UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MIUJIZA MBALIMBALI YA KUSHANGAZA
Alhamdulilahi Mwenyeezi Mungu akipenda NItaanza Mlango huu na Muujiza Wa Kushangaza ambao unahusiana na MVI za Uzeeni lakini Muujiza huu utachukua Muda kuuelezea na kwa hiyo Nitakuwa Nikiongeza Kidogo Kidogo mpaka mwisho.
Baada ya Hapo Nitaanza Muujiza Wa Pili ambao Pia Unashangaza Sana. Utahusu Mbegu ya KHARDALI (MUSTARD SEED).
Miujiza Yote Miwili itachukua Muda kuelezea Habari zake.
Maneno Yote mawili; MVI na Khardali yametajika Katika Kuruani Kiajabu Sana.
Mpango NItakaoufuata Katika Maelezo haya utakuwa kama ufuatao:
1/Kwanza Nitaelezea Sayansi inayohusiana na Maneno haya Mawili.
2/Pili Nitazitaja Aya Za Kuruanii Zenye Maneno haya Mawili na Kisha Tutafasiri Aya Hizi.
3/Nne NMitasherehesha na Kuelezea Muujiza Wa Kushangaza wenye Kuthibitisha Sayansi Ya Meneno Haya Mawili kama tulivyosoma.
———–
Katika Sherehe Zote hizi mbili ninawategemea Wataalamu Na Wanavyuoni, Mashekhe na Walimu Wangu. Mwenyeezi Mungu Awazidishie Elimu na Kila La Kheri Kwa Juhudi Zao Tukufu.
Na Kazi Hii Ninamtegemea Mwenyeezi Mungu Msaada wake. Na pia Ninamuomba Anisamehe iwapo Sherehe hii siyo Muradi wake. Lakini ni Juhudi za Mja wake. Huenda Nitakayoelezea yatatuzidishia Imani.
MUUJIZA WA KWANZA
MVI (UZEE)
Ili kuelewa Vizuri Aya Za Kuruani na hasa Muujiza Wa leo ambao ni MVI itatubidi tuzame katika kuelezea Sayansi Inayohusiana na MVI.
Haiwezekani kuzungumzia Sayansi Ya Nwele yote kwani sio Madhumuni Ya Utafiti Huu bali ni kuelezea tu yale yatakayohusu Muujiza Wa Kuruani na Kwa hiyo moja kwa moja nitaanza na Kugusia Mfumo na Muundo wa Nywele Kwa Ufupi (Structure and Composition of The Hair).
Kwanza Nywele Zimeundwa kwa Asilimia 95% za Keratin, Na Hata Makucha na Manyoya ya Mwilini yameudwa kwa Karatin
(The hair is made up of 95% keratin, a fibrous, helicoidal protein (shaped like a helix) that forms part of the skin and all its appendages (body hair, nails, etc.). Keratin is synthesized by keratinocytes and is insoluble in water, thus ensuring impermeability and protection for the hair).
Unywele Umegawanyika Katika Swhemu Tatu:
Sehemu Ya Kwanza kuanzia Juu Ya Unywele Inaitwa katika Sayansi Ya Human Biology, Cuticle , Sehemu Ya Pili Cortex na Sehemu ya Tatu ni Medulla.
Ndani Ya Cortex kuna Celi (Cells) ambazo zinajulikana kwa jina kama Melanocytes na Hapa ndipo Melanin ambayo Inahusika Na Rangi Ya Nwele Inapoundwa. Katika Melanocytes Kuna Enzyme Inayojulikana kama Tyrosinase Enzyme ambayo Inahusika Katika Kuundwa kwa Melanin (Pigmentation).
(The hair’s structure can be divided into 3 distinct parts: – Medulla: innermost layer of the hair shaft, composed of an amorphous, soft, oily substance – Cuticle: thin protective outer layer that contains the nourishing portion essential to hair growth. It is highly keratinized, composed of cells shaped like scales that are layered one over the other, measuring about 60 micrometers long and about 6 micrometers wide. – Cortex: main component of the hair, containing long keratin chains that add elasticity, suppleness and resistance to the hair. The cells of the cortex are joined together by an intercellular cement rich in lipids and proteins. Each cell is composed of bundles that lie in the direction of the hair length: these are macrofibrils which are made up of microfibrils, which in turn contain protofibrils)
(The role of melanocytes and keratinocytes The hair cortex also contains melanin. Made by specialised cells named melanocytes, melanin is the pigment responsible for the hair color. Situated near the hair bulb the melanocytes inject pigments into keratinocytes of the new hair shaft. The color lasts during the hair cycle, from the genesis to the end, when the hair falls)
Kama Tulivyosema Kinachogeuza rangi ya nywele ni Pigmentation inayojulikana kwa jina kama Melanin Nayo ipo aina mbili
1/Eumelanin
Aina Ya Melanin Hii Inasababisha Nywele kuwa Baina Ya Rangi ya Brown na Rangi Nyinginezo za katikati Mpaka Rangi Nyeusi
2/Pheomelanin
Na Aina Ya Melanin Hii Inasababisha Nywele Kuwa Rangi Baina Ya Rangi Ya Manjano na Nyinginezo za Katikati Mpaka Nyekundu
Kuna wakati mwingine Melanin haitengenezwi na mwili na kwa hiyo Nywele zinageuka na kuanza kuwa Nyeupe na sababu ni wakati Tyrosinase Enzyme ambayo ndiyo inatengeneza Melanine inapoharibiwa mwilini na Peroxyde D’Hydrogen.
