SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Mazungumzo/Profesa-1

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

NAKUKARIBISHENI KATIKA SAFARI MBALIMBALI

MAZUNGUMZO  BAINA YANGU NA PROFESA ALIYEKUWA MUHANDISI  (ENGINEER) KATIKA MECHANICS HUKO  CAIRO (EGYPT)

Al-Hamdililah leo  Tarehe   16/09/2022. Namshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kutupa uzima kuweza kuendelea kuandika haya machache.

Mwenyeezi Mungu akipenda ningependelea  siku ya leo na siku chache zijazo  kuwaletea wasomaji wote wa Website hii  Mazungumzo baina yangu na Profesa Mbalimbali ambao kwa bahati nilipata kuzungumza nao Asili ya Ma Profesa hawa ni kutoka  Misri (Egypt), Syria, Sudan, Algeria, Jordan, Yemen na sehemu Nyinginezo mbalimbali za Dunia.

Umri wa Profesa hawa sio mdogo baadhi yao wana miaka 80 na wengine  zaidi ya 80.  Na pia kuna Wengine Vijana.

Nilipendelea  kukutana na Profesa  Wazee kwani  nadhani wamekula Chumvi nyingi na Hao  wamejaa Elimu mbalimbali za kidunia. Nami nilikuwa na Maswali mengi katika Kuruani Tukufu. Profesa hawa wote wamefanya Utafiti mbalimbali katika Kuruani na Hadithi za Mtume. Kwa hiyo  Milango  inyokuja itahusu Mazungumzo  baina yangu na Wanavyuoni hawa.

Siku ya Leo Mazungumzo yatahusu  Profesa ambaye Asili yake Kutoka Egypt-Cairo. Mazungumzo yalifanyika kwa Lugha ya Kiarabu. Na nimefasiri kwa Kiswahili na kama kawaida Kuna Nyongeza na Pungufu katika Maandishi lakini Muhimu ni Madhumuni ya Mazungumzo Haya. 

Kabla ya kuleta mazungumzo hayo ningependelea kusema kwamba hapa ninapokaa ninasikia  makelele ya  watoto ambao nje ya nyumba yangu wanaendesha  Baiskeli  za Gurudumu moja na kwa kweli inanikera sana kwani makelele hayo yananizuia utulivu wa Fikra zangu katika kuandaa website hii.lakini ni watoto wadogo na kwa hiyo  nitawasamehe kwa leo kwani Jua limechomoza na kwa kawaida hupenda kucheza cheza barabarani. Na Pia sisi tulipokuwa Umri  wao tulifanya  hivyo hivyo.

Mbele yangu kuna Dirisha la kioo na ninaweza kuona Nje ya nyumba Matawi ya Mti mkubwa ambao yanatingishwatingishwa na Upepo mkali. Ni wakati ambao majani yananguka kwa wingi.

Kuanguka kwa majani kunanikumbusha Kauli Ya Mwenyeezi Mungu Sura Namba 6  Aya Namba  59 inayosema:

۞ وَعِندَهُ ۥ مَفَاتِحُ ٱلۡغَيۡبِ لَا يَعۡلَمُهَآ إِلَّا هُوَ‌ۚ وَيَعۡلَمُ مَا فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ‌ۚ وَمَا تَسۡقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعۡلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ۬ فِى ظُلُمَـٰتِ ٱلۡأَرۡضِ وَلَا رَطۡبٍ۬ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِى كِتَـٰبٍ۬ مُّبِينٍ۬ (٥٩)

TAFSIRI

59. Na ziko kwake (Mwenyczi Mungu tu) funguo za siri; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na anajua yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani ila analijua. Wala (haianguki) punje katika giza la ardhi · (ila anaijua). Wala (hakianguki) kilichorutubika wala kilichoyabisika (ila anakijua). (Hapana cho chote), ila kimo katika Kitabu kidhihirishacho (kila jambo).

Kwa kweli Aya hii  inaonyesha uwezo wa Mwenyeezi Mungu. Yaani  kila kinachofanyika  Ulimwenguni  anakijua yaani hakuna asichokijua. Na pia  Kila kitu kimo ndani ya Kuruani.

Samahani ndugu msomaji nitasimama  hapa kwani lengo la leo  ni kuwaletea Mazungumzo baina yangu na Profesa kwa hiyo  tuanze.

Kwanza ningependelea kuwajuulisha kwamba Profesa huyu alinikaribisha kwake. Na nilifurahi sana kukaribishwa na kuweza kukutana naye kwa mzungumzo ambayo  yalikuwa mazuri sana tena sana.

Tulizungumza mambo mbalimbali  ambayo nitachagua baadhi yake ambayo muhimu zaidi na pia kwa ajili ya wakati wenu na pia wangu.

Tulizungumza kuhusu  

1/Kukutana  na Majini

2/Namba za Ukorofi

Ne Miujiza Mingineyo  ikiwezekana.

