UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
1-MAAJABU YA SURA YA AL-KAWTHAR
MAAJABU YA SURA YA AL-KAWTHAR
Chapter (108) sūrat l-kawthar (A River in Paradise)
Sura Ya Alkawthar ni mojawapo ya Sura zilizo fupi kuliko zote katika Kuruni Tukufu. Katika Sura hii fupi kuna Muujiza wa Ajabu kama utakavyoona katika sherehe hapa chini:
Sura Ya Alkawthar
بسم الله الرحمن الرحيم kwa jina la Mwenyeezi Mungu, Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo In the name of Allah , the Entirely Merciful, the Especially Merciful.
1-{ انا اعطينك الكوثر } [الكوثر:]. kwa hakika tumekupa kheri nyingi To thee have We granted the Fount (of Abundance).
———————
2-{ فصل لربك وانحر } [الكوثر. Basi sali kwa ajili ya mola wako na uchinje (kwa ajili ya mola wako.) (Na kila utakalolifanya lifanye kwa ajili ya mola wako siyo mizimu wala mapango wala makaburi) Therefore to thy Lord turn in Prayer and Sacrifice
————————
3-{ ان شانئك هو الابتر } [الكوثر].
Hakika adui yako ndiye atakayekuwa mkiwa. (atakatika na kila kheri) For he who hateth thee, he will be cut off (from Future Hope).
————————————–
Katika Aya hizi 3 tunaona namba 10 inaashiriwa zaidi ya mara moja kwa njia ya ajabu sana!!!
1/Idadi Ya Maneno katika sura hii ni 10
2/Herufi zilizotumika zisizokariri katika Aya ya kwanza ni 10 nazo ni
(ا، ن، ع، ط، ي، ك، ل، و، ث، ر)
( 3) Herufi zilizotumika zisizokariri katika Aya ya pili ni 10 nazo ni
(ف، ص، ل، ر، ب، ك، و، ا، ن، ح)
4/Herufi ya pekee iliyotumika sana zaidi ya herufi zote ni Alif nayo imekariri karika sura hii mara 10 5/Aya zote zimeishia na herufi ya RA nayo ni ya kumi katika mpangilio wa herufi za kiarabu. kama tunavyoona hapa katika table hii.
5/Aya zote zimeishia na herufi ya RA nayo ni ya kumi katika mpangilio wa herufi za kiarabu.
6/Katika Msahafu Sura za kuruani ambazo mwisho wake zinaishia na herufi ya RA na pia ni herufi pekee iliyokariri sana katika maneno yote 10 katika sura hizi ni sura 10 tu zifuatazo:
1. المائدة- قدير
2. الحج- النصير
3. لقمان- خبير
4. الشورى- الأمور
5. القمر- مقتدر
6. الممتحنة- القبور
7. القدر- الفجر
8. العاديات- لخبير
9. العصر- بالصبر
10. الكوثر- الأبتر
7/Tukisoma sura Ya Alkawthar tunaanza na بسم الله الرحمن الرحيم – Bismillahi Arrahmani Arrahiym ambayo pia inatumia herufi 10 tu zisizokariri nazo ni ب، س، م، ا، ل، ه، ر، ح، ن، ي بسم الله الرحمن الرحيم
Na ukihesabu mpangilio wa herufi ya RA katika Aya hii ya Basmala ni ya 10!!
(ب س م ا ل ل ه ا ل ر [10] ح م ن ا ل ر ح ي م):
Na namba 10 ni Muujiza unaoashiria siku ya machinjo ambayo ni tarehe 10 ya mwezi wa Hijja; Katika Sura hii Mwenyeezi Mungu anamuamrisha Mtume aswali na kuchinja. Hii ni Muujiza wa kihesabu ambao unaonyesha kwamba Kuruani Tukufu ni maneno ya Mwenyeezi Mungu na haiwezekani binaadamu kuleta ufundi katika maandishi kama haya. Kwa kweli Mungu yupo na tumwogope sana, habari za kutisha wala sio mzaha.
2-MUUJIZA WA NENO شهرين (Sharayni- Maana yake ni “Miezi Miwili”) KATIKA KURUANI TUKUFU
MUUJIZA WA NENO شهرين (Sharayni- Maana yake ni “Miezi Miwili”) KATIKA KURUANI TUKUFU
Katika kuruani Tukufu Neno شهرين (Shahrayn-Maana Yake Miezi Miwili) limetajwa mara mbili tu katika Aya mbili zifuatazo:
Chapter (4) sūrat l-nisāa (The Women) Ayat Number 92
{ وَ مَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ أَنْ يَقْتُلَ مُؤْمِنًا إِلَّا خَطَأً وَ مَنْ قَتَلَ مُؤْمِنًا خَطَأً فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ وَ دِيَةٌ مُسَلَّمَةٌ إِلَى أَهْلِهِ إِلَّا أَنْ يَصَّدَّقُوا فَإِنْ كَانَ مِنْ قَوْمٍ عَدُوٍّ لَكُمْ وَ هُوَ مُؤْمِنٌ فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ وَ إِنْ كَانَ مِنْ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَ بَيْنَهُمْ مِيثَاقٌ فَدِيَةٌ مُسَلَّمَةٌ إِلَى أَهْلِهِ وَ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مُؤْمِنَةٍ فَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ تَوْبَةً مِنَ اللَّهِ وَ كَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا } [النساء: 92].
ENGLISH TRANSLATION
And never is it for a believer to kill a believer except by mistake. And whoever kills a believer by mistake – then the freeing of a believing slave and a compensation payment presented to the deceased’s family [is required] unless they give [up their right as] charity. But if the deceased was from a people at war with you and he was a believer – then [only] the freeing of a believing slave; and if he was from a people with whom you have a treaty – then a compensation payment presented to his family and the freeing of a believing slave. And whoever does not find [one or cannot afford to buy one] – then [instead], a fast for two months consecutively, [seeking] acceptance of repentance from Allah. And Allah is ever Knowing and Wise.
Chapter (58) sūrat l-mujādilah (She That Disputeth) From Ayat 2-4
{ الَّذِينَ يُظَٰهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَائِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَٰتِهِمْ إِنْ أُمَّهَٰتُهُمْ إِلَّا الَّٰئي وَلَدْنَهُمْ وَ إِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ الْقَوْلِ وَ زُورًا وَ إِنَّ اللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ (2) وَ الَّذِينَ يُظَٰهِرُونَ مِن نِّسَائِهِمْ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُوا فَتَحْرِيرُ رَقَبَةٍ مِّن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا ذَٰلِكُمْ تُوعَظُونَ بِهِ وَ اللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ (3) فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَ رَسُولِهِ وَ تِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ وَ لِلْكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ (4) } [المجادلة: 2 – 4].
ENGLISH TRANSLATION
Those who pronounce dhihar (calling them mothers) among you [to separate] from their wives – they are not [consequently] their mothers. Their mothers are none but those who gave birth to them. And indeed, they are saying an objectionable statement and a falsehood. But indeed, Allah is Pardoning and Forgiving. And those who pronounce thihar from their wives and then [wish to] go back on what they said – then [there must be] the freeing of a slave before they touch one another. That is what you are admonished thereby; and Allah is Acquainted with what you do. And he who does not find [a slave] – then a fast for two months consecutively before they touch one another; and he who is unable – then the feeding of sixty poor persons. That is for you to believe [completely] in Allah and His Messenger; and those are the limits [set by] Allah. And for the disbelievers is a painful punishment.
Jambo lingine la kushangaza ni muujiza wa kihesabu katika Aya hizi mbili. Calendar ya kiislamu inatumia mzunguko wa mwezi katika kuzunguka ardhi na unachukua siku 29.5 ili kukamilisha safari yake kuizunguka dunia na kurudi pale mwanzo ilipoondokea. Kwa hiyo mwezi wa kiislamu una siku 29.5 na siyo siku 30 kama vile Calendar tunayoijua ambayo inaitwa kwa jina Gregorian Calendar nayo inategemea jua kwani siku za mwezi zinatokana na mwezi kuzunguka Jua.
MUUJIZA KATIKA AYA HIZI MBILI
Ukihesabu maneno katika Aya ya kwanza kutoka mwanzo wa Aya mpaka neno شهرين (Shahrayni-Maana yake Miezi Miwili) tunapata idadi ya maneno 59 ambayo ni sawa na (29.5 x2=59). na siku 59 ni jumla ya miezi miwili ya kiislamu. La kushangaza zaidi na pia kithibitisho kwamba jambo hili katika Aya ya mwanzo limekusudiwa tukihesabu maneno kuanzia mwanzo wa aya ya pili mpaka neno شهرين (Shahrayni-Maana yake Miezi Miwili) tunapata maneno 54 na kwa sababu gani 54 na sio 59 ? jawabu ni kwa sababu kafara hapa haikubaliwi ila baada ya kufunga miezi miwili kabla ya kurudiana na mkewe au kwa tafsiri ya kipande hiki saumu iwe kabla ya makutano/muashara na Mkewe (مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا) hili sharti ni lazima ili kafara ikubaliwe, na ajabu kubwa ni kwamba ukihesabu maneno mpaka mwisho wa sharti hili baada tu ya neno Shahrayni unapata maneno 59 ya miezi miwili (29.5 X 2=59). Kwa kifupi huwezi kusimama katika neno shahrayni kwani maana haikutimia na inabidi uongeze ibara hii “ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَاسَّا” Ndugu zangu waislamu Kuruani ina maajabu makubwa. Kila sura, aya, maneno na herufi bali na harakati na namba za sura na aya zote zimehesabiwa na kama mwenyeezi mungu anavyosema amejaalia kila kitu kwa hesabu na sio burebure. Kwa hakika Kuruani ni muujiza mkubwa sana tena sana!!!!!. Tuisome sana ili tupate kubarikiwa.
