UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MIUJIZA MBALIMBALI KATIKA AYA NAMBA 3 YA SURA AL-MAIDAH.
Sura Ya Al-Maidah Namba 5 Aya Namba 3
حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةُ وَٱلدَّمُ وَلَحۡمُ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦ وَٱلۡمُنۡخَنِقَةُ وَٱلۡمَوۡقُوذَةُ وَٱلۡمُتَرَدِّيَةُ وَٱلنَّطِيحَةُ وَمَآ أَكَلَ ٱلسَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيۡتُمۡ وَمَا ذُبِحَ عَلَى ٱلنُّصُبِ وَأَن تَسۡتَقۡسِمُواْ بِٱلۡأَزۡلَـٰمِۚ ذَٲلِكُمۡ فِسۡقٌۗ ٱلۡيَوۡمَ يَٮِٕسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن دِينِكُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِۚ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِى وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَـٰمَ دِينً۬اۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِى مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٍ۬ لِّإِثۡمٍ۬ۙ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬ (٣)
TAFSIRI
Mmeharimishiwa nyamafu na damu na nyama ya nguruwe, na kinyama kilichochinjwa si kwa ajili ya Mwenye1i Mungu, na kilichokufa kwa kusongeka koo, na kilichokufa kwa kupigwa, na kilichokufa kwa kuanguka, na kilichokufa kwa kupigwa pembe (na mwIngine), na alichokila mnyama (kikafa), ila mkiwahi kukichinja (kabla hakijafa). Na (pia mmeharimishiwa) kilichochinjwa panapofanyiwa ibada isiyokuwa ya Mungu (kama mizimuni). Na ni (haramu kwenu) kutaka kujua siri kwa kuagua kwa mabao (na yaliyo kama hayo). Hayo yote ni maasi. Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu. Na mwenye kushurutishwa na njaa, pasipo kuelekea kwenye dhambi, (akala hivi vilivyoharimishwa, basi hapana kitu); hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha (na) Mwingi wa rehema
SHEREHE YA AYA NA MIUJIZA YA KUSHANGAZA SANA
ٱلۡيَوۡمَ يَٮِٕسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن دِينِكُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِۚ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِى وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَـٰمَ دِينً۬اۚ
Kipande hiki cha Aya kutoka katika Aya hapa Juu Namba 3 Sura Ya Al-Maidah kina maana Tofauti na Mengineyo katika Aya hapa Juu. Kipande hiki cha Aya kilishuka Siku ya Arafah wakati Mtume Alipokuwa akitoa Hotuba yake Maarufu inayojulikana kama “Hotuba Ya Kuaga” (Farewell Sermon) Baada ya hotuba hiyo Maswahaba walilia sana kwani Hotuba hiyo iliashiria Mwisho wa Wahyi na Pia Muda wa Mtume (Sala na Amani zake Mola Zimfikie) kuishi hautakuwa mrefu. Na Baada ya Muda si Mrefu akafariki Duniya alipokuwa na Miaka 63.Kuruani Ilishuka kwa Mtume kwa kipindi cha Miaka 23.
Kipande hiki cha Aya Hii kinazungumzia Kushindwa kwa Makafiri na Kukamilika Kwa Wahyi. Na Mengineyo katika Aya Namba 3 Hapa Juu yanazungumzia Maamrisho kuhusiana na Sheria za Dini; Sheria inayohusika na vitu mbalimbali tulivyoharimishiwa kuvila na mengineyo. Kipande cha Aya hii kimepachikwa katika Aya hii namba 3 kiajabu sana kwa hekima yake Mwenyeezi Mungu. Kwa kweli vipande hivi viwili (Yaani Kipande kilichoshuka huko Arafah na Mengineyo katika Aya Hii) vina Madhumuni mbalimbali na Huenda kuna Muujiza Mingine katika mpangilio huu.
Ajabu Ni kwamba Elimu ya Hesabu inatufunulia Muujiza wa Kushangaza na Huenda ndiyo maana Kipande hiki kimepachikwa katika Aya Hii. Yaani Kuwe na Miujiza Mingine kama tutakvyoona na Mwenyeezi Mungu anajua zaidi.
