UTAFITI MBALIMBALI KATIKA DINI NA SAYANSI
IMEANDALIWA NA AL-AMIN ALI HAMAD
MIUJIZA MBALIMBALI YA KUSHANGAZA
Kabla ya Kuanza kuandika Mlango huu ninamuomba Mwenyeezi Mungu atakabali kazi hizi zisiwe isipokuwa kwa ajili yake tu pekee na siyo kutaka tamaa nyingine yeyote ya duniani. Na dua nyingine ni kumshukuru kwa kila alichotupa na pia kwa kila asichotupa. Kwani kila Alichotupa kuna hekima ndani yake na pia asichotupa pia kuna hekima ndani yake. Tunasema “Alhamdulilahi” katika kila hali.
Mlango huu utahusiana na Miujiza Mbalimbali ya Kuruani Tukufu.
Mlango huu na Mingineyo ya Miujiza na Sayansi ni Maoni ambayo huenda tumepata na huenda tumekosa katika Utafiti wetu. Kwa hiyo ipo wazi na kama una maoni yako unaweza kugeuza maana yake kama upendavyo mradi tu uwe katika ukweli.
Nia na Lengo kubwa ya kazi yangu ni kuitakasa kuruani na Kila Uwongo unaosema kwamba kuruani siyo maneno ya Mwenyeezi Mungu au Kuruani imeguswa kwa kubadili, kuzidisha au kuounguza Herufi, Aya au Sura zake.
Friday 15 April 2022=14 Ramadan 1443
MUUJIZA WA SHAHADA NA KUKUA KWA MIMEA
1/MUUJIZA WA SHAHADA
Sura Namba 47 Ya Mohamad Aya Number 19
فَٱعۡلَمۡ أَنَّهُ ۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ وَٱسۡتَغۡفِرۡ لِذَنۢبِكَ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَـٰتِۗ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مُتَقَلَّبَكُمۡ وَمَثۡوَٮٰكُمۡ (١٩)
TAFSIRI
29.Jua ya kwamba hakuna aabudiwaye kwahaki ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na (dhambi) za Waislamu wanaume na Waislamu wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi (Yaani harakati za kila siku) na mahali penu pa kukaa.
Sura Namba 48 Ya Fath Aya Number 29
مُّحَمَّدٌ۬ رَّسُولُ ٱللَّهِۚ وَٱلَّذِينَ مَعَهُ ۥۤ أَشِدَّآءُ عَلَى ٱلۡكُفَّارِ رُحَمَآءُ بَيۡنَہُمۡۖ تَرَٮٰهُمۡ رُكَّعً۬ا سُجَّدً۬ا يَبۡتَغُونَ فَضۡلاً۬ مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٲنً۬اۖ سِيمَاهُمۡ فِى وُجُوهِهِم مِّنۡ أَثَرِ ٱلسُّجُودِۚ ذَٲلِكَ مَثَلُهُمۡ فِى ٱلتَّوۡرَٮٰةِۚ وَمَثَلُهُمۡ فِى ٱلۡإِنجِيلِ كَزَرۡعٍ أَخۡرَجَ شَطۡـَٔهُ ۥ فَـَٔازَرَهُ ۥ فَٱسۡتَغۡلَظَ فَٱسۡتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِۦ يُعۡجِبُ ٱلزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِہِمُ ٱلۡكُفَّارَۗ وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ مِنۡہُم مَّغۡفِرَةً۬ وَأَجۡرًا عَظِيمَۢا (٢٩)
TAFSIRI
Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (pamoja), wakitafuta fadhila za Mwenyezi Mungu na radhi (yake). Alama zao zi katika nyuso zao, kwa taathira, (athari) ya kusujudu.Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika lnjili (umetajwa hivi): Kuwa (wao) ni kama mmea uliotoa matawi yake; kisha (matawi hayo) yakautia nguvu; ukawa mnene ukasimama sawasawa juu ya kigogo chake, ukawafurahisha walioupanda; ili awakasirishe makafiri kwa ajili yao. Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na kutenda mema katika wao; msamaha na ujira mkubwa.