3-MUUJIZA KATIKA MATUMIZI YA NENO LA R’aad
MUUJIZA KATIKA MATUMIZI YA NENO LA R’aad
Mpangilio wa Herufi, Aya na Sura za kuruani ni muujiza mkubwa ambao upo mbele ya macho yetu. Inashangaza sana tena sana, hebu tuangalie aya mbili zifuatazo:
Neno Raa’d (رعد) limetumika katika kuruani mara mbili tu katika aya mbili zifuatazo:
أَوۡ كَصَيِّبٍ۬ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فِيهِ ظُلُمَـٰتٌ۬ وَرَعۡدٌ۬ وَبَرۡقٌ۬ يَجۡعَلُونَ أَصَـٰبِعَهُمۡ فِىٓ ءَاذَانِہِم مِّنَ ٱلصَّوَٲعِقِ حَذَرَ ٱلۡمَوۡتِۚ وَٱللَّهُ مُحِيطُۢ بِٱلۡكَـٰفِرِينَ[البقرة: 19].
Tafsiri Ya Aya Hii namba 19 Sura ya Albakarah. Au(mfano wao pia) ni kama mvua kubwa itokayo mawinguni; ndani yake mkawa na viza na radi na umeme; wakawa wakitia vidole vyao masikioni mwao kwa ajili ya mingurumo, kwa kuogopa kufa; (na kufanya hivyo hakuwasaidii kitu) Na Mwenyeezi Mungu anawajua vyema hao makafiri.
———————————————–
وَيُسَبِّحُ ٱلرَّعۡدُ بِحَمۡدِهِۦ وَٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةُ مِنۡ خِيفَتِهِۦ وَيُرۡسِلُ ٱلصَّوَٲعِقَ فَيُصِيبُ بِہَا مَن يَشَآءُ وَهُمۡ يُجَـٰدِلُونَ فِى ٱللَّهِ وَهُوَ شَدِيدُ ٱلۡمِحَالِ [الرعد: 13].
Tafsiri Ya Aya Hii namba 13 Sura ya Ara’d Na Radi inamsabihi Mwenyeezi Mungu kwa kumshukuru na (pia) Malaika (husabihi) kwa kumuogopa. Na (Mwenyeezi Mungu) hupeleka mapigo ya radi na kumpiga nayo Amtakaye. Na hao (makafiri) wanabishana juu ya Mwenyeezi Mungu (kuwa yuko kweli au hayuko) na hali (ya kuwa yuko na) Yeye ni mkali wa kuadhibu. —————————————————-
-Ajabu ya kwanza ni Aya zote mbili zina maneno 19
-Ajabu ya pili katika hiyo aya ya kwanza (sura ya Albakarah) pia namba yake ni 19
-Ajabu ya tatu ni Aya ya pili (Sura Ya Ra’d) Aya hii ni ya namba 13, ipo katika Juzuu ya 13 na pia sura hii ya -Ara’d ni ya namba 13
-Ajabu ya nne ni kwamba idadi ya herufi katika aya ya kwanza. (katika sura ya Albakarah) zinafanana na jumla ya idadi ya herufi ya aya ya pili (kutoka sura ya Arrad)
Aya ya kwanza sura ya Bakarah
ر =herufi hii ya Ra imetumika mara 4
ع=herufi hii ya ‘ain imetumika mara 4
د =herufi hii ya Dal imetumika mara 1
jumla ni herufi 4 + 4 + 1=9
Aya ya pili sura ya Ar’ad
ر =herufi hii ya Ra imetumika mara 2
ع=herufi hii ya ‘ain imetumika mara 2
د =herufi hii ya Dal imetumika mara 5
jumla ni herufi 2 + 2 + 5=9
-Ajabu ya sita ni kwamba Katika aya ya kwanza (Sura ya Albakarah) ukitumia herufi za “Alif” na “Lam” katika (Al-RAAD)utapata jumla ya idadi za herufi zilizosawa pia.!!!!
Aya ya kwanza sura ya albakarah:
Alif yaani “ا”=Herufi hii imetumika mara 10
Lam yaani “ل”=Herufi imetumika mara 8
ر =herufi hii ya Ra imetumika mara 4
ع=herufi hii ya ‘ain imetumika mara 4
د =herufi hii ya Dal imetumika mara 1
Jumla 10 + 8 + 4 + 4 + 1=27
Na katika aya ya pili ya sura ta Raad.
Alif yaani “ا”=Herufi hii imetumika mara 8
Lam yaani “ل”=Herufi imetumika mara 10
ر =herufi hii ya Ra imetumika mara 2
ع=herufi hii ya ‘ain imetumika mara 2
د =herufi hii ya Dal imetumika mara 5
Jumla 8 + 10 + 2 + 2 + 5=27
Hizi ni dalili dhahiri kwamba kuruani siyo maneno ya mzaha au yaloyotungwa na binaadamu na wala usisikilize wajinga wasioelewa chochote. Uthibitisho huu upo mbele ya macho yako.Kuruani alishushiwa mtume karne ya saba. Je mtume alikuwa anatumia Computer?? ili imsadie kuandika maajabu kama haya ambayo hayana mwisho!!!. kwa kweli inatisha sana tena sana wala sio uongo.
4-MAAJABU YA NENO نُحَاسٌ۬ “SHABA” AU “NUHAS”
Chapter (55) sūrat l-raḥmān (The Most Gracious) Aya Namba 33-35
katika Aya ya kuruani zifuatazo tunakuta maajabu ya neno نُحَاسٌ۬ yaani Shaba au Copper ukihesabu maneno kuanzia mwanzo wa Aya unkuta neno hili ni namba 29 na namba hii inaashiria atomic number ya Shaba ambayo ni 29 pia!!
Mwenyeezi Mungu antuambia sisi binaadamu na majini wote kwamba hatuwezi kuvuka mpaka wa ulimwengu (universe) kwani huko kuna hatari kubwa kutokana na umbali na pia kuna moto na shaba ambazo haiwezekani kupika huko na pia kupenya ardhi kwani Temperature ni kubwa sana na pia uzito wa hali ya juu isipokuwa kwa matakwa yake.
يَـٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ إِنِ ٱسۡتَطَعۡتُمۡ أَن تَنفُذُواْ مِنۡ أَقۡطَارِ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ فَٱنفُذُواْۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلۡطَـٰنٍ۬ (٣٣) فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (٣٤) يُرۡسَلُ عَلَيۡكُمَا شُوَاظٌ۬ مِّن نَّارٍ۬ وَنُحَاسٌ۬ فَلَا تَنتَصِرَانِ (٣٥)
O company of jinn and mankind, if you are able to pass beyond the regions of the heavens and the earth, then pass. You will not pass except by authority [from Allah].
So which of the favors of your Lord would you deny?
There will be sent upon you a flame of fire and copper, and you will not defend yourselves.
1. يمعشر
2. الجن
3. و
4. الانس
5. ان .
استطعتم 6.
7 ان
8. تنفذوا
9. من
10. اقطار
11. السموت
12. و
13. الارض
14. فانفذوا
15. لا
16. تنفذون
17. الا
18. بسلطن
19. فباي
20. الا
21. ربكما
22. تكذبان
23.يرسل
24. عليكما
25. شواظ
26. من
27. نار
28. و
29. نحاس
30. فلا
31. تنتصران

Picha Ya Chembe Ndogo Ya Shaba (Copper) Kama Unavyoona Hapa Ina Atomic Number 29 na ajabu ni kwamba katika Aya Ya Kuruani hapa juu Neno Shaba Ni La 29!!!
KISA CHA NABII DAUWD NA MAAJABU YA KIHESABU NAMBA 100
SURA YA ASWAD NAMBA 38 AYA NAMBA 21-25
۞ وَهَلۡ أَتَٮٰكَ نَبَؤُاْ ٱلۡخَصۡمِ إِذۡ تَسَوَّرُواْ ٱلۡمِحۡرَابَ (٢١) إِذۡ دَخَلُواْ عَلَىٰ دَاوُ ۥدَ فَفَزِعَ مِنۡہُمۡۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ خَصۡمَانِ بَغَىٰ بَعۡضُنَا عَلَىٰ بَعۡضٍ۬ فَٱحۡكُم بَيۡنَنَا بِٱلۡحَقِّ وَلَا تُشۡطِطۡ وَٱهۡدِنَآ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلصِّرَٲطِ (٢٢) إِنَّ هَـٰذَآ أَخِى لَهُ ۥ تِسۡعٌ۬ وَتِسۡعُونَ نَعۡجَةً۬ وَلِىَ نَعۡجَةٌ۬ وَٲحِدَةٌ۬ فَقَالَ أَكۡفِلۡنِيہَا وَعَزَّنِى فِى ٱلۡخِطَابِ (٢٣) قَالَ لَقَدۡ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعۡجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦۖ وَإِنَّ كَثِيرً۬ا مِّنَ ٱلۡخُلَطَآءِ لَيَبۡغِى بَعۡضُہُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَقَلِيلٌ۬ مَّا هُمۡۗ وَظَنَّ دَاوُ ۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّـٰهُ فَٱسۡتَغۡفَرَ رَبَّهُ ۥ وَخَرَّ رَاكِعً۬ا وَأَنَابَ ۩ (٢٤) فَغَفَرۡنَا لَهُ ۥ ذَٲلِكَۖ وَإِنَّ لَهُ ۥ عِندَنَا لَزُلۡفَىٰ وَحُسۡنَ مَـَٔابٍ۬ (٢٥) .
