SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Miujiza Ya Kuruani-1

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

TOFAUTI KATI YA NENO NYOTA NA SAYARI ( كَوۡكَبً۬ )

 سُوۡرَةُ الاٴنعَام فَلَمَّا جَنَّ عَلَيۡهِ ٱلَّيۡلُ رَءَا كَوۡكَبً۬ا‌ۖ قَالَ هَـٰذَا رَبِّى‌ۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَآ أُحِبُّ ٱلۡأَفِلِينَ (٧٦) فَلَمَّا رَءَا ٱلۡقَمَرَ بَازِغً۬ا قَالَ هَـٰذَا رَبِّى‌ۖ فَلَمَّآ أَفَلَ قَالَ لَٮِٕن لَّمۡ يَہۡدِنِى رَبِّى لَأَڪُونَنَّ مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلضَّآلِّينَ (٧٧) فَلَمَّا رَءَا ٱلشَّمۡسَ بَازِغَةً۬ قَالَ هَـٰذَا رَبِّى هَـٰذَآ أَڪۡبَرُ‌ۖ فَلَمَّآ أَفَلَتۡ قَالَ يَـٰقَوۡمِ إِنِّى بَرِىٓءٌ۬ مِّمَّا تُشۡرِكُونَ (٧٨)

Sura Ya Al-Annam Namba 6 Aya 76-78

TAFSIRI

76-Na usiku ulipomwingilia (lbrahimu na hali kakaa na makafiri), akaona Sayari (Neno Nyota limefasiriwa katika Tafsiri Nyinginezo), alinena (makusudi kutaka kuwavuta watumie fikira zao): “(Sayari) hii ni Mola wangu.” Ilipotua (ikapotea), alisema (kuwaambia wale makaftri kama kwamba yu pamoja nao katika ibada ile): “Sipendi wale wanaopotea (hawawepo ila wakati makhsusi tu).”

77-Na (usiku)alipouona mwezi unachomoza alisema (kuwaambia wale marafiki zake wa kikafiri): “Huu (mwezi) ndio Mola wangu.” Ulipotua alisema: “Asiponiongoza Mola wangu, bila shaka nitakuwa miongoni mwa watu wapotofu (wapotevu). (Na mola huyu hawezi kuniongoza kwani anakuwa hayupo wakati mwengine).”

78-Na (asubuhi mapema)alipoliona jua linachomoza alisema (kuwaambia): “Hili (jua) ndilo Mola wangu. Huyu Mola mkubwa kabisa.” Lilipotua alisema: “Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayoyashirikisha (na Mungu).

SHEREHE NA MAONI

Kuna tofauti kati ya Nyota na Sayari. Nyota ina mwanga wake mwenyewe kutokana na Athari za Nyuklia. Hewa ya Hydrogen inapobadilika kuwa Helium basi Kunasababisha Kuzaliwa kwa Nishati zenye kuleta joto kubwa katika nyota na hatimaye kusababisha Mwanga tunaouona. Ama Sayari hazina Harakati wala Nishati hizi na kwa hali hii hakuna Joto wala Mwanga. Lakini Mwanga wa Sayari unatokana na Mwanga Wa Jua. Katika Sayari zinazojulikana Venus ni Mojawapo, Sayari hii haina Mwanga wake na hutegemea Jua. Venus Ni Sayari ya pili baada ya Sayari Inayojulikana kama Mecury. Venus ina mwanga mkali baada ya Jua na Mwezi. Huonekana baada tu ya Jua kuzama na pia ya mwisho kuzama kabla ya Jua kuchomoza.

MAAJABU YA KURUANI AMBAYO HAINA KOSA LOLOTE. SAYARI NI NENO   كَوۡكَبً۬  VENUS NA SIYO NYOTA  (نجم )‎

Katika Aya tatu Sura ya Al-Anaam Aya Namba 76, 77 na 78 tunaelezewa habari za Nabii Ibrahim alipowadokeza jamaa zake ukweli wa Imani zao potovu. Alianza na “Kawkab” kisha “Mwezi” na mwishowe “Jua” akaawaambia wenziwe kwamba ikiwa Maumbile haya matatu yanakuja na kuzama basi siyo “Miungu” kwani Mungu wa Kweli haji na kupotea. Mungu wa kweli huwa kila wakati. Haiwezekani kuja na kutoweka kama vile “Kawkab”, au “Mwezi” au “Jua”. Alitumia Maumbo haya katika kuwalingania dini kwani katika wakati huo watu hao walikuwa wanaabudu Sayari, Jua, Mwezi na Miungu mbalimbali ambayo walichongea Masanamu pia. Waliabudu pia Wafalme na Mengineyo.Katika Mlango huu hatutaelezea Kisa cha Nabii Ibrahimu bali Tutachagua Neno Moja tu ambalo limechaguliwa Na Mwenyeezi Mungu kisayansi nalo ni “Kawkab” Tafsiri nyingi zimefasiri neno hili kama “Nyota” lakini Kisayansi ni “Sayari” Kwa hiyo tafsiri sahii ni kwamba Nabii Ibrahimu alipoona Sayari hii tu basi akaitumia katika kuwafundisha rafiki zake imani ya ukweli iliyo sahihi. Baada ya Sayari hii ambayo ni mara ya kwanza kuonekana akauliza swali la pili kwa kutumia “Mwezi” ambayo kisayansi inajulikana kama Satelite na siyo Planet au Star na kisha akatumia Neno Jua (Sun) Ijapokuwa Mwezi una sifa nyingi za kuweza kuitwa Planet lakini ni mdogo sana na hauna Mvuto au Force of Gravity kama vile Ardhi tunayoishi.Binaadamu tunaweza kufanya makosa katika kufahamu kuruani kwani elimu zetu bado changa lakini kuruani haikosei kabisa. Wafasiri wameandika kwamba “Kawkab” ni Nyota kwani walifuata Sayansi za hapo zamani na walidhani VENUS ni Nyota lakini sayansi na teknologia za leo zimegundua kwamba Venus siyo Nyota (Star) bali Sayari. Wafasiri walifuata Sayansi za hapo nyuma. Ingekuwa Kuruani imeandikwa na Binaadamu lingetumika neno  “Annajm” kwani ni nyota kwa kufuata sayansi za kale lenye maana ya Nyota (Star).  Na Pia Historia zinaashiria kwamba Kawkab  VENUS  ni miongoni mwa Miungu ya wakati huo. (Iliyojulikana kama Star of Ishtar) Kuruani haina kosa kabisa kusahihisha makosa katika fahamu zetu. leo hii ni Planet of Venus na siyo Star.

MUUJIZA WA KISA CHA VIJANA WA PANGO (SURA YA AL-KAHF NAMBA 18 KUTOKA AYA NAMBA 9 MPAKA 26)

Katika Mlango huu tutazungumzia muujiza wa kihesabu katika kisa cha watu wa pango  (Al-Kahf) lakini hawajui siri ambazo anajua mwenyeezi mungu peke yake na kwa hekima gani ametushushia habari ya vijana hao.

Tukichunguza tutaona kwamba mwenyeezi mungu ameweka muujiza mwingine wa kihesabu ambao unaoonyesha kwamba hii kuruani haikuandikwa na binaadamu au labda mtume aliandika.

Haiwezekani kabisa mtu kuweza kutunga kitabu kama hiki. Mfano mdogo ni sura hii, itawezekana vipi kuandika kisa kirefu kama hiki na huku unazingatia idadi ya maneno.

WATU HAWA WALILAZWA NA MWENYEEZI MUNGU KATIKA PANGO SIKU 309!!! NA MWENYEEZI MUNGU KATUMIA MANENO 309!!! YA KURUANI. HAKUNA MWANDISHI YEYOTE KATIKA DUNIA HII ANAYEWEZA KUANDIKA KISA NA HUKU ANAZINGATIA IDADI YA MANENO. NA HUU NI MFANO MMOJA TU KATI YA MIFANO MINGI KATIKA KURUANI.

Idadi ya Maneno yaliyotumika kutuelimisha kisa hiki ni sawa na miaka waliyolazwa hapo pangoni, na huu ni mfano mmoja tu kati ya mifano mingi katika kuruani.

Je mtume alikuwa na Calculator au Mashine ya hesabu ambayo alikuwa akiitumia wakati huo?

KISA CHA WATU WA PANGO NA MUUJIZA WA KIHESABU

Kisa Cha Watu Wa Pango kinahusiana na vijana wachache ambao walikuwa wacha mungu sana, hawa watu walikimbia dhuluma za mfalme ambaye alikuwa haamini mungu na wakaamua kukimbilia katika pango na hapo mwenyeezi mungu kwa hekima yake akawalaza kwa muda wa miaka mia tatu na tisa kwa tarehe za kikiristo au miaka mia tatu za tarehe za kiislamu. (Waislamu walianza kuandaa Calendar kuanzia hijra ya mtume wake wa mwisho Mohamed (Salamu na Amani za mola zimfikie)alipohama Mecca kuenda Madina na hiyo tarehe inakhitalifiana na tarehe za kikiristo kwa siku chache -kiasi cha siku kumi na moja-yaani Tarehe ya kiislamu ipo nyuma kwa siku kumi na moja). Kama tunavyoelewa tarehe za kiislamu zinatokana na hesabu ya mwezi na tarehe za wakiristo zinatokana na hesabu ya jua. Na mwenyeezi mungu anasema katika kisa hiki kuwa sisi waislamu tunahesabu miaka 300 na hao watu wa wakati huo walizidisha miaka tisa yaani jumla ya miaka 309. Dini ya watu hao walitumia tarehe za jua kama wakiristo hivi sasa.

Jambo la kushangaza ni kuwa idadi ya maneno yaliyotumika katika kisa hiki katika kuruani ni 309 pia.

Kuanzia mwanzo wa kisa neno LABITHU-katika aya namba kumi na mbili mpaka neno la pili-LABITHU-katika aya ya ishirini na tano, Baina ya maneno haya mawili maneno yaliyotumika katika kisa hiki ni 309 pia.

Tafsiri ya neno hili ni “Walikaa hapo pangoni””na huku wamelazwa kwa muda huo.

Katika kisa hiki watu hao walikuwa wanapinduliwa kushoto kisha kulia kama kwamba ni wagonjwa hospitalini hawawezi kulala upande mmoja tu bali kupinduzwa kushoto kisha kulia ili wasiumie.