SHEREHE YA MUUJIZA KATIKA NGUZO YA KWANZA KATIKA UISLAMU-SHAHADA
Aya Ya Kwanza Tunapata Kipande cha Ibara ya Shahada لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ na Aya ya Pili tunapata kipande cha pili cha Ibara ya Shahada مُّحَمَّدٌ۬ رَّسُولُ ٱللَّه
Tafsiri Ya لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّه ni “Hakuna Ilaha (Mungu) isipokuwa Allah (Mwenyeezi Mungu)”
Tafsiri Ya مُّحَمَّدٌ۬ رَّسُولُ ٱللَّه ni “Mohamad Ni Mjumbe wa Allah (Mwenyeezi Mungu)”
Vipande Vya Ibara viwili ndivyo vinavyohitajika katika Kuukubali Uislamu. Unapoingia katika dini ya Kiislamu inabiri Ukiri kwamba Mwenyeezi Mungu ni Mmoja Na Mtume wake ni Mohamad.
Ibara Hii pia ina Miujiza yake.
Muujiza wa leo ambao ningependelea kuuzungumzia ni Jumla ya Herufi ya Ibara hii ya Shahada.
Hebu Tuchunguze zaidi ibara hizi mbili
لَاۤ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ
مُّحَمَّدࣱ رَّسُولُ ٱللَّهِ
Herufi ya Alif ni ya Kwanza (Yaani Namba 1) kwa wingi wa kutumika katika kuruani
Herufi Lamu ni Ya Pili (Yaani namba 2) kwa wingi wa kutumika katika kuruani.
Herufi Ha ni ya Saba (Yaani Namba 7) Kwa wingi wa kutumika katika kuruani
Ukijumlisha Thamani Ya Herufi za Ibara لَاۤ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ utapata Jumla ni 29 Herufi Lam zipo 5 kwa hiyo 5 x 2 (Kukariri kutumika katika kuruani) =10 Herufi Alif zipo 5 kwa hiyo 5 x 1 (Kukariri kutumika katika kuruani) =5 Herufi Ha zipo 2 kwa hiyo 7 x 2 (Kukariri kutumika katika kuruani)=14 Jumla ni 29 (10 + 5 + 14)
Na Ukihesabu Ibara ya Pili katika Shahada: مُّحَمَّدࣱ رَّسُولُ ٱللَّهِ kama tulivyofanya hapa Juu utapata Jumla ya Thamani za herufi ni 85. (Yaani Utafute Thamani ya herufi zote za ibara hii. kama vile Herufi Mim, Haa, Dal, Raa, Sin, Waw, Lam na Alif)
Sasa Tujumlishe Thamani Ya Ibara Hizi Mbili za Shahada. 85 + 29= 114 Unaona Ya kushangaza!!!
Yaani Ibara Ya Shahada ambayo ni nguzo ya kwanza katika Uislamu ikifuatiwa na Sala, Zakati, Saumu na Haji (kwenda Hija)
لَاۤ إِلَـٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ مُّحَمَّدࣱ رَّسُولُ ٱللَّهِ (La ilaha ila llah, Mohamad Rasulullah) = 114
Ibara hii inawakilisha Sura zote za kuruani ambazo ni 114.
Huu siyo Muujiza mdogo. Thamani ya Ibara hii ni sawa na Sura zote za kuruani ambazo idadi yake ni Sura 114. Mpangilio huu wa kiajabu siyo wa kawaida hata kidogo. Imepangwa na Aliyeshusha Kuruani Hii. Ameipanga Kiajabu sana. Huwezi Kugeuza,Kupunguza au kuzidisha Sura, Aya au Herufi za Kuruani kwani ingekuwa hivyo basi Mizani hii isingelikuwako. Kuruani Imepimwa mpimo wa hali ya juu sana. Ni Engineering ya hali ya Juu sana hakuna mfano na hakutakuwa na mfano mpaka Mwenyeezi Mungu apende mwenyewe. Amesema kwamba Ataitunza na hivyo ndivyo ilivyo imetunzwa kuanzia karne ya 7 mpaka leo. Karne 14 (Miaka 1400) imepita na kuruani ipo vile vile kama ilivyopokelewa.
