SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Mengineyo Mbalimbali

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

KUTAJWA KWA UJUMBE ATAKAOPEWA MTUME MOHAMED KATIKA BIBLIA

Huu ni Muujiza mwingine Mkubwa sana. Habari anazotueleza Aisha katika Hadithi hapa chini iliyokusanywa na Imamu Bukhari  inawiana na maneno yaliyopo katika Biblia za leo  lakini uwe macho sana kwani katika Biblia maneno yamebadilishwa na muradi wa maana pia umebadilika. Katika Biblia ya zamani sana tunakuta bado ukweli upo. hapa chini Biblia ya zamani sana iliyoandikwa kwa lugha ya Greek (Hii Biblia ni ya Pili baada ya Codex Vaticanus ambazo zimekusanya Agano la kale na Jipya) maneno yanayohusiana na Ujumbe wa Mtume bado hayajaguswa. Angalia Neno  “HIRAA” bado lipo hivyo hivyo. HIRAA ni pango ambalo alilokuwa Mtume Mohamed akifanya Ibada zake na ambalo Jibril alipozungumza naye kwa mara ya Kwanza. Hapo ndipo Aya za Mwanzo za Sura Ya Alfalaq ziliposhuka.   Hapa chini Nimepigia Mstari Neno  HIRAA  na pia majibu ya Mtume Mohamed. Na pia HIvyo Hivyo nimepigia mstari katika Bible  Isaiah  29:12

Al-Bukhari  Book Number 1 (The Book Of Revelation)

Chapter Number 3

كتاب بدء الوحى 

باب حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ بُكَيْرٍ، قَالَ حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ عُقَيْلٍ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّهَا قَالَتْ أَوَّلُ مَا بُدِئَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم مِنَ الْوَحْىِ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ فِي النَّوْمِ، فَكَانَ لاَ يَرَى رُؤْيَا إِلاَّ جَاءَتْ مِثْلَ فَلَقِ الصُّبْحِ، ثُمَّ حُبِّبَ إِلَيْهِ الْخَلاَءُ، وَكَانَ يَخْلُو بِغَارِ حِرَاءٍ فَيَتَحَنَّثُ فِيهِ ـ وَهُوَ التَّعَبُّدُ ـ اللَّيَالِيَ ذَوَاتِ الْعَدَدِ قَبْلَ أَنْ يَنْزِعَ إِلَى أَهْلِهِ، وَيَتَزَوَّدُ لِذَلِكَ، ثُمَّ يَرْجِعُ إِلَى خَدِيجَةَ، فَيَتَزَوَّدُ لِمِثْلِهَا، حَتَّى جَاءَهُ الْحَقُّ وَهُوَ فِي غَارِ حِرَاءٍ، فَجَاءَهُ الْمَلَكُ فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ قَالَ ‏”‏ مَا أَنَا بِقَارِئٍ ‏”‏‏.‏ قَالَ ‏”‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ قُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ‏.‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّانِيَةَ حَتَّى بَلَغَ مِنِّي الْجَهْدَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ اقْرَأْ‏.‏ فَقُلْتُ مَا أَنَا بِقَارِئٍ‏.‏ فَأَخَذَنِي فَغَطَّنِي الثَّالِثَةَ، ثُمَّ أَرْسَلَنِي فَقَالَ ‏{‏اقْرَأْ بِاسْمِ رَبِّكَ الَّذِي خَلَقَ * خَلَقَ الإِنْسَانَ مِنْ عَلَقٍ * اقْرَأْ وَرَبُّكَ الأَكْرَمُ‏}‏ ‏”‏‏.‏ فَرَجَعَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَرْجُفُ فُؤَادُهُ، فَدَخَلَ عَلَى خَدِيجَةَ بِنْتِ خُوَيْلِدٍ رضى الله عنها فَقَالَ ‏”‏ زَمِّلُونِي زَمِّلُونِي ‏”‏‏.‏ فَزَمَّلُوهُ حَتَّى ذَهَبَ عَنْهُ الرَّوْعُ، فَقَالَ لِخَدِيجَةَ وَأَخْبَرَهَا الْخَبَرَ ‏”‏ لَقَدْ خَشِيتُ عَلَى نَفْسِي ‏”‏‏.‏ فَقَالَتْ خَدِيجَةُ كَلاَّ وَاللَّهِ مَا يُخْزِيكَ اللَّهُ أَبَدًا، إِنَّكَ لَتَصِلُ الرَّحِمَ، وَتَحْمِلُ الْكَلَّ، وَتَكْسِبُ الْمَعْدُومَ، وَتَقْرِي الضَّيْفَ، وَتُعِينُ عَلَى نَوَائِبِ الْحَقِّ‏.‏ فَانْطَلَقَتْ بِهِ خَدِيجَةُ حَتَّى أَتَتْ بِهِ وَرَقَةَ بْنَ نَوْفَلِ بْنِ أَسَدِ بْنِ عَبْدِ الْعُزَّى ابْنَ عَمِّ خَدِيجَةَ ـ وَكَانَ امْرَأً تَنَصَّرَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ، وَكَانَ يَكْتُبُ الْكِتَابَ الْعِبْرَانِيَّ، فَيَكْتُبُ مِنَ الإِنْجِيلِ بِالْعِبْرَانِيَّةِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكْتُبَ، وَكَانَ شَيْخًا كَبِيرًا قَدْ عَمِيَ ـ فَقَالَتْ لَهُ خَدِيجَةُ يَا ابْنَ عَمِّ اسْمَعْ مِنَ ابْنِ أَخِيكَ‏.‏ فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ يَا ابْنَ أَخِي مَاذَا تَرَى فَأَخْبَرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم خَبَرَ مَا رَأَى‏.‏ فَقَالَ لَهُ وَرَقَةُ هَذَا النَّامُوسُ الَّذِي نَزَّلَ اللَّهُ عَلَى مُوسَى صلى الله عليه وسلم يَا لَيْتَنِي فِيهَا جَذَعًا، لَيْتَنِي أَكُونُ حَيًّا إِذْ يُخْرِجُكَ قَوْمُكَ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏”‏ أَوَمُخْرِجِيَّ هُمْ ‏”‏‏.‏ قَالَ نَعَمْ، لَمْ يَأْتِ رَجُلٌ قَطُّ بِمِثْلِ مَا جِئْتَ بِهِ إِلاَّ عُودِيَ، وَإِنْ يُدْرِكْنِي يَوْمُكَ أَنْصُرْكَ نَصْرًا مُؤَزَّرًا‏.‏ ثُمَّ لَمْ يَنْشَبْ وَرَقَةُ أَنْ تُوُفِّيَ وَفَتَرَ الْوَحْىُ‏.‏

Translation In English

Narrated ‘Aisha: (the mother of the faithful believers) The commencement of the Divine Inspiration to Allah’s Messenger (ﷺ) was in the form of good dreams which came true like bright daylight, and then the love of seclusion was bestowed upon him. He used to go in seclusion in the cave of Hira where he used to worship (Allah alone) continuously for many days before his desire to see his family. He used to take with him the journey food for the stay and then come back to (his wife) Khadija to take his food likewise again till suddenly the Truth descended upon him while he was in the cave of Hira. The angel came to him and asked him to read. The Prophet (ﷺ) replied, “I do not know how to read.” The Prophet (ﷺ) added, “The angel caught me (forcefully) and pressed me so hard that I could not bear it any more. He then released me and again asked me to read and I replied, ‘I do not know how to read.’ Thereupon he caught me again and pressed me a second time till I could not bear it any more. He then released me and again asked me to read but again I replied, ‘I do not know how to read (or what shall I read)?’ Thereupon he caught me for the third time and pressed me, and then released me and said, ‘Read in the name of your Lord, who has created (all that exists), created man from a clot. Read! And your Lord is the Most Generous.” (96.1, 96.2, 96.3) Then Allah’s Messenger (ﷺ) returned with the Inspiration and with his heart beating severely. Then he went to Khadija bint Khuwailid and said, “Cover me! Cover me!” They covered him till his fear was over and after that he told her everything that had happened and said, “I fear that something may happen to me.” Khadija replied, “Never! By Allah, Allah will never disgrace you. You keep good relations with your kith and kin, help the poor and the destitute, serve your guests generously and assist the deserving calamity-afflicted ones.” Khadija then accompanied him to her cousin Waraqa bin Naufal bin Asad bin ‘Abdul ‘Uzza, who, during the pre-Islamic Period became a Christian and used to write the writing with Hebrew letters. He would write from the Gospel in Hebrew as much as Allah wished him to write. He was an old man and had lost his eyesight. Khadija said to Waraqa, “Listen to the story of your nephew, O my cousin!” Waraqa asked, “O my nephew! What have you seen?” Allah’s Messenger (ﷺ) described whatever he had seen. Waraqa said, “This is the same one who keeps the secrets (angel Gabriel) whom Allah had sent to Moses. I wish I were young and could live up to the time when your people would turn you out.” Allah’s Messenger (ﷺ) asked, “Will they drive me out?” Waraqa replied in the affirmative and said, “Anyone (man) who came with something similar to what you have brought was treated with hostility; and if I should remain alive till the day when you will be turned out then I would support you strongly.” But after a few days Waraqa died and the Divine Inspiration was also paused for a while.

The particular Greek word which deserves special attention is χιραϲ (chiras) , later always referred under a normalized text-form in this font χιρα (chira) 📷. We will go now directly to the manuscript to see how this word presents visually. I have framed it with a red rectangle in the image above.

In Codex Sinaiticus, the original writer – scribe B, section Isa 29:9-30:8, folio 53 – obviously wrote first χιρα (chira), but later, the corrector identified by scholars as Cb3, inserted a small epsilon (ε) and sigma (ς) in order to change its meaning from indeclinable feminine proper noun, “Hira” (χιρα), to a plural feminine noun in accusative case, “hands” (χειραϲ).Now, if we consult the text of Isaiah 29:12 with LXX version preserved in Codex Sinaiticus, we will uncover something interesting. Above the transcription of the Greek text of Isaiah 29:12 exactly as it appears on the official website of the Codex Sinaiticus (KoineGreek font to make transcription in a manuscript-like style)

Katika Isaiah Mlango wa 29 Verse Namba 12 Neno χιραϲ hapa lina maana ya HIRAA ambalo ni pango alilokuwa Mtume akijitenga kwa ibada na ambalo Jibril aliposhusha aya za mwanzo za Sura Ya Alfalaq. Maneno Hapa Juu ni kwa Lugha ya Kigiriki na Tafsiri kwa Kiingereza Biblia hii iliandikwa katika karne ya 4 na ipo mpaka leo katika lugha hiyo hiyo ya KIgiriki. Ukitafuta katika Mtandao utapata Biblia hii yote. Mtume alipoambia asome alijibu kwamba yeye hajui kusoma. kwa hiyo maneno ya Biblia yanalingana na Habari za Mtume katika Hadithi ya Mke wake Aisha ambayo ipo katika Vitabu vya Bukhari.

MJI WA MECCA NA JENGO LA KAABA ZIMETUKUZWA KATIKA KURUANI NA BIBLIA

Mji Wa Mecca na Jengo la Kaaba zimetukuzwa katika Biblia na Pia katika Kuruani Tukufu. Angalia hapa chini  Biblia na Kuruani  kisha ulinganishe.