Ndugu Msomaji fuatilia mazungumzo haya kwa  utulivu lakini ingelikuwa bora  Utayarishe  Chai na Keki kisha usome mazungumzo haya yasiyo na mwisho kwa   Raha Yako.

AL-AMIN ALI HAMAD: Hodi , Hodi  Hodi. Hodi Profesa. Profesa, Je Upo? Hodi.

(Sauti  ya Kufunguliwa kwa Mlango)

PROFESA:Karibu  Ndugu  Al-Amin 

AL-AMIN ALI HAMAD: Salaam Nyingi  zikufikie na Baraka zake Mwenyeezi Mungu (Asalaama Alaykum Warahmatullwahi Wabarakatuh).

PROFESA:Na wewe pia Salaam nyingi za Rahema na baraka ziwafikie (Waa’laykum Asaaalaam Warahmatullahi Wabarakatu Ndugu  Al-Amin  vipi  hali? Miaka mingi imepita tangu tukutane.  Nimefurahi sana tena  sana kukutana tena. Alhamdulilah leo siku kubwa. Nashukuru kwa Mwenyeezi Mungu kutupa Uzima na Afya mpaka Leo

AL-AMIN ALI HAMAD: Asante sana Profesa kwa kweli nimefurahi  kuliko wewe ulivyofurahi. je vipi hali?

PROFESA:Hali mzuri Alhamdulilahi. Nimekualika tupate kuzungumza mambo mbali mbali yanayohusu  Kuruani na Dini. lakini kabla ya hapo ningependelea upumzike  kidogo. Ndugu Al;-Amin ungependelea  kinywaji gani?

AL-AMIN ALI HAMAD:Asante sana kwa kweli  usijihangaishe kabisa kwa matayarisho yeyote makubwa. Kahawa ingetosha.

PROFESA: Unaonaje Kahawa na Tende?

AL-AMIN ALI HAMAD:Mwenyeezi Mungu akubariki hiyo inatosha.

AL-AMIN ALI HAMAD: Asante sana, Tende hizi tamu sana zimetoka wapi?

PROFESA:Hizi ni tende za Madina  huko  alipozikwa Mtume Mohamad. (Saudi Arabia) Mwenyeezi Mungu Amsalie.

AL-AMIN ALI HAMAD: Asante sana kwa makaribisho asante sana. mwenyeezi Mungu Akubariki. Kama ulivyonijuulisha kwamba  Kuna Masuala Mawili  ambayo   ungependelea kuzungumza na pia Mengineyo  ikiwezekana. Je ni  yapi hayo?

PROFESA: Ningependelea tuanze kuzungumzia mambo mawili  nayo ni:

1/Kukutana na Majini

2/Namba za Ukorofi

Na Miujhiza Mingineyo  Ikiwezekana  

AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa Inatisha  sana habari ya majini. Yaani unataka kunikutanisha na Majini?  Yaani leo hii?

PROFESA: Naam. Ndiyo hivyo  Al_Amin

AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa Mimi naogopa sana jambo hili. Ningeone bora  tuanze  na Namba za Ukorofi na Hiyo Ziyara ya  Majini  tufanye mwisho. kwa kweli inatisha. Nipe Muda. 

Eeeeeeeee  bwana Wee  Majini Yanatisha. Tuifanye iwe Topic (Vipengele)ya Mwisho.

PROFESA: Al-Amin sawa bwana  tufanye hivyo. Tuanze na namba za Ukorofi.  Je unazijua?

AL-AMIN ALI HAMAD: Namba za Ukorofi sizijui? Tafadhali Nifahamishe.

PROFESA:Namba za Ukorofi ni Odd Numbers na Namba sizizo na Ukorofi ni Even Numbers. Je unakumbuka haya mambo wanafundishwa watoto katika Shule za Msingi.

AL-AMIN ALI HAMAD: Ahhhhh  ninafahamu  ODD  na Even Numbers. Unaziita ODD numbers  ni namba za Ukorofi?  kwa nini Namba za Ukorofi? na kwa nini Even Numbers Namba zisizo na Ukorofi?

PROFESA: Namba  za Odd ni kama vile  1, 3, 5, 7, 9, 11

na kuendelea yaani  13….

na Namba Even ni kama vile   2, 4, 6, 8, 10  Na kuendelea.  yaani    12, 14….Na kuendelea kama vile 16, 18…..