Peroxyde D’Hydrogen (H202 au oxygenated Water) ambayo ni kama Sabuni Ya mwili Ndiyo Inayosababisha kuivuruga au kuivunja hiyo Tyrosinase.na kuzuia Kuundwa kwa Melanin ambayo inatengenezwa na Tyrosinase. Na Hii Peroxyde D’Hydrogen au H2O2 ndiyo inayosababisha Maradhi ya Vitiligo (Ngozi kuwa na Mabaka Meupe.).
Katika hali ya kawaida yaani tangu Kuzaliwa kwa Binaadamu linalofanyika ni kuvunjwa kwa hii H2O2 (Peroxyde d’Hydrogene au Oxygenated water) na Enzyme inayojulikana kama Catalase Enzyme Na Kufanyika Hivi Kunalinda Tyrosinase ambayo Inatengeneza Melanin.
H2O2 inavunjwa na Catalase na kuwa H20 (Molecule au Tonye dogo la Maji) na 02 (Atoms Mbili za Oxygen) Na hivi ndivyo inavyokuwa katika hali ya kawaida ya maisha ya Binaadamu.
Nywele Zinakuwa na Rangi kwa ajili ya Melanin (C18H10N204). Na bila ya Melanin nywele zinakuwa Nyeupe kwa ajili ya Peroxyde d’hydrogene H2O2 ambayo inasababisha kutoweka kwa Melanin na kusababisha nwele kuwa nyeupe.
Kwa kifupi Peroxyde D’Hydrogen ndiyo sababu ya kufanya nywele ziwe Nyeupe Na Melanine ndiyo sababu inayofanya nywele kuwa na Rangi.
Hebu Nichambue Formula za Melanine na Peroxyde D’Hydrogen ili itusaidie katika Utafiti wetu ufuatao:
MELANIN
Formula ya Melanin =C18H10N2O4
Tukichambua Formula hii utapata kama ifuatavyo:
Carbon (Atoms 18) + Hydrogen (Atoms 10) + Nitrogen (Atoms 2) + Oxygen (Atoms 4)
Ukijumlisha Atoms hizi Zote utapata 34 kama ifuatavyo:
18 + 10 + 2 + 4=34 Atoms
HYDROGEN PEROXYDE
Formula ya Hydrogen Peroxyde=H2O2
Tukichambua Formula hii utapata kama ifuatavyo:
Molar mass au Uzito wa Atoms katika Kila Mole Moja ya Hydroigen Peroxyde ni kama ifuatavvyo:
Hydrogen Atoms (1g/mole + 1g/mole=2g/mole) + Oxygen Atoms (16g/mole x 2 =32grams/mole)
Ukijumlisha Uzito Wa Atoms zote utapata
2 (Hydrogen) + 32 (Oxygen) =34 Grams/Mole
katika Table Ya Elements Tunapata 34 kama ifuatavyo:
Molar mass: 34.0147 g/mol
Kwa Hiyo Molecule Hizi Mbili; Melanin na Hydrogen Peroxyde zinashiriakiana katika Kutumia Namba 34 kama tulivyoona hapa Juu. Yaani Hydrogen Peroxyde ina Grams 34 kwa kila Mole Moja (Mole ni Kipimo cha Vitu Vidogo Vidogo) na Melanin ina Jumla Ya Atoms 34.
Melanin kazi yake ni kusababisha Nywele ziwe na Rangi na Hydrogen Peroxyde Inazuia Kuweko kwa Rangi yaani Inasababisha MVI na zote mbili zinatumia Namba 34.
Je unaona Uwiano. Sasa Tukifanya Utafiti Katika Aya Zifuatazo Utaona Namba 34 Inavyokariri kwa njia Mbalimbali kiajabu sana kama kwamba Aya Za Kuruani Zinaashiria Molecule Hizi Mbili Ya Kwanza Ni ya Ujana na Ya Pili Ni ya Uzee.
Hebu Tuendelee na Maajabu Yasiyo Na Mwisho. Allahu Akbar.
Ningependelea kuendelea Kuzitaja Aya Za Kuruani zenye kuelezea Neno Mvi na Uzee ili niendelee na Utafiti wa Miujiza Ya Kushangaza Sana. Allahu Akbar.
AYA ZA KURUANI NA TAFSIRI
Katika Kuruani Kumetajika neno MVI (UZEE) mara tatu tu katika Aya Tatu Zifuatazo:
1/Sura Ya Maryam Namba 19 Aya Namba 4
قَالَ رَبِّ إِنِّى وَهَنَ ٱلۡعَظۡمُ مِنِّى وَٱشۡتَعَلَ ٱلرَّأۡسُ شَيۡبً۬ا وَلَمۡ أَڪُنۢ بِدُعَآٮِٕكَ رَبِّ شَقِيًّ۬ا (٤)
TAFSIRI
4.Akasema: “Mola wangu. Bila shaka mifupa yangu imekuwa dhaifu na kichwa kinawaka (kinang’ara) kwa mvi, wala sikuwa mwenye bahati mbaya, (mwenye kukasirika) Mola wangu, kwa kukuomba wewe.”