Biblia Zaburi Mlango wa 84 (4-6) 

4-Heri wakaao nyumbani mwako (Ni Kaaba huko Mecca), Wanakuhimidi daima.

5-Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako, Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.

6-Wakipita kati ya bonde la Bakka (Wakalimani wamefasiri neno Bakka kama bonde la kilio lakini Translation iliyo sahihi ni Mji wa Mecca), Hulifanya kuwa chemchemi, Naam, mvua ya vuli hulivika baraka

English Translation Psalm 84 (4-6)

4-Blessed are those who dwell in your house,(Maana iliyo sahihi ni Kaaba) ever singing your praise!

5-Selah Blessed are those whose strength is in You, whose hearts are set on pilgrimage.

6-As they go through the Valley of Bakka (The correct Translation is the town of Mecca and not Valley of Shedding Tears) they make it a place of springs; the early rain also covers it with pools

Chapter (3) sūrat āl ʿim’rān Aya Namba 96(The Family of Imrān)

إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٍ۬ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِى بِبَكَّةَ مُبَارَكً۬ا وَهُدً۬ى لِّلۡعَـٰلَمِينَ (٩٦) .

TAFSIRI KISWAHILI

Kwa yakini Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyoko Makka, yenye baraka na uwongozi kwa ajili ya walirnwengu wote.

Translation English

The first House (of worship) appointed for men was that at Bakka (Mecca): Full of blessing and of guidance for all kinds of beings:

KUTAJIKA KWA MTUME MOHAMED KATIKA DINI NYINGINEZO

MTUME MOHAMED (SALA NA AMANI ZAKE MOLA ZIMFIKIE) KATIKA BIBLIA

Mtume Mohamed (Amani Na Sala Za Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Ametajwa katika Biblia katika sehemu mbalimbali.

Tutataja hapa chini baadhi tu ya sehemu hizo.

USHAHIDI KATIKA AGANO LA KALE (OLD TESTAMENT) KUMBUKUMBU 18:18 (DEUTORONOMY 18:18)

18/Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru.

Hapa Nabii Isa anapewa ahadi na Mwenyeezi Mungu kwamba atakuja Mtume Mwingine kama Yeye (Nabii Isa) na atahifadhishwa maneno (kuruani) na atafundisha kila anachoamrishwa na menyeezi mungu kwa Njia ya kuruani na Hadithi zake.

Na Hakuna Mwengine aliyekuja baada yake ambaye alipewa mafundisho haya isipokuwa Nabii Mohamed Peke Yake.

Mfananisho hapa unakubaliana na Mtume Mohamed kama kidole na pete na siyo Nabii Isa hata kidogo kwani ukiwalinganisha utaona Nabii Musa ni Kama Nabii Mohamed kufuatana na sababu mbalimbali.

Kwanza-Mtume Mohamed na Na Nabii Musa walizaliwa kama kawaida lakini Nabii Isa alizaliwa bila baba

Pili-Mtume Mohamed na Nabii Musa walikuwa wameowa na kuzaa watoto lakini Nabii Isa hakuoa

Tatu-Mtume Mohamed and Nabii Musa walifariki dunia kama kawaida lakini Nabii Isa alipazwa na atarudi mwishoni kumalizia maisha yake duniani.

Nne-Mtume Mohamed na Nabii Isa walilazimishwa kuhama miji (Mtume Mohamed alihama Madina na Nabii Musa Midian)kwa ajili ya usalama wao lakini Nabii Isa hakuhama Mji wowote.

Tano-Nabii Musa na Mtume Mohamed walikubaliwa na watu wao na Nabii Isa alikataliwa na watu wake kama inavyosema Biblia katika Johana-John-11

“Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea”.

Sita-Mtume Mohamed na Nabii Musa walipigana Vita na nabii Isa hakushiriki katika Vita Yeyote.

Saba-Nabii Musa na Mtume Mohamed hawakuitwa watoto wa Mungu au Miungu kama alivyoitwa Nabii Isa.

Hizi ni baadhi ya tofauti wa hawa watukufu watatu.

Kwa hiyo aliyefanana sana na Nabii Musa ni Mtume Mohamed kama tulivyoona hapa.

Na hii inathibitisha Maneno ya Biblia hapa juu kwamba Mtume Mohamed ndiye aliyebashiriwa kuja mwishoni na siyo mwingine.

KUMBUKUMBU 1-2 (DEUTORONOMY 1-2)

1/Hii ndiyo baraka Mose mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake.

2/Alisema:“BWANA alikuja kutoka Mlima Sinai,akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri,akaangaza kutoka Mlima Parani.Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini,kutoka matelemko ya mlima wake.

Nabii Musa anasema kuwa Nuru ya Mola ilizuka huko Sinai kwani hapo ndipo Mwenyeezi Mungu alizungumza na Nabii Musa, na kisha Seir (Nabii Isa) yaani huko Palestine/Bethlehem ambapo Nabii Isa alikuwa Mtume kwa waisraeli na Kisha ikangara tena kutoka Paran (Nabii Mohamed)ambayo ipo Mecca Na alimjaalia Kuja hapo katika kuukomboa akifuatiwa Na Maswahaba10,000 na akawaletea sheria ya Kuruani Tukufu.

Nabii Mohamed alikwenda Miiraj akazungumza Na Mwenyeezi Mungu na akatuletea mafundisho Ya sala 5.

Kuruani inasema kuhusu mazungumzo baina ya Mwenyeezi Mungu na Nabii Musa.

Sura Ya Anisaa Aya Namba 164

And [We sent] messengers about whom We have related [their stories] to you before and messengers about whom We have not related to you. And Allah spoke to Moses with [direct] speech.

Na mazungumzo baina Ya Mwenyeezi Mungu na Nabii Isa yanathibitisha Utume wake kama aya ifuatayo kutoka katika sura ya Maida namba 116.

And [beware the Day] when Allah will say, “O Jesus, Son of Mary, did you say to the people, ‘Take me and my mother as deities besides Allah ?’” He will say, “Exalted are You! It was not for me to say that to which I have no right. If I had said it, You would have known it. You know what is within myself, and I do not know what is within Yourself. Indeed, it is You who is Knower of the unseen.

WIMBO WA SOLOMON 5:16 (THE SONG OF SOLOMON 5:16)

[His mouth is most sweet: yea, he is altogether lovely. This is my beloved, and this is my friend, O daughters of Jerusalem.]

Kinywa chake kimejaa maneno matamu, Ndiye mzuri sana pia pia. Ni huyu mpendwa wangu, ni huyu rafiki yangu, Enyi binti za Yerusalemu. Na katika Biblia za asili yaani za mwanzo zilizokuwa bado kufasiriwa katika lugha ya kigiriki tunapata maneno hapa chini katika lugha ya kiyahudi yanayothibitisha jina la Mtume Mohamed.

 “Hikko Mamittakim we kullo Muhammadim Zehdoodeh wa Zehraee Bayna Jerusalem.

Wakalimani walifasiri neno Muhamadim kwa makosa kwa maana ya

“Ndiye Mzuri Sana Pia Pia”

kwani kwa kutumia utaalamu wa Translation huwezi kulifasiri jina la mtu kwani hapa linaonyesha dhahiri ni jina la Mtume Mohamed kwani herufi mbili za mwisho la Jina hili “im” ni la heshima kufuatana na Lugha ya kiyahudi. Kama vile kumwita mtu kwa kutanguliza neno “bwana” kabla ya Jina na hivyo hivyo hapa tutafasiri hapa kama “Mtukufu Bwana Mohamed” na siyo

“Nzuri Sana”

ISAIAH NAMBA 42

Isaiah Chapter Namba 42 inamzungumzia habari za Mtume Mohamed kwa kirefu. Tutazungumzia baadhi tu ya Chapter Hii:

“Here is my servant, whom I uphold, ( my chosen one in whom I delight; I will put my Spirit on him, and he will bring justice to the nations. He will not shout or cry out,

Tafsiri Kwa Kiswahili

Huyu ni Mja wangu ninayemchagua na chaguzi langu linalonipendezesha nitamtumia Malaika (Jibril) kuwa msaidizi wake katika kufikisha ujumbe na kwa hiyo ataleta haki katika mataifa na hatatumia makelele katika kazi yake.

Na Mtume alikuja na sheria iliyoleta haki katika mataifa na pia alikuwa na uvumilivu na hakuwa akipiga ukelele bila sababu.

Na katika kuruani Mwenyeezi Mungu anamsifu Mtume kwa kumwambia kwamba

“kwa hakika wewe ni mwenye tabia nzuri sana”

USHAHIDI KATIKA AGANO JIPYA (NEW TESTAMENT) YOHANA 16:12-13 (JOHN 16:12-13)

12/Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.

13/Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

Nabii Isa anaambiwa kwamba wakati haujafika wa kupewa ujumbe wa mwisho lakini baadaye Mtume Mohamed atakuja na Kuruani na hatafundisha yake bali aliyoamrishwa na Mwenyeezi Mungu Na Pia Kutujuulisha yatakayokuja baadaye.

YOHANA 14:26 (JOHN 14:26)

26 Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Nabii Isa anasema kwamba huyo msaidizi ni Mtume Mohamed (Sala Na Amani Zimfikie), na hii ni kufuatana na Translations zilizopita katika kufasiri maneno ya Injili za awali katika lugha za kigiriki Neno periklutos/paraclete, lenye maana “Mwenye Kutukuzwa” ambalo kwa lugha ya kiarabu ni Ahmad.

Kithibitisho katika Kuruani Mipango yake mwenyeezi Mungu amejaalia kutajika kwa Mtume Mohamed katika Dini zilizopita.

Kama mwenyeezi Mungu anavyosema hapa katika Sura Ya Alaaraf Aya Namba 157

“Those who follow the messenger, the unlettered Prophet, whom they find mentioned in their own (scriptures),- in the law and the Gospel;- for he commands them what is just and forbids them what is evil; he allows them as lawful what is good (and pure) and prohibits them from what is bad (and impure); He releases them from their heavy burdens and from the yokes that are upon them. So it is those who believe in him, honour him, help him, and follow the light which is sent down with him,- it is they who will prosper.”

KUTAJIKA KWA MTUME MOHAMED KATIKA VITABU VYA DINI YA KIBANIANI (HINDUISM) KUHUSU DINI YA KIBANIANI

Vitabu Vya Dini za Kibaniani vimegawanya katika makundi mawili:

1/Shruti (walichosikia) Na imekusanya Vedas na Upanishads

2/Smriti (kinachokumbukwa) Imekusanya Puranas, Maharabhata, Ramayana etc.

Mabaniani wanaamini kwamba mungu anayejulikana kama Brahman aliwafunulia Vedas (Elimu) kwa watu wenye Busara wanaojulikana kama Kina Rishi yaani walishushiwa Ujumbe.

Wanaamini kwamba Vedas imegawanyika katika sehemu nne nazo ni:

Samhitas/Brahmanas/Aranyakas na Upanishads.

Vitabu hivi ni baadhi tu ya vitabu vingi vya dini hii na pia hapa juu Vedas, Purana na Nyinginezo pia zimegawanyika katika matawi na vitabu mbalimbali. Wataalamu Mbalimbali Kama vile Sheikh Zakir Naik wamefanya Utafiti katika vitabu hivi. Na tumepata faida kwao kubwa.