Namba Odd ni zile ambazo  hazigawanyiki katika mafungu mawili  ya sawa kama vile namba  3  huwezi kugawanya na namba 2 na ukifanya hivyo basi utapata mabaki ya namba 1  na hivyo hivyo huwezi kugawa namba 11  na ukifanya hivyo yaani kugawa mafungu mawili basi utapata mafungu mawili ya namba 5  na  mabaki yaani masalia ya namba 1

lakini Even Numbers zinagawanyika  mafungu mawili na hakuna Masalia au mabaki. Kwa mfano  unaweza kugawa namba 4  katika mafungu mawili ya namba 2 na hakuna masalia au mabaki. Na namba  8 pia unaweza kugawa katika mafungu mawili ya namba 4 bila  ya Masalia au mabaki. Je umefahamu  maana ya Namba  za Ukorofi na zisizo na ukorofi?  Kwa hiyo namba  za Odd ni zile namba zenye Ukorofi yaani zinakataa kugawanywa katika mafungu mawili na namba za Even ni namba sizizo za ukorofi  kwani zinakubali kugawanywa katika mafungu mawili bila tatizo

AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa  leo hii sikutegemea  Utanielezea  habari za Namba  za ukorofi kwani ni  masomo ya watoto  wadogo yaani shule za Msingi. Nilitegemea kunifundisha mambo ya wakubwa na wewe ni Profesa mkubwa. Yaani sikutegemea…. Mimi  nina  Diploma za Vyuo vikuu naona Mazungumzo  haya ni ya watoto wadogo.

PROFESA: Ndugu Al-Amin  usidharau Elimu. Elimu ni Elimu hakuna ya watoto au wakubwa. Haya ninayokuelezea siyo madogo hata kidogo.

AL-AMIN ALI HAMAD: Je kuna Makubwa? 

PROFESA:Nisikilize  vizuri. Fungua Masikio. Kwanza  Je unataka Kahawa kisha tutazungumza?

AL-AMIN ALI HAMAD: Asante Sana kwa kahawa. Kisha Nielezee zaidi Siri ya haya makubwa.

PROFESA: Mimi  sizungumzi  upuuzi. Nimefanya Utafiti katika Kuruani Miaka 40  na Nimefanya utafiti wa Kuruani na Hadithi za Mtume si chini ya Utafiti  Elfu 10.  Sikukukaribishi nikupotezee wakati bure bure nisikilize vizuri haya nitakayokuambia leo hii:

AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa nina hamu sana ya kuelewa tafadhali niambie. nahamu sana kusikiliza habari za Kuruani.

PROFESA:Hebu Tuichunguze Sura Ya Al-Masad au  Abi Lahab katika Kuruani.

Sura Al-Masad, Tafsiri Na Sherehe yake hapa chini:

سُوۡرَةُ لهب / المَسَد

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ۬ وَتَبَّ (١) مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُ ۥ وَمَا ڪَسَبَ (٢) سَيَصۡلَىٰ نَارً۬ا ذَاتَ لَهَبٍ۬ (٣) وَٱمۡرَأَتُهُ ۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ (٤) فِى جِيدِهَا حَبۡلٌ۬ مِّن مَّسَدِۭ (٥)

TAFSIRI

I.Pana kuangamia mikono miwili ya Abu Lahab! Naye amekwisha angamia.

2. Hayatamfaa mali fake wala alivyovichuma.

3. (Atakapokufa) atauingia Moto wenye mwako (mkubwa kabisa)

4. Na mkewe, mchukuzi wa kuni (za fitina), (fattani, anayefitinisha watu wasiingie katika dini; atauingia naye Moto huo) ·

5. (Kama kwamba) shingoni mwake iko kamba iliyosokotwa (anayochukulia kuni za fitina hizo).

SHEREHE

Sura Hii  ilishushwa kwa ajili ya Ami (Uncle) yake Mtume  ambaye alimfanyia UKOROFI  mtume. Hapo mwanzo  wa kupewa Utume Bwana wetu Muhammad (s.a.w.) aliamrishwa awabashirie jamaa zake walio karibu naye kwa kizazi; akawakusanya akawabashiria na kuwakhofisha na adhabu ya Akhera, Abu Lahab, Ami yake, akakasirika, akamwambia ‘Mwana kuangamia wee! Ndilo ulilotwitia hili?’ Ndipo iliposhuka sura hii kuapizwa Abu-Lahab na mke wake, Ummu-jamil, aliyekuwa akijipinda sana katika kumuudhi Mtume, na kuwashakiza makafiri wamuue na kufanya kila aliwezalo katika kuizuilia dini isifuatwe. “Yana kuangamia mikono miwili ya Abu-Lahab!” ni maapizo ya kuapizwa Abu-lahabi aangamie yeye, badali ya Mtume (s.a.w.). Na alipokuwa Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuapiza, imekuwa hapana shaka maapizo hayo tu yenye kumpata, na kwa hivyo Mwenyezi Mungu anatupa habari kuwa “amekwishaangamia.” Huyu mke wa Abu-Lahab alikuwa Msengenyaji(sakubimbi). Kazi yake kuchukua maneno ya huku akipeleka huku kwa  kutia fitina na fisadi. Na mtu namna hii Waarabu humshabihisha na “mchukuzi wa kuni.” Na dasturi, mchukuzi wa kuni huwa na “kamba” katika shingo yake ya kufungia hizo kuni zake, na kuni ndizo zinazowasha moto. Na huyu mwanamke akiwasha moto wa kuwazuilia watu wasisilimu na kuwatoa waliosilimu

PROFESA:Kwa hiyo  Bwana Abu Jahl na Mkewe walikuwa Wakorofi.

