SCIENTIFIC AND ISLAMIC RESEARCHES

Miujiza Ya Kuruani-8

UTAFITI MBALIMBALI  KATIKA DINI NA SAYANSI

IMEANDALIWA NA  AL-AMIN ALI HAMAD

MIUJIZA MBALI YA KURUANI

Saturday 23 April 2022=22 Ramadan 1443

Kwanza kabla ya Kuelezea habari yeyote ningependelea Kumshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kila alichitupa na pia kwa kila asichotupa. Alhamdulilah katika kila hali. Baada ya Dua hii ningependelea kuwaletea Maajabu Ya Kuruani Yafuatayo.

MAAJABU KATIKA SURA YA YASIN

Baada ya uchunguzi wa Sura Kubwa Ya Yasin utashangaa kuona kwamba Namba Ya Sura Ni 36 na Sura Hii Ina Aya 83 na baada ya Ku Multiply namba hiz Mbili  83 X 36  tunapata  Jawabu ni 2988.  Utashangaa zaidi ukiam biwa kwamba Idadi Ya Herfufi za Sura hii ni 2988.   Ndugu Waislamu Unaona  Saini ya Mwenyeezi Mungu hapa. Mpangilio wa kiajabu sana.  Yaani

Namba Ya Sura  X  Idadi Ya Aya Za Sura Hii= Idadi ya Herufi za Sura Hii

yaani    36  X    83=2988

Allahu Akbar.  Utafikiri Mtume alikuwa akitumia Computer lakini wakati huo karne ya Saba kulikuwa hakuna Computer. Wakati huo walikuwa wakitumia Punda na Farasi katika Usafiri wao. Sayansi ilikuwa bado Changa. Huoni Muujiza wa Kiajabu. Kabla hata hatujasoma Sura Hii yaani Mwanzo tu tunakutana na Muujiza sasa je Sura Yenyewe? Na ndiyo Maana Sura Hii ikasifiwa kwamba ndiyo Moyo wa Kuruani. 

Hadithi Ifuatayo imekusanywa katika Jami` at-Tirmidhi Reference Namba 2887

Ni Hadithi Dhaifu kama ilivyopokelewa. Inasema kwamba Kila kitu kina Moyo na Moyo wa Kuruani ni Ni Yasin. Na Yule ambaye ataisoma Sura Ya Yasin Mwenyeezi Mungu atampa Ujira kiasi cha Kisomo cha Kuruani mara 10.  Ni Dhaifu lakini haikukataliwa. Yaani huenda Hadithi ikawa kweli. Yaani Maneno haya Huenda yalisemwa na Mtume Mohamad. ﷺ

حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ وَسُفْيَانُ بْنُ وَكِيعٍ، قَالاَ حَدَّثَنَا حُمَيْدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ الرُّؤَاسِيُّ، عَنِ الْحَسَنِ بْنِ صَالِحٍ، عَنْ هَارُونَ أَبِي مُحَمَّدٍ، عَنْ مُقَاتِلِ بْنِ حَيَّانَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏ “‏ إِنَّ لِكُلِّ شَيْءٍ قَلْبًا وَقَلْبُ الْقُرْآنِ يس وَمَنْ قَرَأَ يس كَتَبَ اللَّهُ لَهُ بِقِرَاءَتِهَا قِرَاءَةَ الْقُرْآنِ عَشْرَ مَرَّاتٍ ‏”‏ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ غَرِيبٌ لاَ نَعْرِفُهُ إِلاَّ مِنْ حَدِيثِ حُمَيْدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ وَبِالْبَصْرَةِ لاَ يَعْرِفُونَ مِنْ حَدِيثِ قَتَادَةَ إِلاَّ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ ‏.‏ وَهَارُونُ أَبُو مُحَمَّدٍ شَيْخٌ مَجْهُولٌ ‏.‏ حَدَّثَنَا أَبُو مُوسَى مُحَمَّدُ بْنُ الْمُثَنَّى، قَالَ حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ سَعِيدٍ الدَّارِمِيُّ، قَالَ حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ، عَنْ حُمَيْدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، بِهَذَا ‏.‏ وَفِي الْبَابِ عَنْ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ، وَلاَ يَصِحُّ مِنْ قِبَلِ إِسْنَادِهِ إِسْنَادُهُ ضَعِيفٌ ‏.‏ وَ فِي البَابِ عَنْ أَبِي هُرَيرَةَ

