SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Mfumo Wa Kuruani

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

MPANGILIO WA SURA, NA AYA KATIKA KURUANI

1/Mpangilio wa Sura na Wahyi Katika Msahafu

1/Sura Ya Al-Muminuun, Sura Namba 23 katika Msahafu ni ya 74 Kushuka na Idadi za Sura zenye Jumla Ya Aya si chini ya 23 katika Msahafu ni 74 na zilizobaki zote zina jumla ya Idadi Ya Aya chini ya Aya 23

2/Sura Ya Al-Zumar Sura Namba 39 Katika Msahafu ni ya 59 Kushuka na Idadi za Sura zenye Jumla Ya Aya si chini ya 39 katika Msahafu ni 59 na zilizobaki zote zina jumla ya Idadi Ya Aya chini ya Aya 59

3/Sura Ya Al-Kafirun Sura Namba 109 Katika Msahafu na ni ya 18 Kushuka na Idadi ya Sura zenye Jumla Ya Aya si chini ya 109 katika Msahafu ni 18 na zilizobaki zote zina jumla ya idadi ya chini ya Aya 109

2/Mpangilio wa Sura Na Idadi ya Aya zake.

1/Sura Ya Nuhu ni ya 71 na Idadi ya Aya zake ni 28.  Idadi ya Jumla za Sura zote katika Msahafu ambazo zina idadi za Aya si chini ya 28 ni 71

2/Sura ya Hud ni ya 11 na idadi ya Aya zake ni 123.

Idadi ya jumla ya Sura zote katika Msahafu ambazo zina idadi za Aya si chini ya 123 ni 11

3/Sura Ya Al-Tawba Sura Namba 9 kushuka na jumla ya idadi ya Aya zake ni 129.

Idadi ya jumla ya Sura zote katika Msahafu ambazo zina idadi za Aya si chini ya 129 ni 9

3/Idadi Za Aya na Idadi ya kukariri kwa namba kwa njia ya kinyume (Opposite)

1/Katika Msahafu Idadi ya Sura  ambazo Idadi Ya Aya zake si chini ya  54 ni 43 na Idadi ya Sura ambazo Idadi Ya Aya zake si chini ya 43 ni 54

2/Katika Msahafu Idadi ya Sura ambazo Idadi Ya Aya zake si chini ya 53 ni 44  na Idadi ya Sura ambazo Idadi Ya Aya zake si chini ya 44 ni 53

3/Katika Msahafu Idadi ya Sura ambazo Idadi Ya Aya zake si chini ya 39 ni 57  na Idadi ya Sura ambazo Idadi Ya Aya zake si chini ya 57 ni 39

Hii ndiyo Saini ya Mwenyeezi Mungu. Mpangilio Uliohesabiwa kiajabu sana tena sana. Hata Super Computer haiwezi kufanya kazi kama hii. Na tuelewe kwamba Kuruani iliposhuka kulikuwa hakuna Namba za Aya na Namba za Sura. Hizi ziliongezwa baadaye. Kuruani ilikuwa katika hifadhi ya Wanavyuoni kimoyomoyo na mpaka leo ipo hivyo hivyo na hata Herufi haikubadilishwa kama Mwenyeezi Mungu alivyoahidi kuitunza. Mpangilio Huu ndiyo Makufuli katika Kuruani. Ni Makufuli ya Kihesabu ambayo kama Mtu angebadilisha chochote basi kusingepatikana Nidhamu na mpangilio wa hali ya juu kama huu. Allahu Akbar.