SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Miujiza/Nyongeza

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

MAAJABU YA CHUMA KATIKA KURUANI-NYONGEZA

Kwanza ningependelea kufupisha kwa ufupi Asili ya chuma katika manyota makubwa makubwa huko Mbinguni.

Nilizungumzia Muujiza wa Chuma katika Kuruani katika Milango mingineyo na leo Alhamdulilahi ningependelea kuongezea maajabu mengineyo kutoka katika Aya za Kuruani. Allahu Akbar.

Hebu kwanza tufanye ufupisho wa Asili ya Chuma katika Manyota Makubwa Mbinguni.

Nitapanga hapa chini hatua kwa hatua ya Elements mbali mbali zinazojenga Chuma.

Yaani Element ya Kwanza ni Hydrogen na zinapokutana Atom Mbili za Hydrogen na kusababisha Muungano (Fusion) basi Huzaa Element ya Helium. Na Hivyo Hivyo Atom ya Helium inapokutana na Atom ya Helium nyingineyo Na kusababisha Muungano (Fusion) basi huzaa Beryllium.

Nimepanga hapa chini Muungano au Fusion kuanzia Hydrogen mpaka Chuma (Iron) kwa njia rahisi= kueleweka:

Hydrogen + Hydrogen=Helium

Helium + Helium=Beryllium

Helium + Beryllium=Carbon

Helium + Carbon=Oxygen

Oxygen + Oxygen=Silicium

Silicium + Silicium=Nickel

Nickel inapopoteza Proton Moja  inageuka na kuwa Cobalt

Nickel =56/ 28/ Ni   

Cobalt= 56 /27 /Co  

Cobalt inapopoteza Proton Moja  inageuka na kuwa Iron

Iron=56 /26 /Fe  (Isotope namba 56/Proton 26)

Iron  (Chuma)haiwezekani kuzaliwa katika Dunia kwani Temperature ya Jua letu ni ndogo sana.

Chuma inataka Joto kali ambalo halipatikani Duniani.

Kwa hiyo Chuma inazalikana kwenye Manyota makubwa.

Na kisha kiwango cha Element za Chuma kikikizidi basi husababisha Nyota kupasuka.

Na mpasuko huo unajulikana kama “Supernova” na baadaye chembe na mapande hayo yaliyosambazwa kwa mripuko huo huja mpaka Duniani.

Na Chuma iliyopo duniani ni hiyo.

Kiwango cha Temperature ndani ya Jua ni 20 Million Degrees Centigrade na Temperature ya Manyota Makubwa huko Mbinguni ni  zaidi ya Jua yaani Mamia ya  Mamilioni  ya  Degrees Centigrade.

Na kiwango cha Chuma kinapozidi katika Nyota basi Nyota hiyo haiwezi kuvumilia bali hupasuka. Hujulikana kama  Supernova.

Na Mapasuko haya ndiyo yanayosababisha Mapande ya Chuma kusambaa Angani na Kuja Ardhini.

Kwa kifupi Chuma iliyopo Ardhini imekuja kwa njia hii. Yaani kwa njia ya Anga baada ya mapasuko kama haya tuliyoyasoma yaani Supernova.

Na Kuruani ni Muujiza huu sio mdogo kwani ilishuka katika karne ya 7 na inazungumzia habari hii ambayo imegunduliwa katika  Wakati  wetu huu wa Kisayansi na Teknologia.

Kwa kweli n iMuujiza sio mdogo. Katika Sura Ya Al-Hadiyd yaani Chuma ni Sura namba 57 ambayo ipo  katikati ya Kuruani katika Aya namba 25. inasema haya tunayosoma katika Sayansi.

لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلَنَا بِٱلۡبَيِّنَـٰتِ وَأَنزَلۡنَا مَعَهُمُ ٱلۡكِتَـٰبَ وَٱلۡمِيزَانَ لِيَقُومَ ٱلنَّاسُ بِٱلۡقِسۡطِ‌ۖ وَأَنزَلۡنَا ٱلۡحَدِيدَ فِيهِ بَأۡسٌ۬ شَدِيدٌ۬ وَمَنَـٰفِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعۡلَمَ ٱللَّهُ مَن يَنصُرُهُ ۥ وَرُسُلَهُ ۥ بِٱلۡغَيۡبِ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِىٌّ عَزِيزٌ۬ (٢٥) 25.

TAFSIRI

Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume Wetu kwa dalili waziwazi na Tukaviteremsha Vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. Na Tumeteremsha (Kutoka Mbinguni)chuma, yenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu; na ili Mwenyezi Mungu Ajulishe anayemnusuru na Mitume yake, na hali ya kuwa hawamuoni Mwenyezi Mungu. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.