Tukienda katika Bhavishya Purana (Aina MojaYa Purana) tutakuta habari za Mtume Mohamed.

Tukichambua Atharvaveda (Moja ya vitabu vya Vedas)tutakuta habari za Mtume Mohamed zimetajwa hapa.

Na hali kadhalika katika Vitabu Vinginevyo kama vile Samveda na Rigveda ambavyo vinatokana na Vitabu maarufu vya Vedas.

Kwa Mfano katika Rigveda Hymn namba 53 Verse namba 9 neno “Sushrana” katika lugha ya Sanskrit lina maana ya “aliyetukuzwa” kwa kiarabu ni Mohamed au Ahmad (Sala Na Amani Za Mwenyeezi Zungu zimfikie).

Katika Samveda Hymn namba 6 Verse Namba 8 inataja jina lake Ahmad ambalo ni Mohamad.

Kwa Lugha ya kiingereza katika Rigveda tunaelezwa hapa chini:

“Ahmed acquired from his Lord the knowledge of eternal law. I received light from him just as from the sun.”

The Prophecy confirms: Explanation of the above Verse From Rigveda -The name of the Prophet as Ahmed since Ahmed is an Arabic name.

Many translators misunderstood it to be Ahm at hi and translated the mantra as “I alone have acquired the real wisdom of my father”. -Prophet was given eternal law, i.e. the Shariah. -The Rishi was enlightened by the Shariah of Prophet Muhammad.

The Qur’an says in Surah Sabaa chapter 34 verse 28

“We have not sent thee but as a universal (Messenger) to men, giving them glad tidings and warning them (against sin), but most men understand not.” [Al-Qur’an 34:28]

Tafsiri Kwa Kiswahili Ahmed (Mtume Mohamed) atapata kutoka kwa mola wake elimu ya sheria Na aliyepokea habari hizi anayejulikana kama Rishi (wahindi wanaamini kwamba kina Rishi ndiyo wale wenye hekima na busara ambao message za Vedas kutoka kwa Mungu zilipitia kwao) alifurahi sana kwa mwanga huu ambao anaufananisha na mwanga wa Jua.

(Watafiti wanatushangaza kugundua habari za Mtume Mohamed katika vitabu vya Mabaniani, kama kwamba labda huko zamani walipelekewa mitume ambao hatuwajui?

Mtume Mohamed anatuambia kwamba mitume waliokuja ardhini walikuwa 125,000 na tunawajua wachache ambao wametajwa katika kuruani na wengine wote hatuwajui.

Je habari hizi za Mtume Mohamed katika vitabu vya zamani vilipokelewa na mitume iliyopita?

Kwa kifupi hatujui kwani muda mrefu umepita na hakuna ushahidi wowote lakini la kushangaza kuna habari za kuja Mtume Mohamed katika maandshi hayo na kwa hiyo Sisi tumfuate Mtume Mohamed na Message ya mwisho na tusifuate message zilizopita kwani zimeguswa na kubadilishwa baada ya muda mrefu.

Kuruani imehifadhiwa kama alivyoahidi mwenyeezi mungu katika kuruani alisema katika Sura ya Alhijr Aya namba 9 Chapter (15)

sūrat l-ḥij’r (The Rocky Tract):

“We have, without doubt, sent down the Message; and We will assuredly guard it (from corruption)”.

Tafsiri Ya Aya

Bila ya shaka tumeshusha ujumbe na tutauhifadhi (usiharibiwe).

NASIHA/TAHADHARINI

KUDAI UTUME

Baada ya kumtukuza mwenyeezi mungu na kumswalia Mtume Mohamed (Sala na Amani zake mwenyeezi Mungu zimfikie) Ningependelea kukujuulisheni kwamba 

Amesema Mwenyeezi Mungu katika Quruani

مَا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَآ أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَكِن رَّسُولَ اللَّهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ وَكَانَ اللَّهُ بِكُلِ‏ّ شَىْ‏ءٍ عَلِيماً

Tafsiri Ya Aya Hii

Mohamed si baba wa yeyote katika wanaume wenu ,bali yeye ni Mtume wa Mungu na mwisho wa mitume, na mwenyeezi mungu ni mjuzi wa kila kitu.

(Sura Ya Al-Ahzab Aya namba 40)

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِى وَ رَضِيتُ‏لَكُمُ الْإِسْلَمَ دِيناً

Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu use dini yenu

(Sura Ya Al-Maidah Aya namba 3)

Hizi Aya mbili zinatosha kuwa shahidi kwamba Mtume Mohamed ndiyo wa mwisho na hakuna tena mtume wala mjumbe atakaye kuja na ujumbe wowote. Ujumbe aliopewa Mtume Mohamed ndiyo umekamilisha ujumbe wake mwenyeezi Mungu tangu alipoumba dunia na ujumbe huu ndiyo wa mwisho mpaka mwisho wa dunia wakati Mola atakaporithi ardhi yake na kila alichokiumba kilichomo baina ya mbingu na ardhi.

Ndugu zangu binaadamu  ulimwenguni kuweni macho na manabii wa uongo wataokuja baada ya Mtume Mohamed. Na kwa kweli wengi wamedai utume na wengine kudai uungu na wote hao kwa ajili ya maslahi yao ya kidunia. 

Watu hao wanatumia njama mbalimbali kuwadanganya watu, na hivi sasa wanatumia mtandao kueneza fikra na madai ya kishetani yenye uongo mtupu.

Ndugu zangu binaadamu tukifuata  kuruani na kila hadithi sahihi za mtume Mohamed hatutapotea kwani mafundisho ya Mtume Mohamed ni Jahazi yetu ya leo mfano wa jahazi ya Nabii Nuhu. Tupande Zahazi hii na hatutapotea.

MASHEKHE WA BANDIA

Kuweni macho sana na watu ambao wanatumia Mtandao kueneza mafundisho ambayo ukiyachinguza utakuta yanapingana na mafundisho sahihi ya dini ya kliislamu. Watu hao wanavaa nguo za kiislamu na wamesoma Kuruani na Uislamu vizuri sana  ili kuwapoteza binaadamu wenzao.

Baadhi ya watu hao wanawakilisha maadui wa kiislamu na wanalipwa mishahara  ili kuwatoa watu katika uislamu.

Na kuna wengine wanafanya hayo kwa ajili ya umashuhuri.

Na wengine wanatoa namba zao za simu ili wapigiwe na kisha kutumia ujanja ili kupora pesa wenzao

HATARI YA MTANDAO

Mtandao unajumuisha binaadamu wote wenye kutumia vyombo mbalimbali vya habari kama vile simu za mkono na compyuta za kila aina. Kuna watu wazuri, majambazi, wizi, walaghai, waongo, wachamungu, magaidi, wauaji, na aina mbalimbali ya watu ambao wanatumia mtandao huu.

Ndugu zangu wacha mungu kuweni macho sana unapotumia mawasiliano kwa kutumia njia ya mtandao huu. Huu ni mtihani mkubwa sana tuliopewa na mwenyeezi mungu mtukufu. Kuna watoto wengi wameuzwa, watoto wengine wameibiwa, wengine wamuawa, watu wengine wamedanganywa na kupoteza mali zao na pia kuna wengine wanatumia mtandao kwa njia nzuri na wamefaidika nayo. Tujiepushe na hatari mbalimbali kama hizi. Na hao wenyekupoteza watu kwa kawaida wanakuwa na maneno mazuri sana na pia huwezi kuwajua kwani wamejiandaa. Na usisahau sheitani alipomuahidi mwenyezi mungu akasema:

(16)قال فبما أغويتني لأقعدن لهم صراطك المستقيم

(17)ثم لآتينهم من بين أيديهم ومن خلفهم وعن أيمانهم وعن شمائلهم ولا تجد أكثرهم شاكرين

Tafsiri Ya Aya Hizi

Akasema “Kwa Kua umenihukumia upotovu basi nitawakalia (waja wako) katika njia yako iliyonyooka (ili niwapoteze). (16)

Kisha nitawafikia kwa mbele yao na nyuma yao na kuumeni (kuliani)kwao na kushotoni kwao. Wengi katika wao hitawakuta (Hutawaona) ni wenye kukushukuru. (17).

Basi tuweni macho sana na Mtandao kwani ni sehemu Sheitani anapowapata wapumbavu. Na usisahau sheitani ana ujuzi (experience) mkubwa sana wa miaka mingi tangu kuumbwa duania mpaka leo. Sisi hatufikii ujuzi wa mashetani kwa hiyo ni kumuomba Mungu kila wakati atusaidie tunapobabaika. Na usisahau kwamba mashetani hao wanashirikiana na makundi ya majambazi tuliyoyataja hapo juu; Waongo, walaghai, wizi  na wengineo ambao wanaeleweka na si lazima kuwataja wote hapa. 

Katika Mtandao kuna  “Dark Web” huu ni mmoja wa misamiati wa Vyombo Vya Habari yenye maana ya “Mtandao Wa Ndani”au “Mtandao Uliojificha Kizani” Kwa mfano majambazi wanatumia Mtandao huo kutumia  VPN (Virtual Private Network) mbalimbali Makhsusi na kisha wanawasiliana katika mipango mbalimbali ya Kijinai na kisha hukamata wajinga wenye kwenda katika mtandao huo au  hutoka nje ya Mtandao wetu wa kawaida na kutafuta wajinga.  (Wajinga ndiyo Waliwao).

Ndugu zangu binaadamu tuwe  macho sana. Tutumie Mtandao kwa mambo ya Elimu zenye faida na pia katika kuwasiliana kwa njia ya kheri. Na Inshaallah namuomba Mwenyeezuii Mungu atulinde na atusaidie atuonyeshe ya kheri na faida katika Mtandao.

Naomba Mwenyeezi Mungu atakabali na abariki Nasiha hizi mbili zipate kufahamika na kufuatwa.

UISLAMU NA MISUKOSUKO YA KIMAISHA

Mwenyeezi Mungu ameumba ulimwengu na kila kitu kwa mpango wa hali ya juu na kila alichoumba ni kwa hekima anayojua yeye peke yake.

Na katika viumbe vyake amemkirimu binaadamu kwa kumpa kheri mbalimbali na mojawapo ya neema hizo ni Akili. Baada ya kumuumba binaadamu akatuma wajumbe mbalimbali (Mitume na Manabii) ambao wamekuja na mafundisho yenye manufaa katika maisha yetu.

Ili kuishi vizuri katika ulimwengu huu inabidi tufuate mafundisho yao na iwapo tutakwenda kinyume tutaendelea kupata misukosuko tusiyotegemea.

Tunamshukuru Mwenyeezi Mungu ambaye ametuachia tiba mbalimbali katika kuruani na pia nasiha alizotuma kwa Mtume Mohamed (Amani na Sala Zimfikie).