2/MUUJIZA WA KUKUA KWA MIMEA-PHOTOSYNTHESIS
كَزَرۡعٍ أَخۡرَجَ شَطۡـَٔهُ ۥ فَـَٔازَرَهُ ۥ فَٱسۡتَغۡلَظَ فَٱسۡتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِۦ
Kipande cha Aya hii kutoka katika Sura Namba 48 Ya Fath Aya Number 29 hapa Juu pia inatufundisha Sayansi ya Kukua kwa Miti. Aya Inasema kwamba Mimea Inazalisha Matawi, Kisha Matawi hayo yanautia Mti nguvu. Aya hii Inatufunulia Sayansi Ya Kukua kwa Mimea. Mashina Ya Mimea inakuwa minene na yenye nguvu kutokana na Matawi Yake. Sayansi inathibitisha Elimu hii kwamba Sababu ya kutia Mashina ya Mimea Nguvu na Kukua Kwake inatokana na chakula chake cha Hewa ya Carbondioxide, Maji na Mwanga wa Jua kutokana na Matawi (pamoja na majani yake) ya Mimea ambayo inachangia katika kubadili vifaa hivi katika Carbonhydrates na Kusababisha Kukua kwa mashina ya mimea. Kuruani Imetupa zawadi ya Kutufahamisha Sayansi hii kwa ufupisho wa Maneno yafuatayo Sita tu Wakati ambao Sayansi za kileo zimendika Vitabu na Vitabu kuhusu Jambo hili.
كَزَرۡعٍ Mimea
شَطۡـَٔهُ Matawi
فَـَٔازَرَهُ Kutia Nguvu
فَٱسۡتَغۡلَظَ Mimea Kuwa Minene (Mukubwa)
فَٱسۡتَوَىٰ Kusimama
سُوقِهِۦ Shina la Mmea
Nyongeza kutoka katika Elimu Ya Sayansi.
(Plants take in carbon dioxide and convert it to energy for growth. When the plant dies, carbon dioxide is given off from the decomposition of the plant. The role of carbon in plants is to foster healthier and more productive growth of the plants Plants absorb carbon dioxide from the air, combine it with water and light, and make carbohydrates — the process known as photosynthesis)
14/05/2022
MUUJIZA WA AYA INAYOZUNGUMZIA “MAONO MAKALI”
Alhamdulilah Leo Mwenyeezi Mungu akipenda Nitazungumzia Aya Namba 22 Kutoka katika Sura Ya Qaf.
لَّقَدۡ كُنتَ فِى غَفۡلَةٍ۬ مِّنۡ هَـٰذَا فَكَشَفۡنَا عَنكَ غِطَآءَكَ فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدٌ۬ (٢٢)
Nitaanza na Tafsiri Ya Aya hii na Kisha nitasherehesha Na kudokeza Muujiza Wa Kisayansi. Ningependelea kusema kwamba Nitaunganisha Sherehe za Wanavyuoni na Maoni Kisayansi. Siwezi kusema kwamba Kuna Maoni bora kuliko Nyingine. Ni jitihada za kibinaadamu na kama ilivyo Binaadamu anaweza kukosea. Nitajitahidi kuweka Rai mbalimbali na wewe msomaji uchague katika Rai hizi ile Rai unayohisi ni nzuri. Kuruani ni Muujiza Mkubwa. Miujiza yake haina mwisho. Allahu Akbar.
Wanavyuoni wamejitahidi sana katika kuelezea Aya Hii. Na utakuta Maoni mbalimbali kuhusu Ibara فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدٌ۬ ya Aya Hii.
TAFSIRI
22. (Aambiwe): “Kwa hakika ulikuwa umo katika ghafla na jambo hili. Basi tumekuondolea (leo) pazia yako; kuona kwako leo kumekuwa kukali.”
SHEREHE
1.Aya hii inahusu mauti yanapomfika Binaadamu. Yaani Siku ya Kufariki Mwenyeezi Mungu atamjaalia mtu yule kuona ukweli wa maisha yake. Ataona Mabaya na Mazuri.
2.Huenda Aya Hii Ina Husiana na Kuruani Tukufu. Hapo mwanzo Mtume Mohamad ﷺ hakujua kitu chochote Yaani Kiliwa na Pazia lakini Mwenyeezi Mungu akamteremshia Kuruani yenye Mwanga na kuona Mazuri ya kutenda na Mabaya ya Kujiepusha.