TAFSIRI YA AYA 21-25
21.Na je imekuwasilia habari ya wagomvi walipopindukia (ukutani kuingia) chumbani (kwake Nabii Daudi)?
22. Walipomuingilia Daudi na akawaogopa. Wakasema: “Usiogope; (sisi ni) wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe; basi tuhukumu, (hukumu baina yetu) kwa haki wala usipendelee, na utuongoe katika njia iliyo sawa.”
23. “Hakika huyu ni ndugu yangu; yeye anaokondoo majike tisiini na tisa, na mimi nina kondoo mmoja tu jike (vile vile) lakini amesema, “Nipe huyu wako nikufugie, (na mimi mwenyewe sitaki), na amenishinda katika maneno.”
24. Akasema: “Kweli amekudhulumu kwa kukuomba kondoo wako kuongeza katika kondoo wake; na bila shaka washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipokuwa wale walioamini na kutenda mema; na hao ni wachache.” Na mara Daudi akaona ya kwamba tumemtia mtihanini (na ameanguka). Akaomba maghufira kwa Mola wake, na akaanguka kunyenyekea na akaelekea (kwa Mola wake).
25. Basi tukamghufuria (tukamsamehe) hayo. Na kwa hakika ana yeye kwetu cheo kikubwa na mahali pazuri (marejeo mazuri) .
MAFUDISHO YA KISA CHA NABII DAWD
Kisa hiki kinatufundisha tusihukumu kwa haraka jambo lolote katika maisha yetu kabla ya kukichunguza. Nabii dauwd latika kisa hiki alifanya kosa na akatoa hukumu ya kumlaumu yule mwenye kondoo 99 kwa kosa la kumdanganya mwenziwe aliyekuwa siyo tajiri na kumchukulia kondoo wake mmoja na akaongeza youle kondoo katika idadi ya 99 na kuwa na 100.
Binaadamu hawatosheki. Na haya tunayaona kila siku katika maisha yetu. Huyu mwenye mali nyingi hatosheki hata mwisho anamnyanganya yule masikini bila kujali wala kumhurumia mwenziwe.
Kisa hiki kina mafundisho makubwa. Hawa wawili waliotajwa hapa walikuwa Malaika katika sura ya kibinaadamu ambao Mwenyeezi Mungu alijaalia waje Kumfanyia Mtihani Nabii Dawuwd. Na mara tu baada ya Nabii Dauwd Kutoa hukumu yake basi walitoweka na Nabii Dawud akatambua kwamba ulikuwa Mtihani na pia Mafundisho. Mara akasujudu Kumuomba Mola amsamehe kwa kutoa Hukumu haraka haraka. Kosa alilofanya lilikuwa kutomsikiliza Yule wa pili. Yaani Hakimu mzuri lazima achunguze pande zote vizuri siyo juju juu. Angewasikiliza wote wawili kisha akapima na kuwajibu.
MUUJIZA WA KIHESABU KATIKA KISA HIKI
Jambo la kushangaza ni kwamba ukihesabu Maneno Ya kisa hiki kuanzia mwanzo wa jkisa hiki (Aya ya 21) mpaka mwisho wa kisa, (Aya namba 25) utapata Maneno 100 tu!!! Je unaona Muujiza Mwingine wa Namba? Kisa kinazungumzia Kondoo 99 na Ukijumlisha yule Kondoo Mmoja unapata Kondoo 100 na ajabu ni kwamba maneno yaliyotumika katika kisa hiki chote ni mia moja tu!! bila ziada wala pungufu. Kwa kweli inashangaza. Aya, Maneno, na Herupi za kuruani zote Zimepangwa kiajabu sana tena sana. Kila mojawapo imehesabiwa na hakuna kosa wala upuuzi. Na ndiyo maana mpaka leo hakuna aliyeweza kuleta mfano wa kuruani kama Mwenyeezi Mungu alivyosema kwamba “laiti sisi Binaadamu na Majini wote tungekusanyika na tuandike mfano wa kuruani basi tusingeweza kabisa” na kwa kweli mpaka leo hatujawahi kuona Aya wala Sura kutoka kwa viumbe Mfano wa Kuruani!!!. Na hii inathibitisha kwamba Kuruani ni maneno yake Mwenyeezi Mungu aliyetukuka.
NENO TALAKA KATIKA KURUANI KUTAJIKA MARA MBILI.
TALAKA MARA MBILI
SURA YA 2 AYA NAMBA 227 MPAKA 230 NA AYA NAMBA 134
وَإِنۡ عَزَمُواْ ٱلطَّلَـٰقَ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ۬ (٢٢٧)
وَٱلۡمُطَلَّقَـٰتُ يَتَرَبَّصۡنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَـٰثَةَ قُرُوٓءٍ۬ۚ وَلَا يَحِلُّ لَهُنَّ أَن يَكۡتُمۡنَ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ فِىٓ أَرۡحَامِهِنَّ إِن كُنَّ يُؤۡمِنَّ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأَخِرِۚ وَبُعُولَتُہُنَّ أَحَقُّ بِرَدِّهِنَّ فِى ذَٲلِكَ إِنۡ أَرَادُوٓاْ إِصۡلَـٰحً۬اۚ وَلَهُنَّ مِثۡلُ ٱلَّذِى عَلَيۡہِنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيۡہِنَّ دَرَجَةٌ۬ۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ (٢٢٨)
ٱلطَّلَـٰقُ مَرَّتَانِۖ فَإِمۡسَاكُۢ بِمَعۡرُوفٍ أَوۡ تَسۡرِيحُۢ بِإِحۡسَـٰنٍ۬ۗ وَلَا يَحِلُّ لَڪُمۡ أَن تَأۡخُذُواْ مِمَّآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ شَيۡـًٔا إِلَّآ أَن يَخَافَآ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِۖ فَإِنۡ خِفۡتُمۡ أَلَّا يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡہِمَا فِيمَا ٱفۡتَدَتۡ بِهِۦۗ تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ فَلَا تَعۡتَدُوهَاۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ (٢٢٩)
فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ ۥ مِنۢ بَعۡدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوۡجًا غَيۡرَهُ ۥۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡہِمَآ أَن يَتَرَاجَعَآ إِن ظَنَّآ أَن يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِۗ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ يُبَيِّنُہَا لِقَوۡمٍ۬ يَعۡلَمُونَ (٢٣٠)
وَٱلَّذِينَ يُتَوَفَّوۡنَ مِنكُمۡ وَيَذَرُونَ أَزۡوَٲجً۬ا يَتَرَبَّصۡنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرۡبَعَةَ أَشۡہُرٍ۬ وَعَشۡرً۬اۖ فَإِذَا بَلَغۡنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا فَعَلۡنَ فِىٓ أَنفُسِهِنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٌ۬ (٢٣٤)
227. Na wakiazimia kuwaacha (basi); Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia (na) Mwenye kujua.
228. Na wanawake walioachwa wangoje (wasiolewe) mpaka tahara tatu zishe. Wala haiwajuzii kuficha (mimba) aliyoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho. Na waume wao Wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya sulhu. Nao (wanawake) wanayo haki kwa Sharia (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hikima.
229. Talaka (unazoweza kumrejea mwanamke) ni (zile zilizotolewa) mara mbili (za kwanza). Kisha ni kumweka kwa wema au kumwacha kwa ihsani. (Wala usiweze kumrejea tena mpaka aolewe na mume mwengine maadam umetimiza mara tatu katika kumwacha ukimrejea). Wala si halali kwenu kuchukua cho chote mlichowapa (wake zenu), isipokuwa (wote wawili) wakiogopa ya kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, hapo itakuwa hapana dhambi kwao (mwanamume wala mwanamke katika) kupokea (au kutoa) ajikomboleacho mwanamke. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiiruke. Na watakaoiruka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhalimu (wa nafsi zao).
230. Na kama amempa talaka (ya tatu) basi (mwanamke huyo) si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine. Na (mwanamume huyo mwengine) akimwacha,basi hapo hapana dhambi kwao (mume yule wa kwanza na mwanamke huyo) kurejeana, wakiona watasimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wajuao (wanaotaka kujua).
234· Na wale wanaofishwa (wanaokufa) miongoni mwenu na kuacha wake; hawa (wake) wangoje (wasiolewe) miezi mine na siku kumi. Na wanapoflkia muda wao (wa kumaliza eda yao hiyo, basi si dhambi juu yenu kwa yale wanayoyafanyia nafsi zao· (hao wanawake) kwa yanayowafiki (kufuata) Sharia. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.