SHEREHE

Katika Miujiza ni kwamba Sayansi inatuambia kwamba kwa wingi sana Chuma ipo katikati Ya Ardhi tunaoishi .Na Ajabu ni kwamba Sura Ya Al-Hadiyd  ipo katikati ya Sura za Kuruani. Yaani Hadiyd maana yake Chuma na ni Sura namba 57 katikati ya Sura 114 za Kuruani Tukufu. Allahu Akbar.

Lingine la kushangaza ni Jina la Sura “AL-Hadiyd”

Jina hili ukigeuza Herufi zake katika Namba ambazo Watu wa wakati huo wa enzi hizo yaani  Mwanzo wa Kuja Uislamu.

(Waarabu na Mataifa mengineyo katika yale yanayotokana na Phoenicians kama vile Greek, Gothic Copt, Cyrillic , Hebrew, au Arameen walikuwa wakitumia Herufi kuwakilisha Namba kwani Wakati huo kulikuwa hakuna Namba ambazo tunatumia leo kama vile 1, 2, 3, 4, 5 au zile namba za Kirumi (Romans). Kwa hiyo wakati huo Herufi zilitumika kama namba.

Kwa mfano Kundi La Herufi za Kwanza

Alif ilikuwa ikitumika kama Namba 1

Ba ilikuwa ikitumika kama Namba 2

Jim ilikuwa ikitumika kama Namba 3

Dal ilikuwa ikitumika kama Namba 4

na hivyo hivyo mpaka namba 9

Kisha Kundi la herufi za Pili

Ya ilikuwa ikitumika kama Namba 10

Kaf ilikuwa ikitumika kama Namba 20

Na hivyo hivyo mpaka namba 90

Kisha kundi la herufi la tatu

Qaf ilikuwa ikitumika kama Namba 100

Raa ilikuwa ikitumika kama Namba 200

Na hivyo hivyo mpaka namba 900

Na Namba Moja ya Mwisho yaani Herufi ya 28 ni Ghayn ilikuwa ikitumika kama Namba 1000.

Hizi ndizo namba za hapo zamani. Kwa hiyo namba za aina hii zilitumika wakati huo wa karne ya 7 katika maisha yao ya kila siku.

Kwa hiyo Herufi hizi ambazo zilitumika kama Namba na kwa hiyo Lugha ya Kiarabu ni mojawapo ya  Alphanumeric Languages  na pia zinaitwa Abjad au ABJD na  hujulikana kama Elimu ya Jumal.

Elimu hii pia hutumiwa na njia mbaya kama vile Kupigia BAO. BAO ni Haramu.

Usipige BAO kwani Unaingilia Kazi ya Mwenyeezi Mungu. Uchawi na Bao ni Haramu. Usisogelee Elimu hizi mbili ni Hatari. Hairuhusiwi katika Uislamu.

Jiepushe na Uchafu huu wa Mashetani.

Hapa tunatumia Thamani ya Herufi ili tusome Sayansi ya wakati huo ambayo inatufunulia Elimu za Kisayansi na Sio Upuuzi mwingine.

Usipoteze wakati katika Mabao na Uchawi. kwani ni Uchafu wa Mashetani. Kuwa macho na Uamke).

Sasa tukifasiri Herufi za Neno AL-Hadiyd kwa kutumia Thamani Hizi utaona Maajabu ya Kushagaza.

ٱلۡحَدِيدَ

Alif=1 Lam=30 Haa=8 Dal=4 Yaa=10 Dal=4

Tukijumlisha tutapata Namba ya kushangaza sana

1 + 30 + 8 + 4 + 10 + 4=57

Je Unaona? Ni Namba ya Sura ni Al-Hadiyd yaani  57

Ukiligeuza Jina hili katika Namba unapata namba ya Sura ambayo ni 57 pia!!!!

Angalia Maajabu ya Kuruani Tukufu.

Muujiza huu haukuishia hapa bali kuna mengi.

Nimetaja baadhi  katika sehemu nyingine ya website hii na hapa nitataja pia mengineyo.

Hebu tugeuze Herufi za neno Hadiyd bila ya Alif na Lam katika Namba  yaani bila ya Definite Article  A and  L

Al-Hadiyd maana yake “The IRON” na Hadiyd maana yake “IRON”

Haa=8

Dal=4

Yaa=10

Dal=4

Jumla ni 8 + 4 + 10 + 4=26

Angalia Maajabu. Muashirio wa kiajabu kwani  Iron au Chuma Ina Proton 26 na Electron pia 26

Na hii namba ndiyo inayojulikana kama Atomic Number ya Iron.

Na Maajabu haya hayakujulikana wakati huo wa Mtume Mohamad ﷺ Je unaona Muujiza ambao siyo mdogo.