Na walikuwa na mbwa ambaye pia alilazwa kama wao. Baada ya miaka 309 wakaamshwa na mwenyeezi mungu na wakabaki wanajadiliana mda waliolala na hali hawajui mda huo bali kukisia tu, baadhi yao wakasema tulilala kwa siku moja na baadhi wakasema chini ya siku moja. Wakaamua kumtuma mmojawao kwa siri sana kwenda mjini kutafuta chakula.

Alipofika mjini akakuta mabadiliko tofauti na hali walioacha kwani mfalme wa wakati huo baada ya miaka 309 ni mtu mungine ambaye alikuwa mcha mungu.

Na huko mjini katika kutoa pesa alizokua nazo ili apate kununua chakula akakamatwa kwani alikuwa na pesa za zamani sana na habari za vijana hao zilikuwa zikijulikana.

Wakamuomba mtu huyo awapeleke katika pango walilolazwa, Watu wakaenda katika pango hilo.

Baada ya hapo vijana hao walifishwa na mwenyeezi mungu kwani ndivyo alivyotaka iwe hivyo, mwenyeezi mungu alipanga hivyo ili watu wapate kujua uwezo na ukubwa wake. wa kuumba na kufisha.

Kisa hiki kinaishia kwamba watu hao walijengewa msikiti hapo walipofariki kama kuruani inavyotuambia.

Pia mwenyeezi mungu anatueleza katika aya ya 22 ya sura hii kuhusu idadi ya vijana hao kwani hakuna anayejua isipokuwa wachache aiyewachagua yeye mwenyeezi mungu peke yake.

Aya hii ni namba 12 ya Sura ya Al-Kahf tafsiri yake; 

“kisha tukawafufua ili tujuulishe ni lipi katika makundi mawili lililohisabu sawasawa muda waliokaa (hawa vujana wa pangomi)

ثم بعثنهم لنعلم اي الحزبين احصي لما لبثوا امدا

Aya inayofuata namba 25 ya Sura ya Al-Kahf tafsiri yake; 

“Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu na wakazidisha (miaka) tisa”. (Miaka 300 kwa hesabu ya miaka ya calendar ya kiislamu ambayo ni Lunar Calendar

Na ni miaka 309 kwa hesabu ya calendar za wakati huo na sasa pia zinaitwa Solar Calendar)

و لبثوا في كهفهم ثلث مايه سنين و ازدادوا تسعا

Baina ya Aya hizi mbili kuna habari za watu hao na kisa kimeelezwa vizuri sana katika kuruani.

Mtume Mohamed alipooulizwa na makafiri kuhusu habari hizi basi hakubabaika kwani mwenyeezi mungu alimshushia kisa na akafundishwa kwa ukamilifu.

KIsa hiki kina miujiza mingne ya kisayansi lakini tutatosheka na huu muujiza mmoja wa kihesabu ambao unatosha kujenga imani zetu.

MAFUNDISHO TUNAYOPATA KUTOKANA NA KISA HIKI

Kwa kifupi kuna siri kubwa katika Kuruani na kisa hiki ni mfano kwetu tunafundishwa tushike ibada sana na tusibabaike na dunia na pia dua nzuri sana walioitumia watu hao hapo pangoni katika aya YA 10 ya sura hii ya Al-Kahf wakisema;

“Mola wetu, tupe rehema zinazotoka kwako na tutengenezee uwongofu katika (kila) jambo letu” (Ni Dua nzuri kuitumia katika maisha yetu)

اذ اوي الفتيه الي الكهف فقالوا ربنا اتنا من لدنك رحمه و هيي لنا من امرنا رشدا

MUUJIZA WA KIWANGO CHA DHAHABU “GOLDEN RATIO” KATIKA KURUANI

Namba  inayojulikana kama 1.618  kwa jina la Kigiriki kama “Phi” (linatokana na Mgiriki anyeitwa Phidias) Namba hii ni kiwango cha mgawanyiko wa namba mbili. Wanasayansi ambao mashabiki wa elimu hii wanatuambia kwamba kila kilicho kizuri duniani ukipima marefu na mafupi yake basi utapata namba hii. Mfano ni kipimo cha urefu kugawa na upana wa uso wa binaadamu au kipimo kutoka midomo mpaka nyusi kugawa na urefu wa pua, au urefu wa uso kugawa na urefu kutoka kidevu mpaka nyusi, au urefu wa mdomo kugawa na upana wa pua na hivyo hivyo viungo vya mwili mzima wantuambia kwamba vikipimwa na ikiwa namba hii inapatikana basi inaonyesha uzuri na kupendeza kwa umbile hilo, na hali kadhalika wachoraji hutumia vipimo hivi katika kazi zao ili wachore picha zinazopendeza. 

Mashabiki wa kisayansi hao wanatuambia kwamba namba hii inaonekana katika kila umbile duniani kama vile maua, miti, wanyama, nyota, na kila kitu. Kiwango hiki cha 1.168 ni kiwango kkinachoonyesha uzuri na ukamilifu wa kila kitu kilichoumbwa duniani. 

Na watafiti hao wamefanya uchinguzi katika maumbile mbalimbali na maandishi mengi na video mbalimbali zimetolewa kuhusu jambo hili.

Namba hii inapatikana katika majenzi makubwa ya Piramidi huko Egypt miaka 4600 iliyopita nayo inaonyesha kwamba namba hii huenda ilianzi wakati huo. Na pia ipo kaika enzi za Ugiriki wana historia wanasema kwamba Phidias alitumia namba hii katika ujenzi wa jengo maarufu linaloitwa  “Parthenon”.huko  Ugiriki (Athens) miaka 440 kabla ya Kipindi cha Ukristo.

Wasanii wengineo waliokuja baadaye waliitumia namba hii katika kazi zao. Mfano ni Msanii Mchoraji maarufu anyejulikana kama Leonardo Da Vinchi aliitumia katika michoro yake.

Angalia picha hapa chini inayoonyesha Nadharia inayoelezea namna ya kuhesabu namba hii ambayo hutumika katika shughuli mbalimbali za kisanii.

Ukigawa Urefu wa umbile lolote jumlisha Ufupi wa umbile hilo chini ya Urefu huo basi ni sawa na kugawa namba ya upande ulio mrefu chini ya namba ya upande mfupi utapata Namba ya Dhahabu ambayo inaitwa Phi kama unavyoona Symbol ya alama hiyo hapa katika picha hii

Video inatufahamisha Golden Ratio kwa ufupi

Mwanachuoni maarufu Liyezaliwa Italia katika mji unaoitwa “Pisa” anyejulikana kama  Leonardo Fibonacci ambaye alikuwa mtaalamu maarufu wa mahesabu ambaye alileta nadharia inyojulikana kama “Fibonacci Senquence” Na ndiye aliyeingiza elimu ya namba za kiarabu na  kihindi katika nchi za ulaya ambazo zinazotumika mpaka leo. Kuanzia namba 0 mpaka 10.

Nadharia yake inauhusiano na namba inayojulikana kama “Kiwango cha Dhahabu”  namba hizo zinaanzia na 1, 1, 2, 3, 5, 8, 13, 21 ukiangalia utaona kwamba namba 2 ni 1+1 , na namba 3  ni 2+1, na namba 5 ni 3+2, hivyo hivyo namba hizi akijuumlisha anapata namba nyingineyo na hali hiyo inaendelea bila mwisho. Lakini ukigawa namba 3  katika 5 utapata namba ya dhahabu ambayo ni 1.6  na hali kadhalika ukigawa 8 katika 13 utapata 1.6  na hivyo hivyo mpaka mwisho namba hii ya dhahabu haibadiliki.

Leonardo pia aliandika na kuchangia katika namba za decimali na aliandika kitabu maarufu cha square numbers kinachojulikana kama “Liber Quadratorum” 

Watafiti wameziangalia namba hizi katika kila kiumbe kama nilivyotaja hapo juu na kukuta kwamba kila kitu kinafuata mpangilio wa namba hizi za Leonardo kuanzia 1, 1, 2, 3, 5, 8, 13, 21.  

Picha za hapa chini zinatufafanulia zaidi kuhusu nadharia hii.

Jengo linaloitwa Parthenon huko ugiriki limejengwa kwa kutumia vipimo vya “Goden Ratio” kama hapa katika mstatili huu wa upimo unavyoonesha kwa mchoro unaofahamika kama Fibonacchi Spiral

Matawi ya miti yameota kufuatana na nadharia ya fibonachi. Kila hatua matawi yanota kwa namba hiyo kuanzia shina kisha matawi 2 kisha 3 mpaka 21 na namba hizi ukizigawa utapata namba ya golden ratio 1.6

matawi katika jani pia ukipima utapata namba 1.6 ya golden ratio

Maua yameota kwa kufuatia namba ya Fibonacchi ambayo inatupa namba 1.6 unapogawa. Petali zimejipanga kufuatana na nadharia ya Fibonacchi

kipimo cha mkono na namba inayopatikana ni ile ile ya Golden Ratio 1.6

Wataalamu wanapima kila kiungo cha binaadamu katika kutafuta namba ya kiwango cha dhahabu.

KATIKA ULIMWENGU JE TUNAPATA NAMBA HII YA “KIWANGO CHA DHAHABU”; Golden Ratio?

Watafiti wanatuambia kwamba Nyota, Galaxies na  Bahari na kila kitu kimeumbwa kufuatana na hesabu hii.

Jambo la kushangaza ni Mji wa Mecca pia inashangaza sana kuona kwamba kipimo katika ramani ya dunia utaona  Mecca ipo katika kipimo hiki cha 1.6 kama ifuatavyo:

HESABU YA NISBA AU RATIO KWA KUTUMIA DEGREES

MECCA

LATITUDE

(Degrees, Minutes and Seconds) 21.43’7273″

LONGITUDE

(Degrees, Minutes and Seconds) 40.51’2714″

————————————————–

KIPIMO CHA LATITUDE

Kutoka North Pole mpaka Mecca (Degrees, Minutes and Seconds) 90.0000-21.437273=68.56’2727″

Kutoka Mecca mpaka South Pole (Degrees, Minutes and Seconds) 90.0000+21.437273=111.43’7273″

Ukigawa Degrees hizi mbili; 111.437273 kwa 68.562727

(Umbali wa kutoka North Pole mpaka Mecca na Umbali kutoka Mecca mpaka SouthPole) utapata Namba 1.6 ambayo ni Golden Ratio.