Dua yeyote ukiiomba mwenyeezi Mungu ameahidi kutukubalia kama alivyosema katika kuruani tukufu:

وَقَالَ رَبُّڪُمُ ٱدۡعُونِىٓ أَسۡتَجِبۡ لَكُمۡۚ (٦٠)

Tafsiri ya Aya (Sura Namba 40 Aya Namba 60) Na Mola Wenu Anasema:”Niombeni Nitakujibuni”

Tukifuata sheria za kuomba dua Mwenyeezi Mungu akipenda atatupa tunayoyataka au hatatupa na kwa hali yoyote ile uchaguzi wowote atakaoufanya una kheri kama anavosema katika kuruani;

وَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـًٔ۬ا وَهُوَ خَيۡرٌ۬ لَّڪُمۡ‌ۖ وَعَسَىٰٓ أَن تُحِبُّواْ شَيۡـًٔ۬ا وَهُوَ شَرٌّ۬ لَّكُمۡ‌ۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ وَأَنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ (٢١٦

Tafsiri ya Aya hii (Sura Namba 2 Aya Namba 216) (Huenda mkachukia kitu, nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyeezi Mungu ndiye anayejua (lakini) nyinyi hamjui)

Tunapopata misukosuko ya maradhi au janga katika majanga ya dunia basi tuamke na kuelewa kwamba kuwa Tiba mbalimbali katika Kuruani na Nasiha za Mtume Mohamed.

Tiba Ya Kwanza ni Dua Ya Nabii Yunus Alipomezwa na chewa aliomba dua ifuatayo na mwenyeezi Mungu akamlinda humo tumboni mpaka alipotapikwa ufukoni na hali yupo mzima wa afya. na dua aliyoiomba ni hii ifuatayo: (Sura Namba 21 Aya Namba 87 na 88)

لَّآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنتَ سُبۡحَـٰنَكَ إِنِّى ڪُنتُ مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ (٨٧)

(La Ilaha Ila Anta Subhanaka Inniy Kuntu Mina Adwalimiiin)

Tafsiri Ya Aya Hii:

“Hakuna aabudiwaye kwa haki isipokuwa wewe, mtakatifu, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu nafsi zao”.

Ndugu waislamu dua hii nzuri sana na inafaa sana kwa wakati wowote unapopata shida ya aina yeyote kama vile COVID-19 (Corona), Ukariri dua hii moyoni mwako kila mara na huku unamnyenyekea Mola wako. Basi Mwenyeezi Mungu akamwondolea Nabii Yunus Msukosuko alioupata ambayo ni mkubwa sana ( Kumezwa na Samaki (Chewa) Je Ni jambo dogo hilo!!!!!!!. kama Aya ifuatayo Mola anasema

فَٱسۡتَجَبۡنَا لَهُ ۥ وَنَجَّيۡنَـٰهُ مِنَ ٱلۡغَمِّ‌ۚ وَكَذَٲلِكَ نُـۨجِى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ (٨٨)

Tafsiri ya Aya hii ni kama ifuatavyo:

“Basi Tukampokelea na Kumwokoa katika huzuni ile. Na namna hiyo ndiyo Tuwaokoavyo walioamini”.

Basi Ndugu waumini tusibabaike na matatizo ya duniani na hali dawa mbalimbali tunazo.

Tiba Ya Pili Dua Ya Nabii Ayyub Dua nyingine nzuri sana ni ile ya Nabii Ayub alipopatwa na Maradhi makubwa naye akaomba dua na kukubaliwa. Kama hapa Aya inavyosema:

وَأَيُّوبَ إِذۡ نَادَىٰ رَبَّهُ ۥۤ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٲحِمِينَ (٨٣)

(Inni Massaniya Addhurru Wa Anta Arhamu Arrahimin) Na (Mtaje) Ayyub, alipomwita Mola wake (Akasema)

“Mimi imenipata dhara, Nawe ndiye unarehemu kuliko wote wanorehemu”

فَٱسۡتَجَبۡنَا لَهُ ۥ فَكَشَفۡنَا مَا بِهِۦ مِن ضُرٍّ۬‌ۖ وَءَاتَيۡنَـٰهُ أَهۡلَهُ ۥ وَمِثۡلَهُم مَّعَهُمۡ رَحۡمَةً۬ مِّنۡ عِندِنَا وَذِڪۡرَىٰ لِلۡعَـٰبِدِينَ (٨٤)

“Basi Tukambubalia (wito wake) na Tukamuondolea dhara aliyokuwa nayo, na Tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao. Ni rehema inayotoka kwetu, na ukumbusho (mzuri) kwa wafanyao ibada”

Hizi dua mbili tu zinatosha kutuondelea shida zote ulimwenguni. Ili kujikinga na madhara ya Covid-19 na Mengineyo ni vizuri kukariri dua ya Nabii Yunus kila mara kwani tumezungukwa na Virusi kila pahali na tupo jangani mfano wa nabii yunus alipokuwa katika tumbo la Chewa, Na dua aliyoiomba ilomwokoa basi nasisi tuiombe dua hii ili Mwenyeezi Mungu atuokoe kama alivyomuokoa Nabii Yunus. Na unapopata Maradhi kama haya na mengineyo usiogope kabisa kwani ukumbuke dua ya Nabii Ayub alipopata Maradhi. Soma dua ya Nabii Ayub kwa imani kama alivyofanya Ayub na Inshaallah Maradhi yataondoka.

Na pia Hadithi za Mtume Mohamed ametaja dua mbalimbali.

Na nasiha zake kutufahamisha dawa mbalimbali kama vile Mbegu za Cini au (Mbegu Nyeusi au Cumin Seeds kwa kiingereza) Hadithi iliyokusanywa na Sheikh Albukhariy anasema Mtume Mohamed (Amani na sala zimfikie) “Mbegu nyeusi (Black seeds au Cumin Seeds) ni dawa ya kila kitu isipokuwa kifo”

Kisayansi inasaidia maradhi mbalimbali, ina vitamins and minerals mbalimbali ambazo zinasaidia kujenga “kinga ya Nidhamu ya Afya” au kwa kiingereza “Immune System” mwilini.

Tiba Ya Tatu Ni Vyakula Vilivyotajwa katika Kuruani Kwa maoni kila aina ya tunda na vinginevyo kama vile asali ambavyo vimetajwa katika kuruani ni nzuri kwa afya na pia dawa. baadhi yake hujenga afya (Immune System) ili isivamiwe na vijidudu kama vile virusi na baadhi yake hutibu maradhi mbalimbali.

Kwa mfano: Matini na Zeituni Matini na Zeituni inafaida kubwa sana na itabidi maandishi mengi kuelezea hapa.

Kwa kifupi zina faida kubwa sana katika kutibu maradhi mbalimbali. Kama vile kupunguza Cholestorel, Kuzuia aina mbalimbali za Cancer, Kupunguza High Blood Pressure, Kupunguza uzito na mengi mengineyo.

(Tafsiri ya Sura namba 95 Aya namba 1)

وَٱلتِّينِ وَٱلزَّيۡتُونِ (١)

“Naapa kwa Tini na Zaituni”

Tende Tende zimetajwa katika kuruani zaidi ya mara moja nazo husaidia kujenga Nidhamu ya Kinga Ya Afya (Immune System). Kusafisha damu na mazuri mengi ambayo inabidi maandishi marefu. Makomamanga Makomamanga yametajwa katika kuruani husaidia kusafisha damu na mengineyo. Asali Asali ni dawa kubwa ya maradhi mbalimbali na ina faida kubwa katika kujenga Nidhamu ya Kinga Ya Afya (Immune System) Mwenyeezi Mungu anasema katika kuruani:

” وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨) ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ فَٱسۡلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلاً۬‌ۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌ۬ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٲنُهُ ۥ فِيهِ شِفَآءٌ۬ لِّلنَّاسِ‌ۗ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَةً۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ (٦٩)

(Tafsiri ya Sura Namba 16 Aya Namba 68 na 69) “Na mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba

“Jitengenezee majumba (yako) katika milima na katika miti na katika yale (majumba) wanayojenga (watu) “Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita) Kunatoka katika matumbo yao kinywaji (asali) yenye rangi mbalimbali, ndani yake mna dawa (ponya au poza) kwa wanaadamu. Hakika hayo muna mazingatio kwa watu wenye fikra”.

BARUA YA MTUME MOHAMED KWA EMPEROR/MFALME WA FARSI (PERSIAN EMPIRE)

Katika Kulingania dini ya Kiislamu Tutazungumzia barua katika barua mbalimbali alizoandikwa Mtume Mohamed (Amani na Salaam za Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Ya kwanza Aliyomwandikia Emperor (Mfalme) Wa Persia (Farsi) aliyejulikana kama Khursaw (Chosroes) Kwa kweli yaliyotokea yanashangaza na utukufu wa Mtume ulithibitishwa na tokeo hilo.Historia inatuambia kwamba barua hizo alizituma katika mwaka wa 6 baada ya Hijra kwenda Meddina. Na ilikuwa baada tu ya Mkataba (Treaty) wa Hudaybiya ambayo ilihusu makubaliano baina Ya Mtume na Makafiri wa Mji wa Mecca kuhusiana na kuruhusiwa kwa Waislamu kwenda Hija.

Barua Ilisema;

Bismillahi Arrahmani Arrahim. Kutoka Kwa Mohamed, Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa Chosroes, Mfalme wa Persia. Amani imfikie yule ambaye anafuata njia ya uongofu, kuamini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake na kuamini kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mmoja na hana Mshirika yeyote. Ninakuomba uje kujiunga na dini ya Kiislamu.Mimi ni Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu aliyetumwa kwa watu wote ili kumjuulisha kila kiumbe kwamba tumuogope Mwenyeezi Mungu na watakaokataa mwito huu watalipwa. Kubali Uislamu kama dini yako ili uishi kwa amani,ama sivyo utakuwa ni sababu ya madhambi ya wanaofuata dini ya Magians au Majus. (Dini hii ni wale wenye kuabudu Moto).

Abdullah bin Hudhafa As-Sahmi (Historia ndivyo inavyosema) alichaguliwa kubeba barua hiyo na akasafiri kwa ngamia mpaka Persia na alipofika katika Jumba la Emperor (Mfalme aliyejulikana kwa jina kama Khursaw Parvez) Aliruhusiwa kukutana naye.Alivaa nguo za Bedouin zilizo za kawaida kama walivyovaa waislamu wa wakati huo na kupeleka barua hiyo huku imani imemjaa na wala hakuogopa chochote. Naye Mfalme/Emperor alivaa nguo za Kifalme kama kawaida ya Wafalme wanavyovaa wakati huo. Abdullah hakukubali barua hiyo apewe yeyote mwingine isipokuwa Mfalme mikononi mwake kama alivyoamrishwa na Mtume Mohamed.

Barua Ilianza Kusomwa kama ifuatavyo;

Bismillahi Arrahmani Arrahim. Kutoka kwa Mohamed, Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu kwa Khussav kiongozi (Emperor) wa Persia. Kipande hiki cha mwanzo wa Barua kilimtoa Jasho Mfalme kwani Jina la Mtume Mohamed katika Barua lipo Juu na Kufuatiliwa na Jina la Mfalme.

Basi hakuvumilia na alichukia sana, akainyakua na kuipasua vipande vipande kwa hasira.

Abdullah hakujali kitakachotokea kwani muhimu kwake yeye ni kufikisha ujumbe na ile barua kusomwa. Kwa bahati aliondolewa na akaweza kucukua Ngamia wake na kurudi huko Medinna.

Hasira za Emperor (Mfalme) zilipotulia akaamrisha Abdullah aletwe tena mbele yake lakini hawakumpata kwani alikwisha ondoka. Bwana Abdallah akamjuulisha Mtume Mohamed yaliyotokea. Mtume Mohamed akamjibu “Mwenyeezi Mungu atalichana (vipande vipande)Taifa lake”.