2/Sura Ya Al-Muzzamil Namba 73 Aya namba 17
فَكَيۡفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرۡتُمۡ يَوۡمً۬ا يَجۡعَلُ ٱلۡوِلۡدَٲنَ شِيبًا (١٧)
TAFSIRI
17.Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujihifadhi na (balaa ya) siku ambayo itawafanya watoto kuwa wenye kutoka mvi (wazee)?
3/Sura Ya Al-Rum namba 30 Aya Namba 54
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن ضَعۡفٍ۬ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ ضَعۡفٍ۬ قُوَّةً۬ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ۬ ضَعۡفً۬ا وَشَيۡبَةً۬ۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡقَدِيرُ (٥٤)
TAFSIRI
54.Mwenyezi Mungu ndiye Aliyekuumbeni katika udhaifu, na baada ya udhaifu Akafanya nguvu, kisha baada ya nguvu Akaufanya udhaifu na uzee. Anaumba apendavyo; naye ni Mjuzi, Mwenye uweza.
MUUJIZA WA KUSHANGAZA KUTOKANA NA TULIYOYASOMA HAPA JUU
Kabla Kuelezea Ningependelea kudokeza kwamba vipimo vya Gram na Mole ni vya Karne ya 18 na 19 na kuruani imeashiria vipimo hivi kuanzia karne ya 7
Na Pia Chembe Ya Atom Imetajika katika Kuruani Kabla ya Kukubaliwa na Nchi za Ulaya katika karne ya 17
Zote hizi zimetajika katikaa Kuruani karibu karne zaidi ya kumi (Miaka 1000) iliyopita. Je unaona Muujiza?
The Gram = 18th Century (1793) Gram is a Unit of Weight adopted in 1795
The Mole=19th Century (1811) The Mole basic unit adopted in 1971 (Avogadros Number)
Na Fikra ya Chembe ya Atom ilichukuliwa Rasmi katika karne ya 17 ijapokuwa ilitajika katika karne kabla ya Enzi Ya ukristo.
(The concept of the atom that Western scientists accepted in broad outline from the 1600s until about 1900 originated with Greek philosophers in the 5th century bce)
Sasa Imafikia wakati wa kuchambua Aya za Kuruani 3 tulizozitaja hapo Awali:
Kwanza
Sura Ya Maryam Namba 19 Aya Namba 4
قَالَ رَبِّ إِنِّى وَهَنَ ٱلۡعَظۡمُ مِنِّى وَٱشۡتَعَلَ ٱلرَّأۡسُ شَيۡبً۬ا وَلَمۡ أَڪُنۢ بِدُعَآٮِٕكَ رَبِّ شَقِيًّ۬ا (٤)
Tukihesabu herufi kuanzia Mwanzo wa Aya Hii mpaka neno MVI (UZEE) utapata Jumla ya Herufi ni 34 na kama tilivyosoma hapo awali namba hii inaashiria Jumla ya Atom za Melanin na Pia Jumla ya Grams/Mole za Hydrogen Peroxyde. Je unaamini haya? hebu tuendelee na Utafiti wetu twende mbele zaidi. Allahu Akbar.
Tukihesabu NUQTA au Points kama vile NUQTA moja ya Herufi BAA au NUQTA tatu za Herufi SHIN na hivyo hivyo ukihesabu NUQTA zote za Aya hii utapata Jumla ni NUQTA 34 pia!!!!!! Je unaona Maajabu. Kama huamini basi tuendelee na Utafiti ili tupate Yakini. Hebu twende mblele.
Sura Ya Maryam Namba 19 Aya Namba 4
قَالَ رَبِّ إِنِّى وَهَنَ ٱلۡعَظۡمُ مِنِّى وَٱشۡتَعَلَ ٱلرَّأۡسُ شَيۡبً۬ا وَلَمۡ أَڪُنۢ بِدُعَآٮِٕكَ رَبِّ شَقِيًّ۬ا (٤)
Sasa Tuhesabu Herufi Za kipande Cha Pili kuanzia Neno شَيۡبً۬ا mpaka Mwisho Wa Aya neno شَقِيًّ۬ا utapata Jumla ya Herufi ni 22. Je namba hii inaashiria kitu gani? Sasa tuona Maajabu Mengine.
Kipande hiki cha Aya kina herufi 22 na namba 22 ni Position Ya Composite Number 34. yaani Ukihesabu namba ya 22 katika Composite Numbers kuanzia Namba ya kwanza ambayo ni 4 utaishia na namba ya 34
(4,6,8,9,10,12,14,15,16,18,20,21,22,24,25,26,27,28,30,32,33,34)
Kwa hiyo 22 inatupa namab 34 tena kiajabu. Katika Elimu ya Hesabu kuna Prime na Composite Numbers. Na hapa Namba 34 ni mojawapo ya Composite Numbers na ni ya 22 ukihesabu kuanzia Composite Number ya Kwanza.
Hebu Tuchunguze Kukariri kwa Herufi za neno شَيۡبً۬ا katika Aya Hii Jumla ni Ngapi?
