswahaba kwenda na Kuuchoma moto Msikiti Huo.
Kwani lengo la hao walioujenga halikuwa zuri. Walimwalika Mtume na kisha walipanga Wamvamie na Kumuua.
Maswahaba hao wakenda katika Msikiti huo na Kuuchoma moto.
Waliokuwa ndani ya msikiti huo wakatoka na kusambaa.
Inasemekana kwamba Huyu Adui aliyesimamia kujenga huo Msikiti wa Wanafiki huko Madina asili yake ni Kutoka katika Ukoo wa Al-Khazraj.
Hapo Mwanzo alikuwa Mkristo kabla ya kubadili dini na kuukubali Uislamu.
Baada ya Msikiti huo Kuchomwa moto na baada ya Vita Vya Badr kufanyika na Waislamu kufanikiwa katika Vita hivyo Abu Amir alichukia sana na akaamua kujiunga na Makafiri wa Mecca katika vita vinginevyo kama vile Vita vya Uhud vilivyofanyika baina ya Makafiri na Waislamu.
Aya ya Pili namba 108 inasifu Msikiti wa Quba Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa kumcha Mungu tangu siku ya kwanza (ya kufika Mtume Madina) unastahiki zaidi wewe usimame humo. Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wajitakasao. (Nao ndio ule msikiti wa Mtume unaosaliwa na Maswahaba watwahirifu). Na Katika Aya Hii Mtume anakatazwa Kuzuru na Kuswali Msikiti huo wa Al-Dhirar.
Kwa kifupi hii ndiyo sababu ya Kuchomwa Moto Msikiti huo wa Al-Dhirar. Ni Msikiti wa Wanafiki waliokuwa na Njama Mbaya.
KISA CHA ALIYEFISHWA NA KUFUFULIWA BAADA YA MIAKA 100 MOJA
KISA CHA KUSHANGAZA SANA
Sura Ya Al-Bakarah Namba 2 Aya Namba 259
أَوۡ كَٱلَّذِى مَرَّ عَلَىٰ قَرۡيَةٍ۬ وَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا قَالَ أَنَّىٰ يُحۡىِۦ هَـٰذِهِ ٱللَّهُ بَعۡدَ مَوۡتِهَاۖ فَأَمَاتَهُ ٱللَّهُ مِاْئَةَ عَامٍ۬ ثُمَّ بَعَثَهُ ۥۖ قَالَ ڪَمۡ لَبِثۡتَۖ قَالَ لَبِثۡتُ يَوۡمًا أَوۡ بَعۡضَ يَوۡمٍ۬ۖ قَالَ بَل لَّبِثۡتَ مِاْئَةَ عَامٍ۬ فَٱنظُرۡ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمۡ يَتَسَنَّهۡۖ وَٱنظُرۡ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجۡعَلَكَ ءَايَةً۬ لِّلنَّاسِۖ وَٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡعِظَامِ ڪَيۡفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكۡسُوهَا لَحۡمً۬اۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ ۥ قَالَ أَعۡلَمُ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ ڪُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬ (٢٥٩
TAFSIRI
259. Au kama yule aliyepita karibu na mji uliokuwa umekufa akasema: “Mwenyezi Mungu atauhuisha vipi (mji) huu (na watu wake) baada ya kufa kwake?” Basi Mwenyezi Mungu alimfisha kwa miaka mia, kisha akamfufua akamwuliza: “Umekaa muda gani?” Akasema: “Nimekaa muda wa siku moja au sehemu ya siku.” · (Mwenyezi Mungu) akasema: “Bali umekaa miaka mia; nawe tazama chakula chako na vinywaji vyako, havikuharibika.Na mtazame punda wako (amekuwa mifupa mitupu iliyolikalika). Na ili tukufanye uwe hoja kwa watu (ndio tumekufufua hivi). Na itazame mifupa (ya punda wako) jinsi tunavyoinyanyua, kisha tunaivisha nyama.” Basi · yalipombainikia (haya yule aliyefufuliwa) alinena: ‘Najua kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza iuu ya kila kitu.”
MAAJABU YA JUMLA YA HERUFI YA KIPANDE CHA AYA HAPA CHINI HIKI 100 NA MIAKA ALIYEFISHWA HUYU MTU NI 100 PIA!!!