AL-AMIN ALI HAMAD:Ahhha sasa nimeanza kukuelewa kidogo. lakini  bado nina swali.Ulinielezea kuhusu  Namba za Ukorofi yaani  ODD NUMBERS  na sasa Sura Ya Al-Masad unasema Bwana  Abu Jahl ambaye Sura Hii ilishushwa kawa ajili yake alikuwa pia Mkorofi  na Mke wake pia.  Lakini  kuna uhusiani gani kati ya Namba za Odd na Sura Hii?

PROFESA:Fanya Subira. Kidogo kidogo.,Wazungu wanasema Step by Step  Na Waswahili wanasema  Haraka Haraka haina Baraka. Kwa hiyo  wewe nisikilize tu. Wewe umekuja Kwangu kwa hiyo niache nikueleze mambo  usiyoyajua.

AL-AMIN ALI HAMAD: Asante Profesa. Mungu akubariki.

PROFESA:Mwenyeezi  Mungu  ameshusha Sura Hii  kiajabu sana. Ni Sura Ndogo lakini ina miujiza isiyo na Mwisho

AL-AMIN ALI HAMAD: Allahu  Akbar. Allahu Akbar.

PROFESA: Hebu Nianze. Sikiliza kwa makini  miujiza ifuatayo katika Sura Hii:

Kwanza  Sura Hii ni Namba 111  na namba  hii ni ODD yaani kama kusema kwamba Namba hii ni namba Ya Ukorofi. Yaani Ukijifanya Mkorofi basi Mwenyeezi Mungu ana Ukorofi zaidi. Ndiyo maana yake. na kwa hiyo ameipanga katika kuruani namba 111

AL-AMIN ALI HAMAD:Hiyo  tu. Mimi sioni Muujiza wowote

PROFESA: Nimekuambia Usiharakishe. Subiri  huu siyo Muujiza Mdogo

AL-AMIN ALI-HAMAD: Samahani  nitasubiri. Profesa endelea.

PROFESA: Sura Hii ina Aya 5 na Hii namba 5  ni Namba ODD yaani Namba ya Ukorofi

Angalia  sasa tuchunguze  Jumla ya Herufi katika Kila Aya ya Sura Hii.

Aya ya Kwanza ina Herufi   15  ambayo ni Namba ODD

Aya ya Pili ina Herufi  19  na hii ni Namba ODD

Aya ya Tatu  ina Herufi  15  na hii ni Namba ODD

Aya ya  Nne ina Herufi  17 na hii ni namba ODD

Aya ya Tano na ni ya Mwisho  ina Herufi 15 na Hii ni Namba ODD

Yaani Jumla ya Herufi katika Kila Aya Ni ODD yaani Ukorofi kama Ukorofi wa yule  aliyeshushiwa hizi Aya yaani  Abu Lahab na Mkewe.

AL-AMIN ALI HAMAD:Allahu Akbar. Profesa  Umenipa Mambo Mapya. Allahu Akbar.  Je ni haya tu?

PROFESA: Tulia. Usiharakishe kwani sijamaliza. Subira yavuta Heri.

AL-AMIN ALI HAMAD: Samahani Profesa siharakishi bali nina hamu ya kuelewa zaidi. Nakusikiliza.

PROFESA: Kwa kweli  haina mwisho usifikiri nakudanganya. Nimesema

Aya ya 1 ina Herufi 15

Aya ya 2 ina Herufi 19 

Aya ya 3 ina Herufi 15

Aya ya 4 ina Herufi 17 

Aya ya 5 ina Herufi 15

Tumeona  Odd Numbers za Herufi  sasa angalia kwa makini  Namba za Aya. Angalia Namba za Aya zenye Herufi  15  utaona Namba  1  ni ODD, Ya 3  ni ODD  na Ya mwisho  ni ODD  pia

Angalia Mpango  wa kushangaza. Angalia Maajabu je binaadamu anaweza kupanga mfano  huu? Je unaona Mwenyeezi Mungu alivyoshusha. Sikiliza Al-Amin  Hatujamaliza niache Niendelee na Safari isiyo na Mwisho. Ebu angalia Namba za Ukorofi  zilivyopangwa katika Kuruani. Ikiwa mtu anajifanya Mkorofi basi ujue Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa Ukorofi. Ukijifanya Mjanja basi  yeye ndiye mwenyewe aliye Mjanja  pia kuliko wewe. Kaishusha Sura Hii na Maajabu. Ukorofi kwa ukorofi. Abu Jahl na Mkewe kashushiwa Aya za kulingana na Ukorofi wake. Hebu tuendelee kama nilivyosema hakuna Mwisho.

AL -AMIN ALI HAMAD: Yaani Hatujamaliza?