SHEREHE FUPI YA AYA
Tunasoma sheria Kutoka kwa Mwenyeezi Mungu inayohusiana na Talaka kwamba Talaka Inapobidi kufanyika basi inaruhusiwa lakini ina masharti yake lazima kufuatwa. Talaka ya mwanzo na ya pili unaweza kurudiana na mkewe bila tatizo lakini Talaka ya tatu huwezi kumrudia Tena kwa ndoa. Ikiwa ataolewa na kuachika basi utaweza kumwoa mara ya tatu lakini itokee bahati hiyo ambayo siyo rahisi. Yaani kwanza Mwanamke aolewe kisha itokee kuachana ni jambo siyo la kusubiri kwani huenda wasiachane na Mume huyo wa pili lakini ikitokea hivyo itakuwa bahati kubwa kwako wewe mume wa kwanza kumrudia mke huyo. Ukichunguza utaona Sheria hii inazuia Talaka zisifanyike hovyo hovyo na pia kulinda ndoa zisivunjike. Tunafundishwa Muda wa Eda Mke lazima asubiri Kabla Ya Kuolewa Tena (anapofiwa na Mumewe) na Pia Muda Mke Anapoachika lazima asubiri Kabla Ya Ndoa Kufanyika tena.
MUUJIZA WA NAMBA ZA KUSHANGAZA KATIKA AYA HIZI HAPA JUU
Ajabu Ya Kwanza Katika Kuruani nzima neno TALAKA “ٱلطَّلَـٰقَ” limekariri mara mbili tu!!! . Neno hili limetajwa katika Aya Namba 227 na 229 ya Sura Hii Ya Bakara.
Ajabu Ya Pili ni kwamba ukitoa Aya Namba 227 kutoka katika Namba 229 (229-227=2) unapata namba mbili. Kwa hiyo Namba mbili hapa inalingana na Talaka Mbili tu zinazoruhusiwa. Je huoni Muujiza namna Kuruani Ilivyopangika. Maajabu Matupu.
Ajabu Ya Tatu ni Kwamba Aya Hizi Za Talaka Zote zipo katika Sura Ya 2 nayo ni Ya Bakara!!!
Ajabu Ya Nne Ni Kwamba neno طَلَّقَهَا (Akimwacha) Pia limekariri mara mbili tu katika Aya moja ya Namba 230 sura ya Bakarah.
Ajabu Ya Tano Ni Kwamba Maneno Mawili yaliyotumika katika kuelezea Sheria hizi za Talaka Pia Yamekariri mara mbili tu يَتَرَبَّصۡنَ بِأَنفُسِهِنَّ (Wangojee) katika Aya Namba 228 na 234 Ya Sura Ya Bakarah.
Kwa Kweli Kuruani inshangaza. Maajabu Juu Ya Maajabu. Aya Zimefanyiwa hesabu ya hali ya Juu na wala sio kienyeji. Vipimo ambavyo binaadamu vimewapita elimu. Kwa kweli Kuruani Ni Muujiza Mkubwa Tulionao.
MLINGANISHO WA KUSHANGAZA KATIKA SURA YA AL-FATIHA
MLINGANISHO WA KUSHANGAZA KATIKA SURA YA AL-FATIHA
Sura Ya Mwanzo katika Kuruani (Chapter 1) Inajulikana kwa majina mbalimbali.
Al-Fatiha-kwa maana ya Ufunguzi (Kianzio au Dibaji)wenye maana ya kuruani yote.
Umm al-Quran na Umm Al-Kitab- Mama au Kitabu cha kuruani kwani imekusanya kwa ufupi maana ya sura zote za Kuruani.
Sab’ul-Mathani-Aya zenye kukariri katika kila sala
Al-Hamd-Kwa maana ya Kumtukuza Mwenyeezi Mungu.
As-Salah-Sura Inayotumika katika Sala
Ash-Shifa-Aya za Tiba ya maradhi mbalimbali (spiritual remedy)
Al-Asas al-Quran-Msingi wa kuruani na sura hii.
Kwa ufupi sura hii ni msingi wa kuruani nzima.
Na Aya ya mwanzo ambayo ni Basmallah = بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (١) ni msingi wa sura hii ya Alfatiha.
Sura hii ina miujiza mbalimbali ambayo katika maandishi haya ya website (tovuti) hii tutagusia tonye tu katika bahari ya Elimu ya Kuruani Tukufu na haya ni machache tu katika yaliyofanyiwa utafiti na mengine mengi bado hayajafanyiwa utafiti.
MUUJIZA WA KUSHANGAZA KATIKA SURA YA AL-FATIHA.
(1)Neno Kuruani Na Jila La Mtume “Mohamed” Tukichunguza idadi za herufi za Jina lake Mtume Mohamed katika Sura hii tutakuta idadi yake ni 39 Na Ukitafuta Idadi za herufi ya Neno “Kuruani” katika Sura hii tutakuta 39 pia. Idadi ya Herufi zinafanana. Na Ukichunguza katika kuruani utapata Aya inayosema Mtume ni Nuru na nyingine inasema Kuruani ni Nuru. Hizi Aya mbili zimewakilishwa na kufanana kwa idadi kama tulivyoona hapa juu.
Hebu tuchunguze Aya hizi mbili.
Aya Namba 8 Sur namba 64
فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلنُّورِ ٱلَّذِىٓ أَنزَلۡنَاۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٌ۬ (٨)
Tafsiri Ya Aya
Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nuru tuliyoiteremsha, (Qurani). Na Mwenyczi Mungu anazo babari za mnayoyatenda yote.
Aya Namba 15 Sura Namba 5
يَـٰٓأَهۡلَ ٱلۡڪِتَـٰبِ قَدۡ جَآءَڪُمۡ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمۡ ڪَثِيرً۬ا مِّمَّا ڪُنتُمۡ تُخۡفُونَ مِنَ ٱلۡڪِتَـٰبِ وَيَعۡفُواْ عَن ڪَثِيرٍ۬ۚ قَدۡ جَآءَڪُم مِّنَ ٱللَّهِ نُورٌ۬ وَڪِتَـٰبٌ۬ مُّبِينٌ۬ (١٥)
Tafsiri Ya Aya
Enyi watu wa Kitabu! Amekwisha kuflkieni Mtume wetu, anayekudhihirishieni mengi mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu, na husamehe mengi. Bila shaka imekwisha kukufikieni nuru kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Kitabu kinachobainisha· (kila jambo)
Na Tukichunguza idadi ya herufi za Neno “Quran au Kuruani” قرآن na Jina Mohamed “ محمد” katika Sura Ya Alfatiha tutapata yafuatayo:
Qaf mara 1 + Raa mara 8 + + Alif (Na Hamzah) mara 19 + Nun mara 11 = Jumla Herufi 39.
Sasa Tuchunguze idadi ya Herufi za Jina “Mohamed” محمد katika Sura Ya Alfatiha. Herufi za Jina Mohamed zimekariri kama ifuatavyo:
Mim mara 15 + Haa mara 5 + Mim mara 15 Dal mara 4 Jumla Herufi 39
Tumeona kwamba Herufi za Jina la Mtume na Herufi za Jina Kuruani zimetumika na kukariri mara 39 sawasawa na kithibitisho katika Aya mbili hapa juu ambazo pia zote zinasema Mtume ni Nuru na Kuruani ni Nuru pia. Hapa Inatuthibitishia ukweli kwamba jina la Sura Ya Alfatiha kwamba ni “Mama Ya kuruani au Msingi wa Kuruani”. Je huoni Aya za kuruani zinavyoonekana katika sura ya Alfatiha? kukariri katika Kuruani (Mtume ni Nuru na Kuruani pia ni nuru) pia inakariri matumizi ya herufi katika Sura ya Alfatiha Je unaona Muujiza huu ambao siyo mdogo. Mtume hakujua haya kwani Muujika kama huu umewekewa watu kama sisi leo hii katika kipindi cha sayansi na elimu mbalimbali za hesabu. Kama tulivyoona Maneno haya mawili katika sura za kuruani yamewakilishwa na sura ya Alfatiha.Na hii inkubaliana na Majina Ya Sura Hii kama vile “Mama wa kuruani” au “Kitabu” na “Msingi wa kuruani”,
(2)Neno “Wahy”وحي lina herufi 3 nazo zimekariri katika sur ya Alfatiha kama ifuatavyo:
Waw=4 + Haa=5 Ya=14 = 23
na hii namba inatupa Miaka ya Kushuka kwa Kuruani kwa Mtume Mohamed (Revelation Period) Na hii ni maajabu mengineyo katika kuruani kwani Namba zinabeba message nyinginezo kimaajabu sana.
(3)Neno “Insan” انسان Lina herufi 5 nazo zimekariri mara 46 katika sura ya Alfatiha
Alif=2 + Nun=11 + Sin=3 + Alif=19 + Nun=11=46
Na hii namba inalingana na Idadi za Chromosmes za binaadamu (Mama ana Chromosomes 23 na Baba ana Chromosomes 23 Jumla ni 46) Kila binaadamu ana Chromosomes 46 katika Nucleus ya Cell (Kiinitete) . (Kila kiumbe cha Mwenyeezi Mungu kina idadi ya Chromosomes tofauti. Miti, Wanyama, na Kila kiumbe kina Chromosomes zake)
(4)Neno “Dhakar”(Kiume) الذكر na “Untha” (Kike) أنثى kila moja herufi zake zimekariri mara 12 Hapa tunapata Message ya Usawa baina Ya Mume Na Mke katika hali zao. Kila mmoja ana haki kutoka kwa mwingine na wote wawili ni Binaadamu.