Kipande kufuatacho kutoka katika Aya hapa Juu kinashangaza sana
لَّبِثۡتَ مِاْئَةَ عَامٍ۬ فَٱنظُرۡ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمۡ يَتَسَنَّهۡۖ وَٱنظُرۡ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجۡعَلَكَ ءَايَةً۬ لِّلنَّاسِۖ وَٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡعِظَامِ ڪَيۡفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكۡسُوهَا لَحۡمً۬اۚ
Tafsiri ya Kipande hiki ni:
Umekaa (Umefishwa) miaka mia; nawe tazama chakula chako na vinywaji vyako, havikuharibika.Na mtazame punda wako (amekuwa mifupa mitupu iliyolikalika). Na ili tukufanye uwe hoja kwa watu (ndio tumekufufua hivi). Na itazame mifupa (ya punda wako) jinsi tunavyoinyanyua, kisha tunaivisha nyama.
SHEREHE NA MAAJABU YA HERUFI 100
Kipande hiki Kinazungumzia Maneno Ya Mwenyeezi Mungu Yenye Kumfahamisha Mtu huyu kwamba Ulikuwa Umefishwa kwa muda wa miaka 100 Moja na pia Jambo la kushangaza ni kwamba Chakula chake alichokuwa amebeba kiko vile vile yaani hakikuoza baada ya muda wote huo, na akaonyeshwa wakati huo huo alipofufuliwa namna Punda wake anavyofufuliwa. Mbele ya macho yake. Namba Mifupa ya huyo punda inavyokusanywa na Kuvishwa nyama. Angalia Muujiza Huu Siyo Mdogo.
Jambo lingine la maajabu ni kwamba Kipande hiki cha Aya kinachosema kwamba mtu huyu alifishwa kwa muda wa Miaka 100 kina Herufi pia 100. (100 Arabic Alphabet). Haya siyo madogo.
Mwenyeezi Mungu anatujuulisha kisa hiki na kisha leo hii tungundua hata Herufi pia zimehesabiwa kuwa 100 pia kama hiyo miaka aliyofishwa huyu mtu.
KWA NINI HUYU MTU ALIFISHWA MUDA WA MIAKA 100
Mwenyeezi Mungu anajibu suala hili katika Aya hii kwa kusema:
وَلِنَجۡعَلَكَ ءَايَةً۬ لِّلنَّاسِۖ
Ili uwe Hoja kwa watu. Yaani watu wakisikia habari hii basi watapata fundisho. Na watajua Kwamba Mwenyeezi Mungu Yupo na Ana uwezo Mkubwa
KISA KUTOKANA NA VITABU VINGINEVYO
Kuruani haikutuelezea Sehemu, Tarehe na Jina la huyu mtu.
Kufuatana na Maelezo mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali tunapata kauli zifuatazo:
KAULI YA KWANZA
Mtu Huyu na wenziwe wa zama zake walikuwa wakikataa katakata kuwa viumbe watafufuliwa.
Waliona kuwa jambo hilo ni muhali kabisa. Basi Mwenyezi Mungu allmwonyesha Mtu huyu hayo katika nafsi yake ill ende akawahadithie hao wenziwe waliokuwa pamoja na yeye, na yeye akawa mkubwa wao.
KAULI YA PILI
Inasemekana kwamba huyu alikuwa Mtume aliyekuwa katika zama zao na alitaka apate yakini bali aliamini Mungu na hakuwa kafiri. Alitaka uhakika.
Na Inasemekana kwamba Huyu ndiyo Uzayr ambaye ametajika katika Kuruani.
Baadhi ya Mayahudi walikuwa wakidai kwamba huyu ni mtoto wa Mwenyeezi Mungu.
Mfano wake ni sawa na Wakristo wa leo wanaodai kwamba Yesu ni mtoto wa Mungu. Kuruani imesema haya kwamba Mayahudi wamesema kwamba Uzair ni mtoto wa Mungu na Wakristo wamesema kwamba Yesu (Isa ni mtoto wa Mungu).
Wenye kudai hii kauli wanasema kwamba huyu Uzair ndiyo Ezra ambaye ametajika katika Biblia na Aliishi baada ya Nabii Musa.
Ibn Kathir ametaja Kwamba Huyu Uzair aliishi katika kipindi baina ya Nabii Suleyman na Zakariah (Zakariah aliyekuwa baba yake Nabii Yahya).
KAULI YA TATU
Kuna Kauli ya Tatu inayosema kwamba alikuwa Siyo Nabii lakini Walii (Mcha Mungu). na alikuwa mtu wa Hekima na Busara kubwa.
KISA NA SABABU YA KUSHUKA AYA HII
Tunasoma pia kwamba Ezra alikwenda katika Shamba lake kama kawaida yake alivyokuwa akifanya.
Ilipofika mchana alifika katika Mji katika sehemu iliyokufa, iliyokuwa haina watu, iliyoonyesha imehamwa na watu wote. Nyumba zote zimeoza na hakuna uhai wowote uliobaki.