PROFESA: Tupo Mwazoni. Bado  sana kama nilivyosema hakuna mwisho.

AL-AMIN ALI HAMAD:  Allahu Akbar

PROFESA:Kuhusu  ODD numbers au Namba za Ukorofi kuna mengi mengineyo  kama ifuatavyo:

SURA HII INA MANENO  23 NA NAMBA HII NI ODD

SURA INA HERUFI  81  NA NAMBA HII NI ODD

JINA LA SURA NI المَسَد  (MASAD) LINA HERUFI 5 NA NAMBA HII NI ODD

JINA المَسَد UKILIGEUZA KATIKA NAMBA ZA ABJAD YAANI THAMANI YA HERUFI ZILIZOTUMIKA KATIKA ENZI YA MTUME KWANI WALIZITUMIA KAMA NAMBA BASI UTAPATA JUMLA YA HERUFI NI 135 NA NAMBA HII NI ODD

JUMLA YA HERUFI  ZA KIARABU NI 28 NA JUMLA YA HERUFI ZILIZOTUMIKA KATIKA SURA HII NI 21 NA NAMBA HII NI ODD

AYA ZOTE 5 ZA SURA HII UKIZIGEUZA KATIKA THAMANI YA ABJAD YAANI THAMANI YA HERUFI ZILIZOTUMIKA KATIKA ENZI YA MTUME KWANI WALIZITUMIA HERUFI KAMA NAMBA BASI UTAPATA JUMLA YA HERUFI ZA SURA HII NI 5431 NA NAMBA HII NI ODD

AL-AMIN ALI HAMAD: Allahu Akbar.  Allahu Akbar. Kwa kweli  siyo mambo madogo. Kwa kweli inatisha. Hebu fikiri ukaidi tunaoufanya katika maisha yetu? Ndiyo maana  Maisha yamejaa matatizo. kwa ajili ya Ukorofi wetu na Mwenyeezi Mungu Mkorofi zaidi yetu. Hii Sura haikushuka Bure. Allahu Akbar. Kumbe kuna Siri kubwa namna hii. Haya siyo madogo  hata kidogo. Profesa  Haya mambo kweli makubwa sana.

PROFESA: Haina Mwisho. Kama nilivyosema kwani kuna Ya Ajabu Zaidi  wewe nisikilize  tu.

AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa  hizi Elimu unazijua   vipi? umesoma wapi

PROFESA: Huko  kwetu Arabuni  kuna wanavyuoni  wanaofanya Utafiti Usiku na Mchana kwa juhudi kubwa sana na kisha Wanasahishishana  kama kuna Makosa katika Utafiti.

AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa Mwenyeezi Mungu akuzidishie  Elimu. Asante Sana kwa Kunikaribisha na kunipa Habari Nzuri Sana

PROFESA: Sijamaliza kwani bado ndiyo mwanzo. Hii Sura ina Mengi. Ukiingia Usiku  basi utalala Kwangu usiwe na wasiwasi.

AL-AMIN ALI HAMAD: Asante sana Profesa. Nitasubiri. Waswahili wanasema “Mtaka cha Uvunguni Sharti Ainame”  basi mimi nitafanya Uvumilivu kwani kwa kweli nina hamu sana ya kusoma Elimu hii kubwa. Allahu Akbar.

Lakini Kuna Mtu Mmoja alisema  “Mwenye Kutaka Cha Uvunguni basi Inua Tanda”  Huyu aligeuza Msemo. Ana  maana ya Kusema Mwenye Kutaka Cha Uvunguni basi Ainue Kitanda yaani Asiiname.  Ha ha   ha ha ha  ha ha ha ha. Huu Ni Utani. Yaani Huyu  aliyegeuza hivi ni Mvivu yaani alikuwa hataki kuinama. Ha  ha Ha Ha Haha (kicheko)

PROFESA: Na sisi Pia kwetu tunapenda kutaniana sana. Watu wanapenda sana Utani baina yao. Kwa mfano wanaposalimiana wanasema 

“KAYFA HALUKA WA ZAMMANI SHOROMBOROM” 

Je unajua maana yake? Yaani  “VIPI  HALI KATIKA HAYA MASIKU YA MVURUGO” Yaani masiku ya Taabu Duniani”. Lakini Lugha inachekesha. Neno  SHOROMBOROM ni neno la kuchekesha. Sijui Warabu walilipata Neno Hili wapi.

Asante sana. Sasa Tuendelee Muujiza. 

Hebu Niilete tena Sura Ya Al-Masad tuichunguze vizuri zaidi.