Dhal=1 + Kaf=3 + Raa=8 Total 12
Alif=1 + Nun=11 + Thaa=0 + Yaa=0= Total 12
(5)Neno Alhaq na Albatil kila moja lina herufi zenye kukariri katika Alfatiha mara 47
Alhaq= Alif=19 + Lam=22 +Haa=5 + Qaf=1 Total 47 Albatil=Alif=19 + Lam=22 + Ba=3 + Twa=2 + Lam=2 Total 47 Na Hizi zipo katika sura namba 47 Aya Namba 3 na inazungumzia Haki Na Batili (Ajabu Kubwa namba za herufi zinaashiria Namba Ya Sura ambayo ni ya 47 Aya Namba 3)
ذَٲلِكَ بِأَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡبَـٰطِلَ وَأَنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّبَعُواْ ٱلۡحَقَّ مِن رَّبِّہِمۡۚ كَذَٲلِكَ يَضۡرِبُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ أَمۡثَـٰلَهُمۡ (٣)
Tafsiri Ya Aya
Hayo ni kwa sababu wale waliokufuru walifuata upotofu (upotevu), na wale walioamini wamefuata haki iliyotoka kwa Mola wao. Namna hivi Mwenyezi Mungu anavyowapigia, (anavyowaeleza) watu mifano yao.
(6)Kuruani Imeshuka kwa muda wa miaka 23. Hebu tutumie namba hii katika utafiti wetu. Tuchukue maneno ya mwanzo wa Sura Ya Alfatiha ambayo ni 23 na kisha tutafute idadi ya herufi za Neno “Kuruani” قرآن Na Jina “Mohamed” محمد tutapata kama ifuatavyo: Yaani namba zenye mlingano wa kiajabu
Kuruani= Qaf=1 + Raa=7 + Hamzah=0 + Alif=15 + Nun=10 Total 33
Mohamed= Mim=12 + Haa=5 + Mim=12 + Dal=12 Total 33
(7)Namba 19 ni namba ya kimiujiza katika kuruani tukufu na pia ni idadi ya herufi ya Aya ya Kwanza, “Basmala” بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ (١)
Na kwa hiyo tukitumia namba hii ya 19 katika kuhesabu Maneno 19 ya Mwanzo wa Sura Ya Al-fatiha. Yaani tutafute idadi ya herufi za Neno “Kuruani” قرآن Na Jina “Mohamed” محمد tutapata kama ifuatavyo: Yaani namba zenye mlingano wa kiajabu kama tulivyoona katika maneno 23 ya mwanzo wa sura hii. Mlingano mwingine wa kiajabu.
Kuruani= Qaf=0 + Raa=6 + Hamzah=0 + Alif=13 + Nun=8 Total 27
Mohamed=Mim=9 + Haa=5 + Mim=9 + Dal=4= 27
(8)Neno “Nabiy” نبي katika maneno 29 kuanzia Mwanzo wa Sura Ya Alfatiha zimetumika Herufi 29
Nun=11 + Baa=4 + Yaa=14 Total 29
na katika maneno 23 kuanzia mwanzo wa Alfatiha Nun=10 + Baa=3 + Yaa=10 Total 23
na katika maneno 19 kuanzia mwanzo wa Alfatiha
Nabiy = Nun=8 + Baa=3 + Yaa=8 Total 19
(9)Jina Allah الله (Kukariri kwa herufi zake katika Sura Ya Alfatiha)
Alif=19 + Lam=22 + Lam=22 Ha=5 Total 68
(10)Jina Alfatiha الفاتحة (Kukariri kwa herufi zake katika Sura Ya Alfatiha)
Alif=19 +Lam=22 + Fa=0 + Alif=19 + Taa=3 +Haa=5 + TaaMarbutta=0 Total 68
(11) Jina Al-Awal الأوَّلُ (Kukariri kwa herufi zake katika Sura Ya Alfatiha)
Alif=19 + Lam=22 + Alif=1 + Waw=4 + Lam=22 Total 68
(12)Al-Akhir الآخِرُ (Kukariri kwa herufi zake katika Sura Ya Alfatiha)
Alif=19 + Lam=22 + Alif=19 + Kha=0 + Raa=8 Total 68
(13)Neno Ikhlas الإخلاص (Kukariri kwa herufi zake katika Sura Ya Alfatiha) pia linaashiria Namba Ya Sura (Al-Ikhlas) ambayo ni ya 112.
Alif=22 + Lamu=22 + Alif=22 + Khaa=0 + Lamu=22 + Alif=22 + Swad=2 na Total ni 112
Sura namba 6 Aya namba 38 inathibitisha kwamba ulimwengu wote upo katika kuruani. Mwenyeezi Mungu anasema:
وَمَا مِن دَآبَّةٍ۬ فِى ٱلۡأَرۡضِ وَلَا طَـٰٓٮِٕرٍ۬ يَطِيرُ بِجَنَاحَيۡهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمۡثَالُكُمۚ مَّا فَرَّطۡنَا فِى ٱلۡكِتَـٰبِ مِن شَىۡءٍ۬ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّہِمۡ يُحۡشَرُونَ (٣٨)
Tafsiri Ya Aya
Na hakuna mnyama katika ardhi wala ndege arukaye kwa mbawa zake mbili. ila ni umati kama nyinyi (tunadhibiti kila walifanyalo). Hatukupuza Kitabuni (mwetu) kitu cho chote. Kisha watakusanywa kwa Mola wao (awalipe).
Je mnaona mpangilo wa kimiujiza katika kuruani tukufu? Kila Aya, Maneno na Herufi zimepangwa kwa makusudio maalum na wala sio bure bure kienyeji. Kuna sababu nyinginezo hakuna ajuaye isipokuwa yeye mwenyeezi Mungu peke yake. Kwa kweli hii inatosha tupate nasiha kwamba ulimwengu haukuumbwa bure bila sababu. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Ndugu binaadamu wenzangu baada ya yote tuliyoyasoma hapa je haitoshi kutuogopesha?
MIUJIZA KATIKA SURA YA MOHAMED
MIUJIZA KATIKA SURA YA MOHAMED
Utafiti katika Aya namba 1 na 2 Ya sura ya Mohamed unatushangaza sana.
Elimu ya Hesabu za juu zimetumika katika Aya hizi mbili.
ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ أَضَلَّ أَعۡمَـٰلَهُمۡ (١)
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَءَامَنُواْ بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ۬ وَهُوَ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّہِمۡۙ كَفَّرَ عَنۡہُمۡ سَيِّـَٔاتِہِمۡ وَأَصۡلَحَ بَالَهُمۡ (٢)
Tafsiri Za Aya
1. Wale waliokufuru na wakajizuilia (na wakazuilia watu) njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavithubutishia uovu vitendo vyao.
2.Na wale walioamini na wakatenda mema na wakaamini yaliyoteremshwa juu ya Muhammad – nayo ni haki iliyotoka kwa Mola wao – hawa atawafutia makosa yao na atastawisha hali yao.
Jina Mohamed limetajika mara moja tu katika sura hii. Katika Aya Namba 2 nayo Ina maneno 9 na Herufi 44.
Ukienda katika Mraba (Table) wa “Prime Numbers” kama katika picha ya Prime Numbers hapa pembeni. (Namba hizi hazigawanyiki isipokuwa kwa namba 1 au kwa namba yenyewe. -Prime Numbers is a number that is divisible only by itself and 1 e.g. 2, 3, 5, 7, 11 etc. Prime numbers are very useful in cryptography and are fundamental to the most common type of encryption used today: the RSA algorithm). Na Ukihesabu Prime Numbers za mwanzo 9 yaani kuanzia namba 2 namba ya mwisho ni 23 ( 2,3,5,7,11,13,17,19,23) na la kushangaza ni namba ya mwisho ambayo ni 23 ni Namba inayoashiria muda wa Wahyi (Revelation) wa Kuruani kushuka Kwa Mtume.
Na herufi 44 Za Aya Namba 2 Ukitafiti katika Mraba au Table ya Prime Numbers kwa kuzihesabu zile namba zisizokuwa Prime Numbers yaani kuanzia namba 4,6,8,9.10.12,14,15,16,18,20,21,22,24,25,26,27,28, Endelea kuhesabu namba 44 na utafikia namba ya Mwisho ni 63 na hii miaka ya umri aliyoishi mtume mohamed. La kushangaza ni kwamba tupo katika Sura Ya Mohamed (Mtume) “Sala na Amani zake Mola zimfikie”. Na hapa tunaona Muda wa Kushuka Kuruani kwa Mtume na pia Umri wake miaka 63. Je unaona muujiza ka Kihesabu? Muujiza Katika Aya Namba Mbili ni idadi ya maneno na idadi ya herufi.
Na kuanzia mwanzo wa sura ya Mohamed mpaka neno Mohamed utakuta herufi zilizotumika ni 23(zilizokariri na zisizokariri) katika herufi za Alphabet za kiarabu ambazo ni 28 na hii inathibitisha muda wa kushuka kuruani Tukufu.
Na pia Aya Namba 2 imetumia herufi 23 (zisizokariri) kutoka katika herufi 28 za Alphabet ya kiarabu.(inaashiria muda wa kushuka kuruani)
Neno “Wahy” الوحي ukihesabu herufi zake katika Aya namba 2 utapata mshangao mwingine nao ni jumla ya herufi kama ifuatavyo:
Alif=8 + Lam=6 + Waw=6 + Haa=2 + Yaa=1=23
Inaashiria muda wa kushuka kuruani
katika Aya Namba 2 Herufi Ya Haa ambayo pia imetumiwa na maneno mawili (Mohamed na Wahyi) ukihesabu matumizi yake kuanzia mwanzo wa Aya namba mbili utashangaa kuona kwamba herufi ya 23 ni ya Haa.