————————————————-

KIPIMO CHA LONGITUDE

Kutoka Mecca (kwa upande wa Magharibi) mpaka International Date Line (Degrees, Minutes and Seconds) 180.0000 + 40.512714=220.51’2714″

Kutoka Mecca (Kwa upande wa Mashariki) mpaka International Date Line (Degrees, Minutes and Seconds) 180.0000-40.512714=139.48’7286″

Ukigawa Degrees hizi mbili:220.51’2714 kwa 139.48’7286 (Umbali wa kutoka Magharibi ya Mecca mpaka International Date Line na Umbali kutoka Mashariki ya Mecca mpaka Internationa Date Line)utapata Namba 1.5808 ambayo ni sawa na 1.6 na ambayo ni Golden Ratio

————————————————–

HESABU YA NISBA AU RATIO KWA KUTUMIA MAILI NA KILOMETERS

Umbali Kutoka South Pole mpaka Mecca ni 7688 miles /12372 km na umbali kutoka Mecca mpaka north pole ni 4742 miles /7632 km

Ukigawa Maili hizi mbili 7688 kwa 4742 utapata namba 1.6 ambayo ni Golden Ratio Na ukigawa Kilometer 12372 kwa 7632 utapata pia 1.6 ambayo ni Golden Ratio.

NAMBA YA NISBA YA DHAHABU (GOLDEN RATIO) KATIKA KURUANI TUKUFU

Tutakuta pia katika kuruani jambo hili la Ratio ya dhahabu katika aya ifuatayo:

إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٍ۬ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِى بِبَكَّةَ مُبَارَكً۬ا وَهُدً۬ى لِّلۡعَـٰلَمِينَ (٩٦)

Tafsiri  ya aya hii katika sura namba 3 Aya namba 96  ni kama ifuatavyo

“kwa yakini nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyoko Mecca, yenye baraka na uwongozi kwa ajli ya walimwengu wote”.

Aya hii ukiigawanya katika mafungu mawili katikati katika neno   MECCA ambalo linajulikana hapa kwa lugha ya kiarabu kama BACCA utapata herufi 29 kuanzia mwanzo wa Aya mpaka neno BACCA na baada ya hapo ni herufi  18. Usisahau kuhesabu  “shadda” kama herufi mbili kwani kiarabu ina maana hiyo. kwa mfano herufi INNA  ina herufi mbili “IN  na NA” na hizi ziliunganishwa zikawa INNA kwa shadda.  Ajabu ni kwamba ukigawa 29 kwa 18  utapata pia namba  1.6 ambayo pia ni “Golden Ratio”.

Mecca ni nji mtukufu na mwenyeezi Mungu ametaja utukufu wake katika Aya hii. Ikiwa namba hii ambayo wataalamu wanasema ni dalili ya uzuri wa maumbile basi itakuwaje kuruani ambacho ni kitabu chake Mola kisiwe kizuri pia.

Na kama tulivyoona katika Aya hii Mwenyeezi Mungu anatuonyesha utukufu wa mji wa Mecca na kithibitisho kwa wana sayansi wa leo waliokuja na hii namba ya kuthibitisha uzuri wa maumbile ulimwenguni.

Kwa hiyo kuruani ina muujiza katika herufu, maneno, mismiati, vishazi na mpangilio wa hivyo vyote, Ni muujiza katika kila sura, aya, na maana ya maneno pia.

Hii inaonyesha kwamba aliyetuumba ndiye yule yule aliyeumba ulimwengu na ndiye aliyeshusha kuruani hii. 

Kama tulivyosema hapo awali ulimwengu ni kuruani tunayoiona na kuruani ni ulimwengu tunaousoma.

Basi baada ya kuelewa haya je wanaadamu wana hoja tena?  

Hatuna mengi isipokuwa kunyamaza na kusema

“marejeo yetu ni kwa mola wetu”

Ndugu waislamu tumche mungu na tumuombe atupe hekima ili itusaidie katika kutupa utulivu katika imani zetu na pia tunamuomba mwenyeezi mungu atutakabalie juhudi hizi.

Kama kuna makosa basi ni yetu wenyewe na kama tumepata basi inatoka kwa mwenyeezi mungu ambaye hakosei.

NImeongeza hapa chini  Utafiti mwingine katika Sura Ya Al-Nahl ambao unashangaza sana. Allahu Akbar.

GOLDEN RATIO KATIKA SURA YA Al-Nahl

Baada ya kugundua Aya Nyingine inayohusiana na Kiwango Cha Dhahabu (Golden Ratio) nimeona Bora nielezezee chini ya Mada  niliyofanya hapa Juu siku za nyuma. Alhamdulilahi. Katika Sura Ya Al-Nahl Aya yenye kuzungumzia Neema za Mwenyeezi Mungu ambazo tukihesabu hazina mwisho inashangaza san kwani tunapata  Goden Ratio kwa wazi wazi na inalingana sana na Madhumuni Ya Aya Hii. Kama vile neema za Mwenyeezi Mungu hazina Mwisho basi  Namba ya Golden Ratio pia ni Irrational Number yaani ni namba isiyo na Mwisho. Angalia Maajabu. Kwa kadiri unavyogawa namba zinazofuatana yaani namba za Fibonacchi (Huyu ni Mtaalamu wa hesabu aliyeishi huko Italia. Yaani ni Mwitalia) basi hupati namba iliyokamilika bali Unapata Namba na sehemu yaani mabaki kama vile Namba ya Decimal. Na utaendelea kupata Mabaki haya bila mwisho. Sasa angalia mfananisho huu wa kiajabu. kwani Aya hii inasema Neema za Mwenyeezi |Mung uhazina Mwisho. Allahu Akbar.

Sura Ya Al-Nahl Namba 16 Aya Namba 18

وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآ‌ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬ (١٨)

TAFSIRI

18.Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamtaweza kuzihisabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu.

SHEREHE YA AYA KUFUATANA NA GOLDEN MEAN AU GOLDEN RATIO

Aya hii inazungumzia Neema alizotupa Mwenyeezi Mungu na ambazo kama anavyosema ni nyingi sana kiasi ambacho huwezi kuzihesabu neema zake zote. Kuna Muujiza Mwingine unajitokeza katika Aya Hii na ambao una uhusiano na Kiwango cha Dhahabu. (Golden Ratio au Golden Mean) Habari hii nimeizungumzia katika Mlango wa “Miujiza Ya Kuruani-1” Ya Website hii. Aya Hii inagawanyika katika Sehemu mbili Sehemu ya kwanza inasema

وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَا

“Na mkihisabu neema za Mwenyezi Mungu hamtaweza kuzihisabu”.  Na sehemu ya pili inasema

إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬

“Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu”.

Uhusiano huu unashangaza kwani unathibitisha Nadharia hii kwamba ni ya kweli. Tunaamini kwamba Kuruani ndiyo Rula au kipimo chetu katika Maisha. Kuruani haikosei katika kila kitu kwani Mwenyeezi Mungu ndiye Muumbaji na hakosei na maneno yake ni sahihi. Tukihesabu Herufi utapata Herufi 24 katika kipande cha kwanza

وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَا

na herufi 15 katika kipande cha pili kinachosema

إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬ .

Ukigawa ili kutafuta Kiwango Cha Dhahabu “Golden Ratio” utapata kama ifuatavyo: 24/15=1.6 na 1.6 ni Golden Ratio

Na ajabu nyingine ni kwamba Namba Ya Sura na Aya inatupa namba ya Golden ratio Pia Yaani Sura na Aya= 16:18 na hii ni Sura namba 16 Aya namba 18 (sawa na namba ya Golden Ratio ambayo ni 1.618) Tukichunguza zaidi kwa kugawa Golden Ratio kwa Jumla ya Herufi za vipande viwili (24 + 15=39) yaani 39 Kugawa kwa 1.618 utapata 24.1 (Idadi ya herufi za kipande cha kwanza ni 24) na nukihesabu maneno utapata maneno 6 katika kipande cha kwanza na maneno 4 katika kipande cha pili. Ukigawa Gokden Ratio na Jumla ya Maneno yote ambayo ni 6 + 4= 10 yaani 10 kugawa kwa 1.618 utapata 6.1 (Idadi ya Maneno katika Kipande cha kwanza ni 6)

Tunasoma katika Elimu ya Hesabu kwamba Namba ya Golden Ratio ni Irrational Number na Haina mwisho kwani ukigawa namba Mbili yaani baina ya namba kubwa na ndogo na kuendelea kufanya hivyo basi namba utakayopata itakuwa namba kamili na sehemu ambazo haziishi. 1.61803398874989484820… (etc.) yaani haina mwisho. Je unaona hii namba haina mwisho na Neema za Mwenyeezi Mungu katika Aya Hii pia Hazina Mwisho na huu mfananisho wake Mwenyeezi Mungu. Allahu Akbar. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi. Hesabu Hapa Zinazungumza. Na mfano huu unakwenda sambamba na Aya Inayohusiana na Neema za Mwenyeezi Mungu ambazo hazina Mwisho. Huu Ni Muujiza unaonekana Kama Jua la mchana. Kwa kweli Aya Hii inathibitisha kuhusu kuwepo kwa Golden Ratio. Katika Elimu ya Hesabu tunasoma kwamba

(The Golden Ratio is equal to:

1.61803398874989484820… (etc.) The digits just keep on going, with no pattern. In fact the Golden Ratio is known to be an Irrational Number. The Golden Ratio is also sometimes called the golden section, golden mean, golden number, divine proportion, divine section and golden proportion).When we take any two successive (one after the other) Fibonacci Numbers, their ratio is very close to the Golden Ratio “φ” which is approximately 1.618034…

Kwa hiyo Golden Ratio ni jawabu unapogawa namba mbili za Fibonacci zinazofuatana ambazo mojawapo huwa ni kubwa na nyingine ni ndogo. Jawabu haliwi kamili na utaendelea kupata jawabu na mabaki bila ya mwisho kwa mfano 1.61803398874989484820… (mabaki yasiyo na Mwisho).

MBINGU NA ARDHI (Expansion and Force of Gravity)

MTANUKO NA MVUTANO WA ULIMWENGU

Wanasayansi Wa Elimu Za Anga walifanya utafiti tangu muda mrefu sana katika kutatua suala la mpanuko wa mbingu (Expansion of The Universe) Na pia Mvuto wa Maumbile angani ambayo yanasababisha Mbingu kujirudia.

Katika Mwaka 1917 Walikubaliana kwamba Ulimwengu Haupanuki (Yaani hakuna harakati zozote) Na kwa hiyo Upo katika Utulivu (Static). 