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ۬ وَتَبَّ (١) مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُ ۥ وَمَا ڪَسَبَ (٢) سَيَصۡلَىٰ نَارً۬ا ذَاتَ لَهَبٍ۬ (٣) وَٱمۡرَأَتُهُ ۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ (٤) فِى جِيدِهَا حَبۡلٌ۬ مِّن مَّسَدِۭ (٥)

Hebu  Tuchague maneno ya ODD na EVEN Katika Sura Hii na Kisha Tuone  Maajabu Yasiyo na Mwisho:

Angalia Maneno niliyoyatia Rangi Nyekundu ni Maneno ya ODD kwani  neno تَبَّتۡ  ni la Kwanza  yaani Namba  1, Neno  أَبِى  ni la tatu yaani namba 3  yaani  ODD  na hivyo hivyo mpaka Mwisho  kwa hiyo  Jumla ya maneno ODD katika Sura Hii ni maneno  12  na Jumla ya Maneno  yaliyobaki ni  EVEN  nayo ni  11

Sasa angalia Muujiza ufuatao:

Ukigeuza maneno  ya ODD katika Namba za Kiarabu  za ABJAD  hapo zamani (kwani walitumia  Herufi kama namba) na kisha ukajumlisha utapata Jumla ni  3049  na Ukigeuza Maneno 11 ambayo yapo katika sehemu (Position)  ya EVEN  Numbers katika Namba za ABJAD utapata Jumla ni 2382

Yaani  ODD=3049  na EVEN =2382

Angalia Maajabu Jumla ya Maneno ODD  namba  tuliyopata ni ODD pia nayo ni 3049  

Na Jumla ya Maneno ya EVEN  Numbers tuliyoyapata ni  EVEN  pia nayo ni  2382

Angalia Maajabu. Katika Kuruani Kila Kitu  Kimehesabiwa. 

Tumehesabu na Kujumlisha Thamani ya Maneno yaliyokuwa ODD tumepata namba ODD na Tumehesabu na kujumlisha Thamani ya Maneno  yaliyokuwa EVEN  na tumepata Namba ya EVEN.

AL-AMIN ALI HAMAD: Allahu Akbar. Haya Maajabu hayana mwisho. Hakuna Mwisho. Allahu Akbar. Hivi Tutamaliza Sura Hii  Leo?

PROFESA: Haiwezekani kabisa. Hakuna Mwisho. Mwenyeezi Mungu Mkubwa.Hii ni Lugha Yake. Inashangaza sana. Allahu Akbar.

Tumeona maneno ya ODD na EVEN  hapo juu yanavyoshangaza. Sasa Tufanye hivyo hivyo na Herufi. Ngoja Nilete zile Aya za Sura Hii ya Al-Masad  kisha Tugawe herufi za ODD na EVEN tuone Maajabu yasiyo na Mwisho:

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ۬ وَتَبَّ (١) مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُ ۥ وَمَا ڪَسَبَ (٢) سَيَصۡلَىٰ نَارً۬ا ذَاتَ لَهَبٍ۬ (٣) وَٱمۡرَأَتُهُ ۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ (٤) فِى جِيدِهَا حَبۡلٌ۬ مِّن مَّسَدِۭ (٥)

Herufi  ODD  ni  TAA  ya kwanza, Kisha TAA inayofuata yaani ya Tatu,  kisha DAL  yaani herufi  ya 5 na ukigechagua Herufi zote hivi mpaka mwisho  na Kisha Uzigeuze katika Thamani Ya Herufi zilizotumika Hapo Zamani. (Waarabu na Mataifa mengineyo  hapo zamani walitumia Herufi kuwakilisha Namba kwa mfano  Alif ilikuwa ikiwakilisha Namba 1, Baa  ilikuwa ikiwakilisha namba 2  na hivyo  hivyo namba zote ziliwakilishwa na Herufi). Ukifanya Hivyo kisha ujumlishe Thamani ya Herufi Hizi utapata Jumla yake   ni  3049.  Na ukifanya hivyo na Herufi za ODD  kwa mfano  Herufi  EVEN  ya kwanza katika Sura Hii ni BAA  kwani ni ya pili  na  YAA  kwani ni ya Nne. Hivyo hivyo  ukikusanya Herufi zote za EVEN katika Sura Hii kisha uzigeuze hatika Thamani ya Namba  za hapo zamani na kisha ujumlishe basi utapata Jumla ni 2382.

Angalia Maajabu  Ya Namba hizi.

Herufi  ODD tumepata namba  ODD pia  yaani 3049

Herufi  EVEN tumepata namba EVEN pia yaani 2382

Yaani  Mpangilio wa Herufi  za ODD na Jumla ya Thamani yake ni ODD na Pia Mpangilio wa EVEN  tumepata Jumla ya Thamani  yajke EVEN

Hebu  sasa Tulinganishe na Utafiti  wa maneno Tuliyofanya hapa Juu.

Tumesema

Maneno ODD ya Sura Hii Thamani Yake ni 3049

Maneno EVEN  ya Sura Hii Thamani Yake ni 2382

Na sasa  Herufi pia inalingana

Herufi  ODD  ya Sura Hii  Thamani Yake ni  3049

Herufi  EVEN ya Sura Hii Thamani Yake ni 2382

Hebu Tushangae.  Allahu Akbar. Mbona Namba za Maneno na Herufi  Zinalingana?  Angalia Muujiza?