Muujiza unaendelea……

Hebu tuhesabu Maneno kuanzia mwanzo wa Sura Ya Al-Hadiyd mpaka Kabla ya kipande cha Aya Kinachosema

وَأَنزَلۡنَا ٱلۡحَدِيدَ (Temeshusha Chuma)

tunapata Jumla ya maneno ni 461 na ukihesabu maneno kuanzia Mwisho wa Kipande hiki mpaka mwisho wa Sura Hii utapata idadi ya maneno ni 111

Jumla ni maneno 461 + 111= 572

na namba hii ni sawa na 22 X 26

Angalia Maajabu kwani Namba 26 ni Atomic Number ya Chuma. Chuma ina Namba za Protons 26 na Electrons 26.

Katika Elimu ya Hesabu Namba 26 ni Composite Number ya 16 katika mfululizo wa Composite Numbers na ajabu ni kwamba Neno Al-Hadiyd ni la 16 Ukihesabu Maneno kuanzia neno hilo  ٱلۡحَدِيدَ  mpaka mwisho wa Aya namba 25 Sura ya Al-Hadiyd inayozungumzia Chuma.

Na Namba 22 ni Composite namba 13 katika mfululizo wa Composite Numbers.

Na Ajabu ni kwamba Ukihesabu Maneno ya Aya Ifuatayo kuanzia Mwanzo wa Aya Hii utakuta neno ٱلۡحَدِيدَ  Al-Hadiyd ni la 13. Allahu Akbar.

Unaona Maajabu.

Hii ndiyo Saini yake Mwenyeezi Mungu. Allahu Akbar.

Angalia Maajabu. Allahu Akbar.

Aya hizi zimepangwa kimuujiza sana tena sana. Mwenyeezi Mungu mwenyewe amezipanga.

Siyo Mchezo au Uongo.

Soma mwenyewe kwani kila kitu kipo wazi. Jisomee kisha uchunguze. Kama huamini basi shauri lako mwenyewe.

لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا رُسُلَنَا بِٱلۡبَيِّنَـٰتِ وَأَنزَلۡنَا مَعَهُمُ ٱلۡكِتَـٰبَ وَٱلۡمِيزَانَ لِيَقُومَ ٱلنَّاسُ بِٱلۡقِسۡطِ‌ۖ وَأَنزَلۡنَا ٱلۡحَدِيدَ فِيهِ بَأۡسٌ۬ شَدِيدٌ۬ وَمَنَـٰفِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعۡلَمَ ٱللَّهُ مَن يَنصُرُهُ ۥ وَرُسُلَهُ ۥ بِٱلۡغَيۡبِ‌ۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِىٌّ عَزِيزٌ۬ (٢٥)

Miujiza isiyo na Mwisho. Hebu tuendelee….

Sasa tuhesabu maneno kuanzia Neno ٱلۡحَدِيدَ   Al-Hadiyd mpaka Mwisho wa Sura. Ukifanya hivyo utapata Jumla  ya Maneno ni 112

Kama huamini hesabu mwenyewe utapata hivyo.

Chuma zipo aina Mbalimbali kufuatana na Uzito yaani Atomic Weight. yaani   ISOTOPE  kama inavyojulikana katika Elimu ya Chemistry.

Kuna Chuma aina ya  57 sawa sawa na Namba ya Sura ya  Alhadiyd. (Angalia Muujiza)

Na Kuna Chuma aina ya 56 

Ukijumlisha Aina Ya Chuma iliyo maarufu kwa wingi wake nayo ni Chuma aina ya 56, Electrons 26 na Kisha Nutrons 30 utapata namba hiyo 112 tulitaja hapa juu. (56 + 30 + 26=112)

Je unaona Ya kushagaza.

Huu ni Muashirio wa kiajabu sana. Inaashiria kwamba Kuruani ni lugha yake Muumba.

Ameumba kila kitu Na ndiye aliyeishusha.

Hakuna aliyeyajua haya wakati huo wa karne za zamani yaani karne ya 7 Mtume  ﷺ

Elimu hizi ni za kisasa baada ya Kupatikana kwa Vyombo vya hali ya Juu katika Teknologia mbali mbali. Huu siyo Muujiza mdogo. Hakuna aliyoyajua haya mpaka hii miaka ya karibuni.

Ni Ujinga mkubwa kudai kwamba Mtume ﷺ alikuwa Profesa wa Elimu ya Physics au Astrophyics au Chemistry. Huo ni Ujinga na uongo Mtupu.

Utafiti Huu Unathibitisha Kwamba

Mtume Mohamad ﷺ ni Mkweli na ujumbe wake ni wa kweli. Kuruani  ni kweli tupu. Mwenyeezi Mungu yupo na Utukufu wake ni mkubwa  sana. Kuruani ni ujumbe wa mwisho na ni Muujiza mkubwa sana tena sana tena  sana. Usipoteze wakati. Tumia kila sekunde katika kumtukuza mwenyeezi mungu. Moyo wako ujaze kwa umuhimu huu kila wakati mpaka mwisho wa maisha. Zama katika ufalme wa Mwenyeezi Mungu na usipoteze wakati katika vilivyoumbwa ukawa umemsahau aliyeviumba.

Kuweni Macho. Allahu Akbar.