Hebu tuchunguze Aya Hii kwa kutumia Elimu ya Hesabu:
حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَيۡتَةُ وَٱلدَّمُ وَلَحۡمُ ٱلۡخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيۡرِ ٱللَّهِ بِهِۦ وَٱلۡمُنۡخَنِقَةُ وَٱلۡمَوۡقُوذَةُ وَٱلۡمُتَرَدِّيَةُ وَٱلنَّطِيحَةُ وَمَآ أَكَلَ ٱلسَّبُعُ إِلَّا مَا ذَكَّيۡتُمۡ وَمَا ذُبِحَ عَلَى ٱلنُّصُبِ وَأَن تَسۡتَقۡسِمُواْ بِٱلۡأَزۡلَـٰمِۚ ذَٲلِكُمۡ فِسۡقٌۗ ٱلۡيَوۡمَ يَٮِٕسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن دِينِكُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِۚ ٱلۡيَوۡمَ أَكۡمَلۡتُ لَكُمۡ دِينَكُمۡ وَأَتۡمَمۡتُ عَلَيۡكُمۡ نِعۡمَتِى وَرَضِيتُ لَكُمُ ٱلۡإِسۡلَـٰمَ دِينً۬اۚ فَمَنِ ٱضۡطُرَّ فِى مَخۡمَصَةٍ غَيۡرَ مُتَجَانِفٍ۬ لِّإِثۡمٍ۬ۙ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ۬ رَّحِيمٌ۬ (٣)
Ukihesabu Maneno Kuanzia Mwanzo wa Aya Mpaka neno دينا yaani mwisho wa neno la kipande cha Aya kilichoshuka huko Mecca siku ya Arafah utapata maneno 63 na namba hii ni Umri wa Mtume. Jambo la kushangaza ni Neno la mwisho linalohusiana na Kukamilika kwa Dini. Na Umri wa Mtume alikuwa na miaka 63 wakati huo na baadaye akafariki kwa kweli inashangaza sana. Maneno 63 yanalingana na Umri wa Mtume!!! Allahu Akbar.
Muujiza Mwingine wa kushangaza ni Kwamba Kipande cha Aya
اليوم ييس الذين كفروا من دينكم فلا تخشوهم و اخشون اليوم اكملت لكم دينكم و اتممت عليكم نعمتي و رضيت لكم الاسلم دين
kinasema kwamba Wahyi umefikia mwisho. Na Ajabu ni kwamba jumla ya maneno ya kipande hiki ni 23. Na namba hii inalingana na miaka 23 ya WAHYI kwani Kuruani imechukua miaka 23 kushuka. (Revelation Period). Sasa tunapata Muujiza wa pili. Allahu Akbar.
Na Muujiza Mwingine wa kushangaza zaidi ni Herufi ya Kipande hiki ambacho kina maneno 23 ni herufi 92 ambazo kihesabu ni sawa na 23 x 4=92 Je unaona
Muujiza wa Tatu? Miaka 23 ya WAHYI inathibitishwa tena mara ya pili katika idadi ya Herufi. Allahu Akbar. Allahu Akbar. Muujiza wa Tatu na kithiitisho mbele ya macho yetu. Kwa kweli inashangaza sana. Allahu Akbar.
Hebu tuendelee na safari yetu. Twende mbele na tuchunguze zaidi maajabu haya yasiyo na mwisho.
Sasa tuhesabu Herufi za Aya Yote ya namba 3 Sura Ya Al-Maidah tutapata herufi 276 na hii namba ni sawa na kusema 23 x 12 =276
Sasa angalia tena Muujiza Mwingine wa Kushangaza. Namba 23 ni muda wa WAHYI (Kushuka kwa kuruani kwa muda wa miaka 23) na 12 ni Miezi Ya mwaka. Ajabu Kubwa Sana.
Namba hii 23 x 12 =276 inatupa habari nyingine kwamba Kuruani ilishuka kwa muda wa miaka 23 ambayo ni sawa na miezi 276!!!! Allahu Akbar. Hapa tunapewa Miezi ya kushuka kuruani.
Hii Kweli ni Miujiza isiyo na Mwisho. Hebu tuendelee na uchunguzi zaidi. Mwenyeezi Mungu amejaalia Mwaka kuwa na Miezi 12. Katika Miezi 12 kuna miezi minane ya kawaida na miezi minne ya HURUM. Kama anavyosema katika Kuruani Tukufu Aya Ifuatayo:
ان عده الشهور عند الله اثنا عشر شهرا في كتب الله يوم خلق السموت و الارض منها اربعه حرم) [التوبة: 36].