Hesabu za Einstein (ambaye alikuwa mwanasayansi mkubwa na pia maarufu) zilionyesha kwamba ulimwengu hauna utulivu na pia upo katika harakati lakini ili kuwaridhisha wanasayansi wa wakati huo aliongeza katika hesabu zake Namba inyojulikana kama LAMBDA (Λ) ambayo ilisaidia katika kuufanya ulimwengu kuwa na utulivu au Static.

Kufanya hivyo ilikuwa kosa kwani hapo awali hesabu zake zilikuwa zinaonyesha ukweli na hapo baadaye alijuta sana na kusema kwamba “Ni kosa kubwa wa maisha Yangu” kwani utafiti wake wa awali ulikuwa sahihi lakini alifuata fikra za wanasayansi wa wakati huo ambao walikosea na pia kulikuwa hakuna vyombo vya utafiti vilivyokuwa nyuma sana.

Na Katika Mwaka 1929 Edwin Hubble akagundua kwamba ulimwengu unatanuka.(In 1929, Edwin Hubble, an astronomer at Caltech, made a critical discovery that soon led to scientific answers for these questions: he discovered that the universe is expanding). Kwa Hiyo Einstain hakukosea katika hesabu zake.

kuna Muujiza katika Kuruani Tukufu kuhusiana na Mwaka 1929 Katika Aya Ifuatayo:

Sura Namba 21 Aya Namba 30

أَوَلَمۡ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ ڪَانَتَا رَتۡقً۬ا فَفَتَقۡنَـٰهُمَا‌ۖ وَجَعَلۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ كُلَّ شَىۡءٍ حَىٍّ‌ۖ أَفَلَا يُؤۡمِنُونَ (٣٠)

Tafsiri Ya Aya

Je! hawakuona wale waliokufuru ya kwamba mbingu na ardhi Vilikuwa Vimeambatana, kisha tukaviambua, (tukavipambanua): Na tukafanya kwa maji kila kitu kilicho hai. Basi jee hawaamini?

Utafiti Katika Kipande cha Aya:  ڪَانَتَا رَتۡقً۬ا فَفَتَقۡنَـٰهُمَا‌ۖ

Hapo zamani Herufi au Alphabet ya Lugha ya Kiarabu na pia lugha nyinginezo za Semitic kama vile Hebrew, au Aramaic zilitumika kuwakilisha namba kwani namba 1 mpaka 9 na 0 zero zilikuwa bado kugunduliwa, Na Ni Elimu inayojulikana kama Elimu Ya Joumal au Gematrical Values. Namba Hizi tukizitumia katika Kufasiri Herufi za Aya Hii tutapata kama ifuatavyo hapa chini: Tutahesabu Herufi Kuanzia Kushoto kwenda kulia kufuatana na sheria ya lugha ya kiarabu. Kwa hiyo Neno ڪَانَتَا Namba zake ni 1+400+50+1+20 , neno رَتۡقً۬ا namba zake ni 1+100+400+200 na neno َفَتَقۡنَـٰهُمَا namba zake ni 1+40+5+50+100+400+80+80 Ukijumliisha Namba Hizi ambazo zinawakilisha Herufi za Aya Tutapata namba 1929 ambayo inalingana na Mwaka ambao Wana Sayansi Waliogundua Na Kuthibitisha Kwa Kutumia Vyombo Vya Sayansi Kwamba Ulimwengu Unatanuka (Expansion of The Universe). 1+40+5+50+100+400+80+80+1+100+400+200+1+400+50+1+20=1929

Na katika mwaka 2011 Wanasayansi watatu Perlmutter (American), Schmidt (American-Australian) and Riess (American) walitunikiwa zawadi kubwa ya Nobel Prize kwa kugundua kwamba Ulimwengu unatanuka lakini kwa mbio mbio (accelerated expansion) na kwa hiyo hiyo Hesabu Aliyofanya Einstain waliigeuza kidogo ili iwiane na waliyoyagundua.

Kwa hiyo tumeona karibu karne nzima wanasayansi mbalimbali wanahangaika kujua habari kama hizi lakini maajabu makubwa ni kwamba katika kuruani tukufu tunaelezwa habari hizi katika Aya mbili tu zifuatazo:

Chapter (51) sūrat l-dhāriyāt (The Wind that Scatter)

 وَٱلسَّمَآءَ بَنَيۡنَـٰهَا بِأَيۡيْدٍ۬ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ (٤٧) 

And the heaven We constructed with strength and we are expanding it.

Chapter (35) sūrat fāṭir (The Originator)

۞ إِنَّ ٱللَّهَ يُمۡسِكُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ أَن تَزُولَاۚ وَلَٮِٕن زَالَتَآ إِنۡ أَمۡسَكَهُمَا مِنۡ أَحَدٍ۬ مِّنۢ بَعۡدِهِۚۦۤ إِنَّهُ ۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورً۬ا (٤١)

God prevents the heavens and the earth from falling apart. If they do fall apart, then, no one besides Him can restore them. He is All-forbearing and All-forgiving.

Yaani katika Aya ya kwanza Sura Ya Adhariyat Mwenyeezi Mungu anatuambia kwamba Ulimwengu anautanua (Expansion) Katika hali ya kuendelea kuutanua.

Na katika Aya Ya pili Mola anatuambia kwamba yeye ndiye anashika mbingu na ardhi zisiondoke au kwa lugha nyingine anahukumu (control) mbingu na ardhi zisisambae wala zisijirudie na hii ina maana ya neno “Yumsiku” يُمۡسِكُ nililopigia mstari katika aya ya 41 sura ya fatir. Neno moja lina maana kubwa kwa lugha ya kisayansi tutasema ana “control expansion na force of gravity” ili kuwe na Balance kwa kutokusambaa wala kujirudia.

Na mpaka leo wanasayansi hawajajuwa kwa nini ulimwengu unapanuka na tena kwa mbio mbio, wanafikiri labda kuna Mada inayojulikana kama “Dark Matter” na hiyo inajulikana katika hesabu kama LAMBDA.(Λ)

Kwa hiyo neno “Yumsiku” (Λ) ndiyo hiyo “Dark Matter” au LAMBDA (Λ) ya kihesabu.

Basi hicho wanasayansi wasichojua na wanachotafuta ni Nguvu yake Mwenyeezi Mungu yeye ndiye anaye control mbingu na ardhi.

Jibu la wanayayansi lipo katika aya mbili hapa juu. Je unaona Muujiza mbele ya macho yako mwenyewe hapa juu? Sasa Mtume Mohamed alipata wapi Elimu kubwa kama hii ambayo imechukuwa muda mrefu wa utafiti  wa Wanasayansi wakubwa ulimwenguni?

Hii ni ushahidi kwamba yule aliyeshusha kuruani ndiyo yule yule aliyeumba ulimwengu au malimwengu.

HERUFI TWA, SIN NA MIN ZINATHIBITISHA KWAMBA IDADI AYA ZA KURUANI TUKUFU NI 6236!!! NA HESABU HII NDIYO PIA INAYOJULIKANA KABLA YA MUUJIZA HUU

Herufi zinazojulikana kama Herufi zisizojumuishwa au zisizoungana na herufi nyinginezo ili kuleta maana yenye kujulikana nazo Kwa Kiarabu hujulikana kama

حُرُوف مُقَطَّعَات au ḥurūf muqaṭṭaʿāt, na kiingereza “disjoined letters” or “disconnected letters. katika wakati huu wa sayansi na technologia hivi leo tunelezwa mengineyo tusiyoyajua . Katika Kuruani hizi herufi zimetajika katika sura 29 (tumezitaja hapa chini).

Utafiti uliofanywa katika herufi tatu Ṭā Sīn Mīm طسم (TWA, SIN, NA MIN) peke yake unatugundulia maajabu mengine mapya ambayo hayakujulikana hapo zamani. Herufi hizi 3 zimetajika katika mwanzo wa sura mbili: Ash-Shuʿārāʾ na pia mwanzo wa sura ya Al-Qaṣaṣ na idadi ya kukariri kwake tukizijumlisha tunapata idadi ya namba za Aya Za Kuruani kiajabu sana tena sana. Soma hapa chini mpangilio huu wa ajabu nao unashangaza sana.

Sura Namba 28 -Alkasas Aya 1-2

طسٓمٓ (١) تِلۡكَ ءَايَـٰتُ ٱلۡكِتَـٰبِ ٱلۡمُبِينِ (٢)

Tafsiri

Hizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha (kila kinachohitajiwa katika dini).

Sura Namba 26 sura -Ashuaraa Aya 1-2 طسٓمٓ (١) تِلۡكَ ءَايَـٰتُ ٱلۡكِتَـٰبِ ٱلۡمُبِينِ (٢)

Tafsiri

Hizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha (kila kinachohitajiwa katika dini).

Katika Kuruani yote kuna Sura 29 za mfano huu ambazo zimetanguliwa na herufi za aina hii (disjointed letters), nazo ni sura namba 2-3-7-10-11-12-13-14-15-19-20-26-27-28-29-30-31-32-36-38-40-41-42-43-44-45-46-50-68

Nazo kwa Majina Ni:

Al-Baqarah ʾAlif Lām Mīm الم /Āl Imrān ʾAlif Lām Mīm الم / Al-Aʿrāf ʾAlif Lām Mīm Ṣād المص / Yūnus ʾAlif Lām Rā الر /Hūd ʾAlif Lām Rā الر /Yūsuf ʾAlif Lām Rā الر /Ar-Raʿd ʾAlif Lām Mīm Rā المر / Maryam Kāf Hā Yā ʿAin Ṣād كهيعص /Ṭā Hā “Ṭā Hā” طه /Ash-Shuʿārā ʾṬā Sīn Mīm طسم /An-Naml Ṭā Sīn طس /al-Qaṣaṣ Ṭā Sīn Mīm طسم /Al-ʿAnkabūt ʾAlif Lām Mīm الم /Ar-Rūm ʾAlif Lām Mīm الم /Luqmān ʾAlif Lām Mīm الم /As-Sajdah ʾAlif Lām Mīm الم /Yā Sīn “Yā Sīn” يس /Ṣād “Ṣād” ص /Ghāfir Ḥā Mīm حم /Fuṣṣilat Ḥā Mīm حم /Ash-Shūrā Ḥā Mīm-Ain Sīn Qāf حم عسق /Az-Zukhruf Ḥā Mīm حم /Al Dukhān Ḥā Mīm حم /Al-Jāthiya Ḥā Mīm حم /Al-Aḥqāf Ḥā Mīm حم /Qāf “Qāf” ق /Al-Qalam Nūn ن /