3. Maoni ya Tatu na ambayo yana ushahidi zaidi ya maoni Mawili niliyotaja hapa juu ni kwamba Aya Hii inahusu Siku ya Kiama. Kwa sababu Aya zilizotangulia Aya Hii na zile zinazofuata zinazungumzia Siku ya Kiama. Kwa hiyo Aya hii inasema kwamba Siku ya Kiama Ndiyo Ukweli utakapodhihirika. Tutaona kila kitu. Mazuri na Mabaya Yote yatakuwa wazi. Macho yatapewa uwezo wa kuona Haki na Batili. Tutaona Tuliyoyafanya yote. Yaani Kila kitendo kizuri na kibaya kitadhihirika. Na siku hiyo tutaona Moto wa Jahannam, Pepo na Mengineyo ambayo tuliyotajiwa katika Kuruani.
SAYANSI KATIKA AYA HII
Na Maoni ya Mwisho Ni Sayansi katika Aya Hii. Kwanza tuizungumzie na kisha Tutaunganisha na Kilinganisha na Maoni niliyotaja hapa Juu.
فَبَصَرُكَ ٱلۡيَوۡمَ حَدِيدٌ Katika Kipande hiki Neno حَدِيدٌ limefasiriwa kwa maana ya “Kali”
Na kwa hiyo Tafsiri inakuwa “Maono yako yanakuwa Makali sana”
Yaani kuona Vizuri sana” Na hii ndiyo Tafsiri inayotupa maana ya kwamba siku ambayo Binaadamu atapewa nguvu ya kuona vizuri sana.
Na neno حَدِيدٌ pia lina maana ya “CHUMA” na ikiwa neno hili lina maana hiyo basi Tafsiri inakuwa “Macho au Maono yako yatakuwa na CHUMA”
Ukifikiri Kisayansi utakuta hakuna kosa kwani Damu inayojulikana kama RED CELLS inabeba Hameoglobin ambayo kazi yake ni Kubeba hewa ya Oxygen na ambayo ndiyo inayozipa Nguvu Vyungo vya Mwili Chuma (Iron) Katika Mwili wa Binaadamu ni Muhimu sana Katika Afya zetu. Sayansi inasema kwamba Maradhi mbali mbali kama vile Anaemia yanasababishwa na Upungufu wa hemoglobin ambayo kazi yake ni kubeba Iron (Chuma).
Mwili wa binaadamu unahitaji Chuma. Kuna faida nyingi za chuma katika mwili wa Binaadamu. Kwa mfano Afya ya Macho na kuona vizuri kunahitaji Chuma (Iron). Kwa hiyo Tafsiri ya Aya inaonyesha kwamba Binaadamu anapofariki basi Mwenyeezi Mungu anajaalia Kuwepo kwa Chuma kwa wingi katika Macho na kusababisha Kuona Vizuri zaidi kuliko siku za kawaida. Na hiyo pia inawezekana kwani hakuna Kisichowezekana Mbele ya Mwenyeezi Mungu. Angalia Hapa Chini Kauli ya Wanasayansi Kuhusu “Chuma” (Iron).
Red blood cells contain a substance called haemoglobin, which transports oxygen around the body.Iron is needed to form hemoglobin, part of red blood cells that carry oxygen and remove carbon dioxide (a waste product) from the body. Iron is mostly stored in the body in the hemoglobin. About one-third of iron is also stored as ferritin and hemosiderin in the bone marrow, spleen, and liver.Anemias occur when the level of healthy red blood cells (RBCs) or hemoglobin (an iron-binding, oxygen-carrying protein within RBCs) is too low.
Iron is a necessary mineral for many of the body’s functions, including vision. But too much iron – or problems with utilizing, storing, or transporting iron properly – can lead to vision loss in the form of conditions such as age-related macular degeneration and hyperferritinemia syndrome, according to recent research findings.
.
21/05/2022
MUUJIZA WA CHROMOSOMES ZA BINAADAMU
Nimeshazungumzia Katika sehemu nyinginezo za Website hii kuhusu Chromosomes za Binaadamu na Pia za baadhi ya Viumbe vinginevyo. Tuelewe kwamba Chromosomes ziligunduliwa mwaka 1888 (karne ya 19) Kutajika katika kuruani Elimu hii ni Muujiza mkubwa sana. Sayansi imefanya kazi kubwa kugundua Elimu hii lakini Kuruani ipo juu ya kila Sayansi za kidunia. Allahu Akbar.
Katika Mlango huu nitafanya uchunguzi katika Aya namba 28 Sura Ya Al-Nisaa Namba 4.