TAFSIRI
Idadi ya Miezi kwa Mwenyeezi Mungu ni Miezi Kumi na Mbili katika Kitabu Chake alipoumba Mbingu na Ardhi na Miongoni mwa Miezi hii kuna miezi Minne ya HURUM
La kushangaza ni kwamba ikiwa katika kila mwaka kuna miezi Minne ya HURUM basi Katika miaka 23 ya Kushuka Kuruani kutakuwa na Miezi Ya HURUM 92 (kwani miaka 23 x Miezi 4= ni sawa na miezi 92) Hii Miezi Minne; Dhulkaedah, Dhulhijjah, Muharram and Rejab Ni Miezi Mitukufu. Ni Miezi Ya Ibada na kujiepusha na Mabaya.
Kufuatana na Utafiti hapo nyuma tumeona kwamba Idadi ya Herufi za Kipande cha Aya hapa chini
اليوم ييس الذين كفروا من دينكم فلا تخشوهم و اخشون اليوم اكملت لكم دينكم و اتممت عليكم نعمتي و رضيت لكم الاسلم دين
ni 92. Na Kihesabu namba hii ni sawa na 23 X 4=92. Ukifikiri utaona Namba 4 katika Hesabu inaashiria Miezi Ya HURUM na namba 23 Ni Miaka Ya WAHYI (Revelation Period) na Huenda Mwenyeezi Mungu anatupa ujumbe kwamba “Kuruani Imekamilika katika muda huo wa WAHYI wa miaka 23 ilikuwa na itakuwa hivyo hivyo mpaka mwisho wa Ulimwengu HARAMU kwa mtu yeyote kuigeuza, kubadili, kuondoa au kuzidisha Aya Za Kuruani Na mpaka Leo imehifadhiwa kama ilivyoshuka. Ni HARAMU kugeuza au kufanyia Upuuzi wowote katika maneno ya Mwenyeezi Mungu Mtukufu. Na Hivyo Hivyo mpaka Ulimwengu utakapokwisha na Mwenyeezi Mungu atakapoirithi Kuruani Yake.
Aya Hii ambayo iliwaliza Mwaswahaba ina Miujiza Mingine Ya Kushangaza. Hebu tuiandike tena hapa chini;
اليوم ييس الذين كفروا من دينكم فلا تخشوهم و اخشون اليوم اكملت لكم دينكم و اتممت عليكم نعمتي و رضيت لكم الاسلم دين
Kipande cha kwanza cha Aya:
اليوم ييس الذين كفروا من دينكم فلا تخشوهم و اخشون
kinasema kwamba “Makafiri Wamekata Tamaa Kuizuia Dini Yenu na Msiwaogope bali Niogopeni mimi” Kipande hiki kina Idadi ya Maneno 10 (Herufi Ya و WAW hapa inahesabiwa kama Neno) Sasa Angalia Muujiza Mwingine wa Kushangaza Allahu Akbar Maneno 10 ya Kipande cha kwanza cha Aya yanaashiria Miaka 10 aliyokaa Mtume hapo Madina na Makafirri walikata Tamaa kuzuia Uislamu Usiendelee.
Na Kipande Cha Pili cha Aya:
اليوم اكملت لكم دينكم و اتممت عليكم نعمتي و رضيت لكم الاسلم دين
Kinasema “ Leo nimewakimilishieni Dini Yenu na Nimewatimizieni Neema Zangu Na Nimewaridhia Uislamu Kuwa Dini Yenu” kina Meneno 13 (Herufi Ya و WAW hapa inhesabiwa kama Neno) Na Muujiza Wa Maneno 13 ya Kipande cha pli cha Aya yanaashiria Muda wa Miaka 13 Ya Kulingania Dini Hapo Mecca.
Muujiza wa Ajabu Sana. Kwani Madina Mtume aliishi miaka 10 na Mecca miaka 13 Jumla Miaka 23 ya WAHYI. Alipewa WAHYI alipokuwa na Umri wa miaka 40 na kwa hiyo alifariki alipokuwa na miaka 63. Allahu Akbar.