Herufi hizi tatu katika طسٓمٓ ukizihesabu kukariri kwake katika herufi zote zisizoungana(disjointed letters) hapa juu utazikuta “twa-sin-mim” zimekariri kama ifuatavyo: TWA imekariri mara 4, SIN mara 5 na MIM mara 17 tukihesabu na kupanaga kufuatana na maandiko ya lugha ya kiarabu “kushoto kwenda kulia” basi tutapanga kama ifuatavyo:

17(Mim-hundreds)5 (Sin-disaines) Twa-4 unites)

Na ukipanga kwenda kushoto:

1754= MIM=17 SIN=5 TWA=4

Katika Sayansi za Hesabu namba 0 mpaka 9 inajulikana kama BASE 10 System. Kwa hiyo 4 na 5 zipo katika 10 BASE System lakini namba 17 haipo katika 10 BASE System, kwani Namba yoyote baada ya 9 inawakilishwa na Herufi. Kwa hiyo 10 ni A , 11 ni B, 12 ni C, 13 ni D, 14 ni E, 15 ni F,16 ni G, 15 ni H. Na kwa hiyo Itabidi tutumie Nidhamu ya 19 BASE (Tunachagua 19 kwani ndiyo namba ilitajwa katika sura ya Mudathir na ambayo imetuonyesha Miujiza mbali mbali kafika Kuruani Tukufu.(Tumeelezea namba 19 katika Video ya Mwaandalizi na pia sehemu nyingineyo katika website hii) Kwa hiyo katika 19 BASE system itaandikwa kama ifuatavyo: H54 (Yaani H hapa ni namba 17 nayo ni kukariri kwa herufi MIM, 5 ni SIN na 4 ni TWA) Kwa hiyo tukibadili kutoka katika 10 BASE System kwenda katika 19 BASE System utapata namba ya kushangaza sana nayo ni = 17 X 19 X19 (HUNDREDS) + 5 X19 (TENS) + 4 (UNITS)=6236 na namba hii inaashiria idadi ya aya za kuruani nzima!!!

Muujiza hapa ni idadi ya aya za kuruani zimehifadhiwa katika herufi hizi tatu (CODIFIED) kama kwamba Namba hizi ni Kufuli ambazo zinaonyesha kwamba kuruani imepimwa na ingepungua au kuzidishwa Aya moja tu basi tusingepata Muujiza huu na wala herufi TWA, SIN na MIM zisingeleta Muujza huu. Na hata katika Calculator Ya Internet (online calculator) unaweza kubadili namba hii H54 From 10 BASE SYSTEM TO 19 BASE SYSTEM na utapata jawabu kama hili hapa juu nililotumia Hesabu za Mkono. (Manually).

Na Mashafu wa Othman na hata Visomo mbalimbalii vyote utakuta jumla ya aya katika kuruani ni 6236.

Na Kithibitisho cha pili ni kwamba Mara ya kwanza Neno la ٱلۡقُرۡءَانُ (Kuruani) kutajika Kuanzia sura Ya Alhamdu ni katika Sura Ya Al-Bakarah namba 2 Aya Namba 185 (2:185) na mara ya mwisho kutajika ni katika Sura ya Al-Inshiqak namba 84 Aya Namba 21 (84:21) Na ukitoa namba hizi mbili (Kuruani ya Mwisho iliyotajika kutoka katika kuruani ya mwanzo kutajika) unapata 8421-2185=6236 ambazo ni idadi ya Aya za kuruani. Kipimo cha pili kinathibitisha idadi ya aya za kuruani tukufu kwamba ni 6236.

Sura Ya 2 Aya Namba 185= 2185

شَہۡرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِىٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلۡقُرۡءَانُ هُدً۬ى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَـٰتٍ۬ مِّنَ ٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡفُرۡقَانِ‌ۚ فَمَن شَہِدَ مِنكُمُ ٱلشَّہۡرَ فَلۡيَصُمۡهُ‌ۖ وَمَن ڪَانَ مَرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ۬ فَعِدَّةٌ۬ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَ‌ۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِڪُمُ ٱلۡيُسۡرَ وَلَا يُرِيدُ بِڪُمُ ٱلۡعُسۡرَ وَلِتُڪۡمِلُواْ ٱلۡعِدَّةَ وَلِتُڪَبِّرُواْ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَٮٰكُمۡ وَلَعَلَّڪُمۡ تَشۡكُرُونَ (١٨٥)

Sura Ya 84 Aya Namba 21=8421 

وَإِذَا قُرِئَ عَلَيۡہِمُ ٱلۡقُرۡءَانُ لَا يَسۡجُدُونَ ۩ (٢١)

Mwenyezi Mungu amehifadhi kuruani kwa njia mbalimbali na pia ameweka makufuli ya kila aina kwa njia mbali mbali. Kuruani imehifadhiwa katika fahamu na wanavyuoni dunia nzima na haiwezekani wala haitawezekana kubadilishwa, kugeuzwa kwa kuzidishwa wala kupunguzwa. Ingekuwa hivo basi tusingepata hesabu tuliyoiona hapa juu. Elimu za kisasa zinaanza kutuonyesha Miujiza katika Kuruani Tukufu.

Watu wenye Elimu kubwa kubwa ulimwenguni wameendeshwa mbio na Kuruani kwani Elimu yake ipo juu ya fahamu zetu.

Kwa hakika Mwenyeenzi Kubwa Ana Elimu Kubwa sana kama alivyosema katika Aya Ya Alkursiy. Kwamba Elimu Yake kubwa sana na wala Hatutaijua yote. Allahu Akbar. Allahu Akbar.

HESABU ZINAASHIRIA LAYLATU ALQADR KUWA NI TAREHE 27 KATIKA MWEZI WA RAMADHANI

Sura Namba 97  Aya Namba 1-5

سُوۡرَةُ القَدر

بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ

إِنَّآ أَنزَلۡنَـٰهُ فِى لَيۡلَةِ ٱلۡقَدۡرِ (١) وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ (٢) لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ خَيۡرٌ۬ مِّنۡ أَلۡفِ شَہۡرٍ۬ (٣) تَنَزَّلُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةُ وَٱلرُّوحُ فِيہَا بِإِذۡنِ رَبِّہِم مِّن كُلِّ أَمۡرٍ۬ (٤) سَلَـٰمٌ هِىَ حَتَّىٰ مَطۡلَعِ ٱلۡفَجۡرِ (٥)

Tafsiri Ya Sura 

Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na kuneemesha neema ndogo ndogo.

1-Hakika Tumeiteremsha (Qurani) katika Laylatul-Qadr (usiku wenye heshima kubwa), (usiku wa mwezi wa Ramadhani). 2. Na jambo gani litakalokujulisha (hata ukajua) ni nini huo usiku wa Laylatul-Qadr? 3· Huo usiku wa hishima (huo) ni bora kuliko miezi elfu. 4· Huteremka Malaika na roho (za viumbe watakatifu) katika (usiku) huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo 5· Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri.

SHEREHE ZA AYA HIZI

Wanavyuoni wanasema Mwenyeezi Mungu ameuficha usiku huu ili watu wazidishe ibada katika masiku 10  ya mwisho wa Ramadhani na pia  Kufuatana na Hadithi Ya Mtume ambayo inatuambia kwamba siku hiyo ipo katika masiku ya Witri au Odd (Tarehe 21, 23, 25, 27 na 29) Ya mwezi wa Ramadhani. Lakini Wanavyuoni kama vile  Cousin wake Mtume  anayejulikana kwa jina Ibn Abbas ameashiria kwamba siku hiyo huenda ni ya Tarehe 27.Kufuatana na Hesabu alizofanya ya Idadi ya maneno katika sura hii ya Alqadr ni 30 yaani inaashiria masiku ya mwezi mzima wa Ramadhani  na mpaka pale inaposema HIYA katika ibara  سَلَـٰمٌ هِىَ      (nimepigia mstari hapo Juu katika Aya ya mwisho) ni neno namba  27 Na neno “Hiya” katika Aya linaashiria  Ule Usiku Wa Alqadr.Yaani Salaama na Amani katika Usiku huo.

Kwa hiyo Huenda ikawa Tarehe 27 kwani Hesabu zinashangaza sana. Kuruani Kila Aya Imepimwa kiajabu Na Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Na Muashirio Mwingine wa Kushangaza ni  Ibara  “LaylatuAlqadr”  لَيۡلَةُ ٱلۡقَدۡرِ  ambayo Ina herufi  9 na  ibara hii imekariri mara 3.  Na ukifanya hesabu 9 mara 3 utapata 27 yaani LaylatuAlqadr katika sura hii imekariri mara 3 na jumla ya herufi zake ni 27

Hesabu hizi ni Kuruani na siyo Tafsiri. Ukitaka kuhesabu basi hesabu maneno ya Kuruani Sura Hapa Juu.

Je unaona Maajabu ya Kuruani. Huenda Ndiyo  tarehe 27 kufuatana na hesabu izi za kiajabu. Na Mwenyeezi Mungu Anaelewa zaidi. Allahu Akbar.

NYOKA NA MAAJABU KATIKA KURUANI TUKUFU

SAYANSI ZA NYOKA

Wataalamu Wanatuelezea Kuhusu Nyoka kwamba Kuna aina or Speshi (Species) zaidi ya 3000 ya Nyoka Duniani. Katika Hizi kuna Speshi 600 ambazo wana Sumu na kuna Speshi zaidi ya 200 ambao wanatumika katika kutengeneza madawa.

Na Nyoka wameumbwa na idadi ya Chromosomes mbalimbali zifuatazo:

Nyoka Nyingi ni Speshi (Species)zenye Chromosomes 36, na nyinginezo zenye Chromosomes 34,32,38,42.

(The vast majority of snakes have diploid numbers (2n) of 36 chromosomes, containing 16 macrochromosomes and 20 microchromosomes. However, variations involving macro and micro karyotypic structure and a diploid number have also been reported in different families across snake lineages)

Na ukichunguza utakuta Speshi (Species) Nyingi (Majority) zina Chromosomes 36

Na Kila Nyoka ana Chromosomes (Chembe Cha Asili Ya Kila Chenye Uhai)36(2 X 18) kama ifuatavyo; 16(2 X 8) Macro-Chromosomes + 20 (2 X 10)Micro-Chromosomes=Chromosomes 36(2 X 18)

AYA ZA KURUANI ZINAZOZUNGUMZIA NYOKA

Sura Namba 7 Al-Araf Aya Namba 107

فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ (١٠٧)

TAFSIRI YA AYA I07.