Kwanza Nitainukulu Aya, Nitafuatia na Tafsiri na Kisha Sherehe Ya Aya Kisayansi.
Na pia Mwenyeezi Mungu akipenda nitaelezea Ujumbe wa Aya hii.
يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمۡۚ وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَـٰنُ ضَعِيفً۬ا (٢٨)
TAFSIRI
28. Mwenyezi Mungu anataka kukukhafifishieni maana mwanaadamu ameumbwa dhaifu (Hana nguvu kubwa kabisa za kiwiliwill wala nguvu kubwa za kupigana na moyo na shetani).
SHEREHE
Mwenyeezi Mungu anatuhakikishia katika Aya hii kwamba Tumeumbwa Dhaifu kiwiliwili na pia Kinafsi. Miili yetu ni Dhaifu na Pia Nafsi zetu pia ni Dhaifu. Na kwa hekima yake kubwa anatunasihi tushikane na Anayotufundisha katika Kuruani na Hadithi za Mtume Mohamad. ﷺ. Shetani wanataka kumharibu binaadamu aharibikiwe na maisha yake na tumeumbwa Dhaifu. Mwenyeezi Mungu anatunasihi na kutujuulisha kwamba Tumeumbwa Dhaifu na anatupa Silaha ya Kujikinga na Hatari za Sheitan. Ili tuwe Salama na hatari hizo inabidi tufuate njia anayotaka yeye na siyo njia tunazotaka sisi. Tumuombe Mwenyeezi Mungu atulinde na Maradhi mbalimbali. Atulinde na Shari zinazotokana na Viumbe vingine kama vile Corrona na Mengine yaliyo hatari zaidi ya Corrona.
MUUJIZA WA KISAYANSI
Aya hii pia inashangaza sana. Tukichambua Herufi, Maneno Yake na Mpangilio wake katika Kuruani tunapata Miujiza Mingine ya Kiajabu.
Hebu Tufanye kazi pamoja ya kuichambua Aya hii. Na kisha Tufikiri na Tuone yenye kushangaza. Nitainukulu tena Aya hii ili tuichambue pamoja na tuone Maajabu.
يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمۡۚ وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَـٰنُ ضَعِيفً۬ا (٢٨)
Namba Ya Aya Hii ni 28 na Ukihesabu Herufi za Aya Hii kuanzia Mwanzo wa Aya Mpaka Neno ٱلۡإِنسَـٰنُ “Insan” utapata Jumla ya herufi ni 28. Suala la Kujiuliza ni Kwamba Aya hii inazungumzia Habari za Binaadamu yaani “INSAN” na kuanzia mwanzo wa Aya hii mpaka mwisho wa Neno “INSAN” wa Aya hii unapata jumla ya Herufi ni 28.
Je unaona ya Maajabu kwamba Namba Ya Aya pia ni 28. Hebu sasa tuchunguze Hii Namba 28 je inaashiria kitu gani? Sasa angalia Yanayofuata.
Katika Elimu Ya Hesabu tunafundishwa kwamba Kuna Number System Mbali Mbali.
Kuhusu Kuruani tumeelezea Miujiza inayoambatana na Namba 19 kwamba Namba hii ni Muujiza mkubwa Katika baadhi ya Milango ya website hii nimedokeza habari za Namba 19.
Kuna Utafiti mbalimbali kuhusu namba hii inayoshangaza katika Kuruani lakini uwe macho kwani Namba hii inaambatana na yule aliyeigundua Aliyejulikana kwa jina kama Rashadi Mtu huyu asili yake ni kutoka Misri, lakini alifanya makosa makubwa kwani baada tu ya kugundua Muujiza wa namba hii katika kuruani akaendelea kufanya makosa kwani aliichukulia kama kipimo cha kupimia Aya za kuruani na kisha kuanza kukosoa Kuruani. Hayo ni makosa ya bwana huyu. Na isitoshe akadai Utume Yaani Unabii.
Mwenyeezi Mung atuipushie Uchafu kama huu. Na mwishowe mtu huyu aliyekuwa akiiishi huko America aliuawa katika Msikiti.
Haya ni makosa siyo madogo kwani Tusichukuwe Kipimo chochote na kisha kuanza Kukosoa Kuruani. Usisahau kwamba Kuruani ni kama Rula ya maisha yetu.