Herufi Shin Imakariri Mara 3
Herufi Yaa Imakariri mara 5
Herufi Baa Imekariri mara 4
Herufi Alif Imekariri mara 10
Jumla 3 + 5 + 4 + 10=22
Na kama Tulivyoona hapo juu kwamba Namba 34 ni Composite Namba ya 22
Na Tukihesabu Herufi Za neno شَيۡبً۬ا kwa kuzigeuza katika Thamani (Values) za Mpangilio wa Herufi za Kiarabu kuanzia Herufi Ya Kwanza Mpaka 28 utapata kama ifuatavyo
Herufi Shin ni Ya 21
Herufi Yaa ni Ya 10
Herufi Baa Ni Ya 2
Herufi Alif Ni ya 1
Jumla 21 + 10 + 2 + 1=34
Je Unaona Muujiza wa Namba 34. Kwa kweli Inashangaza.
Na Ajabu Ni Kwamba Aya Hii ipo katika Sura Ya Maryam na Jina la Maryam limeripiti au limekariri katika Kuruani yote mara 34 pia!!! Allahu Akbar. Je Unaona Hata Jina La MARYAM ambayo Aya Hii ipo katika Sura hiyo pia limekariri katika Kuruani mara 34 pia!!!!
Je unaona Ya Maajabu? Allahu Akbar. Sasa Namba hii 34 ni nini? Je huoni inaashiria Kinachiosababisha MVI na Kile kinachosababisha Nywele kuwa na Rangi? Je huoni yote haya kama ni Maajabu yasiyo na Mwisho?
Sasa Tuendelee na Utafiti. Twende Mbele tuone maajabu yasiyo na mwisho Allahu Akbar. Tutachambua Aya Ya Pili inayotaja MVI (UZEE).
Sura Ya Al-Mzzamil Namba 73 Aya namba 17
فَكَيۡفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرۡتُمۡ يَوۡمً۬ا يَجۡعَلُ ٱلۡوِلۡدَٲنَ شِيبًا (١٧)
Ukihesabu Herufi za Aya hii utapata Jumla Ya Herufi ni 34 Pia!!!! Je unaona Maajabu. Aya Hii Ya Pili Inanherufi 34 Pia na Namba hii inaashiria MELANIN na HYDROGEN PEROXYDE. kama huamini basi tuendelee mbele na Utafiti mpaka utosheke na uamini kwamba Kuruani siyo Mchezo. Siyo kitabu cha Upuuzi. Ni Muujiza ulio mkubwa sana tena sana Allahu Akbar.
Hebu Tuchunguze Aya Ya 3 na Ya Mwisho ambayo imetaja neno MVI (UZEE)
3/Sura Ya Al-Rum namba 30 Aya Namba 54
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن ضَعۡفٍ۬ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ ضَعۡفٍ۬ قُوَّةً۬ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ۬ ضَعۡفً۬ا وَشَيۡبَةً۬ۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡقَدِيرُ (٥٤)
Kipande hiki ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ۬ ضَعۡفً۬ا وَشَيۡبَةً۬ۚ kina herufi 22 na kama tulivyosema kwamba composite namba 34 ni ya 22. kama tulivyoona hapo Juu.
kipande hiki kinaelezea kwamba Mwenyeezi Mungu amejaalia Baada ya Nguvu ni Udhaifu na Uzee. Na Uzee unaashiria MVI au Nwele Nyeupe za Uzeeni. Allahu Akbar.
Na Kipande Cha Kwanza
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن ضَعۡفٍ۬ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ ضَعۡفٍ۬ قُوَّةً۬
Cha Aya Hii kina Herufi 34 Pia!!!! Allahu Akbar.
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن ضَعۡفٍ۬ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ ضَعۡفٍ۬ قُوَّةً۬ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعۡدِ قُوَّةٍ۬ ضَعۡفً۬ا وَشَيۡبَةً۬ۚ يَخۡلُقُ مَا يَشَآءُۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيمُ ٱلۡقَدِيرُ (٥٤)
Ndugu Zanguni Waumini Mnaona Miujiza Ya Kisayansi? Yule yule aliyeumba Ulimwengu ndoye Yule Yule aliyeshusha Kuruani Hii. Hii Ni Saini Yake Mwenyeezi Mungu. Anatuonyesha Alivyoviumba.

Mfumo (Structure) wa Nywele. Melanocytes Ndiyo Melanin inapotoka.

Hydrogen Peroxyde Molecule Inavyovunjwa na Catayse na Kugeuka na kuwa Maji na Oxygen. Na hivi Ndiyo inayosababisha Nywele za Ujana zidumu yaani Za Rangi kama vile Nywele Nyeusi.. Catalyse inapopungua mwilini basi Hydrogen Peroxyde Itazidi na Kusababisha MVI (UZEE)

Hii Ndiyo MELANIN Molecule. Carbon + Hydrogen + Nitrogen + Oxygen na ndiyo inatia Rangi Nywele kuwa Nyeusi au Rangi Nyinginezo. ikipungua MELANIN basi HYDROGEN PEROXYDE itazidi na kusababisha MVI (UZEE). Kwa hiyo Catalyse au Melanin inapopungua basi Hydrogen Peroxyde itazidi na kusababisha MVI. Kutoka katika Chombo cha Utafiti Google tunaona Melanin Formula= Carbon + Hydrogen + Nitrogen + Oxygen= 34 Atoms. (Carbon 18 + Hydrogen 10 + Nitrogen 2 + Oxygen 1=34 Atoms)
Mass (Grams Kwa Kila Mole Moja) ya Hydrogen Peroxyde ni 34 kutoka katika Chombo cha utafiti Google.