Mfalme Khursaw akamwandikia Badhan ambaye alikuwa Mwakilishi au Governor wa Persia huko Yemen. (Yemen ilikuwa inatawaliwa na Persia) kutuma watu wawili walio na nguvu kuenda na kumkamata Mtume Mohamed huko Medinna na kumpeleka huko Persia na pia kufanya uchunguzi wa dini ya kiislamu.

Makafiri waliposikia habari kwamba Khusraw ametuma watu kumkamata Mtume basi walifurahi sana.

Hao wajumbe walikutana na Mtume huko Madinna na wakampa Barua inayotoka kwa Governor wa Yemen anayejukana kwa Jina la Badhan na Kumwambia kwamba Mfalme wa Wafalme bwana Khursaw amemuandikia Badhan tuje tukuchukue na ukikubali itakuwa vizuri kwako kwani atakusamehe na ukikataa basi wewe pamoja na watu wako mtaangamizwa.

Basi Mtume akawaomba warudi siku ya pili. Na walipokuja wakamuuliza iwapo ataondoka nao. Basi Mtume akawajibu kuwaambia habari mpya ya kushangaza na kusema. “Hamtasikia habari za Khursaw kuanzia leo kwani ameshafariki dunia. Mtoto wake anayejulikana kama Shirwaih amechukua Madaraka” (Historia inasema kwamba Khursav alimuua baba yake na kuchukua Madaraka)

“Na muambieni Badhan kwamba Dini yangu ndiyo iliyonijuulisha habari hizi mpya na pia mwambie kwamba akikubali uislamu basi nitamfanya kiongozi katika hiyo sehemu ya Yemen”

Basi maneno hayo yaliwashangaza sana hawa Maaskari wawili na wakamuandikia Badhan. Na Badhan akasema kama aliyosema Mtume Mohamed ni kweli basi Huyu ni Mtume wa Kweli. Na baada ya Muda siyo Mrefu Shirwaih (King) Mtoto wa Khursaw akatuma barua kwa Badhan inayothibitisha aliyoyasema Mtume Mohamed. barua Inasema.

“Nimemuua Khursaw kwa sababu ya Ukatili wake juu ya wananchi. Alikuwa anauwa viongozi, kukamata wake zao na kuchukua mali zao”

Baada ya Badhan kupata barua hii aliingia katika uislamu na Wafarsi (Persians) waliopo hapo Yemen pia wakaingia katika Uislamu. Na hii ndiyo Habari za Mfalme wa Farsi (Persia).

Historia Ya Constitution Ya Kwanza Duniani-Katiba Ya Mtume Mohamed

MAANDISHI YA ARISTOTLE

Kuna wanaosema kwamba Aristotle aliyezaliwa Mwaka 384 B.C.E.(Before Christian Era) ndiye aliyeandika Katiba (Constitution) Ya Kwanza Duniani kwa kweli ukifanya utafiti  utaona kwamba maandishi yake Hayapasi Test  na kwa hivyo hatuwezi kuyapa Jina la Constiution.

KATIBA (CONSTITUTION) YA UINGEREZA

Constitution inayojulikana kama Magna Carter iliandikwa mwaka 1215 huko Uingereza

KATIBA (CONSTITUTION) YA AMERICA

Na ya America iliandikwa mwaka 1787.                              

Hizi  Constitution mbili ndizo zinazotambulikana, na kila mojawapo watu wanapingana kuna wanaosema ya Uingereza ndiyo ya kwanza duniani na kuna wengine wanaodai kuwa ya America ndiyo ya kwanza duniani. Na kila anayedai anatoa sababu zake. kwa kutumia neno “katiba iliyokamilika” au “katiba iliyohusu nchi na wananchi” na mengineyo.

KATIBA YA MTUME MOHAMED

Dibaji

Historia Imesahau kwamba Constitution Ya Kwanza Duniani ni ile iliyoandikwa na Mtume Mohammmed katika Mwaka 622 C.E. (Christian Era) 7th Century yaani katika miaka ya Kikristo. Ni maandishi ya hali ya Juu ambayo leo hii yanajulikana kama “Constitution” Na siyo ya Kwanza tu kuandikwa bali ni ya kisasa na iliandikwa kwa jamii iliyokusanya makabila na dini zao mbalimbali katika kuwapa wananchi haki za usawa na uhuru wa matakwa yao katika serikali ya kiislamu hapo Madinna.

Tangulizi

Vifungo 57 Vya Mkataba Wa Mtume Mohamed kwa Kiswahili Nimefanya Tafsiri ya Mkataba (Constitution) kwa lugha ya kiswahili. Nimebadili na kuongeza baadhi ya maneno ili ipate kueleweka. Nimejitahidi kuweka maneno yangu baina ya Brackets ( ) ili nisichanganye vifungo vya asili vya mkataba na maneno yangu. Nimeongeza, kupunguza na kubadili ili vifungo hivi vieleweke kwani baadhi ya vifungo vya asili sio rahisi kufahamika. Kama kuna makosa basi ni yangu Mwenyewe na siyo Katiba aliyoandika Mtume Mohamed (Amani Na Sala Za Mwenyeezi Mungu Zimfikie Alipo) Namuomba Mweyeezi Mungu anitakabalie Kazi hii Ndogo. Inshaallah Nitairudia tena na kusahihisha iwapo kuna kosa la kilugha au kimaana Mwenyeezi Mungu akinipa uhai na uwezo.

Vifungo 57 Vya Katiba Ya Mtume Huko Madina

1/Hii ni hati kutoka kwa Muhammad Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam), inayosimamia uhusiano kati ya Waumini yaani Waislamu wa Waquraishi na wananchi wa Yathrib na wale waliowafuata na kufanya kazi kwa bidii nao. Wanaunda taifa moja – Ummah

2/Mohajireen wa Kikuraishi wataendelea kulipa pesa za damu, kulingana na kawaida yao ya sasa.

3/Endapo Kutafanyika vita na yeyote basi watawakomboa wafungwa wao kwa wema na haki iliyo kawaida kati ya Waumini. (Sio kulingana na mataifa ya kabla ya Uislamu ambapo matajiri na maskini walichukuliwa tofauti).

4/Bani Awf watashauriana pesa za damu, baina yao, kulingana na kawaida yao iliyopo.

5/Ikiwa kuna vita baina ya makundi yeyote basi pande zote isipokuwa Waislamu watawakomboa wafungwa wao kwa wema na haki kulingana na mazoea yanayofuatwa kati ya Waumini na sio kwa mujibu wa maoni kufuatana na kawaida kabla ya Uisilamu.

6/Bani Saeeda, Bani Harith, Bani Jusham na Bani Najjar watatawaliwa kufuatana na mistari ya hapo juu (kanuni)

7/Bani Amr, Bani Awf, Bani Al-Nabeet, na Bani Al-Aws wataongozwa kwa njia au kanuni hiyo hiyo hapa juu.

8/Waumini watawakomboa wafungwa wao na watalipa pesa za damu kwa niaba yao. Litakuwa jukumu la kawaida la Ummat au taifa na sio la familia ya wafungwa kulipa pesa za damu.

9/Muumini atamfanya Muumini mwingine aliye huru kuwa mshirika wake baada ya kushauriana na kukubaliana na Waumini wengine. (Na kifungu hiki pia kina maana kwamba kila muumini hatachukuliwa kuwa mshirika katika kazi yoyoye ila baada ya mashauriano na makubaliano au baada ya mtihani kama leo CV inapochunguzwa katika kutafuta kazi)

10/Waumini, wanaomcha Mwenyezi Mungu, watapinga mambo ya waasi na yale yanayotia na kuhimiza moyo kufanya dhuluma,dhambi, uadui au ufisadi.

11/Ikiwa mtu yeyote ana hatia ya kitendo chochote hicho Waumini wote watampinga hata ikiwa ni mtoto wa yeyote kati yao.

12/Muumini hataua Muumini mwingine, kwa ajili ya asiyeamini. (yaani hata kama asiyeamini ni jamaa yake wa karibu).

13/Hakuna Mwamini atakayemsaidia asiyeamini dhidi ya Muumini.

14/Ulinzi (unapotolewa)kwa Jina la Mwenyezi Mungu itakuwa kwa kila mtu. Wanyonge kati ya Waumini wanaweza kutoa ulinzi (kwa Jina la Mwenyezi Mungu) na itakuwa ni lazima kwa Waumini wote.

15/Waumini wawe marafiki na kushirikiana baina yao.(kushirikiana katika ibada na mengineyo ya kidunia.Kwani Uislamu umeweka Ibada mbele katika maisha na kila ufanyacho ni ibada. Huwezi kushirikiana na kafiri katika ibada)

16/Wayahudi hao wanaowafuata Waumini watasaidiwa na watatendewa usawa.(Usawa wa kijamii, kisheria na kiuchumi umeahidiwa kwa raia wote waaminifu wa Serikali).

17/Hakuna Myahudi atakayedhulumiwa kwa kuwa Myahudi.

18/Maadui wa Wayahudi wanaotufuata hawatasaidiwa

19/Amani ya Waumini (ya Jimbo la Madinah) haiwezi kugawanywa. (ni amani au vita kwa wote. Haiwezi kuwa sehemu ya idadi ya watu iko vitani na watu wa nje na sehemu ina amani).

20/Hakuna amani tofauti itakayofanywa na mtu yeyote huko Madina wakati Waumini wanapopigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu.

21/Masharti ya amani na vita na urahisi au shida zinazoambatana lazima ziwe sawa na sawa kwa raia wote sawa.

22/Wakati wa kwenda nje kwa safari mpanda farasi lazima amchukue mwanachama mwenzake kutoka Jeshini-Ashiriki safari yake.

23/Waumini lazima walipe kisasi damu ya wenzao wakati wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu.(Wanapokuwa Vitani Waumini wasijiachilie Kuuawa bali wapigane kama wanavyopigwa na kuuawa).

24/Waumini (kwa sababu wanamuogopa Mwenyezi Mungu) ni bora katika kuonyesha msimamo na matokeo yake wanapata mwongozo kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika jambo hili. Wengine lazima pia watamani kufikia kiwango sawa cha uthabiti.

25/Hakuna mtu asiyeamini ambaye ataruhusiwa kuchukua mali ya Maquraishi (adui) chini ya ulinzi wake. Mali ya adui lazima ijisalimishwe kwa Serikali.

26/Hakuna mtu asiyeamini ambaye ataingilia kati kwa kupendelea Waquraishi, (kwa sababu Maquraishi wametangaza vita ni adui).

27/Ikiwa mtu yeyote asiyeamini anaua Muumini, bila sababu ya msingi, atauawa kwa kurudi, isipokuwa kama jamaa ameridhika (kwani inaleta shida za sheria na utaratibu na kudhoofisha utetezi wa Serikali). Waumini wote watakuwa dhidi ya mwenye kudhulumu. Hakuna Mwamini atakayeruhusiwa kumhifadhi mtu kama huyo.

28/Mnapotofautiana kwa chochote (kuhusu Hati hii) jambo hilo litapelekwa kwa Mwenyezi Mungu na Muhammad (Mwenyezi Mungu ambariki na ampe amani).

29/Wayahudi watajishirikisha katika vita wakati wanapigana pamoja na Waumini.