Tumia kuruani kukosoa Kila kitu lakini usitumie vipimo vingine kuikosoa Kuruani.
Hayo na Makosa makubwa. Kuruani ni maneno ya Mwenyeezi Mungu na siyo upuuzi wa Kukosolewa. Allahu Akbar.
Sasa tuendelee na Utafiti wa leo.
NUMBER SYSTEMS (MFUMO WA NAMBA)
Namba zimegawanyika katika Syatems mbalimbali kama ifuatavyo: Kwa mfano
Base-2 (Binary Number System)
3. Base-8 (Octal Number System)
4. Base-10 (Decimal Number System)
5. Base-16 (Hexadecimal Number System)
6 Base-19 (Enneadecimal Number System)
Utashangaa unapogeuza Namba 28 kutoka katika
10 Base System kwenda katika 19 Base System . Ukifanya hivyo kwa kutumia Calculator ya Mtandao utapata Jawabu ni namba 19 ambayo ni namba ya Muujiza. (Nimezungumzia namba 19 kwingineko katika website hii).
Sasa Angalia yanayofuata ambayo yanashangaza zaidi. Utashangaa unapogeuza Namba 28 kutoka katika 19 Base System kwenda katika 10 Base System Utapata Namba 46. Na Namba 46 ni Chromosomes za Binaadamu.
Je unaona ya kushangaza. Chromosomes ni Kanda 46 ambazo asili yake ni 23 za Mbegu ya Mume na 23 za Mbegu ya Mke. Na Katika kanda hizo Kuna GENES ambazo zina habari ya umbile la kiumbe. Kwa mfano Aya tuliyoisoma hapa Juu inazungumzia UDHAHIFU WA BINAADAMU Udhaifu huu upo katika GENES za kanda hizo. Kwa hiyo Aya hii ina mengineyo ya kushangaza ambayo kama tunavyoona hapa ni Udhaifu wa binaadamu ambao upo katika Damu yetu. Kila mtu amezaliwa nao. Yaani sisi wote tuna sifa hiyo. Tuasomeshwa katika Elimu ya Genetics kuhusu Sifa za Urithi wa Maumbile. Lakini Sayansi bado ipo nyuma. Kuruani Inatupa mambo ambayo hata Sayansi bado haijajua. Elimu ya Genetics Haijasema kwamba binaadamu wote ni Dhaifu. Na haijatufundisha kwamba Udhaifu huu unatokana Na GENES lakini Baada ya Utafiti Huu Maoni yangu ni Kwamba Hivyo ndivyo ilivyo. Naam.
Kuruani inatuma mapya na ninaamini hivyo 100% kwamba binaadami wote ni dhaifu na sifa hii ipo katika kila GENES za binaadamu. Ninaamini hivyo kwa sababu kuruani ni maneno ya aliyetuumba. Wataalamu wakisema vinginevyo mimi siamini hata kidogo. Ninaamini Kuruani na Ninajua kwamba Ipo juu ya kila Elimu. Kuruani haina kosa hata moja. Allahu Akbar.
Usifikiri Nimemaliza kuichambua Aya hii. Ndugu wasomaji bado nipo mwanzoni.
Kuna Uthibitisho unaofuata ambao utakutoa Povu mdomoni.
Sasa tuendelee na Utafiti Huu hapa chini wa Aya tuliyoitaja hapa juu. Angalia Maajabu yanayofuata:
tuichambue Aya hii kipande kipande kwa kuhesabu herufi zake.
يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمۡۚ وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَـٰنُ ضَعِيفً۬ا (٢٨)
kutumika na kukariri kwa herufi za kipande hiki وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَـٰنُ ضَعِيفً۬ا peke yake chenye maana ya “Binadamu ameumbwa Dhaifu” katika aya hii yote ni kama ifuatavyo:
Waw imetumika Mara 1
Kha imetumika Mara 2
Lam imetumika mara 4
Qaf imetumika mara 1
Alif imetumika mara 5
Lam imetumika mara 4
Alif imetumika mara 5
Nun imetumika mara 4
Sin imetumika mara 1
Nun imetumika mara 4
Dwad imetumika mara 1
Ain imetumika mara 2
Ya imetumika mara 4
Fa imetumika mara 3
Alif imetumika mara 5
sasa tujumlishe namba hizi
1 + 2 + 4 + 1 + 5 + 4 + 5 + 4 + 1 + 4 + 1 +2 + 4 + 3 + 5=46
je unaona ya kushangaza. Tunapata tena idadi za Chromosomes za binaadamu ambazo ni 46. huu ni ushahidi kwamba hesabu tulizofanya hapa juu ni sahihi. je unaona ya maajabu hebu sasa tuendelee.