AL-AMIN ALI HAMAD: Ma Profesa  wa Vyuo Vikuu Ukiwaonyesha Haya watabaki watashangaa sana. Hebu angalia Maajabu. Huu Muujiza Mkubwa sana. ODD  number ya Maneno  na Herufi  tu inatutoa Povu  Mdomoni.  Profesa  Ninakuomba  Tunywe Kahawa na Ikiwezekana Uniletee zile Tende Za Madina kwani  Mambo  haya Yahitaji Nguvu Mpya . Profesa Umetoa Kubwa Na Ninahitaji  Nguvu Mpya..  Unajua Haya Mambo makubwa sana tena sana.

PROFESA:Ndugu Al-Amin Haya  ni Tonye la Bahari, Kuna mengi yanakuja. Ngojea nilete Kahawa na tende. Nisubiri.

AL-AMIN ALI HAMAD: Asante Sana Profesa Tende  hizi tamu sana. Leo siwezi kulala  kwani Nikinywa kahawa huwi silali. Lakini  Nitakuwa nikifikiri  haya uliyonifundisha.

Kwa vipi? Jumla Maneno Ya ODD  tumepata  namba ODD na Jumla ya maneno ya EVEN tumepata Namba  Even. Na  hivyo hivyo  Jumla ya Herufi pia. Yaani Jumla ya Herufi  ODD tumepata Namba ODD na Jumla Ya Herufi  EVEN tumepata namba EVEN.  Na Ajabu Ni  kwamba Jumla  ya Herufi na Maneno  ODD  ni ile ile  3049 na  Jumla ya Herufi  na Maneno  EVEN ni ile ile 2382.  Angalia Ilivyopangwa. Heiwezekani Binaadamu  kuhesabu na kupanga hivi.

Ngoja Nifupishe na Nipange ili  nione vizuri:

MANENO  ODD=3049

MANENO  EVEN-=2382

HERUFI  ODD=3049

HERUFI EVEN=2382

Allahu Akbar. Angalia  Muujiza. Allahu  Akbar Allahu Akbar.

Hivi Binaadamu anaweza kupanga hivi? Nani duniani anaweza kuandika na kuhesabu mfano huu? Haiwezekani Hata Kidogo. Kuruani  siyo Mchezo.

Profesa Mbona Hakuna Mwisho.  Muujiza baada ya Muujiza katika Sura hii Moja tu. Sasa Je Msahafu? 

Tutafika Huko?

PROFESA: Rafiki yangu hatufiki kabisa. Huko Tunapokwenda kunatisha. Kila kitu kinatisha. Mauti, Makaburini. Yote yanatisha. Kweli siyo uongo, Hatujui lini tutaondoka Dunia, Wapi na Kwa njia gani. Mwenyeezi Mungu ameficha.

AL-AMIN ALI HAMAD: Allahu Akbar. Kwa kweli Inatisha sana tena sana.

PROFESA: Sasa tuendelee na Miujiza  kwani bado mengi ya kuzungumza kuhusu  Sura hii Ya Al-Masad.

Ngojea tuilete ile Sura Tena Ili tuichunguze vizuri zaidi:

تَبَّتۡ يَدَآ أَبِى لَهَبٍ۬ وَتَبَّ (١) مَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُ مَالُهُ ۥ وَمَا ڪَسَبَ (٢) سَيَصۡلَىٰ نَارً۬ا ذَاتَ لَهَبٍ۬ (٣) وَٱمۡرَأَتُهُ ۥ حَمَّالَةَ ٱلۡحَطَبِ (٤) فِى جِيدِهَا حَبۡلٌ۬ مِّن مَّسَدِۭ (٥)

Tumeona kwamba Jumla ya Thamani Ya Maneno Yote Yaliyo katika Sehemu (Position) Ya ODD tumepata Jumla Ya Thamani  yake ni  3049 ambayo namba hii  pia ni ODD  na hivyo hivyo Jumla ya Thamani Ya Maneno Yaliyo katika Sehemu (Position) Ya  EVEN  tumepata Jumla ya Thamani yake ni 2382 na namba hii ni EVEN

Kwa kifupi

POSITION AU SEHEMU YA ODD NUMBER=3049

POSITION AU SEHEMU YA EVEN NUMBER=2382

Sasa  Tupange Namba Zote Tulizopata katika  Sura Hii na kisha Tuchukue Namba ODD na EVEN  kisha Tujumlishe. Hapo Mwanzo tulichukua zile Namba za Positions za Maneno ya ODD na EVEN na hivi sasa tusiangalie Positons au Sehemu ya Maneno bali Namba Peke yake za maneno yote na kisha Tuchunguze namba za Kila Neno na Tuchague  EVEN na ODD.