Angalia Hesabu zinazofafanua Miujiza katika Maandishi ya Kuruani mpaka Umri wa Mtume Umeashoriwa bila yeye mwenyewe kujua haya. Kwani Haya yamekuwa Muujiza kwetu leo hii katika kipindi chetu cha Elimu mbalimbali za Sayansi.
Na Mushrikiyna walipomuuliza Mtume awape Muujiza Mwenyeezi Mungu akashusha Aya ambayo ipo katika Sura Namba 29 Aya namba 51 Inayosema
أَوَلَمۡ يَكۡفِهِمۡ أَنَّآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡڪِتَـٰبَ يُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَرَحۡمَةً۬ وَذِڪۡرَىٰ لِقَوۡمٍ۬ يُؤۡمِنُونَ (٥١)
TAFSIRI
Je Haiwatoshi kwamba sisi tumeshusha kitabu wanachosomewa. Kwa hakika Katika Hayo ni Rehema na Ukumbusho kwa Waumini.
Hii Aya inasema kwamba Kuruani Inatosha Kuwaonyesha wabishi na wakaidi wanaopinga uislamu na pia wanaofanya shaka. Na Muujiza Mwingine katika Aya hii ni kwamba ina Herufi 63!!!! na kama tulivyosema Namba 63 inaashiria Umri wa Mtume Mohamed. (Sala na Amani Ya Mwenyeezai Mungu Zimfikie).
Hili Ni Tonye tu katika Bahari Ya Miujiza Katika Aya Hii. Sasa Je Kuruani yote? Huoni Maajabu Yasiyo na Mwisho. Allahu Akbar. Allahu Akbar.
UTAFITI KUHUSIANA NA MAZIWA YA MAMA UNATHIBITISHA KWAMBA AYA ZA KURUANI NA HADITHI ZA MTUME NI UHAKIKA NA KURUANI NI MUUJIZA MKUBWA.
Katika Mwaka 2007, Mara ya Kwanza Profesa Peter Hartmann, Dakitari Mark Cregan na Timu yao katika University Ya Western Australia waligundua Kuwepo kwa STEM CELLS (Celi za Asili) katika Maziwa Ya Mama.
Na baada ya hapo Dakitari anayejulikana kwa jina Foteini Kakulas katika University Hiyo Hiyo Ya Australia alifanya utafiti na kugundua kwamba STEM CELLS kutoka katika Maziwa Ya Mama Yanaweza kutumika katika kutengenezea Cells (Celi) za Viungo Vinginevyo vya Mwili kama vile Mifupa, Fats, Maini, Na viungo vinginevyo.
Utafiti unaendelea kusema kwamba Maziwa ya Mama siyo chakula chenye kushibisha peke yake bali una sifa zote za Mama.
Maziwa ya Mama Yanamjenga mtoto na mtoto Huyo anachukuwa sifa zote za mama yake.
Nimenakili hapa chini maneno yanayotokana Na Utafiti wa wa Dakitari Foteini Kokulas. Anaendelea kusema kwamba Mwili wa Mtoto Unachukua Habari au sifa zote zilizopo katika GENES za mama yake.
Kwa kiswahili kizuri tutasema Mtoto ana Damu ya Mama Yake.
Kwa kufupi mtoto ana copy (ananakili) kila kitu.
Hapa chini nimechukua Matokeo ya Utafiti aliofanya Dakitari Foteini Kokulas Huko Autralia.
“Mother’s milk contains stem cells, which are able to cross the gut and migrate into the blood of the nursed offspring. From the blood, they travel to various organs including the brain, where they turn into functioning cells. This breastmilk stem cell transfer from mother to offspring appears to be more than just a random event, potentially contributing important developmental attributes. Future research must concentrate on how this phenomenon can be salvaged medically, for example to help preterm infants survive and develop optimally.
What would you think if you were told that your baby contains part of your body? Literally. Or that you actually have inside you part of your baby’s body? Yes, literally. As much as it sounds more of an emotional expression of love between the mother and her baby, some of the cells that contain all our genetic information (not half) are indeed exchanged between the mother and her baby”
Wataalamu Bado wanasoma na hawajamaliza kuhusu yaliyopo katika Maziwa ya Mama. Hivi karibuni wamegundua Mengineyo Kama vile microRNA;s katika maziwa ya mama na Wanaendelea kusoma kwani Elimu zetu bado Changa.