Akashuka kutoka katika punda wake, akachukua Zabibu na Matini aliyokuwa amebeba na akakaa chini ya Mti ili apate kula.
Katika wakati huo akaona Mifupa ya Zamani sana ambayo ilikuwa imesambaa karibu naye na hapo akafikiri na kujisemeza
” Kwa Vipi Mwenyeezi Mungu ataweza kuumba tena Kiumbe kutokana na Mifupa hii?
Yaani kwa vipi Mwenyeezi Mungu ataweza kurudisha uhai wa Kiumbe hiki kutokana na Mifupa hii ambayo imeoza na kukauka miaka na miaka?
Hili ndilo suala alilojiuliza Huyu Bwana Ezra.
Huenda alitamani Ajue ukweli ili kuzidisha imani yake kwani alikuwa Walii au Mtume Mcha Mungu.
Kwa wakati huo huo Mwenyeezi Mungu akamtuma Malaika na Kuja Kumtoa Roho.
Akafishwa kwa muda wa miaka 100 na kisha akafufuliwa tena ili iwe Muujiza.
Mwenyeezi Mungu akamwuuliza baada tu ya Kumfufua kama ilivyo katika Aya hii
قَالَ ڪَمۡ لَبِثۡتَۖ قَالَ لَبِثۡتُ يَوۡمًا أَوۡ بَعۡضَ يَوۡمٍ۬ۖ قَالَ بَل لَّبِثۡتَ مِاْئَةَ عَامٍ۬ فَٱنظُرۡ إِلَىٰ طَعَامِكَ وَشَرَابِكَ لَمۡ يَتَسَنَّهۡۖ وَٱنظُرۡ إِلَىٰ حِمَارِكَ وَلِنَجۡعَلَكَ ءَايَةً۬ لِّلنَّاسِۖ وَٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡعِظَامِ ڪَيۡفَ نُنشِزُهَا ثُمَّ نَكۡسُوهَا لَحۡمً۬اۚ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ ۥ قَالَ أَعۡلَمُ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ ڪُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬
Umekaa (Umekufa)kwa muda gani? Akajibu Siku Moja au Baadhi ya Siku. Mwenyeezi Mungu akamwambia Hapana bali Umekaa (Umekufa) Miaka 100 Moja.
Akamwambia aangalie chakula chake ambacho bado kuzuri na hakikuoza.
Huu ni Muujiza kwani Chakula chake kimetunzwa na Mwenyeezi Mungu kwa muda wa miaka 100 Moja. (Leo hii hebu tufikiri kuna Fridge gani unaweza kutunza chakula kwa muda wa miaka 100 moja!!!! Binaadamu bado hatuna uwezo huo kwani bado tunahangaika hangaika).
Kisa kinaendelea kwamba Ezra Akamchukua Punda wake na kuruni Nyumbani kwake.
Watu katika Mji wake hakuna aliyeweza kumtambua na hata nyumbani kwake isipokuwa Mfanyakazi wa kike ambaye ni Bibi Kikongwe sana zaidi ya Miaka Mia Moja huyu alimtambua Ezra. Ezra Akamhadithia Yule bibi jambo lililomtokea lakini Hata hivyo Bibi Yule alikuwa na shaka kama ni Kweli huyu ndiye yule Ezra aliyekuwa Nyumbani.
Na isitoshe Ezra alipofishwa alikuwa na miaka 40 na baada ya miaka 100 alifufuliwa akiwa na miaka 4o kama hapo zamani, Kwa hiyo alionekana Kijana.
Huyu Bibi alitia shaka kwani itakuwaje Ezra baada ya Miaka 100 kuwa bado anaonekana Kijana.
Kwa hiyo akamuuliza Ezra amuombee Dua ili apate kupona Macho kwani alikuwa haoni na kumponesha maradhi mengineyo.
Huyu Bibi alipoteza Macho kwa uzee. Na alimuuliza amuombee dua kwani Hapo Zamani Ezra alikuwa Dua zake zinakubaliwa na huyu Bibi alikuwa bado anakumbuka. Sasa akampa Ezra Mtihani iwapo kweli ndiyo huyo Ezra aliyemjua hapo zamani.
Ezra Akaomba Dua na mara Bibi huyo akapona Macho ,akapona maradhi mengineyo na akaweza kutembea tena. Ezra alimwambia “Inuka kwa uwezo wake Allah” na akapona.
Na hapo Bibi huyu akasema “Sasa naamini kwamba wewe ni Ezra”.