30/Wayahudi wa Bani Awf watachukuliwa kama jamii moja na Waumini. Wayahudi wana dini yao. Hii pia itatumika kwa watu wao huru.Isipokuwa wale ambao watatenda kinyume cha haki na madhambi. Kwa kufanya hivyo wanajidhulumu wenyewe na familia zao.

31/Hayo hapa Juu (kifungu namba 30)inatumika kwa Wayahudi wa Bani Al-Najjar, Bani Al Harith, Bani Saeeda, Bani Jusham, Bani Al Aws, Thaalba, na Jaffna, (ukoo wa Bani Thaalba) na Bani Al Shutayba.

32/Uaminifu hutoa kinga dhidi ya usaliti. (watu waaminifu wanalindwa na marafiki zao dhidi ya usaliti. Kwa kadiri ya muda ambao mtu ataendelea kuwa mwaminifu kwa Serikali hakutakuwa na uwezekano wa kukubali maoni ya kuwa msaliti. Anajilinda dhidi ya udhaifu).

33/Wafungwa walio huru wa Thaalba watapewa hadhi sawa na Thaalba wenyewe. Hadhi hii ni za shughuli za haki na haki kamili kama haki na jukumu ya usawa katika utumishi wa jeshi.

34/Wale wanaoshirikiana na Wayahudi watapewa watachukuliwa na kuwa sawa na Wayahudi katika kila haki.

35/Hakuna mtu (hakuna kabila ambalo ni mshiriki wa Mkataba huo) atakayekwenda vitani isipokuwa kwa idhini ya Muhammad (Mwenyezi Mungu amfikishie na ampatie amani). Ikiwa kosa lolote limefanywa kwa mtu yeyote au kikundi chochote inaweza kulipizwa.

36/Mtu yeyote anayemuua mwingine bila ya onyo (hakuna sababu ya haki) anajiua yeye mwenyewe na nyumba yake, isipokuwa mauaji hayo yalifanywa kwa sababu ya kosa lililofanywa kwake.(Kwa hali hiyo hukumu itafanywa kufuatana na aliyoyafanya).

37/Wayahudi lazima wabebe gharama zao wenyewe (katika Vita) na Waislamu wachukue gharama zao.

38/Ikiwa mtu yeyote anamshambulia mtu yeyote ambaye ni mshiriki wa Mkataba huu mwingine lazima amsaidie.

39/Wao (wanaohusika na Mkataba huu) lazima watafute ushauri na ushauriana.

40/Uaminifu hutoa kinga dhidi ya usaliti. Wale ambao huepuka mashauriano ya pande zote hufanya hivyo kwa sababu ya ukosefu wa unyofu na uaminifu.

41/Mtu hatabeba makosa ya mwenziwe.

42/Mtu yeyote (mtu yeyote au kikundi) ambaye/ambacho amedhulumiwa/kimedhulumiwa lazima asaidiwe/kisaidiwe.

43/Wayahudi lazima walipe(Gharama za vita) wanapokuwa hawakwenda vitani (kifungu hiki kinaonekana kuwa cha wakati ambapo Wayahudi hawashiriki katika vita. Kifungu cha 37 kinazungumzia baadhi ya wakati wanaposhiriki kwenye vita)

44/Yathrib itakuwa Patakatifu kwa watu wa Mkataba huu.

45/Mgeni ambaye amepewa ulinzi (na mtu yeyote anayefuata Mkataba huu) atachukuliwa kama mwenyeji wake (ambaye amempa ulinzi) wakati (yeye) hafanyi ubaya wowote na hafanyi uhalifu wowote. Wale waliopewa ulinzi lakini wakijiingiza katika shughuli za kupingana na serikali watawajibika kulipwa adhabu kufuatana na uhalifu wao.

46/Mwanamke atapewa ulinzi tu kwa idhini ya familia yake (Mlezi). (tahadhari itafanyika ya kuepukana na mizozo ya kikabila).

47/Ikiwa kuna mzozo wowote au ubishani, ambao unaweza kusababisha shida jambo lazima lipelekwe kwa Mwenyezi Mungu na Muhammad (Mwenyezi Mungu amfikishie salamu na amani), Mtume atakubali chochote katika hati hii, ambayo ni kwa ajili ya (kuleta) ucha Mungu na wema.

48/Maquraishi na washirika wao hawatapewa ulinzi.(hawa ni Makafiri na maadui wa waislamu)

49/Vukundi Vya wanaokubaliana na Mkataba huu lazima visaidiane wakati wa shambulio la Yathrib.

50/Ikiwa wao (wahusika wa Mkataba huo isipokuwa Waislamu) wameombwa kufanya na kudumisha amani (ndani ya Jimbo) lazima wafanye hivyo. Ikiwa mahitaji kama hayo (ya kufanya na kudumisha amani) yametolewa kwa Waislamu, lazima yatekelezwe, isipokuwa wakati Waislamu tayari wako kwenye vita katika Njia ya Mwenyezi Mungu. (ili hakuna mshirika wa siri wa adui anayeweza kumsaidia adui kwa kuwataka Waislamu kumaliza uhasama chini ya kifungu hiki).

51/Kila mtu (mtu binafsi) atakuwa na sehemu yake (ya matibabu) kulingana na kikundi alichopo.Lazima watu wanufaike au wateseke kwa matendo mema au mabaya ya kikundi walichopo.Bila sheria kama hiyo ushirika na nidhamu ya Umoja haiwezi kudumishwa.

52/Wayahudi wa al-Aws, pamoja na wafungwa wao huru, wana msimamo huo huo, kama vikundi vingine vya Mkataba, maadamu ni waaminifu kwa Mkataba huo. Uaminifu ni kinga dhidi ya usaliti.

53/Mtu yeyote anayefanya kwa uaminifu au vinginevyo anafanya kwa faida yake mwenyewe (au hasara)

54/Mwenyezi Mungu anakubali Hati hii.

55/Hati hii (haitatumika) kumlinda mtu ambaye hafuati haki au anafanya uhalifu (dhidi ya vikundi vingine vya Mkataba).

56/Ikiwa mtu atatoka kupigana (kwa mujibu wa masharti ya Mkataba huu) au atabaki nyumbani kwake, atakuwa salama isipokuwa akitenda uhalifu au ni mwenye dhambi. (yaani, hakuna mtu atakayeadhibiwa kwa uwezo wake binafsi kwa kuwa hajatoka kwenda kupigana kulingana na masharti ya Mkataba huu).

57/Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa watu wema na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu, na Muhammad (Mwenyezi Mungu amrehemu na ampe amani) ni Mtume wa Mwenyezi Mungu (Anawahakikishia ulinzi wema wale wanaomcha Mwenyezi Mungu).

KUASHIRIWA KIAJABU KWA MIAKA 63 YA UMRI WA MTUME, (Sala na Amani za Mola Zimfikie)MUDA WA WAHYI (REVELATION) MIAKA 23 , NGUZO TANO ZA KIISLAMU, JUMLA YA SURA ZA KURUANI 114 NA UMRI WA MIAKA 40 MTUME ALIPOSHUSHIWA KURUANI MARA YA KWANZA. MUUJIZA HII INAPATIKANA KWA NJIA YA NAMBA KATIKA AYA TANO ZA MWANZO WA SURA YA AL-Alaq.

 سُوۡرَةُ العَلق

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ (١) خَلَقَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مِنۡ عَلَقٍ (٢) ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ (٣) ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ (٤) عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ (٥)

TAFSIRI

Sura Ya Al-Alaq

Kwajina Ia Mwenyezi Mungu, Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.

1. Soma kwa jina Ia Mola wako Aliyeumba

2. Amemuumba mwanaadamu kwa pande Ia damu.

3· Soma, na Mola wako ni Karimu sana

4· Ambaye Amemfundisha (Binadamu ilimu zote hizi) kwa wasita (msaada) wa kalamu; (zilizoandika vitabu, watu wakapata ilimu)

5. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya) mambo aliyokuwa hayajui.

SHEREHE ZA MUUJIZA KATIKA AYA HIZI TANO

1-MUUJIZA WA KWANZA: (KUASHIRIWA KWA UMRI WA MTUME MOHAMED KATIKA AYA ZA MWANZO KUSHUKA KATIKA SURA NAMBA 96 YA AL-ALAQ)

Tuchunguze Herufi za Ibara Ifuatayo katika Aya tano za Sura Ya AlAlaq. مُحَمَّدٌ رَسُولُ ٱللَّٰهِ (Tafsiri:Mohamed Ni Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu)

Herufi za Jina Mohamad ( مُحَمَّدٌ ) zimekariri katika aya hizi mara 9

Herufi za neno Rasul ( رَسُولُ ) zimekariri katika Aya hizi mara 23

Herufi za Jina Allah (ٱللَّٰهِ ) zimekariri katika Aya Hizi mara 31

Ukijuumlisha Herufi hizi unapata Muujza Mwingine wa kushangaza sana 9 + 23 + 31=63

Namba hii 63 ni umri alioishi Mtume Mohamed. (Amani Na Sala Za Mola Zimfikie)

Je unaona ya Kushangaza. Huu ni Muujiza sio mdogo. Mtume alishushiwa Aya hizi za Mwanzo katika Kilima Cha NUR katika Pango la HIraa huko Mecca (Saudi Arabia) Na Aya Hizi zina Habari nyinginezo zimeashiriwa kiajabu sana ambazo hata mtume hakujua.

Umri atakaoishi Mtume Mohamed umeashiriwa katika Aya Hizi za Mwanzo bila yeye mwenyewe kujua kwani hakuna binaadamu anayejua siku ya kufa.

Sasa tuangalie Aya Namba Tano ambayo inasema

عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ (٥)

Aya hii ni ya 6111 kutoka mwanzo wa Kuruani na kihesabu hii namba ni sawa na (63 X 97)

Na Aya Hii ni ya 126 Kuanzia Mwisho wa Kuruani Tukufu na namba hii kihesabu ni sawa na (63 X 2)

Je unaona Ajabu nyingine kwamba namba hii 63 inakariri tena na tena hata unapohesabu Aya hii ya mwisho. Yaanii Umri wake Mtume umeashiriwa tena na tena kiajabu sana tena sana Allahu Akbar. Angalia maajabu haya yasiwo na mwisho.

2-MUUJIZA WA PILI UMRI WA MTUME MOHAMED MIAKA 63 NA MUDA WA WAHYI MIAKA 23 (QURAN REVELATION) KATIKA AYA HIZI

Jina la Sura ni العَلق (AlAlaq) Limetokana na neno hili katika Aya Namba mbili ya Sura hii ya Al-Alaq.

Sasa tuchunguze Position Ya Herufi za Aya hii katika mpangilio wa herufi za Kiarabu Arabic Alphabet=( ا ب ت ث ج ح خ د ذ ر ز س ش ص ض ط ظ ع غ ف ق ك ل م ن هـ و ي ) kama ifuatavyo:

Alif ni Ya 1 / Lam ni ya 23 / Ain ni ya 18/ Lam ni ya 23 / Na Qaf ni ya 21 Ukijuumlisha namba hizi utapata= 1 + 23 + 18 + 23 + 21=86 Kihesabu Namba hii ni sawa na (63 X 23) Yaani Namba 63 inaashiria Umri wa Mtume Mohamed na 23 Ni Kipindi cha Wahyi. (Yaani Quran Revelation) kipindi cha kushuka Kuruani kwa Mtume Mohamed.