MUUJIZA WA MBEGU YA HARADALI KATIKA KURUANI TUKUFU
Muujiza wa خردل Haradali (Mustard Seed)
Jina Haradali pia Limetumika Kuashiria Gesi ambayo ilitumika katika Vita kama vile Vita vya Kwanza Vya Dunia.
Na Gesi hii (C4H8CI2S0) ni Mchanganyiko unaojulikana kama Dichlorinated Ethyl Sulfide (C4H8CI2S)
Molecule Dichlorinated Ethyl Sulfide (C4H8CI2S) ina Harufu ya Mbegu Ya Haradali.
Tukichambua Formula Hii tutapata kama ifuatavyo:
C4H8 Ni Ethyl (Carbon Na Hydrogen)
Cl8 Ni Dichlore (Clorine)
S Ni Sulphur (Sulphur)
(Mustard seeds are the small round seeds of various mustard plants. The seeds are usually about 1 to 2 millimetres (0.039 to 0.079 in). Mustard is a condiment of a thousand faces. Some are smooth, others almost entirely made from barely cracked seeds.Mustard seeds, both white and brown, are nearly globular in shape, finely pitted, odourless when whole, and pungent-tasting. White mustard seeds are light yellow in colour and about 2.5 mm (0.1 inch) in diameter. Brown mustard seeds are about the same size but are a darker yellow in colour).Sulfur mustard refers to several man-made poisonous chemicals. These chemicals work as blistering agents and can seriously damage skin, eyes, throat, and lungs. Sulfur mustard is more commonly known as “mustard gas”. This name “mustard gas”was first used when the chemical was sprayed during attacks in World War I.
AYA ZA KURUANI ZINAZOTAJA HARADALI
Mbegu Ya Khardali Imetajika Katika Kuruani Mara Mbili tu Katika Aya Zifuatazo:
Sura 21 Aya Namba 47
ونضع الموزين القسط ليوم القيمه فلا تظلم نفس شيا وان كان مثقال حبه من خردل اتينا بها وكفي بنا حسبين
TAFSIRI
47.Nasi tutaweka mizani za uadilifu siku ya Kiama, na nafsi yoyote haitadhulumiwa hata kidogo.Na hata kama likiwa (jambo hilo lina) uzito mdogo wa chembe ya haradali nalo tutalileta; Nasi tunatosha kuwa wajuzi (wazuri kabisa) wa hisabu.
Na Sura Namba 31 Aya Namba 16
يبني انها ان تك مثقال حبه من خردل فتكن في صخره او في السموت او في الارض يات بها الله ان الله لطيف خبير
TAFSIRI
I6.Ewe mwanangu! Kwa hakika jambo lolote lijapokuwa na uzito wa chembe ya haradali, likawa ndani ya jabali au mbinguni au katika ardhi, Mwenyezi Mungu Atalileta (amlipe aliyefanya); hila shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo yaliyofichikana, (na) Mjuzi wa mambo yaliyo dhahiri.
SHEREHE YA AYA KISAYANSI-MUUJIZA WA KUSHANGAZA
Hebu Tuchambue Aya Zifuatazo kwa kuhesabu Herufi zake.
Sura Namba 31 Aya Namba 16
يبني انها ان تك مثقال حبه من خردل فتكن في صخره او في السموت او في الارض يات بها الله ان الله لطيف خبير
Jumla Ya Herufi Ya Aya Hii ni 80
Sura Namba 21 Aya Namba 47
ونضع الموزين القسط ليوم القيمه فلا تظلم نفس شيا وان كان مثقال حبه من خردل اتينا بها وكفي بنا حسبين
Jumla ya Herufi Za Aya Hii ni 79
Ukijumlisha Herufi za Aya Hizi Mbili Utapata Jumla ni 159 (80 + 79=159)
Haya Ni Maajabu Kwani Molecule Ya Gesi Ya Haradali (Mustard Seed) C4H8CI2S Ina Molecular Mass (Uzito katika Mole Moja) 159 Pia!!
Kwani Kufuatana na Table Ya Elements tunapata Hesabu za Kila Element za Molecule C4H8CI2S kama ifuatavyo:
Carbon Ina Mass Ya 14 kwa kila Mole Moja
Hydrogen Ina Mass 1 kwa kila Mole Moja
Chlorine Ina Mass 35.5 kwa kila Mole Moja
Sulphur Ina Mass 32 kwa kila Mole Moja
Kwa hiyo Ukifanya Hesabu na Kujumlisha Elements Hizi utapata Mass au Uzito wa Molecule ni 159 kama ifuatavyo: C4H8CI2S=4 X 12 + 8 X 1 + 2 X 35.5 + 1 X 32=159 Gram Kwa kila Mole yaani 159 Gram/Mole
Huu Ni Muujiza Kwani Kipimo Cha Gram Kilianzishwa Karne ya 18 Mwaka 1793 na Kuruani ni ya Karne Ya 7.
Sasa Tuchunguze kwa kujumlisha Idadi Ya Maneno,, Namba Ya Sura Na Namba Za Aya Tulizozitaja Hapa Juu na ukifanya hivyo Utapata Pia Jumla ni 159!!!!