“A decade after microRNAs were found in mother’s milk, scientists are still trying to work out why they are there and how they affect health”
Kwa hiyo mtoto wa mama mwingine anapokunywa maziwa ya mama basi anachukua sifa hizo pia!! siyo mtoto wa mama yake wa asili bali mtoto akilelewa na mama mwingine basi atachukua sifa hizi zote tulizozotaja hapa juu. Na ndivyo sayansi inatuambia.
Sasa Tuchambue Kuruani Tukufu.
MUUJIZA KATIKA KURUANI KUHUSIANA NA MAZIWA YA MAMA.
Katika Karne ya 7 Kuruani ilishushwa kwa Mtume (S.A.W) na Aya Ikashuka Inayotufundisha na kutukataza/kutuharimishia wale ndugu ambao wasioane na Mtume pia akasema katika hadithi yake hivyo hivyo. Yaani Mwenyeezi Mungu anakataza Kuoana Wale ambao Wamenyonya Maziwa kwa mama mmoja kwani wanakuwa ndugu ijapokuwa mama zao tofauti. Imekatazwa kwani kuna hatari za Maradhi mbalimbali yanayoweza kuzuka kutokana na GENES au zile sifa za Mama zilizopo katika walionyonya au kunywa maziwa yake. Angalia Muujiza Unajitokeza baada ya Utafiti wa Wataalamu. Mtume (S.A.W) alifikisha Ujumbe lakini hakuwa akijua utafiti wetu wa leo kugundia haya, lakini Mwenyeezi Mungu aliyepanga haya alijua yatakayokuja baadaye. Allahu Akbar.
Aya Katika Kuruani Tukufu
Mwenyeezi Mungu anasema katika Sura Ya Al-Nisaa Namba 4 Aya Namba 23
حُرِّمَتۡ عَلَيۡڪُمۡ أُمَّهَـٰتُكُمۡ وَبَنَاتُكُمۡ وَأَخَوَٲتُڪُمۡ وَعَمَّـٰتُكُمۡ وَخَـٰلَـٰتُكُمۡ وَبَنَاتُ ٱلۡأَخِ وَبَنَاتُ ٱلۡأُخۡتِ وَأُمَّهَـٰتُڪُمُ ٱلَّـٰتِىٓ أَرۡضَعۡنَكُمۡ وَأَخَوَٲتُڪُم مِّنَ ٱلرَّضَـٰعَةِ وَأُمَّهَـٰتُ نِسَآٮِٕكُمۡ وَرَبَـٰٓٮِٕبُڪُمُ ٱلَّـٰتِى فِى حُجُورِڪُم مِّن نِّسَآٮِٕكُمُ ٱلَّـٰتِى دَخَلۡتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمۡ تَكُونُواْ دَخَلۡتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡڪُمۡ وَحَلَـٰٓٮِٕلُ أَبۡنَآٮِٕڪُمُ ٱلَّذِينَ مِنۡ أَصۡلَـٰبِڪُمۡ وَأَن تَجۡمَعُواْ بَيۡنَ ٱلۡأُخۡتَيۡنِ إِلَّا مَا قَدۡ سَلَفَۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورً۬ا رَّحِيمً۬ا (٢٣) 23.
TAFSIRI
Mmeharimishwa (kuoa) mama zenu, na watoto wenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na ndugu za mama zenu, na watoto wa ndugu zenu, na watoto wa dada zenu, na mama zenu waliokunyonyesheni, na dada zenu wa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu, waliozaliwa na wake zenu mliowaingilia. Lakini kama nyinyi hamjawaingilia, basi si vibaya kwenu (kuwaoa). Na (mmeharimishiwa) wake wa watoto wenu waliotoka katika migongo yenu. Na (mmeharimishiwa) kuwaoa
Hadithi Ya Mtume
Mtume Amesema Katila Hadithi Iliyokusanywa na Imam Abu `Isa Muhammad at-Tirmidhi katika vitabu vyake vya Jami` at-Tirmidhi
حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ مَنِيعٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيلُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم “ إِنَّ اللَّهَ حَرَّمَ مِنَ الرَّضَاعِ مَا حَرَّمَ مِنَ النَّسَبِ ” . قَالَ وَفِي الْبَابِ عَنْ عَائِشَةَ وَابْنِ عَبَّاسٍ وَأُمِّ حَبِيبَةَ . قَالَ أَبُو عِيسَى حَدِيثُ عَلِيٍّ حَسَنٌ صَحِيحٌ .