(Hapo Nabii Musa) akaitupa fimbo yake (chini).Na mara ikawa nyoka dhahiri.

Sura Namba 26 Al-Shuaraa Aya Namba 32 فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ (٣٢)

TAFSIRI YA AYA 32.

Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka dhahiri. Sura Namba 20 Al-Twaha Aya Namba 20 فَأَلۡقَٮٰهَا فَإِذَا هِىَ حَيَّةٌ۬ تَسۡعَىٰ (٢٠)

TAFSIRI YA AYA 20.

Akaitupa. Mara ikawa nyoka anayekwenda mbio.

SHEREHE ZA AYA KISAYANSI

Sura Namba 7, Al-Araf Aya Namba 107 na Sura Namba 26 Al-Shuaraa Aya Namba 32 zinafanana kimaana na Ukihesabu Herufi Kuanzia Herufi Ya Kwanza “FA” katika neno فَأَلۡقَىٰ mpaka herufi “NUN” Ya Neno ثُعۡبَانٌ۬ utapata Jumla ni Herufi 20 ambazo zinaashiria 20 Micro-Chromosomes Za Nyoka (Snake)

Na Ukihesabu Herufi za Sura Namba 20 Aya Namba 20 kuanzia mwanzo wa Herufi FA katika neno فَأَلۡقَىٰ mpaka katika Herufi “TAA” mwisho wa neno حَيَّةٌ۬ utapata Jumla ya Herufi 16 ambazo zinaashiria 16 Macro-Chromosomes Za Nyoka.

Ukijuumlisha Micro-Chromosomes 20 na Macro-Chromosomes 16 utapata Chromosomes za Nyoka 36 ambazo ni Speshi ya Nyoka mojawapo Maarufu. Huu Kweli Ni Muujiza sio Mdogo kwani Kuruani ilishuka Karne ya 7 na Sayansi hii ya Chromosomes iligundulikana Mwaka 1888 yaani karne ya 19.

Tukizipanga Aya hizi kufuatana na Mpangilio wa Kuruani utapata maajabu Mengineyo;

Sura Namba 7 Al-Araf Aya Namba 107

فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ (١٠٧)

Sura Namba 20 Al-Twaha Aya Namba 20

فَأَلۡقَٮٰهَا فَإِذَا هِىَ حَيَّةٌ۬ تَسۡعَىٰ (٢٠)

Sura Namba 26 Al-Sharaa Aya Namba 32

فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ (٣٢)

Hesabu Ya Kwanza (Muujiza)

Ukihesabu Maneno Kuanzia Aya Ya Kwanza فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ Kuanzia Neno la kwanza فَأَلۡقَىٰ mpaka neno Nyoka yaani ثُعۡبَانٌ۬ Utapata Jumla ya maneno Matano Na ukihesabu kwa kinyume (Reverse) kuanzia Neno مُّبِينٌ۬ Mwisho wa Aya namba 32 فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ Kisha Aya namba 20 فَأَلۡقَٮٰهَا فَإِذَا هِىَ حَيَّةٌ۬ تَسۡعَىٰ mpaka neno ثُعۡبَانٌ۬ katika Aya namba 107 فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ Utapata Maneno 13 na ukijumlisha 5 + 13=18 na hii ni Chrosmosomes za Kizazi au Haploid na Kama inavyoeleweka kwamba Chromosomes za Celi (Cells)zinakuwa Pairs na hujulikana kama Diploid yaani 2n. Kwa hiyo 2 X n(Haploid-Sex Chromosomes kama vile mfano wa Gametes katika Bilogy) ni 2 X 18=36 Muujiza ni Kwamba tunapata Chromosomes 18 ya Kizazi zinazojulikana kama Haploid au Sex Chromosomes.(X2 Haploid Chromosomes= 36 Diploid Chromosomes Kama Vile Mfano wa Somatic Cells katika Elimu ya Biology).

Hesabu Ya Pili (Muujiza)

Ukihesabu Maneno Kuanzia Aya Ya Kwanza namba 107 فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ Kuanzia Neno la kwanza فَأَلۡقَىٰ mpaka neno Nyoka yaani حَيَّةٌ۬ Katika Aya Ya Pili namba 20 فَأَلۡقَٮٰهَا فَإِذَا هِىَ حَيَّةٌ۬ تَسۡعَىٰ Utapata Jumla ya maneno Kumi Na ukihesabu kwa kinyume kuanzia Neno مُّبِينٌ۬ Mwisho wa Aya namba 32 فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ Mpaka Neno حَيَّةٌ۬ katika Aya namba 20 فَأَلۡقَٮٰهَا فَإِذَا هِىَ حَيَّةٌ۬ تَسۡعَىٰ utapata Maneno 8 na ukijumlisha 10 + 8=18 na hii ni Chrosmosomes za Kizazi au Haploid na Kama inavyoeleweka kwamba Chromosomes za Celi (Cells)zinakuwa Pairs na kujulikana kama Diploid yaani 2n. Kwa hiyo 2 X n(Haploid-Sex Chromosomes kama vile mfano wa Gametes katika Bilogy) ni 2 X 18=36 Muujiza ni Kwamba tunapata Chromosomes 18 ya Kizazi zinazojulikana kama Haploid au Sex Chromosomes.(X2 Haploid Chromosomes= 36 Diploid Chromosomes Kama Vile Mfano wa Somatic Cells katika Elimu ya Biology).

Hesabu Ya Tatu (Muujiza)

Ukihesabu Maneno Kuanzia Aya Ya Kwanza namba 107 فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ Kuanzia Neno la kwanza فَأَلۡقَىٰ mpaka neno Nyoka yaani ثُعۡبَانٌ۬ katika Sura namba 26 Aya namba 32 Utapata Jumla ya maneno 16 Na ukihesabu kwa kinyume kuanzia Neno مُّبِينٌ۬ Mwisho wa Aya hii namba 32 فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ mpaka neno ثُعۡبَانٌ۬ ya Aya Hii Hii Utapata Maneno 2 na ukijumlisha 16 + 2=18 na hii ni Chrosmosomes za Kizazi au Haploid na Kama inavyoeleweka kwamba Chromosomes za Celi (Cells)zinakuwa Pairs na kujulikana kama Diploid yaani 2n. Kwa hiyo 2 X n(Haploid-Sex Chromosomes kama vile mfano wa Gametes katika Bilogy) ni 2 X 18=36 Muujiza ni Kwamba tunapata Chromosomes 18 ya Kizazi zinazojulikana kama Haploid au Sex Chromosomes.(X2 Haploid Chromosomes= 36 Diploid Chromosomes Kama Vile Mfano wa Somatic Cells katika Elimu ya Biology).

Kama tulivyoona hapa juu Hizi Hesabu Tatu hapa Juu. (5 + 13=18 na 10 + 8=18 na 16 + 2=18)Ni Namba za kushangaza sana kwani tunapata 18 Pairs za Chromosomes Yaani 18 X 2=36 za Nyoka.

Hesabu Ya Nne (Muujiza)

Sura Namba 26 Al-Sharaa Aya Namba 32

فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ (٣٢)

Namba 26 katika Elimu ya Hesabu inajulikana kama Composite Number nayo ni ya 16 katika mfululizo kuanzia mwanzo wa Composite Numbers. Na namba 16 ni Macro-Chromosomes za Nyoka Namba 32 katika Elimu ya Hesabu inajulikana kama Composite Number nayo ni ya 20 katika mfululizo kuanzia mwanzo wa Composite Numbers. Na 20 Ni Micro-Chromosomes za Nyoka Jumla ya 16 + 20=36 na kama tulivyosema kwamba 36 ni Jumla ya Chromosomes za Nyoka.

Hesabu Ya Tano (Muujiza)

Sura Namba 26 Al-Sharaa Aya Namba 32

فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعۡبَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ (٣٢)

Ukihesabu Nuqta/Dot au Diactritic Points (The i’jām ⟨إِعْجَام) katika Herufi za Aya hii pia zina muujiza wa kushangaza. Herufi Faa Ya kwanza Ina Nuqta 1, Herufi Qaf ina Nuqta 2, Herufi Faa Ya Pili Ina Nuqta 1, Herufi Dhal Ina Nuqta 1, Herufi Yaa ina Nuqta 2, Herufi Thaa ina Nuqta 3, Herufi Baa ina Nuqta 1, Herufi Nun ina Nuqta 1, Herufi Baa Ina Nuqta 1, Herufi Yaa ina Nuqta 2 na Herufi Nun Ya Pili ina Nuqta 1 Ukijumlisha Nuqta Hizi Utapata= 1 + 2 + 1 + 1 + 2 + 3 + 1 + 1 + 1 + 2 + 1=16 na namba hii 16 ni Macro-Chromosomes za Nyoka.

Aya Hii Ina Herufi 24 na namba hii katika Elimu ya Hesabu inajulikana kama Composite Number nayo ni ya 36 katika Mfululizo kuanzia Mwanzo wa namba za Composite. Na kama Tulivyosema namba 36 Ni Chromosomes za Nyoka.

Na kama tulivyosema hapa juu kwamba Namba 26 (Namba Ya Sura) katika Elimu ya Hesabu inajulikana kama Composite Number nayo ni ya 16 katika mfululizo kuanzia mwanzo wa Composite Numbers. Na namba 16 ni Macro-Chromosomes za Nyoka Namba 32 (Namba Ya Aya) katika Elimu ya Hesabu inajulikana kama Composite Number nayo ni ya 20 katika mfululizo kuanzia mwanzo wa Composite Numbers. Na 20 Ni Micro-Chromosomes za Nyoka Jumla ya 16 + 20=36 na kama tulivyosema kwamba 36 ni Jumla ya Chromosomes za Nyoka.

Ndugu Waislamu Aya Hii Peke yake inatosha kuwa ushahidi kwamba Mwenyeezi Mungu ndiye aliyeshusha Kuruani hii naye ndiye aliumba kila kitu. Hapa hakuna Ubishi wala maneno baada ya ufafanuzi wote huu.