Tufanye utafiti wa kipande kinachofuata kama tulivyofanya hapa juu. tuchinguze idadi ya kukariri kwa herufi ya kipande hiki katika aya namba 28 ya sura ya Al-Nisaa.
يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمۡۚ وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَـٰنُ ضَعِيفً۬ا (٢٨)
وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَـٰنُ
kama tulivyofanya hapa juu tuhesabu kukariri ka herufi za kioande hiki katika aya hii. kipande hiki kina maana ya “Binaadamu Ameumbwa” hebu tuone ya kushangaza hapa chini:
Waw Imekariri mara 1
Kha Imekariri mara 2
Lam imekariri mara 4
Qaf imekariri mara 1
Alif imekariri mara 5
Lam imekariri mara 4
Alif imekariri mara 5
Nun imekariri mara 4
Sin imekariri mara 1
Nun imekariri mara 4
Sasa tujumlishe
1 + 2 + 4 + 1 + 5 + 4 + 5 + 4 + 1 + 4=31 Jawabu ni namba 31.
Tusibabaike kwani utajiuliza kwa nini siyo 46. Wewe tulia acha wasiwasi. Kuruani inataka Elimu mbalimbali kwa hiyo usifikiri kuna kosa.
Ukienda katika Composite Numbers. (usisahau nimeelezea prime na composite numbers katika milango mingine ya website hii) utashangaa unapohesabu kuanzia Composite Number ya 1 mpaka ya 31 kwamba ni 46. Yaani Composite Number 46 ni ya 31. Angalia maajabu. Tunapata Chromosomes 46 tena mara nyingine kwa nija ya kiajabu. Je unaona tena na tena inathibitisha kauli tuliyosema hapo juu. Allahu Akbar.
Sasa tuchambue herufi za Neno la ٱلۡإِنسَـٰنُ katika Aya ifuatayo. Tufanye kama tulivyofanya hapo juu. Tuone ya kushangaza tena na tena:
يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمۡۚ وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَـٰنُ ضَعِيفً۬ا (٢٨)
ٱلۡإِنسَـٰنُ
Neno Hili la “Alinsan” lina maana ya “Binaadamu” Ukihesabu herufi zake zilivyotumika na kukariri katika aya hii utashangaa kuona kama ifuatavyo:
Alif imekariri mara 5
Lam imekariri mara 4
Alif imekariri mara 5
Nun imekariri mara 4
Sin imekariri mara 1
Nun imekariri mara 4
5 + 4 + 5 + 4 + 1 + 4=23
Je unaona ya kushangaza. Tunapata namba 23. Namba hii ni Mbegu za baba au mama. Kwani 23 za baba unapochanganya na 23 za mama zinakuwa jumla ni 46. Tena na Tena tunaonyeshwa Muujiza wa kanda 46 za Chromosomes. Angalia ya Kututoa Mapovu midomoni. Hatuna Ujanja. Ukifikiri unaona ukweli kwamba aliyetuumba ndiye yule yule aliyeshusha kuruani. Na Hii ni hotuba yake. Allahu Akbar.
KUKARIRI KWA NENO ٱلۡإِنسَـٰنُ “Insan”
Tunaendelea Kuichambua Aya tuliyoitaja hapa juu katika Muujiza wa Chromosomes za Binaadamu ambazo ni 46.
Katika Kuruani yote Neno ٱلۡإِنسَـٰنُ “Insan” Limetumika na kukariri mara 65 katika Aya 63 ambazo zipo katika Idadi ya Sura 43.
Muujiza Mwingine wa Kushangaza ni Namba 65 ya Idadi ya Neno “INSAN” lilivyotumika katika Kuruani yote.
Ukichunguza Namba hii 65 utaikuta ni Compound Number ya 46.
Yaani ukihesabu Compund Number kuanzia namba 4, 6, 8, 9, 10 mpaka 65 utakuta namba 65 ni ya 46 katika mpangilio wa hesabu za Compound Numbers.