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ
(Namba 23 hapa inaashiria Muda wa kushuka Kuruani Tukufu)
Sura Ya Mohamed yote imetumia herufi 23 za Haa (Namba 23 hapa inaashiria Muda wa kushuka Kuruani Tukufu)
Sura Ya Mohamed ni Sura namba 47 Ina Herufi 2389 na Aya 38
Ukipanga 3847 (Namba Ya Sura 47 kisha Namba Za Aya 38 za sura ya Mohamed-hesabu Kushoto kuenda kulia kufuatana na lugha ya kiarabu)
Ukujumlisha Namba hii 3847 na 2389 Idadi Ya Herufi Ya Sura Ya Mohamed Utapata
3847 + 2389= 6236 ambazo ni idadi za Aya Za Kuruani.

Muujiza Wa Sura Ya Nabii Nuhu na Pia Umri aliyoishi na Jina Lake
Muujiza Wa Miaka Aliyoishi Nabii Nuhu
Nabii Nuhu aliishi na Watu wake katika hali ngumu kwani walikuwa makafiri waliofanya ukaidi kwa muda wa miaka 950
Sura Namba 29 Aya Namba 14
وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَلَبِثَ فِيهِمۡ أَلۡفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمۡسِينَ عَامً۬ا فَأَخَذَهُمُ ٱلطُّوفَانُ وَهُمۡ ظَـٰلِمُونَ (١٤)
Tafsiri Ya Aya
Na bila shaka tulimtuma Nuhu kwa watu wake na akakaa nao myaka elfu kasoro myaka hamsini; (wasikubali kufuata), basi tufani iliwaflka(wakaghariki),na bali walikuwa madhalimu.
Neno سَنَة lina maana ya miaka ya shida na mahangaiko na neno عَامً۬ا lina maana ya miaka ya raha na neema. Kwa hiyo katika Aya hii nabii Nuhu aliishi miaka elfu moja. Miaka 950 ilikuwa kabla ya Mafuriko yaliyokuja kuangamiza watu hao wakaidi na baada ya hapo aliishi miaka 50 ya Neema na Raha yaani baada ya Mafuriko kuisha. Jambo La Kushangaza na Muujiza mwingine ni kwamba idadi ya Herufi katika Sura Ya Nuhu ni 950. (Ukihesabu Alif Na Hamzah kama herufi au fonts moja inayojulikana katika elimu ya lugha au Linguistics kama Diagraph na pia unaweza kuhesabu kama herufi mbili. Utafiti huu umechukua herufi Alif na Hamzah kama ni herufi Moja yaani A (Idadi ya Herufi 950 katika Sura Ya Nabii Nuhu inathibitisha miaka 950 aliyokuwa akilingania nabii Nuhu)
Na Ajabu nyingineyo ni kwamba Aya Hii ambayo ipo katika Sura Ya Ankaboot Sura Namba 29 Aya Namba 14. Ukifanya hesabu ya Multiplication (Namba Ya Sura 29 x Aya Namba 14=406) na namba hii 406 inalingana na Jumla ya Idadi za Namba za Aya zote katika sura Ya Nabii Nuhu
(1+2+3+4+5+6+7+8+9+10+11+12+13+14+15+16+17+18+19+20+21+22+23+24+25+26+27+28=406)
Huu mlinganisho unanyesha kwamba kuruani ni yake Mwenyeezi Mungu kwani kila Herufi na Aya Zimepimwa na Siyo Kienyeji bure bure.
Muujiza Wa Ajabu Sana-Idadi Ya Kutajika Kwa Nabii Nuhu Katika Kuruani Tukufu
Kwanza Nabii Nuhu ametajika katika Kuruani mara 43 kuanzia Mwanzo wa kuruani mpaka Sura Namba 71. (Yaani katika Sura 28 baina ya Sura Ya Al-Imran Na Sura Ya Nuhu).
—————————-
Pili Nabii Nuhu Hakutajika katika Kuruani mara 43 kuanzia Mwanzo wa kuruani mpaka Sura Namba 71. (Yaani baadhi zinazobakia kutoka katika zile zilizomtaja baina ya Sura Ya Al-Imran Na Sura Ya Nuhu).
————-
Tatu Sura za kuruani zinazobaki kutoka katika idadi 114 ya sura za kuruani zote ni 43 (71-114=43) Na hizi Pia hakutajika Nabii Nuhu.(Yaani baada ya Sura Ya Nuhu ambayo ni ya 71 Mpaka Sura Ya Mwisho namba 114 ya Al-Nnas)
—————————–
Nne Katika Mara 43 ya kukariri kwa Jina la Nabii Nuhu.Jina la Nabii Nuhu Limetumika katika Ibara zifuatazo: Mara 14 kama “Watu wa Nabii Nuhu” au Kawmu Nuhu. Mara Moja kama “Mke wa Nabii Nuhu” Mara 28 kama “Nabii Nuhu” (Na namba hii inalingana na Idadi Ya Aya za Sura Hii Ya Nuhu)
——————-
Na la kushangaza ni kwamba Namba ya Sura ni 71 na ukitoa idadi za Aya za Sura hii ambazo ni 28 unapata 43 (71-28=43) Na Nabii Nuhu kabla Sura Ya Nuhu hakutajika katika sura 43 na baada ya Sura Ya Nuhu pia hakutajika katika sura 43. Katika Kuruani nzima Nabii Nuhu ametajika katika Sura 28 Jina lake limeripiti mara 43. Na namba 28 Inalingana na Idadi za Aya za Sura Ya Nuhu ambazo pia ni 28 na namba 43 Inalingana na Namba ya Sura 71 kutoa idadi za Aya (71-28=43)
Huu Mpangilio wa Kuruani wa kiajabu unashangaza na unaonyesha dalili kwamba Kuruani Imepangwa kwa hekima kubwa sana tena sana.Binaadamu yeyote hawezi kupanga hivyo na Kuruani haina mfano wa kitabu chochote ulimwenguni.
SURA TATU AMBAZO NAMBA ZAKE ZINAASHIRIA SURA YA Al-Nisaa Kiajabu.
DONDOO ZA SURA NNE
-Katika Sura ya Al-Abasa Mwenyeezi Mungu anamfundisha na kumkosoa Mtume kosa lake na anafundishwa asitenganishe masikini na matajiri katika mwito wa dini bali wote walinganiwe dini na kufundishwa. (sura ilishuka Mecca)
-Sura Ya Al-Ibrahim inahusiana pia na Kulingania dini na Hekima kubwa aliyotumia Nabii Ibrahim katika Kulingania dini ya Mwenyezi Mungu na kupiga Vita Masanamu.(Ilishuka Mecca)
-Sura Ya Al-Nabaa Mwanzoni wa Kulingania Dini na Makafiri wa Mecca.(Ilishuka Mecca)
-Sura ya Al-Nisaa inahusiana na mafundisho mbalimbali aliyopewa Mtume katika kumsaidia kujenga Taifa la kiislamu huko Madinna Ni kama kwamba Taifa hilo ni Matunda ya kulingania Dini baada ya Juhudi kubwa huko Mecca.(Ilishuka Madina)
HESABU ZA KUSHANGAZA
Ukipanga Namba za sura Tatu (Abasa, Ibrahim, Na Al-Nabaa) katika msahafu na Idadi ya Aya zake kisha ukizipinduza (reverse) na kutoa utapata namba 3762 na pia namba 176 ambazo ni namba za kushangaza kwani 3762 ni Jumla ya idadi ya maneno ya Sura Ya Al-Nisaa na 176 Ni Idadi ya Aya Ya Sura Ya Al-Nisaa.
-Sura ya 24 kushuka ni Abasa(Sura katika Msahafu namba 80 na Aya zake ni 42) 8042 – 4280 =3762
-Sura Ya 72 Kushuka ni Ya Ibrahim (sura katika msahafu namba 14 na Aya zake ni 52) 5214-1452=3762
-Sura Ya 80 Kushuka Ni ya Al-Nabaa(Sura katika msahafu namba 78 na Aya zake ni 40) 7840-4078=3762
-Sura Ya 92 Kushuka Ni ya Al-Nisaa (Sura Katika Msahadu namba 4) Sura Hii Ina Maneno 3762 na Aya 176
Sura zote tatu (Abasa,Ibrahim, na Alnabaa) zinashangaza kwani idadi ya aya na namba za sura zake zikijuumlishwa kisha kutoa namba hiyo inapogeuzwa (Reverse)unapata idadi ya namba inayoashiria jumla ya maneno ya sura ya Anisaa nayo ni 3762.
Na Ukihesabu Jumla ya namba kufuatana na kushuka sura hizi tatu (24 + 72 + 80=176) basi utapata idadi ya Aya za sura ya Anisaa nayo ni 176
Na mwisho ikijumlisha Namba za Sura Hizi Nne (Kufuatana na Msahafu) 80 + 14 + 78 + 4=176
MUASHIRIO UNA SABABU SIO BURE BURE
Ikiwa sura zote tatu zinaashiria kushuka kwa sura ya Al-Nisaa kwa kutaja idadi ya Maneno Ya sura hiyo na Aya zake basi siyo bure bure. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi kama kuna mengineyo lakini ni Muujiza kwani hizi sura tatu zilishuka hapo mwanzoni (huko Mecca) mwa Kulingania dini na huenda zinaashiria kimuujiza Taifa Jipya litakalojengwa huko Madina ambalo ni Taifa la Kiislamu.