Hebu Tuhesabu Kwa Pamoja:
Sura Namba 21 Aya Namba 47 / Aya hii Ina Maneno 20
ونضع الموزين القسط ليوم القيمه فلا تظلم نفس شيا وان كان مثقال حبه من خردل اتينا بها وكفي بنا حسبين
Sura Namba 31 Aya Namba 16 / Aya Hii Ina Maneno 24
يبني انها ان تك مثقال حبه من خردل فتكن في صخره او في السموت او في الارض يات بها الله ان الله لطيف خبير
Sasa Tujumlishe Namba Hizi Sita Kama Ifuatavyo:
Sura Namba 21 + Aya Namba 47 + Jumla Ya Maneno 20 + Sura Namba 31 +Aya Namba 16 + Idadi Ya maneno 24=159!!!
Angalia Maajabu Tunapata tena namba 159 ambayo Inaashiria Mass au Uzito wa Gesi ya Haradali katika Kila Mole Moja.
Kuna Maajabu Mengineyo Katika Aya Hii hebu tuendelee na Utafiti wetu. Allahu Akbar.
Sura Namba 21 Aya Namba 47
ونضع الموزين القسط ليوم القيمه فلا تظلم نفس شيا وان كان مثقال حبه من خردل اتينا بها وكفي بنا حسبين
Namba 47 (Namba Ya Aya) ni Prime Number ya 15 (Katika Hesabu Kuna Prime na Composite Numbers) na Ajabu Kubwa ni kwamba Gesi Ya Haradali Ina Jumla Ya Atoms 15 pia kama ifuatavyo:
C4H8CI2S (Carbon Atom 4 + Hydrogen Atom 8 + Chlorine Atom 2 + Sulphur Atom 1=15 Atoms
Hapa Muujiza Ni Namba Ya Aya ambayo ni 47 inaashiria Idadi ya Atoms 15 za Gesi Ya Mbegu Za Haradali.
Kwa Kweli Inashangaza Sana.
Hebu Tuendelee na Utafiti kwa kuhesabu Maneno.
Sura Namba 21 Aya Namba 47
ونضع الموزين القسط ليوم القيمه فلا تظلم نفس شيا وان كان مثقال حبه من خردل اتينا بها وكفي بنا حسبين
Aya Hii Namba 47 Ukihesabu Maneno Kuanzia Mwanzo Wa Aya Mpaka neno Haradali utapata Jumla ya Maneno ni 15 na hii pia Inashangaza sana kwani 15 ni Jumla Ya ATOMS za Haradali Pia kama tulivyoona hapa Juu
Hebu tuhesabu tena Maneno Kuanzia Mwanzo wa Aya Mpaka Neno خردل Haradali Sura Namba 31 Aya Namba 16
يبني انها ان تك مثقال حبه من خردل فتكن في صخره او في السموت او في الارض يات بها الله ان الله لطيف خبير
Aya Hii Namba 16 Ukihesabu Maneno Kuanzia Mwanzo Wa Aya Mpaka neno Haradali utapata Jumla ya Maneno ni 8 na hii pia Inashangaza sana kwani Composite Namba Ya 8 Ni 15. Ukichunguza Table Ya Prime na Composite Numbers utaona haya ninayozungumza. (Composite na Prime Numbers Table)
Sasa Tufanye Uchunguzi Mwingine wa ndani zaidi.
Tumesema kwamba Neno Haradali Limatajika Mara Mbili.
Mara Ya Kwanza Katika Sura Namba 21 na Mara Ya Pili Katika Sura Namba 31 na Baina Ya Aya Hizi Mbili Kuna Aya 954 ambayo ni sawa na 159 X 6 Yaani Namba 954 inaweza kugawanyika katika Mafungu 6 ya 159 Je unaona Muujiza Wa Kushangaza. Tunapata Tena Namba 159!!!! Allahu Akbar. Hii siyo Bahati Nasibu. Bali Imepangwa kiajabu Sana Tena Sana.
Sasa Tukizama Zaidi Katika Uchunguzi Wetu kwa kutafuta Multiple Ya Namba 159 Tutapata Maajabu Yafuatayo:
Sura Ya Kwanza Kutajika Neno Haradali Ni Namba 21 Na Sura Ya Mwisho ni Namba 31 Na Baina Ya Sura Hizi Mbili kuna Sura 9
1/Ukihesabu Aya Kuanzia Mwanzo Wa Kutajika Neno Haradali katika Sura Namba 21 Aya Namba 47 Mpaka Sura Namba 23 Aya Namba 16 utapata Jumla Ya Aya Ni 159
2/Ukihesabu Kuanzia Sura Namba 23 Aya Namba 16 Mpaka Sura Namba 24 Aya Namba 57 Utapata Jumla Ya Aya ni 318 ambayo Ni sawa na 159 X 2
3/Ukihesabu Kuanzia Sura Namba 24 Aya Namba 57 Mpaka Sura Namba 26 Aya Namba 75 Utapata Jumla Ya Aya ni 477 ambayo ni sawa na 159 X 3
4/ Ukihesabu Kuanzia Sura Namba 26 Aya Namba 75 Mpaka Sura Namba 27 Aya Namba 7 Utapata Jumla Ya Aya ni 636 ambayo ni sawa na 159 x 4
5/Ukihesabu Kuanzia Sura Namba 27 Aya Namba 7 Mpaka Sura Namba 28 Aya Namba 73 Utapata Jumla Ya Aya ni 795 ambayo ni sawa na 159 X 5
6/Ukihesabu Kuanzia Sura Namba 28 Aya Namba 73 Mpaka Sura Namba 31 Aya Namba 15 Utapata Jumla Ya Aya Ni 954 ambayo ni sawa na 159 X 6
Sasa tukihesabu Jumla Ya Sura ambazo Zina Multiple ya Namba 159 kama tulivyoona katika Hesabu Hapa Juu utapata Maajabu mengineyo kama ifuatavyo:
Namba Za Sura Zenye Multiple ya 159 ni Sura Namba 23 + 24 + 26 + 27 + 28 + 31= 159!!!!!