Sasa tukipunguza Herufi moja iliyokariri yaani herufi iliyokariri hapa ni Lam ambayo ni ya 23 katika Arabic Alphabet. tukiiondoa (yaani kuondoa namba 23) basi tunapata tena namba hiyo hiyo ya kushangaza. 1 + 23 + 18 + 21=63 yaani Umri wa mtume Mohamed.

Unaona Ya kuchangaza. Kwa kila njia tulizotumia tunapata Umri wa Mtume tena na tena. Je unaona ya kushangaza. Kuruani siyo maneno ya binaadamu hata kidogo kwani haiwezekani mtu yeyote kuandika na kuhesabu kila herufi kwa njia hii. Na hata Majini pia hawawezi. Allahu Akbar.

3-MUUJIZA WA TATU NGUZO ZA KIISLAMU KATIKA AYA HIZI

Aya hizi za Mwanzo ni Tano na namba hii inaashiria Nguzo Tano za Kiislamu (Islamic Pillars) (Ambazo ni Imani/Sala/Zakat/Kufunga/Kwenda Hija) na Ajabu nyingine ni kwamba Aya ya mwisho katika sura hii namba 96 ya Al-Alaq عَلَّمَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ (٥) imefuatiwa na Jumla ya Aya 125 (yaani mpaka mwisho wa Kuruani) na namba hii n isawa na (5 X 5 X 5)

Je unaona tunapata tena namba 5 ambayo inaashiria Nguzo za Kiislamu ambazo ni Tano.

4-MUUJIZA WA NNE NAMBA 19 IMEKARIRI KIAJABU SANA

Sura Ya Alalaq ina Aya 19 na ni ya 19 kuanzia mwisho wa Kuruani Tukufu/ Aya ya Mwanzo katika Kuruani ni بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ ambayo ina herufi 19/ Sura Ya mwisho kushuka katika Kuruani ni Sura Ya النّصر (Annasr) Nayo ina Idadi ya maneno 19 / Namba ya Kwanza kutajika katika kuruani ni namba 19 katika sura ya Almudathir/

Hii Namba 19 ya maajabu na Inashangaza. Fikiria namba hii ilivyokariri hapa kiajabu sana. Imekariri Mwanzoni mwa Wahyi na Mwisho pia.

5-MUUJIZA WA TANO KUKARIRI KWA HERUFI ZA NENO رَسُولُ (Rasulu) YAANI MJUMBE KATIKA AYA HIZI TANO

(Sura Ya Al-Alaq) MARA 23

Herufi Raa imekariri mara 5/ Herufi Sin Imekariri mara 3/ Herufi Waw Imekariri mara 1/Herufi Lam imekariri mara 14 ukijuumlisha utapata namba 23 ( Yaani 5 + 3 + 1 + 14=23) Neno Rasulu yaani Mjumbe limekariri mara 23 kwa muda wa Ujumbe alioshushiwa Mtume Mohamed. (Kuruani ilishuka kwa muda wa miaka 23)

6-MUUJIZA WA SITA KUKARIRI KWA HERUFI ZA JINA ٱللَّٰهِ (Allah), NA HERUFI ZA NENO القرآن (Kuruani) KATIKA AYA TANO ZA SURA NAMBA 96 YA Al-Alaq

Herufi za Jina ٱللَّٰهِ (Allah), zimekariri katika Aya Hizi Tano Sura Ya Al-Alaq mara 31 na pia Herufi za neno القرآن (Kuruani) zimekariri mara 47 Jumla ya namba hizi mbili ni 78 (47 + 31=78) La kushangaza ni kwamba namba 78 pia ni Jumla ya herufi zote za Aya 5 za Sura ya Alalaq na Pia ni jumla ya idadi ya herufi zote zinazojulikana kama حُرُوف مُقَطَّعَات (ḥurūf muqaṭṭaʿāt) yaani kwa kiingereza “disjoined letters (Mfano: Alif Lam Mim katika Mwanzoni mwa Sura Ya Al-Baqarah na Nyinginezo.) (Hizi Herufi حُرُوف مُقَطَّعَات (ḥurūf muqaṭṭaʿā)t ni Muujiza Mkubwa katika Kuruani Tukufu)

7-MUUJIZA WA SABA JUMLA YA SURA ZA KURUANI NI 114 NA UMRI WA MTUME ALIPOSHUSHIWA WAHYI MARA YA KWANZA ALIPOKUWA NA UMRI WA MIAKA 40 HIZI PIA ZIMEASHIRIWA KATIKA AYA TANO ZA SURA YA AL-ALAQ

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ (١)

Katika Aya Namba 1 Herufi za neno ٱقۡرَأۡ zimekariri kama ifuatavyo:

Alif imekariri mara 18/ Qaf imekariri mara 6 na Raa imekariri mara 5 Na Jumla ni 18 + 6 + 5=28 Na namba hii ni jumla ya Idadi ya Arabic Letters ambazo ni 28 Pia. Kwa kweli mpangilio huu ni wa ajabu sana. Kila Mpangilio una maana na siyo bure bure. Neno hili ٱقۡرَأۡ Iqraa pia lina maajabu mengineyo.

Katika Herufi za Arabic Letters Alif Ni Namba 1/ Qaf ni ya 21 / Raa ni Ya 10 / na Alif ya mwisho ni ya 1/ Ukijuumlisha utapata namba 33 (Yaani 1 + 21 + 10 + 1=33) Namba hii ni Jumla ya idadi ya mpangilio wa herufi hizi katika Herufi za Arabic letters.

Namba hii 33 inakariri tena mara ya pili ukichunguza Herufi za Neno linalofuatia katika Aya ya Kwanza yaani بِٱسۡمِ (Bismi) Herufi za Neno hili katika Aya namba 1 ya zile 5 za mwanzo zimekariri mara 33 Pia kama neno Iqraa. Namba 33 hapa haipo bure bure bali kuna muashirio mwingine tutauelezea hapa chini.

Neno قران (Kuruani) limekariri herufi zake katika Aya hizi 5 za mwanzo mara 33 Pia. Yaani namba hii 33 inarudia tena. (Qaf Imekariri katika Aya hizi za mwanzo mara 6/ Raa Imekariri mara 5/ Alif imekariri mara 17 na Nun imekariri mara 5) Jumla 6 + 5 + 17 + 5=33)

Sasa tuchunguze neno hili القران lenye Definite Article (Alif na Lam) katika mpangilio wa Herufi za Arabic Letters (Huruf Alhijaiya) tutapata kama ifuatavyo;

Herufi za neno القران (Kuruani) katika mpangilio wa herufi za Arabic Letters pia unashangaza (Herufi Alif ni ya 1/ Herufi Lamu ni ya 23/ Herufi Qaf ni ya 21/Herufi Raa ni ya 10, Herufi Alif ni ya 1 / na Herufi Nun ni ya 25 Jumla ya Namba hizi ni 81 ( 1 + 23 + 21 + 10 + 1 + 25=81

Tumeona hapo Juu  kwamba neno Iqraa, Neno Bismi na Neno Kuruani zote zinaashiria namba 33 na sasa tunaona neno Al-Quran linaashiria namba 81 . Tukijumlisha namba hizi mbili tutapata Muujiza wa kushangaza jumla ya namba 114 (81 + 33=114) na namba hii 144 ni idadi ya sura zote za kuruani. Na namba hii 114 inafasiri vizuri sana Aya ya kwanza. Kwani Mwenyeezi Mungu anasema kumwambia Mtume ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ (Iqraa Bismi) yaani “Soma, Kwa Jina” yaani soma kwa jia la mola wako Kuruani ambayo imekusanya Sura 114. Je unaona namba zinavyotamka hapa kimuujiza. Allahu Akbar.

Tukijuumlisha Idadi ya Namba za Sura zote kuanzia Sura namba 1 mpaka Sura Namba 95 utapata idadi ni 4560 (Yaani Ujumlishe namba 1 + 2 + 3 + 4 + 5 mpaka namba 95 Sura ya mwisho kabla ya Sura ya Al-Alaq)

Hapa chini nimetumia FORMULA ya hesabu kurahisisha hesabu hii badala ya kuhesabu  moja moja, yaani namba kwa namba ambapo itachukua musa mrefu.

n(n + 1)/2 = Sum of Integers= (95(95 + 1)/2 = 4,560)

Namba 4560 ni sawa na (114 X 40) na ajabu ni kwamba namba 114 Ni jumla ya idadi ya sura za kuruani tukufu na 40 Umri aliokuwa nao Mtume Mohamed (Sala na Amani za Mola Zimfikie) aliposhushiwa Wahyi mara ya Kwanza.

Kwa kweli haya tuliyosoma leo yanathibitisha kwamba Kuruani ni maneni yake Mwenyeezi Mungu bila shaka. Je huoni mpangilio huu. (CODE language). Kwani kila herufi inawakilisha maana kama Computer Hakuna bure bure. katika kuruani hakuna upuzi wowote. Allahu Akbar Allahu Akbar.

MUUJIZA WA AL-SHAFII NA AL-WITR KATIKA KURUANI TUKUFU

KATIKA ELIMU YA HESABU

Al-Shafi(Even Number) inagawanyika na Namba 2 na kubaki 0 (Zero) na Al-Witr (Odd Number) Ni Namba isiyogawanyika na Namba 2 na mabaki kila mara huwa ni 1

(A number which is divisible by 2 and generates a remainder of 0 is called an even number. An odd number is a number which is not divisible by 2. The remainder in the case of an odd number is always “1”.)

MFANO WA NENO -ASHAFII NA AL-WITR KATIKA SALA

Sala Ya Al-Shafi Ni Sala ya Rakaa Mbili Mbili na Sala ya Al-Witr ni Sala Ya Al-Shafii kuongeza Rakaa Moja yaani Jumla inakuwa Rakaa tatu.

MUUJIZA KATIKA KURUANI

Sura Ya Alfajr Namba 89 Aya Namba 3

وَٱلۡفَجۡرِ (١) وَلَيَالٍ عَشۡرٍ۬ (٢) وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ (٣) وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ (٤) هَلۡ فِى ذَٲلِكَ قَسَمٌ۬ لِّذِى حِجۡرٍ (٥)

Tafsiri 1. Naapa kwa alfajiri 2. Na kwa masiku kumi 3· Na kwa “shafi” na witri (Yaani Naapa Kwa Namba Mbili (mbili Mbili) na Moja (Namba Moja Moja)) 4. Na kwa usiku unapopita. 5. Je Viapo Hivi havitoshi kwa wale wenye Akili?

SHEREHE KISAYANSI (MUUJIZA KATIKA KURUANI TUKUFU)

Mwenyeezi Mungu Kaapia Katika Aya Tatu za Sura Hii Viumbe Vyake Mbali Mbali. Kaanza na Alfajiri, Kisha Masiku Kumi ya Mwanzo Ya Mwezi wa Hija (Dhul-Hijjah) na Kiapo cha Tatu ni Al-Shafi (Namba Mbili Mbili) Na Al-Witr (Namba Moja Moja).