Ukifanya Hivyo  na kizijumlisha zile Namba  ODD utapata Jumla yake ni 3153  na Ukifanya Hivyo hivyo na Even Numbers utapata Namba 2278

Ngojea nipange vizuri kwa mfano namba zote tulizosoma hapa juu ili tupate kuelewa vizuri zaidi Jumla ya Namba  Tulizosoma katika Aya  za Sura Ya Al-Masad.

MPANGILIO KUFUATANA NA THAMANI AU NAMBA YA MANENO ODD=3153   

MPANGILIO KUFUATANA NA THAMANI AU NAMBA YA MANENO EVEN=2278

MPANGILIO KUFUATANA NA SEHEMU AU POSITION  YA MANENO ODD=3049

MPANGILIO KUFUATANA NA SEHEMU AU POSITION YA MANENO EVEN=2382

Hebu tutoe  Namba  za Hapo Juu. Yaani

3153-3049=104

2382-2278=104

Tumetoa Namba hizi mbili na tunaona Muiano wa Kiajabu.

Majawabu Yanafanana.

Yaani  tunapata namba  104

Ajabu Ni kwamba  Jina La Sura Ni Al-MSAD

Neno Masad Lina  Herufi  Tatu yaani

MIM  +  SIN + DAL

Tukiligeuza Neno Hili katika zile Namba za ABJAD utapata namba 104

40  + 6-0 + 4=104

 Angalia Muashirio wa Kiajabu na Namba 104

AL-AMIN: Profesa  Hii Kweli Inashangaza. Yaani Namba 104 Tuliyopata Hapa Juu inaashiria  Jina La Sura Yaani MASAD.

Kwa kweli Inashangaza.

Kwa nini Muiano Huu Profesa?

PROFESA: Kwa kweli sijui. Huu ndiyo mwisho wa Elimu yangu. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi. Labda Kuna Siri Nyinginezo kwa watu wa Baadaye au labda zina maana Kwa  Majini. Je unajua Kwamba Kuruani wameshushiwa Majini Pia?  Siyo binaadamu Tu  peke yao. Mwenyeezi Mungu amesema katika Sura namba 5  Aya 101 

يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَسۡـَٔلُواْ عَنۡ أَشۡيَآءَ إِن تُبۡدَ لَكُمۡ تَسُؤۡكُمۡ وَإِن تَسۡـَٔلُواْ عَنۡہَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلۡقُرۡءَانُ تُبۡدَ لَكُمۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡہَا‌ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ۬ (١٠١)

Katika  Aya Hii Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na kama mtayauliza, maadamu inateremshwa Qurani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mpole sana.

Huenda Mwenyeezi Mungu ametufichia Siri nyinginezo ambazo  laiti tuzingezilijua huenda ingekuwa Habari mbaya na ingekuwa mbaya kuzijua. Kuna Mengine mengi siyo mazuri kuyajua kwani ni kheri kwetu. 

AL-AMIN ALI HAMAD: Profesa mwenyeezi Mungu akubariki. Unasema Kweli. Lakini tubaki tukifikiri kwani Huu siyo muujiza Mdogo. Allahu Akbar.

PROFESA:Tumezungumzia  Namba za Ukorofi. Na kuna Maudhui (Topic)Nyinginezo bado Kuzianza kama Tulivyopanga. Je unajua Sura Ya Masad Hatujaimaliza Kwani ina mengi. Kwa leo nitaishia Hapa. Mwenyeezi Mungu Akipenda  Kesho Asubuhi  tutazungumza  Safari Yetu  kwa Majini

AL-AMIN AKLI HAMAD: Hii Inanitisha. Sijui kama Nitaweza kulala usiku wa leo. Profesa Una Majini Nyumbani kwako.

PROFESA: Nimekuambia Usiwe na Wasiwasi. Utaona Kesho Maajabu Makubwa. Leo Sahau Na Usiogope. Mimi  Sina Majini Nyumbani Kwangu kwani hiyo siyo kazi yangu. Nimesema Safari kwa Majini yaani Safari kwenda katika Sura Ya Kuruani Inayoitwa Al-Jinn   ili tuweze Kusoma Kisa Kizuri Sana Cha Majini kwa hiyo  unielewe vizuri kwani sina maana kwamba  tutakutana na majini. Tafadhali Nielewe. Yaani Twende Tukaisome kwa pamoja yaani Tusafiri  katrika Sura Hiyo. Nadhani Umenifahamu. Sasa Ngojea Tule Chakula Cha JionI, Tuswali sala Ya Ishaa. Na kisha Tulale. Inshaallah Kesho siku mpya na tutaona mapya. Mola akipenda. 

AL-AMIN ALI HAMAD: Alahamdulilah  Nakushukuru Profesa kwa wema wako Mkubwa Sana. Mwenyeezi Mungu Akubariki akupe Afya, Elimu Kubwa na Umri Mrefu. 

PROFESA:Amin

Mazungumzo (Safari Katika Sura Ya Al-Jinn) yataanza karibuni inshaallah katika  Mlango Huu Huu …………………………..