HESABU ZA SURA NA AYA PIA ZINATHIBITISHA IDADI YA CHROMOSOMES ZA NYOKA (Muujiza)

1/SURA NAMBA 7 + SURA NAMAB 20 + SURA NAMBA 26=53 Na Namba 53 katika Elimu ya Hesabu ni ya 16 katika Mfululizo ukihesabu kuanzia Mwanzo wa Prime Numbers. 2/AYA NAMBA 107 + AYA NAMBA 20 + AYA NAMBA 32= 159 Na Namba hii ni sawa na (53 X 3).Na Namba 53 katika Elimu ya Hesabu ni ya 16 katika Mfululizo kutoka Mwanzo wa Prime Numbers. 3/Jina La Sura (Tulizozitaja Hapa Juu Zenye Uhusiano na nyoka) الاٴعرَاف lina Herufi 7 + Jina la Sura طٰه lina Herufi 2 + Na Jina La Sura الشُّعَرَاء lina Herufi 7=16 Na kama tulivyoona namba hii 16 inathibitisha idadi ya Macro-Chromosomes za Nyoka.

Ndugu waislamu mnaona ya kushangaza. Kuruani imekusanya Elimu ya Ulimwengu/Malimwengu. Na Elimu yake haina Mpaka wala kiwango, kwa kweli ni Muujiza Mkubwa sana. Na kwa vipi isiwe hivyo kwani Ni maneno yake Mwenyeezi Mungu Aliyeumba kila kitu. Kwani Kuruani hii ni yake na ameipanga vizuri sana bila mfano wowote. Ni Muujiza katika Miujiza mikubwa sana tena sana. Allahu Akbar. Allahu Akbar.

MFANO WA COMPUTER ZA HALI YA JUU HUKO AKHERA

Katika Aya ifuatayo Kuruani inasema kwamba Huko Akhera watu wema wataruzukiwa (Kupewa) tunavyovijua lakini vizuri zaidi kuliko vya duniani. Na Aya Kutoka Katika Sura Ya Al-Mutafifin (hapa chini)zinathibitisha kwamba Huko Akhera pia Kuna hata Mfano wa Computer za hali ya Juu sana ambazo zitatuonyesha Habari ya maisha yetu mazuri na mabaya.

Sura Ya Al-Bakarah Aya Namba 25

وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ أَنَّ لَهُمۡ جَنَّـٰتٍ۬ تَجۡرِى مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَـٰرُ‌ۖ ڪُلَّمَا رُزِقُواْ مِنۡہَا مِن ثَمَرَةٍ۬ رِّزۡقً۬ا‌ۙ قَالُواْ هَـٰذَا ٱلَّذِى رُزِقۡنَا مِن قَبۡلُ‌ۖ وَأُتُواْ بِهِۦ مُتَشَـٰبِهً۬ا‌ۖ وَلَهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٲجٌ۬ مُّطَهَّرَةٌ۬‌ۖ وَهُمۡ فِيهَا خَـٰلِدُونَ (٢٥)

TAFSIRI YA AYA 25.

Na Wabashirie walioamini na kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake; kila mara watakapopewa malunda humo kuwa ni chakula watasema: “Haya ndiyo yale tuliyopewa zamani (ulimwenguni).” Kwani wataletewa (matunda hayo) hali ya kuwa yamefanana (na yale waliyokuwa wakiyajuwa ulimwenguni. Wataletewa kwa sura hiyo; lakini utamu mwingine kabisa): na humo watapata wake waliotakasika (na kila mabaya na machafu);na watakaa milele humo.

SAYANSI YA COMPUTER (COMPUTER SCIENCE)

Na kama tunavyoelewa kwamba Computer za duniani zinatumia Elimu ya DIGITAL katika kurikodi DATA na mawasiliano kwa mfano Maandishi (Text), Picha (Photo), Video (Film) na Vinginevyo. Computer inatumia DIGITS(Zero na Moja) katika mawasiliano na pia katika kuhifadhi (Storage)Maandishi, Video na Mengineyo na Elimu hii inakujulikana kama BINARY SYSTEM. (0 na 1 au Zero na Moja)Ikiwa Computer Inatumia BINARY SYSTEM basi pia uelewe kwamba Binaadamu tunatumia DECIMAL SYSTEM (Namba 1,2,3,4,5,6,7,8,9 etc)katika mawasiliano yetu ya kihesabu za kila siku na pia tunatumia Lugha Mbalimbali kama vile Swahili, English, Arabic, French, Chinese na nyinginezo.

MFANO WA COMPUTER KATIKA KURUANI

Sura Ya Al-Mutafifin Namba 83 Aya Namba 7 Mpaka 9

كَلَّآ إِنَّ كِتَـٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِى سِجِّينٍ۬ (٧) وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا سِجِّينٌ۬ (٨) كِتَـٰبٌ۬ مَّرۡقُومٌ۬ (٩)

TAFSIRI YA AYA

7.Sivyo hivyo (mnavyofanya)! Kwa hakika maandishi (ya amali) za waovu yamo katika Sijjin

8.Na ni jambo gani litakalokujulisha (hata ujue hiyo) sijjin ni kitu gani? ·

9.ni daftari ambalo zinaandikwa humo(ndani yake amali za watu wabayakw njia ya namba).

Sura Ya Al-Mutafifin Namba 83 Aya Namba 18 Mpaka 21

كَلَّآ إِنَّ كِتَـٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِى عِلِّيِّينَ (١٨) وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ مَا عِلِّيُّونَ (١٩) كِتَـٰبٌ۬ مَّرۡقُومٌ۬ (٢٠) يَشۡہَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ (٢١)

TAFSIRI YA AYA

18.Sivyo hivyo (mnavyofanya: Wacheni mabaya!) Hakika Maandishi ya (amali za) watu wema yamo katika (daftari linaloitwa) lliyyin

I9.Na ni jambo gani litakalo kujulisha hata uijue hiyo (Illiyyin) ni kitu gani

20.(Hilo) ni daftari ambalo zinaandikwa humo (amali za watu wazuri kwa njia ya Namba) 

2I.Wanaliona wale waliokaribishwa (na Mwenyezi Mungu).

SHEREHE YA AYA KISAYANSI

Na katika Aya tulizozitaja hapa juu kutoka katika sura ya Al-Mutafifin tunaelezewa Kwamba vitendo vyetu vyote vinarikodiwa katika vitabu viwili. Cha Kwanza kinajulikana kama “SIJIIN” hiki ni kitabu Kilichokusanya vitendo vibaya.Na Kuna Kitabu cha pili ambacho kinajulikana kwa jina “ILIYYIIN” Nacho kinakusanya Vitendo Vizuri.

Katika Aya hizi Mwenyeezi Mungu anatumia ibara كِتَـٰبٌ۬ مَّرۡقُومٌ۬ yaani kitabu kilichandikwa kwa njia ya Namba. Na  Ibara hii inaashiria “Digital Book”. Yaani ni kitabu kilichoandikwa kwa ufundi kama ule tunaotumia wa Computer hapa Duniani lakini wa hali ya juu zaidi. Na kama tulivyosema hapo juu kwamba baadhi ya vituTunavyovijua hapa duniani tutavikuta huko Akhera na kwa hiyo pia hali kadhalika huenda huko kuna Computer za hali ya juu.

Kithibitisho kwamba Ibara كِتَـٰبٌ۬ مَّرۡقُومٌ۬ (Kitabun Markuum)lina maana ya DIGITAL BOOK ni katika Aya namba 20 hapa chini ambayo inasema Watu wema wataona vitendo vyao sio watasoma bali kuona kama vile Film na kithibitisho cha kuona ni neno ” يَشۡہَدُهُ” lenye maana ya “Kuona kwa Macho”  yaani kuona na kufuatilia kama vile tunavyoangalia film katika Cinema au Video ya Film katika Computer  etc.

Ushahidi Mwingine ni kwamba katika Aya zote mbili hapa Juu ibara   وَمَآ أَدۡرَٮٰكَ  ina maana ya “Na ni jambo gani litakalo kujulisha hata uijue”  Ibara hii ina Mara ya Elimu  Mpya ambacho Mtume alikuwa hajui na ni mara ya kwanza kufundishwa. Na kweli Kuruani iliposhuka ilikuwa haina Namba wala harakati (Diactrical Marks) yoyote kama vile Fatha au Kasra au Dhumma au Sukuun. Na Pia Kulikuwa hakuna Namba yoyote yenye kutujuulisha Sura au Aya. Na Ajabu Ni kwamba Elimu ya “COMPUTER SCIENCE” haikuwapo wakati huo kwani hii ni Elimu mpya ya Karne Hii. Katika Misamiati ya Lugha ya Kiarabu. Mwenyeezi Mungu angetumia Neno

وَمَا يُدْرِيكَ    “WA MA YUDRIYKA” kama alivyotumia katika Sura Namba 33 Aya Namba 33 ya Kuruani basi Maana ingebadilika na ingekuwa Elimu hii ilijulikana. (KIMAANA IBARA “WA MA ADRAKA” NI TOFAUTI NA “WA MA YUDRIYKA” YA KWANZA IN MAANA YA MARA YA KWANZA KUTAJWA KWA KITU NA YA PILI INA MAANA YA KUTAJWA MARA YA PILI AU ZAIDI YAANI JAMBO LINALOJULIKANA NA SIYO GENI) Maneno Katika Kuruani yamechaguliwa kiajabu sana na hakuna kosa katika uchaguzi huo. Alitajiwa  kihekima  Elimu hii wakati huo ambao  Computer Science haikujulikana na pia Kuruani haikuwa na namba yeyote kama tulivyosema. namba za Sura na Aya  pamoja na Harakati zote ziliongezwa baadaye yaani baada ya Kufariki Mtume  Viliongezwa ili kuwasaidia Wageni wa lugha ya kiarabu na pia hata walio asili wa lugha hii. Kutajiwa Mtume kwa Ibara “Kitabun Markuum” ni jambo jipya kwani Kuruani ilikuwa haina Namba na ibara hii inasema “Kitabu Kilichotiwa Namba” na neno  YASHHADU  katika Aya hapa Juu linatupa picha kamili yenye kuleta maana ya VIDEO au FILM ya maisha yetu mazuri au mabaya. Tunafahamu Namba na Kitabu ni  “Kitabu cha Namba au DIGITAL BOOK.  na Neno  YASHHADU lenye maana ya KUONA  au WATCH. Maneno haya yanaleta maana ya FILM ya Vitendo Vyetu.