Kwa Kweli Elimu inayohusiana na ya Aya Hizi ni Kubwa na Hatuwezi kusema Kwamba Tumezijua Yote. Katika Maelezo haya machache tutagusia tu Muujiza wa Aya Namba Tatu na Tutachunguza Herufi Za maneno Haya mawili;Shafi na Witri

Herufi za Aya Hii Namba Tatu Zimetumika na Kukariri katika Sura ya Alfajr Kiajabu Sana

Herufi Za Neno; و الشفع “Wa-Al-Shafi” zimetumika katika Sura Ya Al-Fajr kama ifuatavyo:

Waw=39, Alif=102, Lam=66, Shin=2, Faa=23, na Ain=16

Ukijumlisha herufi hizi unapata namba 248 ambayo inashangaza sana (16 + 23 + 2 + 66 + 102 + 39=248)

Namba hii 248 Ni sawa na (Yaani Multiple of) 2 x 2 x2 x31

Namba 2 hapa imekariri mara 3

Je Unaona Maana Ya Neno Al-Shafi ambalo lina maana ya mbili mbili je huoni Muujiza hapa Kihesabu? Allahu Akbar

Sasa tuangalie Kutumika na kukariri kwa Herufi za Neno Al-Witr katika Sura Ya Al-Fajr

Waw=39, Alif=102, Lam=66, Waw=39, Taa=20, Raa=31

Ukijumlisha herufi hizi unapata namba 297 ambayo inashangaza sana (39 + 102 + 66 + 39 + 20 + 31=297)

Namba hii 297 Ni sawa na (Yaani Multiple of) 3 X 3 X 3 X 297 Tunapata namba Ya AL-Witr

Namba 3 hapa imekariri mara 3 pia!!

Je unaona Ya Maajabu. Je unaona Kuruani mpaka Herufi zimehesabiwa na kuashiria maana za Aya. Tumehesabu Herufi za Neno Wa-Al-Shafi tukapata Namba 2 x 2 x 2 na Mbili hapa ndiyo Al-Shafi

Na Tumehesabu Herufi za neno Al-witr na tukapata Namba 3 X 3 X 3 Yaani Namba Tatu Tatu ambayo hapa ndiyo inaashiria Al-Witr.

Hesabu Zinazungumza. Yaani Hesabu ni Lugha Pia. Elimu Hii Ni yake Mwenyeezi Mungu. Ameipanga Kuruani Yake kama anavyotaka. Allahu Akbar. Je unaona Muujiza. Hii kwa kweli inashangaza.

MIUJIZA KATIKA ADHANA (MAAJABU YASIYO NA MWISHO)

1/Historia Fupi Ya Adhana

Mtume Mohamed (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) aliwauliza Maswahaba Rai au Fikra zao (Opinion) kuhusu namna ya Kuwaita waislamu katika Msikiti katika Nyakati za Sala tano Na baada ya Kusikiliza Fikra mbali mbali Mtume (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) hakuridhika na Fikra hizo kama vile kugonga kengele kama vile wakristo wanavyofanya au Kutumia baragumu (Tarumbeta) kama vile Mayahudi wafanyavyo na nyinginezo. Lakini siku moja Swahaba anayejulikana kwa jina Abdullah Ibn Zaid (RadiAllahu Anhu) alikuja kwa Mtume na kumhadithia ndoto aliyoota ambayo inahusiana na Namna ya kuwaita watu katika nyakati za sala. Akahadithia Maneno hayo aliyoota. Na Umar Ibn Khataab(RadiAllahu Anhu) akasema kwamba naye pia ameota ndoto kama hiyo ambayo Mtume akathibitishiwa kwamba(Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) Maneno hayo Yanatokana na ndoto ya kweli na akaridhika na kuanza kuyatumia, na Maneno hayo ndiyo Adhana tunayotumia mpaka leo katika mwito wa sala zetu. Kwa hiyo Adhana haikufanywa bure bure bali inatoka kwa Mwenyeezi Mungu. Na kila kinachotoka kwa Mwenyeezi Mungu Ni Kizuri na Na Kama vile kuna Miujiza Mikubwa katika Kuruani na Hadithi za Mtume (Sala na Amani Ya Mwenyeezi Mungu Zimfikie) basi pia katika Adhana. Na Mwenyeezi Mungu anajua Zaidi.

Hebu Tuchunguze Mujiza Katika Adhana. Allahu Akbar. Allahu Akbar

2/Muujiza Katika Adhana.

1. الله اكبر الله اكبر

2. الله اكبر الله اكبر

3. اشهد ان لا اله الا الله

4. اشهد ان لا اله الا الله

5. اشهد ان محمدا رسول الله

6. اشهد ان محمدا رسول الله

7. حي علي الصلاه

8. حي علي الصلاه

9. حي علي الفلاح

10. حي علي الفلاح

11. الله اكبر الله اكبر

12. لا اله الا الله

Neno Kuadhini limetumika (kushuka) katika kuruani YOTE mara 5 tu!!!! yaani sawa na idadi ya Swala Tano!!! Angalia Muujiza huu wa kushangaza. Allahu Akbar.

Aya Zifuatazo ni za pekee katika kuruani nzima ambazo zimekusanya Neno Adhana na Maneno Mengine yenye maana hiyo hiyo yanayotokana na neno Adhana. (Derivatives au Mushtaqaat)

{ وَ نَادَى أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ أَنْ قَدْ وَجَدْنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقًّا فَهَلْ وَجَدْتُمْ مَا وَعَدَ رَبُّكُمْ حَقًّا قَالُوا نَعَمْ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَنْ لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى الظَّالِمِينَ }

[الأعراف: 44].

—————————

{ فَلَمَّا جَهَّزَهُمْ بِجَهَازِهِمْ جَعَلَ السِّقَايَةَ فِي رَحْلِ أَخِيهِ ثُمَّ أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ أَيَّتُهَا الْعِيرُ إِنَّكُمْ لَسَارِقُونَ }

[يوسف: 70].

——————————

{ وَ أَذِّنْ فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَ عَلَى كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِنْ كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ }

[الحج: 27].

——————-

Katika Aya Hapa Juu Neno Addhana أذَّنَ Limekariri mara Mbili, Na neno Muanddhinu مؤذِّنٌ Limekariri mara mbili, Ne neno Adhin أَذِّنْ Limekariri mara moja Jumla ni 5 Huu Ni Nuujiza Mwingine mpaka katika Adhana. Angalia ya Kushangaza. Allahu Akbar Haya Maneno matano yana uhusiano na Kuadhini. Yaani Tano hapa inaashiria Sala 5 za kila siku.

Ukihesabu maneno ya Adhana hapa Juu utapata jumla ya maneno 50 na kufuatana na Aya ya Kuruani inayosema

مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ (160)

yaani tafsiri inasema ukifanya zuri moja utalipwa thawabu 10 na ukifanya Jema utalipwa Dhambi Moja tu.(Yaani Huruma Ya Mwenyeezi Munfgu nu kubwa kuliko Adhabu zake) basi Haya maneno 50 ya Adhana ni sawa na Kila Sala Moja unalipwa thawabu 10 na ukifanya hesabu 10 mara 5 (10 X 5=50) utapata 50!! Allahu Akbar.

Herufi zilizitumika katika Adhana katika Herufi 28 za Kiarabu (28 Arabic Letters or Alphabets) ni 17 nazo ni

ا ل هـ ك ب ر ش د ن م ح س و ي ع ص ف

Na Ajabu ni kwamba Rakaa Za Sala 5 ni 17 (sala ya asubuhi rakaa 2 + sala ya adhuhuri rakaa 4 + sala ya Alasiri rakaa 4 + sala ya maghribi rakaa 3 + sala ya ishai rakaa 4 Jumla ni rakaa 17) yaani 2 + 4 + 4 + 5 + 3 + 4=17

Adhana hapa Juu imegawanyika katika mafungu 12 na tunaelewa kwamba Adhana inafanyika kila siku kwa muda wa mwaka mzima ambao una miezi 12

Mstari wa mwisho katika adhana ni ibara inayosema لا اله الا الله ambao una herufi 12 sawa sawa na mistari ya adhana ambayo ni 12 ambayo inaashiria miezi 12 ya mwaka!!!

Adhana imeanzia na jina la mwenyeezi mungu الله na kuishia na jina la mwenyeezi mungu الله na hii ishara kwamba yeye ndiye wa mwanzo na wa mwisho na pia hakuna mwingine anayestahiki kuabudiwa au kuswaliwa isipokuwa yeye tu. Neno lililotumika kwa wingi sana katika adhana ni jina lake mwenyeezi mungu Alah (الله) na Jina hili limetumia herufi tatu ambazo ni Alif, Lam na Haa (ا ل ه) na herufi hizi katika adhana jumla yake ni 112 na namba hii 112 katika kuruani tukufu inaashiria namba ya sura ya Ikhlas ambayo ni ya 112 na hii sura inahusu kumpwekesha mwenyeezi mungu mtukufu yaani TAWHIYD yaani madhumuni ya Sura Hii ni yale yale yaliyopo katika Adhana.

Katika Adhana Herufi A-Alif imetumika mara 47, Herufi Al-Lamu imetumika mara 45 na herufi Al-Haa imetumika mara 20 Jumla 112 (47 + 45 + 20=112)

Na muujiza wa kushangaza ni kwamba namba hii 112 ni sawa na kusema 16 X 7=112 hapa namba 7 kama tulivyozungumza katika website hii Mwenyeezi Mungu Mtukufu ameitukuza sana kama tunavyoona Huko Mecca, Kaaba inazungukwa mara 7, Safwa na Marwa mahujai wanatembea mara 7, Vijiwe vya Kumpigia Shetani katika hija ni 7 na mengi mengineyo kama vile ameumba mbingu 7 na matabaka ya ardhi 7 na mengine ambayo tumeisha kuzungumzia katika sehemu nyingine ya website hii.

Jina Allah (الله) limetumika mara ya kwanza katika sura ya Alfatiha na mara ya mwisho katika sura ya Al-Ikhlas. na baina ya sura hizi mbili kuna sura 112

Kwa kifupi Idadi ya Alif, Lam na Haa (ا ل ه) katika Sura ya Ikhlas ni 112, na mara ya kwanza kutajika Jina Allah ni katika sura ya Alfatiha na mara ya mwisho katika sura ya Al-Ikhlas na baina ya sura hizi mbili kuna sura 112

Sasa tunakuta muujiza mungine wa ajabu sana. Jina Allah (الله) limetumika (limetajika) katika kuruani tukufu katika Sura 85 tu kutoka katika Sura 114. Yaani Sura 29 zilizobaki hazina Jina Allah (الله)

Na hii namba 85 ni sawa na kusema 17 x 5 =85

Namba 17 hapa inaashiria Idadi ya Rakaa za Sala ambazo ni 17 Na namba 5 hapa inaashiria Idadi ya Sala 5 Allahu Akbar, Allahu Akbar. Angalieni maajabu na Miujiza isiyo na Mwisho.

Allah Akbar. Hakuna cha upuuzi katika dini ya kiislamu. Muujiza mpaka katika Adhana. Historia ya Adhana pia inshangaza kwani ilitokana na ndoto wakati wa Mwanzo wa Uislamu na siyo bure bure bila ya mpango. Yote haya yalikuwa ni mipango yake Mwenyeezi Mungu ndiye aliyejaalia hivyo. Allahu Akbar. Allahu Akbar.