Hadithi hii inasema kwamba Mwenyeezi Mungu Ameharimisha Wale ambao wa kunyonya sawa sawa na Wale Wa Nasab yaani Watoto wa Asili. Sheria ni Moja kwa aliyenyonya na Mtoto wa mama mmoja. Hawa wawili wanakuwa ndugu na ni haramu kuonana. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi lakini antuepushia Maradhi mbalimbali. Allahu Akbar.
Angalia Muujiza Wa Kuruani. Tumefundishwa mambo haya na leo Wataalamu wapo katika Utafiti bado hawajapata jibu. Allahu Akbar. Kuruani na Hadithi zinakubaliana na Sayansi na ni ukweli.Allahu Akbar.
MAAJABU YA SURA YA AL-IKHLAS
سُوۡرَةُ الإخلاص
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤)
TAFSIRI
Kwa jina Ia Mwenyezi Mungu, Mwenye kuneemesha neema kubwa kubwa na Mwenye kuneemesha neema ndogo ndogo.
1 : Sema: Yeye ni Mwenyezi Mungu Mmoja (tu).
2. Mwenyezi Mungu (tu) ndiye anayestahiki kukusudiwa (na · viumbe· Vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea).
3. Hakuzaa wala Hakuzaliwa
4· Wala hana anayefanana Naye hata mmoja
MAAJABU KATIKA SURA YA AL-IKHLAS
Neno يَلِدۡ YALID lipo katikati ya maneno yote katika Sura kama tunavyoona hapa Juu. Na herufi LAM ipo katikatiki ya Herufi zote za sura hii. Sasa angalia Mpangilio wa kushangaza. Upande wa kushoto wa Neno YALID kuna Maneno 7 na Upande wa kulia Wa neno YALID kuna maneno 7 pia. Upande wa Kushoto wa Herufi LAM kuna Herufi 23 na Upande wa Kulia wa Herufi LAM kuna Herufi 23 pia. Hii Herufi LAM imetiwa KASRAH chini ya Herufi. Na ni KASRAH ya pekee katika Sura Ya Al-Ikhlas. Hii alama ya KASRAH ni ya Mwanzo kutumika katika Sura Ya Kwanza, Aya Ya Kwanza katika Msahafu katika Sura Ya Al-Fatiha Chini Ya Herufi Ba na Mim Katika neno بِسۡمِ ya Aya بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ na Ni Ya Mwisho kutumika Katika Msahafu katika Sura Ya Al-Nas ambayo ni ya Mwisho Chini ya herufi Sin ambayo ni ya Mwisho katika Neno WANASI وَٱلنَّاسِ katika Aya Ya Mwisho ya Msahafu مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ Kwa kifupi Alama ya KASRAH ndiyo alama ya kwanza kufungulia Kuruani na Ya Mwisho kufungia Kuruani. Na Aya Ya Mwanzo kushuka Katika Kuruani ni Katika Sura Ya Al-ALAQ ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ katika neno ٱقۡرَأۡ (Alif hapa ina Kasrah)Hii ndiyo Aya Ya Kwanza Kushushiwa Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Imfikie) Usisahau kwamba Mpangilio wa Kuruani haufuatani na kushuka kwa Kuruani. Kwani Mpangilio huu tulionao ni Muujiza Mkubwa. Kuruani haikupangwa hovyo hovyo bali ni maamrisho kutoka kwa Mwenyeezi Mungu. Mpangilio wa kuruani haufuatani na mpangilio wa kushushwa kuruani kwa mtume na hii ni hekima ambayo leo hii tunapata miujiza mbali mbali kufuatana na mpangilio huu. Katika Aya Hii Ya Mwanzo Neno ٱقۡرَأۡ lenye maana ya “SOMA” pia limetiwa KASRAH katika Herufi yake ya ALIF ambayo ni ya mwanzo.