Na Kama tunavyoelewa Kwamba Mtume Mohamed (Amani na Sala zimfikie) alipohama Madina alijenga Taifa La Kiislamu na mafundisho ya Sura ya Al-Nisaa yanahusika katika kujenga Taifa hilo.
Sura hii ya Al-Nisaa ilihusika na Nyanja mbalimbali za kujenga taifa jipya la kiislamu huko Madina. (Sura ya Al-nisaa ilihusika na pia maisha yote siku zijazo katika kuimarisha Umma wa Kiislamu katika nyanja mbalimbali kama vile Urithi, Mayatima, Ndoa, tabia, kulingania dini, kuimarisha familia ambayo ndiyo msingi wa Jamii,Maadili Mema. Kufundisha mwelekeo na msimamo sahihi wa kutii Kuruani. Waislamu wamefundishwa wawe wema na kujiepusha na uchoyo, kutunza kwa amana za watu,Subira na Mafundisho ya Sala pia yamefundishwa, Kwa kifupi mengi mengineyo yamefundishwa katika sura hii. Na haikuwa bure kwa sura Tatu (Abasa, Ibrahim na Al-Nabaa kuashiria Sura Hii. Ni Muujiza Sura Tatu Kuashiria Sura itakayoshushwa baadaye na Taifa Jipya La Madina.
CHROMOSOMES ZA NYUKI, FARASI, NYUMBU NA PUNDA KATIKA KURUANI TUKUFU
Katika Sura Namba 16, Al-Nahl Kuna Miujiza Mbalimbali na Leo tutazungumzia Muujiza Mkubwa Wa Chromosomes.
Kila kiumbe kina Chembe zenye Habari ya Maumbile. Na Chembe hizi zinajulikana kama Chromosomes.
(Chromosomes is a structure found inside the nucleus of a cell. A chromosome is made up of proteins and DNA organized into genes)
Majabu ni kwamba Sura Ya Al-nnahl Namba 16 imeashiria Chromosomes za Nyuki, Farasi, Punda na Mbunyu (Mtoto wa Farasi na Punda).
NYUKI
Muujiza ni kwamba Wanasayansi wanasema kwamba Nyuki wana Chromosomes 16 na Katika Kuruani tunakuta muashirio wa Namba hii kiajabu sana.
Kwanza, Sura Inayojulikana kama “Al-Nahl” yaani “Nyuki” ni Sura Namba 16 na Namba hii inaashiria Chromosomes za Nyuki.
Pili, Katika Sura Hii Aya Namba 68 na 69 pia kuna Muujiza wa kushangaza kwani Katika kipande cha Aya Namba 68 kinachosema
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ
Jumla ya herufi ya kipande hiki peke yake chenye kusema “Na Mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba” ni 16 (Namba Hii ni Jumla ya Herufi za Kuruani na Siyo ya Tafsiri)na Jumla ya Herufi zilizotumika za Arabic Alphabets katika Aya yote Namba 68 hapa chini pia ni 16 (Namba Ya Herufi Za Kuruani na Siyo Tafsiri)
وَأَوۡحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحۡلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتً۬ا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعۡرِشُونَ (٦٨) ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٲتِ فَٱسۡلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلاً۬ۚ يَخۡرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌ۬ مُّخۡتَلِفٌ أَلۡوَٲنُهُ ۥ فِيهِ شِفَآءٌ۬ لِّلنَّاسِۗ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَةً۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ (٦٩)
TAFSIRI
68-Na Mola wako akamfahamisha nyuki ya kwamba “jitengenezee majumba (yako) katika milima na katika miti na katika yale (majumba) wanayojenga ( watu).”
69-Kisha ”Kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mota wako zilizofanywa nyepesi (kuzipita).” Kinatoka katika mat umbo yao kinywaji (asali) chenye rangi mbali mbali; ndani yake kina poza kwa wanaadamu. Hakika katika hayo muna mazingatio kwa watu wenye fikra.
FARASI , MBUNYU NA PUNDA
Sasa tuendelee kuchambua Miujiza Mingine yenye kushangaza sana.
Sura hii ina Aya 128 na ukigawa na Namba ya Sura 16 (128 kugawa kwa 16) utapata namba 8,
Na Namba 8 hapa inaashiria kiajabu sana Aya Nyingine katika Sura hii Ya Al-Nahl ambayo inatupa Miujiza Mingine ya Ajabu yenye uhusiano na Chromosmes. Aya Hii namba 8 inazungumzia Farasi, Mbunyu na Punda
Hebu tuichunguze Aya Hii.
وَٱلۡخَيۡلَ وَٱلۡبِغَالَ وَٱلۡحَمِيرَ لِتَرۡڪَبُوهَا وَزِينَةً۬ۚ وَيَخۡلُقُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ (٨)
TAFSIRI
8-Na (amewaumba) farasi na nyumbu na punda ili muwapande na (wawe) mapambo. Na ataumba (vipando vingine) msivyovijua. (Nayo ndio haya mamotokari, meli,Ndege na Mengineyo tusiyoyajua)
Aya Hi ni Namba 8 na katika Aya Hii kuna Muashirio wa Chromosomes kiajabu sana tena sana Allahu Akbar.
سُوۡرَةُ النّحل بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ أَتَىٰٓ أَمۡرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسۡتَعۡجِلُوهُۚ سُبۡحَـٰنَهُ ۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ (١) يُنَزِّلُ ٱلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنۡ أَمۡرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۤ أَنۡ أَنذِرُوٓاْ أَنَّهُ ۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنَا۟ فَٱتَّقُونِ (٢) خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۚ تَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشۡرِكُونَ (٣) خَلَقَ ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ۬ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ۬ مُّبِينٌ۬ (٤) وَٱلۡأَنۡعَـٰمَ خَلَقَهَاۗ لَڪُمۡ فِيهَا دِفۡءٌ۬ وَمَنَـٰفِعُ وَمِنۡهَا تَأۡڪُلُونَ (٥) وَلَكُمۡ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسۡرَحُونَ (٦) وَتَحۡمِلُ أَثۡقَالَڪُمۡ إِلَىٰ بَلَدٍ۬ لَّمۡ تَكُونُواْ بَـٰلِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ ٱلۡأَنفُسِۚ إِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٌ۬ رَّحِيمٌ۬ (٧) وَٱلۡخَيۡلَ وَٱلۡبِغَالَ وَٱلۡحَمِيرَ لِتَرۡڪَبُوهَا وَزِينَةً۬ۚ وَيَخۡلُقُ مَا لَا تَعۡلَمُونَ (٨)
TAFSIRI
1-Amri ya Mwenyezi Mungu itafika (tu); basi msiihimize; (Muitakidi kuwa) Yeye (Mwenyezi Mungu) katakasika na kila mapungufu na Katukuka na ushirikina wa (hao makafrri). 2-Huwateremsha Malaika na Wahyi (kuihuisha Sharia) kwa amri yake (Mwenyezi Mungu) juu ya anaowataka katika waja wake kwamba “Waonyeni (viumbe) kuwa hakuna wa kuabudiwa isipokuwa Mimi, basi Niogopeni.”3-Ameziumba mbingu na ardhi kwa (ajili ya kudhihirisha) haki; ametukuka na ushirikina wao (hao makafiri). 4-Amemuumba mwanaadamu kwa tone la manii. Tahamaki amekuwa mshindani dhahiri (wa kumkataa Mwenyezi Mungu)Na (pia) amewaumba wanyama. Katika hao mnapata (vifaa vitiavyo) joto na manufaa (mengine); na wengine mnawala. 6-Na mnaona raha mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi. 7-Na (wanyama hao pia) hubeba mizigo yenu kupeleka katika miji msiyoweza kuifika isipokuwa kwa mashaka na taabu. Hakika Mola wenu ni Mpole sana (na) Mwenye rehema nyingi. 8-Na (amewaumba) farasi na nyumbu na punda ili muwapande na (wawe) mapambo. Na ataumba (vipando vingine) msivyovijua.
