UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MCHWA JUU YA MBU
Huwezi kuona kwa macho ya kawaida. Inabidi Microscope ikusaidie kuona kadudu kadogo kama hiki. Na Tunavyosoma Microscope ya kwanza kuundwa duniani ni katika Mwaka 1590 na Mtaalamu anayejulikana kwa jina kama Zacharias Janssen
(The development of the microscope allowed scientists to make new insights into the body and disease. It’s not clear who invented the first microscope, but the Dutch spectacle maker Zacharias Janssen (b. 1585) is credited with making one of the earliest compound microscopes (ones that used two lenses) around 1600)
Angalia Picha hapa Chini ya Kadudu kadogo “Mchwa” ambacho kinaishi juu ya Mbu.
Sasa la kushangaza zaidi ni Aya katika Kuruani Tukufu ambayo inazungumzia Maajabu haya. Jambo la Kujiuliza Je Mtume aliona vipi katika Karne ya 7? Tumeona Kwamba Zacharias ndoye aliyegundua Microscope ya kwanza Duniani katika Karne ya 16. Je huoni Maajabu ya Kuruani?
Huu ni Muujiza. Aya Ifuatayo inazungumzia habari hii kiajabu sana. Katika Sura Ya Al-Bakarah Aya namba 26
سُوۡرَةُ البَقَرَة
۞ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَسۡتَحۡىِۦۤ أَن يَضۡرِبَ مَثَلاً۬ مَّا بَعُوضَةً۬ فَمَا فَوۡقَهَاۚ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ فَيَعۡلَمُونَ أَنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّهِمۡۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ڪَفَرُواْ فَيَقُولُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَـٰذَا مَثَلاً۬ۘ يُضِلُّ بِهِۦ ڪَثِيرً۬ا وَيَهۡدِى بِهِۦ كَثِيرً۬اۚ وَمَا يُضِلُّ بِهِۦۤ إِلَّا ٱلۡفَـٰسِقِينَ (٢٦)

Angalia Picha ya Mdudu Mdogo: Mchwa Juu ya Mbu. Kadudu Kadogo Juu ya Mbu. Na anaishi hapo. Huwezi kuona kwa macho ya kawaida kwani ni mdudu mdogo sana. Inabidi Microscope ambayo itakusaidia kuona mdudu huyo. Sherehe ya Aya nimeelezea hapa juu. Allahu Akbar
TAFSIRI YA AYA 26.
Hakika Mwenyezi Mungu haoni haya kutoa mfano wowote wa mbu na ulio Juu yake. Ama wale wanaoamini, wao hujua ya kwamba hiyo ni haki iliyotoka kwa Mola wao; lakini wale waliokufuru husema: “Ni nini analotaka Mwenyezi M.ungu kwa mfano huu?” (Mwenyezi Mungu) huwawachia wengi kupotea .kwa mfano huo na huwaongoza wengi kwa mfano huo pia; lakini hamwachii yo yote kupotea kwa mfano huo (na mwingineo) isipokuwa wale wavunjao amri (Zake)
SHEREHE
Neno فَمَا فَوۡقَهَاۚ “FAMA FAWQAHA” lina maana Ya kilichopo juu ya Mbu kama vile Tulivyosoma kuhusu Mdudu Mchwa. Na pia ina maana nyingine ya Mfano mwingine wa Chochote ambacho kikubwa zaidi ya Mbu. Kwa hiyo maana zipo mbili. Kwa maana ya kwanza Tunapata Muujiza huu wa mbu. Na ukifikiri sana utaona Tafsiri zote mbili ni sahihi.
VITA VYA ROMA NA PERSIA
Sura Ya Al-Rum Namba 30 Aya 1-3
الٓمٓ (١) غُلِبَتِ ٱلرُّومُ (٢) فِىٓ أَدۡنَى ٱلۡأَرۡضِ وَهُم مِّنۢ بَعۡدِ غَلَبِهِمۡ سَيَغۡلِبُونَ (٣)
TAFSIRI
l. Alif Lam Mym.
2.Warumi wameshindwa
3. Katika Ardhi iliyo Chini sana; nao baada ya kushindwa kwao, watashinda
4. KatiKa myaka michache; Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla (yake) na baada (yake); na siku hiyo Waislamu watafurahi
SHEREHE
Roma walikuwa Wakiristo ambao wanafuata Injili, Na Persians Yaani Wafarsi walikuwa wanaabudu Moto na Masanamu yaani walikuwa Makafiri. Waislamu walitamani Warumi washinde vita Na Makafiri walitamani Wafarsi washinde Vita. Makafiri wa Mecca Walikuwa wakiwaambia Waislamu kwamba nao pia watawashinda kama vile Mafarsi walivyowashinda Warumi.
Katika Mwaka 614-615 wa Kikristo yaani Christian Era Wafarsi waliwashinda Vita Warumi katika sehemu inayojulikana kama Dead Sea Basin.
Katika Aya Hapa Juu Mwenyeezi Mungu ana waahidi Wakristo kwamba baada ya Miaka Michache Warumi watawashinda Wafarsi. Hii ni ahadi ya hali ya Juu kutoka kwa Mwenyeezi Mungu.
Inasemekana kwamba katika Mwezi wa 12 Mwaka 627 yaani baada ya miaka 7 ya kushuka kwa Aya tlizozitaja hapa juu Warumi (Romans) wakawashinda Mafarsi (Persians) kama alivyoahidi Mwenyeezi Mungu na Waislamu Walifurahi sana.
Huu siyo muujiza mdogo. Kuruani haikosei. Maneno ya Mwenyeezi Mungu hayana mchezo hata kidogo.
Muujiza mkubwa mwingine ni ibara فِىٓ أَدۡنَى ٱلۡأَرۡضِ ambayo imefasiriwa kwa maana mbili. Ya kwanza ni sehemu karibu na Bara Arabuni (Shamu) na Maana ya pili ni Sehemu ya Ardhi iliyo chini sana duniani kkulinganisha na Sehemu nyinginezo katika Ardhi.
Wataalamu kwa kutumia Vyombo vya utafiti wa hali ya juu wamegundua hivi karibuni kwamba Sehemu hiyo ambayo inajulikana kama Dead Sea Basin ndiyo sehemu ya Chini sana Duniani kwa vipimo vya Bahari. (395 Metres below the sea level).
Huu Muujiza unathibitisha kwamba Mtume Mohamad ﷺ ni wa kweli. Kuruani ni Ya kweli. Dini ya Kiislamu ni ya kweli na ya mwisho. Hatuna budi Ili kuamini na Kuukubali Ujumbe ambao ni wa mwisho.
Angalia Picha hapa Chini ya Sehemu hiyo ya Dead Sea Basin