Tukiendelea na uchambuzi zaidi tutaona maajabu mengi makubwa na ya kushangaza sana. Idadi ya maneno na herufi pia ni Miujiza mikubwa. Namba 23 hapa huenda inaashiria Chromosomes 23 za Kizazi au Miaka 23 ya Kushuka Kwa Kuruani. Na Namba 7 hapa pia huenda inaashiria Stage au Hatua mbali mbali za maumbile ya binaadamu katika tumbo la Kizazi kwani katika Elimu ya Embroyology tunasoma kwamba binaadamu anapitia stages 7 katika tumbo la uzazi na Muujiza mwingine mkubwa ni kwamba Stages 7 za maumbile zimeashiriwa katika Kuruani tukufu (nimezungumzia habari hizi katika swhwmu nyinginezo za website hii). Namba 7 pia nimeizungumzia kwa urefu katika sehemu nyinginezo za website hii. Kwa mfano Mwenyeezi Mungu ameumba Mbingu na Ardhi kila moja katika matabaka 7. Mwanga wa jua una Rangi 7 na Mengineyo ambayo nimezungumzia katika Website hii siku zilizopita. Na Ajabu Ni kwamba tunakuta namba hii katika Dini ya Kiislamu kama vile Mecca katika Hija TAWAF hufanyika mara 7, Safwa na Marwa hufanyika mara 7. Na mengi mengineyo.
Sura Ya Al-Ikhlas ina Jumla ya Maneno 15 na Herufi 47 na ajabu ni kwamba katika Hesabu Prime Number 47 ni ya 15 . Hii kweli inashangaza!!!
Na La kushangaza pia ni Katika Herufi za Kiarabu 28 kuna Herufi 15 ambazo hazikutumika katika Sura Ya Al-Ikhlas. Yaani Herufi zilizotumika katika Sura Ya Al-Ikhlas ni 13 tu peke yake.
Kwa hiyo Namba 15 hapa inaonyesha maajabu. Hii inaonyesha haya ni maneno yake Mwenyeezi Mungu kwani maneno yamepangika kiajabu sana.
Sasa tukihesabu Herufi za Jina la Nwenyeezi Mungu
ٱللَّهُ (ALLAH) katika Sura Ya A-lIkhlas. Herufi ni Tatu nazo ni Alif, Lam na Haa.
Herufi Alif imetumika na Kukariri Katika Sura Ya Al-Ikhlas mara 6, Herufi Laam mara 12 na Herufi Haa mara 4. Ukijumlisha utapata Jumla Herufi 22 Na namba hii ni sawa na (2 X 11) Namba 2 inaashiria Sura mbili zinazofuata Sura Ya Al-Ikhlas yaani Sura Ya Al-Falaq na Al-Nasi na Namba 11 inaashiria Jumla Ya Aya za Hizo Sura Mbili. (Al-Falaq Aya 5 + Al-Nas Aya 6=11). Je unaona ya Kushangaza? Allahu Akbar.
Hebu tulinganishe na Sehemu nyinginezo katika kuruani tukufu;
Sura Ya Al-Ikhlas ni Ya 3 kutoka Mwisho wa Kuruani na Sura Ya Al-Imran ni Ya 3 kutoka Mwanzo wa Kuruani.
إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ ٱللَّهِ كَمَثَلِ ءَادَمَۖ خَلَقَهُ ۥ مِن تُرَابٍ۬ ثُمَّ قَالَ لَهُ ۥ كُن فَيَكُونُ (٥٩)
TAFSIRI
59. Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam; alimwumba kwa udongo kisha akamwambia: “Kuwa”; basi akawa.
Katika Sura Ya Al-Ikhlas Mwenyeezi Mungu amesema kwamba Hakuzaliwa wala hakuzaa Na katika Aya namba 59 Sura Ya Al-Imran Mwenyeezi Mungu anasema Kwamba Adam na Nabii Isa waliumbwa na Mwenyeezi Mungu. Na la kushangaza ni kwamba Aya Namba 59 ina maneno 15 na Herufi 47 sawa sawa na Idadi ya Maneno na Herufi za Sura Ya Al-Ikhlas!!!
Neno la katikati katika Sura Ya Al-Ikhlas ni YALID na Maana ni kwamba Hakuzaa yaani Mwenyeezi Mungu hakuzaa na Katika Aya Namba 59 hapa Juu Neno la katikati ni خَلَقَهُ Kamuumba na katika Aya Hii Mwenyeezi Mungu anasema Amewaumba Adam na Nabii Isa kwa Udongo.