Na Jumla Ni 159 ambayo ni Mass au Uzito wa Haradali tuliyoisoma Hapa.
Je unaona Muujiza? Allahu Akbar.
Namba 159 tena inatajika.Yaani Mass ya Haradali katika Mole Moja.
Je unaona Ya Kushangaza. Je unaona Mushirio wa kiajabu.
Kila Hesabu Tulizozifanya Hapa Juu tunaoata Namba ile ile 159 ambayo ni Mass Ya Gesi Ya Khardali katika Mole Moja.
Kwa kweli inashangaza. Je Tunaashiriwa habari hii kwa lengo gani? Hii ni Gesi Ya Haradali inayotokana na Mustard. Kwa nini Namba 159 Imekariri kila Mara hapa.
Nitawaachia Wasomaji Mfikiri wenyewe. Mimi naona mshangao tu!!! sisemi kitu wala kutoa Maoni yeyote.
Tulichosoma ni Mbegu Ya Haradali na tumeona Gesi Iliyotengenezwa Na Binaadamu Kwa Ajili ya Vita Imetiwa Jina Mustard Gas yaani Gesi Ya Haradali.
Sasa mbona Hesabu Ya Mass katika Mole Moja yaani 159 imaripiti au kukariri katika Aya Hizi zaidi ya mara moja? Je kuna siri gani katika habari hii?
Huu Ni Muujiza kwani Elimu hii haikuwako katika Enzi Ya Mtume Mohamad ﷺ Na karne Tunayoishi tunasoma Elimu za Sayansi Za Hali Ya Juu lakini tunakuta Katika Kuruani.
Yaani Mwenyeezi Mungu anajua Yote haya yanayofanyika mpaka mwisho wa Ulimwengu.
Anatupa Imani turudi katika Dini yake kwa kila njia. Anaturudisha katika Kuruani.
Kama kwamba anatuambia tusighururike na Sayansi. Tujue kwamba Elimu zote ni zake na sisi hatujui chochote.
Je huoni Vipimo Vya Kisasa kama vile Grams au Mole na pia Majina Ya Elements.
Je Enzi ya Mtume Mohamad ﷺ nani alijua haya?
Sasa Mtume ﷺ alisomea wapi Elimu kubwa kama hizi.
Kwa kweli Inatisha. Tumche Mungu.
Allahu Akbar. Allahu Akbar.
Alhamdulilah.

Mustard Molar Mass ni 159 Grams Kwa kila Mole Moja. Jawabu la Chombo Cha Utafiti.

Mbegu Za Haradali au Mustard Seed. Hizi Ndizo Zilizotajwa Katika Kuruani Tukufu. Hii Picha ni mfano mmoja wa Mbegu hizi lakini kuna aina nyinginezo.
MUUJIZA WA UMBALI (MAILI) BAINA YA MASJID AL-HARAM (MECCA) NA AL-AQSA (PALESTINE)NA MUUJIZA WA IDADI ZA RAKAA 17
Sura Namba 9 Al-Tawbah Aya Namba 28
يايها الذين امنوا انما المشركون نجس فلا يقربوا المسجد الحرام بعد عامهم هذا وان خفتم عيله فسوف يغنيكم الله من فضله ان شا ان الله عليم حكيم
TAFSIRI
18.Enyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie huo Msikiti Mtukufu baada ya mwaka wao huu. Na kama mkikhofia umasikini, basi karibuni hivi Mwenyezi Mungu atakutajirisheni kwa fadhila zake akipenda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.
SHEREHE
18.Baada ya Mtume ﷺ kuiteka Makka ilitolewa ilani kuwa wale makafiri waliokuwa wakija Makka kuabudu masanamu yao waliyoyaweka huko Makka hawana ruhusa tena kuja huko Makka kuabudu masanamu hayo. Na masanamu hayo yalivunjiliwa mbali. Mambo yao yote yalikuwa ya najisi; moja katika hayo walikuwa wakihiii tuputupu.Baadhi ya watu ilipotolewa ilani hii waliogopa kuharibikiwa katika kazi zao kwani hao waliozuiliwa kuja walikuwa wakija kibiashara pia; wakileta vya kwao na wakinunua vya Makka. Basi Mwenyezi Mungu anawatuliza nyoyo zao hao waliofazaika kwa haya kuwa wakifunga milango ya shari, Mungu atawafungulia milango ya kheri
Sura Namba 17 Aya Namba 1
سبحن الذي اسري بعبده ليلا من المسجد الحرام الي المسجد الاقصا الذي بركنا حوله لنريه من ايتنا انه هو السميع البصير
TAFSIRI
I.Utukufu ni wake yeye ambaye alimpeleka mja wake usiku (mmoja tu) kutoka Msikiti Mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (wa BaytulMaqdis-Falastini) ambao (tumeubariki na)tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake(Tulimpeleka hivyo) ili tumuonyeshe baadhi ya Alama zetu. Hakika Yeye (Mwenyezi Mungu) ni Mwenye kusikia (na) Mwenye kuona.