Ni hekima yake Mwenyeezi Mungu anataka iwe Muujiza kwetu baada ya Maendeleo ya Kitaalamu katika wakati huu wa Sayansi na Teknologia. Kulikua hakuna Video wala Film. Hizi ni Elimu za kisasa yaani za hivi karibuni. 

Habari Hii inatisha sana kwani tuelewe kwamba vitendo vyetu vyote vinarikodiwa na tutaviona kama Film. Tutajiona wakati tuliokuwa tunatenda mema na pia kama tulifanya baya lolote lile. Kwa njia hii hatuwezi kukana au kubisha. Ukweli utadhihirika. Yaani katika maisha yetu tunarikodiwa maisha yetu yote. Kwa mfano mwizi atajiona wakati aliokuwa akiiba. Mwongo atajiona wakati alipokuwa akidanganya, Kila kitendo tutakiona. Na Mwema atajionea FILM ya maisha yake mfano  alipokuwa akisaidia Masikini au alipokuwa akifanya Ibada na mengineyo mazuri. Basi Ndugu Waislamu Mwenyeezi Mungu anatuambia katika Aya hizi kwamba Kitabu hiki tutakiona kwa macho na hakusema tutakisoma bali kasema tutakiona kama vile Film. Furaha kubwa kwa aliyetenda mema matupu na aibu kubwa kwa aliyetenda mabaya kwani yote yatatolewa. Siri zetu zote zitafichuliwa na hakuna Siri.

Hadithi Ifuatayo inathibitisha habari hizi za kutangazwa habari zetu mbele ya umma na ni za kutisha, Hadithi hii ilikusanywa na kukubaliwa na Imamu Maarufu Wawili Bukhari na Muslim.

Asili Ya Hadithi Hii ipo katika Volumes za Ṣaḥīḥ al-Bukhārī Na Ṣaḥīḥ Muslim

Daraja Ya Hadith Ni: Muttafaqun Alayhi (Authenticity Wamekubaliana) kufuatana na Al-Bukhari na Muslim

عَنِ ابْنِ عُمَرَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا جَمَعَ اللَّهُ الأَوَّلِينَ وَالآخِرِينَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرْفَعُ لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ فَقِيلَ هَذِهِ غَدْرَةُ فُلاَنِ بْنِ فُلاَنٍ

TAFSIRI YA HADITHI

Ibn Umar aliripoti: Mtume wa Mwenyezi Mungu, amani na baraka ziwe juu yake, alisema, “Wakati Mwenyezi Mungu atakusanya vizazi vya awali na vya mwisho (yaani binaadamu wote) Siku ya Kiyama, itainuliwa bendera kwa kila mtu mwenye hila. Itatangazwa kuwa huu ni uhaini wa mtu huyu.

MUUJIZA WA KIHISTORIA WA NENO عَلَّمۡنَـٰهُ KATIKA KURUANI TUKUFU

Aya za Kuruani zimepangwa Kimiujiza na haiwezekani kupangika bila mpango.

Aya nne hapa chini zinazungumzia kufundishwa kwa manabii wanne. Na Sura hizi zipo katika sehemu mbali mbali za Kuruani. Katika Sura Namba 12,18,21 na 36.

Na neno lililotumiwa katika kila Aya ni  عَلَّمۡنَـٰهُ. yaani “Tulimfundisha” Na ukichunguza Neno hili utakuta limetumika mara nne tu katika kuruani yote. (Mara ya Kwanza limeambatana na Nabii Yusuf, Kisha Musa, Kisha Dauwd na Mwisho Nabii Mohmaed) Muujiza wa kushangaza ni kwamba Neno hili limetumika na kupangika kihistoria kwa ajabu sana.

Mara ya kwanza limetumika katika Sura Namba 12 Aya Namba 68 inayosema kwamba Mwenyeezi Mungu alimfundisha Nabii Yusuf Elimu. Na Ajabu kihistoria neno hili عَلَّمۡنَـٰهُ limetumika na nabii Yusuf aliyewatangulia Nabii Musa, Daud na Mohamed. (Amani Na Sala Za Mola Zimfikie)

Mara ya pili neno عَلَّمۡنَـٰه limetumika katika Sura Namba 18 Aya Namba 65 inayosema kwamba Tulimfundisha Nabii Musa Elimu kutoka kwa aliyepewa Rehema ya Elimu na Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Na Ajabu ni kwamba Nabii Musa amemfuatia Nabii Yussuf. Yaani Baada ya Nabii Yussuf. Na mpangilio wa kisa hiki umekuja katika Sura Namba 12.

Mara ya tatu neno عَلَّمۡنَـٰهُ limetumika katika Sura Namba 21 Aya Namba 80 katika kisa cha Nabii Dauwd Aliyefundishwa namna ya kutengeneza mavazi ya Vita. Na Ajabu Neno hili limetumika mara ya tatu Na nabii wa tatu katika wawili waliotangulia. Yaani wa kwanza Nabii Yusuf, kisha Nabii Musa na huyu wa tatu ni nabii Daud

Mara ya Nne neno عَلَّمۡنَـٰهُ limetumika katika Sura namba 36 Aya namba 69 inayosema kwamba Mtume Mohamad hakufundishwa Mashairi bali Ni Kuruani. Na Kihistoria Mtume Mohamed ni wa Mwisho katika mpangilo wa tarehe za Manabii tuliowataja hapa juu.

Kwa kifupi neno hili عَلَّمۡنَـٰهُ  lenye maana ya “Tulimfundisha” limetajika katika Kuruani mara nne tu. Na limeambatana na Manabii Wanne.

Na ukiangalia Namba za Sura utaona limetumika mara ya kwanza katika Sura namba 12 katika kisa cha Nabii Yussuf , kisha Sura Namba 18 katika kisa cha Nabii Musa, kisha Sura Namba 21 katika kisa cha Nabii Dauwd, na Katika Sura Namba 36 katika Kisa cha Nabii Mohamad. Yaani Neno Limepangika kwa mpango kufuatana na Tarehe za kuja kwa hawa Manabii Wanne.

Kwa Kweli Kuruani ni maneno yake Mwenyeezi Mungu. Angalia Neno hili عَلَّمۡنَـٰهُ ambalo limetajika mara nne katika Sura Mbali Mbali za Kuruani lakini ukichunguza utaona linafuata Historia na siyo hovyo hovyo, bali kwa mpangilio wa kushangaza.

Jambo la kushangaza ni kwamba Kuruani iliposhuka Kulikuwa hakuna namba za Sura wala Aya. Hizi Namba ziliongezwa baadaye yaani ziliongezwa ili kuwarahisishia wasomaji wa Kuruani.

Sasa Miujiza mbalimbali imejitokeza baada tu ya kuzipa Sura na Aya Namba. Muujiza juu ya Muujiza. Visa katika Kuruani vimekariri mara kwa mara kwa hekima kubwa. Visa Vingine vimetajika kwa kifupi katika Baadhi ya Sura na kufafanuliwa tena katika Sura Nyinginezo. ili kuwakumbusha waja wake  tena na tena yaliyopita. Na pia Kuwatia na Kuwazidishia watu Imani.

Katika Kuruani hakuna Kukariri bure bure bali ni “Kukamilishana”. Aya hazikukariri kienyeji bali zimekamilishana kimaana. Yaani hakuna Upuzi au maneno yasiyo mpango. Kila Herufi, Maneno na Aya Zimepangwa na Kuhesabiwa kiajabu sana tena sana.

Je unaona ya kushangaza. Allahu Akbar. Allahu Akbar.

Angalia hapa chini Aya hizi Nne. Kila Aya Imetumia neno عَلَّمۡنَـٰهُ lenye maana ya “Tulimfundisha. Na kila Moja Inahusiana Na Nabii kama tulivyoelezea hapa Juu.

Sura Ya Yussuf Namba 12 Aya Namba 68

وَلَمَّا دَخَلُواْ مِنۡ حَيۡثُ أَمَرَهُمۡ أَبُوهُم مَّا ڪَانَ يُغۡنِى عَنۡهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن شَىۡءٍ إِلَّا حَاجَةً۬ فِى نَفۡسِ يَعۡقُوبَ قَضَٮٰهَا‌ۚ وَإِنَّهُ ۥ لَذُو عِلۡمٍ۬ لِّمَا عَلَّمۡنَـٰهُ وَلَـٰكِنَّ أَڪۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ (٦٨)

68-Na walipoingia jinsi alivyowaamrisha baba yao, haikuwafaa kitu kwa Mwenyezi Mungu, · isipokuwa haja iliyokuwa katika nafsi ya Yaaqubu aliitimiza (Alikuwa akitaka. asadifiane na Yusufu – ndugu yake yule khalisa, peke yao. Wakasadifiana hivyo). Na bila shaka yeye (Yaaqubu) alikuwa mwenye ilimu kwa sababu tulimfundisha, lakini watu wengi hawajui.

Sura Ya Al-Kahf Namba 18 Aya Namba 65

فَوَجَدَا عَبۡدً۬ا مِّنۡ عِبَادِنَآ ءَاتَيۡنَـٰهُ رَحۡمَةً۬ مِّنۡ عِندِنَا وَعَلَّمۡنَـٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلۡمً۬ا (٦٥)

65-Basi wakamkuta mja katika waja wetu (Sisi Mwenyezi Mungu) tuliyempa rehema kutoka kwetu na tuliyemuelimisha ilimu (nyingi) zinazotoka kwetu.

Sura Ya Al-Ambiyaa Namba 21 Aya Namba 80

وَعَلَّمۡنَـٰهُ صَنۡعَةَ لَبُوسٍ۬ لَّڪُمۡ لِتُحۡصِنَكُم مِّنۢ بَأۡسِكُمۡ‌ۖ فَهَلۡ أَنتُمۡ شَـٰكِرُونَ (٨٠)

80-Na tukamfundisha (Daudi) matengenezo ya mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini katika mapigano yenu. Je! Mtakuwa wanaoshukuru?

Sura Ya Yasin Namba 36 Aya Namba 69

وَمَا عَلَّمۡنَـٰهُ ٱلشِّعۡرَ وَمَا يَنۢبَغِى لَهُ ۥۤ‌ۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرٌ۬ وَقُرۡءَانٌ۬ مُّبِينٌ۬ (٦٩)

69-Wala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala haiwi kwake (kuwa mtunga mashairi). Haikuwa. (Qurani) ila ni ukumbusho na kitabu kibainishacho (kila yanayohitajiwa)