Katika Sura Ya Al-Ikhlas Mwenyeezi Mungu anasema kwamba Hakuzaliwa na Hakuzaa na katika Aya namba 59 Sura Ya Al-Imran anasema kwamba Ameumba. Yeye ni Muumbaji lakini hakuumbwa.
Sura Ya Al-Ikhlas ilishushwa kumsaidia Mtume (Sala na Amani Yake Mwenyeezi Mungu Imfikie) kuwajibu Makafiri huko Mecca walipomuuliza Mtume Asili ya Mwenyeezi Mungu. Yaani walifikiri Mungu ana Ukoo kama walivyozoea kufanya hivyo na Miungu yao ya Bandia (Masanamu) Na Mwenyeezi Mungu akawajibu kwamba Yeye ni Pekee, Hategemei bali hutegemewa, Hakuzaa wala kuzaliwa na hakuna anayefanana naye.
NYONGEZA YA MIUJIZA KATIKA SURA YA AL-Ikhlas
KATIKA UPANDE WA KUSHOTO NA KULIA WA HERUFI Al-Lam ILIYOPO KATIKATI YA SURA KATIKA NENO يَلِدۡ AMBAYO INA ALAMA YA KASRAH
1/Kuna Alama za Fathah 9 kabla na 9 Baada ya Al-lam iliyotiwa Kasrah
2/Kuna Alama za Dhummah 6 kabla na baada ya Al-lam iliyotiwa Kasrah
3/Kuna Alama ya Tanwin Moja kabla na Nyingine baada ya Al-lam iliyotiwa Kasrah.
SIFA ZA SURA YA AL-IKHLAS
Sura Ya Al-Ikhlas ni Sura Pekee ambayo imejumuisha Kiwakilishi Yaani Pronoun, Jina la Mwenyeezi Mungu na Sifa Zake.
بِسۡمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلرَّحِيمِ قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢) لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤)
Kiwakilishi au Pronoun هُوَ (HUWA)
Jina lake mola ٱللَّهُ (ALLAH)
Sifa zake mbili أَحَدٌ (AHAD) na ٱلصَّمَدُ (ASWAMAD)
Sifa Ahad Maana yake ni Pekee yaani Hana Msaidizi au Mwingine
Sifa Aswamad Maana yake Hategemei Mwingine. Kila Kiumbe kinamuhitaji lakini yeye hahitaji msaada wowote.
Aya Mbili za mwanzo zinathibitisha anayostahiki. Upweke na Kutokutegemea Chochote.
قُلۡ هُوَ ٱللَّهُ أَحَدٌ (١) ٱللَّهُ ٱلصَّمَدُ (٢)
na Aya mbili za mwisho zinakana asiyostahiki. Hakuzaa na Hakuzaliwa. Hakuna kinachofanana na yeye.
لَمۡ يَلِدۡ وَلَمۡ يُولَدۡ (٣) وَلَمۡ يَكُن لَّهُ ۥ ڪُفُوًا أَحَدٌ (٤)
MAJINA YA SURA YA AL-IKHLAS
Sura Ya Al-Ikhlas ina Majina Mbali Mbali kama vile
Al-iKhlas (Kutakasa Nia katika Imani), Al-Tafriyd (Pekee) Al-Tajriyd (Imeepukana na Kila Sifa Mbaya),Al-Tawhiyd (Kumpwekesha Mwenyeezi Mungu),Al-Najah (Kufanikiwa),Alwilayah (Malindo au kujilinda),An-Nisbah(Kujiunga na Mwenyeezi Mungu katika Imani),Al-Maarifah) Elimu, Al-Jamal (Uzuri), Al-Muqashqashah (Kujiponyesha na Maradhi ya Imani ya Kikafiri), Al-Muwaidhah (Kujilinda), Al-Swamad (Kutokutegemea Kingine), Al-Asas (Msingi), Al-Mania’a (Kuzuizi cha adahbu ya kaburi), Al-Muhdhirah (Kikusanyo cha Malaika Sura Inaposomwa). Al-Munfirah (Kinachokimbiza Mashetani Inaposomwa), Al-Braaah (Uhuru kutokana na Ibada za Masanamu na Ibada zisizo sahihi).Al-Mudhakirah (Kikumbusho cha Ibada ya Mungu mmoja asiye na Shirika), Al-Nur (Mwanga), Al-Aman (Usalama), Al-Muqaribah (Kujikurubisha Karibu na Mwenyeezi Mungu.