Kisa kinaendela kwamba Mayahudi wengineo walikuja kusikiliza habari hiyo na Mtoto wake Ezra ambaye alikuwa na Umri wa miaka 118 alikuwa hai na pia alitaka uhakika iwapo Huyu ndiye baba yake.
Basi alikumbuka kwamba baba yake alikuwa na alama ya Kipele (Mole) baina ya Mabega yake. Walipomchunguza Ezra wakakuta alama hiyo ipo sehemu hiyo.
Jambo hili kwa kweli ni la kushangaza na Muujiza sio Mdogo.
Bwana Ezra alikuwa wakati huo ana miaka 40 na mtoto wake alikuwa na miaka 118 angalia maajabu.
Yaani Baba ana umri mdogo kuliko Mtoto!!!!
Allahu Akbar. Angalia Maajabu. Huu sio Muujiza wa kushangaza. Allahu Akbar.
Kisa kinaendelea kwamba Baada ya Hapo akawasaidia Mayahudi Kufukua Kitabu cha Taurati ambacho kilikuwa kimefukiwa na Baba Yake miaka mingi iliyopita.
Kwa wakati huo kulikuwa hakuna Taurati kwani Utawala wa Neabuchadnezzar aliyekuwa Mfame aliunguza Taurati Zote.
Baba Yake Ezra aliyekuwa najulikana kwa Jina kama Sakhura alikifukia Kitabu hicho cha Taurati na Hakuna aliyejua Isipikuwa Ezra.
Ezra alikwenda sehemu hiyo iliyofukiwa Maandishi hayo ya Taurati na kuyafukua lakini muda mrefu umepita na kwa hiyo maandishi yalikuwa siyo rahisi kuyasoma. Kitabu kilioza, Ezra akafanya juhudi kuandika tena Taurati kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu.
Mayahudi wanasema Ezra alipewa Nuru na Mwenyeezi Mungu akaweza kuandika Tena Taurati na Kuweza Kuwasadia Mayahudi katika wakati ambao Taurati zote zilichomwa moto.
Na hii ndiyo sababu ambazo Mayahudi wanadai Kwamba Uzair (Ezra) Ni Mtoto wa Mwenyeezi Mungu kwa Haya tuliyoyasoma katika Kisa Hiki.
Na Kuruani Inasema Kuhusu Habari hii katika Aya Ifuatayo:
وَقَالَتِ ٱلۡيَهُودُ عُزَيۡرٌ ٱبۡنُ ٱللَّهِ وَقَالَتِ ٱلنَّصَـٰرَى ٱلۡمَسِيحُ ٱبۡنُ ٱللَّهِۖ ذَٲلِكَ قَوۡلُهُم بِأَفۡوَٲهِهِمۡۖ يُضَـٰهِـُٔونَ قَوۡلَ ٱلَّذِينَ ڪَفَرُواْ مِن قَبۡلُۚ قَـٰتَلَهُمُ ٱللَّهُۚ أَنَّىٰ يُؤۡفَڪُونَ (٣٠)
Sura Ya Al-Tawbah Namba 9 Aya Namba 30
TAFSIRI YA AYA
30.Na Mayahudi wanasema: “Uzeri ni mwana wa Mwenyezi Mungu;” na Wakristo wanasema “Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu”; haya ndiyo wasemayo kwa vinywa vyao (pasi na kuyapima). Wanayaiga maneno ya wale walio kufuru kabla yao, Mwenyezi Mungu awaangamize. Wanageuzwa namna gani hawa!
UFUPISHO WA KISA
1/Kwa kifupi tumeona uwezo wa Mwenyeezi Mungu. Binaadamu anategemea Mwanga katika kutofautisha kati ya Usiku na Mchana na pia katika kuhesabu Masaa, Masiku, Mieza na na Miaka.
2/Huyu Mtu aliyefishwa Macho yake yalikuwa hayaoni Mwanga Mwanga wowote na kwa hiyo hakuweza kutambua muda aliofishwa. Alipoulizwa muda alijibu Siku au baadhi ya siku.
3/Na jambo ka kushangaza pia ni Kufishwa kwa muda mrefu kaka huo yaani miaka 100 na chakula hakikuaribika. Kuumbwa kwa Punda mbele ya Macho yake.
4/Jumla za Herufi za Maneno ya Mwenyeezi Mungu katika Aya ya kisa hiki pia ni 100. Ni Kithibitisho kwamba kisa hiki sio cha kubuni bali ni ukweli.
5/Na alipoona ukweli akajibu “Sasa Nimesoma na Nimeona ukweli kwamba Mwenyeezi Mungu ana uwezo wa kila kitu”
Allahu Akbar.