AYA ZILIZOTANGULIWA NA VIAPO 

Ndugu Waislamu Hebu tuendelee na Safari Yetu ya Kuchambua  Aya zilizotanguliwa na Kiapo na hizo Jumla yake ni  8.  Mwenyeezi Mungu hafanyi Viapo Bure bure. Kila anachoapia ni Kikubwa na pia kuna Maajabu mengineyo tunayoyajua na tusiyoyajua. Mwenyeezi Mungu ni mkubwa sana na sisi ni Viumbe vyake na hahitaji Kufanya Kiapo na ndiyo Maana  kiapo cha  Neno  “QASAM” kimetanguliwa na Herufi  “LA”  ambayo inajulikana katika Grammar kama LA ZAIDA  na ijapokuwa ni ZAIDA lakini  inaleta maana ya  kusema kwamba  Kwa Ukubwa wake Mwenyeezi Mungu  hana haja ya  Kutuapia Sisi Viumbe wake  walio Dhaifu lakini Jambo hilo analozungumzia ni kubwa na ili tulifikirie na kulitia  maanani.  Herufi  “FA” inajulikana kama  “FA AL- ISTIINAF. 

Allahu Akbar. Kitendo القسم “QASAM” yaani Kiapo kimekariri na kutumika katika kuruani mara 8. Yaani katika Aya 8 zifuatazo. Hebu tuzichambue na Tuone Miujiza iliyobebwa na Aya Hizi. 

AYA YA KWANZA

فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ (75) وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ (76) إِنَّهُ لَقُرْآَنٌ كَرِيمٌ (77) فِي كِتَابٍ مَكْنُونٍ (78) لَا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ (79) تَنْزِيلٌ مِنْ رَبِّ الْعَالَمِينَ

TAFSIRI

75. Basi Ninaapa kwa SEHEMU (POSITIONS AU LOCATIONS)za nyota, 76. Na hakika hicho bila shaka ni kiapo kikubwa, laiti mngalijua! 77. Bila shaka hiki (mnachosomewa) ni Kitabu kilichokusanya kila yanayohitajiwa na Chenye heshima · 78. Kilichotolewa katika hicho Kitabu kilichohifadhiwa kweli kweli, (Lawhul Mahfudh). 79· Hapana akigusaye ila waliotakaswa na mabaya. 8o. Ni uteremsho unaotoka kwa Mola wa walimwengu. 

SHEREHE NA MAONI

Nyota Angani zipo mbali sana lakini mwanga wa nyota unatudangan’ya na tunadhani Nyota ipo karibu. Na Umbali wake unahesabiwa kwa Kutumia Mwanga na siyo Maili au Kilomita. kwa mfano Nyota za karibu sana na Ardhi ni  Alpha Centauri na inachukua Muda wa Miaka  4.35 Ya Usafiri wa Mwanga (Light-Years) Kwa mbio za mwanga wake kutufikia  ardhini yaani kwa kutumia kipimo cha Mwanga. Sasa angalia Maajabu Ya Kuruani. Mwenyeezi Mungu anasema katika Aya hii kwamba anaapa na SEHEMU ZA NYOTA”  kwani sisi tunaona SEHEMU TU HIZO ZILIZOKUWA NA NYOTA HAPO ZAMANI”  Hapo Miaka Mingi iliyopita  na siyo Nyota zenyewe kwani  zilikwisha ondoka muda mrefu uliopita. Yaani sisi tunaona Picha ya Nyota kama ilivyokuwa Miaka Mingi iliyopita na siyo Nyota Zenyewe. Angalia Kuruani ilivyopima. Hakuna Kosa. Allahu Akbar. Huwezi kupata kosa kwani aliyeishusha ndiye Mumbaji wa Kila kitu. 

(The closest star to Earth is a triple-star system called Alpha Centauri. The two main stars are Alpha Centauri A and Alpha Centauri B, which form a binary pair. They are about 4.35 light-years from Earth, according to NASA

AYA YA PILI

Inaendelea karibuni Inshaallah Mwenyeezi Mungu akinipa Uzima na Afya na huenda kabla au baada  ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.