SHEREHE
1.Si ajabu Mwenyezi Mungu kumpeleka Mtume ﷺ Wake kutoka Makka mpaka Palestina na baada ya hapo kupelekwa Mbinguni na akamrejesha katika baadhi ya saa za usiku huo huo na kumuonyesha aliyomuonyesha. Leo Mwenyezi Mungu amewawezesha binaadamu kuzunguka ulimwengu mzima kwa saa chache tu. Na yote haya ni kwa ajili ya kuonyesha ukweli wa Quruani kuwa haisemi jambo la uwongo kama alivyosema Mwenyezi Mungu na kama tunavyoona na tutakavyozidi kuona sisi na kuona watakaokuja baada yetu sisi na watakaokuja baada ya hao na baada ya hao na baada ya hao. Mpaka ulimwengu umalizike kila saa na wakati utakuwa unadhihiri tu ukweli wa dini ya kiislamu kwamba ni Dini iliyonyoka kweli kweli.
MUUJIZA WA UMBALI MAILI 767 BAINA YA MISIKITI MIKUBWA MIWILI. Masjid Al-Aqsa Na Masjid Al-Haram
Ukihesabu Jumla Ya Aya baada tu ya Aya Namba 28 katika Sura Namba 9 (ambayo imetaja Jina La Masjid Al-Haram yaani Kaaba) mpaka Sura Namba 17 Aya Ya Kwanza utapata Jumla za Aya ni 767. Tuelewe kwamba Kuna Aya Nyinginezo Kabla na baada Ya Aya Namba 28 Sura Namba 9 ambazo Zimetaja Jina La Msikiti wa Kaaba. Lakini Maajabu Ni Kwamba Sura Namba 9 Aya Namba 28 ambayo imetaja Msikiti wa kaabah Imefuatiwa na Aya Inayotaja Msikiti wa Jerusalem “Masjid Al-Aqsa” ambao ni Maarufu na Muhimu sana baada ya Msikiti wa Mecca Sura namba 17 Aya Namba 1.
Muujiza Wa kushangaza ni kwamba Umbali Baina Ya Misikiti hii miwili ni Maili 767 pia = 1234 Kilometres sawa sawa na Idadi Ya Aya Kama tulivyohesabu.
Huu Sio Muujiza Mdogo na ushahidi kwamba Mtume ﷺ alifanya safari ya Israa (kutoka Mecca Mpaka Jerusalem) na Miraji. (Kwenda Mbinguni) Huu ni Muujiza Mbele ya Macho yetu. Allahu Akbar.
Vipimo vya Maili ni vya Kisasa na havikuwapo katika Enzi Ya Mtume ﷺ na hakuna aliyevijua vipimo kama hivi wakati huo.
Mwenyeezi Mungu alijua Wakati utafika na Vipimo kama hivi vya Maili na vinginevyo vitatumika na akaweka Miujiza Mfano kama huu ili kutilia Mkazo habari ya Israa na Miraji na wala sio uwongo kama wajinga wengi wanavyodhania. Allahu Akbar.
MUUJIZA WA NAMBA YA SURA YA ISRAA AMBAYO NI 17 INAASHIRIA RUKUU 17
Kithibitisho Kingine cha Kushangaza ni Namba Ya Sura ya Israa ambayo ni 17 hapa tunaona Muujiza Mwingine wa Ajabu kwani Katika Safari Hii Mtume Mohamad ﷺ alifaridhishiwa Sala Tano na baada ya Safari hiyo Malaika Jibril alimfundisha Mtume mohamad ﷺ namna ya Kuswali na Pia akasomeshwa Idadi za Rakaa na Sujudu. Muujiza wa kushangaza ni Kwamba Idadi za Rakaa ni 17 pia kama Namba ya Sura Ya Al-Israa. Je unaona Muujiza. Tuelewe kwamba Namba za Sura Na Aya hazikuwako katika Enzi ya Mtume ﷺ bali ziliongezwa baadaye ili kuwasaidia Wasomaji Wa Kuruani. Angalia Muujiza ambao Umejitokeza baada tu ya Kutiwa Namba za Sura Na Aya Katika Msahafu.Allahu Akbar.
Hii Miujiza Miwili: Umbali baina ya Misikiti Mikubwa Miwili na Namba Ya Sura Inathbitisha kwamba Safari Ya Israa Na Miraji Ni Ya ukweli. Allahu Akbar. Hii Ni Miujiza isiyo na Mwisho na siyo Midogo. Mwenyeezi Mungu anajua zaidi ikiwa hizi namba zinaashiria haya lakini ukifikiri utaona ni Mambo makubwa ya kushangaza. Allahu Akbar.
Habari Hii Haijaisha Bado Inaendelea…..
NITAENDELEA NA HABARI ZA UTAFITI HUU KARIBUNI. MWENYEEZI MUNGU AKIPENDA. Allahu Akbar