Hiki Kibao Ni Katika Sehemu Hiyo. Kinajuulisha Kwamba ni Sehemu ya Chini sana Duniani. Sasa Mtume alisoma wapi habari kama hii ambayo imehitajia Vyombo vya hali ya juu katika Utafiti.

Dead Sea Ndiyo sehemu ambayo Warumi na Wafarsi walipigana Vita. Warumi ni Upande wa Italy (West) na Wafarsi uoande wa Iran.(East)

Hii Picha nyingine ya Dead Sea Basin. Ndiyo sehemu ambayo Warumi walipigana vita na Wafarsi.
02/09/2022
MACHIMBO HUKO UTURUKI (TURKEY-Mediterranean province of Antalya)
Hivi Karibuni Wataalamu wa Historia wamefanya Utafiti wa Jiwe lililochimbuliwa katika Sehemu za Jimbo la Antalia Huko Uturuki. LInasemekana kwamba Jiwe hilo lina umri wa miaka milioni 195 na Juu ya Jiwe hilo wamekuta Jina la Mwenyeezi Mungu بسم الله
Jina hili halikuandikwa na mtu yeyote bali limetokea na kuzuka kwa njia ya Asili (Naturally). Kwa lugha nzuri limezuka kufuatana na mazingara ya Mawe, Udongo Mifupa ya Samaki na Viumbe vinginevyo vinavyoishi Baharini. Watafiti wanasma kwamba Kipindi hicho ni cha Jurassic dinosaurs
Kwa kifupi ni MUUJIZA hakuna anayejua isipokuwa Mwenyeezi Mungu Mtukufu.
Nimenukulu hapa chini habari hizi za utafiti huu kwa lugha ya Kiingereza na Pia Picha Ya Jiwe hilo hapa chini.
(The marking that appear to form Bismillah, or In the name of God, was on a marble slab found in a marble quarry in Turkiye’s Mediterranean province of Antalya. The discovery was made in the marble business area of Antalya Marble Industry and Trade Company in Taskesigi village of the Antalya Korkuteli district. The figure that appeared on the stone attracted the attention of miners while the stone was being processed in the quarry. Removing dust from the stone, workers noticed the marking appeared to spell “Bismillah” in Arabic letters. The slab was then sent to Suleyman Demirel University in Turkiye’s southwestern Isparta province for analysis. Scientists Fuzuli Yagmurlu, Rasit Altindag and Nazmi Sengun made an interesting discovery in their analysis. While 195 million years old remains were found in the content of the marble, the marking is believed to occur naturally. Bioclastic remains of fossils belonging to sea creatures that lived 195 million years ago during the Jurassic dinosaurs period were found on dolomitic limestone that formed the plate. It was also noted that the remains, named after the Jura mountains in the European Alps, are concentrated in parts of the plate. The report said the figures on the plate with Bismillah were completely “natural” formations and the writings were formed as a result of the fragmentation, deformation and arrangement of the remains of heart-shaped shellfish over time. According to a scientific report given by Ahmet Ogke, Dean of Akdeniz University Faculty of Theology, the Arabic figures on the marble are the same character as Bismillah which is mentioned in the Qur’an)

Muujiza wa Jiwe lililofukuliwa Huko Uturuki. Jiwe lina Jina la Mwenyeezi Mungu “BISMILLAH” Angalia Maajabu. Allahu Akbar
Miujiza Inaendelea………