Allahu Akbar Angalia Muujiza tena na tena tunapata Namba 46 ambayo inaashiria Chromosomes tulizozitaja hapa Juu.
Kama tulivyosema kwamba Neno “INSAN” limetajika katika Kuruani Mara 65 katika Jumla za Aya 63 Na zote zipo katika Jumla ya Sura 43.
Lingine la kushangaza ni Namba 63 ambayo ni Compund Number ya 44 katika Mpangilio wa Compound Numebers. Sasa la kushangaza ni Hii Namba 44
ambayo inaashiria Jumla ya Autosomes za Binaadamu. Kama tulivyosema kwamba Binaadamu ana Chromosomes 46 basi pia na Autosomes zipo 44. Ni Nini Autosomes?
Autosomes ni Kanda (Chromosomes) Zinazobeba Genes za sifa za Binaadamu isipokuwa zile Genes za Uzazi (Sex Chromosomes) na ambazo jumla yake ni mbili. (Moja ya Kiume (XX) na Ya Pili ya Kike (XY) )
Kwa kifupi Chromosomes ni kanda 46 na Autosomes kanda 44.
kwa hiyo Namba 65 ni Compound Number 46 na 63 Ni Compund Number 44. (46 ni Chromosomes na 44 ni Autosomes) Jer unaona Muashirio wa kushangaza?
Allahu Akbar. Je unaona Umbile la binaadamu linavyoashiriwa katika Kuruani Tukufu?
Kuna Aya Mbili katika Kuruani ambazo zimetaja neno “INSAN mara mbili na hizo ni kama zifuatazo
Sura Namba 17 Aya Namba 11
ويدع الانسن بالشر دعاه بالخير وكان الانسن عجولا
na
Sura Namba 42 Aya Namba 48
فان اعرضوا فما ارسلنك عليهم حفيظا ان عليك الا البلغ وانا اذا اذقنا الانسن منا رحمه فرح بها وان تصبهم سييه بما قدمت ايديهم فان الانسن كفور
Ukijumlisha Aya hizi mbili zinazotaja Neno “INSAN” na Aya Nyinginezo baina ya Aya hizi mbili ambazo pia zimetumia na Kutaja neno “INSAN” utapata Jumla ni Aya 23.
Yaani kuanzia Sura Namba 17 Aya Namba 11 ambayo imetaja Neno “INSAN” mara mbili na baada ya hapo Aya zote zinazotaja Neno “INSAN” mpaka Sura Namba 42 Aya Namba 48 ambayo pia imetaja Neno “INSAN” mara mbili utapata Jumla Ya Aya ni 23.
Angalia Ya Kushangaza. Tunapata tena Chromosomes 23 ambazo ni za Kiume au Kike. Kwani Baba ana Chromosomes 23 na Mama ana Chromosomes 23. Je unaona Mushirio wa kushagaza? Allahu Akbar.
Ukihesabu Herufi za Lugha Ya Arabic na kuzipa Herufi hizo Namba. Kwa mfano.
Alif=1
Bas=2
Taa=3
Jim=4
Ukiendelea hivyo kisha tugeuze Neno انسٰن “INSAN” katika namba utaona maajabu mengineyo. Hebu tufanye hivyo.
Alif=1
Nun=25
Sin=12
Nun=25
Tukijumlisha tunapata 1 + 25 + 12 + 25=63
Na kama tulivyosema hapo awali kwamba Namba 63 Ni Compound Number ya 44 katika mpangilio wa Kihesabu wa Orodha ya Compound Numbers. Je unakumbuka namba 44? Tulisema ni Autosomes. Nimekwisha Kuzungumzia hapo Juu maana ya Autosomes. Hizi ni kanda 44 za Maumbile zisizokuwa na Sex Chromsomes. Na huenda Muashirio wa namba hii ni Hizi Autosomes ambazo zina sifa za maumbile ya binaadamu.
Pia nakumbuka katika website hii nilikwisha kuzungumzia Kwamba kutumika kwa Herufi za neno “INSAN” katika Sura Ya Al-Fatiha ni mara 46. Na namba hii ni jumla ya Chromosomes za Binaadamu.
Mwenyeezi Mungu anajua zaidi haya tunayozungumzia. Ikiwa muradi ni huo. Sisi hatuna zidi isipokua kushangaa Muujiza wa Kuruani ambao hauna mwisho. Allahu Akbar