Ukihesabu maneno ya Kuruani (Kuruani Yenyewe na Siyo Tafsiri) kuanzia mwanzo wa Sura Hii Aya Namba 1 mpaka Aya Namba 8 utapata
Neno وَٱلۡخَيۡلَ (Farasi) ni neno la 72 kuanzia mwanzo wa Sura Ya Al-Nahl
Neno وَٱلۡبِغَالَ (Mbunyu) ni la 73 kuanzia mwanzo wa Sura Ya Al-Nahl
Neno وَٱلۡحَمِيرَ (Punda) ni la 74 kuanzia mwanzo wa Sura Ya Al-Nahl
Sasa tuchunguze Kipande cha Aya namba 8 kinachohusu Wanyama hawa watatu
وَٱلۡخَيۡلَ وَٱلۡبِغَالَ وَٱلۡحَمِيرَ لِتَرۡڪَبُوهَا وَزِينَةً۬ۚ
TAFSIRI
Na (amewaumba) farasi na nyumbu na punda ili muwapande na (wawe) mapambo. (Hesabu Herufi za Kuruani na Siyo Tafsiri)
وَٱلۡخَيۡلَ (Herufi katika Aya Ni 6= 1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6)
وَٱلۡبِغَالَ (Herufi za neno Katika aya Ni 7= 1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7)
وَٱلۡحَمِيرَ (Herufi za nenoKatika Aya Ni 7=1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7)
لِتَرۡڪَبُوهَا (Herufi za neno Katika Aya Ni 7=1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7)
وَزِينَةً۬ۚ (Herufi Katika Aya Ni 5=1 + 2 + 3 + 4 + 5)
Aya Hii ni Namba 8 na kwa hiyo tukijumlisha Namba za herufi zote pamoja Na namba ya Aya utapata
1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7 + 1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7 +1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 6 + 7 + 1 + 2 + 3 + 4 + 5 + 8 (Namba Ya Aya)=136
Sasa Angalia Maajabu ya kushangaza Yafuatayo:
Ukitoa Namba 72 (Farasi) kutoka katika 136 utapata Jawabu ni 64
Ukitoa Namba 73 (Mbunyu) Kutoka katika 136 utapata Jawabu ni 63
Ukitoa Nammab 72 (Punda)O Katika 136 utapata Jawabu ni 62
Unaona Muujiza huu wa kushangaza.
64 ni Chromosomes za Farasi
63 ni Chromosomes za Mbunyu
62 Ni Chromoseomes za Punda
Wataalamu Wanaelewa Namba hizi 64, 63 na 62 ni Chromosomes na ndivyo wanavyotuambia na Ajabu kubwa ni Kuruani ambayo imedokeza jambo hili.
Angalia Jawabu Kutoka Katika Google Chombo cha utafiti katika Mtandao hapa Chini na Utashangaa haya tunayosema. Utapata namba hizi tatu. Na Pia angalia Picha hapa Chini inayohusiana na Sayansi hii ya Ajabu.
Kuruani kweli imekusanya kila kitu. kama alivyosema Mwenyeezi Mungu katika Sura Namba 6 na Aya Namba 38
وَمَا مِن دَآبَّةٍ۬ فِى ٱلۡأَرۡضِ وَلَا
طَـٰٓٮِٕرٍ۬ يَطِيرُ بِجَنَاحَيۡهِ إِلَّآ أُمَمٌ أَمۡثَالُكُمۚ مَّا فَرَّطۡنَا فِى ٱلۡكِتَـٰبِ مِن شَىۡءٍ۬ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّہِمۡ يُحۡشَرُونَ (٣٨)
TAFSIRI
38-Na hakuna mnyama katika ardhi wala ndege arukaye kwa mbawa zake mbili. ila ni umati kama nyinyi (tunadhibiti kila walifanyalo). Hatukupuza Kitabuni (mwetu) kitu cho chote. Kisha watakusanywa kwa Mola wao (awalipe).
Maneno haya siyo madogo. Mwenyeezi Mungu anasema kwamba hakupuuza chochote katika Kurunini kwani kila alichokitaja kina maana sio bure bure. Muujiza Mkubwa kwani Kuruani ilishuka katika Karne ya 7 Na Elimu ya Chromosomes ilianza katika karne19 yaani miaka 1200 tangu kushuka kwa Kuruani Tukufu.
Hakuna Kiumbe chochote aliyejua haya katika wakati huo na hata Mtume Mwenyewe hakufundisha haya kwani yeye alipokea ujumbe na kuufikisha na aliwafundisha yaliyowahusu tu kwani watu katika wakati huo wasingeelewa habari hizi.
Lakini Muujiza Huu umeashiriwa katika kuruani kwa Makusudi ili leo hii wakati tulionao wa Elimu za Sayansi ya hali ya juu uwe Muujiza kwetu Na ili iwarudishe waliopotea na pia kuwanasihi wasiokubali dini hii ya Kiislamu.
Kwa kweli Kuruani imekusanya Elimu ya Ulimwengu Mzima na Hakuna Mwisho.
Tunayoyajua Leo hii inatuhusu sisi na Miaka Ijayo kutagundulikana Mengineyo.
Na itawafaa wengine hapo baadaye na hivyo hivyo Mpaka Mwisho wa Ulimwengu.
Yaani Mpaka Menyeezi Mungu atakapoirithi Mwenyewe Kuruani Yake kwani Ni Maneno Yake Mwenyewe.
Allahu Akbar Allahu Akbar.

Farasi (kushoto)Chromosome 64 Punda (Katikati)Chromosome 62 na Nyumbu (Kulia)Chromosomes 63

Kithibitisho Kuhusiana na Chromosomes za Farasi, Nyumbu na Punda kutoka katika Mtandao (Internet) Kwa Kutumia Chombo cha Utafiti (Google)

Nyuki wa kike ana Mbegu za Chromosomes 32 na Nyuki wa kiume ana mbegu za Chromosomes 16.

Kithibitisho kutoka katika Google (Chombo cha Utafiti cha Mtandao (Internet). Kwa Asili Chromosomes 16 ni Mbegu za Kiume na za Kike ni 32 (Mchanganyiko 16 Mbegu za Kiume na 16 Mbegu za yai Jumla ni 32
E = mc2 ni Formula Ya Mwana Sayansi Maarufu Duniani anayejulikana kwa jina la Albert Einstein
E = mc2 ni Formula inyotokana na Nadharia Ya Einstain Inajulikana Dunia Nzima. Imeleta Faida na Hasara Pia. Katika Mabaya Ya Nadharia hii ilisababisha kutengenezwa kwa Bomu la Atomic Duniani na hata kuweza kuua Watu bila ya sababu kama ilivyoua watu huko Japan katika Mji wa Hiroshima. Na Kuna Mazuri mbalimbali yaliyozalishwa na Nadharia hii kama vile Electronics za kisasa, GPS Navigation na Nuclear Power.
Wataalamu wanatufasiria Formula hii kama ifuatavyo:
{E = mc2, Equation is from the German-born physicist Albert Einstein’s theory of special relativity that expresses “Energy equals mass times the speed of light squared.” On the most basic level, the equation says that energy and mass (matter) are interchangeable; they are different forms of the same thing}
E = mc2 Energy (Nguvu/Kazi) ni sawa na Mass(Kitu/Uzito) x Mbio za Mwanga Squared.
Formula E = mc2 Katika Kuruani Tukufu
Ajabu Ni kwamba Katika Kuruani Kuna Aya Zinazoashiria Kwa Ujumla vipengele mbali mbali vya Nadharia hii Ya Theory of Relativity na katika maandishi haya tumegusia kipengele kimoja tu cha Formula Hii
Katika Sura Namba 99 Ya Al-Zilzalah Aya Namba 7-8 Mwenyeezi Mungu anasema
فَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ خَيۡرً۬ا يَرَهُ ۥ (٧) وَمَن يَعۡمَلۡ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ۬ شَرًّ۬ا يَرَهُ ۥ (٨)
7-Basi anayefanya wema (hata) wa kiasi cha uzito wa Atom (Chembe) ataona jaza yake
8-Na anayefanya uovu (hata) wa kiasi cha uzito wa Atom (Chembe) ataona jaza yake.
Katika Sura Ya Al-Zilzalah Namba 99 Aya Namba 7-8 Neno يَعْمَلْ lina maana ya Kitendo au Nguvu au Kazi na Neno مِثْقَالَ maana yake ni Uzito wa Kitu.
Mwenyeezi Mungu anafananisha baina ya Vitendo Vyetu Vizuri na Vibaya na Atom ambayo ni chembe ndogo sana. Tukifananisha na Nadharia ya Einstain utaona Vitendo Vyetu ni sawa na Energy Na Malipo ya Vitendo Vyetu “Peponi au Motoni” ni sawa na Mass.
Ni sawa na kusema Vitendo Vyetu ni sawa na E (Energy) Pepo na Moto ni sawa na mc2(Mass X c2 ) Yaani Vitendo Vidogo vitazalisha Malipo Mazuri au Mabaya na kulipwa Pepo au Moto
Na katika Sura Namba 4 Ya Al-Nisaa Aya Namba 40 Mwenyeezi Mungu anasema
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظۡلِمُ مِثۡقَالَ ذَرَّةٍ۬ۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةً۬ يُضَـٰعِفۡهَا وَيُؤۡتِ مِن لَّدُنۡهُ أَجۡرًا عَظِيمً۬ا (٤٠)
40-Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu (viumbe vyake hata kitu kilicho sawa na) uzito wa Atom (Chembe); na kama likiwa ni jambo jema (Yeye Mungu) atalizidisha na kutoa ujira mkubwa unaotoka kwake.
Mwenyeezi Mungu anasema Kwamba Hadhulumu na anafananisha dhukuma hiyo na udogo wa Atom ambayo ni chembe ndogo sana. Na mfananisho huu pia unaenda sambamba na Nadharia tuliyoitaja hapo Juu. Kwani Dhuluma ni Kitendo yaani Kitendo cha dhuluma na Atom ni Mass au Kitu ambacho katika Aya hii inaashiria Malipo ambayo yataonekana kwa macho na kitu chochote kinachoonekana ni Mass.
Kuruani imedokeza Nadharia hii kuanzia Karne ya 7 na Nadharia ya Einstain iliandaliwa mwaka 1905 lakini wengi hawajui. Allahu Akbar